Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024
This by-law is titled the Madaba District Council Environmental Sanitation and Health Inspection By-Law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This by-law is titled the Madaba District Council Environmental Sanitation and Health Inspection By-Law, 2024. This by-law applies throughout the area under the jurisdiction of Madaba District Council. This section defines key terms used in the by-law, including fee, authorized officer, food, improved toilet, nuisance, council, and resident. Mmiliki wa nyumba, kiwanja au biashara lazima ahakikishe eneo lake ni safi, taka zinashughulikiwa vizuri, shimo la taka linachimbwa, choo kinajengwa na kutumika vizuri, na eneo halina mazalia ya wadudu hatarishi. Mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara lazima awe na karo la kuhifadhi maji taka, aonye maji taka karo linapojaa, na asimwage au kuelekeza maji machafu kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024
Showing 23 of 23
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This by-law is titled the Madaba District Council Environmental Sanitation and Health Inspection By-Law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the area under the jurisdiction of Madaba District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including fee, authorized officer, food, improved toilet, nuisance, council, and resident.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya huduma ya kuzoa taka; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote atakayeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa dawa; “choo bora” maana yake ni choo chochote cha maji chenye sakafu inayosafishika, banda imara la imara, kudumu, bomba la kutolea hewa chafu na lenye mfuniko kwenye tundu la choo na shimo salama na safi kwa ajili ya kutupa kinyesi na mkojo wa binadamu, lililojengwa kwa vifaa vya kudumu; lenye mlango lililoezekwa, 1 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) “chukizo au kero” maana yake ni kitu chochote ambacho kipo katika hali yoyote iwe kinatumika, kimewekwa, kimejengwa, au ni kichafu kiasi cha kusababisha: (a) hatari kwa viumbe na maisha ya binadamu; (b) harufu mbaya au harufu ya kuudhi au kuleta kinyaa; (c) kuzaliana kwa wadudu hatari kama vile inzi, mende, sisimizi, panya, nyoka, nyuki, kunguni au viumbe wengine hatari; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Madaba; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “kizimba cha taka” maana yake ni eneo maalum lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuhifadhi taka ngumu; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo lililoko chini ya mamlaka ya Halmashauri na ambaye ama ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “maji taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira. Sura ya 191 Sura ya 191 Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira - 4 Verify source ↗
Kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba,
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba, kiwanja au biashara lazima ahakikishe eneo lake ni safi, taka zinashughulikiwa vizuri, shimo la taka linachimbwa, choo kinajengwa na kutumika vizuri, na eneo halina mazalia ya wadudu hatarishi.
4. Kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba, kiwanja au biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba- (a) mazingira yanayozunguka eneo lake yanakuwa safi wakati wote; (b) taka zote zinakusanywa na kufukiwa au itakayoelekezwa na kuondolewa kwa njia Halmashauri; 2 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) (c) anachimba shimo la kutupia taka litakalokuwa na urefu usiopungua kimo cha futi 3 na upana usiopungua futi 2; (d) anajenga choo imara cha kudumu kilichojengwa kwa matofali na kuezekwa kwa bati, tembe, majani, vigae chenye mlango unaofunga na kufunguka na kuhakikisha kwamba choo kinatumika wakati wote na kuwe na chombo cha maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono; (e) eneo lake halina mazalia ya mbu, panya na wadudu wengine hatarishi. Uhifadhi wa maji taka - 5 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara lazima awe na karo la kuhifadhi maji taka, aonye maji taka karo linapojaa, na asimwage au kuelekeza maji machafu kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.
5. Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara anatakiwa: (a) kuhakikisha kuwa ana karo la kuhifadhi maji taka; (b) kunyonya maji taka pale karo linapojaa; na (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote isiyotengwa kuhifadhia maji taka. Utengenezaji na uuzaji wa vyakula - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika,
AI-assisted research summary: Anyone making, burning, cooking, boiling, or selling food in the Council area must comply with health requirements and regulations.
6. Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa kutimiza masharti na kanuni za afya. Ada ya ukaguzi wa afya - 7 Verify source ↗
Kutakuwa na ada ya ukaguzi wa afya na
AI-assisted research summary: Ada ya ukaguzi wa afya inalipwa na mmiliki au mhudumu wa maeneo yaliyotajwa.
