Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
This by-law is titled the Kilwa District Council Livestock Management By-law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This by-law is titled the Kilwa District Council Livestock Management By-law, 2024. This by-law is for the Kilwa District Council and says it applies in an area, but the text is incomplete. Section 3 defines key terms used in the by-law. Halmashauri lazima isimamie matumizi bora ya ardhi ya vijiji na utekelezaji wa hatua mbalimbali za usimamizi wa mifugo. Kila mfugaji lazima azingatie masharti ya ufugaji ya Sheria Ndogo hii na atimize mahitaji kadhaa ya ufugaji, ikiwemo matumizi ya ardhi, ufugaji wa ndani, lishe na maji, mafunzo, udhibiti wa magonjwa, alama za utambuzi, kadi ya mifugo, kibali cha usafirishaji ikiwa kinahitajika, na kuuza mifugo katika masoko yaliyoruhusiwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Showing 29 of 29
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This by-law is titled the Kilwa District Council Livestock Management By-law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: This by-law is for the Kilwa District Council and says it applies in an area, but the text is incomplete.
2. Sheria Ndogo hii Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa. itatumika eneo la - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama
AI-assisted research summary: Section 3 defines key terms used in the by-law.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri kwa ajili ya kufanya shughuli iliyokusudiwa chini ya Sheria Ndogo hii; “machinjio” maana yake ni sehemu inayomilikiwa na taasisi ya umma au mtu binafsi iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuchinjia mifugo; “meneja wa machinjio” maana yake ni mtu aliyeteuliwa na Halmashauri kusimamia machinjio; “mifugo” maana yake ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, mbwa, paka, kuku na inajumuisha ndege na wanyama wengine wanaofugwa na binadamu; “mkaguzi wa nyama” maana yake ni mtaalam wa afya ya 1 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mifugo aliyeajiriwa na Serikali na kusajiliwa au kuorodheshwa au kuandikishwa na Baraza la Veterinari Tanzania; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri au afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mmiliki wa machinjio” maana yake ni mtu anayemiliki machinjio binafsi katika eneo la Halmashauri; “msafara wa mifugo” maana yake ni kundi au makundi ya mifugo yanayosafiri kutoka eneo moja kwenda eneo jingine; “njia ya mifugo” maana yake ni njia iliyotengwa mahususi kwa ajili ya kupitisha mifugo; “ufugaji wa ndani” maana yake ni ufugaji na ulishaji wa mifugo ndani ya jengo, zizi au eneo lenye uzio; “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, kampuni au taasisi, iliyoingia mkataba kutekeleza jukumu lolote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri; “zizi” maana yake ni jengo au eneo lililozungushiwa uzio ambalo mifugo iliyokamatwa ambalo litatunzwa na kusimamiwa na Halmashauri. linatumika kuhifadhi Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima isimamie matumizi bora ya ardhi ya vijiji na utekelezaji wa hatua mbalimbali za usimamizi wa mifugo.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kusimamia maandalizi na utekelezaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji; (b) kuelekeza idadi ya mifugo ambayo kila mfugaji anaruhusiwa kufuga kulingana na ukubwa wa eneo; (c) kujenga majosho ya mifugo kwa kushirikiana na wananchi; (d) kutoa elimu ya ufugaji bora kwa jamii kwa ajili ya kuongeza tija; (e) kufanya sensa ya mifugo, kuweka alama na kutoa kadi za mifugo; (f) kutoa chanjo kwa kushirikiana na wafugaji kwa ajili ya kudhibiti magonjwa ya mifugo; na (g) kudhibiti mifugo inayozurura katika eneo la 2 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Halmashauri. Wajibu wa mfugaji - 5 Verify source ↗
(1) Kila mfugaji atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila mfugaji lazima azingatie masharti ya ufugaji ya Sheria Ndogo hii na atimize mahitaji kadhaa ya ufugaji, ikiwemo matumizi ya ardhi, ufugaji wa ndani, lishe na maji, mafunzo, udhibiti wa magonjwa, alama za utambuzi, kadi ya mifugo, kibali cha usafirishaji ikiwa kinahitajika, na kuuza mifugo katika masoko yaliyoruhusiwa.
