Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya mwaka 2024
This by-law is called the Kilwa District Council Service Levy By-law 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This by-law is called the Kilwa District Council Service Levy By-law 2024. This provision says the bylaw applies within the area of Kilwa District Council. This section defines key terms used in the bylaw, including the authorized officer, the council, service-levy payer, fiscal year, accounting period, business returns, and related business entities. Halmashauri lazima itozeshe na kukusanya ushuru wa huduma kutoka kwa walipa ushuru wa huduma. Mlipa ushuru wa huduma lazima atunze kumbukumbu, awasilishe hesabu za mwisho kwa Halmashauri ndani ya miezi mitatu, alipe ushuru ndani ya siku 14 baada ya kuwasilisha hesabu, na awasilishe nyaraka au maelezo yanayohitajika ndani ya muda uliowekwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya mwaka 2024
Showing 13 of 13
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This by-law is called the Kilwa District Council Service Levy By-law 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la
AI-assisted research summary: This provision says the bylaw applies within the area of Kilwa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the bylaw, including the authorized officer, the council, service-levy payer, fiscal year, accounting period, business returns, and related business entities.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa; "hesabu" maana yake ni jumla ya mauzo katika mwaka wa mapato; “hesabu za mwisho” maana yake ni taarifa zinazowasilishwa na kampuni au mtu mwenye leseni ya biashara baada ya kipindi cha hesabu ikijumuisha nyaraka, hesabu au maelezo yanayohusu thamani ya kifedha ya bidhaa zilizouzwa au huduma zilizotolewa; Sura ya 212 “kampuni” itakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Kampuni; 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali na.1013 (Linaendelea.) "kipindi cha hesabu" maana yake ni muda ambao mlipa ushuru wa huduma anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara kwa Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa na itajumuisha mtumishi aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mlipa ushuru wa huduma” maana yake ni kampuni, tawi la kampuni au mtu mwenye leseni ya biashara anayefanya shughuli katika eneo la Halmashauri ambaye mauzo yake kwa mwaka ni zaidi ya shilingi milioni nne; “mwaka wa fedha" maana yake ni kipindi cha miezi kumi na mbili kuanzia tarehe 1 Julai hadi tarehe 30 Juni; “taasisi ya kibiashara” maana yake ni taasisi iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni au Sheria ya Majina ya kibiashara inayojihusisha na shughuli za kiuchumi za uzalishaji wa bidhaa au mazao ya kilimo, usambazaji wa bidhaa au utoaji wa huduma na, au biashara ikiwemo uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi. “tawi la kampuni” maana yake ni tawi la kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mtu mwenye leseni ya biashara kwa utaratibu ulioainishwa katika kanuni ya 4; na “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, kampuni au taasisi iliyoingia mkataba kukusanya ushuru wa huduma kwa niaba ya Halmashauri. Ushuru wa huduma - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itozeshe na kukusanya ushuru wa huduma kutoka kwa walipa ushuru wa huduma.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kutoka kwa kila mlipa ushuru wa huduma. 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali na.1013 (Linaendelea.) (2) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu ya mauzo baada ya kutoa kodi ya ongezeko la thamani na ushuru wa bidhaa kutoka kwa mlipa ushuru anayewasilisha hesabu kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. (3) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza kutoka kwa mfanyabiashara mwenye leseni ya biashara ambaye hawasilishi hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. Wajibu wa mlipa ushuru wa huduma - 5 Verify source ↗
(1) Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa na
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa huduma lazima atunze kumbukumbu, awasilishe hesabu za mwisho kwa Halmashauri ndani ya miezi mitatu, alipe ushuru ndani ya siku 14 baada ya kuwasilisha hesabu, na awasilishe nyaraka au maelezo yanayohitajika ndani ya muda uliowekwa.