7. Kutakuwa na ada ya ukaguzi wa afya na italipwa na mmiliki au mhudumu katika majengo ya biashara, vituo vya afya na zahanati za watu binafsi, famasi au maduka ya madawa, hoteli, migahawa, mama aubaba lishe, watoa tiba asili, majengo ya biashara na vioski na maeneo mengine kama ilivyoainishwa katika katika Jedwali la Kwanza. Upimaji wa afya - 8 Verify source ↗
Kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa,
AI-assisted research summary: Wahudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, waokaji mikate, na wauzaji wa vyakula vilivyopikwa lazima wahakikishe wanapima afya yao kila baada ya miezi sita.
8. Kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, muoka mikate au mtu anayeshughulika na kuuza vyakula vilivyopikwa 3 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba anapima afyayake kila baada ya miezi sita. Uwezo wa Afisa Mwidhiniwa Vifaa vya kuhifadhi taka ngumu Ada ya uzoaji taka Ukusanyaji taka ngumu - 9 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa ana uwezo wa kuingia eneo lolote ndani ya Halmashauri wakati wa muda wa kazi ili kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii, na anaweza pia kushauri au kuelekeza watu wasiishi katika jengo linalohatarisha afya au maisha.
9.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo kuingia katika eneo lolote ndani ya Halmashauri wakati wa muda wa kazi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kushauri au kuelekeza watu au mtu kutokuishi katika jengo ambalo linahatarisha afya au maisha ya watu na viumbe hai. - 10 Verify source ↗
(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au
AI-assisted research summary: Wamiliki, wapangaji, na wafanyabiashara ndani ya Halmashauri wanatakiwa kuwa na vyombo vya kuhifadhia taka vyenye mfuniko na kukusanya taka katika maeneo yaliyotengwa; kwa nyumba zilizo kwenye ukanda wa kijani na maeneo ambayo hayajapimwa, pia lazima kuwe na shimo kubwa la taka ngumu.
10.-(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji wa jengo la makazi au mtu yeyote anayefanya biashara katika eneo lolote ndani ya Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo cha kuhifadhia taka chenye mfuniko na atawajibika kukusanya taka hizo kwenye vizimba vya kuzolea taka katika maeneo yaliyoainishwa. (2) Kila mmiliki wa jengo au mpangaji wa nyumba iliyoko katika ukanda wa kijani, katika maeneo ambayo hayajapimwa atalazimika kuwa na shimo kubwa la kukusanyia taka ngumu katika eneo lake. - 11 Verify source ↗
Halmashauri itawajibika kukusanya taka
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikusanye taka ngumu kutoka kwenye vizimba vya taka vilivyoainishwa katika kila kata, na wazalishaji taka lazima walipie ada au ushuru wa ukusanyaji wa taka kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili.
11. Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu kutoka katika vizimba vya taka vilivyoainishwa katika kila kata, na wazalishaji taka watalipia ada au ushuru wa ukusanyaji wa taka kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itawajibika kukusanya taka
AI-assisted research summary: Halmashauri must collect solid waste from designated waste enclosures in each ward, and people must not put liquid or explosive/harmful waste in bins or burn/bury solid waste without council permission.
12.-(1) Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu kutoka katika vizimba vya taka vilivyoainishwa katika kila kata. (2) Taka ngumu zote zitakazokusanywa kwenye mapipa ya taka zitabaki kuwa mali ya mkazi au mmliki wa eneo lile mpaka zitakapokuwa zimefikishwa kwenye kizimba cha taka au zitakapokuwa zimetolewa na Wakala kutoka katika eneo lake. (3) Mtu yeyote hataruhusiwa- 4 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) (a) kuweka uchafu wenye asili ya maji maji kwenye pipa la taka au kitu chochote kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara; au (b) kuchoma au kufukia taka ngumu bila kibali cha Halmashauri. Eneo la kutupa taka - 13 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupia taka, iweke vyombo maalum vya kuhifadhia taka, na itoe huduma ya uzoaji taka kwa malipo.
13.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa: (a) kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupa taka; (b) kuweka vyombo maalum vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye dampo. (2) Halmashauri itatoza gharama za utupaji wa taka katika jalala (dampo) kutoka kwa mawakala, wamiliki wa taasisi mbalimbali, viwanda na kampuni pamoja na wazalishaji wengine wa taka kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu. - 14 Verify source ↗
(1) Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi
AI-assisted research summary: This provision sets the last Saturday of each month as a communal cleaning day and requires residents and every person to keep specified nearby areas clean.
