Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024
This section gives the bylaw’s short title.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the bylaw’s short title. This provision says the subsidiary legislation applies within the jurisdiction of Madaba District Council. This section defines key terms used in the by-law, including authorized officer, extension officer, agricultural produce, the council, director, buyer, seller, levy, and agent. Halmashauri lazima ianzishe utaratibu maalumu wa kuuza na kununua mazao ya kilimo ndani ya mamlaka yake, na wauzaji au wanunuzi lazima wafuate masharti ya ukomavu, uvunaji, bei elekezi, na kipimo cha mzani. Wachuuzi wa mazao ya kilimo ndani ya Halmashauri lazima wawe na leseni, na wanunuzi kutoka nje ya nchi hawaruhusiwi kununua bila kampuni iliyosajiliwa Tanzania.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024
Showing 24 of 24
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the bylaw’s short title.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la
AI-assisted research summary: This provision says the subsidiary legislation applies within the jurisdiction of Madaba District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including authorized officer, extension officer, agricultural produce, the council, director, buyer, seller, levy, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri na Mkurugenzi aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Afisa Ugani” maana yake ni mtaalam wa kilimo, mifugo, uvuvi na nyuki katika ngazi za Wilaya, Kata na Kijiji; “mazao ya kilimo” maana yake ni mahindi, mbaazi, maharage, mtama, uwele, ufuta na mazao mengine; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Madaba; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mnunuzi” maana yake ni mtu, kikundi cha watu, kampuni, taasisi au shirika ambalo linanunua mazao ndani ya Halmashauri; 1 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.9 (Linaendelea.) “muuzaji” maana yake mtu, kikundi cha watu, kampuni, taasisi au shirika lolote linalojishughulisha na uzalishaji au uuzaji wa mazao ya kilimo ndani ya Halmashauri; “ushuru” maana yake ni ushuru wa mazao ya kilimo unaolipwa halmashauri na mnunuzi wa mazao ya kilimo kutokana na kiwango cha ushuru kilichopangwa kwa zao husika. “wakala” maana yake ni kampuni iliyoteuliwa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itaanzisha utaratibu maalumu
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ianzishe utaratibu maalumu wa kuuza na kununua mazao ya kilimo ndani ya mamlaka yake, na wauzaji au wanunuzi lazima wafuate masharti ya ukomavu, uvunaji, bei elekezi, na kipimo cha mzani.
4.-(1) Halmashauri itaanzisha utaratibu maalumu wa uuzaji na ununuzi wa mazao ya kilimo yanayopatikana na kuzalishwa ndani ya mamlaka ya Halmashauri. (2) Mazao ya kilimo yatauzwa au kununuliwa baada ya kukomaa na kuvunwa shambani na sio vinginevyo. (3) Kila muuzaji au mnunuzi wa mazao ya kilimo anawajibika kuuza au kununua mazao ya kilimo na kutoza bei ya zao husika kwa mujibu wa bei elekezi itakayotolewa na Halmashauri na mamlaka husika. (4) Kila zao la kilimo litauzwa, kununuliwa na kutozwa bei yake kwa kuzingatia kipimo cha mzani. - 5 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na leseni ya biashara ya ununuzi
AI-assisted research summary: Wachuuzi wa mazao ya kilimo ndani ya Halmashauri lazima wawe na leseni, na wanunuzi kutoka nje ya nchi hawaruhusiwi kununua bila kampuni iliyosajiliwa Tanzania.
