Tanzania Regulation

Parliament of Tanzania

Kanuni za Uanzishaji na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli za Mwaka 2023

This section names the rules as the 2023 Regulations for the Establishment and Operation of Navigation Equipment for Ships. These regulations apply to implementation of rule 13 of Chapter Five of the Security Agreement…

application of regulationscertificationcomplaintsconsultationcost recoverydesignationexemptionsfee collectionfeesfees and chargesfees and finesinspection authorizationBusiness registrationmarine navigationmarine navigation servicesmarine noticesmarine operationsmaritime infrastructuremaritime navigationmaritime navigation aidsmaritime servicesmaritime transportnavigationnavigation aidsnavigation equipmentnavigation safetyoperational obstructionoverpayment claimsport chargesport clearanceport feesport operationsport servicesregulatory namingregulatory reviewregulatory supervisionripoti za udhibitiservice authorizationservice provider dutiesservice regulationshippingshipping operationstraining accreditationuangalizi wa masharti ya udhibitivessel departurevessel measurementvessel navigation trainingvessel operationswreck marking

Publicly available, excluded from search-engine indexing

This page remains available for direct research for the following reasons:

  • The record does not meet this release's canonical indexing criteria. (market-indexing-disabled)
  • The record does not meet this release's canonical indexing criteria. (emergency-noindex)

Professional statute overview

Enactment structure, operative effect and source provenance

Official source

01

Purpose and legislative effect

“This section names the rules as the 2023 Regulations for the Establishment and Operation of Navigation Equipment for Ships.”

This section names the rules as the 2023 Regulations for the Establishment and Operation of Navigation Equipment for Ships. These regulations apply to implementation of rule 13 of Chapter Five of the Security Agreement and to the maritime zones defined in the relevant sea-boundaries law, but they do not apply to certain government-owned vessels that do not carry cargo or passengers for hire. This section defines the main terms used in the Regulations. Msajili anaweza kuainisha vifaa vya kuongozea meli kwa Notisi ya Usafiri Majini, na Shirika pamoja na watoa huduma wa vifaa hivyo lazima wazingatie Mfumo A wa maboya wa IALA katika uundaji, uanzishaji na usimamizi kwenye maji ya Tanzania. Msajili must supervise navigation aids generally by following the regulations, IALA recommendations and guidance, and Circular No. 107, and must advise the Minister on navigation aids.

02

How the instrument operates

  1. 01

    Start with the recorded version

    Legal dates not recorded. The date shown identifies this source expression and should not be treated as proof that no later change exists.

  2. 02

    Locate the controlling provision

    Use the provision map, part headings and full-text filter to move from the broad subject to the exact legal language.

  3. 03

    Read conditions and exceptions together

    Keep subsections, definitions, provisos and cross-references in context before drawing a legal conclusion.

  4. 04

    Verify currency and official wording

    Confirm later legislation, commencement notices and corrections with the official publisher before advice, filing or reliance.

03

Research entry points

Selected provisions across the instrument. Open any row to continue with the exact stored text.

Jina

This section names the rules as the 2023 Regulations for the Establishment and Operation of Navigation Equipment for Ships.

Section 1

Ukusanyaji wa ada kwa vifaa vya kuongozea meli

Ada za vifaa vya kuongozea meli lazima zikusanywe kwa meli zinazoingia au kutoka bandarini, na afisa sahihi anaweza kuomba nyaraka, uwepo wa mhusika, na ukaguzi wa meli ili kuthibitisha tani jumla.

Section 16

Makosa na adhabu

This section makes several acts involving navigation aids or pilotage services an offence and sets fines and possible prison terms.

Section 23

04

Source and current-law status

Source record view

Source record from oagmis.oag.go.tz · Legal dates not recorded

Verify current force

The source record does not state a definitive current-law status. Check the official publisher and later amendments before relying on this text.

Source-indexed provision map

Sections and provisions

Search by section, heading, part or exact legal wording. Every result remains linked to the stored source record.

Showing 30 of 30 provisions

Provision 29Offence
§ 1JinaProvision

This section names the rules as the 2023 Regulations for the Establishment and Operation of Navigation Equipment for Ships.

1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Uanzishaji na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli za Mwaka 2023.
§ 2MatumiziProvision

These regulations apply to implementation of rule 13 of Chapter Five of the Security Agreement and to the maritime zones defined in the relevant sea-boundaries law, but they do not apply to certain government-owned vessels that do not carry cargo or passengers for hire.

2.-(1) Kanuni hizi zitatumika- (a) kuhusiana na utekelezaji wa kanuni ya 13 ya Sura ya Tano ya Mkataba wa Usalama; na (b) kwa kanda za bahari zilizoainishwa katika Sheria ya Mipaka ya Bahari na Eneo la Ukanda wa Biashara. (2) Bila kuathiri ujumla wa kanuni ndogo ya (1), Kanuni hizi hazitatumika katika chombo kinachomilikiwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano au Serikali ya nchi nyingine, ambacho hakibebi mizigo au abiria kwa gharama au nauli inayotokana na malipo ya ada ya vifaa vya uongozaji meli. Tafsiri
§ 3TafsiriProvision

This section defines the main terms used in the Regulations.