14.-(1) Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi itakuwa ni siku maalamu ya kufanya usafi wa pamoja wa mazingira katika maeneo ya makazi na umma. (2) Kila mkazi katika kijiji na kitongoji atakuwa na wajibu wa kushiriki katika usafi wa mazingira kwa siku iliyopangwa na Halmashauri katika eneo lake na maeneo ya umma. Siku ya usafi wa pamoja vinavyomzunguka, (3) Kila mtu atahakikisha eneo la makazi yake na vichochoro analofanyia biashara, eneo la wazi lililo karibu naye kwa umbali wa mita kumi na eneo la mazingira ya Ofisi ni safi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. eneo Wajibu wa kuwa na na choo kukitumia - 15 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba au mpangaji lazima ahakikishe nyumba ina choo safi na sehemu ya kunawia mikono yenye maji safi na sabuni.
15.-(1) Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba: (a) nyumba yake ina choo safi, imara kwa matumizi ya wakazi wa nyumba hiyo; (b) anaweka sehemu maalum ya kunawia mikono ikiwa na maji safi na sabuni maalum ya kimiminika. 5 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) (2) Mmiliki wa nyumba au jengo atahakikisha kuwa choo kinajengwa umbali wa mita sitini kutoka chanzo chochote cha maji. Vyoo vya umma - 16 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kujenga choo cha
AI-assisted research summary: The Council may build a public toilet or let private people, groups, or institutions build one in places it considers suitable. Any toilet built under this rule must be permanent and include the listed facilities.
16.-(1) Halmashauri inaweza kujenga choo cha umma au kumruhusu mtu binafsi, vikundi vya watu au taasisi kujenga vyoo vya umma katika maeneo ambayo Halmashauri itaona inafaa. (2) Choo kitakachojengwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kitapaswa kuwa cha kudumu na chenye: (a) matundu yasiyopungua mawili kwa wanawake na mawili kwa wanaume; (b) mfumo madhubuti wa maji na uwepo wa maji ya kutosha yaliyo safi na salama; (c) chombo cha kuhifadhia maji ya akiba; (d) bafu ya wanaume na wanawake; (e) chumba maalumu cha kuvutia sigara; (f) sehemu ya haja ndogo kwa wanaume; na (g) chombo maalumu cha kuhifadhia taka zisizoweza kusukumwa na maji. chenye mfuniko Vyoo vya muda katika mikusanyiko Vikundi vya Usafi - 17 Verify source ↗
Ni wajibu wa mtu yeyote, kikundi au taasisi
AI-assisted research summary: Mtu, kikundi au taasisi inayopanga mkutano, sherehe au mkusanyiko lazima iweke au ijenge vyoo vya muda ikiwa eneo halina choo cha kudumu, na inapaswa kuomba Halmashauri.
17. Ni wajibu wa mtu yeyote, kikundi au taasisi yenye lengo la kukusanya watu kwa madhumuni ya mkutano, sherehe au mkusanyiko wowote kuweka au kujenga vyoo vya muda endapo eneo hilo hakuna choo idhini kutoka cha kudumu na atatakiwa kuomba Halmashauri. - 18 Verify source ↗
Halmashauri
AI-assisted research summary: The Halmashauri must encourage and recognize community groups so they can do solid waste control and environmental cleanliness work in streets after contracting with the Halmashauri.
18. Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika mitaa baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. Marufuku - 19 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kufanya shughuli nyingi za usafi na biashara zilizoandikwa hapa, hasa bila leseni, kibali, au ruhusa ya Halmashauri pale panapohitajika.
19. Mtu yeyote hataruhusiwa- (a) kuendesha biashara ya upulizaji dawa au biashara ya kuua wadudu au wanyama waharibifu katika nyumba yoyote au mahali popote bila cheti cha taaluma kinachotambuliwa na Serikali na leseni kutoka Halmashauri; 6 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) (b) kupanga bidhaa nje ya jengo lake la biashara au barabarani au vichochoroni au katika eneo lolote ambalo halikuidhinishwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (c) kutupa taka za aina yoyote barabarani au eneo lolote la wazi au kwenye vichochoro au kwenye chanzo chochote cha maji au katika eneo lolote ambalo halikutengwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (d) aliye ndani ya gari kudondosha taka ngumu nje ya gari likiwa ndani au nje ya kituo cha magari na sehemu yoyote ile ambapo gari hilo linapita; (e) kuweka kitu chochote kwenye maji taka