Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
This section gives the short title of the bylaw.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the bylaw. This bylaw applies throughout the entire area of Namtumbo District Council. This section defines key terms used in the by-law, including the authorized officer, protected areas, the council, environmental protection, factory, forest harvesting, grazing areas, water, forest products, environment, livestock keeper, director, forest, waste, solid waste, industrial waste, and hazardous waste. Halmashauri lazima itenge maeneo ya malisho, iandae njia maalum za kupitisha mifugo, na ifanye sensa ya mifugo pamoja na kutoa kadi za mifugo na elimu ya ufugaji bora. Kila mfugaji ana wajibu wa kufuata masharti ya Halmashauri kuhusu ufugaji wa mifugo yake, pamoja na usajili, malisho, chanjo, majosho, na ulinzi wa miti.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
Showing 28 of 28
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikama kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the bylaw.
1. Sheria Ndogo hii itajulikama kama Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the entire area of Namtumbo District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including the authorized officer, protected areas, the council, environmental protection, factory, forest harvesting, grazing areas, water, forest products, environment, livestock keeper, director, forest, waste, solid waste, industrial waste, and hazardous waste.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha unahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “eneo la hifadhi” ni maeneo ya milima, maeneo ya vyanzo vya maji, hifadhi ya misitu, miteremko na maeneo mengine ambayo yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo; “uhifadhi wa mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi; mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji kwa kuzingatia masharti na maelekezo yatakayotolewa na Afisa Mwidhiniwa chini ya Sheria ya Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote; “kiwanda” maana yake ni jengo, majengo au eneo ambapo vitu vinatengenezwa; 1 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) Sura ya 191 Sura ya 323 Sura ya 191 Sura ya 323 Sura ya 191 “kuvuna misitu” inajumuisha kufyeka, kukata au kung’oa misitu au visiki; “maeneo ya malisho” maana yake ni maeneo yaliyotemgwa kwa ajili ya malisho ya mifugo, pamoja na sehemu zote ambazo zimetengwa na Halmashauri kwa ajili ya malisho; “maji” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mazao ya misitu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Misitu; “mazingira” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mfugaji” maana yake ni mtu yeyote anayejishughulisha na ufugaji wa mifugo katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “misitu” maana yake ni eneo la ardhi ambalo limefunikwa angalau kwa asilimia 10 ya miti, uoto wa asili au iliyopandwa, au asilimia 50 au zaidi ya vichaka na miti inayoota upya ambayo itajumuisha aina yote ya misitu ya hifadhi ambayo itatangazwa chini ya Sheria ya Misitu na mazao yote ya misitu ikijumuisha majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri; “taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi Mazingira; “taka za viwandani” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; na “uchafu hatari” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; Wajibu wa Halmasha uri - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge maeneo ya malisho, iandae njia maalum za kupitisha mifugo, na ifanye sensa ya mifugo pamoja na kutoa kadi za mifugo na elimu ya ufugaji bora.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za malisho ndani ya eneo la Halmashauri. (2) Halmashauri itatenga njia maalum ya kupitisha mifugo kwenda na kurudi malishoni au minadani. (3) Halmashauri itafanya sensa ya mifugo na kutoa 2 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) kadi za mifugo na elimu ya ufugaji bora kwa jamii. Wajibu wa mfugaji - 5 Verify source ↗
Kila mfugaji atakuwa na wajibu ufuatao
AI-assisted research summary: Kila mfugaji ana wajibu wa kufuata masharti ya Halmashauri kuhusu ufugaji wa mifugo yake, pamoja na usajili, malisho, chanjo, majosho, na ulinzi wa miti.
