Kanuni za Vifaa vya Uokozi na Mpangilio za Mwaka 2023
This section says the rules are to be called the Kanuni za Vifaa vya Uokozi na Mpangilio za Mwaka 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Vifaa vya Uokozi na Mpangilio za Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section says the rules are to be called the Kanuni za Vifaa vya Uokozi na Mpangilio za Mwaka 2023. These regulations apply to certain ships and the implementation of Chapter III of the Safety Convention, but several ship types are excluded. This section defines terms used in the regulations, including passenger, passenger ship, short international voyage, the Safety Convention, the Registrar, the Corporation, and the Minister. This section says references to Chapter III of the Security Treaty must be read as references to the amended Chapter III, and if Chapter III has been changed, the reference is to the change. Amendments or changes take effect when they comply with Article VIII of the Treaty. For these Regulations, the ship classes are to be as listed in the Schedule/Table to the Regulations.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Vifaa vya Uokozi na Mpangilio za Mwaka 2023
Showing 22 of 22
- 1
AI-assisted research summary: This section says the rules are to be called the Kanuni za Vifaa vya Uokozi na Mpangilio za Mwaka 2023.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Vifaa vya Uokozi na Mpangilio za Mwaka 2023. Matumizi - 2
AI-assisted research summary: These regulations apply to certain ships and the implementation of Chapter III of the Safety Convention, but several ship types are excluded.
2.-(1) Kanuni hizi zitatumika- (a) kwa ajili ya kutekeleza Sura ya III ya Mkataba wa Usalama; (b) kwa meli za Tanzania, popote zilipo; (c) kwa meli sizizo za Tanzania wakati zinapokuwa katika maji ya Tanzania; na (d) kwa meli ya starehe ya Tanzania inayofanya kazi kwa kukodi au malipo au kwa aina nyingine yoyote ya malipo ya kifedha. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), Kanuni hizi hazitatumika kwa- (a) meli za kivita au msaada wa kijeshi; (b) meli zinazomilikiwa au kutumiwa na Serikali na kujihusisha na shughuli za kiserikali zisizo za kibiashara; (c) meli za abiria Daraja la III, IV, V, VI na VI(A); (d) meli za mbao zilizojengwa kiasili; (e) meli za uvuvi; (f) meli zisizo za Tanzania ambazo ni meli za starehe; (g) meli zenye urefu usiopungua mita 24 au tani 50 za jumla; na 3 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio (h) meli isiyo ya Tanzania ambayo inapeperusha bendera ya Nchi ambayo si mwanachama wa Mkataba wa Usalama na isingekuwa katika maji ya Tanzania isipokuwa kwa dhoruba ya hali ya hewa au mazingira yoyote ambayo nahodha, mmiliki au mkodishaji asingeweza kuzuia. Tafsiri - 3
AI-assisted research summary: This section defines terms used in the regulations, including passenger, passenger ship, short international voyage, the Safety Convention, the Registrar, the Corporation, and the Minister.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “abiria” maana yake ni mtu yeyote aliyebebwa kwenye meli tofauti na- (a) mtu aliyeariliwa au anaejihusisha katika nafasi yoyote katika shughuli za melini; (b) mtu aliye ndani ya meli kwa sababu ya ruhusa iliyotolewa na nahodha kufanya shughuli za kuibua meli, dhoruba au watu wengine au kwa sababu nyingine yoyote ambazo nahodha, mmiliki, au mkodishaji, kama yupo, asingeweza kuzuia au kuepusha; (c) mtoto chini ya mwaka mmoja; “abiria maalum wa biashara” maana yake ni abiria anayesafirishwa kwa biashara maalum katika sakafu wazi ya meli, sakafu ya juu, au kati ya sakafu zinazoweza kubeba zaidi ya abiria nane; na “bahari” maana yake ni mlango wa mto au mkono wa bahari tofauti na aina A, B, C au D ya maji; “chombo cha starehe” maana yake ni- (a) chombo chochote ikijumuisha boti za kuzamia ambacho wakati wa matumizi yake- (i) kinamilikiwa na mtu au watu binafsi na kinatumika kwa ajili ya michezo pekee au starehe ya mmiliki au wanafamilia au marafiki wa mmiliki; au (ii) kinamilikiwa na kampuni ambapo watu wanaokitumia ni waajiriwa, maafisa, au