AI-assisted research summary: Mwombaji anaweza kujenga kituo cha mafuta tu akifuata masharti mengi ya usalama, viwango, vipimo, na alama za tahadhari.
3. Mwombaji anapewa Kibali cha Ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Mafuta katika Kiwanja Na. 6, Kitalu “A”, Eneo la Madiira, Kijiji cha Sing`isi, Kata ya Sing`isi, Halmashauri ya Meru, Mkoa wa Arusha kwa masharti yafuatayo: (a) kituo cha mafuta kitajengwa kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania Na. TZS 1115:2009 na TZS 1079:2008; (b) uangalifu wa kutosha utazingatiwa wakati wa uchimbaji na uwekaji wa matenki ya mafuta chini ya ardhi; 1 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Mafuta kwa Olasiti Investment Co. Ltd Tangazo la Serikali Na. 1027 (Linaendelea) unapaswa (c) mpangilio wa kituo cha mafuta kwa matumizi binafsi umbali wa kiusalama kwa mujibu wa viwango vya la Viwango Tanzania Na. TZS Shirika 1079:2008; kukidhi (d) ufukiaji wa matenki ya kuhifadhi mafuta pamoja na mabomba chini ya ardhi ufanywe kwa namna ambayo italinda usalama wa vifaa hivyo ikiwemo kupata kutu; (e) matenki ya kuhifadhia mafuta, pampu na mabomba husika pamoja na vifaa vyote vinavyounganishwa pamoja navyo vinapaswa kufungwa vizuri ili kuzuia uvujaji wowote wa mafuta; (f) matenki ya kuhifadhia mafuta na pampu ya mafuta inapaswa kufanyiwa uhakiki wa usahihi wa vipimo na Wakala wa Vipimo Tanzania aliyeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Tanzania; Sura ya 340 (g) eneo la mbele la kituo cha mafuta na kuzunguka eneo la pampu litasakafiwa kwa zege madhubuti lisiloweza kupenyeza mafuta na kuhakikisha kuwepo kwa mitaro ambayo itakusanya maji na mafuta wakati wa mvua na kuyaelekeza kwenye chemba ya kutenganisha maji na mafuta; (h) kuweka swichi ya dharura katika eneo linaloonekana na kufikika kirahisi ili wakati wa dharura iwe ni rahisi kuzima umeme wa kituo kizima; (i) kuhakikisha kuwepo na vyoo vya kutosha vya wanawake na wanaume vilivyo safi wakati wote; (j) kuhakikisha usalama zinawekwa sehemu ya kuingia na ya kutoka kwenye kituo cha mafuta na eneo la pampu zikijumuisha “zima injini”, “zima simu” na “usivute sigara”; alama kuwa za (k) kuhakikisha kila tenki la kuhifadhia mafuta linaunganishwa na bomba la kupumulia lenye 2 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Mafuta kwa Olasiti Investment Co. Ltd Tangazo la Serikali Na. 1027 (Linaendelea) urefu wa usiopungua mita 3.6 kutoka ardhini, bomba hilo linatakiwa kuwa angalau mita 1.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja na angalau mita 4 kutoka kwenye dirisha au kifaa chochote cha kuvuta hewa ikiwemo kiyoyozi; (l) pampu za kuuza mafuta na sehemu ya kushushia mafuta zinatakiwa kuwa angalau mita 4.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja, angalau mita 8 kutoka kifaa chochote ambacho kinaweza kuwa chanzo cha moto ikiwemo jokofu na angalau mita 10 kutoka kwenye nyaya za kusafirishia umeme; (m) kuhakikisha kila pampu ya mafuta inalindwa na kizuizi na kizuizi kitapaswa kuwa na urefu wa mita moja kutoka juu ya ardhi; (n) mifumo ya upakuaji wa mafuta kwenye kituo cha mafuta itapaswa kujengwa kwa kufuata kanuni na taratibu zinazokubalika kwenye sekta ya mafuta; (o) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na paa linalofunika eneo lote lenye pampu za linajengwa kwa mujibu wa mafuta na viwango na taratibu zinazokubalika kwenye sekta ya mafuta; na (p) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na bango la bei ambalo litawekwa mahala ambapo panaonekana kirahisi ili wateja waweze kuona bei za mafuta kabla ya kuingia kituoni. Ukomo wa kibali cha ujenzi