Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
This section says the by-law will be known as the Dar es Salaam City Council Markets and Stalls Management and Operation By-law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Act or statute
- Citation
- Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section says the by-law will be known as the Dar es Salaam City Council Markets and Stalls Management and Operation By-law, 2024. This by-law applies throughout the Dar es Salaam City Council area, except for Kariakoo Market Company markets and Soko la Samaki Feri Magogoni. This section gives the meanings of key terms used in the By-laws, such as officer, broker, shop, market, auction, permit, trader, and Council. Halmashauri ina wajibu wa kusimamia masoko na kufanya kazi kadhaa za usimamizi wa masoko. Halmashauri inapaswa kutoza ada au ushuru kwa masoko, minada na magulio kwa huduma na shughuli zilizo kwenye Jedwali la Kwanza.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
Showing 55 of 55
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This section says the by-law will be known as the Dar es Salaam City Council Markets and Stalls Management and Operation By-law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the Dar es Salaam City Council area, except for Kariakoo Market Company markets and Soko la Samaki Feri Magogoni.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam isipokuwa masoko yanayomilikiwa na Shirika la Masoko Kariakoo na Soko la Samaki Feri Magogoni. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo, hii isipokuwa kama muktadha
AI-assisted research summary: This section gives the meanings of key terms used in the By-laws, such as officer, broker, shop, market, auction, permit, trader, and Council.
3. Katika Sheria Ndogo, hii isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “dalali” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa za sokoni kwa niaba ya mwenye bidhaa kwa mujibu wa taratibu za soko; “duka” maana yake ni chumba kilichotengwa kwa ajili ya kupangishwa na Halmashauri kwa matumizi ya kuuzia au kuhifadhia bidhaa; “gulio” maana yake ni eneo maalumu lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuuza na kununua bidhaa kwa kipindi maalumu isipokuwa mifugo na wanyama wa aina yeyote; “gunia” maana yake ni mfuko wenye ujazo usiozidi debe 6 au kilo 100; 1 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; “kamati ya wadau wa soko” maana yake ni kamati itakayoundwa chini ya Sheria Ndogo hii; “kasha” maana yake ni kifaa au kitu kinachotumika kubebea au kuhifadhi bidhaa au mazao na inajumuisha tenga, kiroba, gunia, karatasi ngumu na sanduku la mbao; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii; “kitengo” maana yake ni kikundi cha wafanyabiashara waliopo katika eneo mahsusi ndani ya soko wanaofanya biashara zinazowiana; “kizimba” maana yake ni meza, nafasi au sehemu nyingine katika soko, mnada au gulio inayotumika kwa ajili ya kuuza bidhaa; “kodi ya pango” maana yake ni kiasi cha fedha ambacho kitatozwa na Halmashauri ikiwa ni malipo ya pango, kibanda, meza au kizimba vilivyomo katika soko, gulio, mnada au maeneo yoyote ya Halmashauri kwa kipindi maalumu; “mdau wa soko’’ maana yake ni mfanyabiashara binafsi, taasisi, kampuni, kikundi cha wauzaji au wanunuzi, mnunuzi, dalali au mtumiaji mwingine aliyesajiliwa au mwenye maslahi na shughuli za soko au mtu yeyote anayenufaika na uwepo wa soko; “mfanyabiashara” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa sokoni, mnadani au gulioni kwa jumla au rejareja kwenye eneo ambalo limeruhusiwa chini ya Sheria Ndogo hii; “mkuu wa soko” maana yake ni mtu aliyeteuliwa na Halmashauri kusimamia shughuli mbalimbali katika soko linalomilikiwa na Halmashauri, au mtu anayesimamia soko binafsi ambalo limeidhinishwa na Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam au afisa anayetekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mnada” maana yake soko la wazi lililoidhinishwa na Halmashauri ambalo mali au vitu mbalimbali vinauzwa kwa ushindani wa bei; 2 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) “mpangaji” maana yake ni mtu, taasisi, kikundi au kampuni yoyote iliyopangishwa na Halmashauri ndani ya soko au iliyopangishwa na mmiliki wa soko binafsi na ana idhini ya maandishi kutoka kwa mkataba au Halmashauri au mmiliki binafsi wa soko; “kifaa cha mauzo” maana yake ni kifaa kinachotumika kukusanya ushuru au ada na kutunza kumbukumbu; “soko” maana yake ni eneo maalumu lililotengwa na Halmashauri kwa matumizi ya kuuza na kununua bidhaa na inajumuisha soko linalomilikiwa na mtu binafsi; na “Wakala” maana yake ni mtu au kikundi cha watu, taasisi, kampuni limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. ambalo shirika au Wajibu wa Halmashaur i - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri ina wajibu wa kusimamia masoko na kufanya kazi kadhaa za usimamizi wa masoko.
4.- Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kuanzisha, kuendeleza, kusimamia na kuboresha miundombinu ya masoko; (b) kusimamia ufikishaji wa huduma za kijamii katika soko; (c) kugawa na kupangisha vyumba, meza au vizimba katika masoko ya Halmashauri; (d) kusimamia usafi na usalama wa masoko; (e) kutenga maeneo kwa ajili ya magulio; (f) kukagua namna ya uendeshwaji wa masoko binafsi ili kujiridhisha iwapo sheria, kanuni na taratibu zinazingatiwa; (g) kusajili wafanyabiashara katika masoko ya Halmashauri; na ada (h) kukusanya kwa wafanyabiashara wa masoko, minada na magulio. ushuru kutoka na Ada na ushuru - 5 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ada au ushuru kwenye
AI-assisted research summary: Halmashauri inapaswa kutoza ada au ushuru kwa masoko, minada na magulio kwa huduma na shughuli zilizo kwenye Jedwali la Kwanza.
5.-(1) Halmashauri itatoza ada au ushuru kwenye masoko, minada na magulio kwa huduma na shughuli mbalimbali kama zilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (2) Ushuru utakaotozwa chini ya Sheria Ndogo hii utalipwa kabla, baada au wakati wa mauzo au ununuzi wa bidhaa. 3 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) (3) Ada itakayotozwa chini ya Sheria Ndogo hii italipwa kabla ya huduma kutolewa. Mkuu wa Soko - 6 Verify source ↗
Kutakuwa na Mkuu wa Soko atakayeteuliwa na
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Halmashauri huteua Mkuu wa Soko, na Mkuu wa Soko husimamia uendeshaji wa soko na majukumu yake ya kila siku.
