Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Madaba ya Mwaka 2024
This section gives the short title of the by-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Madaba ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law. This provision says the by-law applies across the entire area of authority of Madaba District Council. This section defines key terms used in the by-law, including the authorized officer, council, permit, slaughterhouse, livestock, meat inspector, director, slaughterhouse owner, and implementing agent. Halmashauri lazima itekeleze majukumu kadhaa ya usimamizi wa mifugo na matumizi ya ardhi. Wafugaji wote ndani ya eneo la Halmashauri lazima wazingatie masharti ya usimamizi wa mifugo, ikiwemo kuoga mifugo, kuhudhuria mafunzo, kuwa na kadi ya mifugo, kulisha na kunywesha vya kutosha, na kuuza/kuelekeza mifugo kama ilivyoidhinishwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Madaba ya Mwaka 2024
Showing 25 of 25
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Madaba ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika eneo lote la mamlaka
AI-assisted research summary: This provision says the by-law applies across the entire area of authority of Madaba District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including the authorized officer, council, permit, slaughterhouse, livestock, meat inspector, director, slaughterhouse owner, and implementing agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama lengo muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “afya” maana yake ni hali timilifu ya kimwili na kiakili ya mnyama; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Madaba; “kaya” maana yake ni familia ya watu akiwemo baba, mama, mtoto au watoto na mtu mwingine yeyote anayeishi na familia hiyo, au watu wanaokaa katika nyumba moja na kuishi kama familia au mtu yeyote anayeishi peke yake katika chumba au nyumba; “kero au chukizo” maana yake ni kitu chochote ambacho kipo katika hali yoyote iwe kinatumika au kimewekwa au kimejengwa au ni kichafu kiasi cha kusababisha: (a) hatari kwa viumbe na maisha ya binadamu; (b) harufu mbaya ya kuudhi; 1 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) (c) kuzaliana kwa wadudu na wanyama hatari kama vile inzi, mende, sisimizi, panya, nyoka, nyuki, kunguni au viumbe wengine hatari; (d) magonjwa kwa binadamu, kuhifadhi mbu, inzi, panya na viumbe wenye madhara; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri kwa ajili ya kufanya shughuli iliyokusudiwa chini ya Sheria Ndogo hii; “machinjio” maana yake ni sehemu iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuchinjia wanyama na kuanika ngozi ikiwa ni pamoja na maeneo ya taasisi ya umma au watu binafsi yaliyopo katika eneo la Halmashauri; “meneja wa machinjio” maana yake ni Meneja wa na Halmashauri yanayomilikiwa Machinjio aliyeteuliwa kwa mujibu wa Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma ya Machinjio ya Halmashauri; “mifugo” maana yake ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku au wanyama wengine wanaofugwa na binadamu; “mkaguzi wa nyama” maana yake ni mtaalam wa afya ya mifugo aliyeajiriwa na Serikali na kusajiliwa, kuorodheshwa au kuandikishwa na Baraza la Veterinari Tanzania; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri afisa yeyote ya au kutekeleza majukumu ya Wilaya ya Madaba atakayeteuliwa Mkurugenzi; “mmiliki wa machinjio” maana yake ni mtu yeyote anayemiliki machinjio binafsi katika eneo la Halmashauri; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi, shirika au kampuni iliyoteuliwa kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa kufanya
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itekeleze majukumu kadhaa ya usimamizi wa mifugo na matumizi ya ardhi.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa kufanya mambo yafuatayo: (a) kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi; 2 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) (b) kuelekeza idadi ya mifugo ambayo kila mfugaji anaruhusiwa kufuga kulingana na ukubwa wa eneo lake; (c) kujenga majosho ya mifugo kwa kushirikiana na wananchi; (d) kutoa elimu ya ufugaji bora kwa jamii ili kuongeza tija; (e) kufanya sensa ya mifugo, kuweka alama na kutoa kadi za mifugo; (f) kutoa chanjo kwa kushirikiana na wafugaji ili kudhibiti magonjwa ya mifugo yasiyoambukiza na yanayoambukiza binadamu; na (g) kudhibiti uzururaji holela wa mifugo na wanyama katika Halmashauri kwa mujibu wa sheria. - 5 Verify source ↗
Kila mfugaji katika eneo la Halmashauri
AI-assisted research summary: Wafugaji wote ndani ya eneo la Halmashauri lazima wazingatie masharti ya usimamizi wa mifugo, ikiwemo kuoga mifugo, kuhudhuria mafunzo, kuwa na kadi ya mifugo, kulisha na kunywesha vya kutosha, na kuuza/kuelekeza mifugo kama ilivyoidhinishwa.