wadau wa kampuni, au wana familia au marafiki; (b) chombo kilichopo safarini ambacho mmiliki wake hapokei pesa kutokana na uendeshaji wa 4 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio TS. Na. 63 la 2019 chombo hicho au kubeba mtu yeyote, tofauti na michango ya moja kwa moja ya gharama za uendeshaji wa chombo zilizotumika wakati wa safari, au chombo chochote kinachomilikiwa moja kwa moja au kwa niaba ya klabu iliyoanzishwa kwa malengo ya michezo au starehe ambacho wakati wa matumizi yake kinatumiwa kwa madhumuni pekee ya michezo au starehe kwa wanachama wa klabu au wana familia wao wa karibu, na kwa matumizi ambayo tozo zake hulipwa katika mfuko wa klabu na kutumika kwa matumizi ya jumla ya klabu; “hatua sawa ya ujenzi” maana yake ni hatua ambayo- (a) ujenzi unaotambulika kwa meli maalum unaanza; na (b) uundwaji wa meli umeanza kwa kujumuisha angalau tani 50 au 1% ya uzito unaotarajiwa wa vifaa vya ujenzi, chochote kitakachokuwa kidogo; “Kundi A, B, C au D” maana yake ni maji yaliyoanishwa katika Kanuni za Ukomo wa Upakiaji za Usafiri Majini; “maili” maana yake ni notiko maili za kimataifa za mita 1,852; “meli maalum ya abiria ya biashara” maana yake ni meli inayoendeshwa kimitambo ambayo idadi kubwa ya abiria maalum wa ya abiria hubeba biashara; “meli mpya” maana yake ni meli ambayo nguzo yake imesimamishwa, au iko katika hatua sawa ya ujenzi, tangu tarehe 1 Julai 1998; “meli ya abiria” maana yake ni meli iliyojengwa kwa, au ambayo kimsingi au katika matukio maalum kubeba zaidi ya abiria 12 na inajumuisha meli ambayo imetolewa kwa usafiri au burudani kwa wageni katika taasisi yoyote, hoteli, nyumba za kupumzikia wageni, nyumba za wageni au matumizi mengine; “Mkataba wa Usalama” maana yake ni Mkataba wa 5 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio Sura ya 415 Sura ya 165 Sura ya 415 Kimataifa wa Usalama wa Maisha Baharini wa mwaka 1974 na Itifaki zake za mwaka 1978 na 1988, pamoja na marekebisho yake, au mbadala wake kama utakavyotumika Tanzania; “Msajili” maana yake ni Msajili aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 31 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania; “Nchi ya Mkataba wa Usalama” maana yake ni Nchi ambayo Serikali yake imeridhia matumizi ya Mkataba wa Usalama na ambayo haijajitoa katika Mkataba huo, au eneo la Nchi ambalo Mkataba huo unatumika na kuendelea kutumika; “Notisi ya Usafiri Majini” maana yake ni Notisi ya inayotolewa na Msajili na Usafiri Majini yoyote nyaraka rejea inajumuisha inayorekebisha au kubadili Notisi hiyo; ya “safari fupi ya kimataifa” maana yake ni safari ya kimataifa- (a) ambayo meli haiko zaidi ya maili 200 za nautiki kutoka bandari au mahali ambapo abiria na wafanyakazi wanaweza kuwekwa salama; na (b) ambayo haizidi maili 600 za nautiki kati ya bandari ya kuondokea na mwisho wa safari, bila kuzingatia mabadiliko yoyote ya njia katika safari yake kutokana na hali mbaya ya hewa au mazingira yoyote ambayo nahodha, mmiliki au mkodishaji wa meli asingeweza kuzuia au kuepusha; “safari ya kimataifa” maana yake ni safari kati ya- (a) bandari ya Tanzania na bandari iliyo nje ya Tanzania; au (b) bandari katika Nchi ya Mkataba, isipokuwa Tanzania, na bandari katika Nchi yoyote au mipaka, iwe au isiwe Nchi ya Mkataba, iliyo nje ya Tanzania; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Usafiri Majini; “Shirika” maana yake ni Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania lililoanzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania; 6 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio “Sura ya III” maana yake ni Sura ya III ya Mkataba wa Kimataifa wa Usalama wa Maisha Baharini wa 1974; na “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya masuala ya usafiri majini. Rejea ya mkataba - 4
AI-assisted research summary: This section says references to Chapter III of the Security Treaty must be read as references to the amended Chapter III, and if Chapter III has been changed, the reference is to the change. Amendments or changes take effect when they comply with Article VIII of the Treaty.
