Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote za Mwaka 2024
This section gives the title and indicates the start of the part on registration of health insurance schemes.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the title and indicates the start of the part on registration of health insurance schemes. Kifungu hiki kinaorodhesha mada za usajili wa skimu za bima ya afya na taratibu zinazohusiana nazo. Kifungu hiki kina kichwa cha majukumu ya mamlaka ya utambuzi chini ya Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote. This section is about a fund’s management and financing health services for people who are unable to pay or otherwise lack capacity. Sehemu hii inaonyesha mada za usimamizi na udhibiti wa huduma za bima ya afya, kanzidata ya vituo vya kutolea huduma za afya, ukaguzi wa skimu za bima ya afya, na usajili wa wanachama.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote za Mwaka 2024
Showing 78 of 78
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: This section gives the title and indicates the start of the part on registration of health insurance schemes.
2. Jina. Tafsiri. SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI SEHEMU YA PILI USAJILI WA SKIMU ZA BIMA YA AFYA
Part
SEHEMU YA PILI
- 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaorodhesha mada za usajili wa skimu za bima ya afya na taratibu zinazohusiana nazo.
12. Maombi na vigezo vya usajili. Maamuzi kuhusu maombi ya usajili. Usajili na cheti cha usajili. Kukataa usajili. Kuhuisha usajili. usajili wa skimu zilizoruhusiwa kuendelea kutoa huduma. Utaratibu kabla ya kufutwa kwa skimu ya bima ya afya. Kuomba kufutiwa usajili. Taarifa ya kufutwa kwa usajili wa skimu ya bima ya afya. Rejesta ya skimu za bima za afya. SEHEMU YA TATU UTAMBUZI NA USAJILI WA WATU WASIO NA UWEZO - 3 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayekusudia kutoa huduma za
AI-assisted research summary: An applicant intending to provide private health insurance services must submit a registration application to Mamlaka using Form No. I.
3.-(1) Mtu yeyote anayekusudia kutoa huduma za bima ya afya kama skimu ya bima ya afya binafsi atawasilisha kwa Mamlaka maombi ya usajili katika Fomu Na. I iliyobainishwa katika Jedwali la Kanuni hizi. (2) Maombi chini ya kanuni ndogo ya (1) yataambatishwa na- (a) nakala ya cheti cha usajili wa kampuni; (b) uthibitisho wa maazimio ya bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya kuanzisha skimu ya bima ya afya; (c) tathmini ya awali ya mpango wa uendeshaji wa skimu ya bima ya afya; (d) taarifa kuhusu maeneo ya kijiografia ambayo kampuni inakusudia kutoa huduma za bima ya afya; (e) taarifa binafsi za mtendaji mkuu wa kampuni; (f) uthibitisho wa malipo ya kodi kwa Serikali; (g) uthibitisho wa mtaji wa skimu ya bima ya afya kwa mujibu wa Kanuni za Bima za Mwaka 2009; T.S Na. 372 la 2009 (h) uthibitisho wa sifa za wakurugenzi na kama kwenye miongozo menejimenti ya zitakavyobainishwa itakayotolewa na Mamlaka; kampuni (i) uthibitisho wa malipo ya ada ya usajili na ada inayotolewa kwa mujibu wa ya mwaka kifungu cha 158 cha Sheria ya Bima; na (j) taarifa nyingine muhimu kwaajili ya usajili ambayo Mamlaka inaweza kuhitaji. Maamuzi kuhusu maombi ya usajili - 4 Verify source ↗
(1) Mamlaka itapaswa, kwa maombi ya usajili
AI-assisted research summary: Mamlaka must process complete registration applications and decide within 30 days; if an application is incomplete, it may ask the applicant to fix it or provide missing information, and it may extend investigation for up to 90 days with written notice.
4.-(1) Mamlaka itapaswa, kwa maombi ya usajili yaliyotimiza vigezo vya maombi, kufanyia kazi maombi ya usajili na kutoa maamuzi, ndani ya siku thelathini tangu kupokea maombi hayo. 5 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote (2) Endapo Mamlaka imepokea maombi ambayo hayajatimiza vigezo vya maombi, inaweza, kabla ya kutoa uamuzi kuhusu maombi hayo, kumtaka mwombaji, ndani ya kipindi kisichozidi siku thelathini- (a) kuwasilisha nyaraka au taarifa zilizokosekana; au (b) kurekebisha makosa hayo ili kukidhi vigezo vya usajili. (3) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (1), endapo Mamlaka itahitaji kufanya uchunguzi zaidi wa maombi yaliyowasilishwa, inaweza kufanya hivyo ndani ya siku tisini tangu tarehe ya kupokea maombi. (4) Mamlaka itakuwa na wajibu wa kumjulisha kwa maandishi mwombaji kuhusu muda wa nyongeza wa uchunguzi. - 5 Verify source ↗
(1) Mamlaka, baada ya kujiridhisha kuwa
AI-assisted research summary: Mamlaka must register a health insurance scheme and issue a registration certificate once the applicant meets all registration criteria.
5.-(1) Mamlaka, baada ya kujiridhisha kuwa muombaji amekidhi vigezo vyote vya usajili, itasajili skimu ya bima ya afya na kutoa cheti cha usajili. (2) Cheti cha usajili kitakachotolewa chini ya kanuni ndogo ya (1) kitakuwa kama kilivyoainishwa kwenye Kanuni za Bima za Mwaka 2009. (3) Cheti cha usajili kilichotolewa chini ya Kanuni hizi kitakuwa halali kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu tarehe ya kutolewa kwake. (4) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (3), Mamlaka inaweza kutoa cheti cha usajili kwa skimu ya bima ya afya kwa kipindi kisichozidi miaka mitano kwa kuzingatia tathmini ya uendelevu wa skimu husika. (5) Endapo Mamlaka itabaini kuwa skimu ya bima ya afya inashindwa kuwa na uhimilivu kulingana na uhai wa cheti cha usajili, inaweza kupunguza muda wa uhai wa cheti cha usajili kukidhi kipindi cha uhimilivu. Usajili na cheti cha usajili T.S Na. 372 la 2009 Kukataa usajili - 6 Verify source ↗
(1) Mamlaka inaweza kukataa maombi ya
AI-assisted research summary: Mamlaka inaweza kukataa maombi ya usajili wa skimu ya bima ya afya ikiwa mwombaji hajakidhi vigezo vya usajili au vigezo vya kanuni ya 4(2).
6.-(1) Mamlaka inaweza kukataa maombi ya usajili wa skimu ya bima ya afya iwapo muombaji- (a) ameshindwa kukidhi vigezo vya usajili chini ya kanuni hizi; au (b) ameshindwa kutimiza vigezo chini ya kanuni ya 4(2). 6 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote (2) Endapo Mamlaka itakataa kusajili skimu ya bima ya afya, itamjulisha mwombaji kwa maandishi sababu za uamuzi kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya - 7 Verify source ↗
(1) Skimu ya bima ya afya, ndani ya kipindi
AI-assisted research summary: A health insurance scheme must apply to renew its registration before expiry and, in some cases, every year, using the specified form; it must also pay the annual fee if it meets the criteria.
7.-(1) Skimu ya bima ya afya, ndani ya kipindi cha siku thelathini kabla ya cheti cha usajili kufikia ukomo, itawasilisha maombi ya kuhuisha usajili: Isipokuwa kwamba- (a) kwa kadri itakavyohitajika, skimu ya bima ya afya inaweza kupatiwa cheti kipya baada ya Mamlaka kuhuisha usajili; na (b) skimu ya bima ya afya haitakuwa na wajibu wa kuomba upya usajili kwa mujibu wa kanuni ya 3. (2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (1), skimu ya bima ya afya yenye cheti cha usajili cha ukomo wa zaidi ya mwaka mmoja itatakiwa kuwasilisha maombi ya kuhuisha usajili kila mwaka. (3) Skimu ya bima ya afya inayokusudia kuomba kuhuisha usajili itawasilisha maombi kwa Mamlaka kupitia Fomu Na. 2 iliyobainishwa kwenye Jedwali la Kanuni hizi. (4) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Mamlaka inaweza kuongeza muda wa kuhuisha usajili kwa kuzingatia miongozo itakayoitoa. (5) Mamlaka inaweza kukataa maombi ya kuhuisha usajili endapo- (a) skimu ya bima ya afya inatakiwa kufutiwa usajili kwa mujibu wa Sheria na Kanuni hizi; au (b) skimu ya bima ya afya haijakidhi vigezo kuhusu uhitaji wa mtaji kwa mujibu wa Kanuni za Bima za mwaka 2009. (6) Skimu ya bima ya afya itakayokidhi vigezo kwa mujibu wa kanuni hii itatakiwa kulipa ada ya mwaka. T.S Na. 372 la 2009 usajili wa skimu zilizoruhusiwa kuendelea kutoa - 8 Verify source ↗
(1) Mamlaka itazitaka skimu ya bima ya afya
AI-assisted research summary: Mamlaka inaweza kuwataka skimu za bima ya afya za umma na binafsi kuwasilisha taarifa kwa ajili ya cheti cha usajili na kumbukumbu za usajili.
