SHERIA NDOGO YA HIFADHI YA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA YA MWAKA 2024
This section gives the by-law its short title.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA HIFADHI YA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA YA MWAKA 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the by-law its short title. This provision says the by-law applies throughout the area of Muheza District Council. This section defines key terms used in the by-law, including the Authorized Officer, toilet, waste container, conservation area, Council, and environmental conservation. The Council must set aside special grazing areas, designate routes for livestock to and from grazing areas or markets, and carry out a livestock census, issue livestock cards, and provide good livestock husbandry education to the community. Mfugaji lazima afuate maelekezo ya Halmashauri kuhusu idadi, njia, malisho, chanjo, usajili na usimamizi wa mifugo.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA HIFADHI YA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA YA MWAKA 2024
Showing 28 of 28
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikama kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the by-law its short title.
1. Sheria Ndogo hii itajulikama kama Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This provision says the by-law applies throughout the area of Muheza District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including the Authorized Officer, toilet, waste container, conservation area, Council, and environmental conservation.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “choo” maana yake ni chumba maalumu ambacho kimejengwa ambacho kitakuwa na shimo pembeni kwa ajili ya kuhifadhia kinyesi au mkojo wa binadamu; “chombo cha taka” maana yake ni chombo cha kuwekea taka kinachoweza chenye mfuniko kuhamishika, unaofunga vizuri na mishikio; “eneo la hifadhi” ni maeneo ya milima, maeneo ya vyanzo vya maji, hifadhi ya misitu, miteremko na maeneo mengine ambayo yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Muheza; “hifadhi ya mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa 1 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) ardhi; mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji vinavyozingatia masharti na maelekezo yatakayotolewa na Afisa Mwidhiniwa chini ya Sheria ya Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote; “kamati”- (a) inapotumika kuhusiana na Halmashauri ya Kijiji au ina maana ya Kamati iliyoteuliwa na Halmashauri ya Kijiji. iliyoanzishwa Sura ya 191 Sura ya 191 Sura ya 323 Sura ya 191 (b) inapotumika kuhusiana na Kamati ya Maendeleo ya Kata ina maana ya Kamati hiyo; na (c) inapotumika kuhusiana na Kamati nyingine ina maana ya Kamati hiyo; “kiwanda” maana yake ni jengo au majengo au eneo ambapo vitu vinatengenezwa; “kuvuna misitu” maana yake ni pamoja na kufyeka, kukata au kung’oa misitu, visiki; “maeneo ya malisho” maana yake ni maeneo yaliyotemgwa kwa ajili ya malisho ya mifugo, pamoja na sehemu zote ambazo zimetengwa na Halmashauri kwa ajili ya malisho; “maji” yatakuwa na maana kama kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi Mazingira; “maji taka” yatakuwa na maana kama yalivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi Mazingira; “mazao ya misitu” yatakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Misitu; “mazingira” yatakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mfugaji” maana yake ni mtu yeyote anaejishughulisha na ufugaji mifugo katika eneo la Halmashauri; “mifugo” maana yake ni mnyama yeyote inayofugwa na binadamu; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “Mwenyekiti”- (a) inapotumika kuhusiana na Halmashauri ya Wilaya maana yake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya. (b) inapotumika kuhusiana na Halmashauri ya Kijiji 2 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) Sura ya 191 Sura ya 191 maana yake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji. (c) inapotumika kuhusiana na kamati, maana yake ni Mwenyekiti wa kamati; “taka” itakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” zitakuwa na maana kama zilivyotafsiwa katika Sheria ya Usimamizi Mazingira; “taka za viwandani” zitakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; na “uchafu hatari” utakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira. Wajibu wa Halmasha uri - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga
AI-assisted research summary: The Council must set aside special grazing areas, designate routes for livestock to and from grazing areas or markets, and carry out a livestock census, issue livestock cards, and provide good livestock husbandry education to the community.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za malisho ndani ya eneo la Halmashauri. (2) Halmashauri itatenga njia maalum ya kupitisha mifugo kwenda na kurudi malishoni au minadani. (3) Halmashauri itafanya sensa ya mifugo na kutoa kadi za mifugo na elimu ya ufugaji bora kwa jamii. Wajibu wa mfugaji - 5 Verify source ↗
Kila mfugaji atakuwa na wajibu ufuatao
AI-assisted research summary: Mfugaji lazima afuate maelekezo ya Halmashauri kuhusu idadi, njia, malisho, chanjo, usajili na usimamizi wa mifugo.
