Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
This section gives the bylaw’s official name.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the bylaw’s official name. This by-law applies in the area of the International Fish Market of Feri Magogoni, under the Dar es Salaam City Council. Sehemu hii inafafanua maneno mbalimbali yanayotumika katika Sheria Ndogo hii, kama vile Afisa Uvuvi, Bodi, dalali, Halmashauri, Mkurugenzi, Mkuu wa Soko, mvuvi, Soko, Wadau wa Soko na watumiaji wa Soko. Halmashauri must carry out several duties for the market, including handling reports, revenue, budgeting, audits, statistics, quality control, staffing, elections, and compliance. Halmashauri huteua Mkuu wa Soko, na Mkuu wa Soko lazima asimamie shughuli na mali za Soko pamoja na kutoa taarifa mbalimbali. Halmashauri pia inaweza kuteua Wakala kufanya baadhi au majukumu yote hayo.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
Showing 43 of 43
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This section gives the bylaw’s official name.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la Soko la
AI-assisted research summary: This by-law applies in the area of the International Fish Market of Feri Magogoni, under the Dar es Salaam City Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni lililopo chini ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha
AI-assisted research summary: Sehemu hii inafafanua maneno mbalimbali yanayotumika katika Sheria Ndogo hii, kama vile Afisa Uvuvi, Bodi, dalali, Halmashauri, Mkurugenzi, Mkuu wa Soko, mvuvi, Soko, Wadau wa Soko na watumiaji wa Soko.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Uvuvi” maana yake ni mtumishi wa Halmashauri mwenye taaluma ya uvuvi aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Bodi” maana yake ni Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni; “dalali” maana yake ni mtu yeyote aliyepewa mamlaka kwa mujibu wa sheria na taratibu za soko anayenadisha samaki kwa niaba ya mvuvi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; “Kamati ya Wadau wa Soko” maana yake ni Kamati ya Wadau wa Soko iliyoundwa chini ya Sheria Ndogo hii; “kanda” maana yake ni eneo mahususi lililotengwa na Halmashauri ndani ya Soko kwa ajili ya kufanya shughuli zinazowiana; 1 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam au afisa yeyote akayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “Mkuu wa Soko” maana yake ni afisa aliyeteuliwa na Halmashauri kuwa mtendaji mkuu wa Soko mwenye dhamana ya kusimamia shughuli zote za biashara na utawala za kila siku katika Soko ; “mvuvi” maana yake ni mtu yeyote anayevua samaki au dagaa katika eneo la bahari, bwawa au ziwa na kuwauza samaki au dagaa hao katika Soko lililopo ndani ya Halmashauri; “Soko” maana yake ni Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni lililopo ndani ya eneo la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ; “Wadau wa Soko” maana yake ni wavuvi, madalali, wauzaji wa samaki, wakaanga samaki na watumiaji wengine wanaotambuliwa na Sheria Ndogo hii; “watumiaji wa Soko” maana yake ni wafanyabiashara au watoa huduma waliosajiliwa na kuidhinishwa kutumia Soko au wateja wanaoingia katika Soko kwa ajili ya kupata huduma chini ya Sheria Ndogo hii au zinazotolewa na sokoni. - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must carry out several duties for the market, including handling reports, revenue, budgeting, audits, statistics, quality control, staffing, elections, and compliance.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kupokea na kujadili taarifa za kila mwezi za matumizi ya Soko; (b) kusimamia mapato na matumizi ya Soko; (c) kupokea na kuthibitisha bajeti, mpango wa manunuzi na ugavi pamoja na mpango kazi wa Soko kwa kila mwaka; (d) kufanya ukaguzi wa hesabu za fedha na rasilimali za Soko; (e) kukusanya takwimu za samaki, wavuvi pamoja na vyombo vya uvuvi; (f) kudhibiti ubora wa mazao ya uvuvi yanayoingia sokoni; (g) kuhakikisha mapato ya Soko hayashuki kwa kuweka usimamizi na udhibiti katika mifumo ya uendeshaji wa Soko; 2 Wajibu wa Halmashaur i Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) (h) kuhakikisha hakuna mtu yeyote atakayefanya ubadhirifu au kuhujumu mapato ya Soko; (i) kushauri Bodi katika utekelezaji wa majukumu yake; (j) kupokea makusanyo yote yatokanayo na vyanzo vya mapato ya Soko; (k) kurudisha asilimia sabini ya mapato ya Soko kwenye akaunti ya matumizi ya Soko kwa ajili ya uendeshaji wa Soko; (l) kuchukua hatua zinazofaa katika usimamizi wa Bodi; (m) kuhakikisha Soko uvuvi zinaendeshwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii na watumiaji wa Soko wanapata huduma bora; shughuli na za (n) kuandaa kanuni, taratibu na miongozo ya usimamizi na uendeshaji wa Soko; (o) kusimamia na kuendesha uchaguzi wa viongozi wa Soko kwa kushirikiana na Bodi; (p) kuhakikisha kuwa Soko kutosha kulingana na kusimamia utekelezaji wao wa majukumu; na lina wafanyakazi wa inayohitajika na ikama Mkuu wa Soko (q) kusimamia na kutekeleza Sheria Ndogo hii na Sheria zote zinazohusiana na uendeshaji wa Soko ikiwa ni pamoja na Sheria zinazosimamia uvuvi na mazingira. - 5 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Mkuu wa Soko atakayeteuliwa na
AI-assisted research summary: Halmashauri huteua Mkuu wa Soko, na Mkuu wa Soko lazima asimamie shughuli na mali za Soko pamoja na kutoa taarifa mbalimbali. Halmashauri pia inaweza kuteua Wakala kufanya baadhi au majukumu yote hayo.
