SHERIA NDOGO YA USHURU WA MAZAO YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA, 2024
This section says the by-law is called the Muheza District Council Produce Cess By-Law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA USHURU WA MAZAO YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA, 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section says the by-law is called the Muheza District Council Produce Cess By-Law, 2024. This bylaw applies throughout the entire area of the Muheza District Council. This section defines key terms used in the by-law, including authorized officer, council, produce, farmer, trader, buyer, director, and produce tax. Halmashauri must charge a 3% produce tax, and the tax is measured by weight rather than sack volume. Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ada au ushuru, na wakala huyo lazima akusanye, apokee, na awasilishe makusanyo na taarifa zinazoelezwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA USHURU WA MAZAO YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA, 2024
Showing 23 of 23
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section says the by-law is called the Muheza District Council Produce Cess By-Law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the entire area of the Muheza District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including authorized officer, council, produce, farmer, trader, buyer, director, and produce tax.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri na Mkurugenzi aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauiri” maana yake ni Halmashauiri ya Wilaya ya Muheza. “mazao” maana yake ni mavuno ya shambani au maliasili au mazao ya baharini yanayozalishwa au yanayoingizwa kwenye soko au ndani ya eneo la mamlaka ya Halmashauri. “mazao ya chakula” maana yake ni mazao yote ya chakula ambayo yatatumika kwa madhumuni ambayo si ya kibiashara; “mazao ya biashara” ni mazao yote ambayo hata kama ni ya chakula lakini yatatumika kwa wakati husika kwa madhumuni ya biashara; 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Tangazo la Serikali Na. 748 (Linaendelea) “mfanyabiashara” - (a) ni mtu yeyote anayeuza bidhaa sokoni au gulioni kwa jumla au rejareja; (b) linapotumika kuhusiana na mkulima maana yake ni mkulima yeyote ambaye anajihusisha na shughuli ya kuuza mazao kama atakavyoyatoa shambani kuyapeleka sokoni; (c) linapotumika kuhusiana mnunuzi ina maana ya mtu yeyote anayejihusisha na shughuli ya kuuza mazao kama atakavyoyanunua kutoka kwa mkulima au mtu yeyote kutoka katika eneo la Halmashauri; (d) linapotumika kuhusiana na mmiliki wa mashamba makubwa ina maana ya mmiliki huyo kutumia mazao hayo kama malighafi katika kiwanda cha mmiliki husika kwa kiwango kilekile alichovuna katika shamba husika; (e) linapotumika kuhusiana na Taasisi ya Umma au Serikali au ya Mtu binafsi au Kampuni ina maana ya Taasisi au Kampuni hiyo inayojihusisha na kilimo cha mazao hayo; “mkulima” maana yake ni mtu yeyote ambaye anajishughulisha na shughuli za kilimo katika eneo la Mamlaka ya Halmashauri; “Mwenyekiti”- (a) linapotumika kuhusiana na Halmashauri ya Wilaya maana yake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya; (b) linapotumika kuhusiana na Kijiji, maana yake ni Mwenyekiti wa Kijiji; (c) linapotumika kuhusiana na Kitongoji, maana yake ni Mwenyekiti wa kitongoji; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mnunuzi” maana yake ni mtu yeyote anayenunua mazao na tafsiri hii itajumuisha mkulima anayefanya biashara ya mazao kutoka shambani kupeleka sokoni; “ushuru” maana yake ni ushuru wa mazao utakaotozwa na 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Tangazo la Serikali Na. 748 (Linaendelea) Utozaji wa ushuru Halmashauri baada au kabla ya kupata huduma. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa mazao kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge a 3% produce tax, and the tax is measured by weight rather than sack volume.
