Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025
This section gives the short title of the by-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law. This bylaw applies throughout the area of the Dar es Salaam City Council authority. This section defines key terms used in the by-law, including the Council, permit, livestock, slaughterhouse, and related officials and actors. Halmashauri must carry out several livestock-management duties, including land-use planning, setting herd limits, building dips with the public, education, livestock census and tagging, vaccination services, and controlling roaming animals. Kila mfugaji lazima azingatie masharti ya ufugaji na udhibiti wa magonjwa ya mifugo yaliyoorodheshwa hapa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025
Showing 30 of 30
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika eneo lote la Mamlaka
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the area of the Dar es Salaam City Council authority.
2. Sheria Ndogo hii itatumika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including the Council, permit, livestock, slaughterhouse, and related officials and actors.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; “kaya” maana yake ni baba, mama na watoto wenye umri usiozidi miaka kumi na nane au mtu yeyote aliyetimiza umri wa kuanzia miaka kumi na nane awe na mtoto au bila mtoto; “kero au chukizo” maana yake ni kitu chochote kinachosababisha- (a) hatari kwa viumbe na maisha ya binadamu; (b) harufu mbaya ya kuudhi; (c) kuzaliana kwa wadudu na wanyama hatari au viumbe wengine hatari; (d) magonjwa kwa binadamu; 1 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri kwa ajili ya kufanya shughuli iliyokusudiwa chini ya Sheria Ndogo hii; “machinjio” maana yake ni sehemu iliyotengwa kwa ajili ya kuchinjia wanyama na kuanika ngozi na inajumuisha maeneo na Halmashauri, taasisi ya umma au mtu binafsi yaliyopo katika eneo la Halmashauri; yanayomilikiwa “meneja wa machinjio” maana yake ni kiongozi wa machinjio na Halmashauri yanayomilikiwa aliyeteuliwa kwa mujibu wa Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma ya Machinjio ya Halmashauri; “mifugo” maana yake ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku, nguruwe na wanyama wengine wanaofugwa na binadamu; “mkaguzi wa nyama” maana yake ni mtaalamu wa afya ya mifugo aliyeajiriwa na Serikali na kusajiliwa, kuorodheshwa au kuandikishwa na Baraza la Vetenari Tanzania; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji ya Dar es Salaam au afisa yeyote ya atakayeteuliwa Mkurugenzi; kutekeleza majukumu “mmiliki wa machinjio” maana yake ni mtu yeyote au taasisi inayomiliki machinjio binafsi katika eneo la Halmashauri; “ufugaji wa ndani” maana yake ni ufugaji wa mifugo wa kulishia mifugo ndani ya jengo lililoruhusiwa; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi, shirika au kampuni iliyoteuliwa kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Katika kuhakikisha usimamizi na udhibiti wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must carry out several livestock-management duties, including land-use planning, setting herd limits, building dips with the public, education, livestock census and tagging, vaccination services, and controlling roaming animals.
4. Katika kuhakikisha usimamizi na udhibiti wa mifugo, Halmshauri itakuwa na wajibu wa- (a) kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi; (b) kuelekeza idadi ya mifugo ambayo kila mfugaji anaruhusiwa kufuga kulingana na ukubwa wa eneo lake; (c) kuanzisha na kujenga majosho ya mifugo kwa kushirikiana na wananchi; 2 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) (d) kutoa elimu ya ufugaji bora ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wafugaji kuvuna mifugo yao kwa kuuza wanyama hai au kwa kuchinja na kuuza nyama ili kuongeza tija; (e) kufanya sensa ya mifugo, kuweka alama na kutoa kadi za mifugo; (f) kutoa huduma za chanjo kwa kushirikiana na wafugaji ili kudhibiti magonjwa ya mifugo yasiyoambukiza na yanayoambukiza kwa binadamu; na (g) kudhibiti uzururaji wa mifugo na wanyama katika Halmashauri. Wajibu wa mfugaji - 5 Verify source ↗
Ili kudhibiti kuenea kwa magonjwa ya mifugo,
AI-assisted research summary: Kila mfugaji lazima azingatie masharti ya ufugaji na udhibiti wa magonjwa ya mifugo yaliyoorodheshwa hapa.
5. Ili kudhibiti kuenea kwa magonjwa ya mifugo, kila mfugaji atahakikisha kuwa- (a) anafuga kwa kuzingatia mipango ya matumizi Sura ya 184 bora ya ardhi (b) anafanya ufugaji wa ndani kulingana na maelekezo yaliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii; (c) mifugo inapata malisho, chakula na maji kwa kuzingatia kanuni bora za ufugaji; (d) anahudhuria mafunzo ya ufugaji bora; (e) anadhibiti magonjwa ya wanyama kwa kuogesha na kuipatia chanjo mifugo (f) mifugo inawekewa alama maalumu kwa ajili ya utambuzi kwa kuzingatia Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Wanyama; (g) anakuwa na kadi ya mifugo itakayoonesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo; (h) ana kibali cha kusafirisha mifugo na mazao ya mifugo; (i) anauza mifugo katika masoko na minada iliyoidhinishwa au eneo lingine kwa taarifa maalum. Kibali cha kufuga mifugo mjini - 6 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayekusudia kufuga mifugo
AI-assisted research summary: Mtu anayetaka kufuga mifugo lazima aombe kibali kutoka kwa Halmashauri; kibali hicho hakitozwi ada na kina muda wa miaka mitatu, na Halmashauri inaweza kukifuta kwa ukiukaji wa taratibu za ufugaji.