5.-(1) Kila mfugaji atakuwa na wajibu wa kuzingatia masharti ya ufugaji yaliyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. (2) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo ya (1), kila mfugaji chini ya Sheria Ndogo hii atahakikisha kuwa: (a) anafuga kwa kuzingatia mipango ya matumizi bora ya ilivyoainishwa na Halmashauri kwa kuzingatia kanuni ya 4 ya Sheria Ndogo hii; ardhi kama (b) anafanya ufugaji wa ndani kulingana na maelekezo yaliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii; (c) analisha na kunywesha mifugo anayomiliki kwa kuzingatia kanuni bora za ufugaji; (d) anahudhuria mafunzo ya ufugaji bora; (e) anadhibiti magonjwa ya wanyama kwa kuogesha na kuipatia chanjo mifugo; (f) mifugo inawekewa alama maalumu kwa ajili ya utambuzi; (g) anakuwa na kadi ya mifugo itakayoonesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo; (h) anapata kibali cha kusafirisha mifugo na mazao ya mifugo iwapo anahitaji kusafirisha mifugo au mazao ya mifugo; na (i) anauza mifugo katika soko, mnada au gulio. Kibali cha kufuga wanyama - 6 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakayetaka kufuga mifugo
AI-assisted research summary: Mtu anayetaka kufuga mifugo lazima apate kibali cha kufuga kutoka kwa Halmashauri; kibali ni bure na hutumika kwa miaka mitatu.
6.-(1) Mtu yeyote atakayetaka kufuga mifugo atalazimika kupata kibali cha kufuga kutoka kwa Halmashauri kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. (2) Kibali kilichotajwa katika kanuni ndogo ya (1) hakitakuwa na gharama na kitakua cha miaka mitatu kuanzia tarehe kilipotolewa. (3) Halmashauri inaweza kufuta kibali cha kufuga iwapo mfugaji atakiuka masharti ya ufugaji yaliyoainishwa katika kanuni ya tano ya Sheria Ndogo hii. (4) Mfugaji aliyefutiwa kibali cha kufuga anaweza kuomba kibali upya kwa Halmashauri baada ya 3 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kurekebisha kasoro zilizosababisha ukiukaji wa masharti ya kibali. Masharti ya Ufugaji - 7 Verify source ↗
Mfugaji hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Mfugaji haruhusiwi kufanya baadhi ya shughuli za mifugo bila maeneo au vibali vinavyohitajika, ikiwemo kuchunga, kusafirisha, kuuza, kununua, kuingiza au kufuga zaidi ya kiwango kilichoainishwa.
7. Mfugaji hataruhusiwa- (a) kuchunga, kulisha au kunywesha maji mifugo katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hiyo; (b) kusafirisha mifugo kwa kuswaga barabarani; (c) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo lingine bila kibali kutoka moja hadi Halmashauri; (d) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (e) kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo siyo mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoidhinishwa bila kibali maalum cha Halmashauri; (f) kufuga mifugo zaidi ya idadi iliyoainishwa katika Sheria Ndogo hii; au (g) kununua, kuuza au kufanya Biashara ya kubadilishana aina yoyote ya mifugo la Halmashauri katika isipokuwa kwenye minada au magulio yaliyotengwa kwa shughuli hiyo na Halmashauri. lolote eneo Kibali cha kusafirisha mifugo - 8 Verify source ↗
(1) Mtu ambaye anataka kusafirisha mifugo na,
AI-assisted research summary: An importer/exporter of livestock or livestock products in a council area must have a special permit. The council issues the permit after proof of ownership and that the animals are healthy, washed, and vaccinated. An authorised officer may seize livestock moved without a permit.
8.-(1) Mtu ambaye anataka kusafirisha mifugo na, au mazao ya mifugo kutoka au kuingia katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuwa na kibali maalumu kilichoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria ndogo hii. (2) Halmashauri itatoa kibali cha kusafirisha mifugo baada ya mfugaji kutoa uthibitisho wa kumiliki mifugo ikiwa na afya nzuri, imeogeshwa na kupatiwa chanjo kabla ya kusafirishwa. (3) Afisa mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kukamata mifugo inayosafirishwa bila kibali. Kudhibiti mifugo inayozurura - 9 Verify source ↗
(1) Kila mfugaji atakuwa na wajibu wa kuzuia
AI-assisted research summary: Wafugaji lazima waizuie mifugo isizurure nje ya maeneo yaliyotengwa; mifugo iliyokamatwa inaweza kuuzwa kwa mnada chini ya masharti ya taarifa, muda na idhini ya mahakama.