6. Kutakuwa na Mkuu wa Soko atakayeteuliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri kusimamia shughuli za uendeshaji wa soko la Halmashauri ikiwa ni pamoja na- (a) kuandaa, kuendeleza na kutunza takwimu sahihi katika soko; (b) kuandaa na kusimamia mpango wa kukusanya ushuru na ada mbalimbali kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (c) kuhakikisha kuwa huduma za ulinzi, maji, umeme na huduma nyingine katika soko zinaimarika; (d) kuandaa na kusimamia utaratibu wa usajili wa wadau wa soko; (e) kuhakikisha kuwa soko linakuwa katika hali ya usafi na kwamba kunakuwa na mpango mzuri wa uondoshaji wa taka katika soko; (f) kuhakikisha kuwa kuna mpango mzuri wa uendeshaji wa biashara kwenye maeneo yote ya soko pamoja na kudhibiti ujenzi holela kwenye soko; (g) kusimamia ujenzi, ukarabati na uboreshaji wa soko na miundombinu yake; na (h) kutekeleza majukumu mengine yoyote atakayopangiwa na Mkurugenzi. Mhasibu wa Soko - 8 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Mhasibu wa Soko atakayeteuliwa
AI-assisted research summary: A Market Accountant is to be appointed by the Director and must manage market revenue and related records and reports.
8.-(1) Kutakuwa na Mhasibu wa Soko atakayeteuliwa na Mkurugenzi kwa ajili ya kusimamia mapato yote ya Halmashauri katika soko chini ya Sheria Ndogo hii atajulikana kama Mhasibu. (2) Mhasibu atakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kukusanya mapato ya soko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii na kuhakikisha yanawasilishwa Benki kila siku; (b) kusimamia rejesta za walipa ushuru na rejesta za madeni ya walipa ushuru; (c) kuandaa na kuhakikisha posho za vibarua wa ushuru na usafi zinalipwa kwa wakati; (d) kusimamia ununuzi wa mahitaji mbalimbali katika soko; 4 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) (e) kuaandaa taarifa ya makusanyo kila mwisho wa wiki na mwezi; na (f) kutunza kumbukumbu sahihi za mizigo yote inayoingia katika soko. Mhasibu Mkuu wa Masoko - 9 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Mhasibu Mkuu wa Masoko
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anateua Mhasibu Mkuu wa Masoko, na Mhasibu Mkuu lazima asimamie mapato na utekelezaji wa kazi mbalimbali za masoko na magulio.
9.-(1) Kutakuwa na Mhasibu Mkuu wa Masoko atakayeteuliwa na Mkurugenzi kwa ajili ya kusimamia mapato yote katika masoko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii na atajulikana kama Mhasibu Mkuu. (2) Mhasibu Mkuu atakuwa na majukumu yafuatayo- (a) kusimamia utendaji kazi wa wahasibu wote wa masoko na magulio yote ya Halmashauri; (b) kusimamia ukusanyaji wa mapato katika masoko na magulio yote ya Halmashauri na masoko binafsi yalioidhinishwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii na kuhakikisha yanawasilishwa benki kila siku; (c) kuhakikisha vifaa vyote vya mauzo ya masoko na magulio vinakuwa mtandaoni ili miamala yote isome katika mfumo wa mapato; (d) kuandaa, kusimamia na kufatilia taarifa ya makusanyo ya kila siku na kiasi kilichopelekwa Benki na kuwasilisha kwa Mhasibu wa Mapato; (e) kufanya usuluhishi wa miamala ya makusanyo katika kifaa cha mauzo na kiasi kilichopelekwa Benki kila siku na kuiwasilisha kwa Mhasibu wa Mapato; (f) kuhakikisha mawakala wote wanaokusanya mapato katika masoko wanatekeleza kwa mujibu wa Mkataba; (g) kuandaa rejesta ya walipa ushuru wote wa vyanzo vyote katika masoko; (h) kusimamia mikataba yote ya wapangaji katika vizimba, vibanda,maduka na kuhakikisha kila Mpangaji ana Mkataba; (i) kusimamia na kutunza taarifa za matumizi yanayofanyika kwenye masoko; (j) kujibu hoja zote za ukaguzi wa ndani na nje zinazohusiana na masoko na magulio; na 5 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) (k) kutekeleza majukumu mengine atakayopangiwa na Mkurugenzi. yeyote Kamati ya Wadau Soko - 10 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Kamati ya wadau wa soko
AI-assisted research summary: Market stakeholders must form a market stakeholders committee, and some members are chosen through elections by registered traders.
10.-(1) Kutakuwa na Kamati ya wadau wa soko ambayo itaundwa na wadau wa soko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Wajumbe wa Kamati ya wadau wa soko watakuwa ni- (a) Mwenyekiti; (b) Makamu Mwenyekiti; (c) Katibu; (d) Mwenyekiti wa kila kitengo sokoni; (e) Katibu wa kila kitengo sokoni; (f) Mhasibu wa soko; na (g) wawakilishi watatu wa wanawake waliopata kura nyingi. (3) Wajumbe wa Kamati ya Wadau wa Soko watapatikana baada ya kuomba kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mkuu na kupigiwa kura na wafanyabiashara wote katika soko waliopo kwenye rejesta ya soko. (4) Wawakilishi waliotajwa watapatikana baada ya kila kitengo kuchagua mwakilishi mmoja ambaye jina lake litawasilishwa katika uchaguzi mkuu kwa ajili ya kupigiwa kura na wafanyabiashara wote wa soko waliopo kwenye rejesta ya soko. (5) Baada ya kupigiwa kura wawakilishi watatu watakaopata kura nyingi ndiyo watakuwa wawakilishi katika Kamati ya Wadau wa Soko. (6) Katibu na Mhasibu wa soko ni wajumbe wa kuteuliwa na hawatakuwa na haki ya kupiga kura katika vikao vya Kamati ya wadau wa soko. Majukumu ya Kamati ya Wadau wa Soko - 11 Verify source ↗
Kamati ya wadau wa soko itakuwa na majukumu
AI-assisted research summary: Kamati ya wadau wa soko must handle market coordination, reporting, sanitation, security, revenue protection, and advice functions.
