Kanuni za Taratibu za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa za Mwaka 2023
These regulations are named the Entry Procedures in Restricted Areas Regulations, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Taratibu za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa za Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
These regulations are named the Entry Procedures in Restricted Areas Regulations, 2023. Kanuni hizi zinatumika kwa meli za Tanzania na meli nyingine zilizo ndani ya maji ya Tanzania, lakini hazitumiki kwa aina fulani za vyombo na meli zilizoorodheshwa kwenye vifungu vya исключение. This section defines key terms used in the regulations, including enclosed area, employer, ship types, Registrar, Notice of Maritime Travel, the Act, the Corporation, tons, and the Minister. Kila mwajiri lazima azingatie masharti ya Kanuni hizi, isipokuwa wajibu huo umepewa mtu mwingine. Pia, ambapo sharti linamweka jukumu mtu asiye na mamlaka juu ya jambo husika, jukumu hilo pia humwangukia mtu mwenye mamlaka juu ya jambo hilo. Nahodha wa meli lazima ahakikishe milango ya maeneo yaliyofungwa yasiyotumika imefungwa au kuzuiwa kuingia, isipokuwa kuingia humo kunahitajika.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Taratibu za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa za Mwaka 2023
Showing 13 of 13
- 1
AI-assisted research summary: These regulations are named the Entry Procedures in Restricted Areas Regulations, 2023.
1. Kanuni hizi zitakulikana kama Kanuni za Taratibu za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa za Mwaka 2023. - 2
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinatumika kwa meli za Tanzania na meli nyingine zilizo ndani ya maji ya Tanzania, lakini hazitumiki kwa aina fulani za vyombo na meli zilizoorodheshwa kwenye vifungu vya исключение.
2.-(1) Kanuni hizi zitatumika kwa meli za Tanzania, popote zilipo na meli nyingine zikiwa ndani ya maji ya Tanzania. (2) Bila kuathiri ujumla wa kanuni ndogo ya (1), Kanuni hizi hazitatumika kwa- (a) chombo cha starehe; (b) meli ambayo haina nahodha, mfanyakazi na mlinzi; (c) meli ya kivita au msaidizi wa majini; (d) meli inayomilikiwa au kuendeshwa na Serikali kwa huduma zisizo za kibiashara; na (e) vyombo visivyopungua urefu wa mita 24 au tani 50 za jumla. (3) Kwa madhumuni ya kanuni hii "chombo cha starehe" maana yake ni chombo ambacho kimsingi hutumika kwa michezo au burudani. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the regulations, including enclosed area, employer, ship types, Registrar, Notice of Maritime Travel, the Act, the Corporation, tons, and the Minister.
3. Katika Kanuni hizi- “eneo fungwa” maana yake ni eneo ambalo halijaundwa 3 Kanuni Za Taratibu Za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa Tangazo la Serikali Na. 499 (Linaendelea.) kukaliwa na mfanyakazi mfululizo na mojawapo au sifa zote zifuatazo: (a) nafasi ndogo za kuingia na kutoka; na (b) isiyoingiza hewa ya kutosha; ina “Kanuni” maana yake ni Kanuni ya Ufanyaji Kazi kwa Vitendo za Mabaharia Wanaosafiri Majini Toleo la 2015 kama ilivyorekebishwa mwaka 2022; “meli ya kubeba gesi” maana yake ni meli iliyotengenezwa au kubadilishwa kwa ajili ya kubeba gesi iliyoyeyushwa kwa wingi au bidhaa nyingine zilizoorodheshwa katika Jedwali la Sura ya 19 ya Kanuni za Kimataifa za Ujenzi na Vifaa vya Meli Zinazobeba Gesi Zilizoyeyushwa kwa Wingi au kwa kifupi chake kinachojulikana kama "Kanuni za IGC"; “meli ya mafuta” maana yake ni meli yoyote iliyotengenezwa au kubadilishwa kwa ajili ya kubeba mafuta au kemikali kwa wingi; “meli ya Tanzania” maana yake ni meli iliyosajiliwa au kupewa leseni chini ya masharti ya Sheria