Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za Mwaka 2024
This provision says these rules are to be called the Credit Provision and Management Regulations for Women, Youth, and Persons with Disabilities, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision says these rules are to be called the Credit Provision and Management Regulations for Women, Youth, and Persons with Disabilities, 2024. These rules apply within Tanzania Mainland local government authorities. This section defines terms used in the Regulations. Mamlaka ya Serikali za Mitaa lazima itenge asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Local authorities must use allocated funds to make loans to women, youth, and persons with disabilities, following set percentage allocations, and the loans must be interest-free.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za Mwaka 2024
Showing 41 of 41
- 1 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: This provision says these rules are to be called the Credit Provision and Management Regulations for Women, Youth, and Persons with Disabilities, 2024.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Matumizi
AI-assisted research summary: These rules apply within Tanzania Mainland local government authorities.
2. Kanuni hizi zitatumika katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara. - 3 Verify source ↗
Tafsiri
AI-assisted research summary: This section defines terms used in the Regulations.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “ajira rasmi” maana yake ni aina ya ajira inayozingatia sheria na taratibu za ajira katika sekta ya umma au sekta binafsi ambapo mfanyakazi huajiriwa kwa mujibu wa mkataba ambao unajumuisha taarifa za mshahara, posho maalumu, saa za kufanya kazi, likizo, haki na wajibu wa mwajiri na mwajiriwa, malipo ya kodi, mchango wa bima ya afya na pensheni; “Kamati ya Huduma za Mikopo” maana yake ni Kamati ya Huduma za Mikopo iliyoanzishwa chini ya Kanuni hizi; “Kamati ya Wilaya ya Uhakiki wa Mikopo” maana yake ni Kamati ya Uhakiki wa Mikopo iliyoanzishwa chini ya Kanuni hizi; “Kamati ya Kudumu ya Fedha, Uongozi na Mipango” maana yake ni Kamati ya Kudumu ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Mamlaka ya Wilaya; 3 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) “Kamati ya Kudumu ya Fedha na Utawala” maana yake ni Kamati ya Kudumu ya Fedha na Utawala ya Mamlaka za Miji; “kijana” maana yake ni mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45; “Mamlaka ya Serikali ya Mitaa” maana yake ni halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji; “mkopo” maana yake ni fedha taslimu, vifaa au fedha pamoja na vifaa vinavyotolewa na mamlaka za serikali za mitaa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa; Sura ya 342 “taasisi ya fedha” itakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha; na “Timu ya Menejimenti” maana yake ni Mkurugenzi na Wakuu wa divisheni na vitengo katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa. SEHEMU YA PILI UTENGAJI, UTOAJI NA UREJESHAJI WA MIKOPO Wajibu wa kutenga fedha Mgao wa fedha za mikopo
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Wajibu wa kutenga fedha
AI-assisted research summary: Mamlaka ya Serikali za Mitaa lazima itenge asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
4.-(1) Mamlaka ya Serikali za Mitaa itakuwa na wajibu wa kutenga asilimia kumi ya mapato yanayokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya ndani vya mapato kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. (2) Katika kutekeleza masharti ya kanuni ndogo ya (1), Mkurugenzi akiwa kama Afisa Masuuli atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa: (a) Mamlaka ya Serikali za Mitaa inatenga asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo; (b) mikopo inatolewa kwa kuzingatia masharti ya Kanuni hizi; na (c) vikundi vilivyokopeshwa vinarejesha mikopo kwa mujibu wa mkataba. - 5 Verify source ↗
Mgao wa fedha za mikopo
AI-assisted research summary: Local authorities must use allocated funds to make loans to women, youth, and persons with disabilities, following set percentage allocations, and the loans must be interest-free.
5.-(1) Mamlaka ya Serikali za Mitaa itatumia fedha zilizotengwa kwa mujibu wa kanuni ya 4 kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. 4 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) (2) Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ndogo ya (1), Mamlaka ya Serikali za Mitaa itatoa mikopo kwa kuzingatia mgawo ufuatao: (a) asilimia arobaini ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya wanawake; (b) asilimia arobaini ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya vijana; na (c) asilimia ishirini ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya watu wenye ulemavu. (3) Endapo fedha zilizotengwa kwa kundi mojawapo kati ya makundi yaliyoainishwa kwenye Kanuni ndogo ya (2), hazikutumika kutokana na kutokupokea maombi au kuwepo kwa fedha zilizobaki kwenye fungu husika, Mamlaka ya Serikali za Mitaa inaweza kutoa mkopo kwa kundi lingine lililoainishwa katika kifungu hiki kutoka katika asilimia iliyotengwa kwa ajili ya kundi jingine lenye mahitaji zaidi. (4) Mikopo itakayotolewa chini ya Kanuni hizi haitatozwa riba. Sifa za kupata mkopo - 6 Verify source ↗
Sifa za kupata mkopo
AI-assisted research summary: Vikundi vya wanawake, vijana au watu wenye ulemavu vinaweza kupata mkopo ikiwa vinatimiza masharti yaliyowekwa.
