Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
This section gives the short title of the bylaw.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the bylaw. This bylaw applies in the area of Kilwa District Council. This section defines key terms used in the by-law. Muegeshaji wa chombo cha usafiri lazima kufuata masharti yaliyowekwa katika Sheria Ndogo hii. Wamiliki wote wa magari ya abiria na mizigo yanayosafiri kwenda au kutoka maeneo ya mjini na nje ya mjini lazima waingie katika eneo lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na mizigo.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Showing 19 of 19
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the bylaw.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la
AI-assisted research summary: This bylaw applies in the area of Kilwa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni malipo yanayolipwa Halmashauri kwa ajili ya kibali cha kuegesha chombo cha usafiri; “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “gari” maana yake ni chombo chochote kinachotumika kusafirisha abiria au mizigo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine isipokuwa mikokoteni, baiskeli na wanyama wanaotumika kubeba watu au mizigo; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, “kituo cha basi” maana yake ni kituo cha basi kilichoidhinishwa na Halmashauri ambapo mabasi yanatoa huduma ya kushusha na kupakia abiria na mizigo; 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa “maegesho” maana yake ni sehemu iliyotengwa au iliyoidhinishwa na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha magari; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa au afisa aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mmiliki” maana yake ni mwenye gari na inajumuisha dereva au kondakta anayetumia gari; “stendi kuu” maana yake ni eneo lililoidhinishwa na Halmashauri ambapo magari yanayotoa huduma ya usafiri kwa umma kuelekea mikoani na maeneo yaliyo ndani na nje ya Halmashauri huanzia na kumalizia safari; “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, kampuni au taasisi iliyoingia mkataba kutekeleza jukumu lolote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. - 4 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa muegeshaji wa chombo
AI-assisted research summary: Muegeshaji wa chombo cha usafiri lazima kufuata masharti yaliyowekwa katika Sheria Ndogo hii.
4. Itakuwa ni wajibu wa muegeshaji wa chombo cha usafiri kufuata masharti yaliyowekwa katika Sheria Ndogo hii. - 5 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa magari ya
AI-assisted research summary: Wamiliki wote wa magari ya abiria na mizigo yanayosafiri kwenda au kutoka maeneo ya mjini na nje ya mjini lazima waingie katika eneo lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na mizigo.
5. Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa magari ya abiria na mizigo yanayotoka au kwenda mikoani na maeneo yaliyo ndani na nje ya Halmashauri, kuingia katika eneo lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na mizigo. - 6 Verify source ↗
Halmashuri itakuwa na wajibu wa kusimamia
AI-assisted research summary: Halmashuri must supervise all parking areas established within the council area and ensure this bylaw is implemented.
6. Halmashuri itakuwa na wajibu wa kusimamia maegesho yote yatakayoanzishwa katika maeneo yote ndani ya Halmashauri na kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Wajibu wa muegeshaji Wajibu wa mmiliki wa magari ya abiria na mizigo Wajibu wa Halmashauri Maeneo ya maegesho - 7 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na uwezo wa kutenga
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kutenga maeneo ya maegesho ya magari na maeneo maalumu kwa pikipiki, bajaji na baiskeli; pia inaweza kubainisha idadi ya magari yanayopaswa kuegeshwa na kuainisha baadhi ya maeneo ya vijiji kuwa maegesho yaliyotengwa.
7.-(1) Halmashauri itakuwa na uwezo wa kutenga eneo lolote la Halmashauri kwa madhumuni ya maegesho ya magari. (2) Halmashauri idadi ya magari yanayotakiwa kuegeshwa katika eneo lililotengwa kwa ajili ya maegesho. itabainisha (3) Halmashauri au wakala anaweza kuainisha 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa baadhi ya maeneo katika vijiji kuwa ni sehemu ya maegesho yaliyotengwa. (4) Halmashauri itatenga maeneo maalumu ya maegesho yatakayotumiwa na pikipiki na bajaji kwa ajili ya biashara na baiskeli. Ada ya kibali - 8 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa chombo cha usafiri cha
AI-assisted research summary: Wamiliki wa vyombo vya usafiri vya biashara wanaotaka kuegesha katika maeneo yaliyotengwa lazima wasajili chombo na wapate kibali, walipe ada ya kibali, na wasiingize chombo bila kibali kutoka Halmashauri.