9.-(1) Kila mfugaji atakuwa na wajibu wa kuzuia au kudhibiti mifugo kuzurura katika maeneo ambayo 4 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa hayakutengwa kwa ajili ya malisho na ufugaji. (2) Kwa kuzingatia mpango wa matumizi bora ya itadhibiti ambayo ardhi ya vijiji ulioandaliwa, Halmashauri mifugo katika maeneo inayozurura hayakupangwa kwa matumizi hayo. (3) Endapo mifugo iliyokamatwa haitachukuliwa na mfugaji ndani ya siku saba kuanzia kukamatwa, Halmashauri itakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mifugo hiyo baada ya kupata idhini ya mahakama, na fedha zitakazopatikana zitakabidhiwa kwa mmliki wa mifugo baada ya kutoa faini inayodaiwa, gharama za kuhifadhi mifugo, gharama ya mahakama na gharama ya mnada. (4) Mmiliki wa mifugo iliyokamatwa atatakiwa kulipa faini ya Shilingi elfu kumi (10,000) kwa siku kwa kila mfugo aliyekamatwa. (5) Kabla ya kuuza mifugo kwa mnada, Halmashauri itatoa taarifa ya siku tatu kwa mmiliki na umma kuhusu kusudio hilo. (6) Baada ya mauzo, Halmashauri itakata fedha ya faini, gharama za utunzaji, gharama za mnada na gharama za kesi. Fedha zitakazobakia atapewa mmiliki wa mfugo. (7) Endapo mifugo itakufa kutokana na sababu yoyote, Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama isipokuwa kama kifo kimesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri. - 10 Verify source ↗
(1) Afisa mwidhiniwa anaweza kukagua
AI-assisted research summary: Afisa mwidhiniwa anaweza kukagua mifugo au mazao ya mifugo, kuzuia kuingia au kuuzwa kwa bidhaa hizo ikiwa kuna sababu za msingi za hatari, na kuingia katika nyumba au jengo kwa ukaguzi ndani ya saa za asubuhi hadi jioni.
10.-(1) Afisa mwidhiniwa anaweza kukagua la mifugo au mazao ya mifugo ndani ya eneo Halmashauri na anaweza kukataa aina yoyote ya mifugo au mazao ya mifugo kuingia au kuuzwa ndani ya eneo la Halmashauri, iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kwamba mifugo au mazao ya mifugo yanaweza kuhatarisha afya au usalama wa mifugo mingine au watumiaji. (2) Afisa mwidhiniwa anaweza kuingia katika nyumba au jengo lolote kati ya saa kumi na mbili kamili asubuhi na saa kumi na mbili kamili jioni kwa lengo la 5 Ukaguzi wa mifugo na mazao ya mifugo Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Operesheni maalum ya ukaguzi wa mifugo Taratibu za biashara ya mifugo na mazao ya mifugo utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. - 11 Verify source ↗
Kutakuwa
AI-assisted research summary: Halmashauri itaandaa operesheni maalumu ya kufuatilia, kukagua, au kukamata mifugo inayozurura au inayofugwa kinyume na matakwa ya Sheria Ndogo hii.
11. Kutakuwa operesheni maalumu na itakayoandaliwa na Halmashauri kwa kushirikiana na wataalamu pamoja na wadau wengine kutoka katika vyombo vya usalama kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji, ukaguzi, au ukamataji wa mifugo inayozurura au inayofugwa bila kuzingatia matakwa ya Sheria Ndogo hii. - 12 Verify source ↗
(1) Kabla ya kuanza biashara ya mifugo na
AI-assisted research summary: Kabla ya kuanza biashara ya mifugo na mazao ya mifugo, mfanyabiashara lazima awe na leseni, utambulisho na vibali vinavyohusika, na shughuli nyingi za uuzaji, usafirishaji na minada ya mifugo zinahitaji vibali vya Halmashauri.