4.-(1) Halmashauri itatoza ushuru wa mazao kwa kiwango cha asilimia tatu ya bei ya kununulia mazao utakaolipwa na mnunuzi wa mazao kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1) na kwa madhumuni ya ukusanyaji wa ushuru kutoka kwa Shirika, Kampuni, Taasisi za Serikali au Taasisi binafsi ambazo zinamiliki mashamba makubwa, Halmashauri itatoza ushuru huo kwa kiwango cha asilimia tatu kwa bei ya kununulia mazao hayo, na kwa utaratibu wa malipo kama utakavyopangwa na Bodi inayosimamia mazao husika kiasi ambacho kitatozwa kutoka kwa Kampuni. (3) Kwa madhumuni ya kurahisisha ukusanyaji wa ushuru, mara baada ya mlipa ushuru kuchukua mazao yake atalazimika kuchukua hati ya kusafirisha mazao kutoka Halmashauri inayothibitisha kiasi cha mazao anachosafirisha ukilinganisha na kile alicholipia ushuru. (4) Bila kuathiri kanuni ndogo za (1), (2) na (3), ushuru wowote utakaotozwa utatozwa kwa kuzingatia uzito na si ujazo wa gunia. Uteuzi wa Wakala - 5 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na Mamlaka ya kuteua
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ada au ushuru, na wakala huyo lazima akusanye, apokee, na awasilishe makusanyo na taarifa zinazoelezwa.
5.-(1) Halmashauri itakuwa na Mamlaka ya kuteua Wakala kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kukusanya ada au ushuru kwa niaba yake. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu- (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri; (c) kuwasilisha makusanyo yote anayowajibika kukusanya kwa kuzingatia mkataba alioingia na Halmashauri; (d) kutoa taarifa kwa Halmashauri kuhusiana na mtu yeyote ambaye kwa makusudi amekataa au 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Tangazo la Serikali Na. 748 (Linaendelea) ameshindwa kulipa ushuru husika; (e) kuwasilisha Halmashauri orodha ya wanunuzi wote aliowakusanya ushuru katika eneo aliloteuliwa kukusanyia ushuru huo (3) Mkusanya ushuru atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii endapo: (a) atashindwa bila sababu ya msingi kuwasilisha kiwango cha fedha alichokusanya kutoka kwa wanunuzi wa mazao; (b) atakuwa anafahamu kiwango kinachostahili kutozwa kutoka kwa mnunuzi na kwa makusudi akakusanya zaidi ya kiwango husika; (c) kwa makusudi akiwasilisha kiwango cha mawasilisho na stakabadhi za malipo na orodha ya wanunuzi aliowaorodhesha; na ukilinganisha pungufu Ushuru wa mazao ya misitu (d) kwa makusudi akishindwa kutekeleza lolote analowajibika kulitekeleza kitendo ambacho kitaathiri mapato hayo. - 6 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa mazao ya
AI-assisted research summary: The council charges a 3% forest products tax on the buyer, based on the purchase or sale price.
6.-(1) Halmashauri itatoza ushuru wa mazao ya misitu kutoka kwa mnunuzi wa mazao ya misitu kwa kiwango cha asilimia tatu ya bei ya kununulia au ya kuuzia mazao hayo. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), mazao ya misitu yatajumuisha mazao ya misitu timbao na mazao ya misitu ambayo si timbao kama inavyoonekana katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (3) Kwa madhumuni ya urahisi wa ukusanyaji wa ushuru wa mazao ya misitu inayomilikiwa na Taasisi ya Umma, Mtu binafsi au Kijiji, muuzaji huyo atawajibika kutoa ushirikiano kwa Halmashauri ili isipoteze ushuru unaopaswa kulipwa na mnunuzi husika; (4) Halmashuri inaweza kumteua kwa maandishi Mtu yeyote katika Taasisi inayohusika na uuzaji wa mazao ya misitu kukusanya ushuru wa mazao ya misitu kwa kiasi na niaba kilichokusanywa kwa Halmashuri. ya Halmashauri kuwasilisha (5) Taasisi inayomiliki mazao ya misitu itakuwa na wajibu wa kutoa taarifa kwa wanunuzi kuwa wanawajibika chini ya Sheria Ndogo hii kulipa ushuru wa 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Tangazo la Serikali Na. 748 (Linaendelea) mazao ya misitu kwa Halmashauri au kutoa taarifa kwa Halmashauri kuwa Taasisi husika inatarajia kuuza mazao ya misitu au kuainisha pamoja na bei watakayomtoza mnunuzi wa mazao ya misitu gharama ya ushuru ambao mnunuzi anawajibika kuwasilisha Halmashauri na kuwasilisha kwa Halmashauri. unaotakiwa ushuru kiasi cha Wajibu wa kutumia vipimo sahihi Sura ya 340 - 7 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabiashara, mkulima au mtu
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara, wakulima, au watu wanaohusika na biashara, ubebaji, au ufungashaji wa mazao lazima watumie vipimo sahihi na kufungasha mazao kwa kuzingatia Sheria ya Vipimo na kanuni za ufungishaji wa bidhaa.
