Sheria Ndogoya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ya Mwaka 2024
This provision gives the short title of the by-law: Morogoro Municipal Council’s Health, Sanitation and Environmental Management By-law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogoya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the short title of the by-law: Morogoro Municipal Council’s Health, Sanitation and Environmental Management By-law, 2024. This bylaw applies throughout the area of the Morogoro Municipal Council. Section 3 gives key definitions used in the by-law, including waste fee, environmental pollution fee, and authorized officer. Halmashauri ina mamlaka ya kusimamia usafi, afya na mazingira, kutoa elimu, kuteua wakala, kufanya ukaguzi, kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaokiuka, na kuingia mikataba kwa ajili ya kazi hizo. Kila mtu lazima ahakikishe usafi wa nyumba, eneo la biashara, taka, maji taka, choo, na kushiriki siku ya usafi.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogoya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ya Mwaka 2024
Showing 54 of 54
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This provision gives the short title of the by-law: Morogoro Municipal Council’s Health, Sanitation and Environmental Management By-law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the area of the Morogoro Municipal Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: Section 3 gives key definitions used in the by-law, including waste fee, environmental pollution fee, and authorized officer.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo: “ada” maana yake ni yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya huduma ya kuzoa taka. “ada ya uchafuzi wa mazingira” maana yake ni malipo yanayotakiwa kulipwa kwa Halmashauri na kampuni, viwanda, kikundi, mtu binafsi na taasisi ambazo shughuli zao zinasababisha uchafuzi wa mazingira; kwa kuzingatia kanuni ya mchafuzi hulipa (Polluter Pay Principle (PPP)). “adha” maana yake hali yoyote mbaya yenye kuleta madhara juu ya afya ya watu na viumbe hai kwa ujumla; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; 1 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) “chakula” maana yake kitu chochote kinacholiwa na binadamu na inajumuisha maji na dawa; “chanzo cha maji” maana yake ni eneo lolote ambalo limetengwa kwa ajili ya kuwa chanzo cha maji kwa matumizi ya jamii na itajumuisha visima, mito, chemchemi, vijito, na maeneo yote yanayopatikana maji; “choo bora” maana yake ni choo chochote cha maji chenye sakafu inayosafishika, banda imara la kudumu, limeezekwa, lina mlango imara, bomba la kutolea hewa chafu na lenye mfuniko kwenye tundu la choo na shimo salama na safi kwa ajili ya kutupa kinyesi na mkojo wa binadamu, lililojengwa kwa vifaa vya kudumu; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro; “uhifadhi wa mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi, mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji unaoozingatia masharti na maelekezo yatakayotolewa na Afisa Mwidhiniwa chini ya Sheria ya Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote; “jengo la biashara” maana yake jengo lolote lililojengwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa ajili ya kufanyia biashara iliyokusudiwa; “kaya” maana yake mtu mzima anayejitegemea mwanamke au mwanaume, na mtoto au watoto inayoishi aidha kwenye nyumba nzima au ndani ya chumba kimoja kwenye eneo la Halmashauri; “kero au chukizo” maana yake ni kitu chochote ambacho kipo katika hali yoyote iwe kinatumika, kimewekwa, kimejengwa, au ni kichafu kiasi cha kusababisha: (a) hatari kwa viumbe na maisha ya binadamu (b) harufu mbaya au harufu ya kuudhi au kuleta kinyaa; (c) kuzaliana kwa wadudu hatari kama vile inzi, 2 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) mende, sisimizi, panya, nyoka, nyuki, kunguni au viumbe wengine hatari; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “kikundi cha mazingira” maana yake ni kikundi chochote cha watu kilichosajiliwa kufanya usafi na usimamizi wa mazingira na udhibiti wa uharibifu wa mazingira katika maeneo ya Halmashauri; “kikundi cha usafishaji” maana yake kikundi cha watu kilichosajiliwa kufanya shughuli za usafi wa mazingira na hasa za udhibiti wa uharibifu wa mazingira katika maeneo ya Halmashauri; “kizimba cha taka” maana yake ni eneo maalum lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuhifadhi taka ngumu; “kituo cha maji machafu” maana yake ni sehemu maalumu iliyotengenezwa kwa ajili ya ukaguzi wa mfereji ambao una mfuniko usioruhusu hewa kutoka; “kuchakata taka” maana kuzichambua, kuzitenganisha na kuzibadili kuwa kitu kingine chenye manufaa kwa jamii; yake ni “bwawa la maji taka” maana yake ni bwawa lililojengwa kwa madhumuni ya kuhifadhi na kutakasa maji taka yanayotokana na kuosha vyombo, matumizi ya vyoo na bafu, kufua