5. Kila mfugaji atakuwa na wajibu ufuatao: (a) kufuga mifugo kuzingatia kwa idadi itakayoamriwa na Halmashauri; (b) kupitisha mifugo yake katika njia zilizopangwa na kutengwa na Halmashauri; (c) kuwa na kadi ya mifugo itakayoonesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo; (d) kufuga na kulisha mifugo yake katika maeneo ya malisho yaliyopangwa na Halmashauri; (e) kupeleka mifugo katika majosho kama atakavyoagizwa na Halmashauri; (f) kupeleka mifugo yake katika vituo vya chanjo kama itakavyoamriwa na Halmashauri, na atalipia chanjo hiyo kama atatakiwa kufanya hivyo; (g) kuchangia gharama za ukarabati wa majosho kama sehemu ya mchango wake, pale itakapobidi gharama kwa na kufanya itakayopendekezwa na Halmashauri; hivyo, (h) kuchangia gharama za uboreshaji wa maeneo ya malisho yaliyotengwa na Halmashauri; (i) kuweka alama kwenye mifugo yake na katika viungo vya mifugo vinavyopendekezwa ili kutoharibu zao la ngozi; (j) kuhudhuria mafunzo ufugaji kama ya atakavyohitajiwa na Halmashauri; (k) kutokata miti kwa lengo la kufukuza mbung’o; na (l) kusajili mifugo katika rejista ya kijiji, kuogesha ratiba katika majosho kama mifugo itakavyopangwa. Marufuku kwa mfugaji - 6 Verify source ↗
Itakuwa marufuku kwa mfugaji yeyote
AI-assisted research summary: Mfugaji yeyote haruhusiwi kuchunga, kulisha, kunywesha, kusafirisha, kuhamisha, kuingiza, kuuza, kununua, au kupitisha mifugo nje ya maeneo au vibali vilivyoidhinishwa na Halmashauri.
6. Itakuwa marufuku kwa mfugaji yeyote: (a) kuchunga, kulisha, au kunywesha maji mifugo katika maeneo yote ambayo hayakutengwa kwa ajili hiyo; (b) kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani zaidi ya kilometa thelathini; (c) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo moja hadi lingine bila kibali kutoka Halmashauri; 3 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) (d) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali kitakachotolewa na Halmashauri; (e) kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo siyo mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoidhinishwa na Halmashauri; na (f) kupitisha mifugo ambayo hayakuidhinishwa na Halmashauri kupitisha mifugo. katika maeneo Kudhibiti mifugo inayozurur a ovyo - 7 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri must seize livestock found roaming in areas not allowed for grazing.
7.-(1) Halmashauri itakamata mfugo wowote utakaoonekana unazurura katika eneo la Halmashauri ambalo halijaruhusiwa kuchungia mifugo. (2) Endapo mfugo uliokamatwa hautachukuliwa na mmiliki ndani ya siku saba tangu kukamatwa kwa mfugo huo, Mkurugenzi wa Halmashauri atakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mfugo au mifugo hiyo baada ya kupata idhini ya Mahakama. (3) Mfugaji wa mifugo yoyote itakayokamatwa chini ya kanuni ndogo ya (1) atalipa faini kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza na baada ya kulipia gharama hizo mfugaji atarudishiwa mfugo wake. (4) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), baada ya mauzo, Mkurugenzi atakata fedha za faini, gharama za mnada na gharama za ulinzi na fedha zitakazobaki atapewa mwenye mifugo. (5) Endapo kutatokea kufa kwa mifugo au mfugo, Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama vifo hivyo vitakuwa vimesababishwa na uzembe wa Halmashauri. Ukaguzi wa mifugo - 8 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakayeteuliwa kusimamia
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa aliyeteuliwa anaweza kuingia katika boma au jengo wakati wa kazi ili kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; kumzuia afisa huyo ni kosa.
8.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii anaweza kuingia katika boma au jengo lolote wakati wa muda wa kazi kwa madhumuni ya kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Mtu yeyote atakayemzuia Afisa Mwidhiniwa katika kutekeleza wajibu wao chini ya Sheria Ndogo hii anatenda kosa. Taratibu za ufugaji - 9 Verify source ↗
(1) Wafugaji wote watatakiwa kuzingatia masharti
AI-assisted research summary: Wafugaji lazima wazingatie masharti ya kufuga; walete mifugo kwenye machinjio, wasiichinje mahali pengine bila taarifa kwa Afisa Mwidhiniwa, na wafugaji hawaruhusiwi kufanya biashara ya mifugo nje ya minada au magulio yaliyotengwa. Pia, mbwa lazima afungwe mchana na afunguliwe usiku kuanzia saa nne, kisha afungwe tena saa kumi na mbili asubuhi.
