Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
This provision gives the by-law its name: the Kilwa District Council Construction Minerals Management By-law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the by-law its name: the Kilwa District Council Construction Minerals Management By-law, 2024. This by-law applies within the area of Kilwa District Council. This section defines key terms used in the by-law, including fees, permits, officers, the Council, construction minerals, the Director, miners, tax/charges, and agents. A person planning to start a building-minerals mine in the council area must apply in writing to the Director for a permit, attach the listed documents, and the Director must inspect the site within seven days before deciding. Mtu aliyepewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi lazima alipe ada ya kila mwaka, azingatie masharti ya sheria ndogo na ya kibali, achimbe bila kuharibu kingo za korongo kwa njia inayosababisha mmomonyoko au madhara ya mazingira, na alipe ushuru na tozo za Halmashauri.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Showing 15 of 15
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This provision gives the by-law its name: the Kilwa District Council Construction Minerals Management By-law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la
AI-assisted research summary: This by-law applies within the area of Kilwa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including fees, permits, officers, the Council, construction minerals, the Director, miners, tax/charges, and agents.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “ada” maana yake ni malipo yanayolipwa Halmashauri kwa ajili ya vibali au leseni mbalimbali kuhusiana na madini ya ujenzi; “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa. “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi inayotolewa na Halmashauri; “madini ya ujenzi” maana yake ni tarazo, moramu, udongo, kifusi, kokoto, mawe, mchanga, chokaa na madini mengine yanayotumika katika ujenzi; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa au afisa aliyeteuliwa ya Mkurugenzi; majukumu kutekeleza 1 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na 1012(Linaendelea.) Maombi ya kibali “mchimba madini” maana yake ni mtu mwenye leseni ya kuchimba madini ya ujenzi; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa shughuli au huduma mbalimbali zinazotolewa katika eneo la Halmashauri; na “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, kampuni au taasisi iliyoingia mkataba kutekeleza jukumu lolote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. - 4 Verify source ↗
(1) Mtu anayekusudia kuanzisha machimbo ya
AI-assisted research summary: A person planning to start a building-minerals mine in the council area must apply in writing to the Director for a permit, attach the listed documents, and the Director must inspect the site within seven days before deciding.
4.-(1) Mtu anayekusudia kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuwasilisha kwa Mkurugenzi maombi ya kibali cha kuchimba madini ya ujenzi kwa mandishi kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (2) Maombi ya kibali yataambatishwa na taarifa zifuatazo: (a) leseni ya uchimbaji wa madini iliyotolewa na mamlaka husika; (b) aina ya madini yanayokusudiwa kuchimbwa; (c) mkataba au uthibitisho wa umiliki pamoja na ukubwa wa eneo linalokusudiwa kuchimbwa madini ya ujenzi; (d) mpango wa utunzaji wa mazingira katika eneo la machimbo; na (e) muhtasari wa Mkutano Mkuu wa Kijiji ambacho uchimbaji wa madini ya ujenzi utafanyika na uchimbaji huo. kukubaliana ukionesha (3) Baada ya kupokea maombi na kabla ya kutoa kibali, Mkurugenzi ndani ya muda wa siku saba atakagua eneo ambalo uchimbaji wa madini ya ujenzi unakusudiwa kufanyika ili kujiridhisha iwapo eneo hilo linafaa kwa shughuli za uchimbaji. (4) Endapo Mkurugenzi ataridhika kwamba eneo linaloombewa kibali linafaa kwa shughuli za uchimbaji atatoa kibali, na iwapo ataona kuwa eneo hilo halifai kwa shughuli za uchimbaji wa madini atakataa kutoa kibali na ataeleza sababu za kukataa maombi. 2 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na 1012(Linaendelea.) Wajibu wa mwenye kibali - 5 Verify source ↗
Mtu atakayepewa kibali cha uchimbaji wa
AI-assisted research summary: Mtu aliyepewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi lazima alipe ada ya kila mwaka, azingatie masharti ya sheria ndogo na ya kibali, achimbe bila kuharibu kingo za korongo kwa njia inayosababisha mmomonyoko au madhara ya mazingira, na alipe ushuru na tozo za Halmashauri.
5. Mtu atakayepewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi atakuwa na wajibu wa- (a) kulipa ada ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi kila mwaka; (b) kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii na masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi; (c) kuchimba madini ya ujenzi pasipo kuharibu kingo za korongo kwa namna itakayosababisha mmomonyoko au athari kwa mazingira; na (d) kulipa ushuru na tozo mbalimbali zinazotozwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii au sheria ndogo nyingine zilizotengenezwa na Halmashauri. Muda wa uchimbaji na masharti ya usafirishaji - 6 Verify source ↗
(1) Shughuli za uchimbaji na usafirishaji wa
AI-assisted research summary: Shughuli za uchimbaji na usafirishaji wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri lazima zifanyike kwa muda uliobainishwa kwenye kibali, na mmiliki au dereva wa chombo cha kusafirisha lazima ahakikishe chombo kimefunikwa wakati wa usafirishaji.