6.-(1) Mtu yeyote anayekusudia kufuga mifugo atapaswa atapaswa kuomba kibali cha kufuga kutoka kwa Halmashauri. 3 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) (2) Kibali cha ufugaji hakitakuwa na gharama na kitakuwa cha miaka mitatu kuanzia tarehe kilipotolewa. (3) Kibali ufugaji ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. cha kitakuwa kama (4) Halmashauri inaweza kufuta kibali cha mtu yeyote atakayekiuka taratibu za ufugaji zilizoainishwa katika Sheria Ndogo hii. - 7 Verify source ↗
Kila mfugaji hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Every livestock keeper is prohibited from grazing, feeding, watering, moving, selling, buying, or keeping livestock above the number allowed in designated places without the required council permission.
7. Kila mfugaji hataruhusiwa- (a) kuchunga, kulisha au kunywesha maji mifugo katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hiyo; (b) kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani; (c) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo lingine bila kibali kutoka moja hadi Halmashauri; (d) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (e) kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo siyo mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoidhinishwa bila kibali maalumu cha Halmashauri; na (f) kufuga mifugo zaidi ya idadi iliyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. - 8 Verify source ↗
(1) Mtu anayekusudia kusafirisha mifugo na
AI-assisted research summary: A person who wants to transport livestock or livestock products into or out of the Council area must have a transport permit, and the Council is to issue it.
8.-(1) Mtu anayekusudia kusafirisha mifugo na mazao ya mifugo kutoka au kuingia katika eneo la Halmashauri kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii. (2) Halmashauri itatoa kibali cha kusafirisha atatakiwa kibali kuwa na Masharti ya kufuga mjini Kibali cha kusafirisha mifugo mifugo kwa kuweka utaratibu ikiwa ni pamoja na- (a) mfugaji kutoa uthibitisho wa kumiliki mifugo kutoka kwa Afisa Mwidhiniwa; na (b) kukagua kibali cha kusafirisha mifugo. (3) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kukamata na kumtoza faini mtu yeyote ambaye atasafirisha mifugo kinyume na Sheria Ndogo hii. Taratibu za ufugaji - 9 Verify source ↗
Mfugaji yeyote atatakiwa kuzingatia masharti ya
AI-assisted research summary: Any livestock keeper must follow the livestock-keeping conditions set out in this by-law.
9. Mfugaji yeyote atatakiwa kuzingatia masharti ya kufuga kama yalivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. 4 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) Kudhibiti mifugo inayozurura ovyo - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakamata mifugo yoyote
AI-assisted research summary: Halmashauri must seize stray livestock, give seven days’ notice before any auction, and may sell unclaimed livestock by auction with court approval.
10.-(1) Halmashauri itakamata mifugo yoyote la ovyo inazurura katika eneo itakayoonekana Halmashauri. (2) Mifugo itakayokamatwa chini ya kanuni ndogo ya (1) italipiwa faini ya shilingi elfu kumi kwa kila siku kwa kila mfugo. (3) Endapo mifugo iliyokamatwa haitachukuliwa na mmiliki ndani ya kipindi cha siku saba tangu kukamatwa, Halmashauri itakuwa na haki ya kuiuza kwa mnada baada ya kupata idhini ya Mahakama, na fedha zitakazopatikana zitarejeshwa kwa mmliki wa mifugo baada ya kutoa faini inayodaiwa, gharama za kuhifadhi mifugo, gharama ya mahakama na gharama ya mnada. (4) Kabla ya kuuza kwa mnada mifugo iliyokamatwa, Halmashauri itatoa taarifa ya siku saba kwa mmiliki na umma kuhusu kusudio hilo. (5) Endapo mifugo itakufa, Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama kifo kimesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri. iliyokamatwa Ukaguzi wa mifugo na bidhaa za mifugo - 11 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kukataa mifugo au mazao ya mifugo kuingia au kuuzwa, na anaweza kuingia kwenye nyumba, jengo, au eneo kwa masharti ya muda na kwa kibali cha Mkurugenzi katika hali fulani.
11.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kukataa aina yoyote ya mifugo au mazao ya mifugo kuingia au kuuzwa ndani ya eneo la Halmashauri, iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kwamba mifugo hiyo au mazao ya mifugo yanaweza kuhatarisha afya au usalama wa mifugo mingine au watumiaji. (2) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika nyumba au jengo lolote kati ya saa moja na nusu asubuhi hadi saa tisa na nusu alasiri kwa lengo la utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (3) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (2), Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo lolote au jengo lolote kwa muda wowote baada ya kupata kibali cha Mkurugenzi. Taratibu za biashara ya mifugo na - 12 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote kabla ya kuanza biashara ya
AI-assisted research summary: Before starting livestock or livestock-products business, a person must have the required licenses and permits and submit them to the Council for verification.