8.-(1) Mamlaka itazitaka skimu ya bima ya afya ya umma na binafsi zinazotambulika hivyo kwa mujibu 7 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote huduma Utaratibu kabla ya kufutwa kwa skimu ya bima ya afya wa kifungu cha 8 na 9(2) cha Sheria, kuwasilisha taarifa mbalimbali zilizorejewa katika kanuni ya 3(2) kwa madhumuni ya kutolewa kwa cheti cha usajili na hifadhi ya kumbukumbu za usajili. (2) Skimu za bima ya afya zilizorejewa chini ya kanuni ndogo ya (1) zitaendelea kuwahudumia wanachama na wanufaika kwa kuzingatia mikataba ya awali hadi itakapofikia ukomo wake, na baada ya hapo utaratibu wa usajili wa wanachama chini ya Kanuni hizi utazingatiwa. (3) Isipokuwa kwa masharti ya kanuni ya 4, 5 na 6 ya Kanuni hizi, skimu zilizoruhusiwa kuendelea kutoa huduma zinapaswa kuzingatia masharti mengine ya usajili ikiwemo masharti kuhusu ulipaji wa ada ya usajili na ada ya mwaka. - 9 Verify source ↗
(1) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 12
AI-assisted research summary: A health insurance scheme’s deregistration notice is treated as received if delivered to the registered address; an objecting scheme may make a written representation within 90 days, and the Authority must decide it before cancelling registration.
9.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 12 cha Sheria, notisi ya kusudio la kufuta skimu ya bima ya afya itathibitika kuwa imepokelewa na skimu ya bima ya afya iwapo imewasilishwa kupitia anuani ya makazi ya kampuni au taasisi iliyotolewa wakati wa usajili wa skimu ya bima ya afya. (2) Skimu ya bima ya afya isiyoridhishwa na kusudio la kufutiwa usajili inaweza, ndani ya siku tisini za notisi, kutoa uwakilishi wake wa maandishi kwa Mamlaka, na Mamlaka itatoa maamuzi ya uwakilishi huo kabla ya kufuta usajili. (3) Katika kulinda maslahi ya wanachama wa skimu ya bima ya afya inayokusudiwa kufutiwa usajili, Mamlaka inaweza kuchukua hatua yoyote kama ilivyoainishwa katika kanuni ya 47 kabla ya kufuta usajili, na skimu ya bima ya afya itakuwa na wajibu wa kuzingatia amri au maelekezo yatokanayo na hatua ya Mamlaka. Kuomba kufutiwa usajili - 10 Verify source ↗
(1) Pale ambapo skimu ya bima ya afya
AI-assisted research summary: A health insurance scheme that wants to cancel its registration must give the Authority 90 days’ notice before stopping services and explain why. The Authority may require supporting information, then decide whether to accept or رفض the application within 90 days.
10.-(1) Pale ambapo skimu ya bima ya afya inakusudia kuomba kufutiwa usajili, itatoa kwa Mamlaka notisi ya siku tisini ya kusudio kabla ya tarehe ya kusitisha huduma za bima ya afya, ikibainisha sababu za kutaka kufutiwa usajili. 8 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote (2) Kabla ya kufuta usajili chini ya kanuni ndogo (1), Mamlaka itaitaka skimu ya bima ya afya kuwasilisha taarifa zifuatazo- (a) taarifa wanachama watakavyohudumiwa mpaka muda wa uanachama wao utakapokoma; namna ya Taarifa ya kufutwa kwa usajili wa skimu ya bima ya afya Rejesta ya skimu za bima za afya (b) taarifa za madai ya vituo vilivyoingia mikataba na skimu ya bima ya afya na namna yatakavyolipwa; na (c) tathmini ya uhai wa skimu ya bima ya afya. (3) Mamlaka ndani ya kipindi cha siku tisini, baada ya kufanya uchambuzi wa taarifa zilizowasilishwa na skimu ya bima ya afya inaweza kukubali au kukataa ombi hilo na kuainisha masharti ya kutekeleza kulingana na miongozo ya Mamlaka. - 11 Verify source ↗
Mamlaka ndani ya siku saba tangu tarehe ya
AI-assisted research summary: Mamlaka lazima itangaze kwa umma, ndani ya siku saba baada ya kufuta usajili wa skimu ya bima ya afya, na iwafahamishe pia wanachama na vituo vilivyoingia mkataba kuhusu namna ya kupata huduma.
11. Mamlaka ndani ya siku saba tangu tarehe ya kufuta usajili wa skimu ya bima ya afya, na kwa kupitia vyombo vya habari vinavyofikia wananchi wengi, itautaarifu umma kuhusu kufutwa kwa skimu na kuwataarifu wanachama na vituo viliyoingia mkataba na skimu hiyo kuhusu namna ambavyo wanachama na wanufaika wa skimu iliyofutwa watakavyopata huduma. - 12 Verify source ↗
(1) Mamlaka itaweka na kutunza rejesta ya
AI-assisted research summary: Mamlaka lazima iandae na itunze rejesta ya skimu za bima ya afya, na rejesta hiyo isasasishwe kila mwaka.
12.-(1) Mamlaka itaweka na kutunza rejesta ya skimu za bima za afya kwa namna iliyobainishwa katika Fomu Na. 3 ya Jedwali la Kanuni hizi. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), rejesta inayotajwa katika kanuni ndogo ya (1) itakuwa na taarifa zifuatazo- (a) jina, anuani na mawasiliano ya skimu ya bima ya afya; (b) namba ya usajili; (c) tarehe ya usajili; (d) idadi ya wanachama na wanufaika waliosajiliwa na skimu ya bima ya afya; (e) taarifa ya waajiri walioingia mkataba na skimu ya bima ya afya; (f) taarifa ya vituo vilivyoingia mkataba na skimu ya bima ya afya; na 9 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote (g) taarifa yoyote ambayo Mamlaka itaona inafaa. (3) Rejesta ya skimu ya bima ya afya itatakiwa kusasishwa kila mwaka. SEHEMU YA TATU UTAMBUZI NA USAJILI WA WATU WASIO NA UWEZO Majukumu ya mamlaka ya utambuzi Kanzidata ya watu wasio na uwezo
Part
SEHEMU YA TATU
- 13 Verify source ↗
Majukumu ya mamlaka ya utambuzi
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kina kichwa cha majukumu ya mamlaka ya utambuzi chini ya Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote.
13. Majukumu ya mamlaka ya utambuzi. 1 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote - 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: This section is about a fund’s management and financing health services for people who are unable to pay or otherwise lack capacity.
16. Kanzidata ya watu wasio na uwezo. Usimamizi wa Mfuko. Ugharamiaji wa huduma za afya kwa watu wasio na uwezo. SEHEMU YA NNE USIMAMIZI NA UDHIBITI WA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA - 13 Verify source ↗
(1) Kwa madhumuni ya fedha za Mfuko
AI-assisted research summary: Wizara lazima iombe orodha ya watu wasio na uwezo, na mamlaka za utambuzi ziandae, zishirikishe wadau kwa uhakiki, na zihifadhi na kuwasilisha kumbukumbu kwa Waziri.
13.-(1) Kwa madhumuni ya fedha za Mfuko kuanza kutumika kugharamia watu wasio na uwezo, Wizara itaziomba mamlaka za utambuzi wa watu wasio na uwezo kuandaa na kuwasilisha kwake, katika muda utakaobainishwa na Wizara, orodha ya watu wasio na uwezo. (2) Mara baada ya kupokea maombi ya Wizara, mamlaka za utambuzi zitaandaa orodha ya watu wasio na uwezo na kuwasilisha Wizarani katika muda uliopangwa. (3) Kwa kuzingatia wigo mpana wa uwakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo makundi yenye mahitaji maalum na kwa kuzingatia muda uliopangwa na utaratibu uliokubalika baina ya Wizara na mamlaka za utamhuzi, mamlaka hizo za utambuzi zitashirikisha wadau kwa ajili ya uhakiki wa orodha ya watu wasio na uwezo iliyoandaliwa. (4) Mamlaka za utambuzi zitatunza kumbukumbu ya orodha ya watu wasio na uwezo na kuwasilisha kwa Waziri kwa kadri itakavyokuwa ikihitajika. - 14 Verify source ↗
(1) Wizara itatunza kanzidata ya watu wasio
AI-assisted research summary: The Ministry must keep a database of eligible people, and recognition authorities must review it and advise the Ministry every three years on who should be removed or added.
14.-(1) Wizara itatunza kanzidata ya watu wasio na uwezo ambao wanakidhi kugharamiwa bima za afya kupitia Mfuko. (2) Kila baada ya miaka mitatu, mamlaka za utambuzi zitafanya tathmini na kuishauri Wizara kuhusu watu wanaopaswa kuondolewa au kujumuishwa katika kanzidata. Usimamizi wa Mfuko - 15 Verify source ↗
(1) Mfuko wa kugharamia bima za afya kwa
AI-assisted research summary: Wizara husimamia na kuratibu Mfuko wa kugharamia bima za afya kwa watu wasio na uwezo, na husimamia majukumu yake ya kila siku yaliyoorodheshwa katika kifungu hiki.