6.-(1)Bila kuathiri masharti ya Kanuni hizi, kikundi cha wanawake, vijana au watu wenye ulemavu kitakuwa na sifa ya kupata mkopo endapo: (a) wanakikundi wake ni raia wa Tanzania wenye akili timamu na umri usio chini ya miaka kumi na nane; (b) kimetambuliwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kupitia mfumo wa kieletroniki wa utoaji na usimamizi wa mikopo; (c) kinajishughulisha na ujasiriamali au za kinakusudia ujasiriamali mdogo au wa kati; kuanzisha shughuli (d) kwa kikundi cha wanawake au vijana, kina idadi ya wanakikundi wasiopungua watano na kwa kikundi cha watu wenye ulemavu, kina idadi ya wanakikundi wasiopungua wawili; kina akaunti ya benki iliyofunguliwa kwa jina la kikundi kwa ajili ya matumizi ya (e) 5 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) kikundi; (f) hakina wajumbe wenye ajira rasmi; na (g) kimepata mafunzo ya ujasiriamali. (2) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (1), kikundi kitahesabika kuwa kimepoteza sifa ya kupata mkopo endapo:- (a) kitapoteza moja wapo ya sifa zilizoainishwa katika kanuni ndogo ya (1); (b) hakijamaliza au kimeshindwa kurejesha mkopo uliotolewa chini ya Kanuni hizi; (c) kimetoa taarifa za uongo kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa lengo la kupata mkopo; (d) kimetumia fedha za mkopo kwa matumizi tofauti na yale yaliyoombewa mkopo bila ya idhini ya Timu ya Menejimenti. - 7 Verify source ↗
Mkopo kwa mtu mwenye ulemavu
AI-assisted research summary: A person with disability may qualify for a loan and be treated as a group member if the listed conditions are met.
7.-(1) Bila kujali masharti ya kanuni ya 6, mtu mwenye ulemavu atakuwa na sifa ya kupata mkopo na kuchukuliwa kuwa ni kikundi cha watu wenye ulemavu endapo: (a) timu ya menejimenti itajiridhisha kuwa mtu huyo amekosa mtu mwingine mwenye ulemavu na sifa ya kuwa mwanakikundi wa kikundi cha watu wenye ulemavu; (b) anajishughulisha anakusudia ujasiriamali mdogo au wa kati; kuanzisha na ujasiriamali shughuli au za (c) ana akaunti ya benki iliyofunguliwa kwa shughuli maalum za lake kwa jina kiujasiriamali; na (d) hana ajira rasmi. (2) Masharti mengine ya Kanuni hizi yatatumika kwa mtu mwenye ulemavu atakayepatiwa mkopo kwa mujibu wa masharti ya kanuni ya 6(1). kutoa - 8 Verify source ↗
Utaratibu wa uombaji wa mikopo
AI-assisted research summary: Local government authorities must announce available loan funds to the public and specified groups, and groups seeking loans must apply to the council through the electronic loan system.
8.-(1) Mamlaka ya Serikali za Mitaa itawajibika kwa tangazo madhumuni ya kuutarifu umma na vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuhusu kuwepo kwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya vikundi. umma kwa 6 Mkopo kwa mtu mwenye ulemavu Utaratibu wa uombaji wa mikopo Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) Utaratibu wa utoaji wa mikopo Matumizi ya fedha za mikopo (2) Kikundi kinachokusudia kuomba mkopo kitatuma maombi kwa Halmashauri kupitia mfumo wa kielektroniki wa utoaji na usimamizi wa mikopo. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2), maombi ya mkopo yatazingatia utaratibu uliobainishwa katika mwongozo wa utoaji na usimamizi wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika mamlaka ya serikali za mitaa. - 9 Verify source ↗
Utaratibu wa utoaji wa mikopo
AI-assisted research summary: Mamlaka ya Serikali za Mitaa lazima ichukue maombi ya mkopo ndani ya miezi miwili na itoe taarifa au kulipa mkopo ndani ya muda uliowekwa baada ya uamuzi.
9.-(1) Mamlaka ya Serikali za Mitaa itatakiwa kushughulikia maombi ya mikopo katika kipindi kisichozidi miezi miwili tangu tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ya mkopo. (2) Endapo maombi ya mkopo yamekubaliwa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa itatakiwa kukitaarifu kikundi kilichokubaliwa kupata mkopo ndani ya muda wa siku saba tangu uamuzi wa kukubali maombi kufikiwa. (3) Endapo maombi ya mkopo yatakataliwa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa itatakiwa kukitaarifu kikundi kuhusu kukataliwa kwa maombi hayo pamoja na sababu zake ndani ya muda wa siku saba tangu uamuzi ulipofikiwa. (4) Endapo maombi ya mkopo yataridhiwa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa itatakiwa kuingiza kiasi cha mkopo kilichoridhiwa katika akaunti ya kikundi husika baada ya kusaini Mkataba na kikundi. - 10 Verify source ↗
Matumizi ya fedha za mikopo
AI-assisted research summary: Fedha za mikopo zinapaswa kutumika kwa miradi iliyoidhinishwa; kikundi kinaweza kubadilisha mradi baada ya kuomba na kupata idhini ya Timu ya Menejimenti.
10.-(1) Fedha za mikopo zitakazotolewa chini ya Kanuni hizi zitatumika kwa miradi iliyoidhinishwa na Timu ya Menejimenti kwa kuzingatia ushauri na mapendekezo ya Kamati ya Huduma za Mikopo katika ngazi ya Halmashauri. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), mkopo utakaotolewa chini ya Kanuni hizi unaweza kutekeleza mradi wa mwanakikundi mmoja mmoja na kikundi kitabaki kuwa dhamana ya mkopo. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), kikundi kinaweza kubadilisha mradi baada ya kuomba na kupata idhini ya Timu ya Menejimenti. 7 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) Urejeshaji wa mikopo - 11 Verify source ↗
Urejeshaji wa mikopo
AI-assisted research summary: Kikundi kilichopata mkopo lazima kianze kurejesha mkopo baada ya miezi mitatu na kifanye marejesho kupitia mfumo wa malipo ya serikali.
