Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam za Mwaka 2024
Read the stored legal text, review its version and status evidence, or ask LexChat a question grounded in exact provisions.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This page preserves the statute’s identified version, provision structure, official source link, and stored legal text for reading and research.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam za Mwaka 2024
Showing 1 of 1
- document Verify source ↗
Document text
Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) TANGAZO LA SERIKALI Na. 1075 la tarehe 20/12/2024 SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA MIJI) (SURA YA 288) __________ KANUNI ZA KUDUMU _________ (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 42(1)) KANUNI ZA KUDUMU ZA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM ZA MWAKA 2024 MPANGILIO WA KANUNI SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI 1. Jina. 2. Tafsiri. SEHEMU YA PILI MIKUTANO YA HALMASHAURI 3. Mikutano ya Kawaida ya Halmashauri. 4. Utaratibu wa uchaguzi. 5. Mkutano Maalum wa Halmashauri. 6. Utaratibu wa kuwasilisha rufaa. 7. Mkutano wa bajeti. 8. Mkutano wa mwaka. 9. Taarifa ya mkutano. 10. Akidi katika mikutano ya halmashauri. SEHEMU YA TATU TARATIBU ZA MIKUTANO 11. Uchaguzi wa Meya na Naibu Meya Halmashauri. 12. Uongozaji wa Mikutano ya Halmashauri. 13. Kumbukumbu ya mahudhurio. 1 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) 14. Kuruhusu watu na vyombo vya habari kwenye mikutano ya Halmashauri. 15. Utaratibu wa shughuli za Mikutano. 16. Kuthibitisha muhtasari. 17. Hoja za Meya. 18. Taratibu za Majadiliano. 19. Fujo zinazosababishwa na Wajumbe. 20. Fujo zinazosababishwa na Umma. 21. Hoja za Marekebisho ya Hoja. 22. Hoja zinazoweza kutolewa bila taarifa. 23. Haki ya kujibu. 24. Maswali. 25. Maswali ya papo kwa papo. 26. Taarifa za Kamati. 27. Taarifa kutoka kwenye Kata. 28. Uhuru wa Kutoa mawazo wakati wa majadiliano. 29. Kauli zenye kashfa. 30. Maamuzi ya Mikutano ya Halmashauri. 31. Mwaliko kwa wasiokuwa Wajumbe kushiriki na kuzungumza kwenye vikao vya Halmashauri 32. Mihtasari ya kamati ya maendeleo ya kata na mitaa. 33. Mihutasari ya Halmashauri kupelekwa kwa Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa. 34. Hoja kuhusu matumizi. 35. Kupokelewa kwa taarifa ya Kamati. 36. Kuidhinishwa kwa taarifa ya Kamati. 37. Uhalali wa majadiliano ya Halmashauri. 38. Uwezo wa Halmashauri kujigeuza kuwa Kamati ya Halmashauri nzima. 39. Hoja zinazohusu watumishi wa Halmashauri. 40. Ushiriki wa umma. 41. Uahirishaji wa vikao. SEHEMU YA NNE KAMATI 42. Kamati za Kudumu. 43. Meya kuwa Mjumbe wa Kamati zote. 44. Uwezo wa Kamati. 45. Kamati za Pamoja. 46. Kukasimu madaraka kwenye Kamati. 2 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) 47. Kamati Ndogo. 48. Mikutano ya Kamati. 49. Mwenyekiti wa Kamati. 50. Mkutano maalum wa Kamati. 51. Agenda za Kamati. 52. Mahudhurio katika Mikutano ya Kamati. 53. Mtoa hoja kualikwa kwenye Mkutano wa Kamati. 54. Waalikwa wasiokuwa Wajumbe kuhudhuria na kushiriki katika Mikutano ya Kamati. 55. Mahudhurio ya Umma na Vyombo vya Habari kwenye Mikutano ya Kamati na Kamati Ndogo. 56. Athari za nafasi wazi kwenye Kamati. 57. Akidi kwenye Mikutano ya Kamati. 58. Kanuni za kudumu kutumika katika Mikutano ya Kamati. 59. Upigaji kura kwenye Mikutano ya Kamati. 60. Muhtasari wa Kamati. 61. Kufikiriwa upya maamuzi. 62. Kutunza siri za majadiliano ya Kamati na Kamati Ndogo. 63. Kujiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Kamati. 64. Kujiuzulu ujumbe wa Kamati na kujazwa kwa nafasi iliyoachwa wazi. SEHEMU YA TANO UNUNUZI WA VIFAA, UPATIKANAJI WA HUDUMA NA UJENZI 65. Taratibu za uagizaji. 66. Kumbukumbu za majadiliano yanayohusu uagizaji. 67. Uzuiaji wa rushwa. 68. Usimamizi wa Mikataba. 69. Uvunjaji wa Mkataba. 70. Rejesta ya Mikataba. 71. Diwani au Afisa kutokuwa na maslahi kwenye Mikataba. SEHEMU YA SITA MASUALA MENGINE 72. Kiapo cha kukubali wadhifa. 73. Majukumu ya Diwani. 74. Nafasi wazi. 75. Kutokuwepo kwa Wajumbe. 76. Taratibu za kutunga Sheria Ndogo. 3 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) 77. Ukaguzi wa nyaraka. 78. Uanzishaji wa Bodi ya Huduma. 79. Diwani kutembelea maeneo, shughuli mbalimbali za ujenzi. 80. Uhifadhi wa lakiri ya Halmashauri. 81. Utiaji muhuri kwenye nyaraka. 82. Uandikishaji wa anwani. 83. Uteuzi wa Wajumbe kwenye taasisi za nje. 84. Kumwondoa Meya madarakani. SEHEMU YA SABA POSHO KWA WAJUMBE 85. Aina za posho. 86. Posho endapo Mkutano utaahirishwa. SEHEMU YA NANE MABADILIKO KWENYE KANUNI ZA KUDUMU 87. Kusitisha utumiaji wa Kanuni za Kudumu. 88. Marekebisho na mabadiliko ya Kanuni za Kudumu. 89. Kanuni za Kudumu kutolewa kwa Wajumbe. 90. Kutafsiri Kanuni za Kudumu. SEHEMU YA TISA ZIARA ZA WAJUMBE 91. Ziara za wajumbe. 92. Wimbo wa Taifa, dua au sala ya kuiombea Halmashauri. 93. Kufutwa kwa Kanuni. _______ MAJEDWALI _______ 4 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) KWA KUWA kauli mbiu ya Halmashauri ni kuendesha shughuli kwa namna inayozingatia demokrasia, ufanisi, tija, ushirikishwaji, uwazi na uwajibikaji; NA KWA KUWA jukumu la Halmashauri ni kuimarisha demokrasia katika ngazi zote na kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia ufanisi, usawa, haki na kwa namna inayochochea maendeleo ya maeneo yaliyo chini ya mamlaka ya Halmashauri kwa kuwashirikisha wananchi; NA KWA KUWA madhumuni ya Kanuni za Kudumu hizi ni kuweka utaratibu wa namna Halmashauri itakavyoendesha Mikutano na shughuli zake kwa kuzingatia misingi ya utawala bora; SASA BASI, Kanuni za Kudumu hizi zinaelekeza kama ifuatavyo: SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI Jina Tafsiri Sura ya 288 1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam za Mwaka 2024. 2. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa wa Serikali za Mitaa” maana yake ni mtu ambaye ameajiriwa au ambaye yumo katika Utumishi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na ambaye anashika au anakaimu katika nafasi ya menejimenti; “akidi” maana yake ni idadi ya Madiwani itakayokamilika baada ya kujiorodhesha katika rejesta ya Mahudhurio ya Mkutano ambayo itaruhusu kufanya maamuzi ya Mkutano kwa mujibu wa kanuni ya 9, 49 au 56; “chama” maana yake ni chama cha siasa chenye uwakilishi katika Baraza la Madiwani; “Diwani” maana yake ni Mjumbe wa Halmashauri aliyetajwa kwa mujibu wa Kifungu 24(2) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji); “fujo” maana yake ni kitendo chochote kinachoweza kufanywa na Mjumbe au Mshiriki wa Vikao vya Halmashauri au 5 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Kamati ya Kudumu ambacho ni kinyume na taratibu za uendeshaji wa vikao, kinachoweza kuvuruga kikao. Mfano kuongea bila ruhusa ya Mwenyekiti, kutoa lugha isiyofaa, kutoa kauli yenye maudhi, kuingia kwenye kikao akiwa umelewa, kuingia na silaha, kutoa lugha ya kashfa, kukaidi amri ya Mwenyekiti, kukaidi kutoka nje pale fujo kutoka alizosababisha; anapoamriwa kutokana na “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; “Kamati”- (a) inapotumika kuhusiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliyoanzishwa au iliyoteuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam chini ya Sheria; ina maana ya Kamati (b) inapotumika kuhusiana na Kamati ya Maendeleo ya Kata ina maana ya Kamati hiyo; (c) inapotumika kuhusiana na Kamati Ndogo maana yake ni Kamati Ndogo hiyo iliyoteuliwa na Kamati; (d) inapotumika kuhusiana na Kamati nyingine ina maana ya Kamati hiyo; na (e) kwa maana ya Bodi ya Zabuni ni Katibu wa Bodi ya Zabuni. “kura ya siri” maana yake ni kura itakayopigwa katika eneo la faragha lililotengwa kwa madhumuni ya kupiga kura, eneo ambalo halitapungua umbali wa mita tano (5) kutoka kwa msimamizi wa kura; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “Mjumbe” maana yake ni Mjumbe wa Halmashauri kama ilivyoainishwa na kifungu cha 27 cha Sheria; “Meya” maana yake ni Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es inajumuisha Naibu Meya wakati Salaam anapotekeleza majukumu ya Meya kwa mujibu wa Kanuni hizi; na “Mwenyekiti”- (a) kwa madhumuni ya Kamati, Bodi au Kamati Ndogo maana yake ni Mwenyekiti wa Kamati, Bodi au Kamati Ndogo; 6 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (b) kwa madhumuni ya Bodi ya Zabuni maana yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni; Sura ya 288 “Sheria” maana yake ni Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji); “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na masuala ya Serikali za Mitaa. Mikutano ya Kawaida ya Halmashau ri SEHEMU YA PILI MIKUTANO YA HALMASHAURI 3.-(1) Mikutano ya Kawaida ya Halmashauri itafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, na itafanyika mahali, tarehe na katika muda kama utakavyokua umepangwa katika kalenda ya Mikutano ya Halmashauri. (2) Mkutano wa kwanza wa kawaida wa Halmashauri utafanyika baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Madiwani wa Kata na uteuzi wa Madiwani wa Viti maalumu, na utafanyika mahali, siku na katika muda utakaopangwa na Mkurugenzi, ilimradi Mkurugenzi atapaswa kuitisha Mkutano huo ndani ya siku thelathini (30) kuanzia tarehe ya matokeo ya uchaguzi wa Madiwani wa Kata na Uteuzi wa Madiwani Viti Maalum yanapotangazwa na Tume ya Uchaguzi ambapo moja ya agenda za Mkutano huo ni kumchagua Meya, Naibu Meya na Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Halmashauri. (3) Katika Mkutano huo Mkurugenzi wa Halmashauri atawasilisha taarifa ya kumbukumbu ya maamuzi ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri zilizofanyika katika kipindi ambacho Baraza la Madiwani lilivunjwa. Wajumbe wa Baraza watapokea na kujadili bila kubatilisha maamuzi yaliyokwisha amuliwa. Utaratibu wa uchaguzi 4. Uchaguzi wa Meya na Naibu Meya utafanyika kwa kupiga kura za siri na upigaji wa kura utafanyikia sehemu ya faragha umbali usiopungua mita (5) kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi na mpiga kura atachukua karatasi ya kupiga kura kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi. Mkutano maalum wa 5.-(1) Mkutano Maalum wa Halmashauri unaweza kuitishwa na Meya ndani ya siku ishirini na moja baada ya 7 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Halmashau ri Utaratibu wa kuwasilisha rufaa kupokea maombi ya maandishi yaliyosainiwa na si pungufu ya theluthi moja ya Wajumbe wote kutaka Mkutano huo ufanyike na maombi hayo yaeleze wazi madhumuni ya kuitishwa kwa Mkutano Maalum. (2) Endapo agenda ya Mkutano huo itahusu kumuondoa madarakani Meya, Mkutano huo utaitishwa na Mkurugenzi baada ya kupokea maombi yaliyosainiwa na Wajumbe wa Halmashauri wasiopungua theluthi mbili ya Wajumbe wote. (3) Baada ya Mkurugenzi kupokea maombi kutaka kufanyika kwa Mkutano wa kujadili agenda ya kumuondoa madarakani Meya, Mkurugenzi atamtaarifu Meya tuhuma na sababu za kutaka kuondolewa Umeya na kumtaka aandae majibu ya tuhuma ndani ya siku tano (5) baada ya kupokea tuhuma hizo. (4) Mkurugenzi katika muda wa siku tatu (3) baada ya kupokea maelezo ya utetezi kutoka kwa Meya, atawasilisha kwa Mkuu wa Mkoa tuhuma pamoja na maelezo ya utetezi. (5) Mkuu wa Mkoa baada ya kupokea taarifa ya Mkurugenzi ndani ya muda wa siku tano (5) ataunda Timu ya Uchunguzi ambayo itakuwa na wajumbe wasiopungua watatu (3) na wasiozidi watano (5). (6) Timu ya Uchunguzi itatakiwa kukamilisha Uchunguzi katika muda wa siku kumi na nne (14) na kuwasilisha taarifa hiyo kwa Mkuu wa Mkoa. (7) Baada ya Mkuu wa Mkoa kupata taarifa ya Timu ya Uchunguzi atairudisha taarifa hiyo kwa Mkurugenzi ambaye naye katika muda wa siku kumi na nne (14) ataiwasilisha kwenye Kikao cha Baraza kwa uamuzi wa tuhuma hizo. (8) Endapo Meya hataridhika na uamuzi wa Baraza, rufaa kwa Waziri kuhusu utaratibu uliotumika atakata kumuondoa madarakani na sio vinginevyo. 