15.-(1) Mfuko wa kugharamia bima za afya kwa watu wasio na uwezo utasimamiwa na kuratibiwa na Wizara. (2) Katika kuratibu na kusimamia Mfuko, Wizara itatekeleza majukumu yafuatayo- 10 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote Ugharamiaji wa huduma za afya kwa watu wasio na uwezo (a) kufuatilia upatikanaji wa fedha za Mfuko; (b) kufuatilia upatikanaji wa wanufaika wa Mfuko; (c) kuratibu usajili wa wanufaika wa Mfuko; (d) kutunza kumbukumbu za wanufaika wa Mfuko; (e) kushauri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Mfuko; na (f) kutekeleza majukumu mengine yoyote kadri itakavyoelekezwa. (3) Uendeshaji wa kila siku wa utasimamiwa na skimu ya bima ya afya umma. Mfuko - 16 Verify source ↗
(1) Watu waliotambuliwa na kuingizwa
AI-assisted research summary: Wizara na Waziri lazima washirikiane kuorodhesha, kuandaa mwongozo wa rufaa, na kutangaza mwongozo huo; skimu ya bima ya afya ya umma lazima isajili watu wasio na uwezo na kuwapa utambulisho, na watu waliosajiliwa wana haki ya kupata huduma za afya chini ya mafao yaliyochangia kupitia Mfuko.
16.-(1) Watu waliotambuliwa na kuingizwa katika kanzidata ya watu wasio na uwezo watapata huduma za afya kwa utaratibu wa bima ya afya chini ya skimu ya bima ya afya ya umma kwa kugharamiwa na Serikali kupitia Mfuko. (2) Wizara itawasilisha katika skimu ya bima ya afya ya umma orodha ya watu wasio na uwezo na michango yao kwa ajili ya kugharamiwa bima ya afya. (3) Skimu ya bima ya afya ya umma, baada ya kupokea orodha na michango ya watu wasio na uwezo itawasajili na kutoa utambulisho ili kuwawezesha watu hao kupata huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya vya umma au vituo vya kutolea huduma za afya vya binafsi vilivyoingia mkataba na Serikali. (4) Watu wasio na uwezo waliosajiliwa watakuwa na haki ya kupata huduma za afya kulingana na kitita cha mafao walichogharamiwa kupitia Mfuko. za ziada (5) Endapo watu wasio na uwezo watahitaji huduma cha mafao ya walichogharamiwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (4), wanaweza kupata huduma hizo kupitia Mfuko kwa kuzingatia utaratibu wa rufaa. kitita nje (6) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo ya (5), Wizara itaandaa mwongozo wa rufaa kwa huduma za ziada nje ya kitita cha mafao walichogharamiwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (4). (7) Waziri, kupitia tangazo la kawaida katika 11 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote gazeti la serikali, atautangaza kwa umma, muongozo wa rufaa unaorejewa katika kanuni ndogo ya (6). SEHEMU YA NNE USIMAMIZI NA UDHIBITI WA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA Usimamizi na udhibiti wa huduma za bima ya afya
Part
SEHEMU YA NNE
- 19 Verify source ↗
Section 19
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaonyesha mada za usimamizi na udhibiti wa huduma za bima ya afya, kanzidata ya vituo vya kutolea huduma za afya, ukaguzi wa skimu za bima ya afya, na usajili wa wanachama.
19. Usimamizi na udhibiti wa huduma za bima ya afya. Kanzidata ya vituo vya kutolea huduma za afya. Ukaguzi wa skimu za bima ya afya. SEHEMU YA TANO USAJILI WA WANACHAMA KATIKA SKIMU ZA BIMA YA AFYA Usajili wa wanachama katika skimu za bima ya afya. - 17 Verify source ↗
(1) Mamlaka itasimamia na kudhibiti skimu
AI-assisted research summary: Mamlaka lazima isimamie na kudhibiti skimu za bima ya afya ili zitoe huduma kwa wanachama na vituo vya afya vilivyoingia mkataba, kwa kuzingatia masharti yaliyotajwa.
17.-(1) Mamlaka itasimamia na kudhibiti skimu za bima ya afya kwa kuhakikisha zinatoa huduma za bima ya afya kwa wanachama wake na vituo vya huduma ya afya vilivyoingia mkataba na skimu kwa kuzingatia yafuatayo- (a) kutoendesha skimu ya bima ya afya bila ya cheti halali cha usajili; (b) wanachama na wanufaika wa skimu ya bima ya afya wanapatiwa huduma bila ya usumbufu wala ubaguzi; (c) mtu anayestahili kujiandikisha katika skimu ya bima ya afya anasajiliwa bila ya vikwazo vyovyote ili mradi ametimiza masharti ya usajili; (d) kutokuwepo kwa vigezo vya usajili kwa wanachama visivyotekelezeka; (e) utoaji wa huduma kwa kuzingatia mpango wa utoaji huduma wa skimu ya bima ya afya ulioidhinishwa na Mamlaka; na (f) ushughulikiaji kwa wakati wa malalamiko kuhusu bima ya afya. Kanzidata ya vituo vya kutolea huduma za afya - 18 Verify source ↗
(1) Mamlaka itatunza kanzidata ya vituo vya
AI-assisted research summary: Mamlaka must keep and regularly update a database of contracted health facilities, and health insurance schemes must submit information to Mamlaka and keep the same database on their websites.
18.-(1) Mamlaka itatunza kanzidata ya vituo vya huduma za afya vilivyoingia mkataba na skimu za bima ya afya ikijumuisha taarifa zifuatazo: (a) jina na anuani ya kituo cha huduma za afya; (b) ngazi ya kituo cha kutolea huduma za afya; (c) umiliki wa kituo cha huduma za afya; (d) namba ya usajili wa kituo cha kutolea huduma za afya; (e) tarehe ya usajili wa kituo cha huduma za afya; (f) tarehe ya kuingia mkataba na skimu ya bima ya afya; (g) muda wa mkataba kati ya kituo cha kutolea 12 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote huduma za afya na skimu ya bima ya afya; (h) jina la skimu iliyoingia mkataba na kituo; na (i) tarifa nyingine yoyote ambayo Mamlaka itaona inafaa. (2) Mamlaka itakuwa na wajibu wa kusasisha kanzidata mara kwa mara kwa kadiri mabadiliko yatakavyojitokeza. (3) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo (1), skimu ya bima ya afya itatakiwa- (a) kuwasilisha kwa Mamlaka kwa namna muongozo katika itakayobainishwa uliowekwa na Mamlaka; na Ukaguzi wa skimu za bima ya afya (b) kutunza na kuweka kwenye tovuti yake, kanzidata ya vituo vya kutolea huduma vilivyoingia mkataba na skimu husika. - 19 Verify source ↗
(1) Mamlaka itafanya ukaguzi wa skimu za
AI-assisted research summary: Mamlaka lazima ikague skimu za bima ya afya kila mwaka na itoe notisi ya siku tatu kabla ya ukaguzi. Pia inaweza kufanya ukaguzi maalum wakati wowote inapouona inafaa.
19.-(1) Mamlaka itafanya ukaguzi wa skimu za bima ya afya kila mwaka kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya ukaguzi iliyowekwa na Mamlaka. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), Mamlaka inaweza kufanya ukaguzi maalum wakati wowote itakapoona inafaa. (3) Katika kutekeleza masharti ya kanuni ndogo ya (1), Mamlaka itapaswa kutoa notisi ya siku tatu kwa skimu ya bima ya afya kabla ya ukaguzi kufanyika. SEHEMU YA TANO USAJILI WA WANACHAMA KATIKA SKIMU ZA BIMA YA AFYA Usajili wa wanachama katika skimu za bima ya afya
Part
SEHEMU YA TANO
- 22 Verify source ↗
Muda wa kusubiri kuanza kupata huduma
AI-assisted research summary: This section refers to the waiting period before service starts.
22. Muda wa kusubiri kuanza kupata huduma. - 28 Verify source ↗
Section 28
AI-assisted research summary: This section is about registering employees in a health insurance scheme and related issues about membership, dependants, stopping health service provision, notices, complaints, and the authority’s decision.
28. Usajili wa waajiriwa katika skimu ya bima ya afya. Ukomo wa uanachama. Ukomo wa mtegemezi. Usitishaji wa skimu ya bima ya afya kutoa huduma. Notisi ya kituo kusitisha kutoa huduma za afya Uwasilishaji wa malalamiko dhidi ya kusudio la kituo kusitisha utoaji huduma. Uamuzi wa Mamlaka kuhusu kusudio la kituo kusitisha utoaji huduma. - 29 Verify source ↗
Section 29
AI-assisted research summary: This section is a heading about contribution rates for an essential service benefits package, but it does not state any specific rule or rate.
29. SEHEMU YA SITA VITITA VYA MAFAO Viwango vya uchangiaji kwa kitita cha mafao ya huduma muhimu. - 20 Verify source ↗
(1) Kila raia au mkazi katika sekta rasmi na
AI-assisted research summary: Raia au mkazi katika sekta rasmi na isiyo rasmi ana haki ya kusajiliwa kwenye skimu ya bima ya afya, na skimu lazima iweke utaratibu, usajili, notisi, utunzaji wa kanzidata, na huisha upya wa uanachama kwa muda uliobainishwa.
