Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ya Mwaka 2024
This section states the short title of the bylaw.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the short title of the bylaw. This bylaw applies throughout the entire council area. This section defines key terms used in the by-law, including fee, Council, permit, construction minerals, Director, levy, and agent. Mtu, taasisi au kampuni inayotaka kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri lazima iwasilishe maombi ya kibali kwa Mkurugenzi kwa fomu maalum. Holders of a construction-minerals mining permit must pay the permit fee every year while mining continues, follow the bylaw and permit conditions, and pay other levies charged by the Council.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ya Mwaka 2024
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This section states the short title of the bylaw.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the entire council area.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including fee, Council, permit, construction minerals, Director, levy, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni malipo yanayolipwa na mtu yeyote kwa Halmashauri kwa ajili ya kupata kibali kinachotolewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi inayotolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “madini ya ujenzi” maana yake ni moramu, udongo, kifusi, kokoto, mawe, mchanga,tofali, chokaa na madini mengine yanayotumika katika ujenzi; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa shughuli zinazohusu ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri; na 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Tangazo la Serikali Na.814 (Linaendelea.) Maombi ya kibali “Wakala” maana yake mtu, taasisi, kikundi cha watu, kampuni au asasi iliyoteuliwa na Halmashauri kukusanya ushuru wa madini ya ujenzi kwa niaba yake. - 4 Verify source ↗
(1) Mtu, taasisi au kampuni inayokusudia
AI-assisted research summary: Mtu, taasisi au kampuni inayotaka kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri lazima iwasilishe maombi ya kibali kwa Mkurugenzi kwa fomu maalum.
4.-(1) Mtu, taasisi au kampuni inayokusudia kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri itatakiwa kuwasilisha kwa Mkurugenzi maombi ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi kupitia fomu maalum itakayotolewa na Halmashauri. (2) Maombi ya kibali yatatakiwa kuambatishwa na taarifa zifuatazo: (a) leseni ya uchimbaji wa madini iliyotolewa na mamlaka husika; (b) aina ya madini yanayokusudiwa kuchimbwa; (c) umiliki pamoja na ukubwa wa eneo linalokusudiwa kuchimbwa madini ya ujenzi; (d) mpango wa utunzaji wa mazingira katika eneo la machimbo; na (e) muhtasari wa kijiji ambacho uchimbaji wa madini ya ujenzi utafanyika kuonyesha kukubaliana na uchimbaji huo. (3) Mkurugenzi, ndani ya muda wa siku saba tangu kupokea maombi, atatakiwa kukagua eneo ambalo uchimbaji wa madini ya ujenzi unakusudiwa kufanyika ili kujiridhisha iwapo eneo hilo linafaa kwa shughuli za uchimbaji wa madini ya ujenzi. (4) Mkurugenzi, ndani ya muda wa siku saba tangu kukamilika kwa ukaguzi wa eneo linaloombewa kibali atatakiwa kukubali au kukataa maombi hayo na endapo atakataa atatakiwa kutoa sababu kwa maandishi za kukataa maombi hayo. Wajibu wa mpewa kibali - 5 Verify source ↗
Mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali cha
AI-assisted research summary: Holders of a construction-minerals mining permit must pay the permit fee every year while mining continues, follow the bylaw and permit conditions, and pay other levies charged by the Council.
5. Mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi atatakiwa: (a) kulipa ada ya kibali ambayo italipwa kila mwaka ambao shughuli ya uchimbaji wa madini ya ujenzi itakuwa ikifanyika; (b) kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii na masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Tangazo la Serikali Na.814 (Linaendelea.) ya ujenzi; na (c) kulipa ushuru tozo mbalimbali zitakazotozwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. na Muda wa uchimbaji na usafirishaji - 6 Verify source ↗
(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji,ununuzi na
AI-assisted research summary: Shughuli za uchimbaji, uuzaji, ununuzi na usafirishaji wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri zinapaswa kufanyika saa za mchana zilizotajwa, isipokuwa Mkurugenzi akitoa kibali maalum; pia magari yanayosafirisha madini hayo lazima yawe yamefunikwa wakati wote wa usafirishaji.