6.-(1) Shughuli za uchimbaji na usafirishaji wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri zitafanyika kulingana na muda uliobainishwa kwenye kibali. (2) Mkurugenzi anaweza kutoa kibali kuruhusu shughuli za uchimbaji na usafirishaji wa madini ya ujenzi kufanyika nje ya muda uliotolewa kwenye kibali. (3) Kila mmiliki au dereva wa chombo kinachotumika kusafirisha madini ya ujenzi atatakiwa kuhakikisha kuwa chombo hicho kimefunikwa wakati wote wa usafirishaji wa madini ya ujenzi. Mamlaka ya afisa mwidhiniwa - 7 Verify source ↗
Afisa mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo
AI-assisted research summary: Afisa mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo la uchimbaji wa madini ya ujenzi ili kufanya ukaguzi na kutoa ushauri wa uendeshaji.
7. Afisa mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo lolote yanapochimbwa madini ya ujenzi kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kutoa ushauri wa uendeshaji wa shughuli za uchimbaji. Ushuru wa madini ya ujenzi - 8 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na ushuru wa madini ya ujenzi
AI-assisted research summary: Wachimbaji au wasafirishaji wa madini ya ujenzi lazima walipe ushuru wa madini ya ujenzi kama ulivyoainishwa na Halmashauri.
8.-(1) Kutakuwa na ushuru wa madini ya ujenzi ambao utalipwa na mchimbaji au msafirishaji wa madini ya ujenzi kama utakavyoainishwa na Halmashauri. (2) Mchimbaji au msafirishaji wa madini ya ujenzi atatakiwa kulipia ushuru wa madini ya ujenzi kwa viwango vilivyoainishwa katika sheria ndogo ya ada na ushuru iliyotengenezwa na Halmashauri. (3) Ushuru wa madini ya ujenzi utatozwa katika eneo la machimbo, barabara zinazoelekea au kutoka 3 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na 1012(Linaendelea.) maeneo ya machimbo au eneo lolote lililo chini ya mamlaka ya Halmashauri. (4) Mchimbaji au msafirishaji atakayeshindwa kulipa ushuru anaotakiwa kulipa atatakiwa kupakua madini ya ujenzi kutoka katika chombo au kutochukua madini hayo mpaka hapo atakapolipa ushuru anaodaiwa. (5) Halmashauri itakuwa na uwezo wa kumzuia mchimbaji au msafirishaji kusafirisha madini ya ujenzi iwapo ikibainika kuna ukwepaji wa kulipa ushuru. - 9 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa malipo ya
AI-assisted research summary: Madereva wa magari yanayobeba madini ya ujenzi lazima wasimame kwenye kituo cha ukaguzi na waoneshe stakabadhi ya kielektroniki ya malipo ya ushuru.
9.(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa malipo ya ushuru wa madini ya ujenzi katika njia zinazoingia au kutoka katika maeneo ya machimbo. (2) Kila dereva wa chombo cha usafiri kilichobeba madini ya ujenzi atatakiwa kusimama katika kituo cha ukaguzi na kuonesha stakabadhi ya kielektroniki inayothibitisha malipo ya ushuru wa madini ya ujenzi yaliyo katika chombo cha usafiri. (3) Endapo dereva wa chombo cha usafiri kilikachokamatwa kwenye eneo la machimbo au wakati wa kusafirisha madini ya ujenzi atatoroka, afisa mwidhiniwa au wakala atazuia chombo hicho hadi faini na ushuru unaodaiwa utakapolipwa. inaweza - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kufuta au kusimamisha kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi ikiwa kuna ukiukwaji wa masharti, lakini kwanza inapaswa kutoa notisi ya siku saba kwa mmiliki wa kibali.
10.(1) Halmashauri au kusimamisha kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi iwapo itajiridhisha kuwa kuna ukiukwaji wa masharti ya Sheria Ndogo hii au masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi. kufuta Vituo vya ukaguzi Kufutwa au kusimamishwa kwa kibali (2) Kabla ya kufuta au kusimamisha kibali, Halmashauri itatakiwa kutoa notisi ya siku saba ya kusudio la kufuta au kusimamisha kibali kwa mmiliki wa kibali. (3) Notisi itakayotolewa itaainisha sababu za kufuta au kusimamisha kibali husika. (4) Endapo kibali kitafutwa au kusimamishwa, mchimbaji atasitisha shughuli za kuchimba madini. Uteuzi wakala wa - 11 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kuteua wakala kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala; wakala huyo lazima akusanye na apokee ada au ushuru, atumie mfumo wa kielektroniki, na atekeleze maagizo ya Halmashauri.
11. (1) Halmashauri inaweza kuteua wakala kwa ajili ya kutekeleza majukumu chini ya Sheria Ndogo hii. 4 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na 1012(Linaendelea.) (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa: (a) kukusanya na kupokea ada au ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kukusanya ada au ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri; na (c) kutekeleza jukumu atakavyoelekezwa na Halmashauri. lingine lolote kadri Hasara wakati wa ukaguzi au ukusanyaji wa ushuru - 12 Verify source ↗
Halmashauri haitawajibika kwa hasara yoyote
AI-assisted research summary: Halmashauri haina jukumu la hasara inayompata mchimbaji au msafirishaji wa madini ya ujenzi wakati wa ukaguzi au ukusanyaji wa ushuru, isipokuwa hasara hiyo imesababishwa na uzembe wa watumishi wake au wakala.