20.-(1) Kila raia au mkazi katika sekta rasmi na isiyo rasmi atakuwa na haki ya kusajiliwa katika skimu ya bima ya afya kwa utaratibu utakaowekwa na skimu ya bima ya afya kupitia miongozo yake ambayo itaidhinishwa na Mamlaka. (2) Skimu ya bima ya afya itahakikisha mifumo ya usajili inamuwezesha mwanachama kupata utambulisho ndani ya siku saba tangu tarehe ya kukamilika kwa usajili. inayotumika (3) Skimu ya bima ya afya itatakiwa kuhakikisha 13 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote Miongozo ya usajili wa wanachama huduma za usajili zinapatikana hadi ngazi ya kijiji na mtaa. (4) Skimu ya bima ya afya itahakikisha inatunza kanzidata ya wanachama waliosajiliwa kulingana na miongozo iliyowekwa na Mamlaka. (5) Skimu ya bima ya afya itatakiwa kutoa notisi ya ukomo wa uanachama kwa mwanachama angalau siku thelathini kabla ya tarehe ya kufikia ukomo wa uanachama. (6) Mwanachama anayechangia kwa utaratibu wa mkupuo kwa mwaka atachukuliwa kuwa amehuisha uanachama wake iwapo atalipia katika skimu ya bima ya afya kiwango cha uchangiaji ndani ya siku thelathini baada ya tarehe ya kufikia ukomo wa uanachama. (7) Mwanachama atakayeshindwa kuhuisha uanachama wake kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (6) atapaswa kujisajili upya kwa kuzingatia utaratibu uliobainishwa katika Kanuni hizi. - 21 Verify source ↗
(1) Bila kuathiri kanuni ya 20(1), na kwa
AI-assisted research summary: Skimu ya bima ya afya lazima iwasilishe miongozo yake ya usajili wa wanachama kwa Mamlaka ili iidhinishwe kabla ya kutumika.
21.-(1) Bila kuathiri kanuni ya 20(1), na kwa kuzingatia miongozo iliyowekwa na Mamlaka, skimu ya bima ya afya itatakiwa kuwasilisha kwa Mamlaka miongozo yake ya usajili wa wanachama kwa ajili ya kuidhinishwa kabla ya kuanza kutumika kwa miongozo hiyo. Mamlaka, katika kuidhinisha miongozo ya usajili wa wanachama itakayowasilishwa kwake na skimu za bima ya afya, itazingatia masuala yafuatayo- (a) nyaraka mbalimbali kwa ajili ya utambuzi na uhakiki wa wanachama; (b) utaratibu wa utambulisho wa wanachama na wanufaika; (c) utaratibu wa usitishaji na urejeshwaji wa huduma kwa wanachama na wanufaika; (d) uhitaji wa kumbukumbu za uanachama wa awali katika skimu ya bima ya afya nyinginezo, kama zipo; na (e) taarifa nyingine muhimu itakavyoelekezwa na Mamlaka. kwa kadri 14 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote Muda wa kusubiri kuanza kupata huduma Usajili wa waajiriwa katika skimu ya bima ya afya - 22 Verify source ↗
(1) Skimu ya bima ya afya inaweza kuweka
AI-assisted research summary: Health insurance schemes may set a waiting period before members and registered beneficiaries receive benefits, but the period must not exceed 30 days from registration.
22.-(1) Skimu ya bima ya afya inaweza kuweka muda wa kusubiri wa mwanachama na mnufaika aliyesajiliwa katika skimu hiyo kabla ya kuanza kunufaika na huduma za bima ya afya Isipokuwa kwamba, muda huo wa kusubiri hautazidi siku thelathini tangu tarehe ya mwanachama au mnufaika kusajiliwa. (2) Masharti ya kanuni ndogo ya (1) hayatawahusu- (a) waajiriwa katika sekta ya umma na sekta rasmi binafsi; (b) watu wasio na uwezo wanaogharamiwa na Serikali; (c) watu wote waliokuwa wanachama hai wa skimu ya umma wakati wa kuanza kutumika kwa Sheria; au (d) wanachama ambao ni wanafunzi wanaojiunga kwa makundi. (3) Katika uwekaji wa muda wa kusubiri, skimu ya bima ya afya itakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa muda huo hauathiri uhai na uendelevu wa skimu ya bima ya afya. (4) Kila skimu ya bima ya afya katika miongozo yake ya usajili wa wanachama, itabainisha muda wa kusubiri. - 23 Verify source ↗
(1) Mwajiri katika sekta rasmi binafsi ataingia
AI-assisted research summary: Mwajiri wa sekta rasmi binafsi lazima aingie mkataba na skimu moja ya bima ya afya kwa ajili ya kusajili waajiriwa, awashirikishe kuchagua skimu, na alipe mchango wa mwajiriwa ifikapo tarehe 15 ya mwezi unaofuata. Pia, anaweza kutumia skimu nyingine kwa huduma za ziada.
23.-(1) Mwajiri katika sekta rasmi binafsi ataingia mkataba na skimu ya bima ya afya moja kwa lengo la kuwasajili waajiriwa wake ili kupata kitita cha mafao cha huduma muhimu au kitita cha huduma za ziada: Isipokuwa kwamba, mwajiri anaweza kuingia mkataba na skimu ya bima ya afya nyingine kwa lengo la kuwawezesha waajiriwa wake kupata huduma za kitita cha ziada. (2) Skimu ya bima ya afya ya umma inaweza kuingia mkataba na mwajiri katika sekta ya umma au binafsi kwa masharti yatakayowekwa kwa mujibu wa Sheria inayosimamia skimu ya bima ya afya ya umma. (3) Katika kutekeleza masharti ya kanuni ndogo ya (1), mwajiri katika sekta rasmi binafsi atawashirikisha 15 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote waajiriwa katika kuchagua skimu ya bima ya afya wanayopaswa kuingia nayo mkataba. (5) Mwajiri ambaye atamsajili mwajiriwa katika skimu ya bima ya afya atawasilisha mchango wa mwajiriwa kwa skimu ya bima ya afya kabla au ifikapo tarehe kumi na tano ya mwezi unaofuata tangu tarehe ya kumsajili mwajiriwa. Ukomo wa uanachama - 24 Verify source ↗
(1) Kwa madhumuni ya kifungu cha 28(1)
AI-assisted research summary: Uanachama hukoma ikiwa mwanachama ataacha kuchangia kwa muda fulani, na wategemezi wa mwanachama anayechangia kupitia mshahara wanaweza kuendelea kunufaika kwa mwezi mmoja baada ya mchango wa mwisho.
24.-(1) Kwa madhumuni ya kifungu cha 28(1) cha Sheria, uanachama utakomo endapo- (a) mwanachama ambaye ni mwajiriwa katika sekta ya umma au sekta rasmi binafsi ataacha kuchangia kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo; na (b) mwanachama kwa mwaka ataacha kuchangia mwezi mmoja baada ya mwaka wa uchangiaji kupita. anachangia ambaye Ukomo wa mtegemezi (2) Endapo mwanachama anayechangia kupitia makato ya mshahara atafikia ukomo wa uanachama, wategemezi wake wataendelea kunufaika kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu kupokea mchango wa mwisho. - 25 Verify source ↗
Kwa kuzingatia kifungu cha 3 cha Sheria,
AI-assisted research summary: A dependent child or blood relative stops being a dependent when they turn 21.
25. Kwa kuzingatia kifungu cha 3 cha Sheria, endapo mtegemezi ambaye ni- (a) mtoto wa mwanachama wa kuzaa, kuasili au wa kambo; au (b) ndugu wa damu wa mwanachama, atafikisha umri wa miaka ishirini na moja, mtegemezi huyo atakuwa amefikia ukomo wa utegemezi. Usitishaji wa skimu ya bima ya afya kutoa huduma - 26 Verify source ↗
Skimu ya bima ya afya inaweza kusitisha
AI-assisted research summary: The health insurance scheme may stop providing services to a member or beneficiary if the member stops contributing for one month, or for a year after the contribution year ends.
26. Skimu ya bima ya afya inaweza kusitisha utoaji wa huduma kwa mwanachama au mnufaika endapo- (a) mwanachama ambaye ni mwajiriwa katika sekta ya umma au sekta rasmi binafsi ataacha kuchangia kwa kipindi cha mwezi mmoja; au kwa mwaka ataacha kuchangia baada ya mwaka wa kuchangia kuisha. (b) mwanachama anachangia ambaye 16 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote Notisi ya kituo kusitisha kutoa huduma za afya Uwasilishaji wa malalamiko dhidi ya kusudio la kituo kusitisha utoaji huduma Uamuzi wa Mamlaka kuhusu kusudio la kituo kusitisha utoaji huduma - 27 Verify source ↗
(1) Kituo cha kutolea huduma za afya kinacho
AI-assisted research summary: A health service facility that wants to stop serving members and beneficiaries of a health insurance scheme must give 90 days’ written notice and explain why.
27.-(1) Kituo cha kutolea huduma za afya kinacho kusudia kusitisha utoaji wa huduma za afya kwa wanachama na wanufaika wa skimu ya bima ya afya kitatoa notisi ya maandishi ya siku tisini kwa skimu na nakala kwa Mamlaka ikibainisha kusudio la kusitisha huduma na sababu za kusudio hilo. (2) Katika kipindi cha notisi, kituo cha kutolea huduma za afya kitatakiwa- (a) kuweka utaratibu wa namna ya kukamilisha au uhamisho wa utoaji wa huduma kwa wanufaika wa skimu ya bima ya afya na nakala ya taarifa hiyo kuwasilishwa kwa Mamlaka; na (b) kupokea na kutekeleza maelekezo ya Mamlaka kuhusiana na taarifa iliyowasilishwa kwake chini ya aya (a) au uamuzi wowote uliotokana na malamiko yaliyowasilishwa kwa Mamlaka. - 28 Verify source ↗
(1) Kwa madhumuni ya kanuni ya 27(2)(b),
AI-assisted research summary: Ukigusia taarifa ya kusudio la kusitisha huduma kwa wanachama wake, skimu ya bima ya afya lazima itangaze kwa umma. Mtu aliyeathiriwa anaweza kuwasilisha malalamiko kwa Mamlaka ndani ya siku 21 tangu tangazo hilo.