5. Kila mfugaji katika eneo la Halmashauri atahakikisha kuwa: (a) anaogesha mifugo yake ili kudhibiti magonjwa ya wanyama kama atakavyoelekezwa na Halmashauri; alama maalumu zinazotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Ustawi wa Wanyama; (b) mifugo inawekwa yake (c) anahudhuria mafunzo ya ufugaji kama atakavyohitajika na Halmashauri; Wajibu wa mfugaji Sura ya 154 (d) anafuga idadi lililoidhinishwa yaliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza; ya mifugo kulingana jengo na maelekezo katika (e) anakuwa na kadi ya mifugo itakayoonesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo; (f) anaipatia mifugo yake malisho au chakula na maji ya kutosha kwa kuzingatia kanuni bora za ufugaji; (g) anafuga kwa kuzingatia mipango ya matumizi bora ya ardhi; (h) anapeleka mifugo yake katika vituo vya chanjo kama itakavyoamriwa na Halmashauri na atalipia chanjo hiyo kama atatakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa viwango vitakavyoainishwa na mamlaka husika; na 3 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) (i) anauza mifugo yake katika masoko na minada taarifa lingine kwa iliyoidhinishwa au eneo maalum. Kibali cha kufuga wanyama - 6 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayekusudia kufuga mifugo
AI-assisted research summary: Mtu anayepanga kufuga mifugo lazima apate kibali kutoka Halmashauri; kibali hutolewa bila malipo na hudumu miaka mitatu.
6.-(1) Mtu yeyote anayekusudia kufuga mifugo atapaswa kupata kibali cha kufuga kutoka kwa Halmashauri kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. (2) Kibali cha ufugaji kitatolewa bure na kitakuwa cha miaka mitatu kuanzia tarehe kilipotolewa. (3) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1) na (2), endapo mtu yeyote atakiuka taratibu za ufugaji zilizoelekezwa chini ya Sheria Ndogo hii, Halmashauri itafuta kibali cha ufugaji cha mtu huyo na atalazimika kuhamisha mifugo yake yote kutoka katika eneo la Halmashauri. Masharti kwa mfugaji - 7 Verify source ↗
Kila mfugaji hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Kila mfugaji hapaswi kufanya shughuli kadhaa za mifugo bila kibali au nje ya maeneo yaliyotengwa.
7. Kila mfugaji hataruhusiwa: (a) kuchunga, kulisha au kunywesha maji mifugo katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hiyo; (b) kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani; (c) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo moja hadi lingine bila kibali kutoka Halmashauri; (d) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (e) bila kibali maalum cha Halmashauri, kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo siyo mnada, masoko ya mifugo yaliyoidhinishwa; na au magulio (f) kununua, kuuza au kufanya biashara ya kubadilishana aina yoyote ya mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali maalum isipokuwa kwenye minada au magulio yaliyotengwa kwa shughuli hiyo na Halmashauri. Kibali cha kusafirisha mifugo - 8 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayekusudia kusafirisha mifugo
AI-assisted research summary: Anyone who wants to transport livestock or livestock products into or out of the Council area must have a special permit.