3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada za vifaa vya kuongozea meli” maana yake ni ada “afisa sahihi” inayotozwa chini ya kanuni ya 16; kuhusiana na majukumu yoyote yatakayotekelezwa chini ya Kanuni hizi, maana yake ni afisa aliyeteuliwa kutekeleza kazi fulani au majukumu pale anapojihusisha na utekelezaji wa kazi au majukumu hayo na inajumuisha mtu 4 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Suara ya 166 yeyote aliyeteuliwa na Waziri au Shirika kutekeleza majukumu ya afisa sahihi chini ya Kanuni hizi; “bandari” ina maana iliyotolewa chini ya Sheria ya Bandari; “chombo” inajumuisha meli yoyote, boti yoyote, jahazi, kivuko au chombo kingine cha maelezo mengine kinachotumika katika safari kwenye maji; “huduma ya kuongoza meli” maana yake ni huduma zinazotolewa chini ya Kanuni hizi ili kuboresha usalama na ufanisi wa huduma za kuongoza meli na kutunza mazingira; “IALA” maana yake ni Jumuiya ya Kimataifa ya Vyombo vya Kuongozea Meli na Mamlaka ya Taa za Kuongoza Meli; “IMO” maana yake ni Shirika la Bahari Duniani; “kifaa cha kuongozea meli” maana yake ni kifaa, mfumo au huduma, nje ya vyombo, kilichoundwa na kuendeshwa kuwezesha usalama na ufanisi wa uongozaji wa vyombo binafsi kwenye maji, lakini hakitatafsiriwa kujumuisha rejea ya huduma za kuongozea meli, isipokuwa kama imeainishwa vinginevyo; “maji ya Tanzania” maana yake ni bahari au maji mengine ndani ya mipaka ya bahari ya nchi ya Tanzania kuelekea baharini; “meli” inajumuisha vyombo vinavyosafiri majini; “Mkataba wa Usalama” maana yake ni Mkataba wa Kimataifa wa Usalama wa Maisha Baharini wa mwaka 1974 na Itifaki zake za 1978 na 1982, pamoja kama yatakavyotumika Tanzania; na marekebisho yake, “mmiliki” maana yake ni mmiliki wa chombo ikijumuisha mmiliki aliyesajiliwa, mtu ambaye anamiliki hisa za meli, mkodishaji, meneja na mwendeshaji wa chombo; “mnara wa taa za kuongoza meli” maana yake ni kifaa cha kuongozea meli kilichoainishwa chini ya kanuni ya 25; “Msajili” maana yake ni Msajili aliyeteuliwa chini ya 5 Sura ya 415 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Sura ya 165 Sura ya 415 kifungu cha 31 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania; “mtoa huduma wa kifaa cha kuongozea meli” maana yake ni mtu anayeendesha bandari, kituo cha mzigo, wanamaji, jeti, mashamba ya mazao ya majini, au miundombinu mingine majini; “mtoa huduma ya kuongoza meli” maana yake ni mtoa huduma wa kuongoza meli aliyeidhinishwa chini ya kanuni ya 7; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Usafiri Majini; “Shirika” maana yake ni Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania lililoanzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania; “taasisi ya mafunzo yenye ithibati" maana yake ni taasisi yoyote ambayo imepewa ithibati na Shirika chini ya kanuni ya 16; “upatikanaji” maana yake ni uwezekano kuwa kifaa cha kuongozea chombo au mfumo wa vifaa vya kuongezea meli, unafanya shughuli zake maalum kwa muda wowote uliopangwa, unaotajwa kama asilimia ya jumla ya muda wote; na “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na usafirishaji majini. lakini (2) Maneno na maelezo yaliyotumika hayajatolewa tafsiri katika Kanuni hizi, na yametolewa tafsiri katika Sheria, yatakuwa na maana sawa na iliyotolewa katika Sheria. SEHEMU YA PILI MAMLAKA NA WAJIBU WA MSAJILI KWENYE VIFAA VYA KUONGOZEA MELI Mamlaka ya kuainisha vifaa vya kuongozea meli

Part

SEHEMU YA PILI

§ 4Mamlaka ya kuainisha vifaa vya kuongozea meliProvision

Msajili anaweza kuainisha vifaa vya kuongozea meli kwa Notisi ya Usafiri Majini, na Shirika pamoja na watoa huduma wa vifaa hivyo lazima wazingatie Mfumo A wa maboya wa IALA katika uundaji, uanzishaji na usimamizi kwenye maji ya Tanzania.