11. Kamati ya wadau wa soko itakuwa na majukumu yafuatayo- (a) kuunganisha wadau wote waliopo sokoni bila kujali tofauti zao za vyama, kabila, dini au vikundi vilivyopo sokoni; (b) kushirikiana na Serikali katika kuwaletea maendeleo wadau wa soko kulingana na sera na mipango iliyopo; 6 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) (c) kutetetea na kulinda maslahi ya haki za wadau kwa kutumia njia na mwenendo sahihi unaokubalika kisheria (d) kuwasilisha taarifa ya kikao cha kamati ya wadau wa soko ya kila miezi mitatu kwa Halmashauri kupitia kwa mkuu wa soko; (e) kushauri kuhusu uboreshaji wa ustawi wa wadau wa soko; (f) kupanga na kusimamia utaratibu thabiti wa uchangiaji wa gharama kutoka kwa kila mdau wa soko katika kugharamia huduma ya ulinzi, usafi, maji na umeme kulingana na mahitaji ya soko; (g) kuhakikisha kwamba nidhamu inakuwepo katika shughuli za soko; (h) kushauri kuhusu ubora wa mfumo wa biashara katika soko; (i) kusimamia usafi katika maeneo ya soko; (j) kudhibiti na kufichua upotevu wa mapato ya soko na kuhakikisha mapato yanapanda na hayapotei kwa kushirikiana na Mkuu wa soko; (k) kuhamasisha watumiaji wa soko kutekeleza wajibu wa ulipaji ada au ushuru pamoja na tozo kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; na (l) kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo katika soko. Kamati Ndogo - 12 Verify source ↗
Kamati ya wadau wa soko itaunda kamati ndogo
AI-assisted research summary: Kamati ya wadau wa soko lazima iunde kamati ndogo zenye wajumbe wanne kutoka miongoni mwa wajumbe wake.
12. Kamati ya wadau wa soko itaunda kamati ndogo zenye wajumbe wanne kutoka miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya wadau wa soko ambazo ni- (a) Kamati Ndogo ya Mipango, Uchumi na Miundombinu; (b) Kamati Ndogo ya Biashara na Utawala; na (c) Kamati Ndogo ya Afya, Usafi, Ulinzi na Usalama, na Mazingira. Kamati ndogo ya - 13 Verify source ↗
Kamati Ndogo ya Mipango, Uchumi na
AI-assisted research summary: Kamati Ndogo ya Mipango, Uchumi na Miundombinu lazima ifuate na kutekeleza maagizo ya kamati ya wadau wa soko, kuboresha ustawi na ufanisi wa wadau, na kutoa mapendekezo ya kuongeza vyanzo vya mapato.
13. Kamati Ndogo ya Mipango, Uchumi na Miundombinu itakuwa na majukumu ya- 7 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) Mipango, Uchumi na Miundombi nu Kamati Ndogo ya Biashara na Utawala Kamati Ndogo ya Afya, Usafi, Ulinzi na Mazingira (a) kufanyia kazi na kutekeleza maagizo yote ya Kamati ya wadau wa soko kuhusiana na mipango, uchumi na miundombinu ya soko; (b) kuimarisha ustawi na ufanisi wa wadau wote wa soko; (c) kutoa mapendekezo ya kuimarisha na kuongeza vyanzo vya mapato; na (d) kutekeleza majukumu yoyote itakayopangiwa na Kamati ya wadau wa soko. - 14 Verify source ↗
Kamati Ndogo ya Biashara na Utawala itakuwa na
AI-assisted research summary: Kamati Ndogo ya Biashara na Utawala lazima itekeleze na kusaidia maagizo na majukumu ya Kamati ya wadau wa soko, kushirikiana katika kufuatilia madeni, kushughulikia migogoro, na kutekeleza majukumu mengine itakayopangiwa.
14. Kamati Ndogo ya Biashara na Utawala itakuwa na majukumu ya- (a) kufanyia kazi na kutekeleza maagizo ya Kamati ya wadau wa soko kuhusiana na Biashara na Utawala; (b) kusaidia utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya wadau wa soko kwa kadri yatakavyotolewa maelekezo na Kamati ya wadau wa soko; (c) kushirikiana na Kamati ya wadau wa soko katika kufuatilia madeni ya wafanyabiashara wote; (d) kushughulikia migogoro itakayojitokeza baina ya wadau wa soko; na (e) kutekeleza majukumu yoyote itakayopangiwa na Kamati ya wadau wa soko. - 15 Verify source ↗
Kamati ndogo ya Afya, Usafi, Ulinzi na Mazingira
AI-assisted research summary: The subcommittee must carry out market committee instructions and handle market health, cleanliness, security, and environmental duties.
15. Kamati ndogo ya Afya, Usafi, Ulinzi na Mazingira itakuwa na majukumu ya- (a) kufanyia kazi na kutekeleza maagizo ya Kamati ya wadau wa soko; (b) kuhakikisha sheria na taratibu zilizopo zinafuatwa; (c) kuimarisha ulinzi na usalama katika soko; (d) kuhakikisha soko linakuwa katika hali ya usafi; (e) kuwaelimisha wadau wa soko na watumiaji wengine juu ya ulinzi, usafi, afya na manzingira; na (f) kutekeleza majukumu yoyote itakayopangiwa na Kamati ya wadau wa soko. Kuanzishw a kwa vitengo vya Soko - 16 Verify source ↗
(1) Kwa madhumuni ya uendeshaji bora wa soko,
AI-assisted research summary: Soko litagawanywa katika vitengo kulingana na bidhaa zinazowiana, na kila mfanyabiashara sokoni lazima ajisajili katika kitengo chake na awe mjumbe wa hicho kitengo.
16.-(1) Kwa madhumuni ya uendeshaji bora wa soko, soko litagawanyika katika vitengo kulingana na bidhaa zinazowiana na kufanana. 8 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) (2) Upangiliaji wa vitengo utafanywa na mkuu wa soko akishirikiana na Kamati ya wadau wa soko. (3) Kila mfanyabiashara aliyeko sokoni atawajibika kujisajili katika kitengo chake na atakuwa mjumbe wa kitengo hicho. (4) Kila kitengo kitakuwa na viongozi wafuatao ambao wataunda kamati tendaji ya kitengo na watachaguliwa kwa mujibu wa katiba ya kitengo husika- (a) Mwenyekiti; (b) Makamu Mwenyekiti; (c) Katibu; (d) Katibu Msaidizi; (e) Mhasibu; na (f) wajumbe wa kitengo kwa idadi kulingana na Katiba ya kitengo husika. Majukumu ya Kamati tendaji ya kitengo ya- - 17 Verify source ↗
Kamati tendaji ya kitengo itakuwa na majukumu
AI-assisted research summary: Kamati tendaji ya kitengo inapaswa kutekeleza majukumu yake ya uendeshaji na uratibu wa kitengo.