28.-(1) Kwa madhumuni ya kanuni ya 27(2)(b), skimu ya bima ya afya itakapopokea taarifa ya kusudio la usitishwaji wa huduma kwa wanachama wake, itatoa tangazo la umma kwa namna itakayoweza kuwafikia wananchi walio wengi kwa lengo la kutoa fursa kwa mtu kutoa pingamizi kwa Mamlaka. (2) Mtu yeyote ambaye ataathirika na usitishwaji wa utoaji wa huduma anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Mamlaka ndani ya kipindi kisichozidi siku ishirini na moja tangu tarehe ya tangazo la umma kutolewa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1). - 29 Verify source ↗
Mamlaka ndani ya kipindi cha siku thelathini,
AI-assisted research summary: Mamlaka lazima itoe uamuzi ndani ya siku 30 baada ya kupokea malalamiko; kituo kinaweza kulazimika kufidia hasara au kusitisha utoaji wa huduma na kutoa taarifa kulingana na masharti yaliyotajwa.
29. Mamlaka ndani ya kipindi cha siku thelathini, baada ya kupokea malalamiko, itatoa uamuzi ufuatao- (a) endapo usitishwaji wa utoaji huduma za afya utaathiri unufaikaji wa huduma au mkataba baina yake na skimu ya bima ya afya, kituo hicho kitakuwa na wajibu wa kufidia hasara kwa mnufaika au skimu ya bima ya afya kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo baina yake na skimu; au 17 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote (b) endapo hakuna pingamizi lolote kutoka kwa mtu, skimu ya bima ya afya au Mamlaka, kituo cha kutolea huduma kitasitisha utoaji wa huduma na kuitaarifu skimu ya bima ya afya na nakala kwa Mamlaka. . SEHEMU YA SITA VITITA VYA MAFAO (a) Kitita Cha Mafao ya Huduma Muhimu Muda wa kunufaika na kitita cha mafao ya huduma muhimu Viwango vya uchangiaji kwa kitita cha mafao ya huduma muhimu
Part
SEHEMU YA SITA
- 30 Verify source ↗
Muda wa kunufaika na kitita cha mafao ya huduma muhimu
AI-assisted research summary: Section title on the period for benefiting from the package of essential service benefits.
30. Muda wa kunufaika na kitita cha mafao ya huduma muhimu. - 32 Verify source ↗
Maboresho ya kitita cha mafao ya huduma muhimu
AI-assisted research summary: Section 32 is titled “Maboresho ya kitita cha mafao ya huduma muhimu.”
32. Maboresho ya kitita cha mafao ya huduma muhimu. - 34 Verify source ↗
Miongozo ya utoaji wa kitita cha mafao ya huduma muhimu
AI-assisted research summary: This section gives guidelines for issuing a package of benefits for essential services.
34. Miongozo ya utoaji wa kitita cha mafao ya huduma muhimu. - 35 Verify source ↗
Section 35
AI-assisted research summary: Section 35 is titled about compliance with appeal procedures and additional service units, within the part on payment procedures for health service facilities.
35. Uzingatiaji wa taratibu za rufaa. Kitita cha huduma za ziada. SEHEMU YA SABA UTARATIBU WA MALIPO KWA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA - 30 Verify source ↗
(1) Mwanachama na mnufaika wa skimu za
AI-assisted research summary: Health insurance scheme members and beneficiaries are entitled to specified service benefits if they meet the stated membership and contribution conditions.
30.-(1) Mwanachama na mnufaika wa skimu za bima ya afya watakuwa na haki ya kupata huduma za kitita kama kilivyobainishwa katika Sehemu A ya Jedwali la Sheria, iwapo ni mwanachama- huduma muhimu cha mafao ya (a) anayechangia kwa utaratibu wa kulipa kwa mkupuo mmoja kwa mwaka, kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu tarehe ya kusajiliwa au baada ya muda wa kusubiri kuisha; na (b) ambaye ni mwajiriwa katika sekta ya umma na sekta rasmi binafsi, kwa kipindi chote cha uanachama wake. (2) Dawa zitakazotolewa kwa wanufaika wa skimu za bima ya afya kwa kitita cha mafao ya huduma muhimu zitaandikwa kwa majina ya asilia na kwa kuzingatia Orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu inayotolewa na Wizara. - 31 Verify source ↗
(1) Kila mwajiri chini ya sekta ya umma na
AI-assisted research summary: Waajiri husajili na kuwasilisha kiwango cha uchangiaji kwa skimu ya bima ya afya ya umma; kwa kawaida wanachangia nusu au zaidi, na mfanyakazi hulipa kiasi kilichobaki.
31.-(1) Kila mwajiri chini ya sekta ya umma na sekta rasmi binafsi aliyejisajili katika skimu ya bima ya afya ya umma atawasilisha katika skimu hiyo kiwango cha uchangiaji kwa mujibu wa sheria ya bima ya afya ya umma, ambapo ndani yake mwajiri atachangia nusu au zaidi ya kiwango hicho, na kiwango kilichosalia kitachangiwa na mwajiriwa: Isipokuwa kwamba, mwajiri anaweza kuchangia kiwango chote cha uchangiaji. (2) Waziri atatoa tangazo la umma kwa namna itakayoweza kuwafikia wananchi walio wengi viwango vya uchangiaji pamoja na huduma zitakazopatikana 18 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote katika kitita cha mafao ya huduma muhimu kwa- isiyo (a) mwanachama kutoka sekta rasmi atakayejisajili katika skimu ya bima ya afya ya umma; (b) mwanachama ambaye anachangia kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) na (2)(a) na anahitaji kusajili mtegemezi mwingine anayeruhusiwa kwa mujibu wa Sheria; (c) mwanachama ambaye ni mwanafunzi anayejiunga kwa makundi. (3) Endapo mwanachama ana mwenza zaidi ya mmoja, mwenza huyo anaweza kusajiliwa kama mwanachama kusajili wategemezi wanaoruhusiwa kwa mujibu wa Sheria. anaweza na (4) Waziri atatoa tangazo la umma kwa namna itakayoweza kuwafikia wananchi walio wengi litakaloainisha aina za Kitita cha Mafao ya Huduma Muhimu ambavyo vitatolewa na Skimu ya Bima ya Afya ya Umma baada ya kuthibitishwa na Mamlaka. Maboresho ya kitita cha mafao ya huduma muhimu - 32 Verify source ↗
(1) Kwa madhumuni ya kuhakikisha huduma
AI-assisted research summary: Waziri anaweza kuboresha kitita cha mafao ya huduma muhimu baada ya kushauriwa na Mamlaka.
32.-(1) Kwa madhumuni ya kuhakikisha huduma za kitita cha mafao ya huduma muhimu zinaendana na mahitaji ya huduma za afya kwa wakati husika, Waziri baada ya kushauriwa na Mamlaka anaweza kufanya maboresho ya kitita cha mafao ya huduma muhimu kwa- (a) kufanya mapitio ya huduma zilizojumuishwa katika kitita hicho; (b) kufanya mapitio ya bei za huduma za afya katika kitita ili ziendane na bei halisi kwa kipindi husika; au (c) kufanya mapitio ya viwango vya uchangiaji katika kitita kwa kuzingatia gharama halisi za utoaji wa kitita hicho. (2) Maboresho ya kitita cha mafao ya huduma muhimu katika kanuni ndogo ya (1) yatazingatia tathmini ya uhai na undelevu wa skimu za bima ya afya. Uzingatiaji wa taratibu za rufaa - 33 Verify source ↗
(1) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha
AI-assisted research summary: A member or beneficiary who does not follow the referral procedure must pay the treatment costs at the health facility, and the health facility must provide services following the referral procedure.
33.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 21 cha Sheria, mwanachama au mnufaika ambaye hatazingatia utaratibu wa rufaa wakati wa kupata huduma 19 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote za afya atawajibika kulipia gharama za matibabu katika kituo cha afya alichohudumiwa. (2) Kituo cha kutolea huduma za Afya, kitatoa huduma zaAfya kwa Mwanachama au mnufaika wa Bima ya Afya kwa kuzingatia utaratibu wa Rufaa (3) Skimu ya bima ya afya haitawajibika kulipa madai yaliyowasilishwa kwake na kituo cha huduma za afya yanayohusu Mwanachama au mnufaika ambaye hatazingatia masharti ya kanuni ndogo (1) na (2) Miongozo ya utoaji wa kitita cha mafao ya huduma muhimu - 34 Verify source ↗
kwa kuzingatia kifungu cha 21 cha Sheria,
AI-assisted research summary: Utoaji wa kitita cha mafao ya huduma muhimu kuanzia zahanati hadi hospitali ya Taifa unapaswa kufuata miongozo ya Wizara.
34. kwa kuzingatia kifungu cha 21 cha Sheria, utoaji wa kitita cha mafao ya huduma muhimu kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya Taifa utazingatia miongozo ya Wizara. (b) Kitita cha huduma za ziada Kitita cha huduma za ziada - 35 Verify source ↗
Kwa madhumuni ya uanzishwaji wa kitita cha
AI-assisted research summary: Mamlaka lazima itaandae mwongozo wa kitita cha huduma za ziada, na izingatie kuwa huduma zake ziwe zaidi ya zile za mafao ya huduma muhimu pamoja na tathmini ya uhai na uendelevu wa skimu.