11.-(1) Kikundi kilichopata mkopo chini ya Kanuni hizi kitatakiwa kuanza kurejesha mkopo baada ya miezi mitatu tangu siku ya kupata mkopo. (2) Marejesho ya mkopo yatafanyika kila mwezi kwa kuzingatia viwango vilivyokubaliwa kati ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa na kikundi kilichopata mkopo. (3) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (1) na (2), Mamlaka ya Serikali za Mitaa inaweza kuingia makubaliano na kikundi kilichopata mkopo kuhusu namna bora ya urejeshaji wa mkopo kulingana na aina ya mradi. (4) Kikundi kilichopata mkopo kitawajibika kuwasilisha marejesho ya mkopo kupitia mfumo wa malipo ya serikali. (5) Kikundi au mwanakikundi ataweka fedha zinazotokana na shughuli anayofanya iliyopatiwa mkopo kwenye akaunti ya benki iliyofunguliwa kila anapopokea mapato baada ya kutoa matumizi kwa ajili ya akiba na kulipa mkopo. (6) Mamlaka ya Serikali za Mitaa zitakusanya au kufuatilia urejeshaji wa mikopo kutoka kwa vikundi kulingana na makubaliano yaliyoainishwa katika mkataba uliosainiwa kati ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa na kikundi. Kuchelewesha marejesho ya mikopo - 12 Verify source ↗
Kuchelewesha marejesho ya mikopo
AI-assisted research summary: Ikiwa kikundi kinachelewesha marejesho ya mkopo, Mamlaka ya Serikali za Mitaa lazima itoe notisi ya siku saba na, ikiwa marejesho hayafanyiki baada ya siku hizo saba, iitie kikundi kwa ushauri na makubaliano ya kurejesha kiasi kisicholipwa.
12.-(1) Mkopo wenye tarehe maalum ya rejesho utachukuliwa kuwa umecheleweshwa wote ikiwa sehemu ya rejesho au malipo yanayodaiwa kimkataba hayajalipwa. (2) Mikopo inayorejeshwa awamu itachukuliwa kuwa yote imecheleweshwa ikiwa awamu yoyote inayotakiwa kurejeshwa imecheleweshwa kwa siku moja au zaidi. kwa (3) Mkopo wa kikundi utachukuliwa kuwa wote ambapo mwanakikundi kinachotakiwa umecheleweshwa ameshindwa kurejeshwa hakijarejeshwa na wanakikundi. pale kurejesha kiasi na (4) Endapo kikundi kitachelewesha marejesho kwa mujibu wa mkataba, Mamlaka ya Serikali za Mitaa itatoa notisi ya siku saba kukitaka kikundi kufanya marejesho. 8 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) Kushindwa kurejesha mkopo Nyongeza ya muda wa kurejesha mkopo (5) Endapo baada ya muda wa siku saba kikundi kitashindwa kafanya marejesho, Mamlaka ya Serikali za Mitaa itakiita kikundi kilichochelewesha marejesho kwa ajili ya ushauri na kuingia makubaliano ya namna ya kurejesha kiasi ambacho hakijalipwa.
Part
sehemu ya rejesho au malipo yanayodaiwa kimkataba
- 13 Verify source ↗
Kushindwa kurejesha mkopo
AI-assisted research summary: Kikundi kikishindwa kurejesha mkopo kwa masharti yaliyokubaliwa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa lazima itoe notisi ya siku 30 ya kuomba urejeshaji. Baada ya muda wa nyongeza kukipita bila kulipa, lazima pia itoe notisi ya kusudio la kufungua shauri mahakamani dhidi ya wanakikundi.
13.-(1) Endapo kikundi kilichopata mkopo kitashindwa kurejesha mkopo kwa mujibu wa makubaliano, mkataba au muda uliopangwa chini ya kanuni ya 12(5), Mamlaka ya Serikali za Mitaa itakipa kikundi hicho notisi ya siku thelathini ya kukitaka kurejesha mkopo unaopaswa kulipwa. (2) Endapo kikundi kitashindwa kurejesha mkopo baada ya muda wa nyongeza, Mamlaka ya Serikali za Mitaa itatoa notisi kwa kikundi hicho kuhusu kusudio la kufungua shauri mahakamani dhidi ya wanakikundi. - 14 Verify source ↗
Nyongeza ya muda wa kurejesha mkopo
AI-assisted research summary: Kikundi kilichopata mkopo kinaweza kuomba kuongezewa muda wa kurejesha mkopo kwa Mkurugenzi.
14. Bila kuathiri masharti ya muda wa kurejesha mkopo ulioainishwa kwenye Kanuni hizi, kikundi kilichopata mkopo kinaweza kuongezewa muda wa kurejesha mkopo huo kwa kuwasilisha maombi maalum kwa Mkurugenzi yakiainisha sababu za kushindwa kurejesha mkopo kwa wakati na mpango uliopo wa kurejesha mkopo katika muda wa nyongeza. SEHEMU YA TATU USIMAMIZI WA MIKOPO Majukumu ya Mkurugenzi
Part
SEHEMU YA TATU
- 15 Verify source ↗
Majukumu ya Mkurugenzi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa lazima atekeleze majukumu ya kusimamia mikopo ya vikundi, kuwasilisha taarifa na mapendekezo, kuchukua hatua kwa ukiukaji, na kuwezesha usimamizi na mafunzo.
15. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa atakuwa na wajibu wa kutekeleza majukumu yafuatayo: (a) kusimamia urejeshaji wa mikopo ya vikundi kwa wakati; (b) kuwasilisha mapendekezo ya maombi ya mikopo ya vikundi kwenye kamati ya wilaya ya uhakiki wa mikopo; (c) kuchukua hatua stahiki kwa vikundi vinavyokiuka masharti ya Kanuni hizi; (d) kuwasilisha taarifa za utoaji na usimamizi 9 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) wa mikopo kwa kila robo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa; (e) kusimamia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi; (f) kuwezesha na kusimamia utendaji kazi wa kamati za huduma za mikopo ya vikundi ngazi ya kata na halmashauri; na (g) kuwezesha mafunzo kwa wasimamizi, kamati na vikundi. Majukumu ya Afisa Maendeleo ya Jamii - 16 Verify source ↗
Majukumu ya Afisa Maendeleo ya Jamii
AI-assisted research summary: Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa lazima awatambue, awaratibu, na awasaidie vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, pamoja na kusimamia na kuripoti mikopo yao.
