Sheria Ndogo ya Usimamizi na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni ya Mwaka 2025
This provision gives the bylaw its title: the Handeni Town Council Roads Management and Use Bylaw, 2025.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Usimamizi na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni ya Mwaka 2025
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the bylaw its title: the Handeni Town Council Roads Management and Use Bylaw, 2025. Sheria Ndogo hii inatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Mji wa Handeni. Sehemu hii inafafanua maneno muhimu yanayotumika katika Sheria Ndogo hii, ikiwemo afisa mwidhiniwa, kibali, maegesho, teksi, lori, na wakala. Watu hawaruhusiwi kuegesha chombo cha usafiri au mkokoteni nje ya eneo lililotengwa. Halmashauri pia lazima iweke alama za barabarani zinazoonyesha maeneo yaliyotengwa ya kuegesha. Taxis must be registered with the Council before carrying passengers, kept inspected and paid up on required fees, and marked with specified features before inspection and registration.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Usimamizi na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni ya Mwaka 2025
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This provision gives the bylaw its title: the Handeni Town Council Roads Management and Use Bylaw, 2025.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usimamizi na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni ya Mwaka 2025. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: Sheria Ndogo hii inatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Mji wa Handeni.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmshauri ya Mji wa Handeni. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: Sehemu hii inafafanua maneno muhimu yanayotumika katika Sheria Ndogo hii, ikiwemo afisa mwidhiniwa, kibali, maegesho, teksi, lori, na wakala.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chombo cha usafiri” maana yake ni chombo chochote kinachotumika kusafirishia bidhaa, abiria au mizigo; lengo “Halmashauri” maana yake ni Halmshauri ya Mji wa Handeni; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi inayotolewa na Halmashauri; “kituo cha mabasi” maana yake ni eneo maalumu lililotengwa au kujengwa na Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria au mizigo; “kituo cha teksi” maana yake ni kituo kilichosajiliwa na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha teksi; “lori” maana yake ni gari yoyote ya kubeba mzigo yenye uzito kuanzia tani tatu na nusu; 1 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni Tangazo la Serikali Na.45 (Linaendelea.) “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilkanuni ya Mji wa Handeni au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza kazi za Mkurugenzi; “maegesho” maana yake ni sehemu au eneo lilotengwa mahsusi na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha vyombo vya usafiri; “mkokoteni” maana yake ni chombo chochote chenye magurudumu kubeba mizigo ambacho hutembea kwa kusukumwa na binadamu au kukokotwa na mnyama, na itajumuisha guta; kinachotumika “mtaa” maana yake ni eneo lolote ndani ya Kata katika Halmashauri na inajumuisha barabara; “teksi” maana yake ni gari yoyote iliyosajiliwa kwa ajili ya biashara ya kusafirisha abiria au watu yenye uwezo wa kubeba abiria wasiozidi wanne; na “wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, shirika, taasisi au kampuni ambayo imeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. Maegesho - 4 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuegesha chombo
AI-assisted research summary: Watu hawaruhusiwi kuegesha chombo cha usafiri au mkokoteni nje ya eneo lililotengwa. Halmashauri pia lazima iweke alama za barabarani zinazoonyesha maeneo yaliyotengwa ya kuegesha.
4.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuegesha chombo cha usafiri au mkokoteni nje ya eneo lililotengwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Usajili wa teksi taasisi (2) Halmashauri, kwa kushirikiana na zingine, itaweka alama za barabarani za kuonesha sehemu iliyotengwa kwa ajili ya kuegesha vyombo vya usafiri au mkokoteni. - 5 Verify source ↗
(1) Teksi zote zitatakiwa kusajiliwa na
AI-assisted research summary: Taxis must be registered with the Council before carrying passengers, kept inspected and paid up on required fees, and marked with specified features before inspection and registration.
5.-(1) Teksi zote zitatakiwa kusajiliwa na Halmashauri kabla ya kuanza biashara ya kusafirisha abiria. (2) Mmiliki wa teksi atahakikisha kuwa teksi yake imekaguliwa na imelipiwa tozo zote zinazotakiwa. (3) Kila mmiliki wa teksi ana wajibu wa kuchora mstari wa kijani ubavuni mwa teksi, kuweka taa juu ya teksi (noon lamp) na anuani kabla ya teksi kukaguliwa na kusajiliwa. (4) Halmashauri itatoa namba za ubavuni na kuainisha kituo ambacho teksi iliyosajiliwa itaegeshwa mara baada ya usajili. 2 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni Tangazo la Serikali Na.45 (Linaendelea.) (5) Usajili wa teksi utadumu kwa muda wa miezi kumi na mbili. (6) Teksi iliyosajiliwa inatakiwa kuwepo katika kituo cha maegesho ilichopangiwa na kama haitakuwepo kituoni kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo inaweza kufutiwa usajili. Usajili wa vituo vya teksi - 6 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatenga na kusajili maeneo
AI-assisted research summary: The council must set aside and register official areas to be used as taxi stands.