katika bandari ya Jamhuri ya Muungano; “Msajili” maana yake ni Msajili aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 31 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania; “mwajiri”, kuhusiana na meli, maana yake ni mtu ambaye kwa wakati huo anamwajiri baharia; “nahodha” inajumuisha mtu yeyote isipokuwa rubani mwenye amri au msimamizi wa meli, ndege ya baharini au chombo kingine kinapokua juu au karibu na maji; “Notisi ya Usafiri Majini” maana yake ni Notisi ya Usafiri Majini iliyotolewa na Msajili; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Usafiri Majini; “Shirika” maana yake ni Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania lililoanzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania; “tani” maana yake ni tani za jumla, na tani za jumla za meli yenye tani mbadala zitachukuliwa kuwa kubwa zaidi ya tani hizo; na 4 Sura ya 415 Sura ya 165 Sura ya 415 Kanuni Za Taratibu Za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa Tangazo la Serikali Na. 499 (Linaendelea.) Watu ambao majukumu yamebainishwa “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya usafiri majini. SEHEMU YA PILI MASHARTI YA MAENEO FUNGWA
Part
SEHEMU YA PILI
- 4
AI-assisted research summary: Kila mwajiri lazima azingatie masharti ya Kanuni hizi, isipokuwa wajibu huo umepewa mtu mwingine. Pia, ambapo sharti linamweka jukumu mtu asiye na mamlaka juu ya jambo husika, jukumu hilo pia humwangukia mtu mwenye mamlaka juu ya jambo hilo.
4.-(1) Itakuwa ni wajibu kwa kila mwajiri kuzingatia masharti ya Kanuni hizi, isipokuwa pale ambapo wajibu huo utabainishwa kwa mtu mwingine yeyote. (2) Endapo sharti lolote la Kanuni hizi limetoa jukumu kwa mtu asiye na mamlaka na jambo husika kwa sababu hana wajibu katika uendeshaji wa meli, jukumu hilo litakuwa pia kwa mtu yeyote mwenye mamlaka na jambo hilo. Milango ya maeneo fungwa - 5
AI-assisted research summary: Nahodha wa meli lazima ahakikishe milango ya maeneo yaliyofungwa yasiyotumika imefungwa au kuzuiwa kuingia, isipokuwa kuingia humo kunahitajika.
5. Nahodha wa meli atahakikisha kwamba milango yote ya maeneo fungwa yasiyotumika kwenye meli yanafungwa au vinginevyo yamezuiwa kuingiwa, isipokua kama ni muhimu kuingia humo. Kuingia kwenye maeneo fungwa - 6
AI-assisted research summary: Ship owners, employers, and related persons must ensure safe systems for confined-space entry and work on board, carry out risk assessments, and follow the specified rules; the captain must make sure those systems are observed, and no one may enter or stay in a confined space unless the systems are followed.
6.-(1) Mmiliki wa meli, mwajiri na mtu mwingine yeyote aliyerejewa chini ya kanuni ya 5 atahakikisha kwamba- (a) mifumo ya kazi zilizowekwa na zinazotumika melini, kuhusiana na afya na usalama kazini, inajumuisha mifumo ya kuingia na kufanya kazi katika maeneo fungwa; na (b) tathmini za vihatarishi vya kuingia na kufanya kazi katika maeneo fungwa zinafanyika. (2) Nahodha atahakikisha kwamba mifumo ya kazi iliyoainishwa katika kanuni ndogo ya (1)(a) inazingatiwa ndani ya meli. (3) Mtu hataingia au kubaki katika eneo fungwa, isipokuwa kwa mujibu wa mifumo ya kazi iliyoainishwa katika kanuni ndogo ya (1)(a). (4) Mmiliki wa meli, mwajiri na mtu mwingine yeyote aliyerejewa chini ya kanuni ya 5, katika kutekeleza majukumu yao chini ya kanuni hii, atazingatia kikamilifu kanuni na miongozo iliyomo kwenye Sura ya 10 ya 5 Kanuni Za Taratibu Za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa Tangazo la Serikali Na. 499 (Linaendelea.) Mazoezi utayari ya Kanuni. - 7
AI-assisted research summary: The captain must make sure certain seamen take part in onboard readiness drills.