5.-(1) Kutakuwa na leseni ya biashara ya ununuzi wa mazao ya kilimo itakayotolewa na Halmashauri. (2) Kila mnunuzi wa mazao ya kilimo ndani ya Halmashauri atalazimika kuwa na leseni ya kuendesha biashara ya ununuzi wa mazao ya kilimo. (3) Mnunuzi yeyote wa mazao ya kilimo kutoka nje ya nchi hataruhusiwa kununua mazao ya kilimo ndani ya Halmashauri bila kuwa na kampuni iliyosajiliwa Tanzania. Utaratibu maalum wa uuzaji na ununuzi wa mazao ya kilimo Leseni ya biashara ya mazao ya kilimo Kibali cha ununuzi wa mazao ya kilimo - 6 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na kibali cha ununuzi wa mazao ya
AI-assisted research summary: Mtu anayeomba kibali cha ununuzi wa mazao ya kilimo lazima alipe ada ya shilingi 5,000, na kibali hicho hutolewa na Halmashauri.
6.-(1) Kutakuwa na kibali cha ununuzi wa mazao ya kilimo ambacho kitatolewa na Halmashauri. (2) Mtu anayeomba kibali cha ununuzi wa mazao atapaswa kulipa ada ya kiasi cha shilingi elfu tano. Wajibu wa Halmashauri - 7 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa Halmashauri kuhakikisha
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ihakikishe kuwa inatoa vibali vya ununuzi na leseni za biashara ya mazao kwa kila mnunuzi wa mazao ya kilimo ndani ya Halmashauri.
7. Itakuwa ni wajibu wa Halmashauri kuhakikisha kwamba inatoa vibali vya ununuzi na leseni za biashara ya 2 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.9 (Linaendelea.) mazao kwa kila mnunuzi wa mazao ya kilimo ndani ya Halmashauri. Wajibu wa Serikali ya Kijiji Wajibu wa mnunuzi wa mazao ya kilimo Wajibu wa muuzaji wa mazao ya kilimo Hifadhi ya Mazao - 8 Verify source ↗
Serikali ya Kijiji itakuwa na wajibu wa kufuatilia
AI-assisted research summary: Serikali ya Kijiji lazima ifuatilie na kujiridhisha kuwa mnunuzi wa mazao ya kilimo ana kibali halali na anatii matakwa ya Sheria ndogo hii.
8. Serikali ya Kijiji itakuwa na wajibu wa kufuatilia na kujiridhisha endapo mnunuzi wa mazao ya kilimo ana kibali halali cha ununuzi wa mazao ya kilimo na anazingatia matakwa ya Sheria ndogo hii. - 9 Verify source ↗
Kila mnunuzi wa mazao ya kilimo atakuwa na
AI-assisted research summary: Kila mnunuzi wa mazao ya kilimo lazima awe na leseni na kibali husika, nunue mazao yaliyoiva na kuvunwa, na alipe ushuru mara tu baada ya kununua.
9. Kila mnunuzi wa mazao ya kilimo atakuwa na wajibu wa- (a) kuwa na leseni ya kuendesha biashara ya ununuzi wa mazao ya kilimo itakayotolewa na Halmashauri; (b) kuwa na kibali cha kununua mazao ndani ya Halmashauri; (c) kununua mazao ya kilimo baada ya kukomaa na kuvunwa shambani na sio vinginevyo; na (d) kulipa ushuru wa mazao kwa afisa mwidhiniwa au wakala mara tu baada ya kuyanunua. - 10 Verify source ↗
Kila muuzaji wa mazao ya kilimo atakuwa na
AI-assisted research summary: Kila muuzaji wa mazao ya kilimo lazima auze kwa mnunuzi mwenye leseni na kibali cha kununua kutoka Halmashauri, na mauzo yafanyike tu baada ya mazao kukomaa na kuvunwa shambani.
10. Kila muuzaji wa mazao ya kilimo atakuwa na wajibu wa- (a) kuuza mazao yake kwa mnunuzi mwenye leseni na kibali cha ununuzi wa mazao ya kilimo kutoka Halmashauri kwa kipindi cha mwaka husika anaonunua mazao; na (b) kuuza mazao ya kilimo baada ya kukomaa na kuvunwa shambani na sio vinginevyo. - 11 Verify source ↗
(1) Kila mkazi atakayelima shamba katika eneo
AI-assisted research summary: Residents who farm in the council area must harvest mature crops and store them safely.