6.-(1) Utaratibu na kushughulikia rufaa iliyowasilishwa na Meya ni ule ulioelezwa kwenye Taratibu za kumuondoa madarakani Meya wa Halmashauri. utakaotumika kuwasilisha (2) Iwapo Meya anakataa kuitisha Mkutano maalum wa Halmashauri baada ya kupokea maombi ya kutakiwa kufanya hivyo, maombi yaliyosainiwa na Wajumbe wa Halmashauri wasiopungua theluthi moja ya Wajumbe wote wakionesha sababu ya kuitisha Mkutano huo maalum na kuwasilishwa kwake, au iwapo bila kukataa, Meya, ndani ya kipindi cha siku 8 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Mkutano wa bajeti Mkutano wa mwaka saba ataendelea kutoitisha Mkutano huo maalum baada ya kupokea ombi la kuitisha Mkutano huo maalum, basi theluthi mbili ya Wajumbe waliotia saini na kuwasilisha kwa Mkurugenzi maombi yao wanaweza kuitisha Mkutano huo maalum mara moja. (3) Taarifa ya Mkutano maalum itatolewa angalau saa ishirini na nne kabla ya Mkutano. (4) Shughuli nyingine yoyote haitajadiliwa katika mkutano maalum wa Halmashauri isipokuwa ile iliyoelezwa katika taarifa ya kuitishwa kwa mkutano huo. 7. Kutakuwa na mkutano wa Halmashauri wa bajeti utakaofanyika kwa muda wa siku mbili mfululizo na utafanyika miezi miwili kabla ya mwaka wa fedha kumalizika na utajadili masuala yafuatayo: (a) utekelezaji wa mipango na bajeti ya mwaka uliopita; (b) mipango na bajeti ya mwaka unaofuata. 8.- (1) Mkutano wa mwaka wa Halmashauri utafanyika tarehe, mahali na muda utakaopangwa na Halmashauri katika kalenda ya mikutano na utaitishwa na Mkurugenzi baada ya kuwasiliana na Meya wa Halmashauri. (2) Mikutano yote ya Baraza itapangwa na Baraza la Madiwani kwa kuzingatia ratiba ya vikao vya Bunge ili kuwezesha wabunge kuhudhuria mikutano ya Baraza la Madiwani. Endapo italazimika kuitishwa kwa mkutano wa Baraza wakati wa vikao vya Bunge, Mkurugenzi atamjulisha au kuwajulisha wabunge husika kuhusu kikao hicho ili wahudhurie. (3) Mkutano wa kwanza wa Uchaguzi wa Meya, Naibu Meya na Wajumbe wa Kamati utaongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri atakuwa Katibu. (4) Katika Mkutano wa kawaida wa Mwaka, Halmashauri itajadili masuala yafuatayo: (a) kumchagua Naibu Meya; (b) kuteua Wajumbe wa Kamati za Kudumu; (c) kujadili taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa Halmashauri kwa Mwaka uliopita;na (d) kupitisha ratiba ya vikao vya Halmashauri na Kamati za Halmashauri. 9 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Taarifa ya mkutano Akidi katika mikutano ya Halmashau ri 9.-(1) Mkurugenzi atatoa taarifa ya mkutano kwa maandishi kwa kila Mjumbe katika muda usiopungua siku saba (7) akieleza mahali, siku na saa ya Mkutano unaokusudiwa na masuala yatakayojadiliwa katika Mkutano huo. (2) Taarifa ya mkutano itaambatana na nyaraka au kumbukumbu muhimu zitakazotumika katika m kutano huo. (3) Isipokuwa kwa idhini ya Meya na au ya idadi ya Wajumbe isiyopungua robo tatu ya wajumbe waliohudhuria mkutano, shughuli yoyote haitafanywa katika mkutano wa Halmashauri mbali na shughuli zilizotajwa katika mwaliko wa mkutano huo. 10.-(1) Mkutano wa kawaida wa Halmashauri hautafanyika isipokuwa kama kutakuwepo idadi ya Wajumbe isiyopungua nusu ya Wajumbe wote waliohudhuria na kujiandikisha kwenye daftari la mahudhurio. (2) Akidi katika Mikutano maalum ya Halmashauri itakuwa ni theluthi mbili ya Wajumbe wote wa Halmashauri na itahesabiwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano. (3) Akidi katika Mkutano wa kawaida wa Mwaka na Mkutano wa kwanza wa Halmashauri itakuwa theluthi mbili ya Wajumbe wote wa Halmashauri. (4) Endapo Wajumbe waliohudhuria Mkutano hawatafikia akidi ya Mkutano, Mkurugenzi atauahirisha Mkutano huo na kuitisha tena ndani ya siku saba (7) na endapo akidi haitatimia tena, idadi yoyote ya Wajumbe waliohudhuria itatengeneza akidi ya Mkutano na Mkurugenzi atamjulisha Waziri kuwepo kwa hali hiyo. (3) Akidi katika Mkutano Maalum wa Halmashauri itakuwa ni theluthi mbili ya wajumbe wote wa Halmashauri na itahesabiwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano. (4) Akidi katika Mkutano wa kawaida wa Mwaka na Mkutano wa kwanza wa Halmashauri itakuwa theluthi mbili ya Wajumbe wote wa Halmashauri. SEHEMU YA TATU TARATIBU ZA MIKUTANO Uchaguzi wa na Meya 11.