Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ya Mwaka 2024
This by-law is called the Tabora Municipal Council Service Levy By-Law of 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This by-law is called the Tabora Municipal Council Service Levy By-Law of 2024. This by-law applies throughout the entire area of Tabora Municipal Council. Sehemu hii inaweka maana ya maneno na istilahi mbalimbali zinazotumika kwenye Sheria Ndogo hii. Halmashauri must collect service tax at 0.3% of sales, after VAT and excise duty, from business licence holders who submit sales returns to the Tanzania Revenue Authority; it must collect a rate set in the First Schedule from business licence holders who do not submit sales returns. Mlipa ushuru wa huduma must pay the service tax, file accurate monthly sales information and records, keep books, and provide records/documents for inspection within the stated deadlines.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ya Mwaka 2024
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This by-law is called the Tabora Municipal Council Service Levy By-Law of 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Tabora Municipal Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaweka maana ya maneno na istilahi mbalimbali zinazotumika kwenye Sheria Ndogo hii.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya lengo Tabora; “hesabu” maana yake ni jumla ya mauzo au manunuzi ikiwa ni pamoja na kodi au ada, katika mwaka wa mapato; “hesabu za mwisho” maana yake ni hesabu za mwisho zinazowasilishwa na taasisi yoyote ya kibiashara 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Tangazo La Serikali Na. 323 (Linaendelea) Sura ya 212 Sura ya 212 baada ya kipindi cha hesabu pamoja na nyaraka au maelezo yatakayotakiwa kutolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “jumuisho” maana yake ni taarifa, nyaraka au hesabu au maelezo yoyote yanayohusu kiasi na thamani ya kifedha ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, zilizosambazwa, zilizotolewa au kuuzwa kibiashara ikiwa ni pamoja na jumuisho la awali au la mwisho; “kampuni” maana yake ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “kipindi maalum cha hesabu” maana yake ni muda ambao mfanyabiashara anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara kwa Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “mlipa ushuru wa huduma” maana yake ni kampuni, tawi la leseni kampuni au mfanyabiashara mwenye anayefanya la Halmashauri; zake katika shughuli eneo “mwaka wa mapato” maana yake ni kipindi cha miezi kumi na mbili ya mwaka wa fedha wa serikali; “taasisi ya biashara” maana yake ni taasisi inayofanya biashara, kazi au kutoa huduma kwa lengo la kupata faida; “tawi la kampuni” maana yake ni tawi la kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara yeyote mwenye leseni ya biashara ambaye mauzo yake kwa mwaka ni zaidi ya shilingi milioni nne kutokana na huduma anazopata na kutumia miundombinu ya umma 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Tangazo La Serikali Na. 323 (Linaendelea) Ushuru wa huduma inayomuwezesha kufanya biashara katika eneo la Halmashauri; “wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni au limeteuliwa na Halmashauri kwa lengo la kukusanya ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. shirika ambalo - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must collect service tax at 0.3% of sales, after VAT and excise duty, from business licence holders who submit sales returns to the Tanzania Revenue Authority; it must collect a rate set in the First Schedule from business licence holders who do not submit sales returns.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu ya mauzo baada ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Thamani na ushuru wa bidhaa kutoka kwa mtu yeyote mwenye leseni ya biashara anayewasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza kutoka kwa wafanyabiashara wenye leseni za biashara ambao hawawasilishi hesabu za mauzo Mamlaka ya Mapato Tanzania. Wajibu wa mlipa ushuru wa huduma wa- - 5 Verify source ↗
(1) Mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa huduma must pay the service tax, file accurate monthly sales information and records, keep books, and provide records/documents for inspection within the stated deadlines.