5.-(1) Kutakuwa na Mkuu wa Soko atakayeteuliwa na Halmashauri ambaye atakuwa Mtendaji Mkuu wa Soko na Katibu wa Bodi. (2) Mkuu wa Soko atakuwa na majukumu ya- (a) kusimamia utekelezaji wa maamuzi yote yanayoamuliwa na Bodi; (b) kusimamia na kuratibu shughuli za kila siku za Soko; (c) kusimamia mali zote za Soko zikiwemo majengo, vifaa na miundombinu; (d) kusimamia ukusanyaji wa mapato yanayotokana na shughuli mbalimbali katika Soko; (e) kusimamia ulinzi na usalama wa Soko; (f) kusimamia utekelezaji wa majukumu ya watumishi katika Soko; (g) kuhakikisha Soko linakuwa safi wakati wote; 3 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) (h) kuandaa mpango na bajeti wa Soko na kuiwasilisha kwenye vikao vya Bodi kabla ya kupitishwa na Halmashauri; (i) kuidhinisha fedha kwa ajili ya matumizi ya uendeshaji wa Soko; (j) kuwasilisha kwa Halmashauri taarifa za utekelezaji wa shughuli za soko za kila robo mwaka wa fedha baada ya kupitishwa na Bodi; (k) kuwasilisha katika Bodi taarifa za mapato na matumizi ya Soko za kila mwezi; (l) kuhakikisha fedha zote za makusanyo ya Soko ya akaunti maalum katika zinawasilishwa Halmashauri; na Kamati ya Wadau wa Soko (m) kujibu hoja za ukaguzi. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri inaweza kuteua Wakala kwa ajili ya kutekeleza baadhi au majukumu yote ya Mkuu wa Soko kwa kadri itakavyoona inafaa. (4) Wakala atakayeteuliwa chini ya kanuni ndogo ya (3) atatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii na kwa mkataba wa uwakala kati yake na Halmashauri. - 6 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Kamati ya Wadau wa Soko ambayo
AI-assisted research summary: A Market Stakeholders Committee must be established, with specified members, three-year terms for the chairperson and members, and meetings every three months.
6.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Wadau wa Soko ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao- (a) Mwenyekiti wa kila kanda ya Soko; (b) Katibu wa kila kanda ya Soko; (c) wawakilishi watatu wanawake watakaochaguliwa na wenyeviti na makatibu wa kanda za Soko; na (d) mwakilishi mmoja wa wavuvi. (2) Kwa madhumuni ya kuwapata wawakilishi wanawake katika Kamati ya Wadau wa Soko, kila kanda itapendekeza jina moja la mwanamke. (3) Mwenyekiti wa Kamati ya Wadau atakuwa madarakani kwa miaka mitatu na anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine kimoja. (4) Wajumbe wa Kamati ya Wadau wa Soko watakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu na wanaweza kuchaguliwa tena kwa vipindi vingine. 4 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) (5) Kamati ya Wadau wa Soko itafanya vikao vyake kila baada ya miezi mitatu. Majukumu ya Kamati ya Wadau wa Soko - 7 Verify source ↗
Kamati ya Wadau wa Soko itakuwa na majukumu
AI-assisted research summary: Kamati ya Wadau wa Soko ina majukumu ya kushirikiana, kuunganisha wadau, kulinda maslahi yao, kusimamia shughuli na usafi wa soko, na kutekeleza maelekezo ya Halmashauri.
7. Kamati ya Wadau wa Soko itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kushirikiana na Halmashauri kuleta maendeleo kwa Wadau wa Soko kulingana na sera na mipango iliyopo; katika (b) kuunganisha wadau wote waliopo sokoni bila kujali tofauti zao za kisiasa, kabila, dini au vikundi walivyonavyo sokoni; (c) kutetetea na kulinda maslahi na haki za wadau kwa kutumia njia na mwenendo sahihi unaokubalika kisheria; (d) kupokea na kujadili taarifa za kamati tendaji ya Kamati ya Wadau wa Soko kabla ya kuwasilishwa kwenye Bodi; (e) kuhakiki biashara na utendaji wa kanda za Soko; (f) kuboresha ustawi wa wadau wa Soko; (g) kuhakikisha nidhamu katika shughuli za Soko; (h) kuinua ubora wa mfumo wa biashara katika Soko; (i) kusimamia usafi katika maeneo ya Soko; (j) kudhibiti na kufichua upotevu wa mapato ya Soko na kuhakikisha mapato yanaongezeka kwa kushirikiana na Mkuu wa Soko; (k) kuhamasisha watumiaji wa Soko kutekeleza wajibu wa ulipaji ada ya leseni na tozo mbalimbali; (l) kupokea na kutekeleza maagizo au maelekezo kutoka Halmashauri; na (m) kusimamia na kutoa miongozo katika vyama na vikundi vyote vilivyopo sokoni vinavyotambuliwa na uongozi wa Soko. Kamati Tendaji ya Wadau wa Soko - 8 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Kamati Tendaji ya Wadau wa Soko
AI-assisted research summary: The Market Stakeholders Executive Committee is made up of specified officers and must meet every month.