-(1) Meya na Naibu Meya watachaguliwa na wajumbe, kutokana na wajumbe wa Halmashauri kwa kura ya 10 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Naibu Meya wa Halmashauri siri itakayopigwa na Mjumbe mmoja mmoja kwenye eneo la faragha litakalotengwa umbali usiopungua mita tano (5) kutoka mahali alipoketi Msimamizi wa Uchaguzi. (2) Mjumbe kabla ya kwenda sehemu ya faragha kwa ajili ya kupiga kura, atapatiwa karatasi ya kupigia kura na Msimamizi wa Uchaguzi kutoka katika chombo maalum kitakachowekwa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi, na atakwenda moja kwa moja kupiga kura kwenye sehemu ya faragha. (3) Mtu atatangazwa kuchaguliwa kuwa Meya au Naibu Meya iwapo atapata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa. (4) Iwapo wakati wa kumchagua Meya au Naibu Meya, jina moja tu limependekezwa, Wajumbe watapiga kura za siri za “ndiyo” au “hapana”na endapo kura za “ndiyo” zitazidi asilimia hamsini ya kura zote zilizopigwa basi mgombea atatangazwa kuwa Meya au Naibu Meya. (5) Iwapo kura za “Hapana” zitazidi asilimia hamsini ya la mgombea mwingine zote kura jina litapendekezwa kwa njia na utaratibu uliotumika hapo awali. zilizopigwa, (6) Iwapo kura zitafanana, uchaguzi utarudiwa kwa mara ya pili na endapo hata baada ya kurudia uchaguzi kura zimefanana, Baraza litaamua kugawana muda wa kuwa madarakani kwa wagombea hao ambao kura zao zimefanana. (7) Kama itatokea nafasi wazi ya Meya au Naibu Meya, Halmashauri itamchagua Meya au Naibu Meya katika muda wa siku zisizozidi sitini (60) tangu nafasi hiyo ilipotokea. Uongozaji wa Mikutano ya Halmashauri 12.-(1) Mkutano wa Halmashauri utaongozwa na:- (a) Meya; au (b) ikiwa Meya hayupo, Naibu Meya; au (c) ikiwa Meya na Naibu Meya wote hawapo, au kama Meya na Naibu Meya wote hawawezi kuongoza Mkutano, Mjumbe yeyote atachaguliwa na Wajumbe kutoka miongoni mwa Wajumbe waliohudhuria kwa ajili ya kuongoza Mkutano huo; (d) Wajumbe wawapo ndani ya ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri watavaa mavazi maalum yaliyochaguliwa na kushonwa maalum kwa ajili hiyo; (e) Endapo vazi maalum lililochaguliwa na Halmashauri ni joho basi litavaliwa juu ya vazi la Mjumbe, na Endapo 11 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Halmashauri haina joho basi Mjumbe atavaa vazi la heshima, na mavazi kama jeans, kofia zinazohusiana na dini na sare za Chama hazitaruhusiwa kuvaliwa wakati wa Mikutano ya Halmashauri na vikao vya Kamati za Kudumu za Halmashauri; (f) Vazi rasmi la Meya, Mkurugenzi na Naibu Meya litakuwa lenye kuonyesha rangi za Bendera ya Taifa na la mazao yanayolimwa kwa wingi katika eneo Halmashauri kadri Halmashauri itakavyoona inafaa. Hata hivyo, Kanuni hii haitaathiri majoho ambayo yanatumika kabla ya Kanuni hii; (g) Endapo katika Mkutano huo Halmashauri itajigeuza kuwa Kamati, Wajumbe watavua majoho; na (h) Endapo Baraza litajigeuza kuwa Kamati taratibu za kuendesha Vikao vya Kamati zitatumika na kikao hicho kitakua cha siri. (2) Madaraka au jukumu lolote la Meya kuhusiana na uendeshaji wa Mikutano yanaweza kutekelezwa na mtu anayeongoza Mkutano huo. (3) Halmashauri itatenga siku mbili kila wiki kwa ajili ya Meya kufika ofisini na kutekeleza majukumu yafuatayo: (a) kusikiliza matatizo ya wananchi; (b) kupata maelezo toka kwa Mkurugenzi kuhusu uendeshaji wa shughuli za Halmashauri ikiwa ni pamoja na masuala ya manunuzi; (c) kusaini mikataba mbalimbali ya Halmashauri; na (d) kushughulikia jambo ambalo Mkurugenzi ataona linahitaji kushughulikiwa au kutekelezwa na Meya. 13.-(1) Kila Mjumbe anayehudhuria Mkutano wa Halmashauri au Kamati yoyote ya Halmashauri ambamo yeye ni Mjumbe hatahudhuria Mkutano huo mpaka awe ameweka saini inayotunzwa na yake kwenye Rejesta ya mahudhurio Mkurugenzi kwa ajili hiyo. (2) Isipokuwa siku ya kufanyika kwa Mikutano ya Baraza au Kamati ambayo Diwani ni Mjumbe au pale atakapoitwa kutekeleza majukumu ya Serikali, si ruhusa kwa Diwani kuwa katika Ofisi za Halmashauri na kufanya shughuli ambazo hazihusiani na Halmashauri au Serikali. 12 Kumbukumb u ya mahudhurio Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Kuruhusu watu na vyombo vya habari kwenye Mikutano ya Halmashauri Utaratibu wa shughuli za Mikutano 14.-(1) Mikutano ya Halmashauri itakuwa wazi kwa watu wote pamoja na vyombo vya habari. (2) Halmashauri itapaswa kuutangazia Umma kuhusu muda, wakati na mahali pa Mkutano na italiweka tangazo hilo mahali panapoonekana kwa urahisi katika eneo la Halmashauri siku zisizopungua tatu kabla ya Mkutano, na kama Mkutano umeitishwa katika muda mfupi zaidi basi wakati wa kuitisha Mkutano huo. 15.-(1) Isipokuwa kama Halmashauri, kutokana na sababu za dharura, itaamua kubadili utaratibu wa shughuli za Mikutano, utaratibu wa shughuli katika kila Mkutano wa kawaida wa Halmashauri utakuwa kama ifuatavyo: (a) Meya akiongozwa na Katibu ataingia ukumbini baada ya Mratibu wa vikao kutoa ishara maalum kuashiria Meya kuingia ukumbini na Wajumbe watasimama na kukaa kimya hadi pale Meya atakaporuhusu Wajumbe kukaa; (b) mkutano utaanza kwa Sala au Dua itakayosomwa na Meya; (c) endapo Meya au Naibu Meya hawatakuwepo, Wajumbe watachagua mtu wa kuongoza kikao; (d) baada ya Sala au Dua kusomwa Mkurugenzi na Meya watajibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Wajumbe wa Baraza la madiwani kwa utaratibu na mpangilio kama ilivyooneshwa kwenye Kanuni hizi; (e) kupokea na kujadili taarifa za kwenye Kata kutoka kwa Madiwani wa Kata husika; (f) kujadili jambo lolote linalotakiwa kwa mujibu wa Sheria kushughulikiwa kabla ya shughuli nyingine yoyote; (g) kupokea inayopaswa kupokelewa taarifa yoyote kisheria kabla ya shughuli nyingine yoyote; (h) kusoma au kuthibitisha muhtasari wa Mkutano wa kawaida wa Halmashauri uliopita na Mikutano yoyote maalum ya Halmashauri iliyofanyika baada ya Mkutano huo wa kawaida. Hata hivyo iwapo nakala za mihtasari zimesambazwa kwa kila Mjumbe kabla au wakati wa kupeleka taarifa ya kuhudhuria Mkutano, mihtasari hiyo itachukuliwa kuwa imesomwa; 13 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (i) (j) kupokea taarifa yoyote ambayo Meya atapenda itolewe kwa Halmashauri; kujibu maswali kufuatana na kanuni ya 23 ya Kanuni hizi; (k) kumalizia shughuli yoyote iliyobaki katika Mkutano wa (l) kawaida uliopita; kupokea na kufikiria taarifa za Kamati za Halmashauri, kutoka kwa Wenyeviti wa Kamati ambao watahusika kujibu maswali ya Wajumbe kuhusiana na kazi za kamati husika; (m) kupokea na kujadili taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri; (n) kuidhinisha utiaji lakiri katika hati; (o) kufikiria hoja binafsi kufuatana na jinsi Kuthibitisha muhtasari zilivyopokelewa; na (p) kushughulikia mambo mengine yaliyoonyeshwa katika taarifa ya Mkutano. (2) Halmashauri inaweza, katika Mkutano wowote wa kawaida, kubadili utaratibu wa hoja za mazungumzo ili kutoa kipaumbele kwa shughuli yoyote ambayo kwa maoni ya Meya na uharaka wa pekee, lakini mabadiliko hayo hayatabadilisha mpangilio wa shughuli zilizotajwa katika aya (c), (f) na (g) za kanuni ya 14(1). 