8.-(1) Kila mmiliki wa chombo cha usafiri cha biashara ambaye anataka kuegesha chombo chake katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya maegesho kwa vyombo vya biashara, atatakiwa kusajili chombo chake na kupewa kibali. (2) Kila mmiliki wa chombo cha usafiri cha biashara atatakiwa kulipa ada ya kibali ambacho kitamuwezesha kuegesha chombo chake kwa muda na kama utaratibu inavyoelekezwa katika Jedwali la Kwanza. na Halmashauri utakaowekwa Usimamizi wa kituo cha mabasi (3) Itakuwa ni marufuku kwa mmiliki yeyote wa chombo cha usafiri cha biashara kuegesha chombo chake katika maegesho yaliyotengwa kwa ajili ya kuegesha vyombo vya biashara bila kuwa na kibali cha kuegesha katika maeneo hayo kutoka Halmashauri. (4) Mtu yeyote atapaswa kuegesha chombo chake cha usafiri katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya maegesho kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. - 9 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni marufuku kwa basi
AI-assisted research summary: Buses may not load or unload passengers in the council area except at designated bus stations, must start trips from designated stations unless specially permitted, and vehicles must not be repaired inside bus stations or designated parking areas.
9.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa basi lolote kushusha au kupakia abiria katika eneo la Halmashauri isipokuwa kwenye maeneo yaliyoainishwa kuwa vituo vya mabasi. lolote (2) Mabasi yote yanatakiwa kuanza safari zake katika vituo vya mabasi vilivyoainishwa na Halmashauri, isipokuwa kwa kibali maalum kutoka Halmashauri. (3) Mabasi yote yanayofanya safari za ndani ya eneo la Halmashauri yatatakiwa kusimama katika kituo cha mabasi kwa lengo la kushusha au kupakia abiria kwa muda usiozidi dakika tano, isipokuwa kwa kituo cha kuanzia na kumalizia safari. (4) Itakuwa ni marufuku kwa mmiliki wa basi au gari la aina nyingine kufanya matengenezo ndani ya kituo 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ushuru wa maegesho Maegesho maalum cha basi au katika eneo lililotengwa kwa ajili ya maegesho. (5) Bila kuathiri masharti mengine ya Sheria Ndogo hii, Halmashauri itakuwa na uwezo wa kutangaza au kutenga eneo lolote kuwa kituo cha mabasi au maegesho kama itakavyoona inafaa. - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru kutoka kwa kila
AI-assisted research summary: The council must charge parking fees from vehicle owners in parking areas or bus stations, using the rates in the Second Schedule.
10.-(1) Halmashauri itatoza ushuru kutoka kwa kila mmiliki wa gari lililoegeshwa katika sehemu za maegesho au kituo cha mabasi kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. (2) Ushuru wa maegesho unaweza kulipwa kwa saa, siku, mwezi au mwaka. (3) Mmiliki wa gari atakayelipia ushuru wa maegesho kwa siku, mwezi au kwa mwaka ataruhusiwa kuegesha gari lake katika eneo lolote lililotengwa kwa ajili ya maegesho kwa muda aliolipia bila kudaiwa tena.
Part
Jedwali la Pili.
- 11 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakayehitaji kupangiwa
AI-assisted research summary: A person seeking private parking allocation must apply to the Council or Agency.
11.-(1) Mtu yeyote atakayehitaji kupangiwa maegesho binafsi atawasilisha maombi kwa Halmashauri au Wakala. (2) Baada ya maombi kukubaliwa, mwombaji atawajibika kulipa ushuru wa maegesho yaliyotengwa kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili na ataruhusiwa kutumia sehemu hiyo peke yake bila kuingiliwa. (3) Mtu aliyetengewa eneo kwa ajili ya maegesho binafsi atalipia ushuru wa maegesho endapo atatumia maegesho tofauti na eneo alilotengewa. Ushuru wa stendi - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa stendi kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri ina mamlaka ya kutoza ushuru wa stendi kwa magari yanayoingia stendi kuu na maeneo yaliyotengwa, na kila mmiliki wa gari au chombo cha usafiri kinachotumia stendi lazima alipe ushuru huo.
