Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ya Mwaka 2024
This section gives the title of the by-law: Kasulu District Council By-law on preventing and controlling sumukuvu, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the title of the by-law: Kasulu District Council By-law on preventing and controlling sumukuvu, 2024. This bylaw applies throughout the area of the Kasulu District Council authority. This section defines key terms used in the by-law. Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na inaweza pia kufanya ukaguzi wa mashamba, vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, viwanda na maeneo ya usindikaji. Anyone intending to cultivate must follow proper field-preparation practices, prepare the field on time, and must not prepare it by burning.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ya Mwaka 2024
Showing 17 of 17
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the title of the by-law: Kasulu District Council By-law on preventing and controlling sumukuvu, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the area of the Kasulu District Council authority.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha unahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri aliyeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu; “kanuni bora za kilimo” maana yake ni uandaaji wa shamba kwa usahihi, upandaji mbegu bora kwa wakati na kwa nafasi sahihi, upaliliaji, utumiaji mbolea kwa usahihi, udhibiti wa wadudu na wanyama waharibifu, uvunaji na hifadhi sahihi ya mazao; “kilimo” maana yake ni shughuli ya uzalishaji wa mazao; “mkulima” maana yake ni mtu, taasisi, kampuni au kikundi cha watu anayejihusisha na shughuli za kilimo; “mfanyabiashara’’ maana yake ni taasisi, kampuni, kikundi cha watu au mtu binafsi anayejihusisha na shughuli za kuuza au kununua mazao ya kilimo; 1 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Tangazo la Serikali Na.791 (Linaendelea.) “Mkurugenzi” Maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “sumukuvu” maana yake ni sumu zinazozalishwa na kuvu wanao ota kwenye mazao; “viashiria vya sumukuvu” maana yake ni dalili zinazoonyesha uwepo wa sumukuvu kwenye mazao; na “viuatilifu” maana yake ni sumu ya kuua au kuzuia wadudu waharibifu wa mazao. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuratibu
AI-assisted research summary: Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na inaweza pia kufanya ukaguzi wa mashamba, vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, viwanda na maeneo ya usindikaji.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo la Halmashauri kwa lengo la kuzuia na kudhibiti sumukuvu. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufanya ukaguzi katika mashamba, vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, kiwanda au eneo la usindikaji kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Uratibu na usimamizi wa shughuli za kilimo na udhibiti wa sumukuvu Uandaaji wa shamba - 5 Verify source ↗
Mtu yeyote anayekusudia kulima atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone intending to cultivate must follow proper field-preparation practices, prepare the field on time, and must not prepare it by burning.
5. Mtu yeyote anayekusudia kulima atapaswa kuzingatia misingi ifuatayo- (a) kuzingatia njia sahihi za uandaaji wa shamba; (b) kutayarisha shamba kwa wakati; na (c) kutotayarisha shamba kwa kuchoma moto. Upandaji wa mazao - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone planting crops must follow proper planting methods, including using good seed, planting when the planting rains begin, and spacing plants correctly.
6. Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa kuzingatia njia sahihi za upandaji ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbegu bora; (b) kupanda mara mvua za kupandia zinapoanza kunyesha; na (c) kupanda kwa nafasi sahihi. Utunzaji wa mazao shambani - 7 Verify source ↗
Mtu yeyote aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza
AI-assisted research summary: Mtu aliyepanda mazao lazima ayatunza kwa njia sahihi, ikiwemo kutumia mbolea, kupalilia kwa wakati, na kudhibiti magonjwa, wadudu na wanyama waharibifu.
7. Mtu yeyote aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza kwa kuzingatia njia sahihi za utunzaji wa mazao ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbolea; 2 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Tangazo la Serikali Na.791 (Linaendelea.) (b) kupalilia kwa wakati; na (c) kudhibiti magonjwa, wadudu na wanyama waharibifu. Uvunaji wa mazao - 8 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa kuvuna
AI-assisted research summary: Anyone harvesting crops must do so using good harvesting practices.
8. Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa kuvuna kwa kuzingatia kanuni bora za uvunaji ikiwa ni pamoja na- (a) kuvuna mara baada ya mazao kukomaa au kukauka; (b) kusafisha mazao na kuyahifadhi vizuri; na (c) kusafisha shamba baada ya kuvuna. Ukaushaji wa mazao - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Anyone who harvests crops must dry them properly right after harvesting.
9. Mtu yeyote atakayevuna mazao anapaswa kuyakausha kwa kutumia njia sahihi mara tu baada ya kuvuna ikiwa ni pamoja na- (a) njia za asili zisizoruhusu kuvu kuota; (b) kutumia maturubai, mikeka na vichanja vinavyozuia uchafuzi wa mazao; na (c) kukausha kwa njia yoyote sahihi itakayoelekezwa na mtaalam. Uhifadhi wa mazao - 10 Verify source ↗
(1) Mtu mwenye mazao atawajibika kuhifadhi
AI-assisted research summary: Mtu mwenye mazao lazima ayahifadhi kwa njia sahihi za kiasili au za kisasa zinazozuia kuota kwa kuvu.
10.-(1) Mtu mwenye mazao atawajibika kuhifadhi mazao kwa kutumia njia sahihi za kiasili au za kisasa ambazo zitazuia kuota kwa kuvu. (2) Njia sahihi za kutumika kuhifadhi mazao ni pamoja na kuhifadhi kwenye- (a) mifuko isiyopitisha hewa; (b) magunia ya kawaida kwa ajili ya mazao yaliyowekwa viuatilifu; (c) kihenge na kichanja bora cha asili; (d) silo au pipa maalum; (e) ghala bora lililo safi; (f) kitu kingine kadri itakavyoshauriwa na wataalamu. Wajibu wa Halmashauri - 11 Verify source ↗
Katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: Halmashauri must carry out several implementation duties under this by-law, including education, safe crop storage, farm records, training centres, storage facilities, and market points.
11. Katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hii, Halmashauri itakuwa na wajibu ufuatao: (a) kuhamasisha na kutoa elimu ya uzalishaji na usimamizi wa mazao; (b) kuhamasisha uhifadhi wa mazao katika eneo salama ili kuepuka uchafuzi wa sumukuvu; 3 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Tangazo la Serikali Na.791 (Linaendelea.) (c) kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo; (d) kutunza kumbukumbu za mashamba yote ya mazao ya kilimo katika Kata na Vijiji ili kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; (e) kuanzisha na kuendeleza mashamba darasa na vituo maalum kwa ajili ya kutolea mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu; (f) kuanzisha na kuhamasisha wakulima na wadau wengine kujenga sehemu za kuhifadhia mazao; na (g) kuandaa uwepo wa vituo maalum vya kuuza na kununua mazao. Wajibu wa mkulima - 12 Verify source ↗
Kila mkulima atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila mkulima lazima afanye kilimo kwa kufuata kanuni bora, atoe taarifa kwa Halmashauri kuhusu dalili za kuvu katika mazao, na ashiriki mafunzo ya Halmashauri na kutumia ujuzi unaopatikana.
12. Kila mkulima atakuwa na wajibu wa- (a) kufanya shughuli za kilimo kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na usimamizi wa mazao kabla na baada ya kuvuna; (b) kutoa taarifa kwa Halmashauri kuhusu uwepo wa dalili za kuvu katika mazao; na (c) kushiriki mafunzo ya na Halmashauri na kudhibiti kutekeleza ujuzi uliopatikana kwenye mafunzo hayo. yaliyoandaliwa sumukuvu Wajibu wa msafirishaji Wajibu wa mfanyabiash ara - 13 Verify source ↗
Mtu yeyote anayesafirisha mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Anayesafirisha mazao lazima ahakikishe vifungashio na vifaa vinabaki vikavu na haviruhusu maji, unyevu, au vumbi kuingia.