4.-(1) Katika Kanuni hizi, rejea yoyote ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama itatafsiriwa- (a) kama rejea ya Sura ya III ilivyorekebishwa; na (b) pale ambapo Sura ya III imebadilishwa, rejea ya mabadiliko. (2) Kwa madhumi ya kifungu kidogo cha (1), Sura ya III itakuwa imerekebishwa au kubadilishwa kama marekebisho au mabadiliko yamefanyika sawa na Ibara ya VIII ya Mkataba. (3) Marekebisho au mabadiliko ya Sura ya III yataanza kutumika wakati marekebisho au mabadiliko hayo yamezingatia matakwa ya Ibara ya VIII ya Mkataba. SEHEMU YA PILI MADARAJA YA MELI NA IDHINI YA VIFAA VYA UOKOZI NA MPANGILIO Madara ya meli
Part
SEHEMU YA PILI
- 5
AI-assisted research summary: For these Regulations, the ship classes are to be as listed in the Schedule/Table to the Regulations.
5. Kwa madhumuni ya Kanuni hizi, madaraja ya meli yatakua kama yalivyoanishwa katika Jedwali la Kanuni hizi. Idhini na kubadilishwa - 6
AI-assisted research summary: Msajili au mtu aliyeidhinishwa naye anaweza kutoa, kuendeleza, kubadilisha, au kufuta idhini za vifaa vya uokozi na baadhi ya idhini za meli za Tanzania; vifaa vilivyo na tarehe ya ukomo vinapaswa kubadilishwa kwa wakati, na Msajili lazima ajiridhishe na utii kabla ya kukubali vifaa visivyoidhinishwa awali.
6.-(1) Vifaa vya uokozi vilivyowekwa katika meli ya Tanzania vitaidhinishwa na Msajili au mtu yeyote aliyeidhinishwa na Msajili. (2) Msajili au mtu yeyote aliyeidhinishwa na Msajili anaweza kutoa idhini kuhusiana na meli ya Tanzania kwa suala lolote katika Sura ya III ya Mkataba wa Usalama endapo inahitaji: (a) kuidhinishwa na Nchi ya usajili wa meli ambayo meli inastahili kupeperusha bendera 7 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio yake; (b) kukidhi matakwa ya Nchi ya usajili wa meli; na (c) kukubalika na Nchi ya Usajili wa meli. (3) Idhini iliyotolewa chini ya kanuni ndogo ya (1) au (2) inaweza, kwa kutoa notisi kuruhusiwa kuendelezwa, kubadilishwa au kufutwa. (4) Idhini, mwendelezo, mabadiliko au kufutwa kulikotolewa chini ya kanuni hii: (a) kutakuwa kwa maandishi; (b) kutabainisha tarehe ya kuanza kutumika; na (c) kutabainisha masharti, kama yapo, ya kutolewa kwake. (5) Sharti idhini, mwendelezo, mabadiliko au kufutwa chini ya kanuni hii kuwa kwa maandishi litatimia pale ambapo maandishi ya idhini: kwamba (a) yamewekwa kielektroniki; (b) yamepokelewa katika mfumo unaosomeka; na (c) yanafaa kutumika kwa marejeo yanayofuata. (6) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (7), kifaa chochote cha uokozi wa maisha chenye tarehe ya ukomo wa matumizi- (a) kitakoma kuidhinishwa kwa madhumuni ya Kanuni hizi katika ukomo wa tarehe ya matumizi; na (b) kitabadilishwa wakati au kabla ya tarehe ya ukomo. (7) Kifungashio cha dharura cha chombo cha uokozi, kilichokaguliwa wakati ukarabati wa mwaka wa chombo cha uokozi na kina maisha ya miezi sita iliyosalia kabla ya tarehe ya ukomo wakati wa muda wa ukaguzi kinaweza kuachwa mpaka kipindi cha ukarabati wa mwaka unaofuata. (8) Msajili atajiridhisha kuwa vifaa vya ukozi wa maisha na mpangilio unazingatia masharti ya Kanuni hizi na za Kimataifa za vifaa vya uokozi wa maisha, kabla ya kukubali vifaa na mpangilio ya uokoaji wa maisha ambavyo havikuwa vimeidhinishwa na msajili hapo awali. 8 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio Misamaha - 7 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: Msajili anaweza kusamehe masharti fulani ya usalama kwa baadhi ya meli, na pia anaweza kurekebisha au kufuta msamaha huo kwa notisi.