12.-(1) Mtu yeyote kabla ya kuanza biashara ya mifugo au mazao ya mifugo atapaswa kuwa na leseni, utambulisho na vibali kutoka Mamlaka husika 5 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) mazao ya mifugo vinavyohusu kuuza na kununua mifugo na mazao ya mifugo na atatakiwa kuwasilisha vibali vyake Halmashauri kwa ajili ya uhakiki. (2) Mtu yeyote anayepeleka au kutoa mifugo mnadani au machinjioni atatakiwa kuwa na kibali maalumu kutoka Halmashauri. (3) Mtu yeyote atakayesafirisha mifugo kutoka nje ya Halmashauri atatakiwa kuwa na kibali kutoka Halmashauri ambayo mifugo hiyo inatoka. (4) Mfanyabiashara wa mifugo katika kusafirisha mifugo vinavyokubalika kwa mujibu wa sheria. vyombo atapaswa usafiri vya (5) Mtu yeyote atapaswa kuuza au kununua mifugo katika minada na masoko yanayotambulika kwa mujibu wa sheria. (6) Mifugo itakayokamatwa ikisafirishwa bila kibali au kuuzwa eneo ambalo halijaidhinishwa kwa ajili ya shughuli hiyo, mhusika atalazimika kulipa faini ya shilingi elfu kumi kwa kila mfugo. (7) Minada yote ya mifugo au soko la mifugo litafanyika kwa kibali maalumu cha Halmashauri na kwenye maeneo yaliyoruhusiwa. - 13 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara wa duka la nyama
AI-assisted research summary: Mmiliki au muuzaji wa duka la nyama lazima ahakikishe duka linatimiza masharti ya leseni, vifaa, usafi, ukaguzi wa nyama, mavazi ya muuzaji, afya ya muuzaji, ushirikiano kwa wakaguzi, na uendeshaji ndani ya bucha au maduka maalumu.
13. Kila mfanyabiashara wa duka la nyama anatakiwa kuhakikisha kuwa- (a) ana leseni na vibali vya kufanya biashara hiyo; (b) katika duka lake kuna kabati la vioo la kuzuia inzi na wadudu wengine wataambao na warukao, jokofu la kuhifadhia nyama na pipa la kuhifadhia taka ngumu na laini; (c) jengo analotumia kwa ajili ya biashara lina mwanga wa kutosha, umeme, maji safi na salama, visu, meza, mzani wa kawaida au mzani wa kielektroniki, na misumeno maalumu ya kukatia nyama; Wajibu wa mfanyabiashara wa bucha na maduka ya nyama (d) nyama imekaguliwa aliyeidhinishwa na kugongwa muhuri; na mkaguzi (e) muuzaji anavaa sare nyeupe muda wote ambazo ni mabuti, koti na kofia; 6 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) Usafirishaji wa nyama Kuingiza mifugo katika machinjio (f) muuzaji anapima afya yake kila baada ya miezi sita na kuhakikisha anakuwa na cheti cha upimaji; (g) mmiliki wa bucha au muuzaji wa nyama anatoa ushirikiano wa kutosha kwa wakaguzi mara atakapotakiwa kufanya hivyo wakati wowote wa ukaguzi; na (h) biashara ya nyama inafanyika ndani ya bucha au maduka maalumu. - 14 Verify source ↗
(1) Mfanyabiashara wa nyama atatakiwa
AI-assisted research summary: Meat traders must use a special vehicle to transport meat from the slaughterhouse, or an approved special container if using a motorcycle or bicycle. Owners or drivers of meat-carrying vehicles must also meet registration, inspection, equipment, and load-limitation requirements.
14.-(1) Mfanyabiashara wa nyama atatakiwa kusafirisha nyama kutoka machinjioni kwa kutumia gari maalum na endapo atatumia usafiri wa pikipiki au baiskeli atatakiwa kubeba nyama kwa kutumia chombo maalumu kilichoidhinishwa na Halmashauri. (2) Kila mmiliki au dereva wa gari la kubeba nyama atahakikisha kuwa gari- (a) limesajiliwa na kupewa cheti maalumu cha ukaguzi na Halmashauri; (b) linakaguliwa kila baada ya miezi mitatu; (c) lina sanduku la aluminiamu lenye mfuniko na limepakwa rangi nyeupe, mstari mwekundu na namba; (d) halibebi kitu kingine tofauti na nyama. - 15 Verify source ↗
(1) Meneja wa machinjio au mmiliki wa
AI-assisted research summary: Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio lazima athibitishe umiliki wa mifugo kabla ya kuingizwa machinjioni, akague kibali cha usafirishaji na nyaraka za umiliki, na atunze rejista ya mifugo iliyopokelewa.
