AI-assisted research summary: Mwombaji anapewa kibali cha kujenga kituo cha mafuta, lakini lazima ajenge na kuendesha eneo hilo kwa kufuata masharti mengi ya usalama na viwango vya TBS.
3. Mwombaji anapewa Kibali cha Ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Mafuta katika Kiwanja Na. 6, Kitalu “A”, Kijiji cha Maramba, Kata ya Maramba, Wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga, kulingana na masharti yafuatayo: (a) kituo cha mafuta kitajengwa kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Na. TZS 1115:2009 na TZS 1079:2008; (b) uangalifu wa kutosha utazingatiwa wakati wa uchimbaji na uwekaji wa matenki ya mafuta chini ya ardhi; 1 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Kituo cha Mafuta kwa Aida Service Station Limited - Maramba Service Station Tangazo la Serikali Na. 744 (Linaendelea) (c) mpangilio wa kituo cha mafuta utapaswa kukidhi umbali wa kiusalama kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Na. TZS 1079:2008; (d) ufukiaji wa matenki ya kuhifadhi mafuta pamoja na mabomba chini ya ardhi ufanywe kwa namna ambayo italinda usalama wa vifaa hiyo ikiwemo kupata kutu; (e) matenki ya kuhifadhia mafuta, pampu na mabomba husika pamoja na vifaa vyote vinavyounganishwa pamoja navyo vitapaswa kufungwa vizuri ili kuzuia uvujaji wowote wa Mafuta; (f) matenki ya kuhifadhia mafuta na pampu ya Mafuta itafanyiwa uhakiki wa usahihi wa vipimo na Wakala wa Vipimo Tanzania aliyeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Tanzania; Sura ya 340 (g) eneo la mbele la kituo cha mafuta na kuzunguka eneo la pampu litasakafiwa kwa zege madhubuti isiyoweza kupenyeza mafuta na kuhakikisha kuwepo kwa mitaro ambayo itakusanya maji na mafuta wakati wa mvua na kuyaelekeza kwenye chemba ya kutenganisha maji na mafuta; (h) kuweka swichi ya dharura katika eneo linaloonekana na kufikika kirahisi ili iwe rahisi wakati wa dharura kuzima umeme wa kituo kizima; (i) kuhakikisha uwepo na vyoo vya kutosha vya wanawake na wanaume vilivyo safi wakati wote; (j) kuhakikisha usalama zinawekwa sehemu ya kuingia na kutoka kwenye kituo cha mafuta na eneo la pampu zikijumuisha “zima injini”, “zima simu” na “usivute sigara”; alama kuwa za (k) hakikisha kila la kuhifadhia mafuta linaunganishwa na bomba la kupumulia lenye urefu usiopungua mita 3.6 kutoka ardhini. tenki 2 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Kituo cha Mafuta kwa Aida Service Station Limited - Maramba Service Station Tangazo la Serikali Na. 744 (Linaendelea) Bomba hilo linatakiwa kuwa angalau mita 1.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja na angalau mita 4 kutoka kwenye dirisha au kifaa chochote cha kuvuta hewa ikiwemo kiyoyozi; (l) pampu za mafuta na sehemu ya kushushia mafuta zinatakiwa kuwa angalau mita 4.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja, anagalu mita 8 kutoka kutoka kifaa chochote ambacho kinaweza kuwa chanzo cha moto ikiwemo jokofu na angalau mita 10 kutoka kwenye nyaya za kusafirishia umeme; (m) kuhakikisha kila pampu ya mafuta inalindwa na kizuizi na kitakuwa na urefu wa mita 1 kutoka juu ya ardhi; (n) mifumo ya upakuaji wa mafuta kwenye kituo cha mafuta itapaswa kujengwa kwa kufuata kanuni na taratibu zinazokubalika katika sekta ya mafuta; (o) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na paa linalofunika eneo lote lenye pampu za mafuta na linajengwa kwa mujibu wa viwango na taratibu zinazokubalika katika sekta ya mafuta; na (p) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na bango la bei ambalo litawekwa mahala ambapo linaonekana kirahisi ili wateja waweze kuona bei za mafuta kabla ya kuingia kituoni. Ukomo wa kibali cha ujenzi