Kanuni za Mawakili na Waendesha Mashtaka katika Mahakama za Mwanzo za mwaka 2022
These regulations are called the Advocates and Prosecutors in Primary Courts Regulations, 2022.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Mawakili na Waendesha Mashtaka katika Mahakama za Mwanzo za mwaka 2022
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
These regulations are called the Advocates and Prosecutors in Primary Courts Regulations, 2022. Kanuni hizi zinahusu usimamizi wa mawakili na waendesha mashtaka katika mahakama za mwanzo. This section defines key terms used in the rules. Cases involving lawyers and prosecutors must be handled according to the applicable court procedure rules. Wakili anayetaka kumwakilisha mhusika lazima awasilishe taarifa na ahadi ya maandishi kwa mahakama; mahakama pia ithibitishe uajiri, na wahusika wa shauri wapate notisi kwa wakati unaofaa kabla ya mwonekano wa kwanza.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Mawakili na Waendesha Mashtaka katika Mahakama za Mwanzo za mwaka 2022
Showing 9 of 9
- 1
AI-assisted research summary: These regulations are called the Advocates and Prosecutors in Primary Courts Regulations, 2022.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Mawakili na Waendesha Mashtaka katika Mahakama za Mwanzo za mwaka 2022. Matumizi - 2
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinahusu usimamizi wa mawakili na waendesha mashtaka katika mahakama za mwanzo.
2. Kanuni hizi zitatumika kusimamia mawakili na waendesha mashtaka katika mahakama za mwanzo. Tafsiri Sura ya 342 Sura ya 430 - 3 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the rules.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vingenevyo- "wakili" maana yake ni kama ilivyotafsiriwa chini ya kifungu cha 2 cha Sheria ya Mawakili na inajumuisha watu waliotajwa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria hiyo; "mahakama" maana yake ni mahakama ya mwanzo; “Mkurugenzi wa Mashtaka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa chini ya Sheria ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka; "hakimu" maana yake ni hakimu mkazi anayesilikiza mashauri katika mahakama; na Sura ya 430 "mwendesha mashtaka" maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. 2 Kanuni za Mawakili na Waendesha Mashtaka Katika Mahakama za Mwanzo Tangazo La Serikali 168 (Linaendelea) Desturi na taratibu Notisi na ahadi ya uwakilishi SEHEMU YA PILI UANZISHAJI, UWAKILISHI NA UTARATIBU
Part
SEHEMU YA PILI
- 4
AI-assisted research summary: Cases involving lawyers and prosecutors must be handled according to the applicable court procedure rules.
4. Namna ya kufungua mashauri, desturi na taratibu za mahakama katika masuala yanayowahusisha mawakili na waendesha mashtaka zitakuwa kwa mujibu wa sheria taratibu zinazotumika katika zinazoongoza desturi na mahakama za mwanzo. - 5 Verify source ↗
Desturi na taratibu
AI-assisted research summary: Wakili anayetaka kumwakilisha mhusika lazima awasilishe taarifa na ahadi ya maandishi kwa mahakama; mahakama pia ithibitishe uajiri, na wahusika wa shauri wapate notisi kwa wakati unaofaa kabla ya mwonekano wa kwanza.
5.-(1) Wakili anayekusudia kumwakilisha mhusika yeyote katika mahakama atatoa taarifa na kuweka ahadi kwa maandishi mahakamani kwamba, ana maelekezo kamili na atahudhuria mahakamani kila mara shauri litakapotajwa au kusikilizwa. (2) Baada ya kupokea taarifa na ahadi ya wakili chini ya kanuni ndogo ya (1), mahakama itajiridhisha iwapo wakili huyo ameajiriwa kumuwakilisha mhusika. (3) Notisi na ahadi chini ya kanuni ndogo ya (1), ilivyoanishwa vitakuwa kadiri itakavyowezekana, kama katika Fomu A kwenye Jedwali la Kanuni hizi. (4) Iwapo Mkurugenzi wa Mashtaka au mtu yeyote aliye chini yake ataona kuwa kuna ulazima wa shauri kuendeshwa na mwendesha mashtaka, ataijulisha na kuiahidi mahakama kwa maandishi kuwa, mwendesha mashtaka atahudhuria mahakamani wakati wowote wa kuendesha shauri hilo kama inavyoanishwa katika Fomu B kwenye Jedwali la Kanuni hizi. (5) Wahusika wote katika shauri watapewa au kujulishwa juu ya notisi chini ya kanuni hii ndani ya wakati unaofaa kabla ya wakili au mwendesha mashtaka kuhudhuria kwa mara ya kwanza mahakamani. SEHEMU YA TATU MASHARTI YA JUMLA Uahirishaji wa mashauri
Part
SEHEMU YA TATU
- 6
AI-assisted research summary: Hearing starts and continues until all witnesses present that day testify, unless the court decides to adjourn.