17. Kamati tendaji ya kitengo itakuwa na majukumu (a) kuandaa na kuratibu vikao vyote vya kitengo; (b) kupokea na kuandaa za kitengo zinazotakiwa kwenda ndani na nje ya soko na kuzifanyia kazi; taarifa (c) kutekeleza maagizo ya Kamati ya wadau wa soko kwa kadri itakavyoelekezwa; (d) kutunza nyaraka zote zinazotoka na kuingia katika kitengo; (e) kushughulikia migogoro itakayojitokeza katika kitengo; (f) kushirikiana na Halmashauri katika kukusanya ushuru kwa kutoa takwimu sahihi za mazao yanayoingia katika kitengo kila siku na idadi kamili ya wafanyabiashara waliopo kwenye kitengo hicho; na (g) kutekeleza majukumu yoyote itakayopangiwa na Kamati ya wadau wa soko. Vikao vya Kamati ya Wadau wa Soko - 18 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na kikao cha Kamati ya wadau wa
AI-assisted research summary: The market stakeholders committee must meet once every three months, with the Market Master as secretary.
18.-(1) Kutakuwa na kikao cha Kamati ya wadau wa soko ambacho kitafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu ambapo Mkuu wa Soko atakuwa Katibu wa kikao. 9 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) (2) Kikao cha Kamati ya wadau wa soko kitaendeshwa na Mwenyekiti na endapo Mwenyekiti atashindwa kuendesha kikao hicho kwa sababu yoyote ile wajumbe waliohudhuria kikao husika watamchagua mjumbe kutoka miongoni mwao kuendesha kikao hicho. (3) Akidi katika kikao cha Kamati ya wadau wa soko itakuwa ni nusu ya wajumbe wote wa Kamati ya wadau wa soko. ….(4) Taarifa ya kikao cha Kamati ya wadau wa soko, itatolewa na Katibu wa Kamati ya wadau wa soko si chini ya siku saba kabla ya tarehe ya kikao. (5) Wajumbe wa Kamati ya wadau wa soko wanaweza, kwa ridhaa yao, kuendelea na kikao ambacho taarifa yake imetolewa chini ya muda wa siku saba. (6) Mwenyekiti wa Kamati ya wadau wa soko anaweza kuitisha kikao cha dharura baada ya kujadiliana na Mkuu wa Soko au Mkurugenzi akieleza sababu ya kikao hicho kuitishwa. (7) Taarifa ya kikao cha dharura cha Kamati ya wadau wa soko, itatolewa ndani ya siku tatu baada ya makubaliano ya Mwenyekiti wa Kamati ya wadau wa soko na Mkurugenzi. (8) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (7), hakutakuwa na kikao cha dharura zaidi ya kimoja kitakachoitishwa ndani ya miezi mitatu. Mikutano mbalimbali ya uendeshaji wa soko - 19 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa vitengo
AI-assisted research summary: Section 19 requires a general meeting of all units every six months and a general meeting of all market stakeholders once a year.
19.-(1) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa vitengo vyote, utakaofanyika kila baada ya miezi sita ambapo wajumbe wa mkutano huu watakuwa viongozi wote wa kila kitengo, na utajadili- (a) kupokea na kujadili taarifa za utendaji kazi za Kamati ya wadau wa soko na Kamati Ndogo zilizoundwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) kupokea taarifa zinazohusu soko; (c) kupokea taarifa za mapato na matumizi za kamati ya wadau wa soko na kuijadili; (d) kujadili namna ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo watu wote walio kwenye vitengo vyao; (e) uboreshaji wa ustawi wa wadau wa soko; (f) kuinua ubora wa mfumo wa biashara katika soko; 10 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) (g) kupokea taarifa za maendeleo ya soko; na (h) kujadili masuala yanayohusu miundombinu na mazingira. (2) kutakuwa na Mkutano Mkuu wa wadau wote wa soko, utakaofanyika mara moja kwa mwaka, wajumbe wa mkutano huu watakuwa ni- (a) kamati ya wadau wa soko; (b) viongozi wote wa kila kitengo kilichopo sokoni; (c) mwenyekiti na katibu wa vyama vyote vilivyoko sokoni vinavyotambulika na Mkuu wa soko na Kamati ya Wadau wa Soko; (d) wadau wote wa soko; (e) waalikwa kutoka nje ya soko; na (f) uwakilishi wa viongozi kutoka Halmashauri. (3) Kazi za Mkutano Mkuu wa wadau wote wa soko zitakuwa ni- (a) kupokea na kutoa ushauri juu ya taarifa mbalimbali za uendeshaji wa soko; (b) kuwasilisha mapendekezo ya ufanyaji wa maboresho ya uendeshaji wa soko, kamati ya wadau na menejimenti ya soko na Halmashauri juu ya uendeshaji bora wa utoaji wa huduma za soko; (c) kupokea taarifa za mapato na matumizi ya kamati ya wadau wa soko na kuijadili; (d) kupokea taarifa za miundombinu ya soko na kuwasilisha mapendekezo ya wadau; na (e) kuishauri Kamati ya wadau wa soko na Halmashauri namna bora ya kuimarisha na udhibiti wa mapato ya soko. - 20 Verify source ↗
Kamati ya wadau wa soko na viongozi wa vitengo
AI-assisted research summary: Kamati ya wadau wa soko na viongozi wa vitengo wanakaa madarakani kwa miaka mitatu kuanzia siku ya kuchaguliwa, na wanaweza kuchaguliwa tena.
20. Kamati ya wadau wa soko na viongozi wa vitengo watakaa madarakani kwa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe ya kuchaguliwa kwao na wanaweza kuchaguliwa tena. - 21 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Uchaguzi Mkuu wa wajumbe wa
AI-assisted research summary: Uchaguzi mkuu wa wajumbe wa Kamati ya wadau wa soko utafanyika kila baada ya miaka mitatu, na ni wafanyabiashara wa soko walio kwenye rejesta pekee ndio watakaopewa ruhusa ya kupiga kura.
21.-(1) Kutakuwa na Uchaguzi Mkuu wa wajumbe wa Kamati ya wadau wa soko utakaofanyika kila baada ya miaka mitatu. 11 Muda wa Madaraka kwa viongozi wa Kitengo na Kamati ya Wadau Uchaguzi Mkuu wa Kamati ya Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) Wadau wa soko Usajili wa wadau Kibali cha watumiaji wa Soko Kufuta kibali (2) Wafanyabiashara wote wa soko waliopo kwenye rejesta ya soko ndiyo watakaoruhusiwa kupiga kura katika Uchaguzi mkuu. (3) Uchaguzi Mkuu wa wajumbe wa Kamati ya wadau wa soko, utasimamiwa na Mkuu wa Soko, Afisa Ushirika, Afisa Uchaguzi, Mkuu wa Masoko, Mwanasheria wa Halmashauri na wajumbe watatu watakaochaguliwa na wafanyabiashara na mmoja kati yao atakuwa mwanamke. na (4) Wajumbe watatu watakaochaguliwa wafanyabiashara kusimamia Uchaguzi mkuu hawatagombea nafasi yoyote ya uongozi katika uchaguzi huo. - 22 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetaka kufanya biashara katika
AI-assisted research summary: Anyone who wants to do business in the market area must be registered by the market officer, working with the market stakeholders committee.