nguo, kuosha nywele au shughuli zozote maeneo ya bishara, nyumbani na viwandani; “magonjwa ya mlipuko” maana yake ni magonjwa yanayotokea kwa muda mfupi ya kuambukiza na kuenea kwa haraka na kuathiri watu wengi ndani ya muda mfupi, magonjwa hayo ni kama vile kupooza, kipindupindu, kuhara, surua na homa ya matumbo; “maji taka” maana yake maji yenye mchanganyiko wa kinyesi, mkojo, na maji kutoka masinki ya kuogea, 3 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) kutema mate na kunawia mikono, pamoja na maji yenye mchanganyiko wa vitu vingine vyenye asili ya chemikali au visisvyo na chemikali; “mazingira” yanajumuisha mazingira ya binadamu ikiwa ni pamoja na hewa, ardhi, maji, hali ya hewa, sauti, mwanga, harufu, ladha, viumbe vidogo, mambo ya kibiolojia ya wanyama na mimea, rasilimali za kitamaduni na sababu za kiuchumi za kijamii na inajumuisha mazingirya asili au kujengwa na jinsi wanavyoingiliana; “mifugo” maana yake ng’ombe, punda, nguruwe, mbuzi, mbwa, kondoo, kuku na wanyama wengine wote wafugwao la Halmashauri; binadamu kwenye eneo na “misitu” maana yake ni eneo la ardhi ambalo limefunikwa angalau kwa asilimia 10 na miti, uoto wa asili au uliopandwa, au asilimia 50 au zaidi ya vichaka na miti inayoota au ambayo itajumuisha na yote ya misitu ya hifadhi ambayo itatangaza chini ya sheria za misitu na mazao yote ya misitu ikijumuisha majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote anayeishi katika eneo la Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “taka” maana yake ni kitu chochote ambacho baada ya kukitumia hakina thamani kwa wakati huo na uwepo wake katika eneo hilo unaweza kusababisha chukizo la kiafya na kuhatarisha afya ya jamii; ”taka hatarishi” maana yake ni taka zote zenye sumu au kemikali; “taka ngumu” maana yake ni vitu visivyo majimaji vitokanavyo na shughuli za majumbani, mitaani, 4 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) biashara, viwandani na kilimo; pia ni pamoja na takataka za mabaki ya chakula na matunda, za ujenzi na ubomoaji, ufyekaji bustani, shughuli za madini, mizoga na mabaki ya magari mabovu; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi au kampuni iliyoteuliwa kukusanya ada na ushuru kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii; Mamlaka ya Halmashauri - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na Mamlaka ya
AI-assisted research summary: Halmashauri ina mamlaka ya kusimamia usafi, afya na mazingira, kutoa elimu, kuteua wakala, kufanya ukaguzi, kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaokiuka, na kuingia mikataba kwa ajili ya kazi hizo.
4.-Halmashauri itakuwa na Mamlaka ya- (a) Kusimamia utekelezaji wa shughuli za usafi afya na mazingira. (b) Kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kufuata kanuni za afya, usafi na kutunza mazingira; (c) Kuteua Wakala kwaajili ya kutekeleza shughuli za usimamizi wa afya, usafi na mazingira kwa niaba ya Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (d) Kufanya ukaguzi ili kubaini endapo kanuni za utunzaji wa mazingira afya, zinazingatiwa ndani ya eneo la Halmashauri. (e) Kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote usafi na anayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hizi. (f) Kuingia mkataba na mtu yeyote, taasisi au Kampuni kutelekeza shughuli za usimamizi wa afya, usafi na mazingira. Usafi wa mazingira - 5 Verify source ↗
(1) Kila mtu anawajibu wa kuhakikisha kwamba
AI-assisted research summary: Kila mtu lazima ahakikishe usafi wa nyumba, eneo la biashara, taka, maji taka, choo, na kushiriki siku ya usafi.
5.-(1) Kila mtu anawajibu wa kuhakikisha kwamba: (a) jengo lake, makazi anayoishi au eneo lake la biashara linasafishwa kikamilifu; (b) taka ngumu zote ikiwa ni pamoja na mifuko ya na kuhifadhiwa lililoruhusiwa na zitakusanywa, plastiki kupelekwa katika Halmashauri; eneo (c) maji taka yanaelekezwa ndani ya mfumo wa maji taka; 5 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) (d) anakuwa na choo bora; (e) atashiriki siku ya usafi ambayo ni Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi (f) mfereji wa maji unaomzunguka au kupita kando ya nyumba yake au eneo la biashara yake, kiwanja chake inakuwa safi wakati wote (g) nyumba yake, eneo lake la biashara au kiwanja chake hakina mazalia ya mbu au wadudu wengine wenye madhara kwa afya ya binadamu na mazingira kuhifadhia (h) Anakuwa na chombo imara chenye mfuniko kwa ajili kabla taka hazijachukuliwa kwa ajili ya kwenda kutupwa katika eneo lilotengwa kwa ajili ya kuhifadhi taka; ngumu Usimamizi wa vyanzo vya maji (i) anatunza na kuhifadhi vyombo vya kuhifadhia taka vinavyowekwa na Halmashauri; - 6 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must protect water sources, plant suitable trees there, and take legal action against damage or pollution. People must not do listed activities near or in water sources, especially within 60 metres.