5. Kila mfugaji atakuwa na wajibu ufuatao: (a) kufuga idadi ya mifugo itakayoamriwa na Halmashauri husika; (b) kupitisha mifugo yake katika njia zilizopangwa na kutengwa na Halmashauri; (c) kuwa na kadi ya mifugo itakayoonyesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo; (d) kufuga na kulisha mifugo yake katika maeneo ya malisho yaliyopangwa na Halmashauri; (e) kupeleka mifugo katika majosho kama atakavyoagizwa na Halmashauri; (f) kupeleka mifugo yake katika vituo vya chanjo kama itakavyoamriwa na Halmashauri, na atalipia chanjo hiyo kama atatakiwa kufanya hivyo; (g) kuchangia gharama za ukarabati wa majosho kama sehemu ya mchango wake, pale itakapobidi kufanya gharama kwa na itakayopendekezwa na Halmashauri; hivyo, (h) kuchangia gharama za uboreshaji wa maeneo ya malisho yaliyotengwa na Halmashauri; (i) kuweka alama kwenye mifugo yake na katika 3 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) viungo vya mifugo vinavyopendekezwa kutoharibu zao la ngozi; (j) kuhudhuria mafunzo ufugaji ya kama ili atakavyohitajiwa na Halmashauri; (k) kutokata miti kwa lengo la kufukuza mbung’o; na (l) kusajili mifugo katika rejista ya kijiji, kuogesha ratiba katika majosho kama mifugo itakavyopangwa. Marufuku kwa mfugaji Kudhibiti mifugo inayozurur a ovyo - 6 Verify source ↗
Itakuwa marufuku kwa mfugaji yeyote
AI-assisted research summary: Mfugaji yeyote haruhusiwi kufanya shughuli fulani za mifugo katika maeneo yaliyokatazwa au bila kibali cha Halmashauri.
6. Itakuwa marufuku kwa mfugaji yeyote: (a) kuchunga, kulisha, au kunywesha maji mifugo katika maeneo yote ambayo hayakutengwa kwa ajili hiyo; (b) kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani zaidi ya kilometa thelathini; (c) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo moja hadi lingine bila kibali kutoka Halmashauri; (d) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali kitakachotolewa na Halmashauri; (e) kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo siyo mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoidhinishwa na Halmashauri; na (f) kupitisha mifugo ambayo hayakuidhinishwa na Halmashauri kupitisha mifugo. katika maeneo - 7 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri must impound livestock found roaming in an unauthorized grazing area, charge a fine of TZS 20,000 per animal, and may auction unclaimed livestock after 7 days with court approval.
7.-(1) Halmashauri itakamata mfugo wowote utakaoonekana unazurura katika eneo la Halmashauri ambalo halijaruhusiwa kuchungia mifugo. (2) Mfugo wowote utakaokamatwa mahali pasipostahili utalipiwa faini ya Shilingi elfu ishirini kwa kila mfugo baada ya kulipia gharama hizo mfugaji atarudishiwa mifugo yake. (3) Endapo mwenye mifugo au mfugo hatatokea ndani ya siku saba tangu kukamatwa kwa mifugo hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri atakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mfugo au mifugo hiyo baada ya kupata idhini ya Mahakama. (4) Baada ya mauzo, Mkurugenzi atakata fedha za faini, gharama za mnada na gharama za ulinzi na fedha zitakazobaki atapewa mwenye mifugo. (5) Endapo kutatokea kufa kwa mifugo au mfugo 4 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) Ukaguzi wa mifugo Taratibu za ufugaji Taratibu za kilimo Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama vifo hivyo vitakuwa vimesababishwa na uzembe wa Halmashauri. - 8 Verify source ↗
(1) Maafisa mifugo wa Halmashauri au Afisa
AI-assisted research summary: Maafisa mifugo wa Halmashauri au afisa mwidhiniwa anaweza kuingia kwenye boma au jengo lolote wakati wa saa za kazi ili kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; mtu yeyote asiwazuie.