16.-(1) Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa atakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kutambua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu; ya (b) kuratibu mikopo vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu; (c) kupokea ya yaliyowasilishwa na vikundi; maombi mikopo vikundi (d) kusimamia uhai na kulinda maslahi ya vikundi na kuvijengea uwezo katika kufanikisha shughuli za uchumi; (e) kufuatilia marejesho ya mikopo; (f) kuhakikisha mikopo inayotolewa inatumika kama ilivyokusudiwa; (g) kuandaa na kuwasilisha taarifa ya mikopo iliyotolewa kwa Kamati ya Huduma za Mikopo; (h) kuandaa taarifa ya kila robo mwaka na kuiwasilisha kwenye vikao vya kisheria vya Mamlaka ya Serikali ya Mitaa; (i) kuwa kiungo kati ya vikundi na Kamati ya Huduma za Mikopo; (j) kutunza kumbukumbu za mikataba, mikopo na marejesho ya vikundi vilivyopewa mikopo; (k) kuhamasisha uanzishaji wa vikundi kwa kuzingatia fursa zilizopo katika maeneo husika; na (l) kushirikiana na afisa biashara katika kuunganisha vikundi na taasisi zenye fursa 10 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) mbalimbali za kiuchumi. (2) Katika kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika kanuni ndogo ya (1), Afisa Maendeleo ya Jamii atatakiwa kushirikiana na wataalamu wa sekta nyingine wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Majukumu ya Afisa Biashara - 17 Verify source ↗
Majukumu ya Afisa Biashara
AI-assisted research summary: Afisa Biashara wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa ana majukumu ya kushirikiana, kuunganisha na kuwezesha vikundi vya biashara na uzalishaji, pamoja na kutafuta masoko na kuhimiza vikundi kujirasimisha kibiashara.
17. Afisa Biashara wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa atakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kushirikiana na wajumbe wengine wa Kamati ya Huduma za Mikopo kuhakikisha vikundi vinavyoibuliwa vinawezeshwa kutumia fursa za kibiashara zilizopo ndani na nje ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa; (b) kuunganisha vikundi na sekta mbalimbali za uzalishaji; (c) kuviwezesha vikundi vinavyojihusisha na uzalishaji wa bidhaa kupata alama za ubora wa biashara; (d) kushirikiana na Afisa Maendeleo ya Jamii katika kuunganisha vikundi na taasisi zenye fursa; (e) kushirikiana na wataalamu wa sekta nyingine kutafuta masoko ya ndani na nje ya Halmashauri kwa bidhaa zinazozalishwa na vikundi; na (f) kuhamasisha vikundi kujirasimisha kibiashara ili kuongeza wigo wa fursa ya soko la bidhaa wanazozalisha. Wajibu wa Mweka Hazina - 18 Verify source ↗
Wajibu wa Mweka Hazina
AI-assisted research summary: The Treasurer of a Local Government Authority must make payments and account for group loan funds.
18. Mweka Hazina wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa atakuwa na wajibu wa kufanya malipo na kuhasibu fedha za mikopo ya vikundi. Wajibu wa Mkaguzi wa Ndani Kamati ya huduma za - 19 Verify source ↗
Wajibu wa Mkaguzi wa Ndani
AI-assisted research summary: The Internal Auditor of a local government authority must audit the funds set aside for group loans, group projects, loan repayment, and loan management every quarter.
19. Mkaguzi wa Ndani wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa atakuwa na wajibu chini ya Kanuni hizi wa kukagua fedha zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya vikundi, miradi ya vikundi, urejeshaji na usimamizi wa mikopo kila robo mwaka. - 20 Verify source ↗
Kamati ya huduma za mikopo ngazi ya kata
AI-assisted research summary: Kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa lazima iwe na Kamati ya Huduma za Mikopo ngazi ya Kata.
20. Kutakuwa na Kamati ya Huduma za Mikopo 11 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) mikopo ngazi ya kata ngazi ya Kata katika kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa itakayokuwa na wajumbe wafuatao: (a) Mtendaji wa Kata Mwenyekiti wa Kamati; ambaye atakuwa (b) Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ambaye atakuwa Katibu wa Kamati; (c) Afisa Ustawi wa Jamii Kata; (d) Maafisa Ugani wa Kata; (e) Afisa Elimu Kata; (f) Polisi Kata; na (g) Watendaji wa vijiji au mtaa. Majukumu ya Kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya Kata - 21 Verify source ↗
Majukumu ya Kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya Kata
AI-assisted research summary: Kamati ya Huduma ya Mikopo lazima ipokee, ijadili, ichambue, ifuatilie, na iwasilishe taarifa kuhusu maombi ya mikopo na marejesho.
21. Kamati ya Huduma ya Mikopo itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kupokea, kujadili na kuchambua maombi ya mikopo yaliyopokelewa; (b) kufanya tathmini ya awali ya maombi yaliyowasilishwa, kutembelea, kuhakiki na kushauri vilivyoomba mikopo ; vikundi kuhusu (c) kuwasilisha taarifa ya maombi ya mikopo kwa Kamati ya Huduma za Mikopo ngazi ya Halmashauri; (d) kufanya ufuatiliaji wa marejesho kwa vikundi vilivyopewa mikopo; (e) kufanya ufuatiliaji wa vikundi kuona maendeleo ya shughuli zao; (f) kushirikisha wadau kutoa mafunzo kwa vikundi; na (g) kuwasilisha taarifa ya mikopo kwa Kamati ya Maendeleo ya Kata. Kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya Halmashauri - 22 Verify source ↗
Kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya Halmashauri
AI-assisted research summary: Kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa ina Kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya Halmashauri, na kamati inaweza kumwalika mtaalamu kusaidia, lakini mtaalamu huyo hana haki ya kupiga kura.