8.- (1) Mtu yeyote anayekusudia kusafirisha mifugo au mazao ya mifugo kutoka au kuingia katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuwa na kibali maalumu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu. (2) Halmashauri itatoa kibali cha kusafirisha mifugo kwa kuweka utaratibu ikiwa ni pamoja na: 4 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) (a) mfugaji kutoa uthibitisho wa kumiliki mifugo kwa ilivyoainishwa katika fomu maalumu kujaza Jedwali la Nne; na (b) kukagua kibali cha kusafirisha mifugo. (3) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kukamata na kutoza faini na adhabu kwa mifugo yoyote inayosafirishwa kinyume na Sheria Ndogo hii. (4) Muda wa kusafirisha mifugo na mazao ya mifugo kutoka Halmashauri itakuwa ni kuanzia saa kumi na mbili kamili alfajiri hadi saa kumi na mbili kamili jioni. Kudhibiti mifugo inayozurura ovyo
Part
Jedwali la Nne; na
- 9 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri may seize stray livestock in the area; the owner must pay a daily fine, and unclaimed livestock may be auctioned with court approval after 7 days.
9.-(1) Halmashauri inazurura itakayoonekana Halmashauri. itakamata mifugo yoyote la ovyo katika eneo (2) Mmiliki wa mifugo itakayokamatwa chini ya kanuni ndogo ya (1) atalipa faini ya kiasi cha shilingi elfu kumi kwa kila siku. (3) Endapo mifugo iliyokamatwa haitachukuliwa na mmiliki ndani ya kipindi cha siku saba tangu kukamatwa, Halmashauri itakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mifugo hiyo baada ya kupata idhini ya Mahakama, na fedha zitakazopatikana zitarejeshwa kwa mmiliki wa mifugo baada ya kutoa faini inayodaiwa, gharama za kuhifadhi mifugo, gharama ya mahakama na gharama ya mnada. (4) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (3), kabla ya Halmashauri kuuza kwa mnada mifugo iliyokamatwa, Mkurugenzi atamjulisha mmliki na umma juu ya kusudio hilo. (5) Endapo kutatokea kufa kwa mifugo kutokana na sababu yoyote, Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama vifo hivyo vitakuwa uzembe wa watumishi wa vimesababishwa Halmashauri. na Ukaguzi wa mifugo na bidhaa za mifugo - 10 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kukataa mifugo au bidhaa kuingia au kuuzwa ikiwa zinaweza kuhatarisha afya au usalama, na anaweza kuingia nyumba au jengo lolote kati ya saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kwa ajili ya utekelezaji wa Sheria Ndogo hii.
10.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kukataa aina yoyote ya mifugo au bidhaa kuingia au kuuzwa ndani ya eneo la Halmashauri, iwapo mifugo hiyo au bidhaa hizo zinaweza kuhatarisha afya au usalama wa mifugo mingine au watumiaji. 5 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) (2) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika nyumba au jengo lolote kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kwa lengo la utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Taratibu za biashara ya mifugo na mazao ya mifugo - 11 Verify source ↗
(1) Kabla ya kuanza biashara ya mifugo au
AI-assisted research summary: Before starting livestock or livestock-product trading, a trader must have the required licence, ID and permits, show the permits to the council for verification, use an accepted transport vehicle, and buy or sell livestock only in recognized markets or auctions.
11.-(1) Kabla ya kuanza biashara ya mifugo au mazao ya mifugo, mfanyabiashara atapaswa kuwa na leseni, utambulisho na vibali kutoka mamlaka husika vinavyohusu kuuza na kununua mifugo au mazao ya mifugo na atatakiwa kuwasilisha vibali vyake Halmashauri kwa ajili ya uhakiki. (2) Mfanyabiashara atakayesafirisha mifugo kutoka nje ya Halmashauri atatakiwa kuwa na kibali kutoka Halmashauiri ambayo mifugo hiyo inatoka. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2), mfanyabiashara wa mifugo atatakiwa kusafirisha mifugo katika vyombo vya usafiri vinavyokubalika kwa mujibu wa sheria. (4) Mifugo yote itauzwa au kununuliwa katika minada na masoko yanayotambulika kwa mujibu wa sheria. Wajibu wa mfanyabiashara wa bucha na maduka ya nyama - 12 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara wa bucha au duka la
AI-assisted research summary: Butcher and meat-shop businesses must meet listed hygiene, equipment, licensing, and inspection requirements.