35. Kwa madhumuni ya uanzishwaji wa kitita cha huduma za ziada, Mamlaka itaandaa mwongozo wa utoaji wa kitita hicho ambapo, pamoja na mambo mengine, masuala yafuatayo yatazingatiwa- (a) huduma zitakazojumuishwa katika kitita cha huduma za ziada zitakuwa ni zaidi ya huduma zilizojumuishwa katika kitita cha mafao ya huduma muhimu; na (b) viwango vya uchangiaji wa kitita cha huduma za ziada vitazingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa skimu katika kutoa huduma hizo. SEHEMU YA SABA UTARATIBU WA MALIPO KWA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA Uwasilishaji wa madai
Part
SEHEMU YA SABA
- 36 Verify source ↗
Section 36
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kina kichwa “Uwasilishaji wa madai.”
36. Uwasilishaji wa madai. 2 Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) - 41 Verify source ↗
Section 41
AI-assisted research summary: This section lists general topics: claims, complaints, dispute resolution, appeals against authority decisions, deposit procedures, and scheme transfer procedures.
41. Ulipaji wa madai. Uchunguzi na usuluhishi wa madai. Ushughulikiaji wa malalamiko. Usuluhishi na utatuzi wa Migogoro. Rufaa dhidi ya maamuzi ya Mamlaka. SEHEMU YA NANE MASHARTI YA JUMLA Utaratibu wa uwekaji wa amana. Utaratibu wa kuhama skimu. - 36 Verify source ↗
(1) Kituo cha kutolea huduma za afya
AI-assisted research summary: Health facilities must submit claims for services to a health insurance scheme within 30 days after the service is completed.
36.-(1) Kituo cha kutolea huduma za afya kitawasilisha katika skimu ya bima ya afya madai ya huduma zilizotolewa kwa mwanachama na mnufaika ndani ya siku thelathini tangu tarehe ya kukamilika kwa huduma kwa mwanachama. (2) Kituo cha kutolea huduma za afya 20 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote Ulipaji wa madai kitawasilisha madai kuzingatia miongozo kwa itakayotolewa na skimu za bima ya afya na kuidhinishwa na Mamlaka. (3) Kituo cha kutolea huduma za afya kitakachowasilisha madai yake nje ya muda uliotajwa katika kanuni ndogo ya (1) kitatakiwa kutoa sababu za msingi kwa skimu ya bima ya afya husika kabla ya madai yake kukubaliwa au kukataliwa: Isipokuwa kwamba, kituo kitatakiwa kuwasilisha madai hayo ndani ya siku thelathini tangu tarehe ya kuisha muda uliorejewa katika kanuni ndogo ya (1). - 37 Verify source ↗
(1) Skimu ya bima ya afya ndani ya siku tatu
AI-assisted research summary: The health insurance scheme must notify the health facility within 3 days of receiving a claim and pay valid claims within 60 days.
37.-(1) Skimu ya bima ya afya ndani ya siku tatu tangu tarehe ya kupokea madai ya kituo cha huduma za afya itakitaarifu kituo husika kuhusiana na madai hayo na itapaswa kulipa madai halali ndani ya kipindi kisichozidi siku Sitini tangu tarehe ya kupokea madai. (2) Bila kujali kanuni ndogo (1), iwapo skimu kwa sababu yoyote ya msingi, itashindwa kulipa madai halali ya kituo cha kutolea huduma za afya ndani ya kipindi kilichorejewa katika kanuni ndogo (1), skimu ya bima ya afya inaweza kuongeza muda wa malipo usiozidi siku kumi na tano: Isipokuwa kwamba skimu ya bima ya afya itapaswa kutoa taarifa ya kusudio la kuongeza muda wa malipo kwa kituo cha kutolea huduma za afya angalau siku kumi na tano kabla ya muda wa malipo kuisha, na itawasilisha nakala ya taarifa hiyo kwa Mamlaka. (3) Skimu ya bima ya afya itaweka utaratibu wa malipo kwa vituo vya kutolea huduma za afya utakaoidhinishwa na Mamlaka kwa kuzingatia maslahi ya vituo vya kutolea huduma za afya na skimu za bima ya afya. (4) Skimu ya bima ya afya itakayoshindwa kulipa madai kwa kituo ndani ya muda ulioainishwa katika kanuni ndogo ya (1) na (2), itawajibika kulipa madai hayo pamoja na faini ya asilimia tano ya madai yanayopaswa kulipwa kwa kituo cha kutolea huduma za afya. 21 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote Uchunguzi na usuluhishi wa madai - 38 Verify source ↗
(1) Endapo skimu imebaini kuwa kuna dosari
AI-assisted research summary: If the scheme finds correctable defects in a claim, it must notify the health provider and set a process to fix them. If it finds suspicious or fraudulent claims, it must suspend payment and follow the stated notice, investigation, response, decision, and complaint steps.
38.-(1) Endapo skimu imebaini kuwa kuna dosari kwenye taarifa ya madai na dosari hizo zinaweza kutatulika, skimu itamtaarifu mtoa huduma za afya kuhusu dosari na kuweka utaratibu wa namna ya kutatua dosari hizo ndani ya kipindi kilichorejewa katika kanuni ya 37. (2) Endapo skimu imebaini uwepo wa madai yenye viashiria vya udanganyifu kutoka kwa mtoa huduma, skimu itaahirisha ulipwaji wa madai hayo na itayashughulikia madai hayo kwa kuzingatia taratibu zifuatazo- (a) skimu ya bima afya itakitaarifu kituo husika cha kutolea huduma za afya kwa maandishi kuhusu kuahirisha kwa malipo ya madai yenye utata au viashiria vya udanganyifu na sababu za kuahirisha malipo hayo; (b) skimu ya bima ya afya itafanya uchunguzi wa madai yenye viashiria vya udanganyifu na itaipa kituo cha huduma za afya taarifa ya matokeo ya uchunguzi na nakala ya taarifa hiyo kwa Mamlaka; (c) endapo kituo za cha huduma afya hakitaridhishwa na taarifa iliyotolewa na skimu ya bima ya afya, kitaijulisha skimu ya bima ya afya ndani ya siku kumi na tano tangu kupokelewa kwa taarifa na kutoa uthibitisho kwa skimu ya bima ya afya juu ya utetezi wake; (d) skimu ya bima ya afya itapaswa kutoa maamuzi ndani ya siku kumi na tano tangu kupokelewa kwa utetezi wa kituo cha huduma za afya; (e) endapo kituo afya hakitaridhishwa na maamuzi ya skimu, kituo hicho kwa kitawasilisha malalamiko Mamlaka ndani ya siku saba baada ya kupokea uamuzi wa skimu. cha huduma za Ushughulikiaji wa malalamiko Sura 394 - 39 Verify source ↗
(1) Kwa kuzingatia mamlaka iliyonayo chini
AI-assisted research summary: The Authority must receive and decide certain complaints, may refer some to the Arbitrator, and the Arbitrator must resolve health insurance disputes.
39.-(1) Kwa kuzingatia mamlaka iliyonayo chini ya kifungu cha 6 (1) cha Sheria ya Bima, Mamlaka 22 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote na kushughulikia itapokea malalamiko yatakayowasilishwa kwake na skimu ya bima ya afya, kituo cha kutolea huduma za afya, mwanachama au mwajiri. (2) Malalamiko yanayoweza kuwasilishwa na (1), watu waliotajwa katika kifungu kidogo cha yatatokana na- (a) malalamiko yatokanayo na kanuni ya 38; au (b) malalamiko mengine itaona yanakidhi kwa ambayo Mamlaka lengo kuhakikisha uwepo wa ufanisi, usawa, usalama na uendelevu wa bima ya afya nchini. yoyote (3) Mamlaka itatolea maamuzi ya malalamiko yaliyowasilishwa kwake kwa maandishi kwa kuzingatia mwongozo wa kushughulikia malalamiko utakaowekwa na Mamlaka. (4) Bila kujali masharti ya kanuni hii, Mamlaka inaweza kuwasilisha malalamiko ambayo itaona kuwa yanakidhi kushughulikiwa na Msuluhishi kwa mujibu wa Sheria ya Bima. 40-(1) Kwa kuzingatia kifungu cha 124(5) cha Sheria ya Bima na kanuni ya 34(4), Msuluhishi atasuluhisha na kutatua migogoro ya bima ya afya kwa kwa mujibu wa Kanuni za Msuluhishi wa Migogoro ya Bima za Mwaka 2013. (2) Mtu yoyote ambaye hajaridhishwa na uamuzi wa Msuluhishi, anaweza kuwasilisha malalamiko yake Mahakama Kuu kwa ajili ya rejea kwa mujibu wa Kanuni za Msuluhishi wa Migogoro ya Bima za Mwaka 2013. Usuluhishi na utatuzi wa Migogoro Sura ya 394 TS. Na. 411 ya mwaka 2013. Rufaa dhidi ya maamuzi ya Mamlaka Sura ya 394 - 41 Verify source ↗
(1) Mtu yoyote ambaye hajaridhishwa na
AI-assisted research summary: A person dissatisfied with an Authority decision may appeal to the Insurance Appeals Board; a health facility may complain to the Authority if a health insurance scheme breaches subrule (2).