6.-(1) Usikilizaji wa shauri utakapoanza, utaendelea hadi mashahidi wote waliohudhuria mahakamani siku hiyo watakapotoa ushahidi, sababu zitakazoandikwa katika mwenendo wa shauri, mahakama isipokuwa kama, kwa 3 Kanuni za Mawakili na Waendesha Mashtaka Katika Mahakama za Mwanzo Tangazo La Serikali 168 (Linaendelea) inaona kuna umuhimu kuahirisha usikilizaji wa shauri hilo hadi siku nyingine. (2) Wakili au mwendesha mashtaka kuhudhuria katika mahakama nyingine au baraza haitakuwa sababu ya kuahirisha shauri. (3) Endapo wakili au mwendesha mashtaka ameshindwa kuhudhuria mahakamani kwa sababu ya kuhudhuria kwake katika mahakama nyingine au baraza, mahakama itamtaka mhusika kuendelea na shauri yeye mwenyewe na akikataa kuendelea au kama hayupo, mahakama itachukulia kwamba mhusika huyo ameshindwa kuhudhuria mahakamani na madhara ya kutokuhudhuria yatatumika. (4) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2), endapo wakili au mwendesha mashtaka hajahudhuria mahakamani au ameomba ahirisho kwa sababu ya ugonjwa au sababu nyingine yoyote, mahakama haitakubali ombi hilo isipokuwa kama imejiridhisha kuwa wakili au mwendesha mashtaka ni mgonjwa au kwa sababu nyingine yoyote, hawezi kuhudhuria, amehudhuria, hawezi kuendelea, na mhusika anayeomba ahirisho hawezi kuendelea mwenyewe kwa sababu zinazofaa na asingeweza kuajiri wakili au kupata mwendesha mashtaka mwingine ndani ya muda. ikiwa au Mavazi T S Na. 118 la Mwaka 2018 Waraka wa utambulish o - 7
AI-assisted research summary: Sheria za mavazi ya uwakili zinatumika kwa mawakili na wanaoendesha mashtaka wanapohudhuria Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za Wilaya.
7. Masharti ya Kanuni za Mwenendo na Miiko ya Kazi ya mawakili kuhusu mavazi ya Uwakili wanapohudhuria mbele ya Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za Wilaya yatatumika kwa mawakili na wanaoendesha mashtaka katika mahakama. - 8
AI-assisted research summary: Wakili au mwendesha mashtaka lazima akitakiwa na mahakama aonyeshe waraka halali au ushahidi mwingine unaothibitisha kuwa anaweza kuhudumu katika wadhifa huo.
8.-(1) Wakili au mwendesha mashtaka atawajibika kuwasilisha mbele ya mahakama waraka halali au ushahidi mwingine wowote unaomruhusu kuhudumu kama wakili au mwendesha mashtaka, iwapo utahitajika kufanya hivyo. (2) Wakili au mwendesha mashtaka atakayeshindwa kutekeleza masharti ya kanuni ndogo ya (1) hatakuwa na haki ya kusikilizwa, isipokuwa kama mahakama, kwa sababu itakazoona zinafaa na kuandikwa katika mwenendo wa shauri, itaamua vinginevyo. 4 Kanuni za Mawakili na Waendesha Mashtaka Katika Mahakama za Mwanzo Tangazo La Serikali 168 (Linaendelea) Ukadiriaji gharama TS Na. 263 la Mwaka 2015 - 9 Verify source ↗
Uahirishaji wa mashauri
AI-assisted research summary: The provision sets how court proceeding costs are assessed and assigns the costs assessor role to certain magistrates, and it lets an unhappy party apply for review in the district court.