6.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa: (a) kusimamia na kulinda vyanzo vya maji; (b) kupanda miti isiyonyonya maji katika vyanzo vya maji kwa kuzingatia maelekezo ya kitaalamu; (c) kuchukuwa hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayeharibu chanzo cha maji, kuchafua chanzo cha maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji bila sababu ya msingi; (2) Mtu yoyote - (a) Atakayena nawa, oga, fulia nguo au kunywesha mifugo karibu au kwenye chanzo cha maji kama vile chemchem, kisima au chanzo kingine chochote cha maji; (b) Atakaye jenga boma la mifugo karibu au kuruhusu mkojo ya mifugo au maji machafu yatokanayo na zizi la mifugo yake kuelekea 6 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) karibu na chanzo cha maji; (c) Atakaye fuga au kuchunga mifugo ya aina yoyote, ndani ya chanzo cha maji (d) Atakaye anzisha na kufanya shughuli za aina yoyote ndani ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji (e) Atakaye lima, kata miti, chunga mifugo, jenga, fanya jambo lolote katika umbali wa mita 60 kutoka chanzo cha maji; (f) Atakaye jimilikisha eneo la chanzo cha maji asili (g) Atakaye elekeza mabomba ya maji machafu kwenye mto, bwawa, kisima, mfereji, chemchem au sehemu yoyote ambayo ni chanzo cha maji (h) kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama au viumbe vingine vilivyo hai; (i) Atakaye weka kitu chochote chenye sumu kwenye chanzo cha maji ambayo yanatumiwa na binadamu au kiumbe chochote chenye uhai. (j) Atakuwa ametenda kosa. Ada ya uzoaji na utupaji taka - 7 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na ada ya uzoaji na utupaji taka
AI-assisted research summary: Mzalishaji wa taka lazima alipe ada ya uzoaji taka kila tarehe 30 ya mwezi; malipo hupokelewa na wakala au Afisa Mwidhiniwa, ambaye hutoa stakabadhi ya kielektroniki na kujaza rejista ya wazalishaji taka.
7.-(1) Kutakuwa na ada ya uzoaji na utupaji taka ambayo itatozwa na Halmashauri kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa mazingira kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (2) Ada ya uzoaji taka italipwa kila tarehe 30 ya kila mwezi na italipwa kwa wakala au Afisa Mwidhiniwa ambaye atatoa stakabadhi ya malipo kwa njia ya kieletroniki na atajaza katika rejista ya wazalishaji taka (3) Iwapo mzalishaji wa taka atashindwa kulipia gharama ya huduma ya uzoaji taka kwa kipindi cha miezi itamchukulia hatua za miwili mfululizo Halmashauri kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani Wajibu - 8 Verify source ↗
(1) Kila mtu, mmiliki wa kiwanda na mmiliki wa
AI-assisted research summary: Kila mtu, mmiliki wa kiwanda na mmiliki wa nyumba lazima wasimwage maji taka mahali pasipoandaliwa, wajenge mifereji ya kuhifadhi maji taka, wasisababishe vumbi/moshi/uchafu kuwafikia watu na kuleta madhara, na waondoe maji taka karo likijaa.
8.-(1) Kila mtu, mmiliki wa kiwanda na mmiliki wa nyumba anawajibu wa- 7 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) (a) kutotiririsha au kumwaga au kuruhusu au kusababisha kutiririka au kumwagika kwa maji taka barabarani, uchochoroni, kwenye mifereji, au sehemu yoyote isiyotengwa kwa ajili ya kuhifadhi maji taka (b) kujenga mifereji na karo kwa ajili ya kuhifadhi maji taka (c) Kutoruhusu taka kama vile vumbi, maganda, moshi na nyingine zinazofanana na hizo kuwafikia watu na viumbe wengine na kuleta madhara (d) kunyonya maji taka pale karo la kuhifadhi maji taka linapojaa (e) Kutosababisha harufu mbaya itakazosababisha kero kwa wakazi wa eneo lolote la Halmashauri. (2) mtu yoyote, mmiliki wa kiwanda na mmiliki wa nyumba atakayekiuka masharti ya kanuni hii atakuwa ametenda kosa. - 9 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote, kampuni, wakala au taasisi
AI-assisted research summary: Watu, kampuni, wakala au taasisi hawaruhusiwi kuchoma taka hatarishi bila kutoa taarifa kwa Halmashauri. Halmashauri au wakala inaweza kuteketeza taka hatarishi kwa gharama ya shilingi 50,000 kwa tani.