5. (1) Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu wa- (a) kutunza kumbukumbu za hesabu; (b) kuwasilisha kwa Halmashauri hesabu za mwisho katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia tarehe ya kumalizika kipindi cha hesabu; (c) kulipa ushuru wa huduma ndani ya siku zisizozidi kumi na nne kuanzia tarehe ya kuwasilisha hesabu za mwisho; na (d) kuwasilisha taarifa, nyaraka au maelezo anayotakiwa kuwasilisha Halmashauri ndani ya muda ulioainishwa. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru wa huduma utaratibu wa kulipa ushuru. (3) Endapo mlipa ushuru hatawasilisha hesabu za mwisho kwa mwaka wa mapato husika na baada ya kutakiwa kufanya hivyo kwa notisi ya siku thelathini, Mkurugenzi anaweza kutathmini na kuamua kiwango cha ushuru wa huduma kwa- (a) kutumia taarifa za mlipa ushuru kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania; au (b) kukadiria kiwango cha ushuru wa huduma kwa kutumia taarifa za hesabu za awali za mlipa ushuru. 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali na.1013 (Linaendelea.) Mamlaka Mkurugenzi ya (4) Kiwango kinachopaswa kulipwa na mlipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (3), kitalipwa ndani ya kipindi cha siku saba kuanzia tarehe ya mlipa ushuru wa huduma kufahamishwa kiwango anachotakiwa kulipa. - 6 Verify source ↗
(1) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuhitaji mlipa ushuru wa huduma alete kumbukumbu za biashara na vitabu vya hesabu, kukataa hesabu zisizo sahihi, kumuagiza afisa mwidhiniwa aingie eneo la mlipa ushuru baada ya taarifa, na kuomba taarifa sahihi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania.
6.-(1) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa masharti ya kanuni ya 5, Mkurugenzi anaweza kumtaka mlipa ushuru wa huduma kuwasilisha kumbukumbu za kibiashara na vitabu vya hesabu kwa ajili ya kupata taarifa sahihi kwa madhumuni ya kufanya tathmini au kukusanya ushuru wa huduma. (2) Endapo Mkurugenzi atakuwa na sababu ya msingi ya kuamini kuwa hesabu zilizowasilishwa na mlipa ushuru wa huduma si sahihi anaweza kukataa hesabu hizo. (3) Mkurugenzi anaweza kumuagiza kwa maandishi afisa mwidhiniwa kuingia kwenye jengo au eneo la mlipa ushuru wa huduma baada ya kutoa taarifa kwa mlipa ushuru kwa ajili ya kupata taarifa na kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu ili kujua kiwango sahihi cha ushuru wa huduma. (4) Mkurugenzi anaweza kuomba kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania taarifa sahihi za mlipa ushuru kwa madhumuni ya kufanya tathmini ya kiwango sahihi cha ushuru wa huduma. Uteuzi wa wakala - 7 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kuteua wakala wa
AI-assisted research summary: Halmashauri may appoint an agent to collect service levy, and the appointed agent must collect, receive, electronically process, and remit the levy as instructed.
7. (1) Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru wa huduma. (2) Wakala atakayeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa: (a) kukusanya na kupokea ushuru wa huduma kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kukusanya ushuru wa huduma kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kwa kuwasilisha makusanyo yote kwa na 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali na.1013 (Linaendelea.) kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri; na (c) kutekeleza jukumu lingine lolote kadri atakavyoelekezwa na Halmashauri. Uteuzi maalumu wa mkusanya ushuru - 8 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumteua Kamishna
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumteua Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania au taasisi nyingine ya Serikali kukusanya na kuwasilisha Halmashauri ushuru wa huduma chini ya Sheria Ndogo hii.
8. Mkurugenzi anaweza kumteua Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania au taasisi nyingine ya Serikali kukusanya na kuwasilisha Halmashauri ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Makosa - 9 Verify source ↗
(1) Mtu ambaye
AI-assisted research summary: This section creates offences for anyone who gives false information, fails to pay the service levy, obstructs levy enforcement, fails to keep records, or intentionally damages information systems or levy collection tools.