7.-(1) Nahodha atahakikisha kwamba mabaharia ambao majukumu yao yanajumuisha kuingia au kuokoa kutoka kwenye maeneo fungwa melini, wanashiriki kwenye mazoezi ya utayari yanayozingatia masharti ya kanuni ndogo ya (3). (2) Mazoezi ya utayari yaliyoainishwa chini ya kanuni ndogo ya (1) yatarekodiwa kwenye kitabu rasmi cha kumbukumbu. (3) Mazoezi ya utayari- (a) yatafanyika melini kwa kipindi kisichozidi miezi miwili; (b) yatapangwa na kufanyika katika hali ya usalama, kwa kuzingatia mwongozo katika Sura ya 15 ya Kanuni; (c) ni pamoja na- (i) ukaguzi na matumizi ya- (aa) vifaa vya kinga binafsi vinavyohitajika kuingia; mawasiliano; kanuni ya 8; (bb) vifaa na taratibu za (cc) vifaa vilivyoainishwa chini ya (dd) vifaa na taratibu za uokoaji; na (ii) mafunzo ya utoaji wa huduma ya kwanza na mbinu za uokozi. Vifaa vya kupima fungwa - 8
AI-assisted research summary: Kwa meli zenye eneo linalofikika, mmiliki wa meli na mwajiri lazima wahakikishe kuna vifaa vinavyobebeka vya kupima hali ya hewa na kwamba vinafanya kazi vizuri kabla ya mtu kuingia eneo hilo.
8. Katika meli ambazo zina eneo linalofikika, mmiliki wa meli na mwajiri watahakikisha kwamba- (a) meli imebeba vifaa vinavyobebeka vya kupima hali ya hewa ambavyo vinamwezesha baharia kupima mgandamizo wowote wa oksijeni, gesi zinazolipuka au mivuke, salfidi hidrojeni na monoksidi kaboni ndani ya eneo hilo kabla baharia yeyote hajaingia katika sehemu hiyo; (b) kifaa kilichoainishwa katika aya ya (a)- (i) kinatunzwa katika utaratibu mzuri wa kufanya kazi; na 6 Kanuni Za Taratibu Za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa Tangazo la Serikali Na. 499 (Linaendelea.) (ii) pale inapohitajika, kinatengenezwa mara kwa mara na kupimwa kulingana na mapendekezo ya mtengenezaji. Misamaha - 9 Verify source ↗
Watu ambao majukumu yamebainishwa
AI-assisted research summary: Shirika linaweza kutoa msamaha wa kutotumika kwa masharti ya kanuni za 7 na 8 kwa meli fulani zikikidhi masharti yaliyotajwa; pia mmiliki wa meli na mwajiri lazima waandae mazoezi ya utayari na kuyarekodi.