9.-(1) Mtu yeyote, kampuni, wakala au taasisi hairuhusiwi kuchoma taka hatarishi bila kutoa taarifa kwa Halmashauri (2) Halmashauri au wakala anaweza kuteketeza taka hatarishi kwa gharama ya shilingi elfu hamsini kwa tani moja ya taka. - 10 Verify source ↗
Mfanyabiashara wa chakula ataandaa, kuchoma,
AI-assisted research summary: A food trader may prepare, roast, cook, boil, and sell any kind of food anywhere or in any house, if health conditions and rules have been met.
10. Mfanyabiashara wa chakula ataandaa, kuchoma, kupika, kuchemsha na kuuza chakula cha aina yoyote mahali popote au kwenye nyumba yoyote ikiwa ametimiza masharti na kanuni za afya. - 11 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayeendesha biashara ya
AI-assisted research summary: Watu wanaoendesha biashara ya vyakula vya kupikwa au kukaangwa lazima wahifadhi vyakula hivyo kwenye sanduku safi linalozuia inzi, vumbi, na wadudu; wauzaji wa vyakula visivyopikwa lazima viuzwe juu ya meza.
11.-(1) Mtu yeyote anayeendesha biashara ya vyakula vya kupikwa au kukaangwa atakuwa na wajibu wa kuhakikisha vyakula hivyo vinahifadhiwa kwenye sanduku safi na lenye kuzuia inzi, vumbi na wadudu waletao madhara kwa afya ya binadamu. (2) Mtu yeyote anayeuza vyakula visivyopikwa 8 Taka hatarishi Utengenezaji na uuzaji vyakula Uuzaji wa vyakula Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) atatakiwa kuuza vyakula hivyo vikiwa juu ya meza. Usalama wa matumizi ya maji Uzuiaji wa shughuli wakati wa magonjwa ya mlipuko Upimaji wa afya - 12 Verify source ↗
(1) Kila mkazi anapaswa kuhakikisha kwamba
AI-assisted research summary: Residents must make sure drinking water is clean and safe, and well owners must test and confirm well water is safe before people or animals use it.
12.-(1) Kila mkazi anapaswa kuhakikisha kwamba maji yote yanayotumika kwa kunywa ni safi na salama bila kujali yanatoka kwenye chanzo gani cha maji. (2) Kila mmiliki wa kisima atapaswa kuhakikisha maji ya kisima yamepimwa na yamethibitika ni salama kabla ya kuruhusu yatumiwe na binadamu na wanyama. - 13 Verify source ↗
(1) Mkurugenzi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kukataza shughuli kwa tangazo la kipaza sauti, maandishi au vyombo vya habari ikiwa ana sababu ya kuamini shughuli hiyo inaweza kusambaza magonjwa ya mlipuko na kuathiri maisha ya binadamu.
13.-(1) Mkurugenzi anaweza kuzuia yoyote isifanyike kwa kutangaza kwa njia ya kipaza sauti, maandishi au kupitia vyombo vya habari endapo atakuwa na sababu ya kuamini kwamba shughuri hiyo inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kuleta athari kwa maisha ya binadamu (2) Mtu yoyote atakayekiuka masharti ya kanuni hii atakuwa ametenda kosa. Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2) Halmashauri inaweza kuviharibu vyakula vitakavyokamatwa wakati wa katazo (3) Halmashauri haitahusika na gharama za uharibifu zozote zitakazotokea isipokuwa kama uharibifu huo utakuwa umesababishwa kwa uzembe wa Afisa wa Halmashauri. - 14 Verify source ↗
(1) kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa,
AI-assisted research summary: Wafanyakazi wa hoteli, migahawa, baa, bucha, sehemu za kuokea mikate, nyumba za kulala wageni, groseri, au watu wanaotengeneza chakula kwa ajili ya kuuza lazima wapimwe afya angalau kila baada ya miezi sita.
14.-(1) kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa, bucha, sehemu za kuokea mikate, nyumba za kulala wageni, grosari au mtu yeyote anayetengeneza chakula kwa ajili ya kuuza atatakiwa kupima Afya kila baada ya miezi sita. (2) Mmiliki wa biashara atakayeruhusu mhudumu yeyote kufanya kazi bila kupimwa afya yake atakuwa ametenda kosa. Ukaguzi - 15 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: An inspection officer may enter any building during the stated hours to inspect it, the Director may give 30 days to fix defects found in inspection, and may close a business or building that is found to breach the regulations.
15.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia katika jengo lolote kuanzia Saa moja na nusu asubuhi hadi Saa kumi na moja kamili jioni kwa lengo la 9 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) kufanya ukaguzi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Mkurugenzi anaweza kutoa muda wa siku thelathini kwa mmiliki wa jengo au biashara kurekebisha mapugufu yatakayoonekana kipindi cha ukaguzi kwa mujibu wa kanuni hii. (3) Mkurugenzi anaweza kufunga biashara yoyote au jengo ambalo limekaguliwa na kukutwa limekiuka masharti ya Kanuni hizi. Udhibiti wa ubebaji kokoto, mawe na mchanga - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayesafirisha mawe, mchanga au
AI-assisted research summary: Anyone transporting stones, sand, or gravel within the Council area must cover the transport vehicle to prevent spillage and environmental pollution.