8.-(1) Kutakuwa na Kamati Tendaji ya Wadau wa Soko itakayokuwa na wajumbe wafuatao: (a) Mwenyekiti wa Kamati ya Wadau wa Soko; (b) Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Wadau wa Soko; (c) Katibu wa Kamati ya Wadau wa Soko; 5 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) (d) Katibu Msaidizi wa Kamati ya Wadau wa Soko; na (e ) Mweka Hazina wa Kamati ya Wadau wa Soko. (2) Wajumbe waliobainishwa katika kanuni ndogo ya (1) watakuwa ndio viongozi wa Kamati ya Wadau wa Soko. (3) Kamati Tendaji ya Soko itafanya vikao vyake kila mwezi. Majukumu ya Kamati Tendaji - 9 Verify source ↗
Kamati Tendaji ya Wadau wa Soko itakuwa na
AI-assisted research summary: The Executive Committee of Market Stakeholders must organize and coordinate market-related meetings, handle reports, manage committee tasks and instructions, keep records, and carry out duties as directed by the committee.
9. Kamati Tendaji ya Wadau wa Soko itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuandaa na kuratibu vikao vyote vinavyohusu Wadau wa Soko; (b) kupokea na kuandaa taarifa zinazotakiwa kwenda ndani na nje ya Soko na kuzifanyia kazi; (c) kusimamia na kutekeleza majukumu yote yanayotokana na vikao vya Kamati ya Wadau wa Soko na maagizo yake; (d) kutunza nyaraka zote zinazotoka na kuingia katika Kamati ya Wadau wa Soko; na (e) kutekeleza majukumu ya Kamati ya Wadau wa Soko kwa kadri itakavyoelekezwa na Kamati hiyo. Kamati Ndogo Kamati ndogo ya Mipango, Uchumi na Miundombi nu - 10 Verify source ↗
Kamati ya Wadau wa Soko itaunda Kamati Ndogo
AI-assisted research summary: Kamati ya Wadau wa Soko lazima iunde kamati ndogo tatu zilizoainishwa.
10. Kamati ya Wadau wa Soko itaunda Kamati Ndogo zifuatazo ambazo zitakuwa na wajumbe wanne kutoka katika Kamati ya Wadau wa Soko na Kamati hizo zitawajibika kwa Kamati ya Wadau wa Soko : (a) Kamati Ndogo ya Mipango, Uchumi na Miundombinu; (b) Kamati Ndogo ya Biashara na Utawala; na (c) Kamati Ndogo ya Afya, Usafi, Ulinzi na Mazingira. - 11 Verify source ↗
Kamati Ndogo ya Mipango, Uchumi na
AI-assisted research summary: Kamati Ndogo ya Mipango, Uchumi na Miundombinu lazima itekeleze majukumu yaliyoorodheshwa katika kifungu hiki.
11. Kamati Ndogo ya Mipango, Uchumi na Miundombinu itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kufanyia kazi na kutekeleza maagizo yote ya Kamati Tendaji ya Wadau wa Soko, Kamati ya Wadau wa Soko na Bodi kuhusiana na mipango, uchumi na miundombinu ya Soko; (b) kuimarisha ustawi na ufanisi wa wadau wote wa soko; (c) kutoa mapendekezo ya kuimarisha na kuongeza vyanzo vya mapato; na (d) kutekeleza majukumu yoyote itakayopangiwa na Kamati ya Wadau wa Soko. 6 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) Kamati Ndogo ya Biashara na Utawala - 12 Verify source ↗
Kamati Ndogo ya Biashara na Utawala itakuwa na
AI-assisted research summary: Kamati Ndogo ya Biashara na Utawala lazima itekeleze maagizo na majukumu yaliyokabidhiwa na kamati na bodi husika, kusaidia utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Wadau wa Soko, kushirikiana katika kufuatilia madeni ya wafanyabiashara, kushughulikia migogoro, na kutekeleza kazi nyingine itakazopangiwa.
12. Kamati Ndogo ya Biashara na Utawala itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kufanyia kazi na kutekeleza maagizo ya Kamati Tendaji ya Wadau wa Soko, Kamati ya Wadau wa Soko na Bodi kuhusiana na biashara na utawala; (b) kusaidia utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Wadau wa Soko kwa kadri yatakavyotolewa maelekezo na Kamati ya Wadau wa Soko; (c) kushirikiana na Bodi, Menejimenti na Kamati ya Wadau wa Soko katika kufuatilia madeni ya wafanyabiashara wote; (d) kushughulikia migogoro Wadau wa Soko; na itakayojitokeza baina ya (e) kutekeleza majukumu yoyote itakayopangiwa na Kamati ya Wadau wa Soko. Kamati Ndogo ya Afya, Usafi, Ulinzi na Mazingira. - 13 Verify source ↗
Kamati Ndogo ya Afya, Usafi, Ulinzi na Mazingira
AI-assisted research summary: The subcommittee must carry out assigned instructions, enforce market rules, improve security and cleanliness, educate market users, and do any other tasks assigned to it.
13. Kamati Ndogo ya Afya, Usafi, Ulinzi na Mazingira itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kufanyia kazi na kutekeleza maagizo ya Kamati Tendaji ya Wadau wa Soko, Kamati ya Wadau wa Soko na Bodi; (b) kuhakikisha sheria na taratibu ziliweka katika Soko zinazingatiwa; (c) kuimarisha ulinzi na usalama wa soko; (d) kuhakikisha soko linakuwa katika hali ya usafi; (e) kuwaelimisha wadau wa Soko na watumiaji wengine kuhusu ulinzi, usafi, afya na manzingira; na (f) kutekeleza majukumu yoyote itakayopangiwa na Kamati ya Wadau wa Soko. Kanda za Soko - 14 Verify source ↗
(1) Kwa madhumuni ya uendeshaji bora wa Soko,
AI-assisted research summary: This provision divides the market into eight zones and states what each zone is for.