9.-(1) Mtu ambaye- (a) atawasilisha Halmashauri taarifa za uongo kwa lengo la kupotosha au kukwepa kulipa ushuru wa huduma; (b) atashindwa kulipa ushuru wa huduma kama ilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (c) atamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru; (d) atamzuia Mkurugenzi, afisa mwidhiniwa au wakala wa Halmashauri kutekeleza masharti ya Sheria Ndogo hii; kutunza (e) atashindwa kumbukumbu au nyaraka za hesabu; (f) ataharibu kwa makusudi taarifa au mfumo wa taarifa; au (g) ataharibu kwa makusudi vitendea kazi vya kukusanyia ushuru, anatenda kosa. (2) Wakala aliyeteuliwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii ambaye- 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali na.1013 (Linaendelea.) (a) atatumia nyaraka za kugushi kwa nia ya kujipatia manufaa yatokanayo na ukusanyaji wa ushuru ndani ya Halmashauri; (b) atashindwa kutoa taarifa au atatoa taarifa za uongo Halmashauri kuhusu bidhaa au huduma zinazotakiwa kulipiwa ushuru; (c) hatawasilisha au atawasilisha kwa kuchelewa huduma makusanyo Halmashauri kulingana na muda aliopewa kwa mujibu wa mkataba; ushuru wa ya (d) atashindwa kutunza kumbukumbu sahihi za malipo ya ushuru wa huduma; au (e) kwa makusudi ataharibu, atapoteza au kuficha mashine ya kukusanyia mapato kwa lengo la kupoteza kumbukumbu sahihi za mauzo ya mlipa ushuru. anatenda kosa. - 10 Verify source ↗
(1) Mtu akipatikana na hatia kwa kosa lolote
AI-assisted research summary: A person convicted of any offence under this by-law must pay a fine, face imprisonment, or both; if the person is an agent, they must also pay the Council amounts owed by the service taxpayer.
10.-(1) Mtu akipatikana na hatia kwa kosa lolote chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. (2) Endapo mtu aliyepatikana na hatia ni wakala, pamoja na adhabu iliyoainishwa katika kanuni ndogo ya (1) atalipa Halmashauri kiasi cha pesa alizopaswa kulipa au zilizopaswa kulipwa na mlipa ushuru wa huduma. - 11 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji hadi shilingi 200,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari, anajaza fomu maalumu ya Jedwali la Pili, na analipa ushuru wa huduma unaodaiwa.
11. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili na kulipa ushuru wa huduma anaodaiwa. Adhabu Kufifilisha kosa Kufutwa kwa TS Na.19 la 2016 - 12 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya
AI-assisted research summary: This section repeals the Kilwa District Council service levy by-law.
12. Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa inafutwa. 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali na.1013 (Linaendelea.) __________ JEDWALI LA KWANZA ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(3)) USHURU WA HUDUMA. Namba Aina ya malipo Leseni ya biashara Kiasi cha malipo ya Ushuru wa Huduma kwa Mwaka (Shilingi)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaonyesha fomu ya kukiri kosa na kukubali kulipa ushuru wa huduma pamoja na faini mbele ya Mkurugenzi.
8. 0 hadi 15,000/= 20,000/= hadi 35,000/= 40,000/= hadi 45,000/= 50,000/= hadi 60,000/= 65,000/= hadi 100,000/= 105,000/= hadi 150,000/= 5000/= 10,000/= 15,000/= 30,000/= 40,000/= 50,000/= 155,000/= hadi 200,000/= 100,000/= Malipo ya leseni za vilabu vya pombe 24,000/= za asili 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali na.1013 (Linaendelea.) _____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 11) FOMU YA KUKIRI KOSA Mimi………………………………………………………NAKIRI KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya ........., kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa kwa kukiuka masharti ya kanuni ya .…… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya ......... ya Mwaka, 20.... NAKUBALI kulipa kiasi cha shilingi.......... cha ushuru wa huduma ninaodaiwa pamoja na faini ya shilingi......... NATHIBITISHA KWAMBA, maelezo niliyotoa hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa MIMI MWENYEWE na kwa hiari yangu kadri ya ufahamu wangu. Leo hii tarehe………….ya mwezi…………..… mwaka 20……………. Jina………………………………..... Saini………........………………...... MBELE YA MKURUGENZI Jina:…………………..................................... Saini:…………………..….............................. Tarehe:.............................................................. 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali na.1013 (Linaendelea.) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia Azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri uliofanyika mnamo tarehe 9/11/2023 mbele ya- HANAN M. BAFAGIH, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya Kilwa MHE. ISSA B. MATEKA, Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya L.S NAKUBALI, Dodoma 29 Oktoba,2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi-OR-TAMISEMI, 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in