12.-(1) Kabla ya kuanza biashara ya mifugo na mazao ya mifugo, mfanyabiashara atatakiwa kuwa na leseni, utambulisho na vibali kutoka mamlaka husika vinavyohusu kuuza na kununua mifugo na mazao ya atatakiwa kuwasilisha vibali vyake mifugo na Halmashauri kwa ajili ya uhakiki. (2) Mfanyabiashara wa mifugo inayopelekwa au kutoka mnadani au machinjioni atatakiwa kuwa na kibali kutoka Halmashauri. (3) Mfanyabiashara atakayesafirisha mifugo kutoka nje ya Halmashauri atatakiwa kuwa na kibali kutoka Halmashauri ambayo mifugo hiyo inatoka. (4) Mfanyabiashara wa mifugo katika kusafirisha mifugo vinavyokubalika kwa mujibu wa sheria. vyombo atatakiwa usafiri vya (5) Mifugo itauzwa au kununuliwa katika minada na masoko yanayotambulika kwa mujibu wa sheria. (6) Minada ya mifugo au magulio ya mifugo itafanyika kwa kibali maalumu cha Halmashauri na kwenye maeneo yaliyoruhusiwa. Bucha au duka la nyama - 13 Verify source ↗
Mfanyabiashara wa bucha au duka la nyama
AI-assisted research summary: Mfanyabiashara wa bucha au duka la nyama lazima akidhi masharti ya usafi, vifaa, ukaguzi, usajili, na afya ya muuzaji.
13. Mfanyabiashara wa bucha au duka la nyama atahakikisha - (a) anamiliki leseni na vibali vya kufanya biashara hiyo; (b) anatumia kabati la vioo la kuzuia inzi na wadudu wengine wataambao; (c) anaweka pipa la kuhifadhia taka ngumu na laini; (d) anaweka jokofu la kuhifadhia nyama; (e) jengo la biashara lina mwanga wa kutosha, 6 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa umeme, maji safi na salama, visu, meza, mzani wa kawaida au mzani wa kielektroniki, na misumeno maalumu ya kukatia nyama; (f) nyama imekaguliwa na mkaguzi aliyeidhinishwa na kugongwa muhuri; (g) muuzaji anavaa sare nyeupe muda wote ambazo ni mabuti, koti na kofia; (h) muuzaji anapima afya kila baada ya miezi sita na kuhakikisha anakuwa na cheti cha upimaji; (i) anatoa ushirikiano kwa wakaguzi mara atakapotakiwa kufanya hivyo wakati wowote wa ukaguzi; (j) anatambuliwa na kusajiliwa na mamlaka nyingine husika za Serikali kwa mujibu wa sheria; na (k) biashara ya nyama inafanyika katika bucha na maduka maalumu. Usafirishaji wa nyama - 14 Verify source ↗
(1) Mfanyabiashara wa nyama atatakiwa
AI-assisted research summary: Mfanyabiashara wa nyama lazima asafirishe nyama kwa gari maalumu; akitumia pikipiki au baiskeli, lazima atumie chombo maalumu kilichoainishwa na Halmashauri.
14.-(1) Mfanyabiashara wa nyama atatakiwa kusafirisha nyama kutoka machinjioni kwa kutumia gari maalumu na endapo atatumia usafiri wa pikipiki au baiskeli atatakiwa kubeba nyama kwa kutumia chombo maalumu kilichoainishwa na Halmashauri. (2) Kila mmiliki au mtumiaji wa gari la kubeba nyama atahakikisha kuwa gari- (a) limesajiliwa na kupewa cheti maalumu cha ukaguzi na Halmashauri; (b) linakaguliwa kila baada ya miezi mitatu; (c) lina sanduku la aluminiamu lenye mfuniko na limepakwa rangi nyeupe, mstari mwekundu na namba; (d) halibebi kitu kingine tofauti na nyama; na (3) Kila mmiliki au mtumiaji wa gari la kubeba usafirishaji gharama za kulipia atapaswa nyama zilizowekwa na Halmashauri. Kuingiza wanyama katika machinjio - 15 Verify source ↗
(1) Meneja wa machinjio au mmiliki wa
AI-assisted research summary: Meneja au mmiliki wa machinjio lazima athibitishe umiliki wa mnyama kabla ya kuingiza mnyama eneo la machinjio, akague kibali cha usafirishaji na nyaraka nyingine za umiliki, na atunze rejista ya wanyama waliopokelewa.
15.-(1) Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atakuwa na wajibu wa kuhakikisha umiliki wa mnyama anayekusudiwa kuchinjwa unathibitishwa kabla ya kuingizwa katika eneo la machinjio. (2) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo ya (1), 7 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atakagua kibali cha usafirishaji wa mnyama na nyaraka nyingine zinazothibitisha umiliki. (3) Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atatunza rejista ya wanyama waliopokelewa machinjioni ambayo itaainisha aina ya mnyama, jinsi, umri na taarifa za mmiliki Taratibu za kutembelea eneo la machinjio - 16 Verify source ↗
Mtu anayetaka kutembelea eneo la machinjio,
AI-assisted research summary: Mtu ambaye hahusiki na shughuli za kila siku za machinjio lazima aombe kibali kwa maandishi kabla ya siku ya kutembelea; meneja au mmiliki anaweza kuruhusu ziara na anaweza kuhitaji mavazi maalum.