15.-(1) Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atakuwa na wajibu wa kuhakikisha umiliki wa mfugo unaokusudiwa kuchinjwa unathibitishwa kabla ya kuingizwa katika eneo la machinjio. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atakagua kibali cha usafirishaji wa mifugo na nyaraka nyingine zinazothibitisha umiliki. (3) Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atatunza rejista ya mifugo iliyopokelewa machinjioni ambayo itaainisha aina ya mifugo, jinsi, umri na taarifa za mmiliki. Taratibu za kuingia machinjioni - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote anaetaka kuingia katika eneo la
AI-assisted research summary: Mtu anayetaka kuingia katika eneo la uzalishaji wa nyama lazima aombe kibali kwa maandishi ndani ya saa 72 kabla ya siku ya kutembelea.
16. Mtu yeyote anaetaka kuingia katika eneo la uzalishaji wa nyama anatakiwa kuomba kibali kwa 7 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) Ukaguzi wa mifugo Sura ya 156 maandishi ndani ya saa sabini na mbili kabla ya siku ya kutembelea na meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio anaweza kumruhusu mtu huyo na kumtaka kuvaa mavazi maalumu yanayopatikana katika eneo la machinjio. - 17 Verify source ↗
(1) Mifugo inayokusudiwa kuchinjwa katika
AI-assisted research summary: Mifugo inayokusudiwa kuchinjwa lazima ikaguliwe kabla ya kuchinjwa, na mifugo yenye ugonjwa hatari au isiyochanjwa iwekwe eneo maalumu kwa matibabu.
17.-(1) Mifugo inayokusudiwa kuchinjwa katika machinjio itafanyiwa ukaguzi wa awali na mkaguzi wa nyama kabla ya kuchinjwa. (2) Endapo baada ya ukaguzi mifugo itagundulika kuwa na magonjwa hatarishi kwa afya ya binadamu au haijachanjwa, mifugo hiyo itahifadhiwa katika eneo maalumu kwa ajili ya matibabu. (3) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na wajibu wa kuchukua kumbukumbu za mfugo aliyebainika kuwa na maradhi na za mmiliki na kumweka alama maalum itakayomtambulisha mfugo huo. (4) Kabla ya mifugo kutengwa, taratibu zilizoainishwa katika Sheria ya Magonjwa ya Wanyama zitafuatwa. (5) Endapo mifugo iliyotengwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (2) itaendelea kuwa na maradhi, Afisa Mwidhiniwa atamtaka mmiliki wa mifugo kuutoa nje ya eneo la machinjio kwa matibabu zaidi. (6) Endapo mmiliki atashindwa kuondoa mifugo iliyotengwa ndani ya muda wa saa kumi na mbili tangu amri ya kuondolewa kwa mifugo itolewe, Afisa Mwidhiniwa anaweza kuamuru mifugo hiyo kuteketezwa kwa gharama ya mmiliki. Uendeshaji wa shughuli za machinjioni - 18 Verify source ↗
(1) Meneja au mmiliki wa machinjio
AI-assisted research summary: Meneja au mmiliki wa machinjio lazima waendeshe machinjio kwa kufuata sheria za afya na usafi. Pia kuna marufuku kwa shughuli fulani za nyama na mifugo ndani na karibu na eneo la machinjio, isipokuwa pale kibali au taarifa maalumu inapohitajika.
18.-(1) Meneja au mmiliki wa machinjio atahakikisha kuwa shughuli za machinjio zinaendeshwa kwa kuzingatia sheria na taratibu za afya ikiwa ni pamoja na (a) watoa huduma kupima afya kila baada ya miezi sita katika hospitali au kituo cha kutolea huduma za afya kwa kadri itakavyoelekezwa na Mkurugenzi; (b) watoa huduma kuwa wasafi na kuvaa mavazi maalumu kwa ajili ya kazi hiyo; 8 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) (c) kutoruhusu mkusanyiko isipokuwa kwa kibali maalumu kitakachotolewa na Halmashauri; (d) kuhakikisha kuwa eneo la machinjio linakuwa katika hali ya usafi wakati wote na kusimamia usafi wa jumla wa machinjio kila siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi; (e) kutoruhusu kufanyika biashara nyingine yoyote katika eneo la machinjio. (2) Mtu hataruhusiwa kuweka bucha, duka la nyama au biashara yoyote ya nyama ndani ya mita mia mbili kutoka eneo la machinjio. (3) Mtu yeyote anayekusudia kuchinja mifugo atatakiwa kupeleka mifugo yake machinjioni au mahali huduma hiyo inapopatikana na itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchinja mifugo kwa madhumuni ya kuuza mahali pengine popote ambapo sio machinjio isipokuwa kwa kutoa taarifa kwa Afisa Mwidhiniwa. (4) Nyama yoyote haitaruhusiwa kutumika kwa matumizi ya binadamu bila kufanyiwa ukaguzi wa mwisho na kuwa na muhuri maalum wa ukaguzi nyama. (5) Mtu yeyote hataruhusiwa kuingiza mifugo katika machinjio kwa ajili ya kuchinja baada ya saa kumi na moja kamili jioni isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa Afisa Mwidhiniwa. (6) Mtu yeyote hataruhusiwa kutoa nje ya eneo la machinjio mifugo hai, iliyokufa au nyama bila ya idhini ya maandishi ya meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio. (7) Mtu hataruhusiwa kuchinja mifugo bila mifugo hiyo kufanyiwa ukaguzi wa awali. Maradhi ya binadamu - 19 Verify source ↗
Mtu anayejua kuwa anauguwa ugonjwa
AI-assisted research summary: A person who knows they have a contagious disease, or has wounds or bruises, must not enter a slaughterhouse or meat production area unless they have a doctor’s permit.