16.-(1) Katibu ataandika muhtasari wa mazungumzo ya kikao unaozingatia majina ya Wajumbe waliohudhuria na wasiohudhuria, jina la mtoa hoja, aliyeunga mkono hoja, mabadiliko ya hoja kwa ufupi, ushauri uliotolewa na azimio lililofikiwa. Muhtasari kurekebishwa, kuthibitishwa na kusainiwa na Mwenyekiti wa Mkutano na kutunzwa katika rejesta maalum ya mihtasari. utasomwa, huo (2) Mara baada ya kusoma Muhtasari, au kama itachukuliwa kama umesomwa Meya atawahoji Wajumbe “Je Muhtasari wa Mkutano wa Halmashauri wa tarehe…………ya mwezi………. Mwaka……..utiwe saini kama kumbukumbu sahihi.” (3)Hakuna hoja au majadiliano yatakayofanywa kuhusiana na muhtasari isipokuwa kuhusiana na usahihi wa muhtasari, kama hakuna swali lililoulizwa, basi mara baada ya kuthibitishwa Meya atatia saini katika muhtasari huo. 14 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (4)Muhtasari ambao utakuwa umesainiwa vilivyo na kama hakuna ushahidi wa kuwepo kwa makosa utakuwa kumbukumbu sahihi na Mkutano utahesabika kuwa umeitishwa na kufanyika vilivyo na Wajumbe waliohudhuria watahesabika halali. (5) Mihtasari ya Halmashauri itakuwa wazi kwa ukaguzi na Wajumbe na kwa umma kwa wakati unaofaa na kwa utaratibu utakaokubaliwa na Halmashauri na kwamba mtu yeyote anaweza kupewa sehemu ya muhtasari huo kama akiomba na baada ya kulipa ada kama itakavyoidhinishwa na Halmashauri. Hoja Meya za 17. Hoja zinazowasilishwa na Meya hazitazidi hoja tatu, bila kuathiri haki yake, kama Mjumbe ya kuwasilisha hoja katika taratibu za kawaida. Taratibu majadiliano za 18.-(1) Isipokuwa kwa idhini ya Halmashauri mtoa hoja atahutubia Mkutano wa Halmashauri kwa dakika zisizozidi kumi. Wajumbe wengine ikiwa ni pamoja na mtoa hoja watazungumza kwa muda usiozidi dakika tano kila mmoja. (2) Mjumbe anaruhusiwa kuzungumza mara moja katika hoja yoyote ile isipokuwa hoja inayowasilishwa bila mjadala. (3) Mtoa hoja atakuwa na haki ya kuzungumza kwa muda usiozidi dakika tano katika kujibu majadiliano na muda huo utaanza kuhesabika mara atakapoanza kuchangia au kujibu. Mratibu wa vikao atatoa ishara maalum kumjulisha mtoa hoja kuwa muda wake umeisha na mjadala juu ya hoja hiyo utafungwa. Utaratibu huu wa kuhesabu muda utatumika pia kwa Mjumbe yeyote atakayepewa muda wa kuchangia hoja na mara tu baada ya kujibu, mjadala juu ya hoja utafungwa. (4) Mjumbe yeyote aliyekwishachangia kwenye hoja hawezi kutoa au kuunga mkono marekebisho, ila marekebisho yakitolewa na kuungwa mkono, Mjumbe aliyekwishazungumza katika hoja ya awali anaweza kuzungumza kwenye hoja iliyorekebishwa kwa muda usiozidi dakika tatu. (5) Iwapo Wajumbe wawili au zaidi watasimama wakati mmoja kuzungumza, Mjumbe atakayetamkwa na Meya ndiye atakayepewa nafasi kwanza. (6) Bila kuathiri masharti ya Kanuni Ndogo ya (5) ya Kanuni hii, Meya atahakikisha kuwa, nafasi ya kuchangia 15 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) inatolewa kwa uwiano unaofaa miongoni mwa aina zote za uwakilishi wa Madiwani walioomba kuchangia hoja hiyo. (7) Mjumbe anapozungumza ataelekeza mazungumzo yake kwa Meya tu na atapaswa kusimama. (8) Mjumbe anapozungumza hatakatizwa, isipokuwa kwa suala la utaratibu, lakini anaweza kutoa nafasi kwa Mjumbe anayetaka kujieleza. (9) Mjumbe anaposimama kutoa taarifa kuhusu utaratibu, Mjumbe anayezungumza ataketi na atabaki ameketi hadi hoja ya utaratibu itakapokuwa imeamuliwa na Meya, isipokuwa kama anasimama kumweleza Meya kuhusu suala la utaratibu. (10) Meya ndiye pekee mwenye uamuzi kuhusu utaratibu katika Mikutano ya Halmashauri, na anayo madaraka ya kuzuia fujo na kuhakikisha kuwa maamuzi yake katika kusimamia usalama yanatekelezwa mara moja. Wakati wa majadiliano Meya akisimama, Mjumbe anayezungumza au aliyesimama ataketi na hakuna Mjumbe atakayesimama hadi Meya aketi. (11) Mjumbe hatabaki amesimama wakati Mjumbe mwingine anaelekeza mazungumzo yake kwa Meya. (12) Mkurugenzi wa Halmashauri atajibu swali lolote atakaloulizwa na Meya kutokana na shughuli zinazoendelea kwenye Mkutano isipokuwa kama atadai haki ya kukataa kujibu swali kwa msingi ya kwamba jibu linaweza kumweka hatiani au kuvunja uaminifu wake au linamhusisha yeye kama mtetezi mahakamani. (13) Mtu kwa niaba yake mwenyewe, au kwa niaba ya watu wengine walio kwenye ujumbe wa watu, hataruhusiwa kuzungumza katika Mkutano wa Halmashauri isipokuwa kwa idhini ya Halmashauri iliyotolewa kwa njia ya azimio. Idhini ya namna hiyo haitatolewa isipokuwa kama mtu huyo au watu hao wanaotaka kuihutubia Halmashauri watakuwa wamempatia Mkurugenzi au Afisa aliyeruhusiwa naye, taarifa ya muda usiopungua siku tisa kabla ya Mkutano wa Halmashauri ambamo wangetaka maombi yao yafikiriwe kupewa idhini, maombi ya kimaandishi linalotarajiwa kujadiliwa, na mpaka taarifa ya kupokelewa kwa maoni hayo itakapokuwa imebandikwa kwenye mbao za matangazo za Halmashauri. ikieleza jambo (14) Hakuna zaidi ya watu wawili watakaokuwa na haki ya kuhutubia Halmashauri kwa niaba ya uwakilishi; na wala 16 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Fujo zinazosababi shwa wajumbe na ujumbe hakuna watakaoruhusiwa. utakaozidi idadi ya watu watano (15) Kiwango cha juu cha muda wa kuzungumza na Halmashauri ikiwa ni pamoja na muda wa kusoma risala hakitazidi dakika kumi. 19.