7.-(1) Msajili anaweza kusamehe- (a) meli au aina za meli ambazo, wakati wa safari, haziendi umbali zaidi ya maili 20 kutoka nchi kavu ya karibu, na pale ambapo msajili ameridhika kwamba eneo la kujistihili na hali ya safari hiyo inalazimisha kutokuwa na umuhimu au ulazima wa kutumia masharti ya Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama; (b) meli ambayo kwa kawaida haifanyi safari za kimataifa lakini katika uhitaji wa kipekee, inatakiwa kufanya safari moja ya kimataifa; (c) meli yenye muundo wa vifaa vya aina ya riwaya kama tafiti kutoka vifaa hivyo na inayofanya mjumuisho wake katika meli safari za Kimataifa unaweza kuzuiliwa pale ambapo meli itapaswa kukidhi matakwa ya Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama. (2) Msajili anaweza, katika mazingira ya kipekee ambayo hayajaainishwa katika kanuni ndogo ya (1), kusamehe kutumika kwa masharti yoyote ya Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama, kwa meli au aina za meli endapo atajiridhisha kwamba uzingatiaji wa masharti hayo hautekelezeki au hauna mantiki kuhusiana na meli au aina za meli hizo. (3) Msamaha chini ya kanuni hii, unaweza kutolewa kwa kuzingatia masharti ya usalama, kama itakavyoonekana la kuhakikisha usalama wa jumla wa meli. inafaa na Msajili kwa lengo (4) Msamaha uliotolewa chini ya kanuni hii unaweza, kwa kutolewa notisi ya msingi, kurekebishwa au kufutwa. (5) Msamaha, mabadiliko au kufutwa kulikotolewa chini ya kanuni hii kutapaswa- (a) kuwa katika maandishi; (b) kufafanua tarehe ambayo utaanza kutumika; na (c) kuainisha masharti yaliyotolewa, kama yapo. (6) Sharti kwamba msahama, mabadiliko au 9 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio kufutwa kulikotolewa chini ya kanuni hii kuwa kwa maandishi litatimia pale ambapo maandishi ya idhini- (a) yamewekwa kwa njia ya kielektroniki; (b) yamepokelewa katika mfumo unaosomeka; na (c) yanafaa kutumika kwa marejeo yanayofuata. (7) Pale ambapo msahama umetolewa kwa kuzingatia masharti ya usalama, msamaha utakoma kutumika endapo masharti hayo hayatazingatiwa. SEHEMU YA TATU MASHARTI KWA MELI ZILIZOJENGWA KABLA YA TAREHE 1 JULAI 1998 ZINAZOFANYA SAFARI ZA KIMATAIFA Matumizi Masharti kwa meli zilizojengwa kabla ya tarehe 1 Julai, 1998
Part
SEHEMU YA TATU
- 8
AI-assisted research summary: Sehemu hii inatumika kwa meli fulani za madaraja yaliyotajwa ambazo zilikuwa zimeanza kujengwa kabla ya 1 Julai 1998 na zinapanga kufanya safari za kimataifa.
8. Sehemu hii inatumika kwa meli za Daraja la I, II, VII, VII(A), VII(T), VIII, VIII(T), IX, XI na XII, ambazo nguzo zilikuwa zimewekwa au zilikuwa katika hatua sawa ya ujenzi, kabla ya 1 Julai, 1998 kufanya safari za kimataifa. - 9
AI-assisted research summary: A ship covered by this section must comply with every requirement of Section B of Chapter III of the Safety Convention, except Class XI and XII ships.
9.-(1) Meli ambayo sehemu hii inatumika itazingatia kila sharti la Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama inayotumika kwake, isipokuwa kwa meli za Daraja la XI na XII. (2) Meli zilizojengwa kabla ya tarehe 1 Julai, 1998 zitakuwa chini ya masharti maalum ya Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama, ikijumuisha kanuni zinazotumika kwa “meli zote”. (3) Maneno “meli zote” maana yake ni meli zilizojengwa kabla, mnamo au baada ya tarehe 1 Julai, 1998; maneno meli zote za abiria na meli zote za mizigo yatatafsiriwa ipasavyo. Ubadilishaji wa vifaa vya uokozi wa maisha na mpangilio - 10 Verify source ↗
Matumizi
AI-assisted research summary: Section 10 exempts ships of Class XI and XII, and requires ships covered by the section to follow the safety-convention rules when life-saving equipment or arrangements are altered or when major structural work affects them.