4.-(1) Msajili anaweza, kwa Notisi ya Usafiri Majini, kuainisha vifaa vya kuongozea meli. (2) Shirika na mtoa huduma yeyote wa vifaa vya kuongozea meli atazingatia mfumo A wa maboya wa IALA katika uundaji, uanzishaji na usimamizi wa vifaa vya kuongozea meli kwenye maji ya Tanzania. (3) Vifaa vikuu vya kuongozea meli ni maboya na bikoni ikijumuisha- 6 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) (a) mnara wa taa ya kuongozea meli; (b) alama zinazofanana zinazoainisha njia za meli; (c) alama zinazong’aa kuonesha sehemu salama za maji katika dira; (d) hatari zilizoainishwa; (e) maji salama na alama maalum; (f) alama za kuainisha michezo ya majini, mashamba ya mazao ya majini na maeneo mengine yaliyotengwa; (g) alama zinazoonekana zinazotumia Mfumo wa Utambuzi wa Kielektroniki; (h) alama za tahadhari na ishara ikijumuisha ukomo wa mwendo, alama za nyaya, maeneo ya hifadhi baharini; (i) redio, ishara za ukungu au vifaa vingine ambavyo havijabebwa melini; na (j) majengo yote, nanga na vifaa vingine vinavyohusiana. (4) Vifaa vya kuongozea meli vinaweza kumilikiwa na kutunzwa na Shirika au mtoa huduma yeyote wa vifaa vya kuongozea meli.
§ 56. Ushauri kuhusiana na masuala ya vifaa vya kuongozea meliProvision

Msajili must supervise navigation aids generally by following the regulations, IALA recommendations and guidance, and Circular No. 107, and must advise the Minister on navigation aids.

5.-(1) Kwa mujibu wa kifungu cha 213 cha Sheria, Msajili anatakiwa, wakati anatekeleza usimamizi wa ujumla wa vifaa vya kuongozea meli, atazingatia masharti ya Kanuni hizi, mapendekezo na miongozo ya IALA na Waraka Na. 107 wa Mfumo wa Maboya Baharini. (2) Msajili atamshauri Waziri kuhusiana na masuala ya vifaa vya kuongozea meli na kutekeleza kazi nyingine kama inavyoweza kuelekezwa na Waziri chini ya Kanuni hizi au Sheria nyingine yoyote. Jukumu la Msajili katika vifaa vya kuongozea meli Ushauri kuhusiana na masuala ya vifaa vya kuongozea meli
§ 6Ushauri kuhusiana na masuala ya vifaa vya kuongozea meliProvision

Shirika lazima kupanga mashauriano na wadau wa vifaa vya kuongozea meli kuhusu mabadiliko, uanzishaji, gharama, miongozo na tozo zinazohusiana.

6.-(1) Shirika litafanya mipango ya kushauriana na wadau wa vifaa vya kuoongozea meli kuhusu masuala yanayohusiana na- (a) kuanzisha au kuweka vifaa vya kuongozea meli au kazi nyingine zinazohusiana; (b) nyongeza kwa au mabadiliko au kuondolewa kwa, kifaa chochote cha kuongozea meli; (c) tofauti kwa kifaa chochote cha kuongozea meli 7 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) au namna ya matumizi yake; (d) gharama ya pendekezo lolote kuhusiana na vifaa vya kuongozea meli; au (e) utoaji au ubadilishaji wa miongozo au tozo za vifaa vya kuongozea meli. (2) Wadau waliorejewa chini ya kanuni ndogo ya (1) watajumuisha: (a) Ofisi ya Rais; (b) Ofisi ya Waziri Mkuu; (c) Wizara yenye dhamana na masuala ya fedha- forodha; (d) Wizara yenye dhamana na masuala ya ulinzi- Jeshi la wanamaji; (e) Wizara yenye dhamana na masuala ya usafiri majini; (f) Wizara yenye dhamana na masuala ya mambo ya ndani-Polisi; (g) Wizara yenye dhamana na masuala ya ardhi- Upimaji na Ramani; (h) Wizara yenye dhamana na masuala ya serikali za mitaa; (i) Shirika; (j) Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania; (k) Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania; na (l) Chuo cha Bandari. SEHEMU YA TATU USIMAMIZI WA VIFAA VYA KUONGOZEA MELI Usimamizi wa vifaa vya kuongozea meli

Part

SEHEMU YA TATU

§ 7Usimamizi wa vifaa vya kuongozea meliProvision

Shirika has general authority over navigation aids in Tanzania’s waters and nearby areas, and it may authorize a person to provide those services after an application, unless another law gives the authority.

7.-(1) Shirika litakuwa na mamlaka ya jumla katika vifaa vya kuongozea meli katika maji ya Tanzania na maeneo ya karibu. (2) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo ya (1), Shirika linaweza kumuidhinisha mtu yeyote kama mtoa huduma wa vifaa vya kuongozea meli au mtoa huduma ya uongozaji chombo baada ya ombi isipokuwa kama mamlaka yanatokana na sheria nyingine. (3) Namna ya ombi la kufanya kazi kama mtoa huduma wa vifaa vya kuongozea meli au mtoa huduma wa uongozaji chombo itaainishwa katika Notisi ya Usafiri 8 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Majini. Mamlaka na majukumu ya Shirika kuhusiana na vifaa vya kuongozea meli ya-
§ 8Mamlaka na majukumu ya Shirika kuhusiana na vifaa vyaProvision

Shirika lina mamlaka na majukumu mengi kuhusu vifaa vya kuongozea meli, na mtu anayepanga kusimika, kuweka, kubadili au kuondoa kifaa cha kuongoza meli lazima aombe ridhaa kwa Msajili.