19. Mtu anayejua kuwa anauguwa ugonjwa unaoambukiza kwa kugusana au kwa njia ya hewa au ana majeraha au michubuko hataruhusiwa kuingia katika eneo la machinjio au eneo la uzalishaji wa nyama isipokuwa kwa kibali cha daktari. Ukaguzi wa nyama - 20 Verify source ↗
(1) Mkaguzi wa nyama atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Mkaguzi wa nyama lazima akague nyama baada ya kuchinjwa ili kuthibitisha kama inafaa kwa matumizi ya binadamu, aweke muhuri kwa nyama salama, ateketeze nyama isiyofaa, na aweke kumbukumbu; pia nyama yenye mashaka ihifadhiwe hadi saa 24 kwa vipimo zaidi, na meneja au mmiliki wa machinjio atunze rejista.
20.-(1) Mkaguzi wa nyama atakuwa na wajibu wa kukagua nyama katika eneo la machinjio baada ya mifugo 9 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) kuchinjwa kwa madhumuni ya kubaini iwapo ubora wa nyama kwa matumizi ya binadamu. (2) Endapo itabainika kuwa nyama iliyokaguliwa- (a) inafaa kwa matumizi ya binadamu, mkaguzi wa nyama hiyo muhuri unaothibitisha kuwa nyama iliyokaguliwa ni salama kwa matumizi ya binadamu; au atagonga nyama (b) haifai kwa matumizi ya binadamu, nyama hiyo itateketezwa kwa kuchomwa moto au kwa njia nyingine itakayoonekana inafaa na mkaguzi atachukua kumbukumbu za nyama hiyo na za mmiliki wake. (3) Endapo matokeo ya vipimo vya awali yatakuwa na mashaka kuhusu usalama wa nyama kwa matumizi ya binadamu, mkaguzi wa nyama atahakikisha kuwa nyama husika inahifadhiwa kwa muda usiozidi saa ishirini na nne ili kuruhusu vipimo zaidi vya kimaabara kufanyika. (4) Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atatunza rejista ya nyama zilizokaguliwa ambayo itaonesha aina ya nyama, jinsi, umri, uzito na taarifa za mmiliki na kama nyama inafaa au haifai kwa matumizi ya binadamu. Rejesta ya mifugo, nyama na mmiliki wa mifugo - 21 Verify source ↗
Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio
AI-assisted research summary: Meneja au mmiliki wa machinjio lazima atunze rejesta ya mifugo, nyama na mmiliki wa mifugo iliyo na taarifa za aina, jinsia, umri, uzito, jina na anwani ya mmiliki.
21. Meneja wa machinjio au mmiliki wa machinjio atakuwa na wajibu wa kutunza rejesta ya mifugo, nyama na mmiliki wa mifugo ambayo inaonesha aina ya mfugo, jinsi, umri, uzito, jina na anuwani ya mmiliki wa mifugo. Ada ya shughuli za machinjio Udhibiti wa ufugaji wa mbwa - 22 Verify source ↗
Halmashauri itatoza ada katika biashara,
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima kutoza ada kwa biashara, leseni mbalimbali za huduma, vibali, na mambo yanayohusiana na machinjio kulingana na viwango vya Jedwali la Nne.
22. Halmashauri itatoza ada katika biashara, leseni mbalimbali zinazotolewa huduma, vibali, au kuhusiana na machinjio kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Nne la Sheria Ndogo hii. - 23 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kufuga mbwa
AI-assisted research summary: No one may keep a dog in the council area without a dog-keeping permit from the Council.
23.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kufuga mbwa katika eneo la Halmashauri bila kibali cha ufugaji kutoka Halmashauri. (2) Kibali cha ufugaji wa mbwa kitalipiwa kiasi cha shilingi elfu kumi na kitadumu kwa mwaka mmoja. (3) Mfugaji wa mbwa atakuwa na wajibu ufuatao: 10 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) (a) kuhakikisha mbwa anayemfuga anapata chanjo mbwa wake na analipa ada ya chanjo kama atakavyoelekezwa na Halmashauri; (b) kuonesha cheti cha chanjo ya mbwa kabla ya kupata au kuhuisha kibali kilichoisha muda wake; (c) kumfungia mbwa wake wakati wote wa mchana na anaweza kumfungulia kuanzia saa nne kamili usiku na kumfungia saa kumi na moja alfajir; (d) kuogesha mbwa kila baada ya siku saba ili kudhibiti magonjwa na wadudu wasumbufu; (e) kumfunga mbwa kwa mnyororo maalumu wakati wa kutembea naye kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa mujibu wa Sheria. (4) Iwapo mfugaji atataka kusafirisha mbwa atalazimika kuwa na kasha maalum la kusafirishia mbwa kabla ya kupewa kibali. inaweza (5) Halmashauri na kumhifadhi kizuizini kwa muda usiozidi siku mbili mbwa anayezurura, na iwapo baada ya muda huo kupita hakuna mmiliki aliyetambulika, Halmashauri inaweza kuchukua hatua nyingine kadri itakavyofaa. kumkamata Kibali cha kutoa huduma za mifugo - 24 Verify source ↗
Mtu anayekusudia kutoa huduma za mifugo
AI-assisted research summary: A person who wants to provide veterinary services in the listed settings within a Halmashauri area must have a special permit to do so.