16. Mtu yeyote atakayesafirisha mawe, mchanga au kokoto katika eneo la Halmashauri atahakikisha kuwa chombo anachotumia kusafirisha kimefunikwa ili kuzuia kumwagika kwa mawe, mchanga au kokoto hizo na kuchafua mazingira. Wajibu wa kupanda miti Ushirikishaji wa jamii katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira - 17 Verify source ↗
Kila mmiliki wa jengo la makazi au biashara, na
AI-assisted research summary: Wamiliki wa majengo ya makazi au biashara, na wamiliki wa mashamba, lazima wapande miti kwenye jengo au shamba lao.
17. Kila mmiliki wa jengo la makazi au biashara, na mmiliki wa shamba atakuwa na wajibu wa kupanda miti kwenye jengo au shamba analomiliki. - 18 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kuingia mkataba na mtu
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuingia mkataba na watu au taasisi fulani ili kuboresha bustani, maeneo ya wazi, na uhifadhi wa mazingira ndani ya ngazi za Mtaa, Kata au Wilaya.
18. Halmashauri inaweza kuingia mkataba na mtu yeyote, taasisi, kikundi binafsi au asasi ya kiraia, ndani ya Halmashauri katika ngazi ya Mtaa, Kata au Wilaya katika kuboresha bustani, eneo la wazi na uhifadhi wa mazingira. Tathimini ya athari kwa mazingira na jamii - 19 Verify source ↗
(1) Miradi yote
AI-assisted research summary: Mradi unaotekelezwa ndani ya Halmashauri haupaswi kuendelezwa bila tathmini ya athari ya mazingira, na mpendekezaji wa mradi analipa Halmashauri asilimia 10 ya thamani ya mradi kama gharama ya tathmini hiyo.
19.-(1) Miradi yote inayotekelezwa ndani ya Halmashauri haitaaendelezwa bila kufanyiwa tathmini ya athari ya mazingira (2) Kila mpendekezaji wa mradi atawajibika kulipa Halmashauri asilimia kumi ya thamani ya mradi ikiwa ni gharama ya tathimini ya athari za mazingira juu ya mradi husika. Udhibiti utupaji wa taka kwenye vyombo vya usfariri - 20 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa chombo cha usafiri wa
AI-assisted research summary: Owners of public transport vehicles must provide a special container or device for passengers’ waste, users must not throw waste outside the vehicle, and anyone who breaches the rule commits an offence.
20.-(1) Kila mmiliki wa chombo cha usafiri wa umma ataweka chombo au kifaa maalumu kwaajili ya kuhifadhia taka za abiria. (2) Watumiaji wa vyombo vya usafiri binafsi au vya 10 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) umma hawataruhusiwa kutupa taka nje ya vyombo wanavyotumia na taka zote zitawekwa kwenye chombo cha kuhifadhia taka kilichomo kwenye chombo husika. (3) Mtu yoyote atakayekiuka masharti ya kanuni hii atakuwa ametenda kosa. Uanzishwaji wa Vikundi Jamii (CBOs) - 21 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na jukumu la kuhamasisha
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ihamasishe na kuitambua Vikundi Jamii ili viweze kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu na usafi wa mazingira, baada ya kuingia mkataba na Halmashauri.
21. Halmashauri itakuwa na jukumu la kuhamasisha uundaji wa Vikundi Jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira baada ya kuingia mkataba na Halmashauri Wajibu wa kuwa na choo na kukitumia - 22 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba ana wajibu wa
AI-assisted research summary: House owners must keep a clean, sturdy toilet for residents and provide a designated handwashing area with clean water and soap. Toilets must be built at least 60 metres from any water source.
22.-(1) Kila mmiliki wa nyumba ana wajibu wa kuhakikisha kwamba: (a) nyumba yake ina choo safi, imara kwa matumizi ya wakazi wa nyumba hiyo; (b) anaweka sehemu maalum ya kunawia mikono ikiwa na maji safi na sabuni. (2) Choo kinatakiwa kijengwe umbali wa mita sitini kutoka chanzo chochote cha maji. Masharti ya ujenzi wa vyoo vya umma - 23 Verify source ↗
Vyoo vya umma vitakavyojengwa kwenye eneo
AI-assisted research summary: Vyoo vya umma vinavyojengwa ndani ya eneo la Halmashauri lazima viwe vya kudumu na viwe na vifaa vilivyoorodheshwa, ikiwemo matundu mawili au zaidi kwa wanawake na mawili au zaidi kwa wanaume.