9.-(1) Shirika linaweza, kwa masharti itakayotoa, kutoa misamaha ya kutotumika kwa masharti ya kanuni ya 7 na 8 kwa meli binafsi au aina ya meli ambazo- (a) ni chini ya tani 500; (b) si meli ya SOLAS au daraja la meli za SOLAS; na (c) zinakidhi masharti yaliyowekwa chini ya kanuni ndogo ya (2). (2) Meli itasamehewa kutotumika kwa masharti kanuni za 7 na 8 chini ya kanuni ndogo ya (1) endapo inakidhi masharti yafuatayo: (a) meli au daraja la meli inaendeshwa kwa mujibu wa- (i) ratiba inayoitaka kurudi bandarini katika kipindi kisichozidi masaa 72; na (ii) utaratibu ambao unahakikisha kwamba hakuna baharia melini anayeingia kwenye eneo fungwa lolote wakati meli hiyo iko baharini; (b) hakuna ulazima wa kuzingatia masharti ya kanuni ya 7(3)(a) kutokana na- (i) utaratibu wa uendeshaji wa meli au daraja la meli; au (ii) mpangilio wa wafanyakazi melini au daraja la meli; na (c) hakuna eneo fungwa kwenye meli au daraja la meli ambalo baharia anapaswa katika hali ya kawaida kuhitaji kuingia, isipokuwa katika mazingira ya kipekee. (3) Endapo meli au daraja la meli limesamehewa kutotumika kwa masharti ya kanuni za 7 na 8 baada ya kukidhi masharti yaliyoainishwa katika kanuni ndogo ya (2)(b) au (c), mmiliki wa meli na mwajiri watahakikisha kwamba- (a) mabaharia wanashiriki katika mazoezi ya utayari sawa na yale yaliyoainishwa chini ya 7 Kanuni Za Taratibu Za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa Tangazo la Serikali Na. 499 (Linaendelea.) kanuni ya 7(3)(b) na (c)- (i) iwapo ni kanuni ndogo ya (3)(b), katika namna nyingine na vipindi kadri inavyoweza kutekelezeka; na (ii) iwapo ni kanuni ndogo ya (3)(c), endapo kuingia kunahitajika katika mazingira ya kipekee, kabla ya ruhusa ya kuingia; na (b) mazoezi ya utayari yaliyoainishwa chini ya kanuni ya 7(2), yanarekodiwa katika kitabu rasmi cha kumbukumbu. (4) Msajili anaweza, kwa kutoa notisi, kubadili au kufuta msamaha wowote uliotolewa chini ya kanuni hii. (5) Msamaha, mabadiliko katika msamaha au ufutaji wa msamaha uliofanyika chini ya kanuni hii- (a) utakuwa katika maandishi; (b) utaainisha tarehe ya kuanza kutumika; na (c) kuhusiana na msamaha, utataja masharti, kama yapo, ambayo yametolewa. (6) Sharti kwamba msamaha, mabadiliko katika msamaha au ufutaji wa msamaha uliotolewa chini ya kanuni hii kuwa kwa maandishi litatimia pale ambapo maudhui ya msamaha huo- (a) yamewekwa kwa njia ya kielektroniki; (b) yamepokelewa kwa mfumo unaosomeka; na (c) yanafaa kutumika kwa marejeo yanayofuata. SEHEMU YA TATU MAKOSA NA ADHABU
Part
SEHEMU YA TATU
- 10 Verify source ↗
Makosa na adhabu
AI-assisted research summary: A master, ship owner, employer, or other person named in the earlier regulations commits an offence if they fail to comply with the listed regulations, and conviction may lead to a fine, imprisonment, or both.
10.-(1) Nahodha ambaye atashindwa kutimiza masharti yoyote ya kanuni ya 5 au 7(1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani atatozwa faini isiyopungua dola za Marekani elfu moja au kiwango kinacholingana katika shilingi za Kitanzania au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi sita na kisichopungua miezi mitatu au vyote kwa pamoja. (2) Mmiliki wa meli, mwajiri au mtu mwingine yeyote aliyeainishwa katika kanuni ya 4 ambaye atashindwa kuzingatia matakwa yoyote ya kanuni ya 6(1) 8 Makosa adhabu na Kanuni Za Taratibu Za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa Tangazo la Serikali Na. 499 (Linaendelea.) atakuwa anatenda kosa na akitiwa hatiani atatozwa faini isiyopungua dola za Marekani elfu moja au kiwango kinacholingana katika shilingi za Kitanzania au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi sita na kisichopungua miezi mitatu au vyote kwa pamoja. (3) Mmiliki wa meli au mwajiri ambaye atashindwa kutimiza masharti yoyote ya kanuni ya 8 au 9(3) atakuwa anatenda kosa na akitiwa hatiani atatozwa faini isiyopungua dola za Marekani elfu moja au kiwango kinacholingana katika shilingi za Kitanzania au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi sita na kisichopungua miezi mitatu au vyote kwa pamoja. SEHEMU YA NNE MASHARTI YA JUMLA Uzuiaji
Part
SEHEMU YA NNE
- 11 Verify source ↗
Uzuiaji
AI-assisted research summary: Kama meli haifuati masharti ya Kanuni hizi, inaweza kuzuiliwa. Mtu anayeizuia lazima ampe nahodha notisi ya kuzuia, na Shirika lazima liwajulishe kwa maandishi mamlaka za nchi ya usajili wa meli nyingine iliyozuiliwa; kama hilo haliwezekani, liwasiliane na ubalozi au mwakilishi wa kidiplomasia wa nchi hiyo.