22. Mtu yeyote anayetaka kufanya biashara katika eneo la soko atatakiwa kusajiliwa na mkuu wa soko akishirikiana na Kamati ya wadau wa soko kwa lengo la kumtambua na kumworodhesha katika rejesta ya wadau wa soko. - 23 Verify source ↗
(1) Mfanyabiashara yeyote anayefanya au
AI-assisted research summary: A trader who is doing or wants to do business must apply to the council for a permit by filling out the prescribed form.
23.-(1) Mfanyabiashara yeyote anayefanya au anayetaka kufanya biashara ataomba kibali kwa Halmashauri kwa kujaza fomu kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Pili. (2) Kibali hicho kitatolewa kwa mwombaji kupitia kwa Mkuu wa soko na kamati ya wadau wa soko bila gharama na kitadumu kwa muda wa mwaka mmoja tangu siku ya kutolewa. - 24 Verify source ↗
(1) Mkurugenzi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufuta kibali baada ya notisi ya siku 30 ikiwa mwenye kibali ana madeni ya ada/ushuru, amesimamisha shughuli kwa miezi mitatu, anakiuka masharti, anawahamasisha wengine kutofuata sheria, au anatumia sehemu iliyopangiwa kinyume na mkataba au maelekezo.
24.-(1) Mkurugenzi kibali kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hii, baada ya kutoa notisi ya siku thelathini, endapo mwenye kibali- anaweza kufuta (a) atakuwa na malimbikizo ya ada au ushuru kinyume na Mkataba wake na Halmashauri; (b) atakuwa amesimamisha shughuli zake kwa miezi mitatu bila taarifa; (c) atakuwa na mwenendo unaokiuka masharti ya Sheria Ndogo hii; (d) atawashawishi wengine kutofuata Sheria Ndogo hii au kusababisha uvunjaji wa amani; au wafanyabiashara (e) atatumia chumba, kibanda, meza au kizimba alichopanga kinyume na madhumuni ya kufanyia 12 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) biashara kama yalivyoainishwa kwenye mkataba wa upangishaji au maelekezo yatakayotolewa na Halmashauri. (2) Baada ya kufutiwa kibali mfanyabiashara anaweza kuomba kibali upya kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Wajibu wa wadau wa soko - 25 Verify source ↗
Kila mdau wa soko katika eneo la soko atakuwa na
AI-assisted research summary: Wadau wote wa soko ndani ya eneo la soko lazima wajisajili, walinde miundombinu, wafanye biashara maeneo yanayoruhusiwa, waweke usafi, walipe ushuru au ada kwa wakati, na wafuate masharti na kanuni za soko.
25. Kila mdau wa soko katika eneo la soko atakuwa na wajibu wa- (a) kusajiliwa na mkuu wa soko katika rejesta ya wadau wa soko; (b) kulinda na kuhifadhi miundombinu ya soko; (c) kufanya biashara katika maeneo yanayoruhusiwa; (d) kufanya usafi katika eneo lake la biashara; (e) kulipa ushuru au ada kwa wakati; (f) kutobandika au kubandua tangazo bila idhini ya mkuu wa soko; (g) kutotumia lugha ya matusi, kuudhi au kashfa katika eneo la soko; (h) kushiriki usafi wa jumla wa soko; (i) kutotupa taka ovyo au kutiririsha maji machafu; (j) kutowasha moto maeneo yasiyoruhusiwa ndani ya soko; (k) kuzingatia masharti ya upangaji yaliyowekwa katika soko; na (l) kuzingatia kanuni na taratibu nyingine zitakazoelekezwa na viongozi wa soko. Ujenzi na ukarabati - 26 Verify source ↗
(1) Mtu hataruhusiwa kufanya ujenzi, ukarabati au
AI-assisted research summary: A person may not build, repair, or alter certain market structures without written approval from the Council. The market officer may close the market for maintenance or other emergency reasons after consulting the Director. If closure is for maintenance, seven days’ notice must be given to market stakeholders.
26.-(1) Mtu hataruhusiwa kufanya ujenzi, ukarabati au marekebisho ya chumba, kibanda, meza au kizimba bila idhini ya maandishi ya Halmashauri. (2) Mkuu wa soko, kwa kushauriana na Mkurugenzi, anaweza kufunga soko kwa ajili ya matengenezo au sababu nyingine yoyote ya dharura pale itakapoonekana inafaa. (3) Endapo soko linakusudiwa kufungwa kwa ajili ya matengenezo, mkuu wa soko atatoa notisi ya siku saba kwa wadau wa soko kuhusu kusudio la kufunga soko. Muda wa biashara - 27 Verify source ↗
Soko litakuwa wazi kila siku kuanzia saa kumi na
AI-assisted research summary: The market must be open every day from 6:00 a.m. to 6:00 p.m.
27. Soko litakuwa wazi kila siku kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni. 13 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) Kodi ya pango Usimamizi wa vyombo vya usafiri katika soko Kibali cha minada na magulio - 28 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabishara katika soko atalipa kodi ya
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wa soko wanapaswa kulipa kodi ya pango kwa vibanda au vizimba vya soko; mfanyabiashara anayekusudia kupanga pia hulipa kwa Halmashauri au Wakala kulingana na Jedwali la Kwanza. Halmashauri inaweza, kwa makubaliano maalum, kuruhusu mtu yeyote kujenga banda la biashara katika eneo la soko.
28.-(1) Kila mfanyabishara katika soko atalipa kodi ya pango kwa ajili ya kupangishwa kizimba au kibanda katika soko. (2) Mfanya biashara anayekusudia kupanga katika soko atalipa kodi ya pango kwa Halmashauri au Wakala kama inavyoonekana kwenye Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (3) Halmashauri inaweza, kwa makubaliano maalum, kumruhusu mtu yeyote kujenga banda la biashara katika eneo la soko. - 29 Verify source ↗
(1) Msafirishaji anayeingiza mazao au bidhaa
AI-assisted research summary: Msafirishaji anayeingiza mazao au bidhaa sokoni kwa kutumia chombo cha usafiri lazima ashushe bidhaa katika maeneo yaliyoainishwa, na Mkuu wa soko ana mamlaka ya kupanga na kusimamia idadi ya magari yanayoruhusiwa kushusha bidhaa au mazao sokoni.