23. Vyoo vya umma vitakavyojengwa kwenye eneo lolote la Halmashauri vitatakiwa view vya kudumu na vitatakiwa kuwa na (a) Matundu yasiyopungua mawili kwa wanawake na mawili kwa wanaume (b) Mfumo madhubuti wa maji na uwepo wa maji ya kutosha yaliyo safi na salama; (c) Chombo cha Kuhifadhia maji ya akiba; (d) Bafu la wanaume na wanawake; (e) kuwepo na Sehemu ya haja ndogo kwa wanaume; na (f) kuwepo na chombo maalumu chenye mfuniko cha kuhifadhia taka zisizoweza kusukumwa na maji. 11 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) Vyoo vya muda katika mikusanyiko - 24 Verify source ↗
(1) Ni wajibu wa mtu yeyote, kikundi au taasisi
AI-assisted research summary: Watu, vikundi au taasisi zinazoandaa mkutano, sherehe au mkusanyiko lazima ziweke vyoo vya muda ikiwa eneo halina choo cha kudumu.
24.-(1) Ni wajibu wa mtu yeyote, kikundi au taasisi yenye lengo la kukusanya watu kwa madhumuni ya mkutano au sherehe au mkusanyiko wowote kuweka vyoo vya muda endapo eneo hilo hakuna choo cha kudumu (2) Mtu yeyote, kikundi au taasisi inayotaka kuweka idhini kutoka choo cha muda itatatakiwa kuomba Halmashauri kabla ya kuweka choo hicho. Vyoo katika majengo ya biashara - 25 Verify source ↗
Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya 23 ya
AI-assisted research summary: Kila mmiliki wa jengo la biashara anatakiwa kujenga vyoo kwa ajili ya matumizi ya wateja wake, kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya 23.
25. Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya 23 ya Kanuni hizi, kila mmiliki wa jengo la biashara atatakiwa kujenga vyoo vyenye kwa ajili ya matumizi ya wateja wake. Uteuzi wa Wakala - 26 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua
AI-assisted research summary: Halmashauri ina mamlaka ya kuteua Wakala wa kusimamia utekelezaji wa kanuni hizi, na Wakala aliyeteuliwa lazima akusanye ada na atekeleze mkataba wake.
26.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua Wakala wa kusimamia utekelezaji wa kanuni hii ikiwemo kukusanya ada kwa niaba ya Halmashauri (2) Wakala atakayeteuliwa chini ya Sheria Ndogo hii atakuwa na wajibu wa (a) Kukusanya, kwa niaba ya Halmashauri, ada mbalimbali zinazohusiana na afya, usafi na usimamizi wa mazingira, katika eneo lake alilopangiwa na kwa viwango vilichoidhinishwa chini ya Sheria Ndogo hii. (b) kukusanya ada kwa kutumia mfumo wa kielekitroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. (c) Kutekeleza masharti yote ya mkataba wake na Halmashauri - 27 Verify source ↗
Mtu yeyote atakaye
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kutupa taka, kuchafua maeneo ya umma, kufanya shughuli fulani kwenye maeneo yasiyoruhusiwa, au kuchoma taka hovyo ndani ya eneo la Halmashauri.
27. Mtu yeyote atakaye; (a) Tupa taka au uchafu wowote au kuacha taka au uchafu kwenye nyumba, kiwanja, mfereji wa maji ya mvua, barabara au eneo linalopakana na nyumba yoyote au ardhi yoyote au karibu na maeneo ya nyumba au mahali popote pasipotengwa kwa shughuli hiyo; 12 Makosa Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) (b) au kujaribu kumzuia au atamshawishi mtu au kundi la watu kumzuia Afisa Mwidhiniwa asitekeleze wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii (c) Osha magari, kufua, kunywesha mifugo na kukoroga dawa za mimea ndani ya mito, mabwawa au ndani ya chanzo au kisima kinachotumika kwa matumizi ya binadamu; (d) Atapika vyakula pembezoni ya barabara au nje ya majengo mengine (e) Atauza vyakula maeneo yasiyo rasmi kwa biashara hiyo; (f) Kushindwa kuhifadhi chakula kwenye kabati safi lililofunikwa na lenye kioo; (g) Atafanya matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo, katika maeneo yasiyotengwa kwa shughuli hizo; (h) Atavuta Sigara hadharani au kwenye vyombo vya usafiri (i) Atatema mate hovyo au kutema mate barabarani au hadharani; (j) Ataacha chombo cha usafiri katika hali ya uchafu; (k) Ataenda haja ndogo au kubwa kwenye maeneo mengine tofauti na chooni; (l) Atachunga mifugo kwenye eneo lolote lililopandwa miti au misitu iliyohifadhiwa; (m) Atalima au kukata miti katika vyanzo vya maji, milima, kando ya njia, makorongo na sehemu nyingine zozote zinazohifadhiwa ili kupunguza mmomonyoko wa udongo. (n) Atachoma taka hovyo ndani ya eneo la Halmashauri. Adhabu - 28 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevunja masharti yaliyowekwa
AI-assisted research summary: Anyone who breaks the by-law conditions commits an offence and may be fined up to 300,000 shillings, jailed up to 12 months, or both.