12. Kila mfanyabiashara wa bucha au duka la nyama anatakiwa kuhakikisha kuwa: (a) ana leseni na vibali vya kufanya biashara hiyo; (b) kuna kabati la vioo la kuzuia nzi na wadudu wengine wataambao; (c) kuna pipa la kuhifadhia taka ngumu na laini; (d) kuna jokofu la kuhifadhia nyama; (e) jengo lake la biashara lina mwanga wa kutosha, umeme, maji safi na salama, visu, meza, mzani wa kawaida au mzani wa kielektroniki na misumeno maalumu ya kukatia nyama; imekaguliwa mkaguzi aliyeidhinishwa na imegongwa muhuri na inauzwa ndani ya jengo; (f) nyama na (g) muuzaji anavaa sare nyeupe muda wote inayojumuisha mabuti, koti na kofia; 6 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) Usafirishaji wa Nyama Kuingiza wanyama katika machinjio (h) muuzaji anapima afya yake kila baada ya miezi sita na kuhakikisha anakuwa na cheti cha upimaji; (i) mmiliki wa bucha au muuzaji wa nyama anatoa ushirikiano wa kutosha kwa wakaguzi mara atakapotakiwa kufanya hivyo wakati wowote wa ukaguzi; na (j) biashara ya nyama inafanyika katika bucha au duka maalumu na sio vinginevyo. - 13 Verify source ↗
(1) Mfanyabiashara wa nyama atatakiwa
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wa nyama lazima wasafirishe nyama kwa gari maalumu; ikiwa wanatumia pikipiki au baiskeli, lazima watumie chombo maalumu kilichoidhinishwa na Halmashauri.
13.-(1) Mfanyabiashara wa nyama atatakiwa kusafirisha nyama kutoka machinjioni kwa kutumia gari maalumu na endapo atatumia usafiri wa pikipiki au baiskeli atatakiwa kubeba nyama kwa kutumia chombo maalumu kilichoidhinishwa na Halmashauri. (2) Kila mmiliki wa gari la kubeba nyama atahakikisha kuwa gari lake: (a) limesajiliwa na kupewa cheti maalumu cha ukaguzi na Halmashauri; (b) linakaguliwa kila baada ya miezi mitatu; (c) lina sanduku la aluminiamu lenye mfuniko na limepakwa rangi nyeupe, mstari mwekundu na namba; na (d) halibebi kitu kingine tofauti na nyama. (3) Mmiliki wa gari la kubeba nyama atapaswa kulipia gharama za usafirishaji kama zitakavyowekwa na Halmashauri. - 14 Verify source ↗
(1) Meneja wa machinjio au mmiliki wa
AI-assisted research summary: Meneja au mmiliki wa machinjio lazima athibitishe umiliki wa mnyama kabla ya kuingizwa machinjioni, akague kibali cha usafirishaji na nyaraka nyingine, na atunze rejista ya wanyama waliopokelewa.
14.-(1) Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa umiliki wa mnyama anayekusudiwa kuchinjwa unathibitishwa kabla ya kuingizwa katika eneo la machinjio. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atawajibika kukagua kibali cha usafirishaji wa mnyama na nyaraka nyingine zinazothibitisha umiliki. (3) Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atatunza rejista ya wanyama waliopokelewa machinjioni ambayo itaainisha aina ya mnyama, jinsi, umri na taarifa za mmiliki. 7 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) Ukaguzi wa wanyama Sura ya 156 - 15 Verify source ↗
(1) Mnyama yeyote anayekusudiwa kuchinjwa
AI-assisted research summary: Animals intended for slaughter in a slaughterhouse must be inspected before slaughter, and the authorized officer has duties and powers for diseased animals.