8.-(1) Maafisa mifugo wa Halmashauri au Afisa Mwidhiniwa atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii ataweza kuingia katika maboma au jengo lolote wakati wa muda wa kazi kwa madhumuni ya kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Mtu yeyote atakayewazuia Maafisa Mifugo au Afisa Mwidhiniwa katika kutekeleza wajibu wao chini ya Sheria Ndogo hii anatenda kosa. - 9 Verify source ↗
(1) Wafugaji wote watatakiwa kuzingatia masharti
AI-assisted research summary: Wafugaji lazima wazingatie masharti ya kufuga, wachinje mifugo kwenye machinjio au sehemu iliyotengwa, na watu hawaruhusiwi kuuza, kununua, au kubadilishana mifugo ndani ya Halmashauri isipokuwa kwenye minada au magulio yaliyotengwa. Mbwa na nguruwe hawapaswi kuachiliwa wazurure; mbwa pia lazima wafungwe katika muda ulioelezwa.
9.-(1) Wafugaji wote watatakiwa kuzingatia masharti ya kufuga kama yalivyo katika Sheria Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote inayohusu utaratibu wa ufuigaji. (2) Kila mfugaji atatakiwa kuchinja mifugo yake machinjioni au mahali palipotengwa kwa ajili ya huduma hiyo. (3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kununua, kuuza au kufanya biashara ya kubadilishana aina yoyote ya mifugo katika eneo lolote la Halmashauri isipokuwa kwenye minada au magulio yaliyotengwa kwa shughuli hiyo. (4) Itakuwa marufuku kwa mbwa na nguruwe kuachiliwa wakizurura, Mbwa watatakiwa kufungiwa kuanzia Saa kumi na mbili kamili asubuhi na kuachiwa Saa nne kamili usiku. - 10 Verify source ↗
(1) Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za kilimo
AI-assisted research summary: An applicant or operator of agricultural activities in the Council must follow the agricultural procedures set out in laws and regulations, and the Agricultural Officer may enter any farm during working hours to inspect and check compliance.
10.-(1) Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za kilimo katika Halmashauri atatakiwa kuzingatia taratibu za kilimo zilizoainishwa kwenye sheria na kanuni mbalimbali. (2) Itakuwa halali kwa Afisa Kilimo kuingia katika shamba lolote wakati wa muda wa kazi kwa madhumuni ya kufanya ukaguzi na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Makatazo - 11 Verify source ↗
Ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kufanya vitendo vilivyotajwa, ikiwemo kulima maeneo hatarishi, kutumia ardhi kinyume na mpango wa kilimo, kuchoma shamba bila kibali maalum, kutupa mabaki ya viuatilifu majini, kumiliki eneo la chanzo cha maji bila ruhusa, kutumia mifuko ya plastiki, kutumia mifuko mbadala isiyoidhinishwa, au kujenga bila kibali cha Halmashauri.
11. Ni marufuku kwa mtu yeyote- (a) kulima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, mabwawa na maziwa au kufanya jambo lolote litakalo haribu hifadhi ya mazingira. (b) kutumia ardhi kinyume na matumizi ya kilimo kama ilivyopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri. 5 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) (c) kusafisha shamba kwa ajili ya kilimo kwa njia ya kuchoma moto isipokuwa kwa kibali maalum kutoka kwa Halmashauri. (d) kutupa mabaki ya vifungashio vya Viuatilifu, kusafisha vipulizi au kumwaga mabaki ya viuatilifu katika vyanzo vya maji yanayotiririka au mito. (e) kumiliki eneo Halmashauri. la chanzo cha maji isipokuwa (f) kutumia mifuko ya plastiki katika eneo lote la Halmashauri na matumizi ya vifungashio vya mifuko ya plastiki kama vibebeo. (g) kutumia mifuko mbadala isiyokidhi viwango na kuwa na alama ya inayooneshwa kuthibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania. (h) kujenga nyumba kiholela au kujenga jengo lolote katika eneo la hifadhi bila kibali cha Halmashauri. - 12 Verify source ↗
Mtu hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Mtu haruhusiwi kuchimba mchanga, kifusi au kuchoma tofali, kujenga, au kufanya shughuli za kiuchumi na uchimbaji katika maeneo yaliyozuiliwa bila ruhusa maalum ya Halmashauri.