16. Mtu anayetaka kutembelea eneo la machinjio, iwapo mtu huyo hahusiki na shughuli za kila siku katika machinjio, atatakiwa kuomba kibali kwa maandishi kabla ya siku ya kutembelea na meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio anaweza kumruhusu mtu huyo na kumtaka kuvaa mavazi maalum yanayopatikana katika eneo la machinjio. Ukaguzi wa wanyama - 17 Verify source ↗
(1) Mkaguzi wa nyama atakagua mfugo
AI-assisted research summary: Mkaguzi wa nyama lazima akague mifugo inayoingia machinjioni, na afisa mwidhiniwa anaweza kuchukua hatua za kuwatenga, kuwahamishia matibabu, au kuamuru kuteketezwa ikiwa mmiliki hatatii maelekezo ndani ya saa 12.
17.-(1) Mkaguzi wa nyama atakagua mfugo unaoingizwa katika machinjio kwa ajili ya kuchinjwa. Sura ya 156 (2) Endapo mfugo utagundulika kuwa na magonjwa hatarishi kwa afya ya binadamu, mkaguzi atamhifadhi katika eneo maalum kwa ajili ya matibabu au taratibu nyingine. (3) Kabla ya mnyama kutengwa, taratibu zilizoainishwa katika Sheria ya Magonjwa ya Wanyama zitafuatwa. (4) Endapo mnyama aliyetengwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (2) ataendelea kuwa na magonjwa yaliyosababisha atengwe, afisa mwidhiniwa atamtaka mmiliki wa mnyama huyo kumtoa nje ya eneo la machinjio kwa matibabu zaidi. (5) Endapo mmiliki atashindwa kumwondoa mnyama aliyetengwa ndani ya muda wa saa kumi na mbili tangu kutolewa kwa maelekezo ya kuondolewa, afisa mwidhiniwa anaweza kuamuru mnyama huyo kuteketezwa kwa gharama ya mmiliki. (6) Afisa mwidhiniwa atakuwa na wajibu wa kuchukua kumbukumbu za mmiliki na mnyama aliyebainika kuwa na magonjwa na kumweka alama maalum itakayomtambulisha mnyama huyo. Udhibiti wa shughuli za machinjio - 18 Verify source ↗
(1) Meneja au mmiliki wa machinjio
AI-assisted research summary: Meneja au mmiliki wa machinjio lazima aendeshe shughuli za machinjio kwa kuzingatia taratibu za afya, na watu mbalimbali wanazuiwa kufanya biashara, kuchinja, kuingiza au kutoa mifugo/nyama kinyume na masharti yaliyotajwa.
18.-(1) Meneja au mmiliki wa machinjio atahakikisha kuwa shughuli za machinjio zinaendeshwa 8 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa kuzingatia sheria na taratibu za afya ikiwa ni pamoja na- (a) watoa huduma kupima afya kila baada ya miezi mitatu; (b) watoa huduma kuwa wasafi na kuvaa mavazi maalumu kwa ajili ya kazi hiyo; (c) kutoruhusu mkusanyiko isipokuwa kwa kibali maalumu kitakachotolewa na Halmashauri; (d) kutoruhusu kufanyika biashara nyingine yoyote katika eneo la machinjio. (2) Mtu hataruhusiwa kuweka bucha, duka la nyama au biashara yoyote ya nyama ndani ya mita mia mbili kutoka eneo la machinjio. (3) Mfanyabiashara ya nyama anapaswa kuwa amesajiliwa na Bodi ya Nyama na awe na leseni ya biashara. (4) Mtu hataruhusiwa kuchinja mifugo bila mifugo hiyo kufanyiwa ukaguzi. (5) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchinja mifugo mahali pengine ambapo sio machinjio isipokuwa kwa kutoa taarifa kwa afisa mwidhiniwa. (6) Mtu yeyote hatoruhusiwa kuingiza mifugo katika machinjio kwa ajili ya kuchinja baada ya saa kumi na moja kamili isipokuwa kwa kibali cha Halmashauri. jioni (7) Mtu hataruhusiwa kutoa mifugo hai, iliyokufa au nyama nje ya eneo la machinjio bila ya idhini ya maandishi ya meneja au mmiliki wa machinjio. (8) Haitakuwa ruksa kwa mtu mwenye majeraha, michubuko au ugonjwa unaoambukiza kwa njia ya hewa au kugusana kuingia katika eneo ya machinjio au eneo la uzalishaji wa nyama isipokuwa kwa kibali cha daktari. - 19 Verify source ↗
(1) Mkaguzi wa nyama atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Mkaguzi wa nyama lazima akague nyama baada ya kuchinjwa, aweke muhuri nyama inayofaa, ashughulikie nyama isiyofaa, na meneja au mmiliki wa machinjio lazima atunze rejesta ya nyama zilizokaguliwa.