22.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya Halmashauri katika kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa itakayokuwa na wajumbe wafuatao: (a) Mkuu wa Divisheni au Kitengo atakayeteuliwa na Mkurugenzi ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati; (b) Mweka Hazina; (c) Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu; 12 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) (d) Afisa Ushirika; (e) Afisa Ustawi wa Jamii; (f) Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii ambaye atakuwa Katibu wa Kamati. (g) Mratibu wa Mikopo; (h) Afisa Biashara; na (i) Afisa Vijana. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Kamati inaweza kumwalika mtaalamu yeyote kuisaidia Kamati, isipokuwa mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura. Majukumu ya Kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya Halmashauri - 23 Verify source ↗
Majukumu ya Kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya
AI-assisted research summary: Kamati ya Huduma ya Mikopo ya ngazi ya halmashauri lazima ishughulikie maombi ya mikopo, itoe mapendekezo, ifuatilie vikundi na marejesho, na kuwasilisha taarifa kwa menejimenti.
23. Kamati ya Huduma ya Mikopo n g a z i y a H a l m s h a u r i itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kupokea na kujadili taarifa ya uchambuzi wa vikundi vilivyoomba mikopo kutoka katika kamati ya huduma ya mikopo ya kata; (b) kufanya maombi yaliyowasilishwa na kutoa mapendekezo ya kutoa mikopo kwa vikundi na waombaji waliokidhi vigezo; tathmini ya (c) kuandaa taarifa ya maombi ya vikundi na mapendekezo ya kupewa au kutopewa mikopo na kuwasilisha kwenye timu ya menejimenti ya halmashauri; (d) kuhakikisha kuwa wanufaika wa mikopo wanapata taarifa kuhusu kufunguliwa kwa dirisha la mikopo kwa wakati; za kiuchumi, (e) kuratibu mafunzo ya uendeshaji wa na shughuli usimamizi wa fedha kwa vikundi; ufuatiliaji vikundi shughuli vilivyopewa mikopo zinazotekelezwa na kutoa ushauri wa kitaalamu pale inapohitajika; kwa kuona (f) kufanya biashara (g) kufuatilia marejesho ya mikopo na kutoa ushauri katika eneo la urejeshaji na utunzaji wa kumbukumbu za mikopo; (h) kuibua na kujadili fursa zilizopo ndani ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ili ziweze kutumiwa katika kuhamasisha uanzishaji 13 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) wa vikundi kwa ajili ya kupata mikopo; na (i) kutekeleza suala linalohusu utekelezaji wa Kanuni hizi kwa kadri itakavyoelekezwa na Timu ya Menejimenti. lolote Kamati ya Wilaya ya Uhakiki wa Mikopo Majukumu ya Kamati ya Wilaya ya Uhakiki wa Mikopo - 24 Verify source ↗
Kamati ya Wilaya ya Uhakiki wa Mikopo
AI-assisted research summary: Kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa lazima iwe na Kamati ya Uhakiki.
24. Kutakuwa na Kamati ya Uhakiki kwa kila Mamlaka za Serikali za Mitaa ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao: (a) Katibu Tawala Wilaya ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati; (b) mjumbe mmoja kutoka Ofisi ya Usalama ya Wilaya; (c) mjumbe mmoja kutoka Ofisi ya TAKUKURU Wilaya; (d) mjumbe mmoja kutoka Kamati ya Uratibu wa Mikopo ngazi ya Mkoa; na (e) Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambaye atakuwa Katibu wa Kamati. - 25 Verify source ↗
Majukumu ya Kamati ya Wilaya ya Uhakiki wa Mikopo
AI-assisted research summary: Kamati ya uhakiki lazima ipokee na ijadili mapendekezo ya vikundi vya mkopo, kisha iishauri timu ya menejimenti kuhusu vikundi vinavyopendekezwa kupewa mkopo.
25. Kamati ya uhakiki itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kupokea na kujadili taarifa ya mapendekezo ya vikundi vilivyowasilisha maombi ya mkopo kutoka timu ya menejimenti; na (b) kutoa ushauri kwa timu ya menejimenti kuhusu vikundi vilivyopendekezwa kupewa mkopo. Majukumu ya Timu ya Menejimenti - 26 Verify source ↗
Majukumu ya Timu ya Menejimenti
AI-assisted research summary: Timu ya Menejimenti lazima ishughulikie maombi ya mikopo kwa kufanya mapokezi, uchambuzi, uwasilishaji, uhakiki, uidhinishaji, ufuatiliaji wa marejesho, na utoaji wa taarifa kwa mamlaka husika.