29.-(1) Msafirishaji anayeingiza mazao au bidhaa sokoni kwa kutumia chombo cha usafiri atashusha bidhaa katika maeneo yaliyoainishwa kwa shughuli hiyo. (2) Mkuu wa soko atakuwa na mamlaka ya kupanga na kusimamia idadi ya magari yatakayoruhusiwa kushusha bidhaa au mazao sokoni. - 30 Verify source ↗
(1) Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kutoa kibali maalum kwa magulio katika maeneo yaliyotengwa, na shughuli za minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine zinaruhusiwa kufanyika sokoni kwa kibali maalum kinachoombwa kwa fomu maalum.
30.-(1) Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine itaruhusiwa kufanyika kwenye masoko kwa kibali maalum cha Halmashauri ambacho kitaombwa kwa kutumia fomu maalum inayopatikana katika Jedwali la Pili. (2) Halmashauri inaweza kutoa kibali maalum cha kufanyika kwa magulio katika maeneo yatakayotengwa na Halmashauri. Usafi wa soko - 31 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabiashara anayefanya biashara
AI-assisted research summary: Market traders must keep their stall area clean at all times and follow health rules.
31.-(1) Kila mfanyabiashara anayefanya biashara katika eneo la soko atawajibika- (a) kuweka eneo lake katika hali ya usafi wakati wote; na (b) kuzingatia kanuni za afya. (2) Mkuu wa soko kwa kushirikiana na Kamati ya wadau wa soko atasimamia usafi wa jumla wa soko siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Uingizaji wa bidhaa sokoni au gulioni - 32 Verify source ↗
(1) Mfanyabiashara anayekusudia kuingiza bidhaa
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa sokoni au gulioni lazima wazihifadhi kwenye makasha maalumu, na bidhaa zilizoharibika haziruhusiwi kuingizwa. Bidhaa zilizofungwa kwa majani lazima yaondolewe kwa gharama ya muingizaji.
32.-(1) Mfanyabiashara anayekusudia kuingiza bidhaa katika soko au gulio atapaswa kuhifadhi bidhaa husika kwenye makasha maalumu ya kusafirishia bidhaa. (2) Mkulima, mfanyabiashara, dalali au mtu mwingine hataingiza bidhaa zilizoharibika katika soko au gulio. 14 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) (3) Mtu atakayeingiza sokoni bidhaa zilizofungwa kwa majani atahakikisha kuwa majani hayo yanaondolewa kwa gharama zake. Biashara ya mifugo - 33 Verify source ↗
Mfanyabiashara anayeingiza mifugo katika soko,
AI-assisted research summary: Mwenye kuingiza mifugo sokoni, gulioloni au mnadani lazima apeleke mifugo hiyo katika sehemu maalumu iliyotengwa na Halmashauri kwa biashara ya mifugo.
33. Mfanyabiashara anayeingiza mifugo katika soko, gulio au mnada atapaswa kuingiza mifugo husika katika sehemu maalumu iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya biashara ya mifugo. Tahadhari ya moto Uteuzi wa Wakala Makosa
Part
sehemu maalumu iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya
- 34 Verify source ↗
Mtu hataruhusiwa kufanya shughuli inayohusisha
AI-assisted research summary: Mtu haruhusiwi kufanya shughuli inayohusisha matumizi ya moto isipokuwa akiwa na idhini ya maandishi ya Halmashauri.
34. Mtu hataruhusiwa kufanya shughuli inayohusisha matumizi ya moto isipokuwa kwa idhini ya maandishi ya Halmashauri. - 35 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kuingia mkataba na
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kufanya mkataba na wakala ili asimamie uendeshaji wa soko kwa niaba yake, na wakala anatakiwa kufanya hivyo kwa kufuata masharti ya Sheria Ndogo hii na mkataba wa uwakala.
35.-(1) Halmashauri inaweza kuingia mkataba na wakala kwa ajili ya kusimamia uendeshaji wa soko kwa niaba ya Halmashauri. (2) Wakala atasimamia shughuli za uendeshaji wa soko kwa kuzingatia masharti yaliyoainishwa katika Sheria Ndogo hii na masharti ya mkataba wa uwakala kati yake na Halmashauri. - 36 Verify source ↗
Mtu atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu anafanya kosa akitenda mojawapo ya vitendo vilivyoorodheshwa ndani ya soko, kama vile kubandika tangazo bila idhini ya Mkuu wa soko, kuharibu miundombinu, kutumia lugha ya matusi, kutupa taka ovyo, kuwasha moto kwenye maeneo yasiyoruhusiwa, au kutumia chumba cha biashara kinyume na mkataba au leseni.
36. Mtu atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atabandika au atabandua tangazo lolote bila ya idhini ya Mkuu wa soko; (b) ataharibu miundombinu ya soko; (c) atatumia lugha ya matusi ndani ya soko; (d) atafanya shughuli yeyote kwenye eneo ambalo haliruhusiwi au halijatengwa kwa shughuli hiyo; (e) atatupa taka ovyo au kutiririsha maji machafu; (f) atawasha moto maeneo yasiyoruhusiwa ndani ya soko; au (g) atatumia chumba cha biashara kwa matumizi mengine tofauti na yaliyoainishwa katika mkataba au leseni. Adhabu - 37 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa
AI-assisted research summary: Anyone convicted of an offence under this bylaw is liable to a fine, imprisonment, or both.
37. Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi miezi kumi na mbili au vyote. 15 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) Kufifilisha kosa Kufutwa kwa Sheria Ndogo TS Na. 525 la 2019 - 38 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii hadi shilingi 200,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari, yuko tayari kujaza fomu maalum, na analipa ada na ushuru unaodaiwa.
38. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu na kulipa ada na ushuru anaodaiwa. - 39 Verify source ↗
Sheria Ndogo za (Ushuru na Uendeshaji wa
AI-assisted research summary: These bylaws on market and auction operations for Ilala Municipal Council from 2019 are repealed.
39. Sheria Ndogo za (Ushuru na Uendeshaji wa Masoko na Magulio) za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za mwaka 2019 zimefutwa. 16 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) _____________ JEDWALI LA KWANZA _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5(1)) USHURU WA MASOKO i. Gharama za eneo katika Soko la Kisasa kwa mita za mraba SEHEMU A: SOKO LA KISASA Namba. Chanzo
Part
SEHEMU A: SOKO LA KISASA
- 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: The text lists market-related fees and charges, including monthly amounts for different floor levels and other market spaces.