15.-(1) Mnyama yeyote anayekusudiwa kuchinjwa katika machinjio atafanyiwa ukaguzi wa awali na Mkaguzi wa Nyama kabla ya kuchinjwa. (2) Mnyama ambaye baada ya ukaguzi atagundulika kuwa na ugonjwa unaohatarisha afya ya binadamu atahifadhiwa katika eneo maalum la kuhifadhi wanyama wenye magonjwa kwa ajili ya matibabu. (3) Kabla ya mnyama kutengwa, taratibu zilizoainishwa katika Sheria ya Magonjwa ya Wanyama zitafuatwa. (4) Endapo mnyama aliyetengwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (2) ataendelea kuwa na ugonjwa uliosababisha atengwe, Afisa Mwidhiniwa atamtaka mmiliki wa mnyama huyo kumtoa nje ya eneo la machinjio kwa matibabu zaidi. (5) Endapo mmiliki atashindwa kumwondoa mnyama aliyetengwa ndani ya muda wa saa kumi na mbili tangu amri ya kuondolewa kwa mnyama itolewe, Afisa Mwidhiniwa huyo kuteketezwa kwa gharama ya mmiliki. kuamuru mnyama anaweza Udhibiti wa uchinjaji machinjioni (6) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na wajibu wa kuchukua taarifa za mmiliki na kumbukumbu za mnyama aliyebainika kuwa na ugonjwa na kumweka alama maalum itakayomtambulisha mnyama huyo. - 16 Verify source ↗
(1) Watu wote wanaohusika na shughuli za
AI-assisted research summary: Sectioni hii inaweka masharti ya usafi, ukaguzi, vibali, na marufuku mbalimbali katika eneo la machinjio.
16.-(1) Watu wote wanaohusika na shughuli za machinjio, watatakiwa kupima afya kila baada ya miezi sita. (2) Watu wanaohusika na machinjio wanatakiwa kuwa wasafi na kuvaa mavazi maalumu kwa ajili ya kazi hiyo. (3) Mtu yeyote hataruhusiwa kukaa au kufanya mkusanyiko wa aina yoyote katika eneo la machinjio isipokuwa kwa kibali maalumu kitakachotolewa na Halmashauri. (4) Meneja au mmiliki wa machinjio atahakikisha kuwa shughuli za uendeshaji wa machinjio zinazingatia sheria na taratibu za afya. 8 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) (5) Mtu hataruhusiwa kufanya biashara ya aina yoyote katika eneo la machinjio. (6) Mtu hataruhusiwa kuweka bucha, duka la nyama au biashara yoyote ya nyama ndani ya mita 200 kutoka eneo la machinjio. (7) Mfanyabiashara wa nyama atapaswa kuwa na utambulisho kutoka Bodi ya Nyama na leseni halali ya biashara. (8) Kila mfugaji atatakiwa kupeleka mifugo yake machinjioni au mahali huduma hiyo inapopatikana na itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchinja mifugo mahali pengine popote ambapo sio machinjio isipokuwa kwa kutoa taarifa kwa Afisa Mwidhiniwa na mfugaji atalazimika kulipia gharama za machinjio kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. (9) Nyama yoyote haitaruhusiwa kutumika kwa matumizi ya binadamu bila kufanyiwa ukaguzi wa mwisho na kuwa na muhuri maalumu wa ukaguzi nyama. (10) Mtu yeyote hataruhusiwa kuingiza mifugo katika machinjio kwa ajili ya kuchinja baada ya saa kumi na moja kamili jioni isipokuwa kwa kibali maalumu cha Halmashauri. (11) Mtu yeyote hataruhusiwa kutoa nje ya eneo la machinjio mnyama aliye hai au aliyekufa au nyama bila ya idhini ya maandishi ya meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio. (12) Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio hataruhusu mifugo yoyote kuchinjwa bila kufanyiwa ukaguzi wa awali. (13) Mtu yeyote hataruhusiwa kutoa lugha za kashfa, kuudhi, kudhalilisha au matusi kwa mtaalamu au mtu yeyote katika eneo la machinjio. Ukaguzi wa nyama - 17 Verify source ↗
(1) Mkaguzi wa Nyama atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Mkaguzi wa Nyama lazima akague nyama baada ya kuchinjwa ili kubaini kama inafaa kwa matumizi ya binadamu, na nyama isiyofaa itateketezwa.