10.-(1) Kanuni hii haitumiki kwa meli za Daraja la XI na XII. (2) Pale ambapo katika meli Sehemu hii inatumika- (a) vifaa vya uokozi wa maisha au mpangilio unabadilishwa; au (b) meli inafanyiwa ukarabati, mabadiliko au uboreshaji mkubwa wa muundo unaohusisha 10 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio ubadilishaji wa, nyongeza yoyote kwa, vifaa vyake vya uokozi wa maisha au mpangilio, kubadilishwa au kuongezwa kwa vifaa vya uokoaji wa maisha au mpangilio kwa namna ilivyozoeleka, kutapaswa kuzingatia masharti ya Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama. maisha (3) Pale ambapo- (a) chombo cha uokoaji, tofauti na kifaa cha kinachoelea lakini kifaa chake cha uokozi wa kimebadilishwa kutumbukiza majini hakijabadilishwa; au (b) kifaa cha kutumbukiza chombo cha uokoaji majini tofauti na chombo cha uokoaji, kimebadilishwa lakini chombo cha uokoaji hakijabadilishwa, chombo cha uokoaji au chombo cha kutumbukiza majini, kama ile iliyobadilishwa. itakavyokuwa, kitapaswa kuwa cha aina SEHEMU YA NNE MASHARTI KWA MELI ZILIZOJENGWA KABLA YA TAREHE 1 JULAI 1998 ZISIZOFANYA SAFARI ZA KITAIFA Matumizi
Part
SEHEMU YA NNE
- 11 Verify source ↗
Matumizi
AI-assisted research summary: Sehemu hii inatumika kwa meli fulani za daraja la II(A), VII(A), VIII(A), VIII(A)(T), IX, IX(A), IX(A)(T), XI na XII zilizokuwa zimeanza kujengwa kabla ya 1 Julai 1998 na zisifanye safari za kimataifa.
11. Sehemu hii inatumika kwa meli za Daraja la II(A), VII(A), VIII(A), VIII(A)(T), IX, IX(A), IX(A)(T), XI na XII, ambazo nguzo zilikuwa zimewekwa au zilikuwa katika hatua sawa ya ujenzi, kabla ya tarehe 1 Julai, 1998 zisizofanya safari za kimataifa. Masharti kwa meli zilizojengwa kabla ya tarehe 1 Julai, 1998 - 12 Verify source ↗
Masharti kwa meli zilizojengwa kabla ya Tarehe 1 Julai 1988
AI-assisted research summary: Meli ambazo sehemu hii inawahusu lazima zizingatie masharti yote ya Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama yanayowahusu.
12. Meli ambayo sehemu hii inatumika itazingatia kila sharti la Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama inayotumika kwake. SEHEMU YA TANO MASHARTI KWA MELI MPYA ZINAZOFANYA SAFARI ZA KIMATAIFA Matumizi
Part
SEHEMU YA TANO
- 13 Verify source ↗
Matumizi
AI-assisted research summary: Sehemu hii inatumika kwa meli mpya za madaraja maalum zinazofanya safari za kimataifa.
13. Sehemu hii inatumika kwa meli mpya za Daraja la I, II, VII, VII(T), VIII, VIII(T), IX, XI na XII 11 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio zinazofanya safari za kimataifa. Masharti kwa meli mpya zinazofanya safari za kimataifa - 14 Verify source ↗
Masharti kwa meli mpya zinazoshiriki safari za kimataifa
AI-assisted research summary: New ships in specified classes must comply with all applicable requirements of Part B of Chapter III of the Safety Convention when making international voyages.
14. Meli mpya za Daraja la I, II, VII, VII(T), VIII, VIII(T) au IX, wakati zinapofanya safari za kimataifa, zitazingatia mashatri yote ya Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama yanayotumika kwake. Ubunifu mbadala na mipangilio kwa meli mpya - 15 Verify source ↗
SEHEMU YA SITA
AI-assisted research summary: Kwa meli mpya zinazotumika chini ya kanuni ya 14, vifaa vya uokozi wa maisha na mipangilio vinaweza kutokuwa na fuata masharti ya Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama ikiwa ubunifu mbadala unatoa usalama sawa na unatimiza masharti husika.
15.-(1) Vifaa vya uokozi wa maisha na mipangilio kwa meli mpya ambazo kanuni ya 14 inatumika, vinaweza kutofuata masharti ya Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama, ikizingatiwa kwamba ubunifu mbadala na mipangilio inakidhi masharti ya Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama na kutoa kiwango sawa cha usalama. (2) Kuhusiana na meli ambazo kanuni ya 14 inatumika- (a) ubunifu mbadala au mpangilio itafanyiwa uchambuzi wa uhandisi kwa mujibu wa aya ya - 38 Verify source ↗
3 ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama
AI-assisted research summary: Shirika linaweza kukagua na kuidhinisha uchambuzi wa uhandisi wa ubunifu mbadala au mpangilio, na linaweza pia kuendelea, kurekebisha au kufuta idhini kwa notisi ya msingi.