14.-(1) Kwa madhumuni ya uendeshaji bora wa Soko, kutakuwa na kanda nane za Soko kama ifuatavyo: (a) kanda namba 1 itakayokuwa na- (i) Sehemu A ambayo ni ukumbi wa mnada, vyumba vya kuhifadhia barafu, samaki, vyumba vya ofisi na ukumbi wa mikutano; (ii) Sehemu B ambayo ni kwa ajili ya wamiliki wa vyombo vya uvuvi; 7 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) (b) kanda namba 2 ambayo ni eneo kwa ajili ya maandalizi ya samaki kutolewa utumbo, magamba na kuoshwa pamoja na vioski; (c) kanda namba 3 ambayo ni eneo kwa ajili ya kuuzia samaki wabichi wa rejareja; (d) kanda namba 4 ambayo ni eneo kwa ajili ya huduma ya chakula, baba na mama lishe na maduka ya rejareja; (e) kanda namba 5 ambayo ni eneo kwa ajili ya kuuzia mbogamboga, nyingine matunda, zinazoruhusiwa, maegesho ya magari na huduma za fedha kwa mitandao ya simu; bidhaa (f) kanda namba 6 ambayo ni eneo kwa ajili ya kukaangia samaki; (g) kanda namba 7 ambayo ni eneo kwa ajili ya maduka na biashara mchanganyiko; na (h) kanda namba 8 itakayokuwa na- (i) Sehemu A ambayo ni eneo kwa ajili ya shughuli za uvuvi, wavuvi na shughuli za ziada za maduka ya vifaa vya uvuvi, baba na mama lishe, utengenezaji wa mashine za vyombo vya baharini, utengenezaji na uundaji wa maboti, ngalawa na mitumbwi, maboksi ya kubebea samaki na barafu ; na (ii) Sehemu B ambayo ni eneo kwa ajili ya shughuli za kuhifadhi samaki kwa barafu na ushushaji wa samaki. Uongozi wa Kanda - 15 Verify source ↗
(1) Kila Kanda itakuwa na viongozi wafuatao
AI-assisted research summary: Each Kanda must have specified leaders, those leaders are elected by registered members of the relevant market’s stakeholder list, and they serve for three years with one possible re-election.
15.-(1) Kila Kanda itakuwa na viongozi wafuatao: (a) mwenyekiti wa Kanda; (b) makamu Mwenyekiti wa Kanda; (c) katibu wa Kanda; (d) katibu Msaidizi wa Kanda; (e) mweka Hazina wa Kanda; na (f) wajumbe wanne wa Kanda. (2) Viongozi wa kanda watachaguliwa na wajumbe waliosajiliwa katika orodha ya wadau wa Soko wa kanda husika. (3) Viongozi wa kanda watashika madaraka kwa muda wa miaka mitatu na wanaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine kimoja. 8 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) Mkutano Mkuu wa kanda za Soko - 16 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Mkutano wa kanda za Soko ambao
AI-assisted research summary: Mkutano Mkuu wa kanda za Soko lazima ufanyike kila baada ya miezi sita.
16.-(1) Kutakuwa na Mkutano wa kanda za Soko ambao wajumbe wake watakuwa ni viongozi wa kila kanda waliochaguliwa chini ya kanuni ya 15. (2) Mkutano Mkuu wa kanda za Soko utajadili yafuatayo: (a) taarifa za utendaji kazi za Kamati Tendaji ya Wadau wa Soko, Kamati ya Wadau wa Soko na Kamati Ndogo zilizoundwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) taarifa mbalimbali zinazohusu Soko; (c) maendeleo ya wafanyabiashara wote walio kwenye kanda za Soko; (d) taarifa zote zinazowasilishwa kutoka katika kila kanda; (e) uboreshaji wa ustawi wa wadau wa Soko; (f) kuinua ubora wa mfumo wa biashara katika Soko; (g) kupokea na kujadilili taarifa za maendeleo ya Soko; na (h) kujadili masuala yanayohusu miundombinu na mazingira ya Soko. (3) Mkutano Mkuu wa kanda za Soko utafanyika kila baada ya miezi sita. - 17 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa wadau wa Soko
AI-assisted research summary: There must be a General Meeting of market stakeholders, made up of the listed members, and it must meet once a year.
17.-(1) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa wadau wa Soko ambao wajumbe wake watakuwa ni: (a) wajumbe wa Kamati ya Wadau wa Soko; (b) viongozi wote wa kanda za Soko; (c) wawakilishi wanne wa wavuvi; (d) mwenyekiti na Katibu wa vyama vyote vilivyoko sokoni vinavyotambulika na Mkuu wa Soko na Kamati ya Wadau wa Soko; (e) waalikwa wote kutoka ndani na nje ya Soko; (f) wawakilishi wa Serikali Kuu au Halmashauri au wote kwa pamoja; na (g) wajumbe wa Bodi. (2) Mkutano Mkuu wa wadau wa Soko utakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kupokea na kutoa ushauri kuhusu taarifa mbalimbali za uendeshaji wa Soko; 9 Mkutano Mkuu wa wadau wa Soko Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) Usajili wa wadau wa Soko (b) kuwasilisha mapendekezo ya maboresho ya uendeshaji wa Soko na utoaji wa huduma kwa Kamati ya Wadau na Menejimenti ya Soko, Bodi, Halmashauri na Serikali Kuu; (c) kupokea taarifa za miundombinu ya soko na kuwasilisha mapendekezo ya Wadau; na (d) kuishauri Kamati ya Wadau wa Soko na na Halmashauri namna bora ya kuimarisha na kudhibiti mapato ya Soko. (3) Mkutano Mkuu wa wadau wa Soko utafanyika mara moja kwa mwaka. - 18 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayekusudia kufanya biashara
AI-assisted research summary: Watu wanaotaka kufanya biashara katika eneo la soko lazima wasajiliwe, wapate kibali, walipe ada, na wafanye usajili wa eneo husika.
