Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
Kifungu hiki kinaweka jina la Sheria Ndogo.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Kifungu hiki kinaweka jina la Sheria Ndogo. This provision says the by-law applies throughout the Dar es Salaam City Council area. This section defines key terms used in the by-law. The Halmashauri must control beggars across its area and identify beggars. A person is treated as a beggar if found in public asking for money or food, or if found in public displaying wounds or disability to persuade others to give money or to beg for money.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
Showing 11 of 11
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaweka jina la Sheria Ndogo.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This provision says the by-law applies throughout the Dar es Salaam City Council area.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “eneo la wazi” maana yake ni eneo lolote la ardhi lenye bustani au ambalo halijaendelezwa ambalo lipo kwa ajili ya matumizi ya umma; lengo “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; “kituo cha hifadhi” maana yake ni kituo, mahali au jengo lolote linatumika limetengwa kuwahifadhi ombaomba, wazee, watoto au watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwapa mahitaji ya msingi; ambalo au “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mtaa” maana yake ni eneo lolote lililopo ndani ya inajumuisha maeneo yote ya Halmashauri na 1 Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1007 (Linaendelea.) barabara, hifadhi za barabara na njia ya waenda kwa miguu; “ombaomba” maana yake ni mtu yeyote anayeishi kwa kutegemea kuomba chakula, fedha au vitu vingine kutoka kwa mtu mwingine kwenye mitaa, kando ya barabara na maeneo ya wazi yaliyoko ndani ya eneo la Halmashauri; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi au kampuni iliyoteuliwa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii. Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: The Halmashauri must control beggars across its area and identify beggars.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kudhibiti ombaomba kwenye eneo lote la Halmashauri; na (b) kuwatambua ombaomba. Kutambuliwa kama ombaomba - 5 Verify source ↗
Mtu yeyote atatambulika kuwa ombaomba
AI-assisted research summary: A person is treated as a beggar if found in public asking for money or food, or if found in public displaying wounds or disability to persuade others to give money or to beg for money.
5. Mtu yeyote atatambulika kuwa ombaomba endapo- (a) atakutwa mtaani au kwenye eneo la wazi akiomba fedha au chakula kwa mtu au watu wengine; au (b) atakutwa mtaani, kando ya barabara au kwenye maeneo ya wazi akiwa amekaa, amesimama au amelala akionesha vidonda au ulemavu kwa madhumuni ya kushawishi kupewa fedha au kuomba fedha. Uteuzi wa Wakala - 6 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kumteua wakala ambaye
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumteua wakala wa kusaidia kudhibiti ombaomba ndani ya sehemu au eneo lote la Halmashauri.
6. Halmashauri inaweza kumteua wakala ambaye atatekeleza jukumu la kudhibiti ombaomba kwenye sehemu au eneo lote la Halmashauri kwa niaba ya Halmashauri. Taratibu za kuwakamata ombaomba - 7 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakayekutwa mtaani au maeneo
AI-assisted research summary: People found begging in streets or open areas may be arrested, their basic details recorded, and their photo taken for identification.
7.-(1) Mtu yeyote atakayekutwa mtaani au maeneo ya wazi akiomba fedha, chakula au kitu kingine chochote atakamatwa na kuchukuliwa taarifa zake muhimu ikiwemo- (a) jina kamili; (b) jinsi na umri; (c) kijiji, wilaya na mkoa anaotoka; na (2) Ombaomba atakayekamatwa atapigwa picha kwa ajili ya kumbukumbu, na picha hiyo itatumika kwa 2 Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1007 (Linaendelea.) matumizi ya ofisi ili kurahisisha utambuzi iwapo atarudia kuwa ombaomba. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), ombaomba na inaweza Halmashauri waliokamatwa kwenye Mikoa wanayotoka kuwakabidhisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa husika. kuwarejesha Makosa - 8 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Kuna kosa kwa mtu yeyote kufanya au kusaidia vitendo vya kuombaomba vilivyoorodheshwa, au kuzuia Afisa Mwidhiniwa au Wakala kutekeleza majukumu yao.
8. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) ataomba na kupokea msaada wa fedha, chakula au kitu kingine chochote mtaani, kando ya barabara au kwenye maeneo ya wazi na mahali popote ambako siyo kituo cha hifadhi; (b) atarudi na kuendelea kuombaomba katika Halmashauri baada ya kurejeshwa katika Mkoa aliotoka; (c) atamtembeza mtu mwingine barabarani, mtaani au maeneo ya wazi kwa miguu au kwa kutumia chombo chochote kwa lengo la kuombaomba; (d) atamsafirisha kutoka eneo moja hadi jingine mtu yeyote kwa lengo la kumtumia kuombaomba mtaani; (e) atamtumikisha mtoto kwa shughuli za kuomba kwenye magari, barabarani, mtaani au mahali pengine popote; au (f) atamzuia Afisa Mwidhiniwa au Wakala kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Adhabu Kufifilisha kosa - 9 Verify source ↗
Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa lolote
AI-assisted research summary: A person convicted of any offence against these by-laws must pay a fine, face imprisonment, or both.
9. Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa lolote kinyume cha Sheria Ndogo hii, atawajibika kilipa faini ya kiasi kisichopungua shilingi laki mbili na kisichozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 10 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kutoza hadi shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalum iliyo katika Jedwali.
10. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalum kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Sheria Ndogo hii. 3 Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1007 (Linaendelea.) Kufutwa kwa Sheria Ndogo TS Na. 529 la 2019 - 11 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya
AI-assisted research summary: The 2019 Ilala municipal bylaw on begging control is repealed.
11. Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ya Mwaka 2019 inafutwa. 4 Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1007 (Linaendelea.) _______ JEDWALI _______ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 10) FOMU YA KUKIRI NA KUFILILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya ………………………………………….ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, NINAKUBALI kulipa kiasi cha shilingi …………………….. kama faini ya kufifilisha kosa. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. Jina……………………………….. ya Mwezi…………..… Mwaka ………… Saini……………………… MBELE YA MKURUGENZI: Jina: ……………………………………..……………………… Saini………………………….…………………………..……… Tarehe…………………………………………………………. 5 Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1007 (Linaendelea.) Lakiri ya Jiji la Dar es Salaam imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutao wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam uliofanyika tarehe 6/3/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- JOMAARY MRISHO SATURA, Mkurugenzi wa Jiji, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam MHE. OMARY KUMBILAMOTO, Msahiki meya, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Agosti, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 6
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in