6.-(1) Halmashauri itatenga na kusajili maeneo rasmi kwa ajili ya kutumika kama vituo vya teksi. (2) Halmashauri teksi zitakazoruhusiwa kuegeshwa katika kituo kimoja kwa wakati mmoja kwa kuzingatia ukubwa wa eneo husika. itabainisha idadi ya Malori Uoshaji wa chombo cha usafiri - 7 Verify source ↗
(1) Lori au kontena litaingia katikati ya eneo la
AI-assisted research summary: Lori au kontena linaweza kuingia katikati ya eneo la mji kwa kibali maalumu.
7.-(1) Lori au kontena litaingia katikati ya eneo la mji kwa kibali maalumu kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (2) Kibali kilichotolewa kitatumika kwa safari moja kwa siku moja kwa muda uliotajwa kwenye kibali na kwa barabara zitakazoainishwa ndani ya kibali hicho. (3) Kibali cha kuingiza lori au kontena kitatolewa na Mkurugenzi baada ya kupokea maombi ya maandishi kutoka kwa mwombaji yakiainisha lengo, muda na mahali linapokwenda.
Part
Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii.
- 8 Verify source ↗
(1) Chombo cha usafiri kitatakiwa kuoshwa
AI-assisted research summary: Magari au vyombo vya usafiri lazima vioshwe katika eneo lililotengwa; vikioshwa mahali pasipotengwa vinaweza kuvutwa na kuhifadhiwa, na baada ya siku 14 bila kuchukuliwa vinaweza kuuzwa kwa mnada kwa amri ya Mahakama.
8.-(1) Chombo cha usafiri kitatakiwa kuoshwa katika eneo lililotengwa kwa ajili ya kuosha vyombo vya usafiri. (2) Chombo cha usafiri kitakachokutwa kikioshwa katika eneo ambalo halikutengwa kwa ajili hiyo kitavutwa na kuhifadhiwa katika eneo la Halmashauri. (3) Chombo kilichohifadhiwa kisipochukuliwa na mmiliki ndani ya siku kumi na nne kinaweza kutangazwa kwa ajili ya kupigwa mnada na kuuzwa baada ya kupata amri ya Mahakama na pesa itakayopatikana baada ya mauzo katika mnada itafidia gharama zote zilizotumika katika kuvuta, kuhifadhi na gharama za mnada na kiasi kitakachobakia atakabidhiwa mmiliki wa chombo cha usafiri. (4) Endapo mmiliki wa chombo cha usafiri atajitokeza kabla ya mnada atatakiwa kulipa faini 3 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni Tangazo la Serikali Na.45 (Linaendelea.) Ufungaji wa barabara Uwekaji wa vifaa vya ujenzi barabarani Kukata barabara Kuharibu kingo za barabara na mifereji Makosa iliyoainishwa chini ya Sheria Ndogo hii na gharama ya kuvuta na kuhifadhi chombo cha usafiri. - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote anaweza kufunga barabara kwa ajili
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anaweza kufunga barabara kwa ajili ya sherehe, msiba au shughuli nyingine, lakini lazima apate kibali cha maandishi kutoka kwa Halmashauri.
9. Mtu yeyote anaweza kufunga barabara kwa ajili ya sherehe, msiba au shughuli nyingine yoyote baada ya kupata bila kibali cha maandishi kutoka kwa Halmashauri kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. - 10 Verify source ↗
Mtu yeyote hataweka au kumwaga vifaa vya
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kuweka au kumwaga vifaa vya ujenzi barabarani, katika hifadhi ya barabara, au eneo lisiloruhusiwa bila idhini ya maandishi ya Mkurugenzi.
10. Mtu yeyote hataweka au kumwaga vifaa vya ujenzi kama kokoto, mchanga, kifusi, mawe na vifaa vingine vya ujenzi kwenye barabara, hifadhi ya barabara au eneo lisiloruhusiwa bila ya idhini ya maandishi ya Mkurugenzi. - 11 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kukata barabara kwa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kukata barabara kwa kupitisha mabomba ya maji, nyaya za umeme, simu, au shughuli nyingine bila kibali cha maandishi kutoka kwa Meneja wa Wilaya wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini.
11. Mtu yeyote hataruhusiwa kukata barabara kwa ajili ya kupitisha mabomba ya maji, nyaya za umeme, simu au shughuli nyingine yoyote bila kibali cha maandishi kutoka kwa Meneja wa Wilaya wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini. - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetumia barabara hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Anyone using a road must not damage the road, break its edges, or damage road drains built to maintain and preserve the road.
12. Mtu yeyote anayetumia barabara hataruhusiwa kubomoa barabara au kuvunja kingo za barabara au mifereji ya barabara iliyojengwa kwa ajili ya kutunza na kuhifadhi barabara. - 13 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Anyone commits an offence if they carry out any of the listed road, vehicle, taxi, permit, or obstruction acts.
13. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) ataegesha chombo cha usafiri au mkokoteni katika sehemu isiyoruhusiwa; (b) atafanya biashara ya teksi kwa kutumia gari ambalo halijasajiliwa; (c) ataegesha teksi kwenye eneo ambalo si kituo cha teksi; (d) ataendesha gari tani kubwa katika barabara ya uwezo mdogo ambazo zimezuiliwa kupitisha gari kubwa; lenye (e) atachoma tairi, atamwaga mafuta au maji machafu au kuchoma kitu chochote katika barabara chochote kitakachosababisha uharibifu wa barabara; kufanya au 4 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni Tangazo la Serikali Na.45 (Linaendelea.) (f) ataharibu au kutoa kibao cha alama za barabarani; (g) ataingiza lori au kontena katika eneo la Halmashauri bila kibali; (h) ataosha chombo cha usafiri katika eneo la barabara, hifadhi ya barabara au eneo la wazi ambalo matumizi yake si ya kuoshea magari; (i) atafunga barabara kwa shughuli za sherehe, msiba au shughuli nyingine yoyote bila kibali cha maandishi kutoka kwa Mkurugenzi; (j) atakata barabara bila kibali cha maandishi kutoka kwa Mkurugenzi; (k) ataweka au kuzuia matumizi ya barabara au kumwaga vifaa vya ujenzi kwenye barabara, hifadhi ya barabara au eneo lisiloruhusiwa; au (l) atamzuia afisa au wakala wa Halmashauri kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria Ndodo hii, na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja. Kufifilisha kosa - 14 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji hadi shilingi elfu hamsini, ikiwa mkosaji anakiri kosa na kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Tatu.
14. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii. 5 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni Tangazo la Serikali Na.45 (Linaendelea.) ________________ JEDWALI LA KWANZA ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 7(1)) KIBALI CHA KUINGIZA LORI AU KONTENA KATIKATI YA MJI Kwa MMILIKI WA LORI AU KONTENA, Lenye Namba ya Usajili…………………………. Ndugu:…………………………………………… Tarehe…………………………………………… Mkurugenzi Mtendaji amepitia maombi yako na kuridhika kuwa unayo sifa ya kupewa kibali cha kuingiza na Lori / Kontena katikati ya Mji. Nakiri kuwa nitatii Sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na Halmashauri kwa muda wote nitakapokuwa ndani ya Mji. Mimi:……………………………………………(Mmiliki/Dereva) Tarehe:………………………………..Saini:……………………… Kibali hiki kimetolewa leo tarehe…………Mwezi………..20….. Jina:……………………………………….. Wadhifa:………………………………….. Saini:……………..……………………….. Muhuri:…………………………………… 6 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni Tangazo la Serikali Na.45 (Linaendelea.) _______________ JEDWALI LA PILI ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 9) KIBALI CHA KUFUNGA BARABARA MJINI HANDENI Kwa Ndugu………………………………………………….. Kata ya:………………….Mtaa wa:…………………….. Barabara ya ………………………………………………… Halmashauri ya Mji -Handeni Mkurugenzi Mtendaji amepitia maombi yako ya kufunga barabara kwa muda usiozidi siku ………na kuridhika kuwa unayo sifa ya kupewa kibali cha kufunga barabara hiyo kwa ajili ya shughuli ya ……………………………………………….ndani ya Mamlaka ya Halmashauri ya Mji wa Handeni. Unapewa taarifa kuwa kutokana na maombi hayo na kwa ajili ya shughuli ya ……………………. umepewa kibali cha kufunga kipande cha barabara ya …………………………..iliyopo mkabala na ………………………kwa muda wa siku ……….na si zaidi. Ninakiri kuwa nitalipa ushuru uliowekwa kwa mujibu wa Sheria na nitazingatia Sheria, Kanuni na taratibu zote. Mimi………………………………………………….Saini………………………… Tarehe:……………Mwezi……………Mwaka………….. Kibali hiki kimetolewa leo hii tarehe…………Mwezi:……..20……….. Jina:………………………………………….. Wadhifa……………………………………… Saini:……………….……………………….. Muhuri:……………………………………… 7 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni Tangazo la Serikali Na.45 (Linaendelea.) ______________ JEDWALI LA TATU _______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 16) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya ……ya Sheria Ndogo ya Usimamizi na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni ya Mwaka 2025. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni, niko tayari kulipa faini ya ufifilishaji wa kosa ya kiasi cha shilingi ............................. na ada au ushuru ninaodaiwa wa shilingi ........................... NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Leo tarehe…………. Saini……………………… Jina……………………………….. MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………… 8 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni Tangazo la Serikali Na.45 (Linaendelea.) Nembo ya Halmashauri ya Mji Handeni imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia azimio lililopitishwa katika mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji uliofanyika tarehe 7/2/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- MARYAM A. UKWAJU, Mkurugenzi wa Halmashauri, Halmashauri ya Mji Handeni MUSSA A. MKOMBATI, Mwenyekiti wa Halmashauri, Halmashauri ya Mji, Handeni NAKUBALI, L.S Dodoma, 9 Disemba, 2023 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Usimamizi na Matumizi ya Barabara ya Halmashauri ya Mji wa Handeni ya Mwaka 2025
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in