18.-(1) Mtu yeyote anayekusudia kufanya biashara katika eneo la soko atatakiwa kusajiliwa na Mkuu wa Soko akishirikiana na Kamati ya Wadau wa Soko kwa lengo la kumtambua na kumworodhesha katika rejesta ya Wadau wa Soko. (2) Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ndogo ya (1), kila mdau wa Soko atakayesajiliwa atapewa kibali cha kufanya biashara katika Soko kutoka kwa Mkuu wa Soko kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (3) Kibali kitatatolewa kwa mdau wa Soko baada ya- (a) kuthibitisha kumiliki leseni au kibali kinachohusiana na shughuli anazotaka kufanya katika eneo la Soko kilichotolewa na Halmashauri au mamlaka nyingine kwa mujibu wa Sheria; na (b) kulipa ada. (4) Kibali kitakachotolewa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (3) kitadumu kwa muda wa miaka mitatu tangu siku ya kutolewa na endapo mdau wa Soko atataka kuendelea na biashara katika Soko atatakiwa kuomba kibali kingine kwa Mkuu wa Soko. (5) Ada ya kibali itakuwa ni shilingi elfu thelathini. (6) Mdau wa Soko aliyepata kibali kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (3) atatakiwa kujisajili katika kanda ya Soko inayohusika na shughuli anazofanya. Kufuta kibali - 19 Verify source ↗
(1) Mkuu wa Soko, baada ya kushauriana na Kamati
AI-assisted research summary: Mkuu wa Soko anaweza kufuta kibali baada ya kushauriana na Kamati Tendaji na kutoa notisi ya siku 30 ikiwa masharti yaliyotajwa yatatokea; mwenye kibali anaweza kupinga ndani ya siku 14, na Mkurugenzi lazima aamue ndani ya siku 7.
19.-(1) Mkuu wa Soko, baada ya kushauriana na Kamati Tendaji ya Wadau wa Soko, anaweza kufuta kibali 10 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hii, baada ya kutoa notisi ya siku thelathini, endapo mwenye kibali hicho- (a) atakuwa na malimbikizo ya madeni ya kodi au tozo nyingine yoyote kwa muda wa miezi mitatu bila sababu za msingi; (b) atakuwa amesimamisha shughuli zake kwa muda wa miezi mitatu mfululizo bila taarifa ya maandishi kwa Mkuu wa Soko na Kamati ya Wadau wa Soko; (c) ataendelea kukiuka Sheria ndogo hii au sheria (d) atawashawishi nyingine hata baada ya kupewa onyo; wafanyabiashara wengine kutozingatia Sheria Ndogo hii au kusababisha uvunjaji wa amani; (e) atatumia chumba, kibanda, meza au kizimba alichopanga kinyume na madhumuni ya kufanyia biashara kama yalivyoainishwa kwenye mkataba wa upangishaji au maelekezo yatakayotolewa na Halmashauri; (f) ataharibu miundombinu ya Soko kwa makusudi na kushindwa kugharamia ukarabati wake; au (g) atahamisha umiliki wa kibali chake kwa mtu mwingine bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa Mkuu wa Soko. (2) Mdau wa Soko ambaye hataridhika na uamuzi wa kufutiwa kibali anaweza kuwasilisha pingamizi lake kwa Mkurugenzi katika kipindi cha siku kumi na nne tangu tarehe ya kufutwa kibali. (3) Baada ya kupokea pingamizi, Mkurugenzi atatakiwa kutoa uamuzi wa pingamizi ndani ya siku saba tangu tarehe ya kupokea pingamizi husika. - 20 Verify source ↗
(1) Kila mdau wa Soko atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila mdau wa Soko lazima asajiliwe, afuate masharti ya usafi na matumizi ya eneo la soko, alipe ushuru na ada kwa wakati, na asiweze kufanya au kuweka vitu vilivyokatazwa ndani ya soko.
20.-(1) Kila mdau wa Soko atakuwa na wajibu wa- (a) kusajiliwa na Mkuu wa Soko katika rejesta ya Wadau wa Soko; (b) kusajiliwa katika orodha ya Wadau wa Soko ya kanda anayofanyia shughuli zake; (c) kulinda na kuhifadhi miundombimu ya Soko; (d) kufanya biashara katika maeneo yanayoruhusiwa; (e) kufanya usafi katika eneo lake la biashara; (f) kulipa ushuru na ada kwa wakati; 11 Wajibu wa mdau wa Soko Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) (g) kutobandika au kutobandua tangazo bila idhini ya Mkuu wa Soko; (h) kutotumia lugha ya matusi, kuudhi au kashfa katika eneo la Soko; (i) kutoweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la Soko; (j) kutotupa taka ovyo au kutiririsha maji machafu; (k) kushiriki usafi wa jumla wa Soko; (l) kutofanya shughuli za kisiasa katika eneo la Soko; (m) kutowasha moto maeneo yasiyohusika ndani ya Soko; na (n) kuheshimu masharti ya upangaji na maelekezo atakayopewa na Halmashauri, Mkuu wa Soko na Kamati ya Wadau wa Soko. (2) Mdau wa Soko atakayekiuka masharti ya kanuni ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. - 21 Verify source ↗
(1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa kumi
AI-assisted research summary: The market must stay open every day from 12:00 a.m. to 12:00 p.m., and special after-hours entry or exit needs special permission and approval.