11.-(1) Kila mkazi atakayelima shamba katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuvuna mazao yaliyokomaa na kuyahifadhi kwa njia salama. (2) Kila mkazi atahakikisha kuwa anahifadhi chakula cha kutosha kwa angalau mwaka mmoja au zaidi. (3) Kila mkazi atahakikisha kuwa ana ghala la kuhifadhia chakula ambalo ni imara na salama. Vituo vya kuuza na ukaguzi wa - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itaanzisha vituo mbalimbali
AI-assisted research summary: The Halmashauri must set up centers to sell and inspect agricultural produce transported inside and outside the Halmashauri.
12.-(1) Halmashauri itaanzisha vituo mbalimbali kwa madhumuni ya kuuza na kukagua mazao ya kilimo yanayosafirishwa ndani na nje ya Halmashauri. 3 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.9 (Linaendelea.) mazao ya kilimo Usafirishaji wa mazao ya kilimo Uteuzi wa Wakala Makosa (2) Ukaguzi wa mazao ya kilimo katika vituo utahusisha uhakiki wa nyaraka za ununuzi wa zao husika, ushuru uliolipwa pamoja na vibali vilivyotolewa na Halmashauri kuruhusu ununuzi wa mazao husika yanayosafirishwa. - 13 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayesafirisha mazao ya kilimo
AI-assisted research summary: Anayetumia kusafirisha mazao ya kilimo ndani au nje ya Halmashauri lazima awe na nyaraka fulani.
13. Mtu yeyote atakayesafirisha mazao ya kilimo ndani au nje ya Halmashauri atahakikisha kuwa ana nyaraka zifuatazo: (a) leseni ya biashara ya mazao ya kilimo iliyotolewa na Halmashauri; (b) nakala ya stakabadhi ya ushuru uliolipwa na mnunuzi wa mazao hayo; (c) vibali vya ununuzi wa mazao ya kilimo vilivyotolewa na Halmashauri kwa mnunuzi; na (d) kibali cha kusafirisha zao husika. - 14 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua Wakala kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kukusanya ada au ushuru kwa niaba yake.
14. Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua Wakala kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kwa ajili ya kukusanya ada au ushuru kwa niaba yake kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. - 15 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Anyone who does any of the listed acts involving agricultural produce commits an offence.
15. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo: (a) atauza au kununua, kuingia mikataba au makubaliano yoyote ya kuuza mazao ya kilimo yakiwa bado hayajakomaa shambani; (b) atalazimisha kupita katika vituo vya ukaguzi wa mazao ya kilimo kwa nguvu bila kukaguliwa; (c) atamshawishi mtu au kundi la watu kukwepa au kukataa kulipa ada au ushuru; (d) atamzuia Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa au Wakala kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (e) ataendesha biashara ya mazao ya kilimo bila kuwa na leseni ya biashara iliyotolewa na Halmashauri; au (f) atanunua mazao ya kilimo bila kulipa ushuru wa zao husika kwa Halmashauri. 4 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.9 (Linaendelea.) Adhabu Kufifilisha kosa - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote akipatikana na hatia kwa kosa chini ya Sheria Ndogo hii anaweza kupewa faini ya hadi shilingi 300,000, kifungo cha hadi miezi 12, au vyote viwili.
16. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja. - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji shilingi 50,000 ikiwa anakiri kosa na yuko tayari kujaza fomu ya Jedwali la Sita.
17. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Sita la Sheria Ndogo hii. 5 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.9 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA KWANZA ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 6(1)) KIBALI CHA KUNUNUA MAZAO YA KILIMO
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Jina la Mnunuzi: __________________________________________________
AI-assisted research summary: This section is a blank line for the buyer’s name.