12.-(1) Halmashauri itatoza ushuru wa stendi kwa magari yote yanayoingia katika Stendi Kuu ya mabasi na maeneo mengine yaliyotengwa kwa matumizi ya stendi kwa namna na kiasi kilichoainishwa katika Jedwali la Tatu. (2) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa gari au chombo chochote cha usafiri kinachotumia stendi kuu au eneo lingine linalotumika kama stendi kulipa ushuru wa stendi. (3) Ushuru wa stendi utalipwa kila gari linapotoka kituoni kuanza au kuendelea na safari zake. 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ushuru wa kulaza gari Gari lililotelekezw a - 13 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa kulaza gari
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge a parking fee for vehicles parked at a stand or other designated area.
13.-(1) Halmashauri itatoza ushuru wa kulaza gari stendi au katika eneo lingine lililotengwa kwa matumizi hayo. (2) Ushuru wa kulaza gari utatozwa kwa kila gari lililolazwa stendi au eneo lililotengwa kwa siku kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Nne . - 14 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kuegesha gari zaidi ya muda aliolipia ushuru.
14.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuegesha gari zaidi ya muda aliolipia ushuru. (2) Mtu yeyote atakayekiuka kanuni ndogo ya (1) atahesabika kuwa ametelekeza gari na Halmashauri au Wakala anaweza kulifunga gari hilo kwa minyororo hadi hapo mtu huyo atakapolipa ushuru anaodaiwa pamoja na faini. (3) Gari ambalo litakuwa limefungwa minyororo zaidi ya saa mbili bila kulipiwa ushuru pamoja na faini litavutwa na kupelekwa kwenye eneo litakaloainishwa na Halmashauri na gharama za kulivuta zitakuwa juu ya mmiliki. (4) Mmiliki wa gari ambalo litavutwa na kuhifadhiwa na Halmashauri ataruhusiwa kuchukua gari baada ya kulipa ushuru unaodaiwa, gharama ya utunzaji, gharama za uvutaji na gharama nyingine ambazo kwa namna moja au nyingine Halmashauri au Wakala atakuwa amegharimia na mmiliki atapewa gari hilo baada ya kutoa uthibitisho wa umiliki wa gari. (5) Gharama ya utunzaji wa gari itakuwa ni shilingi elfu thelathini kwa siku. Zuio la kuegesha gari. - 15 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kuzuia maegesho ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuweka alama za “hakuna kuegesha hapa” au “no parking” na kuzuia maegesho ya magari katika sehemu fulani.
15. Halmashauri inaweza kuzuia maegesho ya magari katika sehemu yoyote kwa kuweka alama “hakuna kuegesha hapa” au “no parking” kwa sababu zifuatazo: (a) kurahisisha mzunguko wa magari; (b) ujenzi au ubomoaji unafanyika katika eneo husika; na (c) ikiwa magari kuegeshwa katika sehemu hiyo inayofanyika kwa shughuli kutakwamisha wakati huo. 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Magari yaliyosamehe wa kulipa ushuru Makosa - 16 Verify source ↗
(1) Magari yafuatayo yamesamehewa kulipa
AI-assisted research summary: Certain vehicles are exempt from parking fees, and the Council may exempt other vehicles with special approval.