5. Ghorofa ya chini (ground floor), ghorofa ya kati (mezzanine), ghorofa ya kwanza na ghorofa ya pili tatu hadi Ghorofa ya ghorofa ya nne Vizimba Maegesho Kodi ya huduma Ukubwa wa eneo (mita za mraba) Mita Moja ya mraba Mita Moja ya mraba Mita Moja ya mraba - Mita Moja ya mraba Ada (Shilingi) Muda wa malipo 15,000 Kwa mwezi 13,000 Kwa mwezi 15,000 Kwa mwezi 500 3,000 Kwa saa kwa gari Kwa mwezi ii. Ushuru wa Masoko ya Kisasa Namba. Chanzo Ushuru kwa siku (Shilingi) Ushuru kwa mwezi (Shilingi) 1 2 3 4 5 Mkungu wa ndizi Vizimba Vizimba vya kuku Vyumba vya Biashara au Duka au kioski au Bucha Namba 1 au Vibanda vya sokoni au Sehemu ya kuhifadhia Mizigo au Stoo au Ofisi za sokoni au Vyumba vya barafu a) Eneo lenye mita za mraba 0 – 9 b) Mita za mraba 10 – 15 c) Mita za mraba 16 -20 d) Mita za mraba 21– na kuendelea Kuingiza sokoni Gunia, Tenga, Robota la mitumba na Kiloba • Tafsiri ya Tenga
Part
Sehemu ya kuhifadhia Mizigo au Stoo au Ofisi
- 6 Verify source ↗
Mzigo mmoja wa miwa ni miwa 10
AI-assisted research summary: Mizani ya miwa: mzigo mmoja wa miwa ni miwa 10.
6. Mzigo mmoja wa miwa ni miwa 10 1,000 1,000 1,000 2,000 3,000 4,000 5,000 500 17 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) - 7 Verify source ↗
Masanduku ya mbao ya kubebea
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaonyesha maneno kuhusu masanduku ya mbao ya kubebea nyanya na gari linaloingiza mizigo yenye tani, lakini haionyeshi sheria au wajibu ulio wazi.
7. Masanduku ya mbao ya kubebea nyanya 6 Gari inayoingiza mizigo yenye tani: a. - 4 Verify source ↗
6.9
AI-assisted research summary: The provision lists market-related fees and charges for different goods, services, and stall or space uses.
4 – 6.9 d. 7 - na kuendelea Eneo la Matenga 7 8 9 10 11 12 13 14 15 Uuzaji wa vichwa na miguu ya ng’ombe, mbuzi na kondoo Mama lishe au Baba lishe Eneo la kutengenezea na kusuka Matenga Ada ya kutumia eneo la Machinjio ya Kuku kwa mtu Ada ya kuchinja kuku kwa kila kuku na wanyama wengine wa jamii ya ndege. Wachukuzi wa mizigo kwa mtu Maegesho katika soko Madalali Mafundi Nguo kwa Cherehani 1,000/= 2,000/= 3,000/= 4,000/= 500/=kwa mtu 1,000/= 500/= 100/= 300/= 500/= kwa saa 1,000/= kwa mtu 1,000/= kwa mtu SEHEMU B: SOKO LA KAWAIDA 70,000/= Namb a. Chanzo Ushuru kwa siku (Shilingi) Ushuru kwa mwezi (Shilingi) 1 3 4 5 6 7 Mkungu wa ndizi (a) Mkubwa (b) Mdogo Vizimba Wapanga chini Mabanda ya kuku Vyumba vya Biashara au Duka au kioski au Bucha Namba 1 au Vibanda vya sokoni au Sehemu ya kuhifadhia Mizigo au Stoo au Ofisi za sokoni au Vyumba vya barafu a) Eneo lenye mita za mraba 0 – 9 b) Mita za mraba 10 – 15 c) Mita za mraba 16 – 20 d) Mita za mraba 21 na kuendelea. Kuingiza sokoni Gunia, Tenga, Robota la mitumba na Kiloba • Tafsiri ya Tenga - 5 Verify source ↗
Tenga la maboga 15
AI-assisted research summary: The text lists amounts under Section 5, but it does not clearly state a rule on its own.
5. Tenga la maboga 15 18 500/= 300/= 500/= 300/= 500/= 1,500/= 2,500/= 3,500/= 4,500/= 500/= Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) - 7 Verify source ↗
Masanduku ya mbao ya kubebea nyanya
AI-assisted research summary: The text gives a heading about wooden crates for carrying tomatoes, followed by a fragment about a vehicle carrying cargo measured in tons.
7. Masanduku ya mbao ya kubebea nyanya Gari inayoingiza mizigo yenye tani: a. - 4 Verify source ↗
6.9
AI-assisted research summary: This provision lists market and related local charges for different activities and stalls.
4 – 6.9 d. 7 – na kuendelea Uuzaji wa vichwa na miguu ya ng’ombe, mbuzi na kondoo. Mama lishe au Baba lishe Eneo la kutengenezea na kusuka Matenga Ada ya kutumia eneo la Machinjio ya Kuku ya kuku kwa mtu Ushuru wa kuchinja kuku kwa kila kuku nawanyama wengine wa jamii ya ndege. 8 9 10 11 12 13 500/= 1,500/= 2,500/= 3,500/= 500/= kwa mtu 500/= 500/= 100/= 14 Wachukuzi wa mizigo walipe kwa mtu 15 16 Maegesho ya Sokoni Madalali Magulio Mafundi Nguo kwa Cherehani 17 18 19 Wakaanga kuku, samaki na dagaa. 300/= 500/= kwa saa 1,000/= kwa mtu 500/= kwa mtu 500/= kwa mtu 500/= kwa mtu SEHEMU C: SOKO NJE YA MJI 50,000/= Namba. Chanzo Ushuru Kwa siku (Shilingi) Ushuru kwa mwezi (Shilingi) 500/= 500/= 300/= 500/= 1 2 3 4 5 6 Mkungu wa ndizi Vizimba Wapanga chini Vizimba vya kuku Vyumba vya Biashara au Duka au Bucha Namba 1 au Vibanda vya sokoni au Sehemu ya kuhifadhia Mizigo au Stoo au Ofisi za sokoni au Vyumba vya barafu a. Eneo lenye mita za mraba 0-9 b. Mita za mraba 10-15 c. Mita za mraba 16-20 d. Mita za mraba 21- na kuendelea. Kuingiza sokoni Gunia, Tenga, Robota la mitumba, boksi la ndizi mbivu, boksi la nyanya na Kiloba • Tafsiri ya Tenga
Part
SEHEMU C: SOKO NJE YA MJI
- 4 Verify source ↗
Tenga la Staferi 25
AI-assisted research summary: This section lists several monetary amounts/fees, including 25 500/=, 20,000/=, 30,000/=, 45,000/=, and 60,000/=.