38.3 ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama kuhusiana na vipengele vya uchambuzi wa uhandisi; na (b) nakala ya uchambuzi wa uhandisi itawasilisha kwa Shirika na mliki. (3) Kuhusiana na ubunifu mbadala au mpangilio na uchambuzi wa uhandisi uliorejewa katika kifungu kidogo cha (2)- (a) Shirika litatathmini na iwapo litajiridhisha kwamba masharti ya aya ya 38.3 cha Sura ya III ya Mkataba wa Usalama yamezingatiwa, litaidhinisha uchambuzi wa uhandisi; na (b) marekebisho yoyote ya ubunifu mbadala au mpangilio yataidhinishwa na Shirika kwa kujiridhisha kuwa ubunifu mbadala au mpangilio ni angalau sawa na inavyohitajika na Kanuni hizi. (4) Pale ambapo dhana na vikwazo vya uendeshaji vilivyotajwa katika ubunifu mbadala au mpangilio chini ya kanuni ndogo ya (2) vinabadilishwa, uchambuzi wa ziada wa uhandisi utafanyika kwa kuzingatia mabadiliko ya dhana na vikwazo vya 12 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio uendeshaji. (5) Pale ambapo ubunifu mbadala au mpangilio uliotajwa chini ya kanuni ndogo ya (2) unahitaji marekebisho, utafanyiwa tathmini na kuidhinishwa na Shirika, endapo litajiridhisha kuwa ubunifu mbadala au mpangilio ni angalau sawa na inavyohitajika na Kanuni hizi. (6) Idhini iliyotolewa chini ya kanuni hii inaweza, kwa kutolewa notisi ya msingi, kuendelea, kurekebishwa au kufutwa. (7) Idhini ya kuendelea, kurekebishwa au kufutwa iliyotolewa chini ya kanuni hii- (a) itakuwa kwa maandishi; (b) itafafanua tarehe ambayo itaanza kutumika; na (c) itafafanua masharti yaliyotolewa, kama yapo. (8) Sharti kuwa idhini ya kuendelea, mabadiliko au kufutwa kulikorejewa chini ya kanuni hii, kuwa kwa maandishi litatimia pale ambapo maudhui ya idhini- (a) yamewekwa kwa njia ya kielektroniki; (b) yamepokelewa katika mfumo unaosomeka; na (c) yanafaa kutumika kwa marejeo yanayofuata. (9) Nakala ya idhini ya kuendelea au kubadilishwa iliyotolewa chini ya kanuni hii, na ambayo inathibitisha kuwa ubunifu mbadala au mpangilio umezingatia Sura ya III ya Mkataba wa Usalama, itabebwa ndani ya meli. SEHEMU YA SITA MASHARTI KWA MELI MPYA ZINAZOFANYA SAFARI ZISIZO ZA KIMATAIFA NA MELI MPYA ZINAZOFANYA SAFARI ZA KIMATAIFA AMBAZO SEHEMU B YA SURA YA III YA MKATABA WA USALAMA HAITUMIKI Matumizi
Part
SEHEMU YA SITA
- 16 Verify source ↗
Matumizi
AI-assisted research summary: Sehemu hii inatumika kwa baadhi ya meli mpya kulingana na daraja lao na kama zinafanya safari za kimataifa; pia kuna ubaguzi kwa meli za mizigo chini ya tani 500 za jumla, na sehemu B ya Sura ya III inatumika kwa meli zote za abiria.
16.-(1) Sehemu hii inatumika kwa meli mpya za- (a) daraja la II(A), VIII(A), VIII(A)(T), IX, IX(A), IX(A)(T), XI na XII ambazo hazifanyi safari za kimataifa; na (b) daraja la I, II, VII, VII(T), VIII, VIII(T) na IX ambazo zinafanya safari za kimataifa lakini sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa 13 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio Usalama haitumiki. (2) Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama haitatumiki kwa meli za mizigo chini ya tani za jumla 500 isipokuwa ikiwa imeelezwa vinginevyo katika Sura ya III. (3) Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama itatumika kwa meli zote za abiria. Masharti kwa meli mpya
Part
sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa
- 17 Verify source ↗
Masharti kwa meli mpya
AI-assisted research summary: Meli ambazo kifungu hiki kinawahusu lazima zifuate kila kifungu cha Sehemu B cha Sura ya III ya Mkataba wa Usalama unaotumika kwao.