12. Mtu hataruhusiwa- (a) kuchimba mchanga, kifusi au kuchoma tofali katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri kama vile katika maeneo ya makazi ya watu, maeneo yaliyohifadhiwa, kando kando ya mito au ndani ya mto, bwawa au ziwa isipokuwa kwa ruhusa maalum ya Halmashauri; (b) kujenga nyumba, jengo lolote au kufanya shughuli zozote za kiuchumi katika eneo la hifadhi; na Uchimbaji mchanga na kokoto (c) kufanya shughuli zinazohusiana na uchimbaji kutoka kibali maalum na bila kuwa Halmashauri. Uhifadhi wa uoto wa asili - 13 Verify source ↗
Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa
AI-assisted research summary: Residents in damaged areas must restore the natural environment by planting trees; the council also has a duty to protect water sources.
13. Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira ya eneo husika yameharibiwa, kuhakikisha wanalirudisha katika hali yake ya kawaida kwa kupanda miti ili kutoendelea kuharibu mazingira na kurejesha uoto katika hali yake ya asili. Wajibu wa Halmasha uri kulinda vyanzo vya maji - 14 Verify source ↗
(1)
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ianzishe, isimamie na ilinde vyanzo vya maji, na pamoja na jamii husika ipande miti isiyonyonya maji kwa maelekezo ya Afisa Misitu.
14.-(1) Halmashauri itawajibika kuanzisha, kusimamia na kulinda vyanzo vya maji. (2) Halmashauri itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayeharibu chanzo cha maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji bila 6 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) Kulinda eneo la hifadhi Uchafuzi wa vyanzo vya maji Kuchoma au kusababish a moto sababu ya msingi. (3) Halmashauri na jamii husika itakuwa ni wajibu wa kupanda miti isiyonyonya maji katika vyanzo vya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Misitu. - 15 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kulima, kukata miti,
AI-assisted research summary: Anyone is prohibited from farming, cutting trees, grazing livestock, or otherwise damaging water sources and the environment within 60 meters of water sources.
15. Mtu yeyote hataruhusiwa kulima, kukata miti, kuchunga mifugo katika umbali wa mita 60 kutoka vyanzo vya maji au kufanya jambo lolote linaloharibu kwa namna yoyote chanzo cha maji na hifadhi ya mazingira. - 16 Verify source ↗
Mtu, kiwanda,
AI-assisted research summary: Mtu, kiwanda, taasisi au shirika lolote haliruhusiwi kuelekeza maji machafu kwenye vyanzo vya maji au kuweka kitu chenye sumu ndani ya maji yanayotumiwa na watu au viumbe hai.
16. Mtu, kiwanda, taasisi au shirika lolote haliruhusiwi- (a) kuelekeza mabomba ya maji machafu kwenye mito, mabwawa, visima, mifereji, ziwa, chemchemi au sehemu yoyote ambayo ni chanzo cha maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama au viumbe vingine vilivyo hai; au (b) kuweka kitu chochote chenye sumu ndani ya maji ambayo yanatumiwa na binadamu au kiumbe chochote hai. - 17 Verify source ↗
(1) Mtu hataruhusiwa kuchoma au kusababisha
AI-assisted research summary: Watu hawaruhusiwi kuwasha au kusababisha moto katika misitu ya eneo la Halmashauri, na wananchi wanapaswa kuzima moto unaoonekana kuwaka katika eneo hilo.