7.-(1) Kila mfanyabiashara, mkulima au mtu yeyote atakayehusika na biashara ya mazao au ubebaji wa mazao atakuwa na wajibu wa kutumia vipimo sahihi katika ubebaji wa mazao hayo. (2) Kila mfanyabiashara, mkulima au mtu yeyote atakayefungasha mazao anawajibika kufungasha mazao kwa kuzingatia Sheria ya Vipimo na kanuni za ufungishaji wa Bidhaa. Eneo la kuuza na kununulia mazao - 8 Verify source ↗
(1) Pale ambapo itatokea umuhimu wa kuuza
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuelekeza mahali pa kuuza mazao, na ni marufuku kuuza mazao yaliyochukuliwa kabla ya kukomaa au katika eneo lisiloelekezwa.
8.-(1) Pale ambapo itatokea umuhimu wa kuuza mazao tofauti na shambani, mazao yote yatauzwa katika maeneo ambayo Halmashauri itaelekeza. (2) Ni marufuku kwa mfanyabiashara, mkulima, au mtu yeyote: (a) kuuza mazao ambayo hayajakomaa, kupepea mazao au kuyachemsha kwa lengo ya kuyakomaza au kufanya jambo lolote ambalo litaathiri ubora wa mazao hayo; au (b) kuuza mazao katika eneo ambalo halijaelekezwa na Halmashauri. (3) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa katika maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya kuuza na kununua mazao ya kilimo kunakuwepo na mzani utakaotumika uliohakikiwa na wakala wa vipimo. - 9 Verify source ↗
(1) Halmashauri itamtoza ushuru mnunuzi wa
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumtoza ushuru mnunuzi wa mazao ikiwa mazao yamepatikana bila ushuru kulipwa.
9.-(1) Halmashauri itamtoza ushuru mnunuzi wa mazao endapo mazao yaliyonunuliwa yatakamatwa kuwa hayajalipiwa ushuru na ikithibitika mnunuzi atatakiwa kulipa ushuru anaodaiwa. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), endapo mnunuzi atashindwa kulipia ushuru anaodaiwa, mazao yake yatakamatwa na kuhifadhiwa kwa masaa kumi na mbili na baada ya muda huo kupita bila ya 5 Adhabu kwa utoroshaji mazao Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Tangazo la Serikali Na. 748 (Linaendelea) mnunuzi kuyakomboa mazao hayo yatauzwa kwa mnada au kugawiwa kwa taasisi za Serikali baada ya kupata kibali cha Mahakama. (3) Fedha zitakazopatikana baada ya mauzo ya mazao yaliyokamatwa na kunadiwa chini ya kanuni ndogo ya (2), Halmashauri itachukua ushuru wake, gharama za utunzaji wa mazao kwa wakati wote mazao yalipokuwa chini ya uangalizi wa Halmashauri pamoja na gharama za mnada na kiasi kitaka chobaki atarudishiwa mnunuzi. - 10 Verify source ↗
Endapo mazao yaliyokamatwa chini ya kanuni
AI-assisted research summary: If seized produce loses value, the Council is not responsible for that loss while the produce is under its care.
10. Endapo mazao yaliyokamatwa chini ya kanuni ya (9) yatapoteza thamani, Halmashauri haitahusika na upotevu wa thamani kwa mazao yaliyokuwa chini ya uangalizi wake. - 11 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote ambaye anawajibika kutoa
AI-assisted research summary: Mtu anayehusika kutoa taarifa za malipo ya ushuru lazima azitoe kwa mamlaka husika; pia mamlaka hizo zinaweza kumuita mtu yeyote kufika mbele yao kwa ajili ya kupata taarifa.