1. Jina la Mnunuzi: __________________________________________________ - 2 Verify source ↗
Anuani S.L.P_____Mji/Kijiji_______Kitongoji___________Simu__________
AI-assisted research summary: Hii ni mstari wa fomu unaoonyesha sehemu za kuingiza anuani, mji/kijiji, kitongoji na simu.
2. Anuani S.L.P_____Mji/Kijiji_______Kitongoji___________Simu__________ - 3 Verify source ↗
Mahali anapoishi Mji/Kijiji___________________Kitongoji: ______________
AI-assisted research summary: Fomu inaonyesha sehemu ya kuandika mahali pa kuishi: mji/kijiji na kitongoji.
3. Mahali anapoishi Mji/Kijiji___________________Kitongoji: ______________ - 4 Verify source ↗
Aina ya zao analotaka kununua: ______________________________________
AI-assisted research summary: This section asks for the type of crop to be bought.
4. Aina ya zao analotaka kununua: ______________________________________ - 5 Verify source ↗
Kiasi cha Mazao kinachonunuliwa: ___________________________________
AI-assisted research summary: Section heading about the quantity of produce purchased.
5. Kiasi cha Mazao kinachonunuliwa: ___________________________________ - 6 Verify source ↗
Namba ya leseni ya biashara ya mazao ya kilimo_________________________
AI-assisted research summary: This section is about the number for an agricultural produce business license.
6. Namba ya leseni ya biashara ya mazao ya kilimo_________________________ - 7 Verify source ↗
Kibali hiki kitaanza kutumika tarehe______________hadi tarehe____________
AI-assisted research summary: Mwenye kibali anatakiwa kununua mazao ya kilimo kwa kuzingatia Sheria Ndogo husika na kutumia kipimo cha kilo katika kutoza bei. Ununuzi kinyume na masharti hayo unatajwa kuwa kosa linalostahili adhabu.
7. Kibali hiki kitaanza kutumika tarehe______________hadi tarehe____________ (Mnunuzi wa Mazao) MIMI________________________________________ NAAPA/NATHIBITISHA kwamba nitanunua mazao ya kilimo kwa kuzingatia matakwa ya Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024 kwa kuzingatia kipimo cha kilo katika kutoza bei na sio vinginevyo. Ninatambua pia kuwa kununua mazao kinyume na matakwa ya Sheria Ndogo hiyo ni kosa na nitastahili adhabu. Saini ya Mwombaji: _________________Alama ya dole gumba_______________ Tarehe ya kusaini kibali: ______________________________________________ KWA MATUMIZI YA OFISI TU Maoni ya Afisa Muidhiniwa: Nakubali/ Nakataa kwa kuwa amekidhi /hajakidhi masharti ya Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024. Jina la Afisa Mwidhiniwa: ___________________________________________ Saini na mhuri wa ya Afisa Mwidhiniwa: _________________________________ 6 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.9 (Linaendelea.) ____________ JEDWALI LA PILI ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 17) HATI YA KUFIFILISHA KOSA MWENYEWE Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU ya ………………………………………….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Madaba, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya mwaka 2024. mbele Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, niko tayari kulipa kiasi cha ushuru au ada ninayodaiwa kwa kiasi cha shilingi ……………….. pamoja na faini ya kufifilisha kosa ya kiasi cha shilingi ………………………... NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe………….ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………… MBELE YANGU : Jina: ……………………………………..…………… Saini………………………….………………………… Wadhifa: ……………………………………………… Tarehe…………………………………………………… 7 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.9 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imegongwa katika Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio la Mkutano wa Baraza la Madiwani ulioketi katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Madaba tarehe 28/7/2023 na kushuhudiwa lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- SAJIDU IDRISA MOHAMED, Mkurugenzi mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, Madaba TEOFANES TADEI MLELWA, Mwenyekiti, Halmashauri ya wilaya, Madaba L.S NAKUBALI, Dodoma, 30 Januari, 2024. MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Biashara ya Mazao ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in