26. Katika kushughulikia maombi ya mikopo inayotolewa chini ya Kanuni hizi, Timu ya Menejimenti itakuwa na majukumu yafuatayo: (b) kuwasilisha (a) kupokea na kujadili mapendekezo ya mikopo kutoka Kamati ya Huduma ya Mikopo ya Halmashauri; orodha vikundi vilivyopendekezwa kupewa mikopo kwa Kamati ya Wilaya ya Uhakiki wa Mikopo; (c) kupokea taarifa ya uhakiki wa mikopo kutoka Kamati ya Wilaya ya Uhakiki wa Mikopo; ya (d) kuidhinisha mikopo kwa vikundi 14 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) vilivyokidhi vigezo baada ya kuhakikiwa na kamati ya wilaya ya uhakiki; (e) kufuatilia marejesho ya mikopo; (f) kupokea taarifa za hali ya utoaji na urejeshaji wa mikopo kutoka Kamati ya Huduma ya Mikopo ya Halmashauri; ya orodha (g) kuwasilisha vikundi vilivyopendekezwa kupewa mikopo kwa Kamati ya Wilaya ya Uhakiki wa Mikopo; (h) kujadili na kuwasilisha taarifa ya robo mwaka ya utekelezaji wa Kanuni hizi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Majukumu ya Kamati ya Kudumu ya Fedha, Uongozi na Mipango na kamati ya kudumu ya fedha na utawala - 27 Verify source ↗
Majukumu ya Kamati ya Kudumu ya Fedha, Uongozi na Mipango
AI-assisted research summary: Kamati husika za fedha, uongozi na mipango lazima zipokee taarifa za fedha zilizotengwa na kutolewa kwenye vikundi, na zikague miradi ya vikundi vilivyopata mikopo.
27. Kamati ya Kudumu ya Fedha, Uongozi na Mipango katika mamlaka ya wilaya na Kamati ya Kudumu ya Fedha na utawala katika mamlaka za miji zitakuwa majukumu yafuatayo: (a) kupokea taarifa ya fedha zilizotengwa na kutolewa kwenye vikundi; (b) kukagua miradi ya vikundi vilivyopata mikopo kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa ukaguzi wa miradi ndani ya eneo la Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Majukumu ya Baraza la Madiwani Wajibu wa Kamati ya Bajeti ya Halmashauri - 28 Verify source ↗
Majukumu ya Baraza la Madiwani
AI-assisted research summary: Baraza la Madiwani lazima lipokee taarifa ya mikopo.
28. Baraza la Madiwani litakuwa na jukumu la kupokea taarifa ya mikopo. - 29 Verify source ↗
Wajibu wa Kamati ya Bajeti ya Halmashauri
AI-assisted research summary: Kamati ya Bajeti ya Halmashauri lazima itenge asilimia 10 ya mapato ya ndani yasiyolindwa kwa mikopo ya vikundi na ichunguze utekelezaji wa bajeti hiyo.
29. Kutakuwa na Kamati ya Bajeti ya Halmashauri itakayokuwa na majukumu yafuatayo: (a) kutenga bajeti ya asilimia kumi ya mapato ya ndani yasiyolindwa kwa ajili ya mikopo ya vikundi; (b) kutenga fedha ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ya yasiyolindwa kwa ajili ya mikopo ya vikundi; na (c) kutathmini utekelezaji wa bajeti ya asilimia kumi. Kamati ya uratibu wa Mikopo ngazi ya Mkoa - 30 Verify source ↗
Kamati ya uratibu wa Mikopo ngazi ya Mkoa
AI-assisted research summary: A Regional Credit Coordination Committee must exist, with specified members and a chairperson and secretary.
30. Kutakuwa na Kamati ya Uratibu wa Mikopo ngazi ya Mkoa itakayokuwa na wajumbe wafuatao: (a) Mkuu wa Sehemu au Kitengo ambaye 15 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) atateuliwa na Katibu Tawala wa Mkoa na atakuwa Mwenyekiti wa Kamati; (b) Katibu tawala msaidizi sehemu ya mipango na uratibu ambaye atakuwa Katibu wa Kamati; (c) Katibu tawala msaidizi sehemu ya Majukumu ya kamati ya uratibu wa mikopo ngazi ya mkoa menejimenti, ufuatiliaji na ukaguzi; (d) Afisa Maendeleo ya Jamii anayeratibu mikopo; (e) Afisa kutoka sehemu ya uchumi na uzalishaji; (f) Afisa kutoka sehemu ya viwanda, biashara na uwekezaji; (g) Afisa Ustawi wa Jamii; na (h) Afisa Usimamizi wa Fedha. - 31 Verify source ↗
Majukumu ya kamati ya uratibu wa mikopo ngazi ya mkoa
AI-assisted research summary: Kamati ya uratibu wa mikopo ngazi ya mkoa lazima isimamie, iratibu na itoe taarifa kuhusu mikopo ya vikundi, pamoja na kushauri na kufuatilia utekelezaji.
31. Kamati ya uratibu wa mikopo ngazi ya mkoa itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuhakikisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa zinatenga asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo kwa vikundi; (b) kusimamia utoaji wa mafunzo katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa; (c) kuchambua na kuandaa taarifa ya utoaji, usimamizi na urejeshaji wa mikopo ngazi ya mkoa; (d) kutoa taarifa ya utoaji na urejeshaji wa mikopo kwa Katibu Tawala wa Mkoa; (e) kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa kuchukua hatua stahiki kwa halmashauri zisizozingatia sheria, kanuni na taratibu za mikopo; (f) kuhakikisha kuwa halmashauri zinasimamia uundaji wa vikundi kulingana na fursa za kiuchumi zilizopo katika maeneo yao; (g) kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa kufanya tathmini kabla na baada ya kikao cha utekelezaji wa utoaji na urejeshaji wa mikopo shughuli za vikundi pale pamoja na inapohitajika na kuwasilisha taarifa kwa Wizara; 16 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) (h) kufuatilia utekelezaji wa miradi ya vikundi vilivyoanzishwa kutokana na mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kubaini mafanikio na changamoto na kutoa ushauri; na (i) kutekeleza majukumu mengine yanayohusu utoaji, usimamizi na urejeshaji wa mikopo. Kitengo cha uratibu wa utoaji na usimamizi wa mikopo ya vikundi - 32 Verify source ↗
Kitengo cha uratibu wa utoaji na usimamizi wa mikopo ya vikundi
AI-assisted research summary: Section hii inaweka Kitengo cha Uratibu wa Utoaji na Usimamizi wa Mikopo ya Vikundi na kukipa majukumu ya kuratibu, kusimamia, kufuatilia, kuchambua taarifa, kujenga uwezo, na kushauri kuhusu mikopo ya vikundi.