19.-(1) Mkaguzi wa nyama atakuwa na wajibu wa kukagua nyama katika eneo la machinjio baada ya mnyama kuchinjwa kwa ajili ya kubaini ubora wa nyama kwa matumizi ya binadamu. (2) Endapo itabainika kuwa nyama iliyokaguliwa- (a) inafaa kwa matumizi ya binadamu, mkaguzi 9 Ukaguzi wa nyama Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wa nyama atagonga nyama hiyo muhuri unaothibitisha kuwa nyama iliyokaguliwa ni salama kwa matumizi ya binadamu; au (b) haifai kwa matumizi ya binadamu, nyama hiyo itateketezwa kwa kuchomwa moto au kwa njia nyingine itakayoonekana inafaa na mkaguzi wa nyama atachukua kumbukumbu za nyama hiyo na za mmiliki wake. (3) Endapo matokeo ya vipimo vya awali yatakuwa na mashaka kuhusu ubora wa nyama kwa matumizi ya binadamu, mkaguzi wa nyama atahakikisha kuwa nyama husika inahifadhiwa kwa muda usiozidi saa ishirini na nne ili kuruhusu vipimo zaidi vya kimaabara kufanyika. (4) Meneja au mmiliki wa machinjio atatunza rejesta ya nyama zilizokaguliwa ambayo itaonesha aina ya nyama, jinsi, umri, uzito na taarifa za mmiliki na kama nyama inafaa au haifai kwa matumizi ya binadamu. - 20 Verify source ↗
Meneja au mmiliki wa machinjio atakuwa na
AI-assisted research summary: Meneja au mmiliki wa machinjio lazima atunze rejesta ya mifugo iliyochinjwa na isiyochinjwa, ikionyesha taarifa maalum za kila mfugo na mmiliki wake.
20. Meneja au mmiliki wa machinjio atakuwa na wajibu wa kutunza rejesta ya mifugo iliyochinjwa na ambao haijachinjwa ikionesha aina, jinsi, umri, uzito wa mfugo, na jina na anwani ya mmiliki wa mfugo. - 21 Verify source ↗
(1) Mtu anayefuga au anayekusudia kufuga
AI-assisted research summary: Mtu anayefuga au anayekusudia kufuga mbwa lazima amjulishe Halmashauri, na mfugaji lazima achanje, alipe ada ya chanjo kama ataelekezwa, amzuie mbwa asizurure au kudhuru wengine, amuoshe, na amfunge kwa mnyororo maalumu anapotembea naye. Akikusudia kumpeleka mbwa, lazima awe na kasha maalumu.
21.-(1) Mtu anayefuga au anayekusudia kufuga mbwa atapaswa kutoa taarifa kwa Halmashauri kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya umiliki wa mbwa huyo. (2) Mfugaji atawajibika kumpatia chanjo mnyama wake na kulipa ada ya chanjo kama atakavyoelekezwa na Halmashauri. (3) Mfugaji atawajibika kuhakikisha mbwa anayemfuga hazururi na kuleta madhara kwa wakazi wengine. (4) Mfugaji atawajibika kuogesha mbwa ili kudhibiti magonjwa na wadudu wasumbufu. (5) Mfugaji atalazimika kumfunga mbwa kwa mnyororo maalumu wakati wa kutembea nae kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa mujibu wa Sheria. 10 Rejesta ya mifugo Udhibiti wa ufugaji wa mbwa Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (6) Endapo mfugaji anakusudia kusafirisha mbwa atalazimika kuwa na kasha maalumu. inaweza (7) Halmashauri na kumhifadhi kizuizini kwa muda usiozidi siku saba mbwa anayezurura, na iwapo baada ya muda huo kupita pasipo mmiliki kutambulika, Halmashauri inaweza kuchukua hatua nyingine kadri itakavyofaa. kumkamata Uanzishwaji wa cha kilimo ufugaji wa samaki Kibali cha kutoa huduma za mifugo Makosa
Part
sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa mujibu wa
- 22 Verify source ↗
Halmashauri itahakikisha
AI-assisted research summary: The Council must promote fish farming, set up model fish ponds in every ward, support access to fisheries extension officers, create a fingerling production center, and work with stakeholders on fish farming projects and research.