11.-(1) Mtu yeyote ambaye anawajibika kutoa taarifa kuhusiana na malipo ya ushuru anawajibika kutoa taarifa hizo kama alivyotarajiwa kwa Halmashauri, Kijiji, mkusanya ushuru, Wakala au Kamati ya ukasimiaji ushuru iliyoundwa chini ya Sheria kwa madhumuni ya kukasimia kiwango cha ushuru au ukusanyaji ushuru. (2) Kwa madhumuni ya kupata taarifa chini ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri, Kijiji, mkusanya ushuru, Wakala au Kamati ya ukasimiaji ushuru kwa kadiri itakavyokuwa anayehusika na utoaji wa wito huo, inaweza kumuita mtu yeyote kufika mbele yake katika muda na mahali ambapo pametajwa katika barua ya wito. - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayetaka kukusanya ushuru chini ya Sheria Ndogo hii lazima awe na ruhusa ya maandishi kutoka Halmashauri au Kijiji; kukusanya au kujaribu kukusanya ushuru bila ruhusa hiyo, au kwa kiwango ambacho hakijatajwa, ni kosa.
12. Mtu yeyote ambaye: (a) hajaruhusiwa na Halmashauri au Kijiji kwa maandishi kukusanya ushuru unaokusanywa chini ya Sheria Ndogo hii;na (b) amekusanya au amejaribu kukusanya ushuru kwa kiwango ambacho hakijatajwa chini ya Sheria Ndogo hii, anatenda kosa chini ya Ndogo hii. Mazao kupoteza thamani wajibu wa kutoa taarifa Kukusanya ushuru bila ruhusa Makosa kwa kukataa kutoa taarifa - 13 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote ambaye atatakiwa kutoa taarifa
AI-assisted research summary: A person required to provide information under this by-law must not give false information or refuse, without good reason, to provide the required information; a person required to appear before certain local tax bodies must do so.
13.-(1) Mtu yeyote ambaye atatakiwa kutoa taarifa chini ya Sheria Ndogo hii: (a) kwa makusudi akatoa taarifa ya uongo au taarifa ya uongo kwa amejaribu kutoa 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Tangazo la Serikali Na. 748 (Linaendelea) Halmashauri, Kijiji, Wakala, mlipa ushuru au Kamati ya ukasimiaji ushuru, juu ya suala lolote linalohusiana na ukusanyaji ushuru; au (b) amedharau, amekataa au bila ya sababu za msingi ameshindwa kutoa taarifa zinazotakiwa, atakuwa anatenda kosa. (2) Mtu yeyote ambaye ametakiwa kufika mbele ya Halmashauri, Kijiji, mkusanya ushuru, Wakala au Kamati ya ukasimiaji ushuru na hajafanya hivyo, anatenda kosa. Halmashauri kuchukua hatua za kisheria - 14 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufungua
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kufungua shauri la jinai kuhusu malipo ya ushuru au adhabu katika mahakama yenye mamlaka, mradi kufanya hivyo hakutaathiri haki za mtu yeyote au mamlaka nyingine ya kufungua shauri hilo chini ya Sheria Ndogo hii.
14. Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufungua shauri la jinai kuhusiana na malipo ya ushuru au adhabu kwenye Mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, endapo kufanya hivyo hakutaathiri haki ya mtu yeyote au Mamlaka nyingine ya kufungua shauri la jinai chini ya Sheria Ndogo hii. Makosa - 15 Verify source ↗
Mtu yeyote ikiwa ni mnunuzi, muuzaji, wakala
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinasema kwamba mnunuzi, muuzaji, wakala au mkusanya ushuru anatenda kosa akishindwa kutimiza wajibu wa ushuru, akikusanya bila kibali, akitoa taarifa za uongo, akizuia ukusanyaji, au akishindwa kuhifadhi kumbukumbu zinazohitajika.
15. Mtu yeyote ikiwa ni mnunuzi, muuzaji, wakala au mkusanya ushuru anatenda kosa endapo: (a) atashindwa, atadharau, au atakaidi kulipa ushuru chini ya Sheria Ndogo hii; (b) atashindwa, atadharau, au atakaidi kuwasilisha ushuru aliokusanya kwa Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii; (c) atakusanya ushuru bila kuwa na kibali cha kukusanya ushuru; (d) atashindwa, atadharau au atakaidi kuwasilisha taarifa au atatoa taarifa za uongo ambazo zinahitajika kuthibitisha makusanyo ya ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (e) atamshawishi mtu yeyote asilipe ushuru au kumzuia mkusakusanya ushuru kufanya kazi yake; (f) atashindwa kuhifadhi kumbukumbu ikiwa ni pamoja na rejesta ya mazao na mahesabu yanayohitajika chini ya Sheria Ndogo hii; au (g) atadanganya, kuhusiana na kitendo chake hicho kama ataikosesha Halmashauri mapato ilivyokusudiwa. 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Tangazo la Serikali Na. 748 (Linaendelea) Adhabu Kufifilisha kosa - 16 Verify source ↗
Mtu atakayekwenda kinyume na masharti
AI-assisted research summary: A person who acts against the rules in this subsidiary legislation is liable to a fine, imprisonment, or both.