32.-(1) Katika kusimamia utekelezaji wa Kanuni hizi, kutakuwa na Kitengo cha Uratibu wa Utoaji na Usimamizi wa Mikopo ya Vikundi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Kitengo cha Uratibu wa Utoaji na Usimamizi wa Mikopo ya Vikundi kitakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuandaa na kusimamia mifumo ya uendeshaji na utoaji wa mikopo ya vikundi ; (b) kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya Serikali na Taasisi za Fedha kuhusu utoaji, usimamizi na urejeshaji wa mikopo; (c) kufanya ufuatiliaji na kuhakikisha Ofisi za Wakuu wa Mikoa zinatekeleza majukumu ya uratibu na usimamizi wa shughuli za mikopo; (d) kupokea taarifa, kuzichambua na kushauri juu ya utekelezaji wa utoaji na urejeshaji wa mikopo; (e) kufanya ufuatiliaji shirikishi wa utengaji, utoaji na urejeshaji wa mikopo kwa mujibu wa kanuni hizi; (f) kuandaa n a kufanya mapitio ya sheria, kanuni na miongozo inayohusu utoaji na urejeshaji wa mikopo; (g) kujenga uwezo wa wasimamizi wa mikopo katika ngazi za mikoa na halmashauri; (h) kuhakikisha mamlaka za serikali za mitaa zinatenga fedha za mikopo kwa mujibu wa Sheria; (i) kuratibu vikao vya tathmini ya utoaji na kadri urejeshaji wa mikopo itakavyohitajika; kwa 17 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) (j) kutekeleza majukumu mengine yanayohusiana na mikopo kwa vikundi; (k) kufanya utafiti na uchambuzi wa shughuli za utoaji wa mikopo ya vikundi; na (l) kushauri masuala ya kisera kuhusu shughuli za utoaji wa mikopo ya vikundi. 18 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) SEHEMU YA NNE UTOAJI WA MIKOPO KWA UTARATIBU WA TAASISI ZA FEDHA Utoaji wa Mikopo kwa utaratibu wa taasisi za fedha Ufuatiliaji na Ukusanyaji wa Marejesho Majukumu ya pande zote
Part
SEHEMU YA NNE
- 33 Verify source ↗
Utoaji wa Mikopo kwa utaratibu wa taasisi za fedha
AI-assisted research summary: A local government authority may provide loans through financial institutions, but if it uses that method it must first sign a contract with the financial institution, and the institution must lend only after analyzing the submitted groups.
33.-(1) Mamlaka ya Serikali za Mitaa inaweza kutoa mikopo kwa utaratibu wa kutumia taasisi za fedha. (2) Endapo Mamlaka ya Serikali za Mitaa itatumia utaratibu wa kutoa mikopo wa kutumia taasisi za fedha, itatakiwa kuingia makubaliano ya kimkataba na taasisi za fedha kabla ya kuanza mchakato wa utoaji wa mikopo. (3) Mkataba utabainisha masharti na vigezo vya utoaji wa mikopo, majukumu na haki za pande zote, na utaratibu wa utekelezaji na usimamizi wa mikopo hiyo. (4) Taasisi ya fedha itatoa mikopo baada ya kufanya uchambuzi wa vikundi vilivyowasilishwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa. - 34 Verify source ↗
Ufuatiliaji na ukusanyaji wa marejesho
AI-assisted research summary: Taasisi za fedha lazima zifuatilie na kukusanya marejesho kulingana na mkataba; kikundi kilichopokea mkopo lazima kirejeshe mkopo kwa wakati na kwa kiwango kilichokubaliwa.
34.-(1) Taasisi za fedha zitakuwa na jukumu la msingi la kufuatilia na kukusanya marejesho kwa mujibu wa masharti yaliyoainishwa katika mkataba uliosainiwa kati ya taasisi za fedha na kikundi husika ambacho kimepokea mkopo. (2) Kila kikundi husika kinachopokea mkopo kitawajibika kurejesha mkopo kwa wakati na kwa kiwango kilichokubaliwa kama ilivyoainishwa katika mkataba. (3) Utaratibu wa ukusanyaji wa marejesho utabainishwa katika mkataba, ukiwa na vipengele vya kushughulikia ucheleweshaji na kutokurejesha mikopo. - 35 Verify source ↗
Majukumu ya pande zote
AI-assisted research summary: Mamlaka ya Serikali za Mitaa na taasisi za fedha zinapaswa kushirikiana katika utekelezaji wa utoaji wa mikopo, na taasisi za fedha zitoe taarifa za mara kwa mara kuhusu hali ya mikopo.
35.-(1) Mamlaka ya Serikali za Mitaa na taasisi za fedha zinapaswa kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa utoaji wa mikopo. (2) Mamlaka ya Serikali za Mitaa itakuwa na jukumu la kutoa ushirikiano kwa taasisi za fedha katika ufuatiliaji wa mikopo. (3) Taasisi za fedha zinapaswa kutoa taarifa za mara kwa mara kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuhusu hali ya mikopo iliyotolewa, ikijumuisha taarifa za marejesho na changamoto zinazojitokeza. 19 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) Tathmini na uboreshaji - 36 Verify source ↗
Tathmini na uboreshaji
AI-assisted research summary: Mamlaka ya Serikali za Mitaa na taasisi za fedha lazima zifanye tathmini za mara kwa mara za utekelezaji wa utoaji wa mikopo, na mapendekezo ya maboresho yazingatiwe na kutekelezwa kwa wakati.