21.-(1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), wadau wa Soko wanaweza kuruhusiwa kuingia au kutoka sokoni kabla au baada ya muda wa kazi iwapo kutakuwa na sababu maalumu ya kufanya hivyo na baada ya kupata ruhusa maalumu kutoka kwa Kamati ya Wadau wa Soko na kuidhinishwa na Mkuu wa Soko. (3) Mkuu wa Soko kwa kushauriana na Mkurugenzi, anaweza kufunga Soko kwa ajili ya matengenezo au sababu nyingine yoyote ya dharura pale itakapoonekana inafaa. (4) Isipokuwa kwa sababu nyingine za dharura, Mkuu wa Soko hatakuwa na mamlaka ya kufunga soko kwa sababu za matengenezo isipokuwa baada ya kutoa notisi ya siku saba kwa wadau wa soko kuhusu kusudio la kufunga soko kwa ajili ya matengenezo. (5) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kanuni ndogo ya (2) atakuwa ametenda kosa. Muda wa kazi Usafi wa soko - 22 Verify source ↗
(1) Kila mdau wa Soko anayefanya biashara katika
AI-assisted research summary: Market participants must keep their area clean, join the monthly general cleaning, follow health rules, and violations are an offence.
22.-(1) Kila mdau wa Soko anayefanya biashara katika eneo la Soko atawajibika kuweka eneo lake katika hali ya usafi wakati wote na kushiriki usafi wa jumla wa kila mwisho wa mwezi. 12 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) (2) Mkuu wa Soko kwa kushirikiana na Kamati ya Wadau wa Soko atasimamia usafi wa jumla wa Soko kila siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi. (3) Kila mdau wa Soko anayefanya shughuli zake katika eneo la Soko atatakiwa kuzingatia kanuni za afya ikiwa ni pamoja na: (a) kupima afya; (b) kuvaa sare; (c) kuweka mazingira safi ; na (d) kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kila wanapotoka chooni. (4) Mdau wa Soko atakayekiuka masharti ya kanuni ndogo ya (1) au (3) atakuwa ametenda kosa. - 23 Verify source ↗
(1) Vyombo vitakavyoruhusiwa kubebea samaki
AI-assisted research summary: For carrying fish for the market, only a bucket or any container in the covered area is allowed. Anyone who violates that rule commits an offence.
23.-(1) Vyombo vitakavyoruhusiwa kubebea samaki la Soko ni ndoo au chombo chochote katika eneo kilichofunikwa. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kanuni ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. - 24 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabiashara atakayeuza mazao ya bahari
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wanaouza mazao ya bahari kwenye mnada lazima walipe ushuru wa asilimia 3 ya mauzo yote; wanaouza sehemu nyingine ya soko hulipa ushuru kwa viwango vya Jedwali la Pili kulingana na kilo za bidhaa zinazoingia sokoni.
24.-(1) Kila mfanyabiashara atakayeuza mazao ya bahari sehemu ya mnada atatakiwa kulipa ushuru wa asilimia tatu ya mauzo yote. (2) Kila mfanyabiashara atakayeuza mazao ya bahari sehemu nyingine yoyote ya Soko atalipa ushuru kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii kulingana na kilo zitakazopatikana kwa mazao yatakayoingizwa sokoni. Ubebaji wa samaki Ushuru wa mazao ya bahari Ada za pango kwa maeneo ndani ya soko na ukodishaji wa vifaa
Part
sehemu nyingine yoyote ya Soko atalipa ushuru kwa viwango
- 25 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakayetumia sehemu ya Soko
AI-assisted research summary: People using market space for business or fish storage must pay a fee to the Council. People renting Council equipment in the market area must also pay a fee to the Council.
25.-(1) Mtu yeyote atakayetumia sehemu ya Soko kufanya shughuli za kibiashara au kuhifadhia samaki atalipa ada kwa Halmashauri kwa viwango vilivyoainishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. (2) Mtu yeyote atakayekodisha vifaa vya Halmashauri vilivyoko ndani ya eneo la Soko atalipa ada kwa Halmashauri kwa viwango vilivyoainishwa kwenye Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii. Ada za leseni
Part
Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii.
- 26 Verify source ↗
Mwombaji yeyote wa leseni atatakiwa kulipa ada ya
AI-assisted research summary: A license applicant must pay the license fee according to the existing law and procedures.
26. Mwombaji yeyote wa leseni atatakiwa kulipa ada ya leseni kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo. 13 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) Muda wa leseni Ushuru wa maegesho - 27 Verify source ↗
Muda wa leseni yeyote itakayotolewa chini ya Sheria
AI-assisted research summary: Most licenses issued under this provision are valid from 1 July to 30 June of the next year, no matter when they are issued; fishing licenses use 1 January to 31 December instead.
27. Muda wa leseni yeyote itakayotolewa chini ya Sheria Ndogo hii itakuwa ni mwaka mmoja kuanzia tarehe 1 Julai ya kila mwaka hadi tarehe 30 Juni ya mwaka unaofuata bila kujali tarehe ya kutolewa kwa leseni isipokuwa leseni za uvuvi ambayo zitatolewa kuanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 31 Disemba ya kila mwaka. - 28 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na ushuru wa maegesho wa shilingi
AI-assisted research summary: A parking fee of TZS 1,000 per hour must be paid at the gate for any car entering the market area, and no one may park a car there without permission from the Market Master.