11.-(1) Meli ambayo haitazingatia masharti ya Kanuni hizi inaweza kuzuiliwa. (2) Pale ambapo meli imezuiliwa chini ya kanuni ndogo ya (1), masharti ya kifungu cha 409 cha Sheria yatatumika, isipokuwa masharti yaliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (7) hayatatumika. (3) Pale ambapo meli inapaswa kuzuiliwa chini ya kanuni hii, mtu anayeizuia meli hiyo atatoa notisi ya kuzuia kwa nahodha ambayo- (a) inaeleza sababu za kuwekwa kizuizini; na (b) inahitaji masharti ya notisi kuzingatiwa hadi meli itakapoachiwa na mtu yeyote aliyetajwa chini ya kifungu cha 409 (1) cha Sheria. (4) Pale ambapo meli nyingine ambayo si ya Tanzania imezuiliwa, Shirika litaifahamisha mara moja mamlaka ya nchi ya usajili wa meli husika kwa maandishi. (5) Pale ambapo haiwezekani kuijulisha mamlaka ya nchi ya usajili wa meli kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (4), Shirika litaifahamisha ofisi ya Ubalozi wa mamlaka ya nchi iliyosajili meli, au endapo hakuna ofisi ya Ubalozi, mwakilishi wa karibu wa kidiplomasia wa nchi iliyosajili meli. (6) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo ya (4) na (5), "mamlaka ya usajili" kuhusiana na meli maana yake ni 9 Kanuni Za Taratibu Za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa Tangazo la Serikali Na. 499 (Linaendelea.) Nchi ambayo meli inastahili kupeperusha bendera yake. Tathmini na utoaji wa taarifa - 12 Verify source ↗
13. Ushughulikiaji wa malalamiko
AI-assisted research summary: Msajili lazima afanye tathmini ya masharti ya udhibiti ya Kanuni hizi, aandaye taarifa ya matokeo, na awasilishe taarifa hiyo kwa Waziri.
12.-(1) Msajili- (a) atafanya tathmini ya masharti ya udhibiti yaliyomo katika Kanuni hizi; taarifa (b) atandaa inayoainisha hitimisho la tathmini; na (c) atawasilisha taarifa kwa Waziri. (2) Taarifa ya kwanza chini ya kanuni hii itachapishwa kabla ya mwaka wa tano wa maadhimisho wa siku ambayo Kanuni hizi zitaanza kutumika. (3) Taarifa zinazofuata zitachapishwa kwa kipindi kisichozidi miaka mitano. (4) Taarifa iliyoandaliwa na kuwasilishwa chini ya kanuni hii: (a) itaanisha malengo yanayokusudiwa kufikiwa na masharti ya udhibiti yaliyoainishwa chini ya kanuni ndogo ya (1)(a); (b) itatathmini kiwango ambacho malengo hayo yanafikiwa; (c) itatathmini endapo malengo yaliyoainishwa yana tija; na (d) pale ambapo malengo yanatija, kiwango itatathmini kufikiwa kwa njia nyingine masharti mepesi ya udhibiti. ambacho taarifa yanaweza inayohusisha Ushughulikiaji wa malalamiko TS. Na. 338 ya 2018 - 13 Verify source ↗
Ushughulikiaji wa malalamiko
AI-assisted research summary: A dissatisfied person may submit a review application to the Agency.
13. Mtu ambaye hajaridhika na uamuzi uliotolewa chini ya Kanuni hizi anaweza kuwasilisha maombi ya mapitio kwa Shirika kwa mapitio kwa mujibu wa Kanuni za Ushughulikiaji wa Malalamiko za Wakala wa Meli Tanzania. Dodoma, 28 Juni, 2023 MAKAME M. MBARAWA, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi 10
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Taratibu za Uingiaji Katika Maeneo Fungwa za Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in