-(1) Katika Mkutano wowote wa Halmashauri kama Mjumbe wa Halmashauri ataonyesha kukosa heshima kwa madaraka aliyonayo Meya au kudharau Kanuni za Kudumu za Halmashauri kwa kuzuia kwa makusudi shughuli za Halmashauri zisiendelee au vinginevyo, Meya ataelekeza Mkutano kwa tukio hilo kwa kumtaja jina mtu anayehusika. (2) Endapo baada ya kutajwa jina mjumbe ataendelea kudharau madaraka ya Meya, basi Meya ataliomba Baraza kuahirisha shughuli za Mkutano na Meya atatafakari jambo hilo na kuagiza yafuatayo: (a) Mjumbe atolewe nje ya Mkutano; au (b) Mjumbe asihudhurie vikao vitatu mfululizo. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ya 18(2)(a) na (b), Mjumbe huyo ataendelea kupokea posho ya mwezi ya udiwani. (4) Iwapo kutatokea fujo kubwa katika Mkutano wowote wa Halmashauri, Meya anaweza kama ataona ni muhimu kufanya hivyo, kuahirisha Mkutano bila majadiliano au swali, au kusimamisha Mkutano kwa muda atakaoona unafaa. Fujo zinazosababi shwa umma na 20.-(1) Iwapo mtu yeyote kati ya umma unaohudhuria Mkutano wa Halmashauri atavuruga Mkutano wa Halmashauri, Meya atamuonya mtu huyo aache kufanya hivyo. Endapo mtu huyo ataendelea kuvuruga Mkutano, Meya ataamuru mtu huyo atolewe kwenye chumba cha Mkutano. (2) Endapo kutakuwa na vurugu katika sehemu yoyote ya chumba cha Mkutano kinachotumika na umma, Meya ataamuru kuondolewa kwa watu wote walio katika eneo hilo. Hoja na marekebisho ya hoja 21.-(1) Taarifa ya kila hoja, isipokuwa hoja iliyowasilishwa chini ya Kanuni ya 21, itawasilishwa kwa maandishi yaliyowekwa saini na Diwani au Madiwani waliotoa taarifa, na itapelekwa kwa Mkurugenzi angalau siku nne kabla ya Mkutano wa Halmashauri unaofuata na akishaipokea, Mkurugenzi atagonga tarehe na kuipa namba na kuiingiza 17 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) kwenye daftari kadri hoja zilivyowasilishwa, na daftari hiyo itakuwa wazi kukaguliwa na Mjumbe yeyote wa Halmashauri. (2) Mkurugenzi ataonyesha katika taarifa ya kila Mkutano wa Halmashauri hoja zilizowasilishwa na kwa kadri zilivyopokelewa isipokuwa kama Diwani aliyetoa hoja hiyo ameeleza kwa maandishi wakati alipoleta hoja hiyo, kwamba anataka kuitoa katika Mkutano utakaofanyika baadaye, au baada ya kuwasilisha ameifuta hoja hiyo kwa maandishi. (3) Iwapo hoja ambayo imeonyeshwa katika taarifa ya Mkutano haiwezi kutolewa na Mjumbe aliyewasilisha taarifa; au na Mjumbe mwingine yeyote kwa niaba yake, basi hoja hiyo, isipokuwa kama imeahirishwa kwa idhini ya Halmashauri, na itachukuliwa haitawasilishwa tena bila ya kutoa taarifa upya. imeondolewa kama (4) Iwapo hoja itahusu jambo linalohusu Kamati au Kamati mbalimbali baada ya kupendekezwa na kuungwa mkono, hoja hiyo itapelekwa bila majadiliano kwenye Kamati ambayo Halmashauri iweze kufikiriwa na kutayarishiwa taarifa. itaelekeza ili (5) Ni lazima kila hoja ihusu jambo ambalo Halmashauri ina uwezo na wajibu nalo, au iwe inahusu Halmashauri husika. (6) Marekebisho ya hoja yaliyopendekezwa na kuungwa mkono yanaweza kuondolewa tu kwa ridhaa ya Wajumbe wa Halmashauri walio wengi waliopo katika Mkutano. (7) Marekebisho ya hoja yanapokuwa yamethibitishwa, hoja ya msingi kama ilivyorekebishwa itatolewa na Meya kama ndiyo hoja ya msingi ambayo nayo inaweza kufanyiwa marekebisho. Kama marekebisho ya hoja hayakukubaliwa, rekebisho lingine linaweza kupendekezwa. (8) Kwa idhini ya Meya, zaidi ya rekebisho moja linaweza kutolewa kwa wakati mmoja mbele ya Mkutano wa Halmashauri, lakini kila rekebisho la namna hii litatolewa moja baada ya jingine kufuatana na jinsi mapendekezo hayo yalivyotolewa. (9) Rekebisho halitachukuliwa kuwa sahihi kama litakuwa sawa na kuikataa hoja moja kwa moja au kama si rekebisho la hoja ya msingi linalokusudiwa kurekebisha. (10) Rekebisho taarifa, ambalo halitapendekezwa baada ya mjadala wa hoja inayozungumzwa kuendelea kwa nusu saa, ila kwa mujibu wa sharti hili, taarifa ya idadi yoyote ya marekebisho inaweza kutolewa. halikutolewa 18 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (11) Hoja ya kufuta azimio itapitishwa na Wajumbe wasiopungua theluthi mbili ya Wajumbe wote. (12) Hoja ya kuzingatia taarifa ya Kamati au kuidhinisha majadiliano au mapendekezo ya Kamati inaweza kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati husika, au na Mjumbe yeyote wa Kamati husika kwa niaba yake. inaweza (13) Mjumbe yeyote ambaye hajachangia katika mjadala wa hoja, au hajaitolea marekebisho, anaweza kupendekeza “kwamba Halmashauri iendelee na shughuli inayofuata”. Hoja tu kuzingatiwa baada ya hoja ya aina hiyo kupendekezwa na kuungwa mkono. Hoja inapotolewa, itaamuliwa bila marekebisho au mjadala, na kama ikikubaliwa, shughuli iliyokatizwa na azimio hilo haitaendelea kujadiliwa katika kikao hicho. Hoja ya kupendekeza kuendelea na shughuli inayofuata haitatolewa zaidi ya mara moja katika mjadala wa jambo lolote. (14) Baada ya mjadala kuhusu hoja kuendelea kwa muda usiopungua nusu Saa, Mjumbe ambaye hajachangia katika majadiliano anaweza kuomba idhini ya kutoa hoja “kwamba suala lililo mbele yetu sasa liamuliwe” na kama idhini hiyo itatolewa kwa kukubaliwa na si chini ya Wajumbe watano, hoja “kwamba suala lililo mbele yetu sasa liamuliwe” itawasilishwa mara moja, na kama ikiafikiwa, mtoa hoja ya msingi anaweza kuzungumza kwa dakika zisizozidi tano, na baada ya hapo swali au maswali yaliyo mbele ya Halmashauri yatafanyiwa uamuzi. (15) Hoja “kwamba suala lililo mbele yetu sasa liamuliwe” haitatolewa zaidi ya mara moja katika mjadala unaoendelea kuhusu lolote mpaka hapo mjadala utakapokuwa umeendelea kwa angalau nusu Saa tangu kuwekwa mbele ya Mkutano hoja ya aina hiyo ilipopendekezwa awali. jambo 22.