8.-(1) Shirika litakuwa na mamlaka na majukumu (a) kuanzisha na kutunza vifaa vya kuongozea meli; (b) kuongeza, kubadili, kutofautisha au kuondoa kifaa chochote cha kuongozea meli; (c) kuidhinisha ukaguzi wa vifaa vya kuongeza meli ambavyo vinaweza kuathiri usalama wa uongozaji meli (d) kuidhinisha uingiaji wa eneo lolote, la umma au binafsi, kwa madhumuni ya ukaguzi wa vifaa vya kuongezea meli; (e) kusafirisha, au kuwezesha usafirishaji, wa bidhaa kupitia eneo lolote, la umma au binafsi, kwa dhumuni lolote kuhusiana na uanzishaji na ukarabati wa kifaa chochote cha kuongozea meli; (f) kumuidhinisha mtoa huduma wa vifaa vya kuongozea meli ambaye ataanzisha na kutunza vifaa vya kuongozea meli katika eneo lililoidhinishwa; (g) kutwaa ardhi kwa madhumuni ya kuanzisha na kukarabati vifaa vya kuongozea meli; (h) kumuelekeza mtoa huduma wa bandari, kubadilisha au kuondoa vifaa vya kuongozea meli na kama kuna umuhimu kurejeshewa gharama zilizoingiwa; (i) kuhakikisha uwiano na miongozo ya kimataifa katika vifaa vya kuongozea meli; na (j) kuhakikisha wajibu wa kimataifa unafikiwa kwa kuwa na mfumo rasmi wa uidhinishaji. (2) Mtu mwenye nia ya kusimika, kuweka, kubadili au kuondoa kifaa cha kuongoza meli ataomba ridhaa kwa Msajili. (3) Shirika linaweza kuidhinisha afisa sahihi kwa maandishi kufanya kazi zake chini ya kanuni ndogo ya (1). 9 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kazi na majukumu ya mtoa huduma wa vifaa vya kuongozea meli
§ 9Kazi na majukumu ya mtoa huduma wa vifaa vya kuongozea meliProvision

A navigation-aids service provider must establish, repair, and manage navigation aids in its area, get approval before certain installations or changes, notify the Commission when changes happen, and charge only approved fees.

9.-(1) Mtoa huduma wa vifaa vya kuongozea meli atawajibika kuanzisha, kukarabati na kusimamia vifaa vya kuongozea meli katika eneo lake. (2) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (1), mtoa huduma wa vifaa vya kuongozea meli- kitu (b) atawezesha (a) ataongeza, kubadilisha au kuondoa kifaa chochote cha kuongozea meli katika eneo lake; kinachoelea, kinachozama kilichokwama kinachochukuliwa kuwa hatarishi katika uongozaji meli katika eneo lake kinafungwa, kuhifadhiwa, kufunguliwa, kuwekwa au kuondolewa; chochote kidogo, nanga, kutia au (c) atapata idhini kutoka kwa Msajili ya kuanzisha, kuweka au kubadilisha kifaa cha kuongozea meli; na (d) atalitaarifu Shirika pale kifaa cha kuongozea meli kiliposimikwa, kuwekwa, kubadilishwa au kuondolewa. (3) Mtoa huduma wa vifaa vya kuongozea meli atatoza ada iliyoidhinishwa na Shirika kuhusiana na kazi, huduma au masuala yoyote anayofanya kuhusiana na kifaa chochote cha kuongozea meli. Usimamizi wa huduma za uongozaji chombo
§ 10Usimamizi wa huduma za uongozaji chomboProvision

Shirika lina mamlaka ya kusimamia na kuendeleza huduma za uongozaji wa chombo, ikiwemo kuidhinisha watoa huduma, mafunzo na vyeti, na kuanzisha au kuendesha huduma inapofaa.

10. Shirika litakuwa na mamlaka kuhusiana na uendelezaji, ukarabati na usimamizi wa huduma za uongozaji wa chombo- (a) kutamka na kuidhinisha mtoa huduma za eneo chombo katika uongozaji wa lililoidhinishwa; (b) kutoa idhibati na kuidhinisha mafunzo ya huduma za uongozaji wa chombo na utoaji vyeti; (c) kuanzisha na kuendesha huduma za uongozaji meli, inapoonekana inafaa; na (d) kuongeza, kubalisha, au kutaka mtu mwingine chochote kuongeza kinachohusiana na huduma za uongozaji wa chombo. kubadilisha au 10 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Viwango vya uanzishaji na uendeshaji wa huduma za uongozaji wa chombo
Section 10Verify source
§ 11Viwango vya uanzishaji na uendeshaji wa huduma za uongozaji waProvision

The provision says pilotage service establishment and operating standards in the United Republic must follow the Maritime Transport Notice and IMO-approved guidance.