12. Halmashauri haitawajibika kwa hasara yoyote atakayopata mchimbaji au msafirishaji wa madini ya ujenzi wakati wa ukaguzi au ukusanyaji wa ushuru isipokuwa kama hasara hiyo itasababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri au wakala. Makosa - 13 Verify source ↗
Mtu ambaye
AI-assisted research summary: Mtu anayefanya vitendo hivi kuhusu madini ya ujenzi anatenda kosa.
13. Mtu ambaye- (a) ataanzisha machimbo au kuchimba madini ya ujenzi bila kibali; (b) atasafirisha madini ya ujenzi bila kulipa ushuru; (c) atachimba madini ya ujenzi nje ya muda ulioainishwa kwenye kibali; (d) atasafirisha madini ya ujenzi katika chombo ambacho hakijafunikwa; (e) atamshawishi mtu au kundi la watu kutolipa ushuru; (f) atakataa kutii agizo atakalopewa na afisa mwidhiniwa wakati wa utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; (g) atamzuia afisa mwidhiniwa au wakala kutekeleza wajibu wake; (h) atakataa au kukwepa kulipa ushuru; 5 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na 1012(Linaendelea.) Adhabu Kufifilisha kosa (i) atachimba madini katika maeneo yasiyoidhinishwa;au (j) atachimba madini ya ujenzi kwa namna inayoharibu kingo za korongo. anatenda kosa. - 10 Verify source ↗
Mtu akipatikana na hatia kwa kosa lolote chini
AI-assisted research summary: A person found guilty of any offence under this by-law may be fined, imprisoned, or both.
10. Mtu akipatikana na hatia kwa kosa lolote chini ya Sheria Ndogo hii atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 11 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mkosaji kiasi kisichozidi shilingi laki mbili ikiwa mkosaji anakiri kwa hiari, anajaza fomu maalumu, na analipa ada au ushuru unaodaiwa.
11. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili na kulipa ada au ushuru wa madini ya ujenzi unaodaiwa. 6 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na 1012(Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA KWANZA _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 4(1)) KIBALI CHA UCHIMBAJI WA MADINI YA UJENZI hiki kimetolewa kwa Bw/Bi: ………………………………………….……wa Kibali S.L.P………………,.....………. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ameridhia Ndugu mtajwa hapo juu, aendeshe shughuli za kuchimba madini ya ujenzi katika eneo la …………………….……Kijiji cha………………………. kata ya …………………………… baada ya kufanya ukaguzi katika eneo husika ili kutathimini athari za mazingira. Kutokana na uzingatiaji wa athari za mazingira mchimbaji anaruhusiwa kuchimba madini ya ujenzi katika eneo hilo kwa muda wa miezi kumi na mbili tu. Mwombaji analazimika kuomba tena kibali baada ya muda huo kuisha na ukaguzi utafanyika tena. TAMKO LA MWOMBAJI: MIMI………………………nipo tayari kufuata masharti ya kibali hiki cha Uchimbaji wa Madini ya Ujenzi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya………. kwa lengo la kutunza na kuhifadhi mazingira. Nathibitisha kwa hiari yangu nimeelewa vema masharti ya kibali hiki. Jina: ………… Saini ………………….. Tarehe ………………… KWA MATUMIZI YA OFISI TU: Mwombaji amelipia Shilingi ……… tarehe……….mwezi…….Mwaka………… (Ambatanisha stakabadhi ya malipo na fomu hii) Jina la Afisa aliyetoa kibali………… Saini …………… Tarehe …………… Muhuri: ………………………………… 7 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na 1012(Linaendelea.) __________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 11) FOMU YA KUKIRI KOSA Mimi……………………………………………………….…NAKIRI KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa kwa kukiuka masharti ya kanuni ya .…… ya Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka, 2024 NAKUBALI kulipa kiasi cha shilingi.......... cha ada au ushuru ninaodaiwa pamoja na faini ya shilingi......... NATHIBITISHA KWAMBA, maelezo niliyotoa hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa MIMI MWENYEWE na kwa hiari yangu kadri ya ufahamu wangu. Leo hii tarehe………….ya mwezi………….… mwaka 20……………. Jina………………………………..... Saini………........………………...... MBELE YA MKURUGENZI Jina:…………………..................................... Saini:…………………..….............................. Tarehe:.............................................................. 8 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na 1012(Linaendelea.) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia Azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri uliofanyika mnamo tarehe 9/11/2023 mbele ya- MKURUGENZI MTENDAJI (W), Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa MWENYEKITI, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Oktoba, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA (Mb.), Waziri wa Nchi- OR-TAMISEMI, 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in