-Hoja zifuatazo zinaweza kutolewa bila taarifa: (a) kumchagua Mwenyekiti wa Mkutano ambao hoja imetolewa; (b) hoja kuhusu usahihi wa muhtasari, kufunga Mkutano, kuahirisha Mkutano, utaratibu wa Mkutano, au suala linalofuata; (c) kuteua Kamati au Wajumbe wa Kamati, au wawakilishi katika taasisi za nje, unaotokana na jambo lililotaarifiwa katika wito wa Mkutano; 19 Hoja zinazoweza kutolewa bila taarifa Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (d) kukubali taarifa na mapendekezo ya Kamati na maazimio yote yanayotokana na taarifa au mapendekezo hayo; (e) kutoa idhini ya kuiondoa hoja; (f) kusahihisha hoja; (g) kuongeza muda wa hotuba; (h) kuwa, jambo lililotajwa katika taarifa ya kuitisha Mkutano litangulie; (i) kusimamisha Kanuni za kudumu; (j) kwamba Mjumbe asisikilizwe tena au aondoke katika Mkutano; (k) kumwomba Mjumbe abakie Mkutanoni; na (l) kutoa idhini ya Halmashauri pale ambapo idhini inatakiwa kwa mujibu wa Kanuni za kudumu hizi. Haki kujibu ya 23.-(1) Mtoa hoja atakuwa na haki ya kujibu maswali wakati wa kufunga mjadala juu ya hoja; kabla ya hoja kupigiwa kura au kabla ya hoja kutolewa “kwamba kikao kiahirishwe. (2) Mjumbe anayetumia haki yake ya kujibu hataanzisha hoja nyingine mpya. (3) Baada ya kutolewa kwa jibu ambalo linahusiana na Kanuni hizi, uamuzi utafikiwa bila majadiliano zaidi. Maswali 24.-(1) Mjumbe anaweza kumuuliza Mwenyekiti wa Kamati swali lolote kuhusu muhtasari wa Kamati uliofikishwa mbele ya Halmashauri. (2) Kila swali litaulizwa na kujibiwa bila majadiliano. (3) Swali au maswali yatajibiwa na Mwenyekiti wa Kamati mara moja, na Mjumbe anayeuliza swali au maswali hayo hatanyimwa haki yake ya kujadili hoja ambayo maswali hayo yanarejewa au kutoa hoja ya marekebisho. (4) Pale ambapo swali la maandishi limeelekezwa kwa Mwenyekiti wa Kamati, au Mkutano na taarifa inayotakiwa imo katika moja wapo ya mihtasari ya Halmashauri, kuonesha sehemu ya muhtasari ambapo habari hiyo imeoneshwa, kutachukuliwa ni jibu la kutosha. Maswali ya papo kwa papo 25.-(1) Halmashauri itatenga muda wa angalau dakika thelathini katika kila Mkutano wa Kawaida wa Halmashauri ambapo Meya na Mkurugenzi wa Halmashauri watajibu 20 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Wajumbe kabla ya kuanza kwa shughuli ya kawaida ya Mkutano wa Halmashauri. (2) Wajumbe ambao watataka kuuliza maswali ya papo kwa papo kwa Meya na Mkurugenzi watatakiwa kujiorodhesha kwanza kwa Meya angalau Saa ishirini na nne (24) kabala ya Mkutano wa Halmashauri kuanza. (3) Mjumbe yoyote ambae hatajiorodhesha kwa Meya ndani ya Saa ishirini na nne atahesabika kuwa amechelewa na hataruhusiwa kumuuliza Mkurugenzi au Meya swali la papo kwa papo. (4) Kabla ya kuanza kwa kipindi cha maswali ya papo kwa papo Meya atataja majina ya Wajumbe waliojiorodhesha kuuliza maswali ya papo kwa papo na idadi ya maswali. (5) Meya ataweka utaratibu ambao ataona unafaa na kuridhiwa na Wajumbe wa namna bora ya kuendesha kipindi cha swali la papo kwa papo. (6) Mjumbe hataruhusiwa kuuliza zaidi ya swali moja la papo kwa papo. (7) Maeneo ya muhimu ambayo Wajumbe watatakiwa kuuliza maswali ya papo kwa papo: (a) Uendeshaji wa jumla wa Halmashauri; (b) Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo; (c) Mipango ya kimkakati ya Halmashauri kuwaondolea wananchi umaskini; (d) Mipango ya baadaye ya maendeleo ya Halmashauri; (e) Usimamizi na utekelezaji wa Mipango na Bajeti kwa Mwaka husika; (f) Utoaji wa huduma za jamii kama vile elimu, afya, maji, barabara na madaraja; (g) Hifadhi ya mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji; (h) Usalama wa Chakula, Raia na Mali zao; na (i) Utawala Bora na utatuzi wa kero za wananchi. (8) Baada ya kujibiwa kwa swali, Mjumbe aliyeuliza swali atapewa fursa ya kuuliza swali moja tu la ufafanuzi na maswali yatajibiwa bila mjadala. 21 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (9) Meya atakua na uwezo wa kuruhusu au kukataa swali lolote la papo kwa papo ambalo litaonekana linahitaji takwimu au utafiti zaidi au swali ambalo linalenga kumdhalilisha Meya au mjumbe yeyote wa Baraza na uamuzi wake utakuwa wa mwisho. (10) Mara nusu Saa kumalizika,kipindi cha maswali ya papo kwa papo kitamalizika na kuruhusu shughuli zingine za kikao kuendelea. ya muda wa baada Taarifa Kamati za 26.-(1) Kila Kamati au Kamati ya pamoja iliyoteuliwa chini ya Kanuni hii itatoa taarifa ya majadiliano yanayohusiana na utekelezaji majukumu iliyokasimiwa katika mojawapo ya vikao viwili vya Halmashauri iliyoiteua kwa ajili ya ujulisho wa Halmashauri. (2) Muhtasari wa Kamati unaohitaji idhini ya Halmashauri, na taarifa zozote zinazohusiana na muhtasari huo, na ambazo zinaonekana kwa Kamati kuwa zinastahili, zitapelekwa kwa kila Mjumbe wa Halmashauri angalau siku saba kabla ya Mkutano wa Halmashauri ambamo utafikiriwa. (3) Mwenyekiti wa Kamati au Mjumbe mwingine wa Kamati kwa niaba yake, wakati wa kupendekeza kuidhinishwa kwa muhtasari wa Kamati, anaweza kusema kuwa hakusudii kuwasilisha kipengele au vipengele fulani vya muhtasari huo kwa lengo la kupata idhini ya Halmashauri. Katika hali hiyo Mjumbe yeyote hataweza kukizungumzia kipengele hicho na muhtasari utawasilishwa bila vipengele hivyo kuondolewa kwa kipengele cha aina hiyo kutatolewa taarifa kwenye Mkutano unaofuata. (4) Taarifa ya Kamati inapokuwa imepokelewa na itamaanisha kuwa hatua zilizochukuliwa na Halmashauri Kamati husika zimekubaliwa na mapendekezo yaliyo kwenye taarifa hiyo yatatekelezwa na kwamba Mkurugenzi atakuwa ameelekezwa ipasavyo. za Taarifa kutoka kwenye kata 27.