6.-(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji,ununuzi na usafirishaji wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri zitafanyika kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni ya kila siku. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), Mkurugenzi anaweza kutoa kibali maalum kuruhusu shughuli za uchimbaji, uuzaji,ununuzi na usafirisahji wa madini ya ujenzi kufanyika nje ya muda ulioainishwa katika kifungu kidogo cha (1). (3) Kila mmiliki wa gari linalosafirisha madini ya ujenzi atatakiwa kuhakikisha kuwa gari hilo limefunikwa wakati wote wa usafirishaji wa madini ya ujenzi. Ushuru wa madini ya ujenzi - 7 Verify source ↗
Kutakuwa na ushuru wa madini ya ujenzi
AI-assisted research summary: Ushuru wa madini ya ujenzi utalipwa na mnunuzi au msafirishaji wa madini hayo kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza.
7. Kutakuwa na ushuru wa madini ya ujenzi ambao utalipwa na mnunuzi au msafirishaji wa madini ya ujenzi kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. Vituo vya ukaguzi - 8 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa malipo
AI-assisted research summary: Vigari vinavyobeba madini ya ujenzi lazima visimame katika kituo cha ukaguzi na dereva aonyeshe stakabadhi ya kielektroniki ya kuthibitisha ushuru umelipwa.
8.-(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa malipo ya ushuru wa madini ya ujenzi katika njia zinazoingia au kutoka katika maeneo ya machimbo ya madini ya ujenzi. (2) Kila dereva wa gari au chombo chochote cha usafiri kinachobeba madini ya ujenzi atatakiwa kusimama katika kituo cha ukaguzi wa malipo ya ushuru wa madini ya ujenzi na kuonesha stakabadhi ya kielektroniki kuthibitisha kulipwa kwa ushuru wa madini ya ujenzi yaliyo katika gari au chombo cha usafiri anachoendesha. Matumizi ya stakabadhi ya kielektroniki - 9 Verify source ↗
Halmashauri au Wakala atatakiwa kutoza ada
AI-assisted research summary: Halmashauri au Wakala lazima kutoza ada au ushuru kwa kutumia mashine za kielektroniki.
9. Halmashauri au Wakala atatakiwa kutoza ada au ushuru kwa kadri itakavyokuwa kwa kutumia mashine za kielektroniki. Kufutwa au kusimamishwa kwa kibali - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kufuta au kusimamisha kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi ikiwa kuna ukiukwaji, lakini lazima itoe notisi ya siku saba kabla yake.
10.-(1) Halmashauri au kusimamisha kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi inaweza kufuta 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Tangazo la Serikali Na.814 (Linaendelea.) endapo itajiridhisha kuwa kuna ukiukwaji wa masharti ya Sheria Ndogo hizi au masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi. (2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (1), Halmashauri kabla ya kufuta au kusimamisha kibali itatakiwa kutoa notisi ya siku saba kwa mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali ya kusudio la kufuta au kusimamisha kibali. (3) Notisi itakayotolewa kwa mujibu wa kifungu itaainisha sababu za kufuta au kidogo cha kusimamisha kibali husika. (2) Uteuzi wa Wakala Makosa na adhabu (4) Endapo kibali kitafutwa au kusimamishwa, mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi itakoma kuchimba madini hayo. - 11 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kuteua mtu, kikundi cha
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua mtu, kikundi cha watu, taasisi au kampuni kukusanya ushuru kwa niaba yake.
11. Halmashauri inaweza kuteua mtu, kikundi cha watu, taasisi au kampuni kukusanya ushuru kwa niaba yake. - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayefanya shughuli za madini ya ujenzi bila kibali, bila kulipa ushuru, kwenye muda usioruhusiwa bila kibali maalum, au kwa gari lisilofunikwa anatenda kosa.
12. Mtu yeyote ambaye: (a) ataanzisha machimbo ya madini ya ujenzi bila kuwa na kibali kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hii; (b) atasafirisha madini ya ujenzi bila kulipa ushuru; (c) atachimba, atauzaji,atanunua au kusafirisha madini ya ujenzi kabla au baada ya muda ulioruhusiwa isipokuwa kama amepata kibali maalum cha Mkurugenzi cha kuruhusiwa ,kununua au kusafirisha kuchimba, kuuza madini ya ujenzi baada ya muda uliowekwa (d) atasafirisha madini ya ujenzi katika gari ambalo halijafunikwa; au (e) atamshawishi mtu au kundi la watu kutolipa ushuru; (f) anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki Mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kizichozidi miezi ishirini na nne au vyote. 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Tangazo la Serikali Na.814 (Linaendelea.) Kufililisha kosa - 13 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufililisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtenda kosa shilingi laki mbili ikiwa anakiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu maalum na kutimiza wajibu wake.