17.-(1) Mtu hataruhusiwa kuchoma au kusababisha moto katika misitu iliyoko eneo la Halmashauri. (2) Kila mwananchi atakuwa na wajibu wa kuzima moto ambao utaonekana kuwaka katika eneo la Halmashauri yenye kuleta viashiria vya hatari. (3) Kila mkazi wa eneo hilo atawajibika kushiriki katika zoezi la kuzima moto huo endapo atatakiwa kufanya hivyo, kama atashindwa kushiriki katika kuzima moto bila sababu ya msingi atakuwa ametenda kosa. Ukataji miti - 18 Verify source ↗
(1) Mtu hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Watu hawaruhusiwi kukata miti katika misitu iliyohifadhiwa kwa matumizi yoyote bila kibali kutoka Halmashauri, au kuvuna miti katika msitu uliohifadhiwa kwa viumbe hai maalum. Afisa Misitu lazima ahakikishe miti inayovunwa imekomaa na inafaa kwa matumizi.
18.-(1) Mtu hataruhusiwa- (a) kukata miti katika maeneo ya misitu iliyofadhiwa kwa ajili ya matumizi ya aina yoyote bila kupata kibali kutoka Halmashauri; na (b) kuvuna miti katika msitu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe hai maalum ambao ni rasilimali kwa Taifa. (2) Afisa Misitu atahakikisha miti inayovunwa imekomaa na inafaa kwa ajili ya matumizi. (3) Watu wanaovuna miti kwa ajili ya kuchoma mkaa 7 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) watatakiwa kuwa na eneo maalum Halmashauri kwa ajili ya kuchoma mkaa. lililoidhinishwa na Wajibu wa kupanda miti Utupaji wa taka ngumu na laini Uendeshaj i wa viwanda, vituo vya mafuta, huduma za ujenzi - 19 Verify source ↗
Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika
AI-assisted research summary: Kila mkazi wa Halmashauri lazima apande na kutunza miti katika eneo lake, makazi yake, na mashamba anayomiliki; eneo lake pia linaweza kuongozwa na Halmashauri.
19. Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika- (a) kupanda na kutunza miti katika eneo lake kama atakavyoelekezwa na Halmashauri; (b) kupanda na kutunza miti katika makazi yake; na (c) kupanda na kutunza miti katika shamba au mashamba anayomiliki; - 20 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatenga eneo kwa ajili ya kutupa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupa taka na kusimamia usafi; watu na baadhi ya maeneo lazima wahifadhi taka vizuri na wasitupe taka au uchafu ovyo.
20.-(1) Halmashauri itatenga eneo kwa ajili ya kutupa taka ngumu na laini na kusimamia kwa karibu usafi katika eneo husika. (2) Mtu atakayetupa ovyo taka ngumu au laini, au kujisaidia katika kingo za mabwawa au kwenye vyanzo vya maji vilivyoko katika Halmashauri atakuwa anatenda kosa. (3) Taka zote katika eneo la Halmashauri zitatupwa katika eneo maalum au lililotengwa au litakalotengwa na Halmashauri kwa ajili hiyo na Halmashauri itawajibika kusimamia usafi katika eneo lake. jalala kuu (4) Kila Kaya, eneo la biashara, ofisi, Karakana na vyombo vya usafiri wa abiria lazima viwe na chombo cha kuhifadhia taka ndani ya eneo la mji na katika maeneo ya vijijini lazima yawe na mashimo ya taka nyuma ya nyumba. (5) Kila mtu anawajibu wa kuwa na choo salama, na kwa misingi hiyo si ruhusa kwa mtu kujisaidia haja ndogo au kubwa, au kumwaga mkojo, kinyesi au matapishi katika mtaa, eneo la jamii, uchochoroni, njiani, barabarani, sehemu yoyote au katika eneo lolote isipokuwa katika choo na kwa kuzingatia usafi wa choo hicho. - 21 Verify source ↗
(1) Mtu anayeendesha shughuli za karakana,
AI-assisted research summary: Operators of listed workshop and industrial activities in residential areas must follow building procedures and environmental precautions; violating these rules is an offence.