28.-(1) Kutakuwa na ushuru wa maegesho wa shilingi elfu moja kwa saa utakaolipwa getini kwa gari lolote litakaloingia ndani ya eneo la Soko (2) Mtu yeyote hataruhusiwa kulaza gari katika eneo la Soko bila ya idhini ya Mkuu wa Soko. (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kanuni ndogo ya (2) atakuwa ametenda kosa. Kanuni na miongozo ya uendeshaji wa shughuli za Soko - 29 Verify source ↗
Uongozi wa Soko, kwa kushirikiana na kamati ya
AI-assisted research summary: Uongozi wa Soko unaweza kutengeneza kanuni na miongozo kuhusu uendeshaji wa soko na wa kamati zake, lakini itaanza kutumika baada ya kuidhinishwa na Halmashauri.
29.Uongozi wa Soko, kwa kushirikiana na kamati ya wadau wa soko, utakuwa na uwezo wa kutengeneza kanuni na miongozo ya- (a) uendeshaji wa shughuli za soko; na (b) uendeshaji wa kamati, kamati ndogo na uongozi wa wafanyabiashara, ambayo itatumika baada ya kuidhinishwa na Halmashauri. Kushindwa kulipa tozo Makosa - 30 Verify source ↗
Bila kuathiri masharti ya Sheria Ndogo hii kuhusu
AI-assisted research summary: A person who does not pay a licence fee, tax, or levy on time must pay the amount due plus a 50% charge.
30. Bila kuathiri masharti ya Sheria Ndogo hii kuhusu ulipaji wa ada, ushuru na tozo, mtu yeyote atakayeshindwa kulipa ada ya leseni, ushuru au tozo yoyote katika muda uliopangwa chini ya Sheria Ndogo hii, atalipa ada au ushuru au tozo hiyo pamoja na tozo ya asilimia hamsini ya ada au ushuru au tozo anayotakiwa kulipa. - 31 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Ni kosa kwa mtu yeyote kufanya vitendo vilivyoorodheshwa katika soko, ikiwemo kuuza au kunywa pombe, kuuza au kuvuta sigara, kukwepa ushuru, kuingia na kufanya biashara bila usajili au kibali, na kuuza au kuhamisha mali ya Halmashauri bila idhini.
31. Itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote- (a) kuuza au kunywa pombe katika eneo la Soko; (b) kuuza au kuvuta sigara; (c) kukwepa kulipa ushuru au kutoa taarifa za uongo kwa lengo la kukwepa ushuru; (d) kuingia sokoni na kufanya biashara yoyote bila ya kusajiliwa au kuwa na kibali; 14 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) (e) kuuza, kuhawilisha, kurithisha au kupangisha kizimba au mali yoyote ya Halmashauri bila idhini ya Halmashauri; (f) kufanya kwenye shughuli hairuhusiwi kwa shughuli hiyo; kanda ambayo (g) kuuza samaki na mazao mengine ya bahari nje ya eneo la mnada; (h) kuchukua samaki za wateja mara baada ya kushinda dau la kununua samaki katika eneo la mnada; au (i) kufanya kitendo chochote kitakacholeta bughudha au kero kwa wateja au wageni wanaoingia sokoni kwa lengo la kupata huduma za soko. Adhabu Kufifilisha kosa - 32 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa
AI-assisted research summary: Mtu akipatikana na hatia kwa kosa kinyume cha Sheria Ndogo hii, anaweza kupewa faini, kifungo cha miezi 12 hadi 24, au vyote.
32. Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa lolote kinyume cha Sheria Ndogo hii, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 33 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kutoza mtu aliyekosa hadi shilingi laki mbili, ikiwa mkosaji anakiri kwa hiari, anajaza fomu maalumu, na analipa ada au ushuru anaodaiwa.
33. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Nne la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. Kufutwa kwa TS Na. 603 la 2019 - 34 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya Ushuru na Uendeshaji wa Soko la
AI-assisted research summary: This section repeals a named by-law on fish market management and fees.
34. Sheria Ndogo ya Ushuru na Uendeshaji wa Soko la Samaki Feri Magogoni ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ya Mwaka 2019 inafutwa. 15 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) PICHA _______________ JEDWALI LA KWANZA ______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 18(2)) KIBALI CHA KUTUMIA SOKO Jina la Mwombaji:……………………………………………………...
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 2 Verify source ↗
Anuani ya mwombaji:………………………………………………
AI-assisted research summary: The form asks for the applicant’s address.
2. Anuani ya mwombaji:……………………………………………… - 3 Verify source ↗
Namba ya Simu ya Mwombaji
AI-assisted research summary: Section label for the applicant’s phone number.
3. Namba ya Simu ya Mwombaji:............................................................ - 5 Verify source ↗
Kanda ambayo kibali hicho kinatumika:………………………………
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaonyesha kanda au eneo ambalo kibali hicho kinatumika.
5. Kanda ambayo kibali hicho kinatumika:……………………………… - 6 Verify source ↗
Muda wa kibali ni kuanzia tarehe:…………………hadi tarehe:………
AI-assisted research summary: This section sets the permit period from a start date to an end date.
6. Muda wa kibali ni kuanzia tarehe:…………………hadi tarehe:……… - 7 Verify source ↗
Masharti ya kutumia kibali hicho
AI-assisted research summary: This section lists conditions for using the permit, but the specific conditions are left blank in the source text.
7. Masharti ya kutumia kibali hicho: a) ……………………………………………………………………… b) ……………………………………………………………………… c) ……………………………………………………………………… d) ……………………………………………………………………… e) ……………………………………………………………………… - 8 Verify source ↗
Tarehe ya kikao iliyoidhinisha kibali:………………………………………
AI-assisted research summary: This section is a label for the date of the meeting that approved the permit.