11. Viwango vya kuanzisha na kuendesha huduma za uongozaji wa chombo katika Jamhuri ya Muungano vitakuwa kama vilivyoainishwa katika Notisi ya Usafiri Majini kwa kuzingatia miongozo katika huduma za uongozaji wa chombo zilizoridhiwa na IMO. Makatazo kwa shughuli zinazokwamisha uendeshaji wa vifaa vya kuongozea meli
Section 11Verify source
§ 12Makatazo kwa shughuli zinazokwamisha uendeshaji wa vifaa vyaProvision

Shirika linaweza kutumia Notisi ya Usafiri Majini kuainisha makatazo kwa shughuli zinazoingilia uendeshaji wa kifaa cha kuongozea meli ndani ya umbali ulioainishwa.

12.-(1) Shirika linaweza, kupitia Notisi ya Usafiri Majini, kuainisha makatazo katika shughuli ambazo zinakwamisha au kuzuia uendeshaji wa kifaa chochote cha kuongozea meli ndani ya umbali ulioaInishwa kwa kifaa hicho cha kuongozea meli. (2) Bila kuathiri chochote kilicho katika Sheria nyingine, pale ambapo ufanyajikazi wa kifaa chochote cha kuongozea meli au huduma za uongozaji wa chombo imezuiwa moja kwa moja au siyo moja kwa moja, Shirika linaweza pale litakapoona muhimu kutoa maelekezo ya kuondoa au kubadilisha zuio hilo. Mtu anayeendesha au kufanya kazi katika vifaa vya kuongozea meli na huduma za kuongozea meli kuwa na cheti halali SEHEMU YA NNE MAFUNZO NA UTOAJI VYETI
Section 12Verify source

Part

SEHEMU YA NNE

§ 13Mtu anayeendesha au kufanya kazi katika vifaa vya kuongozea meliProvision

A person must not operate or work in a vessel pilotage device or pilotage service-related activity unless they have a valid certificate from or recognized by Shirika showing they have been trained.

13.-(1) Mtu hataendesha au kufanya kazi katika kifaa cha kuongozea meli au huduma ya uongozaji wa chombo ikijumuisha shughuli zinazoendana, isipokuwa akiwa na cheti halali kilichotolewa au kinachotambulika na Shirika kikithibitisha kwamba mtu huyo amepata mafunzo ya kuendesha kifaa hicho cha kuongozea meli au huduma za uongozaji wa chombo. (2) Shirika, kupitia Notisi ya Usafiri Majini, litaainisha shughuli zinazoendana kuhusiana na vifaa vya kuongozea meli na shughuli zinazoendana kuhusiana na huduma za uongozaji wa chombo. (3) Notisi ya Usafiri Majini iliyorejewa chini ya kanuni ndogo ya (2) itajumuisha muundo wa cheti, uhalali na yaliyomo katika masomo yatakoyotolewa katika mafunzo. Utoaji ithibati kwa vyuo vya mafunzo
Section 13Verify source
§ 14Utoaji ithibati kwa vyuo vya mafunzoProvision

Training on ship steering equipment and vessel navigation services must be carried out by an accredited or recognized training institution.

14.-(1) Mafunzo kuhusu vifaa vya kuongozea meli na huduma za uongozaji wa chombo yatafanywa na taasisi ya mafunzo yenye ithibati au inayotambulika. 11 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) TS. Na. 243 la 2016 Utambuzi wa vyeti vya vinavyotolewa na taasisi nyingine zinazotambulika (2) Shirika litatoa ithibati kwa taasisi ya mafunzo na programu za kufanya mafunzo au tathmini katika uendeshaji wa vifaa vya kuongozea meli au huduma za uendeshaji wa chombo. (3) Taasisi inayorejewa chini ya kanuni ndogo ya (2) itakidhi vigezo vya kupata ithibati vilivyoainishwa katika Kanuni za Mafunzo, Utoaji vyeti na Ufanyaji Kazi Melini.
Section 14Verify source
§ 15Utambuzi wa vyeti vinavyotolewa na taasisi nyingineProvision

Mwombaji wa utambuzi wa cheti lazima atume maelezo ya masomo na nakala iliyothibitishwa ya cheti, na shirika litatoa cheti cha utambuzi baada ya kujiridhisha na kulipwa ada.

15.-(1) Ombi la utambuzi wa cheti cha uendeshaji au kufanya kazi katika vifaa vya kuongozea meli au huduma za uongozaji wa chombo kilichotolewa na taasisi nyingine inayotambulika litawasilisha- (a) yaliyomo katika masomo; na (b) nakala ya cheti kilichothibitishwa. (2) Shirika baada ya kijiridhisha na malipo ya ada yaliyolipwa na mwombaji litatoa cheti cha utambuzi wa tuzo. SEHEMU YA TANO ADA KWA VIFAA VYA KUONGOZEA MELI Ukusanyaji wa ada kwa vifaa vya kuongozea meli TS. Na. 293 la 2005
Section 15Verify source

Part

SEHEMU YA TANO

§ 16Ukusanyaji wa ada kwa vifaa vya kuongozea meliProvision

Ada za vifaa vya kuongozea meli lazima zikusanywe kwa meli zinazoingia au kutoka bandarini, na afisa sahihi anaweza kuomba nyaraka, uwepo wa mhusika, na ukaguzi wa meli ili kuthibitisha tani jumla.