13. Mtu yeyote anayesafirisha mazao anapaswa kuhakikisha vifungashio na vifaa anavyotumia kusafirisha mazao ni vikavu na visivyoruhusu maji, unyevu na vumbi kuingia ndani ili kuepusha kuvu kuota kwenye mazao. - 14 Verify source ↗
Mfanyabiashara wa mazao ana wajibu wa
AI-assisted research summary: Mfanyabiashara wa mazao lazima ahakikishe ananunua, anahifadhi au kuuza mazao yasiyo na viashiria vya sumukuvu.
14. Mfanyabiashara wa mazao ana wajibu wa kuhakikisha ananunua, anahifadhi au kuuza mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama inanyoonekana katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. Wajibu wa msindikaji - 15 Verify source ↗
Msindikaji atakuwa na wajibu wa kusindika
AI-assisted research summary: Msindikaji must process crops that do not show signs of sumukuvu, as described in the first schedule referenced by the provision.
15. Msindikaji atakuwa na wajibu wa kusindika mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama inanyoonekana katika Jedwali la Kwanza la Sheria 4 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Tangazo la Serikali Na.791 (Linaendelea.) Ndogo hii. Makosa na adhabu - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Any person who mishandles crops in the listed ways commits an offence and, if convicted, may be fined, imprisoned for up to 12 months, or both.
16. Mtu yeyote ambaye- (a) hatavuna kwa wakati mara baada ya mazao kukomaa; (b) anachelewa kuondoa mazao shambani baada ya kuvuna bila kuwa na sababu ya msingi; (c) anaanika kwenye udongo, vumbi au mchanga; (d) anakausha mazao katika mazingira yanayoweza kusababisha sumukuvu; (e) anatumia viuatilifu vilivyozuiliwa kwenye mazao; (f) anauza mazao yenye viashiria vya sumukuvu; (g) anasafirisha mazao kwa njia zitakazosababisha mazingira ya kuvu kuota; au (h) anatumia mazao yenye viashiria vya sumukuvu wakati wa usindikaji, anatenda kosa na endapo atapatikana na hatia atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kutumikia kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au adhabu zote kwa pamoja. Kufifilisha kosa - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyekiuka Sheria Ndogo hii faini isiyozidi shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari kwenye fomu maalum ya Jedwali la Pili.
17. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kinyume na Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa fomu maalum kwa hiari na kuwa iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. tayari kujaza 5 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Tangazo la Serikali Na.791 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA KWANZA ___________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 14 na 15) VIASHIRIA VYA SUMUKUVU Namba AINA YA MAZAO Mahindi HALI YA UNYEVU AU KUVU Punje kuwa na unyevu MWONEKANO WA PUNJE Punje kuwa na ukungu au kuvu - rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo Punje kuwa na ukungu au kuvu – rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo 1 2 Karanga Punje kuwa na unyevu 6 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Tangazo la Serikali Na.791 (Linaendelea.) ____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 17) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi ………………………………………………..………………. Nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya…………………………………….…ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kwamba mnamo tarehe…………ya Mwezi….......... Mwaka ……………. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya ………. ya Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ya Mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Niko tayari kulipa kiasi cha shilingi………......…… kama faini ya ufifilishaji wa kosa nililotenda chini ya Sheria Ndogo za Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ya Mwaka 2024. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe………..ya Mwezi……………………Mwaka………………….. Jina………………………………..…………….Saini………………………. MBELE YA: Jina……………………………………………….….. Wadhifa………………………..…………………….….. Saini…………………………………………………… Tarehe…………………………………………………. 7 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Tangazo la Serikali Na.791 (Linaendelea.) Mhuri wa Halmashauri umewekwa katika Sheria Ndogo hizi kwa kuzingatia Azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Halmashauri uliofanyika tarehe 11/11/2022 mbele ya:- JOSEPH KASHUSHULA RWIZA, Mkurugenzi mtendaji, Halmashauri ya wilaya, Kasulu ELIYA CHARLES KAGOMA, Mwenyekiti, Ha;lmashauri ya wilaya, Kasulu L.S NAKUBALI, Dodoma, 31 Januari, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB.), Waziri wa Nchi-OR-Tamisemi, 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in