Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ya Mwaka 2024
Sheria Ndogo hii inatambulisha Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ya Mwaka 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Sheria Ndogo hii inatambulisha Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ya Mwaka 2024. This provision says the by-law applies throughout the entire area of Dar es Salaam City Council. This section defines key terms used in the bylaw, including the municipal council, director, service levy, taxpayer, reporting periods, and agent. Halmashauri must levy and collect service levy from licensed businesses and individuals operating in the area whose annual turnover is above shilingi milioni nne. Mlipa ushuru wa huduma lazima alipe ushuru, awasilishe taarifa na hesabu sahihi, atunze kumbukumbu, na azionyeshe kwa uchunguzi inapohitajika.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ya Mwaka 2024
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: Sheria Ndogo hii inatambulisha Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ya Mwaka 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This provision says the by-law applies throughout the entire area of Dar es Salaam City Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam. Tafsiri Sura ya 212 - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the bylaw, including the municipal council, director, service levy, taxpayer, reporting periods, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; “hesabu” maana yake ni jumla ya mauzo au manunuzi ikiwa ni pamoja na kodi au ada katika mwaka wa mapato; “hesabu za mwisho” maana yake ni taarifa zinazowasilishwa na kampuni au mtu yeyote mwenye leseni ya biashara baada ya kipindi cha hesabu zikijumuisha nyaraka au maelezo yanayohusu thamani ya kifedha ya bidhaa zilizouzwa au huduma zilizotolewa; “kampuni” itakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Kampuni; “kipindi maalum cha hesabu” maana yake ni muda anatakiwa ambao mfanyabiashara 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1005 (Linaendelea.) kuwasilisha hesabu za biashara kwa Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na aliyeteuliwa inajumuisha kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; yeyote afisa Sura ya 212 Ushuru wa huduma “mlipa ushuru wa huduma” maana yake mtu au kampuni inayopaswa kulipa ushuru chini ya Sheria Ndogo hii; “mwaka wa mapato” maana yake ni kipindi cha miezi kumi na mbili ya mwaka wa fedha wa Serikali; “tawi la kampuni” maana yake ni tawi la kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara yeyote mwenye leseni ya biashara kwa utaratibu ulioainishwa katika kanuni ya 4; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi au kampuni iliyoteuliwa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru
AI-assisted research summary: Halmashauri must levy and collect service levy from licensed businesses and individuals operating in the area whose annual turnover is above shilingi milioni nne.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kutoka kwa kila ni kampuni au mtu binafsi mwenye leseni ya biashara anayefanya shughuli zake katika eneo la Halmashauri ambaye mauzo yake kwa mwaka ni zaidi ya shilingi milioni nne. (2) Ushuru wa huduma utatozwa katika kila kipindi cha hesabu kwa viwango vifuatavyo: (a) kwa kampuni au mtu yeyote mwenye leseni ya biashara anayewasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu ya mauzo ya bidhaa au huduma yanayofanyika katika la Halmashuri; au eneo (b) kwa mfanyabiashara wenye leseni ya biashara ambaye hawasilishi hesabu za mauzo Mamlaka 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1005 (Linaendelea.) Tanzania ya Mapato kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (3) Ushuru wa huduma kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (2)(a) utakokotolewa baada ya kutoa kodi ya ongezeko la thamani na ushuru wa bidhaa. kiwango kwa Wajibu wa mlipa ushuru wa huduma Mamlaka ya Mkurugenzi - 5 Verify source ↗
(1) Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa huduma lazima alipe ushuru, awasilishe taarifa na hesabu sahihi, atunze kumbukumbu, na azionyeshe kwa uchunguzi inapohitajika.
5.-(1) Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu wa- (a) kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ya kila mwezi endapo anawasilisha taarifa za hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania; (c) kuwasilisha hesabu sahihi na za kweli; (d) kuwasilisha nyaraka au taarifa inayotakiwa kuwasilishwa Halmashauri ndani ya muda uliowekwa; (e) kutunza kumbukumbu za kitabu cha hesabu; na (f) kuonesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi. (2) Kila mlipa ushuru wa huduma atatakiwa kulipa ushuru huo si zaidi ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kuwasilisha taarifa za mauzo ya kila mwezi. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru wa huduma utaratibu wa kulipa ushuru huo. (4) Kila mlipa ushuru atatakiwa kuwasilisha kwa Halmashauri hesabu za mwisho katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa kipindi cha hesabu. - 6 Verify source ↗
(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa huduma anaweza kupewa notisi ya kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ndani ya siku 30, na ushuru uliotathminiwa hulipwa ndani ya siku 30 tangu tathmini.
6.-(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma atashindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo kwa wakati, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka mlipa ushuru wa huduma kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku thelathini kuanzia tarehe ya kutolewa kwa notisi. (2) Endapo mlipa ushuru hatawasilisha hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha husika na ametakiwa kufanya hivyo kwa notisi ya siku thelathini, Mkurugenzi anaweza kwa kadri atakavyoona inafaa, 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1005 (Linaendelea.) kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (3) Ushuru uliofanyiwa tathmini kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii utalipwa katika kipindi cha siku thelathini tangu tarehe ya kufanya tathmini. (4) Mkurugenzi anaweza, kumtaka kwa maandishi mtu yeyote mwenye taarifa kuhusu mfanyabiashara anayepaswa kulipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumika kama taarifa sahihi. (5) Mkurugenzi anaweza, kumuagiza kwa maandishi Afisa Mwidhiniwa kuingia kwenye jengo au eneo la mlipa ushuru wa huduma kwa nia ya kufanya uchunguzi na tathmini ya kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu na taarifa kwa ajili ya kupata na kujua kiwango sahihi cha ushuru anachotakiwa kulipa. - 7 Verify source ↗
(1) Bila kuathiri mamlaka ya Halmashauri
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuteua Wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri.