28. Mtu yeyote atakayevunja masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana 13 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. kufifilisha kosa - 29 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa na kutoza Shilingi laki mbili ikiwa mkosaji anakiri kosa, anakubali kujaza fomu maalum ya Jedwali la Pili, na analipa ada au ushuru anaodaiwa.
29. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au ushuru anaodaiwa 14 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) ________________ JEDWALI LA KWANZA __________________ (limetengenezwa chini ya kanuni ya 7(1)) Namba Aina ya Biashara SEHEMU A: ADA YA UZOAJI WA TAKA Ada kwa mwezi (Shilingi)
Part
SEHEMU A: ADA YA UZOAJI WA TAKA
- 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: This section is about food stations for passengers of transport vehicles.
8. Vituo vya chakula kwa abiria wa vyombo vya usafiri - 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: This provision lists “Super market” followed by several numeric amounts, but it does not clearly state a rule.
10. Super market 500,000 200,000 50,000 50,000 80,000 30,000 100,000 150,000 20,000 30,000 - 11 Verify source ↗
Maduka ya dawa za binadamu (wauzaji wa jumla/jumla na
AI-assisted research summary: This section names human medicine pharmacies, including wholesale and retail sellers.
11. Maduka ya dawa za binadamu (wauzaji wa jumla/jumla na 30,000 rejareja) - 12 Verify source ↗
Maduka ya dawa muhimu (wauzaji wa rejareja)
AI-assisted research summary: Section title for essential medicines shops (retail sellers).
12. Maduka ya dawa muhimu (wauzaji wa rejareja) - 13 Verify source ↗
Nyumba ya kulala wageni yenye Baa na jiko
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kina kichwa: “Nyumba ya kulala wageni yenye Baa na jiko.”
13. Nyumba ya kulala wageni yenye Baa na jiko - 16 Verify source ↗
Baa pekee
AI-assisted research summary: Section 16 lists “Baa pekee” followed by several monetary amounts.
16. Baa pekee 6,000 30,000 10,000 50,000 15,000 15 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) - 27 Verify source ↗
Wakaanga Chipsi ,Kuku, Ndizi, Mishikaji
AI-assisted research summary: Kichwa cha kifungu kinaorodhesha “Wakaanga Chipsi, Kuku, Ndizi, Mishikaji.”
27. Wakaanga Chipsi ,Kuku, Ndizi, Mishikaji - 30 Verify source ↗
Nyumba za kuishi yenye kaya moja/ familia moja
AI-assisted research summary: This section is titled “Residential houses with one household/family.”
30. Nyumba za kuishi yenye kaya moja/ familia moja - 31 Verify source ↗
Kila kaya/Mpangaji kwenye nyumba ya kuishi yenye
AI-assisted research summary: This section heading refers to each household/tenant in a residential building with tenants.
31. Kila kaya/Mpangaji kwenye nyumba ya kuishi yenye wapangaji - 36 Verify source ↗
Shule za msingi na sekondari
AI-assisted research summary: The provision lists amounts for primary and secondary schools.
36. Shule za msingi na sekondari 20,000 10,000 10,000 10,000 6,000 6,000 10,000 6,000 6,000 10,000 6,000 6,000 6,000 3,000 80,000 40,000 15,000 15,000 80,000 - 37 Verify source ↗
Ofisi za Bima ya magari/Majengo za watu binafsi n.k
AI-assisted research summary: This line lists a fee of 15,000 for “Ofisi za Bima ya magari/Majengo za watu binafsi n.k.”
37. Ofisi za Bima ya magari/Majengo za watu binafsi n.k 15,000 16 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) - 49 Verify source ↗
ATM (ikiwa haiku kwenye tawi la benki husika)
AI-assisted research summary: Sehemu hii inataja ATM iliyoko nje ya tawi la benki husika.
49. ATM (ikiwa haiku kwenye tawi la benki husika) - 52 Verify source ↗
Duka la jumla na Rejareja
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaonyesha kichwa cha ‘Duka la jumla na Rejareja’ na orodha ya namba/fedha, lakini maana ya viwango hivyo haipo wazi katika maandishi yaliyotolewa.
52. Duka la jumla na Rejareja 15,000 20,000 20,000 80,000 80,000 6,000 10,000 10,000 10,000 10,000 6,000 20,000 6,000 6,000 10,000 - 53 Verify source ↗
Wakala wa huduma za kifedha (Tigo,Holotel Mpesa,Airtel
AI-assisted research summary: The section heading refers to financial services agents.