22. Halmashauri itahakikisha- (a) inahamasisha wananchi juu ya uanzishaji wa kilimo cha ufugaji wa samaki; (b) inaanzisha mabwawa ya mfano ya samaki katika kila kata; (c) inawezesha upatikanaji wa Maafisa Ugani wa Uvuvi kwenye kata na vijiji; (d) inaanzisha kituo cha kuzalisha vifaranga vya ili kurahisisha upatikanaji pindi samaki wafugaji wanapohitaji kununua; na (e) inashirikiana na wadau, mashirika na taasisi mbalimbali kwa ajili ya uanzishaji wa miradi ya ufugaji samaki na tafiti za samaki. - 23 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye anataka kutoa huduma za
AI-assisted research summary: Anayepanga kutoa huduma za mifugo kupitia biashara au vituo vilivyotajwa katika eneo la Halmashauri lazima awe na kibali maalumu.
23. Mtu yeyote ambaye anataka kutoa huduma za mifugo kwa kuanzisha duka la kuuza vyakula vya mifugo, ghala la kuhifadhia vyakula vya mifugo, kiwanda cha kutengeneza vyakula vya mifugo, vituo vya huduma za mifugo au zahanati na vituo vya kutotolesha vifaranga katika eneo la Halmashauri atalazimika kuwa na kibali maalumu kitakachoruhusu kutoa huduma hiyo kama ilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. - 24 Verify source ↗
Mtu anatenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu anafanya kosa akifanya mojawapo ya vitendo vilivyoorodheshwa, ikiwemo kushindwa kuchanja au kuogesha mifugo, kulisha maeneo yasiyoruhusiwa, kuingiza mifugo bila kibali, kufanya biashara fulani ya mifugo bila kibali, kushindwa kutoa taarifa za magonjwa au vifo, au kuzuia maafisa kutekeleza majukumu yao.
24. Mtu anatenda kosa endapo- (a) atashindwa au kukataa kuogesha au kuchanja mfugo au mifugo yake ili kuzuia magonjwa; (b) atalisha mifugo kwenye maeneo yasiyoruhusiwa; (c) ataingiza mifugo kutoka nje ya Halmashauri bila ya kibali; (d) ataanzisha duka la kuuza vyakula vya mifugo, ghala la kuhifadhia mifugo, kiwanda cha kutengeneza vyakula vya mifugo, vituo vya 11 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa huduma za mifugo au zahanati na vituo vya kutotolesha vifaranga bila kuwa na kibali kutoka Halmashauri; (e) atashindwa au kwa makusudi hatatoa taarifa juu ya uwepo wa au dalili za ugonjwa au kifo cha ghafla cha mfugo au mifugo katika banda lake; (f) atashindwa kuwasilisha taarifa ya mwezi ya uuzaji wa vyakula vya mifugo, utengenezaji wa vyakula vya mifugo au ghala, vituo vya huduma za mifugo au zahanati na vituo vya kutotolesha vifaranga; (g) atauza au kufuga mifugo sehemu ambayo haijaruhusiwa; (h) ataruhusu mifugo kuzurura; (i) atakataa kutoa ushirikiano wa uwekaji wa alama kwa mifugo; au (j) atamzuia Mkurugenzi, afisa mwidhiniwa, mkaguzi wa nyama, meneja au mmiliki wa machinjio kutekeleza majukumu kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Adhabu - 25 Verify source ↗
Mtu akipatikana na hatia atawajibika kulipa faini
AI-assisted research summary: A person found guilty must pay a fine, go to prison, or both.