9.-(1) Ukadiriaji wa gharama za uendeshaji mashauri utakuwa kama ilivyoainishwa kati ka Amri ya Ujira wa Mawakili. (2) Hakimu mfawidhi wa mahakama atakuwa ofisa mkadiriaji gharama chini ya masharti ya Amri ya Ujira wa Mawakili. (3) Endapo hakimu mfawidhi siyo hakimu mkazi, hakimu mkazi yeyote aliye na cheo kikubwa zaidi katika mahakama hiyo atakuwa ofisa mkadiriaji gharama. (4) Mhusika yeyote ambaye hajaridhika na uamuzi wa ofisa mkadiriaji gharama, anaweza kuwasilisha maombi ya mapitio katika mahakama ya wilaya. 5 Kanuni za Mawakili na Waendesha Mashtaka Katika Mahakama za Mwanzo Tangazo La Serikali 168 (Linaendelea) ______ JEDWALI ______ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5(3) na (4)) FOMU A Katika Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya……………………………….………… Kituo cha ……………………………………….………… *Shauri la jinai/madai/ ndoa/ mirathi/maombi Na. …………………………..……. ………………………………………… (mlalamikaji/mdai/mwombaji/mrufani) Dhidi ya …………………………………………………. (mshtakiwa/mdaiwa/mjibu maombi/mrufaniwa) Au Shauri la Rufaa Na. ……………………………..…. (Kutoka Baraza la Kata la……………..katika shauri la madai/jinai Na…la 20…) …………………………………………. mrufani Dhidi ya …………………………………………………. Mrufaniwa NOTISI YA UWAKILISHI NA AHADI YA KUHUDHURIA MAHAKAMANI Mimi…………………, wakili wa mahakama kuu na mahakama zilizo chini yake, mwenye namba ya usajili …….. na mwenye leseni hai ya uwakili iliyotolewa tarehe……mwezi ….. mwaka 20……, ninaijulisha mahakama hii kwamba, nimeajiriwa kama wakili katika shauri hili na nina maelekezo kamili ya (jina)……...mlalamikaji/mshtakiwa/mwombaji/mrufani/mjibu maombi/ katika shauri/ shauri tarajiwa la jinai/madai/mirathi/ndoa . Pia, ninaiahidi Mahakama kwamba nitahudhuria mahakamani kumuwakilisha ………………… katika tarehe itakayopangwa. Saini…………………………... Tarehe............mwezi ………………mwaka 20……. Futa isiyohitajika 6 Kanuni za Mawakili na Waendesha Mashtaka Katika Mahakama za Mwanzo Tangazo La Serikali 168 (Linaendelea) FOMU B Katika Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya…………………………………….………… Kituo cha ………………………………………….………………. Shuri la jinai/rufaa/maombi Na. ………………………………..…. ……………….………………………….……………. (mlalamikaji/mrufani) Dhidi ya …………………………………….………. (mshtakiwa/mjibu maombi/mrufaniwa) Au Shauri la Rufaa Na. …………………………………..……. (Kutoka Baraza la Kata la………katika shauri la Madai/Jinai Na…la 20…) ……………………………………..……………………. Mrufani Dhidi ya …………………………………….……………………. Mrufaniwa NOTISI YA KUENDESHA SHAURI NA AHADI YA KUHUDHURIA MAHAKAMANI Mimi …………………………. Mkurugenzi wa Mashtaka/Mkuu wa Mashtaka wa mkoa/wilaya …………… ninaiarifu mahakama hii kwamba, shauri la jinai/maombi/rufaa Na. ……………. la/ya mwaka ……… litaendeshwa na mwendesha mashtaka. Pia, ninaiahidi mahakama kwamba nitahakikisha kwamba mwendesha mashtaka anahudhuria mlalamikaji/mwombaji/mjibu kumwakilisha maombi/mrufani/mrufaniwa katika tarehe itakayopangwa. Saini………... mahakamani Mkurugenzi wa Mashtaka/Wakili wa Serikali/Mwendesha Mashtaka wa Serikali Mfawidhi …………………………………………………………wilaya/mkoa Tarehe...........mwezi ..………………mwaka 20…… Futa isiyohitajika Dar es Salaam, 27 Februari, 2023 IBRAHIM HAMIS JUMA, Jaji Mkuu 7
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Mawakili na Waendesha Mashtaka katika Mahakama za Mwanzo za mwaka 2022
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in