17. Meli ambayo Sehemu hii inatumika inapaswa kuzingatia kila kifungu cha Sehemu B cha Sura ya III ya Mkataba wa Usalama inayotumika kwake. Uzuiaji SEHEMU YA SABA MASHARTI YA JUMLA
Part
SEHEMU YA SABA
- 18
AI-assisted research summary: A ship that does not comply with the stated rules may be detained, and the detaining person must give the master a detention notice. The Organization must also notify the ship’s registered country, or its embassy/diplomatic representative if direct notice is not possible.
18.-(1) Meli ambayo haitazingatia masharti ya Kanuni hizi au Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama inaweza kuzuiliwa. (2) Pale ambapo meli imezuiliwa chini ya kanuni ndogo ya (1), masharti ya kifungu cha 409 cha Sheria yatatumika, isipokuwa masharti yaliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (6) hayatatumika. (3) Pale ambapo meli inapaswa kuzuiliwa chini ya kanuni hii, mtu anayeizuia meli hiyo atatoa notisi ya kuzuia kwa Nahodha ambayo- (a) inaeleza sababu za kuwekwa kizuizini; na (b) inahitaji masharti ya notisi kuzingatiwa hadi meli itakapoachiwa na mtu yeyote aliyetajwa chini ya kifungu cha 409 (1) cha Sheria. (4) Pale ambapo meli nyingine ambayo siyo ya Tanzania imezuiliwa, Shirika litaifahamisha mara moja mamlaka ya nchi iliyosajili meli kwa maandishi. (5) Pale ambapo haiwezekani kuijulisha mamlaka ya nchi iliyosajili meli kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (4), Shirika litaifahamisha ofisi ya Ubalozi wa mamlaka ya nchi iliyosajili meli, au endapo hakuna ofisi ya Ubalozi, mwakilishi wa karibu wa kidiplomasia wa nchi iliyosajili meli. (6) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo za (4) na (5), "mamlaka ya nchi iliyosajili" kuhusiana na meli ina 14 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio maana kupeperushwa na meli husika. ambayo nchi bendera yake inastahili Tathmini na utoaji wa taarifa Makosa na adhabu - 19 Verify source ↗
20. Makosa na adhabu
AI-assisted research summary: Msajili must assess the regulatory requirements in these Regulations, prepare a report with the assessment findings, and submit the report to the Minister.
19.-(1) Msajili- (a) atafanya tathmini ya masharti ya udhibiti yaliyomo katika Kanuni hizi; (b) atandaa ripoti inayoainisha hitimisho la tathmini; na (c) atawasilisha ripoti kwa Waziri. (2) Ripoti ya kwanza chini ya kanuni hii itachapishwa kabla ya mwaka wa tano wa maadhimisho ya siku ambayo Kanuni hizi zitaanza kutumika. (3) Ripoti zinazofuata zitachapishwa kwa kipindi kisichozidi miaka mitano. (4) Ripoti iliyoandaliwa na kuwasilishwa chini ya kanuni hii- (a) itaainisha malengo yanayokusudiwa kufikiwa na masharti ya udhibiti yaliyoanishwa chini ya kanuni ndogo ya (1)(a); (b) itatathmini kiwango ambacho malengo hayo yanafikiwa; (c) itatathmini endapo malengo yaliyoanishwa yana tija; na (d) pale ambapo malengo yanatija, ripoti itatathmini kiwango ambacho yanaweza inayohusisha kufikiwa kwa njia nyingine masharti mepesi ya udhibiti. - 20 Verify source ↗
Makosa na adhabu
AI-assisted research summary: If a ship enters or tries to enter the sea, any voyage, or Tanzanian waters while breaking the cited rules, the owner and master each commit an offence and may be fined or imprisoned.
20. Pale ambapo meli inaingia au kujaribu kuingia baharini au safari yoyote, au kuwasili ndani ya maji ya Tanzania, ikiwa imekiuka masharti yoyote ya Kanuni hizi au Sehemu B ya Sura ya III ya Mkataba wa Usalama unaotumika katika meli hiyo, mmiliki na nahodha kila mmoja atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani atatozwa faini isiyopungua dola za Marekani elfu tano au kiwango kinacholingana katika shilingi za Kitanzania au kifungo kwa kipindi kisichozidi miaka miwili na kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. 15 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio Ushughulikiaji wa malalamiko TS. Na. 338 la 2018 - 21 Verify source ↗
Kushughulikia malalamiko
AI-assisted research summary: A person dissatisfied with a decision under these regulations may apply to the Agency for review.