41.-(1) Mtu yoyote ambaye hajaridhishwa na uamuzi wa Mamlaka chini ya Kanuni hizi, anaweza kukata rufaa kwa Baraza la Rufaa la Bima kwa mujibu wa Sheria ya Bima na Kanuni chini ya Sheria hiyo. (2) Masharti ya kifungu cha 126(7) cha Sheria ya Bima yatatumika endapo mtu hajaridhishwa na uamuzi wa Baraza la Rufaa la Bima. (3) Endapo skimu ya bima ya afya itakiuka 23 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote masharti ya kanuni ndogo ya (2), kituo cha huduma za afya kinaweza kuwasilisha malalamiko kwa Mamlaka kwa kuzingatia utaratibu ulioainishwa katika Sheria ya Bima. SEHEMU YA NANE MASHARTI YA JUMLA Matumizi ya Kanuni za Bima T.S Na. 372 la 2009
Part
SEHEMU YA NANE
- 45 Verify source ↗
Mamlaka za Serikali za Mitaa kukusanya michango
AI-assisted research summary: Local government authorities may collect contributions.
45. Mamlaka za Serikali za Mitaa kukusanya michango. - 46 Verify source ↗
Makosa na adhabu dhidi ya skimu za bima ya afya
AI-assisted research summary: This section concerns offences and penalties relating to health insurance schemes.
46. Makosa na adhabu dhidi ya skimu za bima ya afya. - 47 Verify source ↗
Section 47
AI-assisted research summary: Mamlaka inaweza kuchukua hatua dhidi ya skimu ya bima ya afya, ikiwemo kufuta.
47. Hatua ambazo Mamlaka inaweza kuchukua dhidi ya skimu ya bima ya afya. Kufuta. - 48 Verify source ↗
Section 48
AI-assisted research summary: This text is a heading for the 2024 Health Insurance for All Regulations and introductory section, not a substantive rule.
48. 3 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote SHERIA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE, NA.13 YA 2023 ____________ KANUNI ___________ (Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 35) KANUNI ZA BIMA YA AFYA KWA WOTE ZA MWAKA 2024 Jina Tafsiri Sura ya 394 Na. 13 ya 2023 Sura ya 351 Sura ya 394 SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI - 42 Verify source ↗
Masharti ya Kanuni za Bima za Mwaka 2009,
AI-assisted research summary: This section says the Insurance Regulations of 2009, together with necessary amendments, apply alongside these regulations.
42. Masharti ya Kanuni za Bima za Mwaka 2009, pamoja na mabadiliko yanayobidi, yatatumika pamoja na Kanuni hizi. Utaratibu wa uwekaji wa amana T.S Na. 372 ya mwaka 2009 Utaratibu wa kuhama skimu Mamlaka za Serikali za Mitaa kukusanya michango Makosa na adhabu dhidi ya skimu za bima ya afya - 43 Verify source ↗
Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 26 cha
AI-assisted research summary: The deposit procedure for a private health insurance scheme is to follow the method set out in the 2009 Insurance Regulations, subject to section 26 of the Act.
43. Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 26 cha Sheria, utaratibu wa uwekaji wa amana kwa skimu bima ya afya binafsi utakuwa kama ulivyoainishwa katika Kanuni za Bima za Mwaka 2009. - 44 Verify source ↗
Endapo mwanachama aliyejiunga katika
AI-assisted research summary: A member of a health insurance scheme who wants to move to another scheme must follow the registration procedures.
44. Endapo mwanachama aliyejiunga katika skimu ya bima ya afya ataamua kuhama katika skimu husika na kuhamia skimu nyingine, atafuata taratibu za usajili kwa mujibu wa kanuni na miongozo ya Mamlaka. - 45 Verify source ↗
Bila kuathiri masharti ya Sheria, mamlaka za
AI-assisted research summary: Mamlaka za serikali za mitaa zinaweza kuratibu ukusanyaji wa michango ya wananchi kwa ajili ya kuwasajili katika skimu ya bima ya afya.
45. Bila kuathiri masharti ya Sheria, mamlaka za serikali za mitaa zinaweza kuratibu ukusanyaji wa michango ya wananchi kwa ajili ya kuwasajili katika skimu ya bima ya afya kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na vitita mbalimbali vitolewavyo na skimu za bima ya afya. - 46 Verify source ↗
Endapo, kwa maoni ya Mamlaka, skimu ya
AI-assisted research summary: If, in the Authority’s view, a health insurance scheme acts in specified non-compliant ways, it commits an offence and must pay a fine of between TZS 10 million and TZS 50 million.
46. Endapo, kwa maoni ya Mamlaka, skimu ya bima ya afya- (a) inaendesha shughuli za bima ya afya pasipo kuzingatia misingi ya undeshaji bima inayokubalika; (b) inaendesha shughuli zake pasipo kujali maslahi ya wanachama na wanufaika; (c) inaendesha shughuli za bima kwa kutozingatia miongozo inayotolewa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni hizi; (d) imeshindwa kuwasilisha taarifa zinazohitajika na Mamlaka katika muda uliowekwa; 24 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote (e) kwa makusudi, imetoa taarifa za upotoshaji kwa Mamlaka; (f) imeshidwa kuzingatia vigezo na masharti ya usajili au kushindwa kutii maelekezo yoyote ya awali yaliyotolewa kwake, Skimu hiyo itakuwa imetenda kosa na itawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi na isiyozidi shilingi milioni hamsini. Hatua ambazo Mamlaka inaweza kuchukua dhidi ya skimu ya bima ya afya. - 47 Verify source ↗
(1) Mamlaka, pamoja na hatua nyingine
AI-assisted research summary: Mamlaka inaweza kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya skimu ya bima ya afya, ikiwemo uangalizi, katazo la kusitisha, maelekezo, kuteua msimamizi wa muda, kutoza faini, au kusitisha usajili; mtu asiye ridhika na amri au maelekezo anaweza kukata rufaa ndani ya siku 30.
47.-(1) Mamlaka, pamoja na hatua nyingine yoyote inayoweza kuchukuliwa, inaweza- (a) kuiweka skimu ya bima ya afya chini ya uangalizi; (b) kutoa amri ya katazo ya kusitishwa kwa skimu; (c) kutoa maelekezo kwa skimu ya bima ya afya; (d) kuteua msimamizi wa muda kwa lengo la kusimamia uendeshaji wa skimu ya bima ya afya, na itabainisha malipo ya usimamizi ambayo yatapaswa kulipwa na skimu ya bima ya afya; (e) kuzuia uendeshaji wa skimu ya bima ya afya lililopelekea hadi pale ambapo jambo kuwekewa zuio limetatuliwa; (f) kusitisha idhini yoyote inayokusudiwa kutolewa na Mamlaka; hatua kumuondoa (g) kuchukua au za kumsimamisha mtu yeyote katika nafasi ya uongozi wa skimu ya bima ya afya au kumzuia mtu huyo kushiriki katika shughuli za uendeshaji wa skimu ya bima ya afya; (h) kutoza faini kwa mujibu wa masharti ya Sheria na Kanuni hizi. (i) kusitisha usajili wa skimu ya bima ya afya; au (j) kuchukua hatua yoyote nyingine muhimu lolote la kurekebisha jambo lengo kwa linalohitaji kurekebishwa. (2) Mtu yeyote ambaye hajaridhika na amri au maelekezo ya Mamlaka chini ya kanuni hii, anaweza, 25 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote ndani ya siku thelathini, kukata rufaa kwa Baraza la Rufaa la Bima. Kufuta TS Na 359 ya 2004 - 48 Verify source ↗
Kanuni za Mfuko wa Afya ya Jamii za mwaka
AI-assisted research summary: The 2004 community health fund regulations are repealed.
48. Kanuni za Mfuko wa Afya ya Jamii za mwaka 2004 zinafutwa. 26 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote _________ JEDWALI __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 3(1)) JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA TANZANIA FOMU NA. 1 FOMU YA MAOMBI YA KUSAJILIWA KWA SKIMU YA BIMA YA AFYA SEHEMU A: TAARIFA ZA SKIMU YA BIMA YA AFYA
Part
SEHEMU YA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Bima ya Afya
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote za Mwaka 2024.
1. Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote za Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the regulations.
2. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Baraza la Rufaa la Bima” maana yake Baraza la Rufaa la Bima lililoanzishwa chini ya kifungu cha 126 cha Sheria ya Bima; “Sheria” maana yake Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote; “rejesta” maana yake rejesta inayotunzwa na Mamlaka kwa mujibu wa Sheria, ambamo kutahifadhiwa taarifa za skimu za bima za afya au wanachama wake waliosajiliwa na walio katika mfumo wa maandishi au kieletroniki; “Mamlaka” maana yake Mamlaka ya Usimamizi wa Bima iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bima; “mamlaka za utambuzi wa watu wasio na uwezo” maana yake ni Ofisi ya Taifa ya Takwimu iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Takwimu, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), na inajumuisha mamlaka nyingine yoyote yenye dhamana Nchini ya kusimamia programu inayohusika na utambuzi wa watu wasio na uwezo; “Msuluhishi” maana yake Msuluhishi wa Migogoro ya Bima anayerejelewa chini ya Sehemu ya Tisa ya Sheria ya Bima; na 4 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote “Mfuko” maana yake mfuko wa kugharamia watu wasio na uwezo ulioanzishwa chini ya Sheria. SEHEMU YA PILI USAJILI WA SKIMU ZA BIMA YA AFYA Maombi na vigezo vya usajili
Part
SEHEMU A: TAARIFA ZA SKIMU YA BIMA YA AFYA
- 1 Verify source ↗
Jina la skimu ya bima ya afya
AI-assisted research summary: This section is a form heading for the name of a health insurance scheme and related contact/location details.