8. Tarehe ya kikao iliyoidhinisha kibali:………………………………………. - 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: This text shows the heading for a second schedule listing fees and charges for fish market services.
9. Muhtasari Namba:……………………. Imesainiwa na: Jina:………………………………. Saini:……………………………… Tarehe ……………………………. Mkuu wa Soko Mhuri :…………………………….. Jina:...................................... Saini:……………………… Tarehe:…………………..… Mwombaji 16 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA PILI ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 24(2) na 25(1)) VIWANGO VYA ADA NA USHURU Namba Aina ya Huduma
Part
JEDWALI LA PILI
- 23 Verify source ↗
Section 23
AI-assisted research summary: This provision lists monthly and other service fees for different market stalls, businesses, and facilities.
23. 24 25 26 27 28 29 Dalali Mchuuzi wa samaki Mpaaji wa nje au ndani au muoshaji samaki Mkaanga samaki Matunda na mbogamboga Mgahawa mdogo Mgahawa mkubwa Muuza mkaa Sehemu ya kuhifadhi samaki Ofisi ya ushirika Huduma ya choo (i) (ii) (iii) Kuoga- 500/= Haja ndogo-200/= Haja kubwa -200/= Chumba cha kuhifadhia barafu Kontena la kuhifadhi samaki lenye urefu wa futi 40 Kontena la kuhifadhi samaki futi lenya urefu wa futi 20 Kizimba Kioski Eneo la kutengenezea Maboksi ya kuhifadhi samaki Saluni Ofisi ya nje ya jengo la Utawala Ofisi ya ndani ya jengo la Utawala Kasha au tenga la kubebea samaki zinazoletwa kwa njia ya usafiri wa barabara Tenga kubwa la kubebea samaki zinazoletwa kwa njia ya usafiri wa barabara Kasha dogo la kubebea samaki zinazoletwa kwa njia ya usafiri wa barabara Duka la kuhifadhi samaki Meza ya kuuzia samaki waliogandishwa na Samaki wabichi Karakana Duka la kuuza vifaa vya uvuvi Eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kupika chakula Ada ya kuhifadhia mitungi ya gesi ya kupikia 17 Kiwango cha Ada au ushuru kwa mwezi (Shilingi) 30,000/= 10,000/= 10,000/= 10,000/= 8,000/= 10,000/= 70,000/= 30,000/= 10,000/= 100,000/= kulingana mkataba na 100,000/= 120,000/= 80,000/= 10,000/= 30,000/= 100,000/= 80,000/= 50,000/= 100,000/= Asilimia tatu (3%) ya bei ya soko kwa siku husika Asilimia tatu (3%) ya thamani kilo zilizomo kwenye tenga Asilimia tatu (3%) ya thamani kilo zilizomo kwenye kasha hilo 80,000/= 15,000/= 200,000/= 100,000/= 100,000/= 20,000/= ya ya Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) 30 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44 Duka la kuuza gesi Ushuru wa biashara ya huduma za fedha mtandao Muuzaji wa barafu Eneo la wakausha dagaa au wauza dagaa Stoo ya kuhifadhia vifaa vya uvuvi Pikipiki au bajaji Baiskeli Mng’arisha viatu Muuza maboksi Muuza mitumba Dobi Mbebaji au muoshaji au mtembezaji wa toto kapu au vyanzo vingine visivyotajwa Gari la mizigo lenye uwezo wa kubeba tani tatu na kuendelea Ushuru wa kushusha na kupakia mizigo Maegesho ya magari vyanzo vingine kulingana na makubaliano ya mkataba 80,000/= 50,000/= 15,000/= 40,000= 50,000/= 500/= kwa siku 200/= kwa siku 10,000/= 10,000 30,000/= 35,000/= 15,000/= kwa mwezi 500/= kwa siku 1000/= kwa tripu 5000/= kwa tani 1 500/= kwa saa kwa mkataba ____________ JEDWALI LA TATU ____________ (Limetengezwa chini ya Kanuni ya 25(2)) ADA YA KUKODISHA VIFAA VYA HALMASHAURI Na. Aina ya kifaa
Part
JEDWALI LA TATU
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Section 4 lists monthly fees for different fish-transport and fish-storage items, and the page also includes a form for admitting an offence and agreeing to pay the amount owed plus a compounding fine.
4. Mkokoteni wa kubeba samaki Kontena la kubeba samaki Boksi maalumu la kuhifadhia samaki (dogo). Boksi maalumu la kuhifadhia samaki (kubwa). Kiwango cha Ada kwa mwezi (Shilingi) 30,000/= 30,000/= 10,000/= 20,000/= 18 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) _____________ JEDWALI LA NNE _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni cha 33) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ………...………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………..……. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kwamba mnamo tarehe ......… ya mwezi .......….…. Mwaka ....…….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Kanuni cha…......... cha Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, NAKUBALI kulipa kiasi cha shilingi ……………….. ya ada au ushuru ninaodaiwa pamoja na faini ya kufifilisha kosa ya kiasi cha shilingi …………………. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe:…........... ya Mwezi:.……… Mwaka………….. Jina:…………………………………..………………...……. Saini:…………………………..…………………...………… MBELE YA MKURUGENZI: Jina:…………………………….………..…………………… Saini:……………………………………………………… Tarehe:………………………………………………………. 19 Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1010 (Linaendelea.) Lakiri ya Jiji la Dar es Salaam imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutao wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam uliofanyika tarehe 6/3/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- JOMAARY MRISHO SATURA, Mkurugenzi wa Jiji, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam MHE. OMARY KUMBILAMOTO, Msahiki meya, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Agosti, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 20
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in