5.-(1) Mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu (a) kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ya kila mwezi iwapo anawasilisha taarifa za hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania; (c) kuwasilisha hesabu sahihi na za kweli; (d) kuwasilisha nyaraka au inayotakiwa kuwasilishwa Halmashauri ndani ya muda uliowekwa; taarifa (e) kutunza kumbukumbu za kitabu cha hesabu; na (f) kuonesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi. 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Tangazo La Serikali Na. 323 (Linaendelea) (2) Mlipa ushuru wa huduma atatakiwa kulipa ushuru ndani ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kuwasilisha taarifa za mauzo ya kila mwezi. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru wa huduma utaratibu wa kulipa ushuru huo. (4) Mlipa kuwasilisha Halmashauri hesabu za mwisho katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa kipindi cha hesabu. atatakiwa ushuru (5) Endapo mlipa ushuru hajawasilisha hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha husika na ametakiwa kufanya hivyo kwa notisi ya siku kumi na nne, Mkurugenzi anaweza kwa kadri atakavyoona inafaa, kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (6) Ushuru uliotathminiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii utalipwa katika kipindi cha siku kumi na nne tangu tarehe ya kufanya tathmini. (7) Endapo mlipa ushuru hajawasilisha majumuisho ya hesabu zake kwa mwaka wowote wa mapato na endapo Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa anafikiri kwamba mlipa ushuru ana wajibu wa kulipa ushuru kwa mwaka husika, anaweza kwa kadri atakavyoona inafaa kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru, isipokuwa tathmini hiyo haitaathiri wajibu wowote wa mlipa ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kwa kushindwa kwake kuwasilisha hesabu hizo. Mamlaka ya Mkurugenzi ushuru wa - 6 Verify source ↗
(1) Endapo mlipa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuwataka walipa ushuru wa huduma kutoa taarifa, hesabu, na kumbukumbu za biashara; pia anaweza kutoa notisi, kuagiza ukaguzi, na kuteua afisa au kamishna kwa ajili ya tathmini na ukusanyaji wa ushuru.
6.-(1) Endapo mlipa huduma anayetakiwa kuwasilisha taarifa ya mauzo chini ya Sheria Ndogo hii atashindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo kwa wakati, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka mlipa ushuru wa huduma kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya kutolewa kwa notisi. 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Tangazo La Serikali Na. 323 (Linaendelea) (2) Mkurugenzi anaweza kumtaka kwa maandishi taarifa kuhusu mfanyabiashara mtu yeyote mwenye anayepaswa kulipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumika kama taarifa sahihi. (3) Mkurugenzi anaweza kumuagiza kwa maandishi Afisa Mwidhiniwa kuingia kwenye jengo au eneo la mlipa ushuru wa huduma kwa nia ya kufanya uchunguzi na tathmini ya kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu na taarifa kwa ajili ya kupata na kujua kiwango sahihi cha ushuru anachotakiwa kulipa. (4) Mkurugenzi anaweza kumteua Kamishna wa Kodi ya Forodha au Kodi ya Mapato kwa ajili ya kutathmini na kukusanya ushuru wa huduma na kuwasilisha Halmashauri kwa lengo la kupata ushuru wa huduma pamoja na madeni yake. (5) Mkurugenzi anaweza, kwa taarifa ya maandishi, kumtaka mlipa ushuru yeyote kuwasilisha hesabu zenye taarifa kamili za shughuli za kibiashara zikionesha thamani ya kiasi na thamani ya kifedha ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, kutolewa, kusambazwa au kuuzwa kibiashara na taarifa ya fedha katika kipindi maalumu kisichozidi siku thelathini tangu tarehe ya taarifa hiyo. siku (6) Mkurugenzi anaweza, kwa taarifa ya maandishi ya saba, kumtaka mlipa ushuru kuwasilisha kumbukumbu za kibiashara na vitabu vya hesabu kwa nia ya kupata taarifa kwa ajili ya kufanyiwa tathmini au kukusanya ushuru wa huduma. Uteuzi wa Wakala - 7 Verify source ↗
(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya Sheria
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri, na wakala aliyeteuliwa lazima akusanye na kupokea ushuru katika eneo alilopangiwa na kuwasilisha makusanyo kwa kuzingatia mkataba wa uwakala.
7.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya Sheria Ndogo hii, Mkurugenzi anaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa- 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Tangazo La Serikali Na. 323 (Linaendelea) (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii; na (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. - 8 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa anaweza
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo au jengo la mlipa ushuru, kuchunguza taarifa na vitabu, kupokea na kukagua hesabu, na kukataa hesabu za mwisho ikiwa ana sababu za msingi kuamini haziko sahihi.