24. Mtu anayekusudia kutoa huduma za mifugo kwa kuanzisha duka la kuuza vyakula vya mifugo, ghala la kuhifadhia vyakula vya mifugo, kiwanda cha kutengeneza vyakula vya mifugo, vituo vya huduma za mifugo au zahanati na vituo vya kutotolesha vifaranga katika eneo la Halmashauri atalazimika kuwa na kibali maalumu kitakachoruhusu kutoa huduma hiyo kama ilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. Makosa - 25 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa iwapo
AI-assisted research summary: This section says a person commits an offence if they do any of the listed livestock, slaughterhouse, or environmental acts.
25. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa iwapo- (a) atashindwa au kukataa kuogesha au kuchanja mifugo yake; (b) yasiyoruhusiwa; atalisha mifugo kwenye maeneo 11 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) (c) ataanzisha duka la kuuza vyakula vya mifugo, ghala la kuhifadhia mifugo, kiwanda cha kutengeneza vyakula vya mifugo, vituo vya huduma za mifugo au zahanati na vituo vya kutotolesha vifaranga bila utaalamu na bila kuwa na kibali kutoka Halmashauri; (d) atafuga mifugo bila kibali cha ufugaji; (e) atashindwa au atazembea kutoa taarifa kuhusu uwepo wa ugonjwa wa mifugo katika banda lake; (f) atauza, atalisha au atafunga mifugo pembezoni ambayo au barabara sehemu mwa haijaruhusiwa; (g) atasababisha kero au chukizo kwa jamii; (h) ataruhusu mifugo yake kuzurura ovyo; (i) atashindwa kutoa ushirikiano wa uwekaji wa alama kwa mfugo au mifugo yake; (j) ataingia katika eneo la machinjio akiwa amelewa au atatumia au kuingiza kilevi katika eneo la machinjio; (k) atatumia lugha za kashfa, kuudhi, kudhalilisha au matusi ndani ya machinjio au kufanya udhalilishaji wa aina yoyote; (l) atabandika au kubandua tangazo lolote bila idhini ya meneja au mmiliki wa machinjio; (m) atahatarisha amani au kushiriki kwa namna yeyote kuhatarisha amani katika eneo la machinjio; (n) atafanya au kushiriki kufanya uchafuzi wa mazingira; (o) atamzuia Afisa Mwidhiniwa kutekeleza majukumu yake. Adhabu - 26 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa
AI-assisted research summary: Anyone convicted of an offence against these by-laws is liable to a fine of up to TZS 300,000, imprisonment of up to 12 months, or both.
26. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa kinyume na Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini ya kiasi kisichozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote. Kufifilisha kosa - 27 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza kiasi kisichopungua shilingi 50,000 ili kufifilisha kosa fulani, ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari, anajaza fomu maalumu ya Jedwali la Tano, na analipa ada inayodaiwa.
27. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya 12 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) Sheria Ndogo hii kiasi kisichopungua shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Tano la Sheria Ndogo hii na kulipa ada anayodaiwa. Kufutwa kwa TS Na. 533 la 2019 - 28 Verify source ↗
Sheria Ndogo za Udhibiti na Usimamizi wa
AI-assisted research summary: This section repeals the 2019 Ilala Municipal livestock control and management bylaws.
28. Sheria Ndogo za Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za Mwaka 2019 zimefutwa. 13 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) ____________ JEDWALI LA KWANZA ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5(4)) IDADI YA MIFUGO ILIYORUHUSIWA KUFUGWA Na.
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Mfugaji anaweza kupewa kibali cha kufuga mifugo kulingana na ukubwa wa eneo lake, bila kusababisha kero au chukizo kwa jamii.