16.-(1) Kutakuwa na utozaji na ukusanyaji wa ada kwa vifaa vya kuongozea meli, kwa viwango vilivyoainishwa katika Kanuni za Ada za Usafiri Majini. (2) Ada ya vifaa vya kuongozea meli inayotozwa chini ya kanuni ndogo ya (1) itakusanywa na Shirika au mtoa huduma wa vifaa vya kuongozea meli kwa kila meli inayowasili au kuondoka katika bandari yoyote ya Jamhuri ya Muungano, kutoka kwa mtu huyo na kwa namna ambayo inaweza kuainishwa katika Notisi ya Usafiri Majini. (3) Kwa madhumuni ya kutoza ada ya vifaa vya kuongozea meli, ukubwa wa jumla ya tani wa chombo utatumika. (4) Ili kuhakiki ukubwa wa jumla ya tani wa chombo kwa dhumuni la kutoza ada ya vifaa vya kuongozea meli, afisa sahihi anaweza, akiona inafaa, kutaka utolewaji wa nyaraka, kuhudhuria kwa mhusika na ukaguzi wa meli. 12 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Marejesho ya ada ya vifaa vya kuongozea meli
Section 16Verify source
§ 17Marejesho ya ada ya vifaa vya kuongozea meliProvision

If the vessel owner refuses or neglects to pay the required fee for ship guidance equipment, the proper officer may stop the ship from leaving the port.

17. Pale ambapo mmiliki wa chombo anakataa au kupuuza kulipa ada kwa vifaa vya kuongozea meli inayopaswa kulipwa chini ya Kanuni hizi kuhusiana na chombo, afisa sahihi anaweza kuzuia meli kuondoka bandarini. Kuzuia kuondoka bandarini
Section 17Verify source
§ 18Kuzuia kuondoka bandariniProvision

Afisa anayetoa ruhusa ya chombo kuondoka bandarini hapaswi kutoa ruhusa hadi ada za vifaa vya kuongozea meli, faini zilizowekwa, au dhamana ya malipo hizo iridhishe.

18. Afisa aliyepewa jukumu la kutoa ruhusa kwa chombo kuondoka bandarini hatatoa ruhusa hiyo hadi- (a) kiwango cha ada kwa vifaa vya kuongozea meli kitakapolipwa; (b) faini zilizowekwa zitakapolipwa; au (c) dhamana ya malipo hayo imetolewa kwa kwa kiwango cha kumridhisha. Utatuzi wa mgogoro kuhusu uwajibaki kwa malipo
Section 18Verify source
§ 19Utatuzi wa mgogoro kuhusu uwajibaki kwa malipoProvision

If there is a dispute about whether ship-related fees or costs are payable, or about their amount, any party may ask the local court to hear and decide it.

19. Unapotokea mgogoro iwapo ada au gharama zinapaswa kulipwa kuhusiana na meli chini ya Kanuni hizi au kwa kiwango cha ada au gharama hiyo, mgogoro huo, kwa ombi litakalofanywa na upande wowote katika mgogoro, utasikilizwa na kuamriwa na mahakama yenye mamlaka katika eneo mgogoro ulipotokea. Urejeshaji wa ada ya uongozaji meli inayodaiwa katika bandari nyingine (2) (1) If Msamaha
Section 19Verify source
§ 20Urejeshaji wa ada ya uongozaji meli inayodaiwa katika bandariProvision

If a vessel leaves port without paying the port navigation aids fee, a proper port officer may ask, in writing, another proper officer at the vessel’s destination port in Tanzania to recover the unpaid fee; that officer must continue charging it as required under the rules.

20.-(1) Pale ambapo nahodha wa chombo ambacho kinapaswa kulipa ada ya vifaa vya kuongozea meli katika bandari atasababisha chombo kuondoka pasipo kulipa ada hiyo, afisa sahihi wa bandari hiyo anaweza kumtaka kwa maandishi afisa sahihi katika bandari nyingine yoyote katika Jamhuri ya Muungano ambayo meli inaelekea, kudai ada ya vifaa vya kuongozea meli ambayo haikulipwa. (2) Afisa sahihi ambaye ombi lililorejewa chini ya kanuni ndogo ya (1) limeelekezwa, ataendelea kutoza fedha hiyo kama vile ilivyotakiwa kulipwa chini ya Kanuni hizi, katika bandari ambayo yeye ni afisa sahihi.
Section 20Verify source
§ 21MsamahaProvision

Waziri anaweza, kwa notisi, kusamehe meli au chombo fulani kulipa ada ya vifaa vya kuongozea meli, kikamilifu au kwa kiwango kilichoainishwa kwenye notisi.