ambacho kinaweza kuathiri mtu yeyote au kuharibu mfumo wa tiba ya maji taka au kinachoweza kusababisha kuzuia mtiririko wa maji taka; (f) kulima kilimo cha matuta yanayosababisha maji kutuama ndani ya eneo la katikati ya mji; (g) kuchimba mchanga au kokoto au mawe katika vyanzo vya maji au mito barabarani; (h) kuchafua au kuoga au kufulia au kuvuruga maji yanayotumika kwa ajili ya matumizi ya binadamu au wanyama; (i) kuuza mchanga au kokoto na mawe kandokando mwa barabara; (j) kufanya biashara ya pombe ya aina yoyote katika nyumba au kwenye maeneo ya akiba za barabara au mitaani; (k) kuuza matunda au bidhaa nyingine za vyakula barabarani au kuanzisha masoko au magenge ya kuuzia matunda au vyakula au biashara nyingine ndogo bila ruhusa ya Halmashauri; (l) kuunganisha bomba la taka vimiminika katika mifereji ya maji ya mvua; (m) kufungulia au kutiririsha maji ya choo au taka vimiminika katika mkondo asili wa maji ya mvua au barabara au mfereji wa barabara wa maji ya mvua; (n) kujisaidia haja ndogo au haja kubwa barabarani au mitaani au sehemu yoyote isiyokusudiwa kwa madhumuni hayo; 7 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) (o) kubomoa jengo lolote kwa njia yeyote ile bila kupata kibali cha Halmashauri; (p) kufanya mikusanyiko ya kidini au kiutamaduni au kijamii wakati wa milipuko ya magonjwa ya kuambukiza, isipokuwa kwa ruhusa maalum ya Halmashauri na usimamizi wa Afisa Afya; na (q) kuweka uchafu wenye asili ya maji maji kwenye pipa la taka au kitu chochote kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara. Makosa
Part
sehemu yoyote ile ambapo gari hilo linapita;
- 20 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: This section makes it an offence for anyone to do a list of sanitation-related acts, including unsafe toilet placement, dumping waste or wastewater, failing to pay waste fees for two months, operating without Council permission, or lacking required waste and toilet facilities.
20. Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa mtu yeyote- (a) kujenga choo chini ya umbali wa mita 60 kutoka kisimani, bwawani, mtoni, au chanzo kingine cha maji yanayotumika, kwa matumizi ya binadamu; (b) kutoa kinyesi au kusababisha kinyesi, mkojo, maji machafu, yenye kinyesi kutoka kwenye choo chake au bafu lake au karo la kuoshea vyombo au nguo au kutoka kwenye bomba lolote linalochukua maji machafu na kuyatitirisha kwenye barabara, mitaa, au kwenye mifereji ya maji ya mvua, au mfereji wowote uliowazi; (c) kutupa taka au kusababisha mtu mwingine atupe na pasiporuhusiwa popote taka mahali Halmashauri; (d) kutolipa ada ya taka kwa miezi miwili mfululizo; (e) kutembeza vyakula mitaani bila kibali cha Halmashauri; (f) kutokuwa na pipa la taka lenye mfuniko katika eneo la biashara; (g) kutokuwa na choo au kukutwa na choo kibovu au kilichojaa; (h) kukutwa na shimo la maji taka lililojaa au ambalo halina mfuniko; na (i) kutokuwa na chombo maalum cha kukusanyia taka ndani ya gari la abiria (j) kufanya biashara ya kuosha gari, pikipiki au mtambo wowote katika eneo la makazi, eneo la wazi au eneo ambalo halikutengwa kwa shughuli hiyo au kuruhusu eneo lake kutumika kwa 8 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) shughuli za kuosha vyombo vya moto katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hizo bila kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri. Adhabu Kufifilisha kosa - 21 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa
AI-assisted research summary: A person found guilty of an offence under this subsidiary legislation is liable to a fine, imprisonment, or both.
21. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili. - 22 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu maalum ya Jedwali la Nne.
22. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Nne la Sheria Ndogo hii. 9 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) ____________ JEDWALI LA KWANZA ______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 7) Ada ya Ukaguzi wa Afya Namba Aina/ Eneo la Ukaguzi Kiwango cha Ada Kwa mwezi (Shilingi)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: This section lists monthly waste collection and disposal fees for different business types and for waste taken to the council landfill.