7.-(1) Bila kuathiri mamlaka ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii, Mkurugenzi anaweza kuteua Wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa- (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa kwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria Ndogo hii; na (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. - 8 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa anaweza
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia eneo au jengo la mlipa ushuru, kuchunguza taarifa na hesabu, kupokea na kutathmini hesabu zisizo sahihi, na kukataa hesabu za mwisho zenye sababu za kuamini kuwa si sahihi.
8. Afisa Mwidhiniwa anaweza- (a) kuingia kwenye eneo au jengo lolote la mlipa ushuru kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni kwa ajili ya kupata taarifa au kuchunguza hesabu au vitabu au taarifa zozote kama ataona inafaa kwa ajili ya kulipa ushuru wa huduma; 4 Uteuzi wa Wakala Uwezo wa Afisa Mwidhiniwa Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1005 (Linaendelea.) Ukokotoaji wa ushuru wa huduma Makosa (b) kupokea na kukubali hesabu za mlipa ushuru na kuzifanyia tathmini kuhusu kiwango cha hesabu cha mlipa ushuru endapo hesabu hizo zitakuwa si sahihi; au (c) kukataa hesabu za mwisho iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hesabu hizo siyo sahihi. - 9 Verify source ↗
Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikokotoe ushuru wa huduma wa mlipa ushuru anayewasilisha taarifa za mauzo kwa TRA.
9. Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma wa mlipa ushuru anayewasilisha taarifa za mauzo Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuzingatia taarifa zinazowasilishwa na mlipa ushuru wa huduma katika kipindi cha hesabu. - 10 Verify source ↗
Mtu atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: A person commits an offence if they fail to submit correct sales information or pay service tax on time, give false information, obstruct an authorized officer or agent, interfere with tax payment, destroy tax-related information or tools, or otherwise breach these by-laws.
10. Mtu atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atashindwa kuwasilisha Halmashauri taarifa sahihi za mauzo ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) atawasilisha Halmashauri taarifa zisizo sahihi; (c) atashindwa kulipa ushuru wa huduma ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii ; (d) atamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru; (e) atamzuia Afisa Mwidhiniwa au Wakala kutekeleza wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii; (f) atatoa taarifa ya uongo kuhusu jambo lolote linaloweza kuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa ushuru; (g) ataharibu kwa makusudi taarifa au mfumo wa taarifa; (h) ataharibu kwa makusudi vitendea kazi vya kukusanyia ushuru; au (i) atashidwa kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii. Adhabu - 11 Verify source ↗
Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa
AI-assisted research summary: A person convicted of any offence against this bylaw is liable to a penalty.
11. Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa lolote kinyume cha Sheroa Ndogo hii, atawajibika 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1005 (Linaendelea.) Kufifilisha kosa kulipa faini kiasi kisichopungua shilingi laki mbili na kisichozidi au kifungo shilingi milioni moja kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 12 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtenda kosa kiasi kisichozidi shilingi laki mbili, ikiwa mkosaji anakiri kwa hiari, anajaza fomu maalum ya Jedwali la Pili, na analipa ushuru unaodaiwa.
12. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalum kam ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa ushuru anaodaiwa. Kufutwa kwa Sheria Ndogo TS. Na. 531 la 2019 TS. Na. la 2017
Part
Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa ushuru
- 13 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya
AI-assisted research summary: This section repeals two service levy by-laws for Ilala Municipality and Dar es Salaam City Council.
13. Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ya Mwaka 2019 na Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2017 zinafutwa. 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1005 (Linaendelea.) _____________ JEDWALI LA KWANZA ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(2)(a)) USHURU WA HUDUMA Na. Ada ya Leseni ya biashara kwa Mwaka (Shilingi) Kiwango Ushuru (Shilingi) cha Muda wa malipo
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: This form lets a person confess to breaching a specified by-law and agree to pay the service levy owed plus a compounding fine to the City Council Director.
3. 50,001/= hadi 100,000/= 15,000/= Robo Mwaka 100,001/=hadi 200,000/= 30,000/= Robo Mwaka 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1005 (Linaendelea.) _____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 12) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi………………………………………………………nakiri YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ya Mwaka, 2024. HIARI KWA Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, NINAKUBALI kulipa shilingi ............................ ya ushuru wa huduma ninaodaiwa pamoja na faini ya kififilisha kosa ya shilingi .................................... NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………… MBELE YA MKURUGENZI: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….………………………….……… Tarehe………………………………………………… 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1005 (Linaendelea.) Lakiri ya Jiji la Dar es Salaam imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutao wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam uliofanyika tarehe 6/3/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- JOMAARY MRISHO SATURA, Mkurugenzi wa Jiji, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam MHE. OMARY KUMBILAMOTO, Msahiki meya, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Agosti, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in