21. Waziri anaweza, kwa notisi, kusamehe chombo chochote au aina ya meli au meli zinazofanya safari maalum kulipa ada ya vifaa vya kuongozea meli kwa ujumla au kwa kiwango kinachoweza kuainishwa kwenye notisi hiyo. 13 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kurejeshwa malipo yaliyozidi Makosa na adhabu
Section 21Verify source
§ 22Kurejeshwa malipo yaliyozidiProvision

A claim to recover an overpaid vessel-conveyance fee is not accepted unless it is made within 12 months from the payment date.

22. Pale ambapo ada ya vifaa vya kuongozea meli imelipwa kuhusiana na meli yoyote kwa kuzidisha kiwango kinachopaswa kulipwa chini ya Kanuni hizi, madai yaliyozidi hayatakubaliwa, isipokuwa kama yamefanyika ndani ya miezi kumi na miwiliu kuanzia tarehe ya malipo hayo. kurejeshewa malipo hayo ya SEHEMU YA SITA MASHARTI YA JUMLA
Section 22Verify source

Part

SEHEMU YA SITA

§ 23Makosa na adhabuOffence

This section makes several acts involving navigation aids or pilotage services an offence and sets fines and possible prison terms.

23.-(1) Mtu anayefanya au kutofanya kitendo kwa makusudi kitakachosababisha kukwamisha, kupunguza au kuzuia ufanisi wa kifaa cha kuongozea meli au huduma ya uongozaji wa chombo anatenda kosa na atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua dola za Marekani elfu moja au kiwango kinacholingana katika shilingi za Kitanzania, na mia tano au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi sita au vyote kwa pamoja. (2) Mtu anayefanya au kutofanya kitendo chochote kwa uzembe kitakachosababisha kukwamisha, kupunguza au kuzuia ufanisi wa kifaa cha kuongozea meli au huduma ya uongozaji wa chombo anatenda kosa na atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua dola za Marekani mia tano au kiwango kinacholingana katika shilingi za Kitanzania, au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu au vyote kwa pamoja. (3) Mtu anayefanya au kutofanya kitendo chochote kwa makusudi kitakachosababisha hasara au uharibifu wa kifaa cha kuongozea meli au huduma ya uongozaji wa chombo anatenda kosa na atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua dola za Marekani elfu mbili au kiwango kinacholingana katika shilingi za Kitanzania, au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na miwili au vyote kwa pamoja. (4) Mtu anayefanya au kutofanya kitendo chochote kitakachosababisha, hasara au uharibifu wa mnara wa urithi wa taa za kuongoza meli anatenda kosa na atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua dola za Marekani elfu moja au kiwango kinacholingana 14 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) katika shilingi za Kitanzania, au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi sita au vyote kwa pamoja. (5) Mmiliki wa meli au nahodha anayekwepa au kujaribu kukwepa kulipa ada za vifaa vya kuongozea meli au gharama zinazopaswa kulipwa na meli chini ya Kanuni hizi, anatenda kosa na atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua dola za Marekani elfu moja au kiwango kinacholingana katika shilingi za Kitanzania, au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi sita au vyote kwa pamoja. (6) Mmiliki wa meli au nahodha, anayeshindwa kutekeleza maelekezo yoyote yaliyotolewa na mtoa huduma za uongozaji wa chombo kuhusiana na huduma za uongozaji wa chombo chini za Kanuni hizi anatenda kosa na atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua dola za Marekani elfu moja au kiwango kinacholingana katika shilingi za Kitanzania, au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi sita au vyote kwa pamoja. (7) Mtu anayeendesha au kufanya kazi katika vifaa vya uongozaji meli na huduma za uongozaji wa chombo ikijumuisha shughuli zinazoendana na hizo pasipo kuwa na cheti halali kilichotolewa au kinachotambuliwa na Shirika anatenda kosa na atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua dola za Marekani elfu moja au kiwango kinacholingana katika shilingi za Kitanzania, au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi sita au vyote kwa pamoja.
Section 23Verify source
§ 24Uwekaji na urejeshaji wa alama kwa mabaki ya meliProvision

Msajili anaweza kuagiza afisa sahihi kuweka alama kwa mabaki ya meli, na kituo cha majini, mwendeshaji wa bandari, pamoja na mmiliki wa meli iliyozama, wanawajibika kuweka alama za maeneo ya mabaki yanayoweza kuhatarisha usalama wa uongozaji.

24.-(1) Msajili anaweza kutoa maelekezo kwa afisa sahihi kuweka alama katika mabaki ya meli kwa namna inayoweza kuainishwa. (2) Itakuwa jukumu la kituo chochote cha majini au mwendesha bandari na mmiliki wa meli iliyozama kuweka alama za maeneo mabaki ya meli yalipo yanayoweza kuhatarisha usalama wa uongozaji. (3) Gharama za kuweka alama za maeneo mabaki ya meli yalipo zitatolewa au kurejeshwa kutoka kwa mmiliki au mwendeshaji wa meli hiyo. 15 Uwekaji na urejeshaji wa alama kwa mabaki ya meli Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Mamlaka ya Waziri kushauri vifaa vya kuongozea meli kutumika kama maeneo ya urithi
Section 24Verify source
§ 34Section 34Provision

Kifungu hiki kinaelekeza kinga kwa vitendo vinavyofanywa kwa nia njema.