21.-(1) Mtu anayeendesha shughuli za karakana, mashine ya kusaga, kuranda mbao, kukamua maji ya matunda, kuchomelea vyuma au kuendesha shughuli yoyote inayozalisha uchafu ambao unaleta athari kwa binadamu na viumbe wengine katika maeneo ya makazi ya watu atatakiwa kuzingatia taratibu za ujenzi. (2) Endapo mtu atataka kuendesha shughuli za viwanda, vituo vya mafuta, vituo vya huduma mbalimbali za ujenzi atatakiwa kuzingatia tahadhari ya athari za mazingira. (3) Mtu yeyote akienda kinyume na kanuni ndogo ya (1) na (2) atakuwa anatenda kosa. 8 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) Jukumu la kaya kuvuna maji ya mvua Uhifadhi wa korongo Wajibu wa kuweka miundomb inu ya kuvuna maji kwenye mchoro - 22 Verify source ↗
(1) Kila kaya itakuwa na jukumu la kuweka
AI-assisted research summary: Households must set up rainwater harvesting during the rainy season, and certain institutions must install rooftop rainwater-harvesting structures. Landowners are entitled to build and store rainwater for home use.
22.-(1) Kila kaya itakuwa na jukumu la kuweka utaratibu wa kuvuna maji ya mvua wakati wa kipindi cha mvua ili kukabiliana na ukame wakati wa kipindi cha kiangazi. (2) Kaya hizo zitaandaa mpango wa uvunaji maji hayo katika hali ya usafi kwa kuzingatia afya ya mtumiaji na jamii kwa ujumla. (3) Kila Taasisi, Shule za Msingi, Sekondari, Zahanati na Vituo vya Afya vitakuwa na wajibu wa kuweka miundo mbinu ya kuvuna maji ya mvua kwenye mapaa ya majengo yao kwa faida ya kutumia maji kwa jamii. (4) Mmiliki wa ardhi yoyote atakuwa na haki ya kujenga miundo mbinu ya uvunaji wa maji ya mvua na kuhifadhi maji hayo kwa matumizi ya nyumbani. (5) Hakutakuwa na miundombinu ya kuvuna maji ya mvua ambayo itakuwa na uwezo zaidi ya uwezo wa kanuni zilizotolewa na mamlaka husika. - 23 Verify source ↗
Kila mwananchi atakuwa na jukumu la kuhifadhi
AI-assisted research summary: Kila mwananchi lazima ahifadhi makorongo yanayopitisha maji wakati wa mvua na aache mita 60 kutoka kila upande wa kingo zake wakati korongo hilo linaelekeza maji kwenye bwawa kwa matumizi ya binadamu, kilimo, na mifugo.
23. Kila mwananchi atakuwa na jukumu la kuhifadhi makorongo yote yanayopitisha maji katika msimu wa mvua, na kuyalinda kwa kuacha mita 60 kutoka kila upande wa kingo ya korongo ili mradi liwe linapeleka maji kwenye bwawa kwa matumizi ya binadamu, kilimo na mifugo. - 24 Verify source ↗
(1) Kila mwenye ardhi anayetaka kujenga nyumba
AI-assisted research summary: Mwenye ardhi anayetaka kujenga nyumba au jengo la biashara au makazi lazima aonyeshe miundombinu ya kuvuna maji ya mvua kwenye michoro yake.
24.-(1) Kila mwenye ardhi anayetaka kujenga nyumba au jengo la biashara au makazi ni lazima katika michoro yake abainishe na kuonyesha miundombinu ya kuvuna maji ya mvua. (2) Usanifu, uratibu na usimamizi utazingatia miongozo, kanuni na viwango vilivyopendekezwa au vilivyoainishwa na Serikali kupitia miongozo mbalimbali. (3) Mchoro ambao hautaonyesha na kubainisha miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua utakuwa ni batili na hautopitishwa na Halmashauri kwa ajili ya ujenzi hadi hapo utakapoonyesha na kubainisha miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua. (4) Wakati wowote Halmashauri kupitia Idara ya Ujenzi na ikiihusisha Idara ya Maji itafanya ukaguzi kuhakikisha kuwa nyumba zote zilizojengwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, zinajengwa na miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua na miundombinu hiyo inatumika baada ya 9 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) ukamilikaji wake. Makosa - 25 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Anyone is prohibited from carrying out the listed livestock, environmental, waste, fire, forestry, water, plastic bag, and waste-container acts without the required permission or in prohibited places.
25. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo: (a) ataingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (b) atasafirisha mifugo bila kuwa na kibali; (c) atalisha mifugo katika maeneo yasiyoruhusiwa; (d) atafuga mifugo zaidi ya idadi iliyoruhusiwa; (e) atakiuka masharti ya kilimo, kuchimba mchanga, katika maeneo mawe yasiyoruhusiwa na Halmashauri; kokoto, madini (f) ataharibu vyanzo vya maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji; (g) atachoma au kushiriki katika kuanzisha moto au, hatashiriki katika shughuli ya kuzima moto bila ya sababu ya msingi; (h) atavuna mazao ya misitu katika misitu iliyohifadhiwa au isiyohifadhiwa bila kibali; (i) atachoma mkaa na kukata kuni bila kibali; (j) atafyeka nyasi, kung’oa vichaka, na kung’oa visiki katika misitu bila kibali; (k) atatupa ovyo taka ngumu au laini katika maeneo yoyote yasiyoruhusiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; (l) atajisaidia haja kubwa au ndogo sehemu isiyo kuwa chooni au atatupa uchafu wa aina hiyo mahali pasipostahili au mahali ambapo siyo chooni; (m) atatiririsha maji machafu yanayoweza kuleta madhara kwa binadamu na viumbe vingine hai; (n) ataendesha shughuli za kiwanda au viwanda vidogo, karakana, kituo cha kuoshea magari, mashine za kusaga na kukoboa nafaka mashine za kuranda mbao katika makazi ya watu bila kuzingatia taratibu za mipango miji; (o) atachafua maji yaliyohifadhiwa kwa matumizi ya baadae na kusababisha madhara kwa watu, mifugo, mazao, bustani na mazingira ambayo yanamwagiliwa na maji hayo au kwa njia yoyote ile ambayo italeta uharibifu na uchafuzi kwa kutumia maji; 10 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) (p) mkuu wa taasisi au kaya zitakazoshindwa kuweka utaratibu wa kuvuna maji ya mvua watakuwa wamevunja taratibu zilizoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (q) atamzuia kwa namna yoyote ile mtumishi wa Halmashauri kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (r) atauza, atanunua, atasambaza au kutumia mifuko ya palastiki; na (s) ataendesha kaya, ofisi, eneo la biashara, karakana ambayo haina chombo cha kuhifadhia taka katika eneo la mji. - 26 Verify source ↗
Mtu anayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: A person who breaches this by-law is liable to a fine, imprisonment of up to 12 months, or both.
26. Mtu anayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au vyote. - 27 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtenda kosa shilingi 50,000 ikiwa anakiri kosa na yuko tayari kujaza fomu maalum ya Jedwali la Kwanza.
27. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. - 28 Verify source ↗
Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira na Vyanzo
AI-assisted research summary: Hii sehemu inafuta Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira na Vyanzo vya Maji za Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.
28. Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira na Vyanzo vya Maji za Halmashauri ya Wilaya ya Muheza zinafutwa. Adhabu Kufifilisha kosa Kufutwa kwa Sheria Ndogo T.S Na. 121 la 2012 11 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) __________ JEDWALI __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 27) FOMU YA KUKIRI NA KUFILILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka ……… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ya Mwaka, 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………….……………………….. Saini………………………… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe………………………… 12 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tangazo la Serikali Na. 750 (Linaendelea) Lakari ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Halmashauri uliofanyika mnamo tarehe 29 mwezi 07 Mwaka 2022 na lakari hiyo ilibandikwa mbele ya;- DR JUMAA MOHAMED MHINA, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya Muheza ERASTO JEROME MHINA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Muheza NAKUBALI, / L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA, 25 Machi, 2024 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 13
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA HIFADHI YA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA YA MWAKA 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in