9.-(1) Wafugaji wote watatakiwa kuzingatia masharti ya kufuga kama yalivyo katika Sheria Ndogo hii au Sheria 4 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) nyingine yoyote inayohusu utaratibu wa ufuigaji. (2) Kila mfugaji atatakiwa kupeleka mfugo au mifugo yake machinjioni au mahali huduma hiyo inapopatikana na itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchinja mfugo au mifugo mahali pengine popote ambapo sio machinjio isipokuwa kwa kutoa taarifa kwa Afisa Mwidhiniwa na atalazimika kulipia gharama za machinjio kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. (3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kununua, kuuza au kufanya biashara ya kubadilishana aina yoyote ya mifugo katika eneo lolote la Halmashauri isipokuwa kwenye minada au magulio yaliyotengwa kwa shughuli hiyo. (4) Mfugaji atawajibika kumfungia mbwa wakati wote wa mchana na atamfungulia kuanzia saa nne kamili usiku na kumfungia saa kumi na mbili asubuhi. - 10 Verify source ↗
(1) Mtu anayetaka kuendesha shughuli za kilimo
AI-assisted research summary: A person who wants to carry out agricultural activities in the Halmashauri must follow the agricultural procedures set out in laws and regulations.
10.-(1) Mtu anayetaka kuendesha shughuli za kilimo katika Halmashauri atatakiwa kuzingatia taratibu za kilimo zilizoainishwa katika sheria na kanuni mbalimbali. (2) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika shamba lolote kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kwa madhumuni ya kufanya ukaguzi na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Taratibu za kilimo Makatazo - 11 Verify source ↗
Ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mtu yeyote hapaswi kulima au kufanya shughuli zinazoathiri maeneo ya hifadhi ya mazingira na vyanzo vya maji, kutumia ardhi kinyume cha matumizi ya kilimo yaliyoidhinishwa, kuchoma moto kusafisha shamba bila kibali maalum, kumwaga mabaki ya viuatilifu kwenye maji yanayotiririka au mito, au kumiliki eneo la chanzo cha maji.
11. Ni marufuku kwa mtu yeyote- (a) kulima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, mabwawa na maziwa au kufanya jambo lolote litakalo haribu hifadhi ya mazingira; (b) kutumia ardhi kinyume na matumizi ya kilimo kama ilivyopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri; (c) kusafisha shamba kwa ajili ya kilimo kwa njia ya kuchoma moto isipokuwa kwa kibali maalum kutoka kwa Halmashauri; (d) kutupa mabaki ya vifungashio vya viuatilifu, kusafisha vipulizi au kumwaga mabaki ya viuatilifu katika vyanzo vya maji yanayotiririka au mito; au (e) kumiliki eneo la chanzo cha maji. Uhifadhi wa uoto - 12 Verify source ↗
Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa
AI-assisted research summary: Wakazi wa eneo lililoharibiwa lazima warejeshe uoto au mazingira kwa kupanda miti.
12. Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira ya eneo husika yameharibiwa, kuhakikisha 5 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) wa asili wanalirudisha katika hali yake ya kawaida kwa kupanda miti ili kutoendelea kuharibu mazingira na kurejesha uoto katika hali yake ya asili. Uchimbaji mchanga na kokoto - 13 Verify source ↗
Mtu hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Watu hawaruhusiwi kuchimba mchanga, kifusi au kuchoma tofali katika maeneo yaliyokatazwa, kujenga au kufanya shughuli za kiuchumi katika eneo la hifadhi, au kufanya shughuli za uchimbaji bila kibali maalum na bila kuwa Halmashauri. Halmashauri pia ina wajibu wa kulinda vyanzo vya maji na eneo la hifadhi.
13. Mtu hataruhusiwa- (a) kuchimba mchanga, kifusi au kuchoma tofali katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri kama vile katika maeneo ya makazi ya watu, maeneo yaliyohifadhiwa, kando kando ya mito au ndani ya mto, bwawa au ziwa isipokuwa kwa ruhusa maalum ya Halmashauri; (b) kujenga nyumba au jengo lolote au kufanya shughuli zozote za kiuchumi katika eneo la hifadhi; na (c) kufanya shughuli zinazohusiana na uchimbaji kutoka kibali maalum na bila kuwa Halmashauri. Wajibu wa Halmasha uri kulinda vyanzo vya maji Kulinda eneo la hifadhi Uchafuzi wa vyanzo vya maji - 14 Verify source ↗
Section 14
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ianzishe, isimamie na ilinde vyanzo vya maji, ichukue hatua kali za kisheria dhidi ya waharibifu au wasioshiriki uhifadhi bila sababu ya msingi, na pamoja na jamii husika ipande miti isiyonyonya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Misitu.