3. 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 Nyumba za kulala wageni (guest houses) Hoteli, mighahawa,nyumba za kuuzia vyakula vilivyopikwa Bucha za kuuzia nyama Kibanda na maeneo ya kuchomea nyama Vibanda au maeneo na ya kuchomea nyama, kukaanga chips, nyama na mayai Kumbi za muziki (disko, dansi), Baa Vibanda vya biashara na maeneo ya biashara nyinginezo Maghala ya bidhaa za vyakula Vinywaji. Nyumba za makazi na mazingira ya nyumba za makazi Maduka ya madawa baridi ya binadamu au mifugo Zahanati, kliniki na vituo vya Afya vya na taasisi za watu binafsi Maeneo ya biashara yaliyofungwa baada ya ukaguzi wa awali na kuomba kufanyiwa ukaguzi mpya Duka au kibanda cha biashara ya jumla Ukaguzi wa vioski (groceries) Majengo ya taasisi Vyoo vya kibiashara vinavyoendeshwa na watu binafsi. Karakana na gereji za magari na mitambo Karakana za vyuma na viwanda vya mbao Mtoa tiba asilia Saluni ya kiume 5,000/= 3,000/= 3,000/= 1,000/= 1,000/= 5,000/= 3,000/= 5,000/= HAKUNA MALIPO 5,000/= 3,000/= 3,000/= 3,000/= 2,000/= 2,000/= 3,000/= 3,000/= 2,000/= 1,000/= 2,000/= 10 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) __________ JEDWALI LA PILI ______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 11) Ada ya Huduma ya Ukusanyaji na Uzoaji wa Taka Namba. Aina ya Biashara/ mchangiaji Kiwango cha Ada kwa Mwezi (Shilingi) 1 2 3 4 5 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 Mgahawa mdogo/ kibanda cha kuuzia chai au chakula Kioski na Glosari Nyumba ya kulala wageni (Guest house) Zahanati (Taka zisizo hatari) Kituo cha Afya (Taka zisizo hatari) Fundi Seremala Fundi chuma Karakana au gereji za magari Karakana nyinginezo Duka la jumla/ Super markets au mini Super markets Duka la reja-reja Duka dogo la vyakula Duka kubwa la vyakula Baa (Bar) Kumbi za Starehe/ disko Duka la kuuza samaki au nyama (bucha ya samaki au nyama) Kibanda au kituo cha Nyama choma/ chips kinachojitegemea Duka la Dawa (Jumla na rejareja) Duka la dawa la rejareja Kiwanda kidogo kwa kila trip 5 tu Fundi cherehani Saluni ya Wanaume au Wanawake Kibanda au mwavuli wa kuuza vocha za simu Kituo cha Kuuzia nishati ya mafuta (Filling station) Washona viatu Wauza viatu vya mitumba/ dukani Wauza nguo za mitumba Toroli la bidhaa au matunda Stoo za mkaa Stoo za mbao Mama/ Baba Lishe Duka la kuuzia vipuli vya magari Kila kaya Kila meza ndani ya Soko Ofisi za Taasisi kama benki, posta na nk Duka la vifaa vya kuandikia na duka la kuuza vitabu Duka la dawa baridi za binadam, duka la dawa za mifugo au pembejeo za kilimo Maghala 11 3,000/= 3,000/= 3,000/= 3,000/= 3,000/= 5,000/= 2,000/= 5,000/= 5,000/= 5,000/= 2,000/= 2,000/= 3,000/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= 3,000/= 2,000/= 1,000/= 30,000/= 2,000/= 3000/= 500/= 5,000/= 2,000/= 1,000/= 1,000/= 1,000/= 5,000/= 5,000/= 2,000/= 10,000/= 1,000/= 200/= 10,000/= 5,000/= 3,000/= 5,000/= Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) ____________ JEDWALI LA TATU ______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 13(2)) ______________ Gharama za Utupaji Taka Kwenye Jalala la Taka la Halmashauri. Namba. 1 2 Kiasi cha Taka Ada kwa Mwezi (Shilingi)) Taka za aina yoyote kwa kiwango cha ujazo chini ya tani moja Taka za aina yoyote kwa kiwango cha ujazo kuanzia tani moja hadi tani saba 10,000/= 20,000/= 12 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) ______________ JEDWALI LA NNE ______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 22) HATI YA KUFIFILISHA KOSA Mimi;………………………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya;…………………………………….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, kwamba mnamo tarehe…… ya Mwezi….…. Mwaka…….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, niko tayari kulipa kiasi cha ada ninayodaiwa kwa kiasi cha shilingi ……………….. pamoja na faini ya kufifilisha kosa ya kiasi cha shilingi ………………………... NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe;…....... ya Mwezi;………… Mwaka;………….. Jina;…………………………………..……………………. Saini;…………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jina:…………………………….………..…………………… Wadhifa:…………………………………………………..……. Saini:………………………………………………………… Tarehe:………………………………………………………. 13 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Tangazo la Serikali Na.11 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imegongwa katika Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio la Mkutano wa Baraza la Madiwani ulioketi katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Madaba tarehe 28/7/2023 na kushuhudiwa lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- SAJIDU IDRISA MOHAMED, Mkurugenzi mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, Madaba TEOFANES TADEI MLELWA, Mwenyekiti, Halmashauri ya wilaya, Madaba L.S NAKUBALI, Dodoma, 30 Januari, 2024. MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 14
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira na Ukaguzi wa Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in