5. Mbuzi au kondoo Nguruwe Mbwa Wanyama wa jamii ya ndege Idadi - - 4 - - Maelezo Mfugaji atapewa kibali cha kufuga kulingana na ukubwa wa eneo alilonalo bila kusababisha kero au chukizo kwa jamii Mfugaji atapewa kibali cha kufuga kulingana na ukubwa wa eneo alilonalo bila kusababisha kero au chukizo kwa jamii Nguruwe watoto wakiachishwa kunyonya wauzwe au kuondolewa Mfugaji atapewa kibali cha kufuga kulingana na ukubwa wa eneo alilonalo bila kusababisha kero au chukizo kwa jamii Mfugaji atapewa kibali cha kufuga kulingana na ukubwa wa eneo alilonalo bila kusababisha kero au chukizo kwa jamii ________________ JEDWALI LA PILI ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 6(1)) KIBALI CHA KUFUGA MIFUGO Jina la Mfugaji:……………………………………………………….. Anuani:………………Nama ya simu…………………………........... Kata:…………………………………… Mtaa …………………......... Namba ya nyumba:………………………… Namba ya kitalu:…………… Ameruhusiwa kufuga Mifugo ifuatao katika eneo la…........…...........…….. Na. Aina ya Mfugo Koo Idadi ya Mifugo Jike Dume Jumla 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Paka Farasi Sungura Mbwa Kuku au Bata Wanyama wengine ambao hawakutajwa 14 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) Kibali hiki kimetolewa kwa Ndugu: ………………………………………kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) kwa mifugo kuanzia tarehe……………..hadi tarehe…………… Kimetolewa na: Jina la Afisa Mwidhiniwa…………………………………..Saini……… Wadhifa:……………………………………………………………….. Tarehe:………………… Muhuri:…………………………………………… 15 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) __________ JEDWALI LA TATU __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 8(1)) KIBALI CHA KUSAFIRISHA MIFUGO Jina:……………………………………………. Anuani:………………………………………… Ameruhusiwa kusafirisha mifugo ifuatayo kutoka ………………kupitia njia za……….......hadi…………..….. Idadi ya Mifugo Namba
Part
JEDWALI LA TATU
- 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaweka ada mbalimbali za shughuli za machinjioni, huduma za nyama, huduma za mifugo, na leseni/ada za shughuli za ngozi.
12. Aina ya Mfugo Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Paka Farasi Sungura Mbwa Kuku au Bata Mifugo mingine ambayo haikutajwa Kibali hiki kitakuwa cha muda wa siku…..... kuanzia tarehe….......hadi tarehe………. Kimetolewa na : Jina la Afisa Mwidhiniwa:………………………………………. Saini:…………………………………………………………….. Wadhifa:………………………………………………………… Tarehe:………………………………………………………….. Muhuri:………………………………………............................ ________________ JEDWALI LA NNE ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 22) ADA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA MACHINJIONI A. Ada ya ukaguzi wa nyama katika machinjio Na. Aina ya mnyama Aina ya machinjio 1 Kwa kila ng’ombe cha Kijiwe kuchinjia (slaughter slab) 4,000 Nyumba kuchinjia (slaughter house) 5,000 16 ya Machinjio ya kisasa (Abattoir) Matumizi ndani ya nchi Matumizi nje ya nchi 15,000 20,000 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) 2 3 4 Kwa kila mbuzi au kondoo Kwa kila nguruwe Kwa kila kuku 1,000 2,000 500 2,500 4,000 500 5,000 5,000 1,000 10,000 10,000 1,500 B. Ada za huduma ya Machinjio B1. Soko la ndani au nje (kupoza nyama) Na. Aina ya chanzo 1 Ada ya kupoza nyama ya ng’ombe mmoja chini ya saa 24 2 3 4 Ada ya kupoza nyama ya ng’ombe mmoja baada ya saa 24 Ada ya kupoza nyama ya mbuzi na kondoo mmoja chini ya saa 24 Ada ya kupoza nyama ya mbuzi na kondoo mmoja baada ya saa 24 Kiasi (kwa shilingi) 15,000 kwa kila siku 20,000 kwa kila siku 10,000 kwa kila siku 15,000 kwa kila siku B2. Soko la ndani au nje (kugandisha nyama) Na. Aina ya chanzo 1 2 Kiasi (kwa shilingi) 20,000 kwa kila siku Ada ya kugandisha nyama nyama ya ng’ombe mmoja Ada ya kugandisha nyama nyama ya mbuzi na kondoo mmoja 15,000 kwa kila siku B3. Kulipua nyama (blasting) ya ng’ombe, mbuzi na kondoo Na. Aina ya chanzo 1 2 Ada ya kulipua nyama ya ng’ombe mmoja Ada ya kulipua nyama ya mbuzi na kondoo mmoja Kiasi (kwa shilingi) 10,000 kwa masaa 12 5,000 kwa masaa 12 B4. Soko la ndani na nje (kupoza mazao mengine ya nyama) Na. Aina ya chanzo 1 Ada ya kupoza mazao ya nyama ya ng’ombe mmoja chini ya masaa 12 Ada ya kupoza mazao ya nyama ya ng’ombe mmoja baada ya masaa 12 Ada ya kupoza mazao ya nyama ya mbuzi na kondoo mmoja chini ya masaa 12 Ada ya kupoza mazao ya nyama ya mbuzi na kondoo mmoja baada ya masaa 12 2 3 4 Kiasi (kwa shilingi) 5,000 kwa kila siku 5,000 kwa kila siku 2,500 kwa kila siku 2,500 kwa kila siku C. Ada nyingine za huduma za machinjio na mabucha Na. Aina ya chanzo 1 2 3 Ada ya kutunza ng’ombe