14.- (1) Halmashauri itawajibika kuanzisha, kusimamia na kulinda vyanzo vya maji. (2) Halmashauri itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayeharibu chanzo cha maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji bila sababu ya msingi. (3) Halmashauri na jamii husika itakuwa na wajibu wa kupanda miti isiyonyonya maji katika vyanzo vya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Misitu. - 15 Verify source ↗
Mtu hataruhusiwa kulima, kukata miti, kuchunga
AI-assisted research summary: Mtu haruhusiwi kulima, kukata miti, kuchunga mifugo, au kufanya vitendo vinavyoharibu chanzo cha maji na hifadhi ya mazingira ndani ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji.
15. Mtu hataruhusiwa kulima, kukata miti, kuchunga mifugo katika umbali wa Mita Sitini kutoka vyanzo vya maji au kufanya jambo lolote linaloharibu kwa namna yoyote chanzo cha maji na hifadhi ya mazingira. - 16 Verify source ↗
Mtu, kiwanda,
AI-assisted research summary: Mtu, kiwanda, taasisi au shirika lolote halitaruhusiwa kuelekeza maji machafu kwenye vyanzo vya maji au kuweka kitu chenye sumu kwenye maji yanayotumiwa na watu au viumbe hai.
16. Mtu, kiwanda, taasisi au shirika lolote halitaruhusiwa- (a) kuelekeza mabomba ya maji machafu kwenye visima, mifereji, ziwa, mito, mabwawa, chemchemi au sehemu yoyote ambayo ni chanzo cha maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama au viumbe vingine vilivyo hai; au 6 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) (b) kuweka kitu chochote chenye sumu ndani ya maji ambayo yanatumiwa na binadamu au kiumbe hai chochote. Kuchoma au kusababish a moto - 17 Verify source ↗
(1) Mtu hataruhusiwa kuchoma au kusababisha
AI-assisted research summary: Mtu haruhusiwi kuchoma au kusababisha moto katika misitu ya eneo la Halmashauri; wananchi lazima wazime moto unaoonekana kuwaka na wakazi wanaweza kuhitajika kushiriki kuzima moto.
17.-(1) Mtu hataruhusiwa kuchoma au kusababisha moto katika misitu iliyoko eneo la Halmashauri. (2) Kila mwananchi atakuwa na wajibu wa kuzima moto ambao utaonekana kuwaka katika eneo la Halmashauri yenye kuleta viashiria vya hatari. (3) Kila mkazi wa eneo hilo atawajibika kushiriki katika zoezi la kuzima moto huo endapo atatakiwa kufanya hivyo, kama atashindwa kushiriki katika kuzima moto bila sababu ya msingi atakuwa anatenda kosa. Taarifa ya kuchoma moto - 18 Verify source ↗
Mtu aliyepata
AI-assisted research summary: A person who has permission to burn fire must give nearby neighbors two days’ notice before burning and take steps to stop the fire spreading to other areas.
18. Mtu aliyepata ruhusa ya kuchoma moto atalazimika kutoa taarifa ya siku mbili kabla ya kuchoma moto kwa majirani walioko katika eneo analotaka kuchoma na ataweka njia za kuzuia moto kusambaa maeneo mengine. Ukataji miti - 19 Verify source ↗
(1) Mtu hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Kanuni hii inakataza kukata au kuvuna miti katika maeneo fulani ya misitu bila ruhusa, na inaweka wajibu kwa Afisa Misitu kuhakikisha miti iliyovunwa imekomaa na inafaa matumizi.
19.-(1) Mtu hataruhusiwa- (a) kukata miti katika maeneo ya misitu iliyofadhiwa kwa ajili ya matumizi ya aina yoyote bila kupata kibali kutoka Halmashauri; na (b) kuvuna miti katika msitu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe hai maalum ambao ni rasilimali kwa taifa. (2) Afisa Misitu atahakikisha miti inayovunwa imekomaa na inafaa kwa ajili ya matumizi. (3) Watu wanaovuna miti kwa ajili ya kuchoma mkaa lililoidhinishwa na watatakiwa kuwa na eneo maalum Halmashauri kwa ajili ya kuchoma mkaa. Wajibu wa kupanda miti - 20 Verify source ↗
Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika kupanda
AI-assisted research summary: Residents of the Council must plant and care for trees in their area when directed by the Council.
20. Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika kupanda na kutunza miti katika eneo lake kama atakavyoelekezwa na Halmashauri. Uhifadhi wa korongo - 21 Verify source ↗
Kila mwananchi atakuwa na jukumu la kuhifadhi
AI-assisted research summary: Kila mwananchi lazima ahifadhi makorongo yanayopitisha maji wakati wa mvua, na aache mita 60 kutoka kila upande ili kuyalinda.
21. Kila mwananchi atakuwa na jukumu la kuhifadhi makorongo yote yanayopitisha maji katika msimu wa mvua, na kuyalinda kwa kuacha mita 60 kutoka kila upande wa 7 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) Wajibu wa Halmasha uri ya Kijiji kingo ya korongo ili mradi liwe linapeleka maji kwenye bwawa kwa matumizi ya binadamu, kilimo na mifugo. - 22 Verify source ↗
Kwa madhumuni ya utekelezaji wa Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: Kila kijiji lazima kitekeleze hatua za kuhifadhi misitu na kupanda miti, ikiwemo kutenga eneo la hifadhi, kusimamia upandaji wa miti, na kulinda maeneo ya vilima na ya taasisi.
22. Kwa madhumuni ya utekelezaji wa Sheria Ndogo hii, kila Kijiji kitapaswa- (a) kutenga eneo la hifadhi ya msitu wa asili kwa ajili ya matumizi ya baadaye; (b) kutunza miti yote inayopandwa katika eneo la kijiji; (c) kusimamia kila kaya kupanda miti katika maeneo yao kila mwaka; (d) kupanda na kumiliki shamba la miti lenye ukubwa wa ekari mbili kila mwaka na kulitunza; (e) kuhakikisha kila taasisii ndani ya Halmashauri inapanda miti ya kukinga upepo kuzunguka majengo yake na kuwa na shamba lisilopungua miti hekta mbili; (f) kutunza na kuhifadhi miti na nyasi kwenye milima, ili kuzuia makorongo na vyanzo vya maji mmomonyoko wa udongo; (g) kuhakikisha kuwa kila anayeandaa shamba kwa ajili ya kilimo hatumii moto bila kibali na anapanda miti kwenye mipaka ya shamba lake kama kinga upepo; (h) kuhahakikisha kuwa kila Mwenyekiti wa Kitongoji, Mtendaji wa Kijiji, mkuu wa taasisi yoyote wilayani ana msitu wa hifadhi ya miti ya kupandwa au ya asili kwa madhumuni ya kuhifadhi ardhi na mazingira; na (i) kuhakikisha kuwa maeneo yote ya vilima na yenye vipara ambayo yanamilikiwa na watu binafsi au Serikali ya Kijiji yanapandwa miti. Utupaji wa taka ngumu na laini - 23 Verify source ↗
(1) Halmashauri ina wajibu wa kutenga eneo kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupa taka ngumu au laini na kusimamia usafi; kila mtu lazima ahakikishe taka laini zinatupwa katika maeneo yaliyotengwa na Halmashauri.
23.-(1) Halmashauri ina wajibu wa kutenga eneo kwa ajili ya kutupa taka ngumu au laini na kusimamia kwa karibu usafi katika eneo lake. (2) Ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha kuwa taka laini zinatupwa katika maeneo ambayo ngumu na yametengwa na Halmashauri kwa ajili hiyo. Makosa - 24 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa anatenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akifanya mojawapo ya vitendo vilivyoorodheshwa, kama kuingiza au kusafirisha mifugo bila kibali, kutupa taka ovyo, kuchafua maji, au kutumia mifuko ya plastiki.