8. Afisa Mwidhiniwa anaweza- (a) kuingia kwenye eneo au jengo lolote la mlipa ushuru kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni kwa ajili ya kutafuta taarifa au kuchunguza hesabu au vitabu au taarifa zozote kama ataona inafaa kwa ajili ya kulipa ushuru wa huduma; (b) kupokea na kukubali hesabu za mlipa ushuru na kuzifanyia tathmini kuhusu kiwango cha hesabu cha mlipa ushuru endapo hesabu hizo zitakuwa si sahihi; na (c) kukataa hesabu za mwisho iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hesabu hizo si sahihi. - 9 Verify source ↗
Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma wa
AI-assisted research summary: Halmashauri inakokotoa ushuru wa huduma kwa mlipa ushuru anayewasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka.
9. Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma wa mlipa ushuru anaewasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka taarifa ya Mapato zinazowasilishwa na mlipa ushuru wa huduma katika kipindi maalum ucha hesabu. kuzingatia Tanzania kwa - 10 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa anatenda kosa iwapo
AI-assisted research summary: Any person commits an offence if they miss required sales information, give false information, fail to pay service levy on time, obstruct officers, damage records or equipment, or otherwise fail to comply with these by-laws.
10. Mtu yeyote atakuwa anatenda kosa iwapo- (a) atashindwa kuwasilisha Halmashauri taarifa sahihi za mauzo ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; 6 Mamlaka ya Afisa Mwidhiniwa Ukokotoaji wa ushuru wa huduma Makosa Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Tangazo La Serikali Na. 323 (Linaendelea) (b) atawasilisha Halmashauri taarifa zisizo sahihi; (c) atashindwa kulipa ushuru wa huduma ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (d) atamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru; (e) atamzuia Afisa Mwidhiniwa au wakala wa Halmashauri kutekeleza masharti ya Sheria Ndogo hii; (f) atatoa taarifa isiyo sahihi kuhusu suala lolote linaloweza kuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa ushuru; (g) ataharibu kwa makusudi taarifa au mfumo wa taarifa; (h) ataharibu kwa makusudi vitendea kazi vya kukusanyia ushuru; au (i) atashidwa kwa namna yoyote kutekeleza Sheria Ndogo hii. Adhabu Kufifilisha kosa - 11 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetenda kosa na kutiwa hatiani
AI-assisted research summary: A person who commits any offence under this subsidiary law and is convicted must pay a fine, serve a prison term, or both.
11. Mtu yeyote atakayetenda kosa na kutiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote kwa pamoja. - 12 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: The Director may compound an offence by charging up to TZS 200,000 if the offender admits the offence voluntarily, is ready to fill the prescribed form, and pays the tax owed.
12. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kinyume cha Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili na kulipa ushuru anaodaiwa. Kufutwa kwa TS. Na. 360 la 2015 - 13 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii inafuta Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This section repeals the 2015 Tabora Municipal Council service charge bylaw.
13. Sheria Ndogo hii inafuta Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Huduma) ya Halmashauri ya Manispaa ya 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Tangazo La Serikali Na. 323 (Linaendelea) Tabora ya Mwaka 2015. _________ JEDWALI LA KWANZA ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(2)) ___________ USHURU WA HUDUMA Namba. Aina ya malipo ya Leseni ya biashara (Shilingi) Kiwango cha Ushuru kwa Mwaka (Shilingi)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: This section includes a confession-and-appeal form and a table of monetary amounts in Tanzanian shillings.
6. 40,000/= hadi 60,000/= 60,001/= hadi 80,000/= 80,001/= hadi 100,000/= 100,001/= hadi 120,000/= 120,001/= hadi 150,000/= 150,001/= na kuendelea 30,000/= 40,000/= 50,000/= 60,000/= 80,000/= 100,000/= ____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 12) _____________ FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi………………………………………………………nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, niko tayari kulipa kiasi cha ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Leo tarehe…………. Saini……………………… Jina……………………………….. 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Tangazo La Serikali Na. 323 (Linaendelea) MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 9 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Tangazo La Serikali Na. 323 (Linaendelea) Lakari ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufutia Azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Halmashauri ya Manispaa ya Tabora uliofanyika tarehe 12 mwezi 05 Mwaka 2023 na kushuhudiwa lakari hiyo ikigongwa mbele ya;- ELIAS MAHWAGO KAYANDABILA Mkurugenzi wa Manispaa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora MHE. RAMADHANI S. KAPELA Mstahiki Meya Halmashauri ya Manispaa Tabora NAKUBALI L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) 20 Februari, 2024 Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 10
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in