34. Kinga kwa vitendo vinavyofanywa kwa nia njema
Section 34Verify source
§ 25Mamlaka ya Waziri kushauri vifaa vya kuongozea meli kutumikaProvision

Waziri anaweza kumshauri Waziri mwenye dhamana ya masuala ya mambo kale kuteua maeneo ya kuongozea meli kama mnara wa urithi wa taa za kuongoza meli.

25. Waziri anaweza kumshauri Waziri mwenye dhamana ya masuala ya mambo kale kuteua maeneo ya kuongozea meli kama mnara wa urithi wa taa za kuongoza meli.
Section 25Verify source
§ 26Kinga kwa vitendo vinavyofanywa kwa nia njemaProvision

No proceedings may be brought for acts done under these Regulations in good faith.

26. Shauri halitafunguliwa dhidi ya Shiriki au afisa sahihi chini ya Kanuni hizi kwa kitendo chochote kilichofanywa chini ya Kanuni hizi kwa nia njema. Uchapishaji wa taarifa kuhusiana na vifaa vya kuongozea meli
Section 26Verify source
§ 27Uchapishaji wa taarifa kuhusiana na vifaa vya kuongozea meliProvision

Shirika lazima lichapishe taarifa kuhusu vifaa vya kuongozea meli na kuzipa jamii ya usafirishaji majini.

27.-(1) Shirika litachapisha taarifa kuhusiana na vifaa vya kuongozea meli na kuzitoa kwa jamii ya usafirishaji majini. Tathmini na utoaji wa taarifa (1), (2) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya mabadiliko katika usambazaji wa wa mifumo ya kurekebisha nafasi inayoweza kuathiri kwa kiasi kikubwa utendaji wa vifaa vya kupokea taarifa vilivyowekwa melini yataepukwa na yanaweza kutekelezwa baada ya notisi kutolewa kwa notisi inayojitosheleza na kwa wakati.
Section 27Verify source
§ 28Tathmini na utoaji wa taarifaProvision

Msajili anapaswa kutathmini masharti ya udhibiti ya Kanuni hizi, kuandaa na kufichua hitimisho la tathmini, na kuwasilisha taarifa kwa Waziri.

28.-(1) Msajili- (a) atafanya tahmini ya masharti ya udhibiti yaliyopo katika Kanuni hizi; (b) ataandaa taarifa na kuweka wazi hitimisho la tathmini; na (c) atawasilisha taarifa kwa Waziri. (2) Taarifa ya kwanza chini ya Kanuni hii itatatolewa kabla ya mwaka wa tano wa maadhimisho ya tarehe ambayo Kanuni hizi zimeanza kutumika. (3) Taarifa zitakazofuata zitatolewa kwa vipindi visivyozidi miaka mitano. (4) Taarifa iliyoandaliwa na kuwasilishwa chini ya Kanuni hizi- (a) itaweka wazi dhumuni linalolengwa kufikiwa na mashari ya udhibiti yaliyorejewa chini ya kanuni ndogo ya (1)(a); (b) itafanya tathmini ya kiwango ambacho malengo hayo yamefikiwa; (c) itathmini iwapo malengo hayo yataendelea kuwa na tija; na 16 Kanuni Za Uanzishaji Na Uendeshaji wa Vifaa vya Kuongozea Meli Tangazo la Serikali Na. 497 (Linaendelea.) (d) pale malengo yataendelea kuwa na tija, itatathmini kiwango ambacho malengo hayo yatafikiwa kwa njia nyingine ambayo itahusisha masharti mepesi ya udhibiti. Ushughulikiaji wa malalamiko TS. Na. 338 la 2018
Section 28Verify source
§ 29Ushughulikiaji wa malalamikoProvision

A dissatisfied person may ask Shirika to review a decision made under these Regulations.

29. Mtu ambaye hataridhishwa na uamuzi uliotolewa chini ya Kanuni hizi anaweza kuomba Shirika kupitia upya uamuzi huo kwa mujibu wa Kanuni za Ushughulikiaji wa Malalamiko za Uwakala wa Meli Tanzania. Dodoma, 28 Juni, 2023 MAKAME M. MBARAWA, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi 17
Section 29Verify source

Legislative relationships

0 referenced instruments

Names are derived from the stored provision headings and citation-enrichment layer. Treat this as a research index and verify each relationship against the source text.

No structured legislative relationships were detected

The statute remains fully searchable by provision. Consult the source text for amendments and cross-references that have not yet been indexed.

Recorded versions and source checkpoint

1 version available in this collection

Current-law checkpoint
  • Undated version · currentSwahili

Source-linked research

Ask AI about this statute

The overview, provisions, and source records above are public. Continue in a separate conversation with this statute’s jurisdiction and source version attached.

About this LexChat collection

Statute information is organised from identified legislative sources for professional research. Corrections can be reported to hello@esheria.ai.