36.-(1) Mamlaka ya Serikali za Mitaa na taasisi za fedha zitafanya tathmini ya mara kwa mara ya utekelezaji wa utoaji wa mikopo kubaini mafanikio na changamoto zinazojitokeza. (2) Mapendekezo ya maboresho yatapaswa kuzingatiwa na kutekelezwa kwa wakati kuhakikisha ufanisi na tija katika utoaji wa mikopo. Akaunti Maalum ya Mikopo Mafunzo na ufuatiliaji wa mikopo ya vikundi SEHEMU YA TANO MASHARTI YA JUMLA
Part
SEHEMU YA TANO
- 37 Verify source ↗
Akaunti Maalum ya Mikopo
AI-assisted research summary: Mamlaka ya Serikali za Mitaa lazima ifungue na kuendesha Akaunti Maalum ya Mikopo katika benki inayotoa huduma ndani ya eneo lake, na Mkurugenzi lazima ahakikishe fedha za mikopo na marejesho zinawekwa humo.
37.-(1) Kwa kuzingatia sheria na taratibu za usimamizi wa fedha za umma, kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa itatakiwa kufungua na kuendesha Akaunti Maalum ya Mikopo itakayofunguliwa katika mojawapo ya benki zinazotoa huduma katika eneo la Mamlaka ya Serikali za Mitaa. (2) Mkurugenzi atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya mikopo inayotolewa chini ya Kanuni hizi na fedha za marejesho ya mikopo hiyo zinahifadhiwa katika Akaunti Maalum ya Mikopo. - 38 Verify source ↗
Mafunzo na ufuatiliaji wa mikopo ya vikundi
AI-assisted research summary: Local government authorities must train borrower groups, monitor loans and group progress, and set aside specified percentages of loan funds each year.
38.-(1) Mamlaka ya serikali za mitaa itakuwa na wajibu wa- (a) kutoa mafunzo kwa vikundi vinavyotarajiwa na vilivyokubaliwa kupata mkopo ikiwemo masuala ya uwekaji wa akiba, uundaji wa vikundi vyenye tija, uongozi, usimamizi wa fedha, uendeshaji wa miradi na utoaji wa taarifa miradi inayotekelezwa na mkopo husika; na zinazohusu hususan (b) kufanya ufuatiliaji wa mikopo na tathmini ya maendeleo ya vikundi vilivyopata mikopo. (2) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa masharti ya kanuni ndogo ya (1), mamlaka ya serikali za mitaa itatenga fedha kutoka katika fedha za mikopo kwa uwiano ufuatao: (a) halmashauri inayochangia asilimia 70 ya mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo itatenga asilimia 5 ya fedha zinazotarajiwa kutolewa kwa ajili ya mikopo kwa mwaka husika; 20 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) (b) halmashauri inayochangia asilimia 60 ya mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo itatenga asilimia 10 ya fedha zinazotarajiwa kutolewa kwa ajili ya mikopo kwa mwaka husika; (c) halmashauri inayochangia asilimia 40 ya mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo itatenga asilimia 15 ya fedha zinazotarajiwa kutolewa kwa ajili ya mikopo kwa mwaka husika; na (d) halmashauri inayochangia asilimia 20 ya mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo itatenga asilimia 20 ya fedha zinazotarajiwa kutolewa kwa ajili ya mikopo kwa mwaka husika. Kuhitimu ukopaji Makosa na adhabu - 39 Verify source ↗
Akaunti Maalum ya Mikopo
AI-assisted research summary: Vikundi vinafikia hatua ya kuhitimu kunufaika na mikopo baada ya tathmini kuonyesha vinaweza kujisimamia na kujiendesha kibiashara.
39.-(1) Kwa mujibu wa anuni hizi vikundi vitafikia hatua ya kuhitimu kunufaika na mikopo, baada ya taarifa ya tathmini kubaini uwezo wa kikundi kujisimamia na kujiendesha kibiashara. (2) Taratibu za kuhitimisha vikundi zitafafanuliwa kwenye mwongozo wa utoaji na usimamizi wa mikopo. - 40 Verify source ↗
Mafunzo na ufuatiliaji wa mikopo ya vikundi
AI-assisted research summary: Kikundi au mtu yeyote haruhusiwi kutumia mkopo kwa matumizi ambayo hayajaidhinishwa au kutoa taarifa za uongo ili kupata mkopo; akitiwa hatiani anaweza kutozwa faini, kifungo, na kikundi kinaweza kulazimika kurejesha fedha kilizopokea.
40.-(1) Kikundi au mtu yeyote- (a) atakayetumia fedha za mkopo uliotolewa chini ya Kanuni hizi kwa matumizi ambayo hayakuidhinishwa na Timu ya Menejimenti; au (b) atakayetoa taarifa za uongo kwa lengo la kupata mkopo unaotolewa chini ya Kanuni hizi, (c) atakuwa ametenda kosa na endapo atatiwa hatiani atawajibika kulipa faini ya kiasi kisichopungua na kisichozidi shilingi milioni moja au kutumikia kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne. laki mbili shilingi (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), kikundi kitakachopatikana na hatia kwa kosa chini ya kanuni ndogo ya (1) kitapaswa kurejesha fedha sawa na kiwango kilichopokea. Kufutwa kwa Kanuni TS Na. - 41 Verify source ↗
Kuhitimu ukopaji
AI-assisted research summary: These regulations repeal the 2019 loan regulations, and loans made before these regulations must be handled using the repayment process set out here.
41.-(1) Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za mwaka 2019 zinafutwa. 21 Kanuni za Utoaji Na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Tangazo la Serikali Na. 856 (Linaendelea) 286 la 2019 (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), mikopo iliyotolewa kabla ya Kanuni hizi itasimamiwa kwa utaratibu wa marejesho ulioainishwa katika Kanuni hizi. Dodoma, 2 Oktoba, 2024 MOHAMED O. MCHENGERWA, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 22
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in