mmoja katika machinjio Ada ya kutunza mbuzi au kondoo mmoja katika machinjio Ada ya kusafirisha nyama kwa gari chini ya tani moja tani 1 hadi 5 zaidi ya tani 5 4 5 6 7 Ada ya pikipiki inayobeba nyama (mabuchani) Ada ya damu mbichi (isiyo na maji) katika machinjio Ada ya damu iliyokaushwa Ada ya matumbo kwa ng’ombe 17 Kiasi (kwa shilingi) 10,000 kwa siku moja 5,000 kwa siku moja 6,000 kwa safari 8,000 kwa safari 10,000 kwa safari 1,000 kila safari 10,000 – 15,000 kwa kila pipa moja 2,000 kwa kilo moja 500 kwa kila moja tumbo Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) 9 Ada ya kichwa kwa mbuzi au kondoo cha ng’ombe cha mbuzi au kondoo tumbo 200 kwa kila moja 500 kwa kila kichwa 200 kwa kila kichwa 1000 la ya 10 11 12 14 15 16 17 kutumia Ada ya miguu ya ng’ombe, mapafu, maini, ulimi na mazao mengine kwa ng’ombe Ada bucha Halmashauri kwa nondo moja kwa mbuzi na kondoo Ada ya masalia ya nyama (vyakula vya mbwa) katika machinjio Ada ya nyongo katika machinjio Ada ya pembe, kwato na mfupa ya ng’ombe, mbuzi na kondoo 100 kwa kilo Ada ya mbolea (Organic Manure) katika machinjio Ada ya jiwe la nyongo (Gallstones) kwa gramu moja (mwenye ng’ombe atajulishwa) Ada ya mazagazaga (vitabu, mikia, via vya uzazi na mengine) 500 100 5,000 10,000 Ada ya gari la kubeba mifugo (parking) 18 19 Mkojo (animal urine) kwa lita 20 1000 kwa siku 500 kwa siku 5000/= kwa kilo 50,000 kwa lori moja 50,000 2,000 kwa kila lita moja chini ya tani 7 kuanzia tani 7 mpaka 10 zaidi ya tani 10 15,000 D. Ada za huduma nyingine za mifugo Na. Aina ya chanzo 1 2 3 Ada ya huduma za ndani kliniki ya mifugo Ada ya huduma za nje kliniki ya mifugo Ada ya uhamilishaji kwa kila ng’ombe au nguruwe mmoja 4 5 Ada ya chanjo za mifugo Ada ya utambuzi, uandikishaji na usajili wa mifugo (uvalishaji hereni) Kiasi (kwa shilingi) 5,000 10,000 kwa mujibu wa miongozo itakayotolewa na Serikali kwa mujibu wa miongozo itakayotolewa na Serikali kwa mujibu wa miongozo itakayotolewa na Serikali E. Ada za leseni za eneo, uchunaji wa ngozi na upangaji madaraja Kiasi (kwa shilingi) 10,000 kwa mwaka 5,000 kila ombi 10,000 kwa mwaka 5,000 kila ombi 10,000 kwa mwaka Na. Aina ya chanzo 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 Ada ya leseni ya uchunaji Ada ya maombi ya leseni ya uchanaji Ada ya leseni ya upangaji wa madaraja ya ngozi Ada ya maombi ya leseni ya kupanga madaraja Ada ya leseni ya banda la kukaushia ngozi Ada ya fomu ya maombi ya leseni ya banda la kukaushia ngozi 20,000 kwa fomu Ukaguzi wa afya Usajili wa vikundi vinavyojihusisha na zao la ngozi Leseni ya ghala la kuhifadhia ngozi zaidi ya 500 Leseni ya ghala la kuhifadhia ngozi 100 - 500 Leseni ya ghala la kuhifadhia ngozi chini ya 500 i. Kuuza ngozi mbichi kwa wakusanyaji (machinjioni) ii. Kuuza ngozi zenye chumvi (wasindikaji) i. Kibali cha kusafirisha ngozi zilizosindikwa zaidi ya tani 5 150,000 kwa safari 40,000 kwa mwaka 100,000 kwa mwaka 100,000 kwa mwaka 50,000 kwa mwaka 10,000 kwa mwaka 100 kwa kipande 200 kwa kipande 13 18 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) ii. Kibali cha kusafirisha ngozi zilizosindikwa tani 1 hadi tani 100,000 kwa safari 5 iii. Kibali cha kusafirisha ngozi zilizosindikwa chinii ya tani 1 25,000 kwa safari _____________ JEDWALI LA TANO _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 27) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kwamba mnamo tarehe …… ya Mwezi ………. Mwaka ……….…… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni …… ya Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, NINAKUBALI kulipa kiasi cha shilingi .............................................. kama faini ya ufifilishaji wa kosa na kiasi cha shilingi ....................... cha ushuru au ada ninayodaiwa. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Saini……………………… Jina……………………………….. MBELE YA MKURUGENZI: Jina:……………………………………..…………………… Saini: ………………………….………………………….…. Tarehe…………………………………………………….… 19 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.43 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Jiji la dar es Salaam imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la dar es Salaam uliofanyika tarehe 6/3/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- JOMAARY MRISHO SATURA, Mkurugenzi wa Jiji, Halmashauri ya Jiji, Dasr es Salaam MHE. OMARY KUMBILAMOTO, Mstahiki Meya, Halmashauri ya Mji, Handeni L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Agosti, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 20
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in