17.-(1) Mkaguzi wa Nyama atakuwa na wajibu wa kukagua nyama katika eneo la machinjio baada ya mnyama kuchinjwa kwa madhumuni ya kubaini iwapo nyama inafaa kwa matumizi ya binadamu. (2) Endapo itabainika kuwa nyama iliyokaguliwa: (a) inafaa kwa matumizi ya binadamu, Mkaguzi wa hiyo muhuri atagonga Nyama nyama 9 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) Udhibiti wa ufugaji wa mbwa unaothibitisha kuwa nyama iliyokaguliwa ni salama kwa matumizi ya binadamu; au (b) haifai kwa matumizi ya binadamu, nyama hiyo itateketezwa kwa kuichoma moto au kwa njia nyingine inafaa na Afisa Mwidhiniwa atachukua kumbukumbu za nyama hiyo na za mmiliki wake. itakayoonekana (3) Endapo matokeo ya vipimo vya awali yatakuwa na mashaka kuhusu usalama wa nyama kwa matumizi ya binadamu, Mkaguzi wa Nyama atahakikisha kuwa nyama husika inahifadhiwa kwa muda usiozidi saa ishirini na nne ili kuruhusu vipimo zaidi vya kimaabara kufanyika. (4) Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atatunza rejesta ya nyama zilizokaguliwa ambayo itaonesha aina ya nyama, jinsi, umri, uzito na taarifa za mmiliki na kama nyama inafaa au haifai kwa matumizi ya binadamu. - 18 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kufuga mbwa
AI-assisted research summary: You may not keep a dog in the council area without a dog-keeping permit from the council.
18.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kufuga mbwa katika eneo la Halmashauri bila kibali cha ufugaji kutoka Halmashauri. (2) Kibali cha ufugaji kitatolewa bure na kitadumu kwa muda wa mwaka mmoja. (3) Mfugaji atawajibika kumpatia chanjo mbwa wake na kulipa ada ya chanjo kama atakavyoelekezwa na Halmashauri. (4) Mfugaji atalazimika kuonesha cheti cha chanjo ya mbwa kabla ya kupata au kuhuisha kibali kilichoisha muda wake. (5) Mfugaji atawajibika kumfungia mbwa wake wakati wote wa mchana na anaweza kumfungulia kuanzia saa nne kamili usiku na kumfungia saa kumi na moja alfajiri. (6) Mfugaji atawajibika kuogesha mbwa kila baada ya siku saba ili kudhibiti magonjwa na wadudu wasumbufu kwa gharama zake na kama atakavyoelekezwa na Halmashauri. (7) Mfugaji atalazimika kumfunga mbwa kwa mnyororo maalumu wakati wa kutembea nae kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. 10 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) (8) Iwapo mfugaji anasafirisha mbwa, atalazimika kuwa na kasha maalumu kama atakavyoelekezwa na Afisa wa Mwidhiniwa la kusafirishia mbwa kabla ya kupewa kibali. Mbwa anaezurura Makosa
Part
sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
- 19 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kukamata na kuhifadhi
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kukamata na kuweka kizuizini mbwa anayezurura kwa muda usiozidi siku mbili, kisha inaweza kutaifisha au kuchukua hatua nyingine kisheria.
19. Halmashauri inaweza kukamata na kuhifadhi katika kizuizi kwa muda usiozidi siku mbili mbwa atakayepatikana anazurura, na baada ya hapo, Halmashauri inaweza kutaifisha au kuchukua hatua nyingine kisheria kwa kadri itakavyoona inafaa. - 20 Verify source ↗
Mfugaji yeyote atakuwa ametenda kosa iwapo
AI-assisted research summary: Mfugaji yeyote anaweza kutenda kosa ikiwa anakiuka masharti mbalimbali ya usimamizi wa mifugo, vibali, taarifa, na uendeshaji wa machinjio.