1. Jina la skimu ya bima ya afya...................................................... (a) (b) (c) (d) (e) (f) (g) Halmashauri/ Manispaa................................... Wilaya……………………………………………… Mkoa.............................................................. Makao makuu ya skimu ya bima ya afya......................... Anuani ya skimu ya bima ya afya............................ Namba ya simu................................. Barua pepe..................................................................... (h) afya……………………………………… Mwaka fedha wa wa skimu ya bima ya - 2 Verify source ↗
Mtendaji Mkuu
AI-assisted research summary: This section asks for details about the Chief Executive, including name, address, phone number, email, nationality, and education.
2. Mtendaji Mkuu (a) Jina......................................................................... (b) Anuani.................................................................... (c) Namba ya simu................................................... (d) Barua pepe.......................................................... (e) Uraia..................................................................... (f) Elimu.................................................................... SEHEMU B: TAARIFA ZA UMILIKI NA WAMILIKI WA SKIMU YA BIMA YA AFYA - 1 Verify source ↗
Jina na mahali ilipo skimu ya bima ya afya
AI-assisted research summary: This section is a form-style heading asking for the name and location details of a health insurance scheme.
1. Jina na mahali ilipo skimu ya bima ya afya (i) (j) Jina la skimu ya bima ya afya...................................................... Halmashauri/ Manispaa................................... (k) Wilaya……………………………………………… (l) Mkoa.............................................................. (m) Makao makuu ya skimu ya bima ya afya......................... (n) (o) (p) Anuani ya skimu ya bima ya afya............................ Namba ya simu................................. Barua pepe..................................................................... (q) Mwaka afya……………………………………… fedha wa wa skimu ya bima ya - 2 Verify source ↗
Mtendaji Mkuu
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaorodhesha taarifa zinazohitajika kwa Mtendaji Mkuu, ikiwemo jina, anuani, namba ya simu, barua pepe, uraia, na elimu.
2. Mtendaji Mkuu (g) Jina......................................................................... 29 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote (h) Anuani.................................................................... (i) Namba ya simu................................................... (j) Barua pepe.......................................................... (k) Uraia..................................................................... (l) Elimu.................................................................... SEHEMU B: TAARIFA ZA UMILIKI NA WAMILIKI WA SKIMU YA BIMA YA AFYA
Part
SEHEMU B: TAARIFA ZA UMILIKI NA WAMILIKI WA SKIMU YA BIMA YA
- 1 Verify source ↗
Aina ya skimu ya afya (weka alama ya √)
AI-assisted research summary: This section is a choice between public and private health scheme options.
1. Aina ya skimu ya afya (weka alama ya √) 27 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote (a) (b) Umma Binafsi - 2 Verify source ↗
Wamiliki
AI-assisted research summary: This section lists the company and owner information to be provided.
2. Wamiliki (a) Taarifa za Kampuni [ ] i. ii. iii. iv. Jina la Kampuni............................................................. Mahala Ofisi kuu ilipo...................................................... Kiasi cha mtaji................................................................ Taarifa za wajumbe wa Bodi ya wakurungezi wa skimu ya bima ya afya…… v. Taarifa za wafanyakazi wa skimu ya bima ya afya……………………………….. vi. Idadi na maeneo ya ofisi za skimu ya bima ya afya ………………………………. vii. Taarifa za kibenki za skimu ya bima ya afya………………………………………… viii. Taarifa za mkaguzi wa nje wa skimu ya bima ya afya…………………………… ix. Taarifa za mshauri wa kisheria wa skimu ya bima ya afya………………………. x. Nakala zilizothibitishwa za vyeti za hisa kwa wanahisa………………………… xi. Majina ya wanazomiliki................................................ wanahisa pamoja na hisa (b) Taarifa binafsi [ ] (i) (ii) (iii) (iv) Jina la Mmiliki............................................................................ Anuani........................................................................................ Namba ya Simu....................................................................... Uraia.......................................................................................... - 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Section heading about the number of shares issued by the Health Insurance Scheme.
3. Idadi ya hisa zilizotolewa na Skimu ya Bima ya Afya……………………………………….. 28 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinahusu idadi na thamani ya hisa za Skimu ya Bima ya Afya zilizolipiwa.
4. Idadi na thamani ya hisa za Skimu ya Bima ya Afya zilizolipiwa………………………… - 5 Verify source ↗
Wawekezaji kwenye Skimu ya Bima ya Afya na idadi ya hisa
AI-assisted research summary: Fomu hii inahusu waombaji na skimu za bima ya afya, ikiwemo maelezo ya mwombaji, tarehe, jina, saini, wadhifa, na muhuri wa skimu.
5. Wawekezaji kwenye Skimu ya Bima ya Afya na idadi ya hisa zao………………………… Tamko la Mwombaji: Maelezo yaliyotolewa hapo juu ni ya kweli kwa kadri ya ufahamu wangu Tarehe………………………………mwezi……………………………. mwaka……………. Jina la mwombaji…………………………………………………………saini………… Wadhifa wake…………………………………………… Mhuri wa Skimu (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 7(3)) FOMU NA. 2 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA TANZANIA FOMU YA MAOMBI YA KUHUISHA USAJILI/CHETI KIPYA SEHEMU A: TAARIFA ZA SKIMU YA BIMA YA AFYA - 1 Verify source ↗
Aina ya skimu ya afya (weka alama ya √)
AI-assisted research summary: The form asks the user to mark the type of health scheme as public or private.
1. Aina ya skimu ya afya (weka alama ya √) (c) (d) Umma Binafsi - 2 Verify source ↗
Mmiliki/Wamiliki
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaorodhesha taarifa za mmiliki/wamiliki zinazohusiana na kampuni na taarifa binafsi zinazohitajika, ikiwemo maelezo ya bodi, wanahisa, wafanyakazi, ofisi, taarifa za benki, na maelezo ya FIU na wakaguzi/washauri.
2. Mmiliki/Wamiliki (c) Taarifa za Kampuni [ ] xii. Taarifa za wajumbe wa Bodi ya wakurungezi wa skimu ya bima xiii. Taarifa ikiwemo uraia………………………………………… wamiliki za uthibitisho wa xiv. Nakala zilizothibisha wanahisa…………………………… za vyeti vya hisa kwa xv. Uthibitisho wa mtaji wa skimu ya bima ya afya kwa skimu binafsi…..................... xvi. Jina la Wakurugenzi............................................................................. Mkurugenzi/ xvii. Majina ya wanahisa pamoja na hisa wanazomiliki................................................ xviii. Taarifa za wafanyakazi wa skimu ya bima ya afya……………………………….. xix. Idadi na maeneo skimu ya bima ya afya yenye ofisi………………………………. xx. Taarifa za kibenki za skimu ya bima ya afya………………………………………… 30 Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote xxi. Taarifa za mkaguzi wa nnje wa skimu ya bima ya afya……………………………………. xxii. Taarifa za mthamini ya skimu ya bima ya afya…………………………………… xxiii. Taarifa za mshauri wa kisheria wa skimu ya bima ya afya………………………. xxiv. Taarifa za madai ya skimu ambayo hayajalipwa mpaka Tarehe ya kuhuhisha usajili … xxv. Taarifa ya kutokuwa na pingamizi kutoka FIU kwa mtu aliyeteuliwa kuwasilisha taarifa FIU….. (d) Taarifa binafsi [ ] (v) (vi) Jina la Mmiliki............................................................................ Anuani........................................................................................ (vii) Namba ya Simu....................................................................... (viii) Uraia................................................................................... - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Inahusu idadi ya hisa zilizotolewa na Skimu ya Bima ya Afya na idadi pamoja na thamani ya hisa zilizolipiwa.
4. Idadi ya hisa zilizotolewa na Skimu ya Bima ya Afya……………………………………….. Idadi na thamani ya hisa za Skimu ya Bima ya Afya zilizolipiwa………………………… - 5 Verify source ↗
Wawekezaji kwenye Skimu ya Bima ya Afya na idadi ya hisa
AI-assisted research summary: Hii ni fomu ya kuandikisha taarifa za wawekezaji kwenye Skimu ya Bima ya Afya na idadi ya hisa zao; mwombaji anatakiwa kuwasilisha taarifa hizi zikitokea mabadiliko.
5. Wawekezaji kwenye Skimu ya Bima ya Afya na idadi ya hisa zao………………………… (Zingatia:Taarifa hizi zitawasilishwa endapo kuna mabadiliko yaliyojitokeza) Tamko la Mwombaji: Maelezo yaliyotolewa hapo juu ni ya kweli kwa kadri ya ufahamu wangu Tarehe………………………………mwezi……………………………. mwaka……………. Jina la mwombaji…………………………………………………………saini………… Wadhifa wake…………………………………………… Mhuri wa Skimu (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 12(1)) REJESTA YA SKIMU ZA BIMA YA AFYA FOMU NA. 3 NA Jina la Skimu na Namba ya Simu na Namba na tarehe ya Idadi ya wanacham 31 Taarifa za Taarifa za vituo Taarifa nyinginez Tangazo la Serikali Na. 809 (Linaendelea) Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote Anuani barua pepe usajili a na wanufaika waliyosaji liwa waajiri walioingi a mkataba na skimu o vilivyoin gia mkataba na skimu Dodoma, 11 septemba, 2024 JENISTA J. MHAGAMA Waziri wa Afya 32
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in