24. Mtu yeyote atakuwa anatenda kosa endapo- (a) ataingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila 8 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) kibali; (b) atasafirisha mifugo bila kuwa na kibali; (c) atalisha mifugo katika maeneo yasiyoruhusiwa; (d) atafuga mifugo zaidi ya idadi iliyoruhusiwa; (e) atakiuka masharti ya kilimo, kuchimba mchanga, katika maeneo kokoto, madini mawe yasiyoruhusiwa na Halmashauri; (f) ataharibu vyanzo vya maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji; (g) atachoma au kushiriki katika kuanzisha moto au hatashiriki katika shughuli ya kuzima moto bila ya sababu ya msingi; (h) atavuna mazao ya misitu katika misitu iliyohifadhiwa au isiyohifadhiwa bila kibali; (i) atachoma mkaa na kukata kuni bila kibali; (j) atafyeka nyasi, kung’oa vichaka au kung’oa visiki katika misitu bila kibali; (k) atatupa ovyo taka ngumu au laini katika maeneo yoyote yasiyoruhusiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote; (l) atajisaidia haja kubwa au ndogo sehemu isiyo kuwa chooni au atatupa uchafu wa aina hiyo mahali pasipostahili au mahali ambapo siyo chooni; (m) atatiririsha maji machafu yanayoweza kuleta madhara kwa binadamu na viumbe vingine hai; (n) ataendesha shughuli za kiwanda au viwanda vidogo, karakana, kituo cha kuoshea magari, mashine za kusaga na kukoboa nafaka mashine za kuranda mbao katika makazi ya watu bila kuzingatia taratibu za mipango miji; (o) atachafua maji yaliyohifadhiwa kwa matumizi ya baadae na kusababisha madhara kwa watu, mifugo, mazao, bustani na mazingira ambayo yanamwagiliwa na maji hayo au kwa njia yoyote ile ambayo italeta uharibifu na uchafuzi kwa kutumia maji; (p) atavua samaki kwa kutumia sumu au nyavu zenye matundu madogo au kokoro; (q) atamzuia kwa namna yoyote ile mtumishi wa 9 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) Halmashauri kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (r) atauza, atanunua, atasambaza au kutumia mifuko ya palastiki; au (s) ataendesha kaya, ofisi, eneo la biashara au karakana ambayo haina choo au chombo cha kuhifadhia taka katika eneo la mji. Adhabu - 25 Verify source ↗
Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa chini
AI-assisted research summary: A person convicted of an offence under this subsidiary legislation faces a fine, imprisonment of up to 12 months, or both.
25. Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au vyote kwa pamoja. Kufifilisha kosa - 26 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kutoza hadi shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa na yuko tayari kujaza fomu maalum ya Jedwali la Pili.
26. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kinyume na Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Pili. - 27 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya
AI-assisted research summary: This section repeals the Namatumbo District Council environmental bylaw and refers to the repeal of T.S. No. 270 of 2008.
27. Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namatumbo inafutwa. Kufutwa kwa T.S Na. 270 la 2008 10 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA KWANZA _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 7(3)) FAINI NA GHARAMA YA ULINZI WA WANYAMA WATAKAOKAMATWA KATIKA MAENEO YASIYORUHUSIWA Namba Aina ya mnyama Kiwango cha faini kwa siku (Shilingi)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaonyesha ada/gharama za fedha kwa aina mbalimbali za wanyama, pamoja na gharama ya ulinzi kwa kila mnyama.
5. Ng’ombe/Punda Mbuzi/Kondoo Nguruwe Mnyama mwingine yeyote 50,000/= kwa ng’ombe/punda mmoja 20,000/= kwa mbuzi/kondoo mmoja 10,000/= kwa nguruwe mmoja 5,000/= kwa mnyama mmoja Gharama za ulinzi kwa mnyama yeyote 10,000/= kwa kila mnyama 11 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) ____________ JEDWALI LA PILI ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 26) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA nakiri KWA HIARI YANGU Mimi ……………………………………………………… MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, niko tayari kulipa kiasi cha shilingi ............................ kama faini ya ufifilishaji kosa badala ya kushtakiwa mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Leo tarehe…………. Saini……………………… Jina……………………………….. MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 12 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo la Serikali Na.790 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ulioitishwa na kufanyika tarehe 10/6/2022 na kushuhudiwa na lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- CHIRIKU HAMISI CHILUMBA, Mkurugenzi mtendaji, Halmashauri ya wilaya, Namtumbo JUMA ALFAN PANDU, Mwenyekiti Halmashauri ya wilaya, Namtumbo NAKUBALI, L.S Dodoma, 31 Januari, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB.), Waziri wa Nchi-OR-Tamisemi, 13
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in