20. Mfugaji yeyote atakuwa ametenda kosa iwapo: (a) atashindwa au kukataa kuogesha au kuchanja mifugo yake ili kuzuia magonjwa; kwenye mifugo (b) atalisha maeneo yasiyoruhusiwa; (c) kuanzisha duka la kuuza vyakula vya mifugo, ghala la kuhifadhia mifugo, kiwanda cha kutengeneza vyakula vya mifugo, vituo vya huduma za mifugo au zahanati na vituo vya kutotolesha vifaranga bila kuwa na kibali kutoka Halmashauri; (d) atafuga mifugo katika eneo la Halmashauri bila kuwa na kibali cha ufugaji; (e) atashindwa au atazembea kutoa taarifa kuhusu uwepo wa au dalili za ugonjwa au kifo cha ghafla katika mifugo yake; (f) atashindwa kuwasilisha taarifa ya mwezi ya uuzaji wa vyakula vya mifugo, utengenezaji wa vyakula vya mifugo au ghala, vituo vya huduma za mifugo au zahanati na vituo vya kutotolesha vifaranga kwa afisa mwidhiniwa; (g) atauza na kufuga mifugo pembezoni mwa barabara au sehemu ambayo haijaruhusiwa; (h) atasababisha kero ya harufu mbaya na kelele ya mifugo yake kwa jamii; (i) ataruhusu mifugo yake kuzurura ovyo; (j) ataweka vyakula vya mifugo wazi; (k) atashindwa kutoa ushirikiano wa uwekaji wa alama kwa mifugo yake; 11 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) (l) atatumia au kuingiza kisichoruhusiwa katika eneo la machinjio; (m) atatumia lugha inayoudhi ndani ya machinjio au chochote kilevi kufanya udhalilishaji wa aina yoyote; (n) atabandika au kubandua tangazo bila idhini ya meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio; (o) atahatarisha amani au kushiriki kwa namna la yeyote kuhatarisha amani katika eneo machinjio; (p) atafanya au kushiriki kufanya uchafuzi wa mazingira; (q) atafanya shughuli za kisiasa ikiwa ni pamoja na kupandisha bendera ya chama cha siasa; au afisa mwidhiniwa (r) atamzuia kutekeleza majukumu yake. Adhabu Kufifilisha kosa - 21 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa
AI-assisted research summary: Anyone convicted of an offence under this bylaw is liable to a fine, imprisonment, or both.
21. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kwa faini ya kiasi kisichopungua shilingi elfu hamsini na kisichozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja. - 22 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza faini mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza faini mtu yeyote aliyevunja Sheria Ndogo hii, kwa kiasi cha shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Tano.
22. Mkurugenzi anaweza kumtoza faini mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii, kiasi cha shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoambatanishwa kwenye Jedwali la Tano. _______________ JEDWALI LA KWANZA _______________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 5(d)) IDADI YA MIFUGO ILIYORUHUSIWA KUFUGWA Namba Aina ya Mfugo Idadi
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Mfugaji anaweza kupewa kibali cha kufuga kulingana na ukubwa wa eneo alilonalo, mradi ufugaji huo usilete kero ya harufu au kelele kwa jamii.
1. Ng’ombe - Maelezo Mfugaji atapewa kibali cha kufuga kulingana na ukubwa wa eneo alilonalo bila kusababisha kero ya harufu na kelele kwa jamii 12 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Mfugaji anaweza kupewa kibali cha kufuga au kusafirisha mifugo, kwa kuzingatia ukubwa wa eneo na masharti ya kibali.
5. Mbuzi au Kondoo Nguruwe Mbwa Wanyama wa jamii ya ndege - 4 - - Mfugaji atapewa kibali cha kufuga kulingana na ukubwa wa eneo alilonalo bila kusababisha kero ya harufu na kelele kwa jamii Nguruwe Watoto wakiachishwa kunyonya wauzwe au kuondolewa Mfugaji atapewa kibali cha kufuga kulingana na ukubwa wa eneo alilonalo bila kusababisha kero ya harufu na kelele kwa jamii Mfugaji atapewa kibali cha kufuga kulingana na ukubwa wa eneo alilonalo bila kusababisha kero ya harufu na kelele kwa jamii 13 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA PILI ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 6(1) KIBALI CHA UFUGAJI Jina la Mfugaji:……………………………………………………….. Anuani:………………………………………………………… Kata:…………………………………… Mtaa ………………… Namba Nyumba:…………………………………… Namba Kitalu:…………… Ameruhusiwa kufuga Mifugo ifuatao katika eneo la………….. Na Aina ya Mfugo Koo Idadi ya Mifugo Jike Dume Jumla Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Paka Farasi Sungura 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Mbwa Kuku au Bata 11 12 Wanyama wengine Kibali hiki kimetolewa kwa Ndugu:………………………………………kwa muda wa miezi ………………….kwa Mifugo kuanzia tarehe……………..hadi tarehe………….. Kimetolewa na: Jina la Afisa Mwidhiniwa………………………………………. Tarehe………………………………. Muhuri: 14 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) __________ JEDWALI LA TATU ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 8 (1)) KIBALI CHA KUSAFIRISHA MIFUGO Jina:……………………………………………. Anuani:………………………………………… Ameruhusiwa kusafirisha Mifugo ifuatayo kutoka ………………kupitia njia za……………………..hadi…………..….. Idadi ya Mifugo Aina ya Mfugo Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Paka Farasi Sungura Namba
Part
JEDWALI LA TATU
- 12 Verify source ↗
Mifugo wengine
AI-assisted research summary: This section contains permit forms for moving livestock and for a livestock owner’s declaration admitting an offence and agreeing to pay fees and a compromise fine.