16. Mtu atakayekwenda kinyume na masharti katika Sheria Ndogo hii atatakiwa kulipa faini ya kiasi kisichopungua Shilingi laki mbili na kisichozidi Shilingi Milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza kiasi cha shilingi laki mbili ili kufifilisha kosa, lakini tu kama mkosaji anakiri kwa hiari, anakubali kujaza fomu maalum ya Jedwali la Pili, na analipa ada au ushuru unaodaiwa.
17. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. Kufutwa kwa Sheria Ndogo TS. Na. 299 la 2008 - 18 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya
AI-assisted research summary: This section repeals the Muheza District Council Produce Tax By-Laws of 2010.
18. Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ya Mwaka 2010 inafutwa. ___________________ JEDWALI LA KWANZA __________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(1)) SEHEMU YA I: USHURU WA MAZAO YA CHAKULA NA BIASHARA NAMBA AINA YA MAZAO MAELEZO
Part
SEHEMU YA I:
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: Mazao yaliyoorodheshwa yanatozwa ushuru wa 3% ya bei ya kununulia mazao shambani.
2. Mazao ya chakula Mazao ya biashara Mazao yanayotumika kwa chakula na matunda tu Mazao yanayotumika kwa biashara (karafuu, pilipili chai, manga, mdalasini, na korosho, kokoa, yanayohusiana) KIASI CHA USHURU USHURU (SHILINGI) 3% ya bei ya kununulia mazao shambani 3% ya bei ya kununulia mazao shambani SEHEMU YA II: Ushuru wa Mazao ya Misitu Timbao NAMBA ZAO AINA YA ZAO USHURU 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Tangazo la Serikali Na. 748 (Linaendelea)
Part
SEHEMU YA II:
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This section lists forest-product charges, including a 3% royalty on certain forest products and a 5% charge for non-timber forest products, based on the purchase price.
1. Mbao, mkaa, kuni, nguzo magogo, fito, Zao la msitu timbao Mrahaba wa mapato ya maduhuli ya mazao ya misitu asili ya [leseni/mauzo] 3% ya bei ya kununulia SEHEMU III: USHURU WA MAZAO YA MISITU ISIYO MBAO NAMBA ZAO AINA YA ZAO KIASI CHA USHURU (SHILINGI) Zao la msitu isiyo timbao 5% ya bei ya kununulia
Part
SEHEMU III:
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This text fragment lists several items and introduces Section IV on tax for fishing activities.
1. Uyoga, asali, nta, utomvu, mbenu, ukindu, kamba, madawa ya mitishamba, masambu SEHEMU IV: Ushuru wa Shughuli za Uvuvi NAMBA
Part
SEHEMU IV:
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: This section appears to be a heading about fish-related tax and a fishing licence.
2. ZAO Ushuru wa samaki mnadani Leseni ya uvuvi - 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Ushuru umewekwa kuwa 5% ya bei ya kununua samaki mnadani, kwa kuzingatia viwango vya Serikali Kuu.
3. Leseni ya usajili wa vyombo vya kuvulia samaki KIASI CHA USHURU (SHILINGI) 5% ya bei ya kununua samaki mnadani Kulingana na viwango vilivyotolewa na Serikali Kuu Kulingana na viwango vilivyotolewa na Serikali Kuu _________________ JEDWALI LA PILI _______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 17) FOMU YA KUKIRI NA KUFILILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka ……… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ya Mwaka 2024. 9 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Tangazo la Serikali Na. 748 (Linaendelea) Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………….……………………….. Saini………………………… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 10 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Tangazo la Serikali Na. 748 (Linaendelea) Lakari ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Halmashauri uliofanyika mnamo tarehe 29 mwezi 07 Mwaka 2022 na lakari hiyo ilibandikwa mbele ya;- DR JUMAA MOHAMED MHINA, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya Muheza ERASTO JEROME MHINA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Muheza NAKUBALI, L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA, 25 Machi, 2024 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA USHURU WA MAZAO YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA, 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in