25. Mtu akipatikana na hatia atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichopungua miezi sita jela na kisichozidi miezi kumi na mbili jela au vyote kwa pamoja Kufililisha kosa - 26 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa na kumtoza aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii, lakini kiasi hakipaswi kuzidi shilingi laki mbili na mkosaji lazima akiri kosa kwa hiari na ajaze fomu maalumu.
26. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Nne la Sheria Ndogo hii. 12 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ____________ JEDWALI LA KWANZA ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5(2)(b)) MAELEKEZO KUHUSU UFUGAJI WA NDANI Aina ya mifugo Idadi Maelekezo Namba
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: The permit allows a livestock keeper to raise listed animals in a specified area, taking into account the animal type, the number allowed for the area size, local customs, and any nuisance the livestock may cause.
3. *Maelekezo yajikite kueleza aina ya mifugo, idadi kulingana na ukubwa wa eneo, mila na desturi za wakazi wa eneo husika kwa kuzingatia adha inayoweza kusababishwa na ufugaji* 13 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa _____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 6(1)) KIBALI CHA KUFUGA MIFUGO Jina la Mfugaji:……………………………………………………….. Anuani:…………………………………………………………........... Kata:…………………………………….......Kijiji:…………………......... Namba ya Nyumba:………………………. Namba ya Kitalu:……………... Ameruhusiwa kufuga Mifugo ifuatayo katika eneo la …………........... Namba Aina ya Mfugo Koo Idadi ya Mifugo Jike Dume Jumla
Part
JEDWALI LA PILI
- 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: Hii ni fomu ya kibali cha kusafirisha mifugo, inayotaja taarifa za mwenye kibali, njia ya usafirishaji, na mifugo husika.
12. Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Paka Farasi Sungura Mbwa Kuku/Bata Wanyama wengine Kibali hiki kimetolewa kwa ndugu……………………………………leo tarehe…………na kitamaliza muda wake tarehe ….………………. Kimetolewa na: Jina.......................................................................................................... Saini……….............................................................................................. Wadhifa: ……………………………………………………………….... Tarehe: …………………........................................................................... Muhuri: …………………………………………...................................... 14 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa __________ JEDWALI LA TATU _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 8(1)) A. KIBALI CHA KUSAFIRISHA MIFUGO Jina:……………………………………………. Anuani:………………………………………… Ameruhusiwa kusafirisha mifugo ifuatayo kutoka ………………kupitia njia za……………………..hadi…………..….. Aina ya mifugo Idadi ya Mifugo
Part
JEDWALI LA TATU
- 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: The text provides a livestock entry permit form and a voluntary offence-admission form for Kilwa District Council.
12. Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Paka Farasi Sungura Mbwa Kuku/Bata Wanyama wengine Kibali hiki kitakuwa cha muda wa siku…....... kuanzia tarehe…..........hadi tarehe………. Kimetolewa na : Jina:………………………………………. Saini:……………………………………… Wadhifa:…………………………………… Tarehe:……………………………………… Muhuri:……………………………………… B. KIBALI CHA RUHUSA YA KUINGIZA MIFUGO KATIKA ENEO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA Na Aina ya mnyama Idadi 1 2 3 4 5 6 7 8 9 Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Paka Farasi Sungura Kundi moja Kundi moja 15 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa 10 11 12 Mbwa Kuku /Bata Wanyama wengine Kundi moja Kulingana na aina ya wanyama husika ____________ JEDWALI LA NNE _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 26) FOMU YA KUKIRI KOSA HIARI Mimi………………………………………………………NAKIRI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa kwa kukiuka masharti ya kanuni ya .…… ya Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. KWA NAKUBALI kulipa ada ninayodaiwa ya kiasi cha shilingi .................... pamoja na faini ya kufifilisha kosa ya kiasi cha shilingi ...................... NATHIBITISHA KWAMBA, maelezo niliyotoa hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa MIMI MWENYEWE na kwa hiari yangu kadri ya ufahamu wangu. Leo hii tarehe………….ya mwezi…………..… mwaka 20……………. Jina………………………………..... Saini………........………………...... MBELE YA MKURUGENZI Jina:…………………..................................... Saini:…………………..….............................. Tarehe:.............................................................. 16 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia Azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa uliofanyika tarehe 9/11/2023 mbele ya- HANAN M. BAFAGHI, Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa MHE. ISSA B. MATEKA, Mwenyekiti, Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa NAKUBALI, L.S Dodoma, 29 Agosti, 2024. MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 17
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in