12. Mifugo wengine Kuku au Bata Kibali hiki kitakuwa cha muda wa siku….. kuanzia tarehe…....hadi tarehe………. Kimetolewa na : Jina la Afisa Mwidhiniwa:………………………………………. Saini:…………………………………………………………….. Wadhifa:…………………………………………………………….. Tarehe:………………………………………………………….... Muhuri:……………………………………… 15 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) __________ JEDWALI LA NNE ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 8(2)(a)) KIBALI CHA MFUGAJI CHA KUTHIBITISHA UHALALI WA KUMILIKI MIFUGO ANAYOTAKA KUSAFIRISHA KWENDA MNADANI/KUHAMIA ENEO LINGINE A. Jina la Mfugaji/Mmiliki: ………….………………Jina la msafirishaji………………………… Mahusiano ya msafirishaji na Mmiliki…………………………………………. B. Anuani…………Kijiji cha………………Kitongoji cha…………… Ranchi ya…………………. Kitalu Namba………..…….. Ameruhusiwa kusafirisha wanyama wake wafuatao kwenda Mnada wa/Kijiji cha…………… kutoka ……………… kupitia njia za………………hadi………………… Idadi Aina ya mnyama Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Paka Farasi Sungura Na 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Mbwa 11 12 Wanyama wengine (wataje) Kuku /Bata Kwa muda wote wa saa za mchana kwa kipindi cha kuanzia ………….. hadi ……….. Namba ya gari……………. Namba ya trela…………… Kibali hiki kitakuwa cha muda wa siku……….. kuanzia tarehe ………….. hadi tarehe ………….. Barua toka kwa Afisa Mtendaji /Afisa Mifugo Kijiji/Kata inayothibitisha uhalali wa kumiliki mifugo /wanyama hao imeambatanishwa. Kimetolewa na : Jina la Afisa Mwidhiniwa : ……………………………… Cheo ……………………. Tarehe : …………………………………. Muhuri na Saini: 16 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) NB: KIBALI HIKI AMBACHO ATAPWEWA MWENYE MIFUGO NI MAHSUSI KWA AJILI YA KUTHIBITISHA UHALALI WA MIFUGO INAYOPELEKWA MNADANI KUUZWA/KUHAMIA ENEO LINGINE 17 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) ____________ JEDWALI LA TANO __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 22) _______ FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, kwamba mnamo tarehe …… ya Mwezi ………. Mwaka ……….…… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, niko tayari kulipa kiasi cha ada ninayodaiwa kwa kiasi cha shilingi ……………….. pamoja na faini ya kufifilisha kosa ya kiasi cha shilingi ………………………... NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Saini……………………… Jina……………………………….. MBELE YANGU: Jina:……………………………………..……………………..... Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa:………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………… 18 Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.10 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imegongwa katika Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio la Mkutano wa Baraza la Madiwani ulioketi katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Madaba tarehe 28/7/2023 na kushuhudiwa lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- SAJIDU IDRISA MOHAMED, Mkurugenzi mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, Madaba TEOFANES TADEI MLELWA, Mwenyekiti, Halmashauri ya wilaya, Madaba L.S NAKUBALI, Dodoma, 30 Januari, 2024. MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 19
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Madaba ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in