4. Tenga la Staferi 25 500/= 19 20,000/= 30,000/= 45,000/= 60,000/= Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) - 7 Verify source ↗
Masanduku ya mbao ya kubebea
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaorodhesha ada mbalimbali za soko, mnada, machinjio, maegesho, na shughuli nyingine, pamoja na viwango vya shilingi kwa kila kipengele.
7. Masanduku ya mbao ya kubebea nyanya 50,000/= 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 Uuzaji wa vichwa na miguu ya ng’ombe, mbuzi na kondoo Mama lishe au Baba lishe Eneo la Matenga Ada ya kutumia Eneo la Machinjio ya Kuku kwa mtu Ada ya kuchinja kuku kwa kila kuku na wanyama wengine wa jamii ya ndege. Wachukuzi wa mizigo walipe kwa mtu Maegesho ya sokoni Madalali Magulio Mafundi Nguo kwa Cherehani Wakaanga kuku, samaki na dagaa 500/= kwa mtu 500/= 500/= 100/= 300/= 500/= kwa saa 1000/= kwa mtu 500/= kwa mtu 500/= kwa mtu 500/= kwa mtu SEHEMU D: ADA YA MIFUGO KATIKA MNADA Namba Aina ya Mnyama 1 2 3 4 Ada ya soko au mnada wa wanyama wakubwa (ng’ombe, punda) kwa kila mnyama Ada ya soko au mnada wa wanyama wadogo (mbuzi au kondoo) kwa kila mnyama Tozo ya dalali (garagaja) katika minada ya mifugo kwa mwezi Ada ya ukaguzi na kibali cha usafirishaji mifugo Kiwango cha Ada (Shilingi) 1,000 500 200,000 Kwa mujibu wa kanuni, miongozo itakayotolewa na Serikali 20 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) __________________ JEDWALI LA PILI ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni za 23(1) na 30)) KIBALI CHA KUTUMIA SOKO (Nakala Tatu-Halmashauri, Uongozi wa wadau, Mtumiaji) Sehemu ya Kwanza: Ijazwe na Mwombaji na Mkuu wa Soko
Part
Sehemu ya Kwanza: Ijazwe na Mwombaji na Mkuu wa Soko
- 1 Verify source ↗
Jina la Mwombaji …………………………………………………………
AI-assisted research summary: Hii ni kichwa cha sehemu kinachoonyesha kuwa fomu inahusu jina la mwombaji.
1. Jina la Mwombaji ………………………………………………………….......... - 2 Verify source ↗
Mahali unapoishi /Utambulisho
AI-assisted research summary: Fomu hii inaomba taarifa za makazi na utambulisho, ikiwemo mtaa, kata, wilaya, mkoa, anuani ya makazi/posti kodi, namba ya simu, sanduku la barua, na namba ya kitambulisho cha NIDA.
2. Mahali unapoishi /Utambulisho Mtaa……………………Kata.………………Wilaya………Mkoa…………. Anuani ya Makazi/posti kodi……………………..Namba ya simu………… Sanduku la Barua…………………………………………………................. Namba ya Kitambulisho cha NIDA…………………………………………. - 3 Verify source ↗
Aina ya Biashara /Huduma utakayofanya ………………………………………
AI-assisted research summary: Section heading for the type of business or service to be carried out.
3. Aina ya Biashara /Huduma utakayofanya ……………………………………… - 4 Verify source ↗
Jina la Soko na Kitengo ambacho kibali hicho kitatumika ……………………
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kina kichwa kinachohusu jina la soko na kitengo ambacho kibali hicho kitatumika.
4. Jina la Soko na Kitengo ambacho kibali hicho kitatumika …………………….. - 5 Verify source ↗
Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe…………………hadi tarehe………………
AI-assisted research summary: The permit period runs from one date to another date.
5. Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe…………………hadi tarehe……………….. - 6 Verify source ↗
Uthibitisho
AI-assisted research summary: Mwombaji anasema taarifa alizotoa ni za ukweli na sahihi, na anakubali kutii sheria ndogo za masoko na kanuni za soko.
6. Uthibitisho: Nakiri kuwa taarifa zote nilizotoa ni za ukweli na sahihi. Nakubali kutii na kuzingatia Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Kanuni za Uendeshaji wa Soko. Jina la Mwombaji………………….. …………… Saini ya Mwombaji………………… ……………………… Tarehe ……………………………… Tarehe……………………… Mkuu wa Soko Saini Sehemu ya Pili: Ijazwe na Uongozi wa Kamati ya Wadau wa Soko
Part
Sehemu ya Pili: Ijazwe na Uongozi wa Kamati ya Wadau wa Soko
- 7 Verify source ↗
Tarehe ya kikao kilichoidhinisha kibali…………….…… Muhtasari Na..…………
AI-assisted research summary: A section heading about the date of the meeting that approved the permit, with a summary number.
7. Tarehe ya kikao kilichoidhinisha kibali…………….…… Muhtasari Na..………… - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Sehemu hii ina fomu ya kukiri kosa na kulipa ada/ushuru pamoja na faini ya kufifilisha kosa mbele ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.
8. Mwenyekiti wa Kitengo……………………. Saini Imethibitishwa na kusajiliwa na: Katibu wa Kitengo……………….. Saini ……………………………... ………………………………. Tarehe …………………………… Tarehe……………………………… 21 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) Katibu wa Soko………………….. Mwenyekiti wa Soko……………………. Saini …………………………………… Tarehe …………………………………. Tarehe……………………………… Saini ……………………………… (Tafadhali ambatanisha nakala ya kitambulisho cha NIDA, Barua ya utambulisho kutoka kwa Mjumbe wa Mtaa unapoishi, Barua ya Utambulisho kutoka kwa Serikali ya Mtaa unapoishi, Picha Passport size nne) 22 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) _____________ JEDWALI LA TATU _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 38) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kwamba mnamo tarehe …… ya Mwezi ………. Mwaka ……….…… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni …… ya Sheria Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, niko tayari kulipa kiasi cha shilingi..................... cha ada au ushuru ninayodaiwa pamoja na kiasi cha shilingi............................cha faini ya kufifilisha kosa. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………….. MBELE YA MKURUGENZI: Jina:……………………………………..……………………...... Saini………………………….…………………………...……… Wadhifa…………………………………………………………. Tarehe……………………………………………………………. 23 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Saalam Tangazo la Serikali Na.1015 (Linaendelea.) Lakiri ya Jiji la Dar es Salaam imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutao wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam uliofanyika tarehe 6/3/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- JOMAARY MRISHO SATURA, Mkurugenzi wa Jiji, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam MHE. OMARY KUMBILAMOTO, Msahiki meya, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Agosti, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 24
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in