21. Mtu ambaye hajaridhika na uamuzi uliotolewa chini ya Kanuni hizi anaweza kuwasilisha maombi ya mapitio kwa Shirika kwa mapitio kwa mujibu wa Kanuni za Ushughulikiaji wa Malalamiko za Wakala wa Meli Tanzania. _______ JEDWALI _______ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5) MADARAJA YA MELI Mchanganuo wa Madaraja ya Meli Meli za Abiria Daraja la I meli zinazofanya safari zozote ndefu za kimataifa; Daraja la II meli zinazofanya safari fupi za kimataifa pekee; Daraja la II(A) meli zinazofanya safari za aina yoyote isipokuwa safari za kimataifa ambazo si- (i) meli za Daraja la III hadi VI(A) kama zilivyotafsiriwa katika Kanuni za Ujenzi wa Meli za Abiria: Meli za Daraja la III hadi VI(A) za Mwaka 1998; (ii) Meli za Daraja A, B, C au D kama zilivyotafsiriwa katika Kanuni za Meli za Abiria za Safari za Ndani za Mwaka 2000 na zinazofanya safari za ndani kwa madhumuni ya Kanuni hizo; Daraja la III Daraja la IV Daraja la V meli zinazojihusisha na safari pekee nyakati zikiwa si zaidi ya maili 70 baharini kutoka eneo la kuondokea na si zaidi ya maili 18 kutoka pwani ya Jamhuri ya Muungano, na ambazo ziko bahari wakati wa hali nzuri ya hewa na kipindi kilichozuiliwa; meli zinazofanya safari za maji katika Kundi A, B, C au D pekee; meli zinazofanya safari za maji katika Kundi A, B au C pekee; 16 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio Daraja la VI meli zinazofanya safari pekee na abiria wasiozidi 250 ndani ya meli, baharini au katika maji ya Kundi A, B, C, au D, kwa namna yoyote katika hali nzuri ya hewa na kipindi cha muda kilichozuiliwa, katika wakati meli haipo umbali wa maili 15, isipokuwa katika maji ya kundi lolote la A, B, C, au D, kutoka katika eneo la kuondokea lisilo zaidi ya maili 3 kutoka nchi kavu. Daraja la VI(A) meli inayobeba abiria wasiozidi 50 kwa safari za umbali usiozidi maili 6 kwenda au kutoka katika jamii zilizotengwa kwenye visiwa au pwani ya Jamhuri ya Muungano na ambazo haziingii kwa umbali usiozidi maili 3 kutoka nchi kavu. Meli zisizo za abiria Mchanganuo wa Madaraja ya Meli Daraja la VII meli, isipokuwa meli za Daraja la I, VII(A), VII(T), XI, na XII, zinazofanya safari yoyote ndefu ambayo ni ya kimataifa; Daraja la VII(A) meli zinazohusika na kusindika samaki au kuzikausha samaki, na meli zinazotumika kubeba watu walioajiriwa katika viwanda vya kusindika au kukausha samaki; Daraja la VII(T) meli za mafuta zinazofanya safari zozote ndefu za kimataifa; Daraja la VIII meli, isipokua meli za daraja la II, VIII(T), IX, XI na XII, zinazofanya safari fupi za kimataifa pekee; Daraja la VIII(A) meli isipokuwa meli za Daraja la II(A) hadi VI(A) kwa pamoja, VIII(A)(T), IX, IX(A), IX(A)(T), XI na XII, zinazofanya safari pekee ambazo sio safari za kimataifa; Daraja la VIII(T) Daraja VIII(A)(T) meli za mafuta zinafanya safari fupi za kimataifa pekee; meli za mafuta zisizofanya safari fupi za kimataifa pekee; Daraja la IX tagi na meli ya tenda, isipokua meli za Daraja la II, II(A), III, VI na VI(A), ambazo zinaingia baharini lakini hazifanyi safari ndefu za kimataifa; Daraja la IX(A) meli, isipokuwa meli za Daraja la IV hadi VI kwa pamoja, ambazo haziingii baharini; Daraja la IX(A)(T) meli za mafuta ambazo haziingii baharini; 17 Tangazola Serikali Na. 497 (Linaendelea.) Kanuni Za Vifaa vya Uokozi Na Mipangilio Daraja la XI meli zinazoelea, tofauti na meli za uvuvi na meli za Daraja la XII, ambazo zinaingia baharini; Daraja la XII meli za starehe zevye urefu wa mita 13.7 au zaidi. Dodoma, 28 Juni, 2023 MAKAME M. MBARAWA, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi 18
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Vifaa vya Uokozi na Mpangilio za Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in