53. Wakala wa huduma za kifedha (Tigo,Holotel Mpesa,Airtel 6,000 n.k) - 55 Verify source ↗
Wakala wa mabasi (Wakatisha tiketi-ofisi)
AI-assisted research summary: Section 55 is titled “Wakala wa mabasi (Wakatisha tiketi-ofisi)”.
55. Wakala wa mabasi (Wakatisha tiketi-ofisi) - 60 Verify source ↗
Section 60
AI-assisted research summary: This line lists amounts for a casino-related item, but the column meanings are not clear from the text.
60. Jumba la kucheza Kamari (Casino) 17 6,000 6,000 6,000 6,000 6,000 50,000 50,000 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) - 61 Verify source ↗
Wachezeshaji Kamari (slot, mashine, Betting)
AI-assisted research summary: This section is titled “Wachezeshaji Kamari (slot, mashine, Betting)”.
61. Wachezeshaji Kamari (slot, mashine, Betting) - 63 Verify source ↗
Duka la kuuza pikipiki, Toyo, Bajaji
AI-assisted research summary: Section title: “Duka la kuuza pikipiki, Toyo, Bajaji.”
63. Duka la kuuza pikipiki, Toyo, Bajaji - 71 Verify source ↗
Vituo vya kulelea watoto (Day care), wanafunzi 1-20
AI-assisted research summary: Section 71 lists amounts for day care centres with 1–20 students.
71. Vituo vya kulelea watoto (Day care), wanafunzi 1-20 10,000 6,000 15,000 6,000 6,000 30,000 10,000 200,000 100,000 20,000 6,000 - 72 Verify source ↗
Vituo vya kulelea watoto (Day care) wanafunzi 21 na
AI-assisted research summary: This section refers to day care centres and mentions the figures 21 and 15,000 onward.
72. Vituo vya kulelea watoto (Day care) wanafunzi 21 na 15,000 kuendelea - 10 Verify source ↗
000
AI-assisted research summary: 10.000 10,000 10,000 6,000 6,000 10,000 10,000 10,000 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea)
10.000 10,000 10,000 6,000 6,000 10,000 10,000 10,000 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) - 83 Verify source ↗
Hostel , watu 21 na kuendelea
AI-assisted research summary: The text mentions hostels with 21 or more people and shows amounts of 10,000 and 15,000, but it does not state the rule clearly.
83. Hostel , watu 21 na kuendelea 10,000 15,000 - 84 Verify source ↗
Duka la pembejeo za kilimo,mifugo, vyakula vya mifugo
AI-assisted research summary: The section is titled “Duka la pembejeo za kilimo, mifugo, vyakula vya mifugo” and includes the figure 10,000.
84. Duka la pembejeo za kilimo,mifugo, vyakula vya mifugo 10,000 - 102 Verify source ↗
Wafanyabiashara sokoni
AI-assisted research summary: Section 102 is headed “Wafanyabiashara sokoni” and includes several listed amounts, but the text shown does not make the rule clear.
102. Wafanyabiashara sokoni 19 6,000 30,000 6,000 6,000 6,000 6,000 15,000 3,000 3,000 6,000 6,000 10,000 6,000 10,000 6,000 6,000 6,000 6,000 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) - 103 Verify source ↗
Uzoaji mwingine ambao haujatajwa
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaweka ada ya kutupa taka/dampo kwa baadhi ya shughuli, ikiwemo viwanda vikubwa kwa Shilingi 50,000 kwa tani moja.
103. Uzoaji mwingine ambao haujatajwa 10,000 SEHEMU B: ADA YA KUTUPA TAKA DAMPO Namba Aina ya Biashara 1 Viwanda vikubwa Ada kwa tani moja (Shilingi) 50,000 JEDWALI LA PILI (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 29) KUFIFILISHA KOSA Mimi…………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwamba la mnamo kukiuka masharti ya kanuni ya ………………………ya Sheria Ndogo ya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ya Mwaka 2024. tarehe……………ya mwezi……………..Mwaka ……………………….nilitenda kosa Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninayodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo Tarehe…ya Mwezi……………Mwaka……. Jina…………………………………..….. Saini…………………………………..…. Mbele ya: Jina……………………………………….. wadhifa……………………………………… Saini……..……………………………….. Tarehe: …………………………………. 20 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Tangazo La Serikali Na. 297 (Linaendelea) Muhuri/Lakari ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufutia azimio liliopitishwa kwenye mkutano wa Halmashauri mnamo tarehe 28 mwezi 2022. Mbele ya ALLY HAMU MACHELE Mkurugenzi wa Halmashauri Halmashauri ya wilaya ya Morogoro PASCAL MWENDISHULE KIHANGA Mstahiki meya Halmashauri ya manispaa ya Morogoro NAKUBALI L.S Dodoma MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) 02 februari, 2024 Waziri wa Nchi -Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa 21
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogoya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in