16.-(1) Magari yafuatayo yamesamehewa kulipa ushuru wa maegesho chini ya Sheria Ndogo hii: (a) magari yote ya mabalozi na wanadiplomasia; (b) magari ya kubebea wagonjwa; (c) magari ya Serikali; (d) magari ya Jeshi; (e) magari ya Zimamoto; na (f) magari yote yanayotumika kwa ajili ya usafi katika eneo la Halmashauri. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri inaweza kusamehe gari lingine lolote kulipa ushuru wa maegesho iwapo itaridhika na sababu za mwombaji na msamaha huo utatolewa kwa kibali maalum kutoka kwa Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa. - 17 Verify source ↗
Mtu yeyote anatenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaweka makosa kwa mtu yeyote au wakala aliyeteuliwa na Halmashauri akishindwa kulipa, akihamasisha ukwepaji wa ada/ushuru, akizuia maafisa kutekeleza majukumu, au akikiuka masharti ya maegesho na taarifa za ukusanyaji.
17. Mtu yeyote anatenda kosa endapo- (a) atashindwa kulipa ada au ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) atamshawishi mtu au kundi la watu kukwepa au kukataa kulipa ada au ushuru; (c) atamzuia Mkurugenzi, afisa mwidhiniwa au wakala kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (d) atashindwa, atadharau, atakaidi au kukataa kutekeleza na Halmashauri kuhusiana na ulipaji wa ada au ushuru chini ya Sheria Ndogo hii; alilopewa lolote agizo (e) ataegesha gari, pikipiki au bajaji bila kulipa ushuru wa maegesho; (f) ataegesha gari, pikipiki au bajaji katika eneo lisiloruhusiwa; (g) ataegesha gari nje ya mstari uliochorwa kuainisha eneo la kuegesha gari; (h) ataosha gari, pikipiki au bajaji kwenye maegesho; (i) atafanya matengenezo ya gari, pikipiki au bajaji kwenye kituo cha basi au kwenye eneo la maegesho; au 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (j) ataegesha vibaya na kuzuia magari mengine kuegeshwa au kutoka kwenye eneo la maegesho. (2) Wakala aliyeteuliwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii atatenda kosa endapo- (a) atatumia nyaraka za kugushi kwa nia ya kujipatia manufaa yatokanayo na ukusanyaji wa ada au ushuru ndani ya Halmashauri; (b) atashindwa kutoa taarifa au atatoa taarifa za uongo Halmashauri kuhusu bidhaa au huduma zinazotakiwa kulipiwa ada au ushuru; (c) hatawasilisha au atawasilisha kwa kuchelewa makusanyo ya ada au ushuru Halmashauri kulingana na muda aliopewa kwa mujibu wa mkataba; au (d) atashindwa kutunza kumbukumbu sahihi za malipo ya ada au ushuru. - 18 Verify source ↗
(1) Mtu atakayepatikana na hatia kwa kutenda
AI-assisted research summary: A person convicted of an offence under this bylaw may be fined, imprisoned, or both; if the convicted person is an agent, they must also pay the Council the amount related to the fee or tax that should have been paid.
18.-(1) Mtu atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote. (2) Endapo mtu aliyepatikana na hatia ni wakala, pamoja na adhabu iliyoainishwa katika kanuni ndogo ya (1) atalipa Halmashauri kiasi cha pesa alizopaswa kulipa au zilizopaswa kulipwa na mlipa ada au ushuru. Adhabu Kufifilisha kosa - 19 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji hadi shilingi laki mbili ikiwa mkosaji anakiri kwa hiari na kujaza fomu maalumu.
19. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tano. 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ___________ JEDWALI LA KWANZA _________ (Limetenegenezwa chini ya kanuni ya 8(2) ADA YA KIBALI Na. i. ii. iii. iv. v. vi. vii. viii. ix. Aina ya Gari Teksi Gari dogo la mizigo Lori kuanzia chini ya tani 5 Lori kuanzia tani 5 hadi tani 10 Lori zaidi ya tani 10 Pick up Aina nyingine za magari Pikipiki ya matairi mawili Pikipiki ya matairi matatu/Bajaji Kiasi cha Ada 7,500/= 6,500/= 8,000/= 10,000/= 15,000/= 5,000/= 10,000/= 5,000/= 5,000/= ______________ JEDWALI LA PILI ______________ (Limetenegezwa chini ya kanuuni ya 10(1) na 11(2)) USHURU WA MAEGESHO Na. Aina ya Gari i. ii. iii. iv. v. vi. vii. viii. ix. x. Teksi Gari dogo Lori kuanzia chini ya tani 5 Lori kuanzia tani 5 hadi tani 10 Lori zaidi ya tani 10 Pick up Aina nyingine za magari Pikipiki ya matairi mawili Pikipiki ya matairi matatu Magari mengine ambayo hayakutajwa Kiasi cha ushuru kwa saa 200/= 200/= 300/= Kiasi cha ushuru kwa siku 1,000/= 1,000/= 2,000/= Kiasi cha ushuru kwa mwezi 20,000/= 20,000/= 50,000/= Egesho lililotengwa kwa mwaka 200,000/= 200,000/= 500,000/= 400/= 4,000/= 100,000/= 1,000,000/= 500/= 200/= 200/= 100/= 100/= 200/= 5,000/= 1,000/= 1,000/= 100/= 100/= 1,000/= 130,000/= 20,000/= 20,000/= 3,000/= 3,000/= 20,000/= 1,300,000/= 200,000/= 200,000/= 36,000/= 36,000/= 200,000/= _____________ JEDWALI LA TATU _______________ (Limetenegezwa chini ya kanuni ya 12(1)) USHURU WA MAGARI YANAYOINGIA STENDI 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Na. i. ii. iii. iv. v. vi. vii. viii. ix. x. xi. Aina ya Gari Teksi Bajaji Pikipiki Basi la abiria kuanzua 5-15. Basi la abiria chini ya 25 Basi la abiria kuanzia 26-65 Gari dogo la mizigo Gari kubwa la mizigo Magari mengineyo madogo Magari mengineyo makubwa Magari mengine ambayo hayakutajwa Kiasi cha ushuru kwa safari moja (Tripu) 500/= 300/= 200/= 500/= 1,000/= 3,000/= 500/= 2,000/= 500/= 2,000/= 2,000/= _____________ JEDWALI LA NNE ______________ (Limetenegezwa chini ya kanuni ya 13(2)) USHURU WA KULAZA MAGARI Na. Aina ya Gari Kiasi cha ushuru kwa siku i. Basi la abiria zaidi ya 40. ii. Basi la abiria chini ya 40 iii. Basi la abiria chini ya 20 iv. Teksi v. Gari dogo la kawaida vi. Pick up/ Station Wagon vii. Guta viii. Pikipiki ya matairi mawili ix. Pikipiki ya matairi matatu x. Gari la mizigo chini ya tani 5 xi. Gari la mizigo kuanzia tani 5 hadi 10 xii. Gari la mizigo zaidi ya tani 10 xiii. Magari mengineyo madogo xiv. Magari mengineyo makubwa 10,000/= 5,000/= 2,000/= 1,500/= 1,000/= 1,500/= 200/= 400/= 500/= 3,000/= 5,000/= 10,000/= 1,000/= 2,000/= xv. Magari mengine ambayo hayakutajwa 5,000/= 9 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ______________ JEDWALI LA TANO _______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 19) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi …………………………………………… NAKIRI KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya ………………………….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Kilwa, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. NAKUBALI kulipa ada au ushuru ninaodaiwa kwa kiasi cha shilingi ................ pamoja na faini ya kufifilisha kosa kwa kiasi cha shilingi ................... NATHIBITISHA KWAMBA, maelezo niliyotoa hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa MIMI MWENYEWE na kwa hiari yangu kadri ya ufahamu wangu. Leo hii tarehe………….ya mwezi…………..… mwaka 20……………. Jina………………………………..... Saini………........………………...... MBELE YA MKURUGENZI Jina:…………………..................................... Saini:…………………..….............................. Tarehe:.............................................................. 10 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia Azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa uliofanyika tarehe ......... mwezi ......... 20.... mbele ya- HANAN M. BAFAGHI, Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa MHE. ISSA B. MATEKA, Mwenyekiti, Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa NAKUBALI, L.S Dodoma, 29 Agosti, 2024. MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in