13. Mkurugenzi anaweza kufililisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi laki mbili iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kuwa tayari kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Kufutwa TS. Na. 209 la 2018 - 14 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya (Ada na Ushuru wa Madini
AI-assisted research summary: This section revokes the Kalambo District Council by-law on building materials and blocks, and it includes a form showing the Director may accept Tshs 200,000 for an admitted offence instead of court prosecution.
14. Sheria Ndogo ya (Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi) ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo inafutwa. 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Tangazo la Serikali Na.814 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA KWANZA ___________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 6) USHURU WA MADINI YA UJENZI NA TOFALI Na Aina ya Madini ya Ujenzi Kiwango 1 Mawe 2 Kokoto 3 Udongo/Tofali 4 Mchanga (a) (b) (c) (d) Tshs 5,000/=kwa kila tripu ya ujazo au uzito usiozidi tani tatu Tshs 8,000/= kwa kila tripu ya ujazo au uzito wa zaidi ya tani tatu na usiozidi tani nne Tshs 10,000/= kwa kila tripu ya ujazo au uzito wa zaidi ya tani nne na usiozidi tani saba Tshs 15,000/= kwa kila tripu ya ujazo inayozidi tani saba (a) Tshs 5,000/=kwa kila tripu ya ujazo au uzito usiozidi tani tatu (b) Tshs 10,000/= kwa kila tripu ya ujazo au uzito wa zaidi ya tani tatu na usiozidi tani nne (c) Tshs 15,000/= kwa kila tripu ya ujazo au uzito wa zaidi ya tani nne na usiozidi tani saba (d) Tshs 20,000/= kwa kila tripu ya ujazo inayozidi tani saba (a) Tshs 5,000/=kwa kila tripu ya ujazo au uzito usiozidi tani tatu (b) Tshs 8,000/= kwa kila tripu ya ujazo au uzito wa zaidi ya tani tatu na usiozidi tani nne (c) Tshs 10,000/= kwa kila tripu ya ujazo au uzito wa Zaidi ya tani nne na usiozidi tani saba (d) Tshs 10,000/= kwa kila tripu ya ujazo inayozidi tani saba (a) Tshs 5,000/=kwa kila tripu ya ujazo au uzito usiozidi tani tatu (b) Tshs 8,000/= kwa kila tripu ya ujazo au uzito wa zaidi ya tani tatu na usiozidi tani nne (c) Tshs 10,000/= kwa kila tripu ya ujazo au uzito wa zaidi ya tani nne na usiozidi tani saba (d) Tshs 15,000/= kwa kila tripu ya ujazo inayozidi tani saba 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Tangazo la Serikali Na.814 (Linaendelea.) _________ JEDWALI LA PILI ________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 12) FOMU YA KUFILILISHA KOSA Mimi …………………………………….……….. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya ………………………………………… ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, kwamba tarehe……ya mwezi …………….. mwaka …………. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Kifungu cha ……………………… cha Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya Kalambo ya Mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo nipo tayari kulipa kiasi cha shilingi laki mbili na kutimiza wajibu wangu kwa mujibu wa Sheria Ndogo hiyo badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo Tarehe…………………ya Mwezi…………………Mwaka……………………….. Jina………………………………….. Saini…………………………………. Mbele ya: Jina……………………………………….. Cheo……………………………………… Saini……………………………………… Tarehe …………………………………… 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Tangazo la Serikali Na.814 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo uliofanyika tarehe 4/11/2022 na kushuhudiwa lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- SHAFI K. MPENDA, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, Kalambo DAUDI NZELANI SECHOME, Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya, Kalambo NAKUBALI, L.S Dodoma, 19 Julai, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB.) Waziri wa Nchi-OR-TAMISEMI, 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in