-(1) Kila Kata itatakiwa kuwasilisha taarifa za utekelezaji katika Mkutano wa Halmashauri ulioitishwa chini ya Kanuni ya 3(1) ya Kanuni hizi. 22 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (2) Taarifa za utekelezaji kutoka katika Kata zitawasilishwa na Diwani wa Kata husika, au kama diwani hayupo, taarifa hiyo itawasilishwa na Diwani wa Viti Maalum anayeishi katika Kata hiyo na kama Diwani Viti Maalum hayupo, Meya atamtaarifu mapema Diwani yeyote ili ajiandae kuwasilisha taarifa hiyo. (3) Kutakuwa na aina tatu za taarifa zitakazowasilishwa: (a) Taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata ambayo itajumuisha ujenzi wa Madarasa, Nyumba za Walimu, Matundu ya Vyoo, Maabara, Viwanja vya Michezo, Vituo vya Afya, Zahanati, Madaraja, Barabara, Mashamba darasa, Ofisi za Mitaa, Kata na Tarafa; Idadi ya watu na vizazi. (b) Taarifa zinazohusu hali ya Kata ambazo zitajumuisha: (i) Maendeleo ya Elimu katika Kata kuhusiana na uandikishaji wa watoto wenye umri wa kwenda Shule, ufundishaji, utoro, hali ya mahudhurio, mimba mashuleni, ukaguzi na uratibu wa Shule; (ii) Hali ya majanga kama vile magonjwa ya mlipuko, mafuriko, njaa, na hali ya uhalifu na vifo; (iii) Maendeleo ya Kilimo, mifugo na uvuvi ambayo itajumuisha upatikanaji wa wataalamu, zana za kisasa na pembejeo za kilimo, mifugo na uvuvi; na (iv) Uimarishaji wa dhana ya uzalendo na utaifa kwa kuhamasisha vijana kuanzisha na kujiunga na vikundi vya Vijana, Wagani, kazi na mafunzo ya Jeshi la Mgambo, Ulinzi shirikishi na Polisi jamii. (c) Taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo na taarifa ya hali ya Kata sharti ijumuishe pia taarifa za shughuli za kiuchumi, taarifa ya mavuno ya mazao ya chakula na biashara pamoja na taarifa ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji. (4) Mkurugenzi wa Halmashauri atahakikisha taarifa kutoka kwenye Kata zinaandaliwa na kuwasilishwa na Diwani wa Kata hiyo kwenye Baraza la Madiwani ili ipitiwe na kuchambuliwa kwa nia ya kupata hoja zitakazowasilishwa katika Vikao vya Kamati husika na kutoa mrejesho. 23 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (5) Mwasilishaji wa taarifa atatakiwa kuelezea mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizo jitokeza na mbinu za kukabiliana nazo. (6) Mbinu za kukabiliana na changamoto sharti ziwekewe malengo na muda maalum wa kuzitatua. (7) Taarifa za mapokeo ya fedha na matumizi yake zitakazokuwa zimeandaliwa na Afisa Mtendaji wa Kata, zitawasilishwa sanjari na miradi iliyotekelezwa na gharama zake. (8) Baada ya taarifa kutoka kwenye Kata kupokelewa na Halmashauri, itamaanisha kuwa taarifa hizo zimeidhinishwa na taarifa yatatekelezwa na mapendekezo yaliyomo kwenye Halmashauri, na Kata kupewa taarifa ya utekelezaji wa majukumu hayo. 28. Kutakuwepo na Uhuru wa kutoa mawazo wakati wa majadiliano katika Mikutano ya Halmashauri na Uhuru huo hautahojiwa katika Mahakama yoyote au mahali popote nje ya Mkutano wa Halmashauri. 29.-(1) Inapotokea, kulingana na maoni ya Mwenyekiti au mtu yeyote anayeongoza Mkutano, kuwa kauli iliyotolewa na inamkashifu mtu yeyote, Mwenyekiti atamtaka Mjumbe Mjumbe aliyetoa kauli hiyo kufuta kauli yake na kumwomba msamaha mtu aliyekashfiwa kwa maandishi ndani ya siku saba (7) tangu kauli hiyo ya kashfa ilipotamkwa. (2) Endapo Mjumbe aliyetoa kauli ya kashfa atakataa kufuta kauli yake na kuomba msamaha kwa maandishi kama inavyoelekezwa katika Kanuni Ndogo (1), ya Kanuni hii. Meya wa Mkutano, atamsimamisha Mjumbe huyo kuhudhuria vikao vitatu mfululizo vya Halmashauri. (3) Mjumbe aliyesimamishwa kwa mujibu wa Kanuni Ndogo (2) ya Kanuni hii atapoteza haki zake zote ikiwa ni pamoja na posho, nauli na upendeleo na kinga kwa muda wote wa kusimamishwa kwake. wa Uhuru kutoa mawazo wakati majadiliano wa Kauli zenye kashfa Maamuzi ya Mikutano ya Halmashauri 30.-(1) Masuala yote yaliyojadiliwa na kupendekezwa katika Mkutano wowote wa Halmashauri yataamuliwa kulingana na wingi wa kura za Wajumbe waliohudhuria Mkutano huo, na ikitokea kura za Wajumbe zimelingana, Meya 24 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) au Mjumbe yeyote mwingine anayeongoza Mkutano, atapiga kura ya turufu mbali ya kura ya kawaida. (2) Iwapo suala linalopigiwa kura linahusu kutokuwa na imani au kumwondoa Meya madarakani, au jambo lolote lingine kama itakavyoamuliwa na Halmashauri, kura zitapigwa kwa siri. Mwaliko kwa wasiokuwa Wajumbe kushiriki na kuzungumza kwenye vikao vya Halmashauri 31.-(1) Meya, baada yakushauriana na Wajumbe, anaweza kumwalika mtu yeyote kuhudhuria na kuzungumzia jambo lolote, au kushiriki kwa njia yoyote, katika Mkutano wowote wa Halmashauri lakini mwalikwa huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura katika Mkutano huo. (2) Wakuu wa Idara wa Halmashauri na Maafisa Tarafa wanapaswa kuhudhuria Mikutano yote ya Halmashauri lakini hawatakuwa na haki ya kupiga kura katika Mikutano hiyo. Mihutasari ya Kamati ya Maendeleo ya Kata na Mitaa 32. Mkurugenzi wa Halmashauri atahakikisha mihutasari yote ya Kamati za Maendeleo ya Kata, na Mikutano Mikuu ya Mitaa inapitiwa na kuchambuliwa kwa nia ya kupata hoja zitakazowasilishwa katika vikao vya Kamati husika na kutoa mrejesho inavyopaswa. Mihtasari ya Halmashauri kupelekwa kwa Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa 33.-(1) Mihutasari ya Halmashauri itatolewa na kupelekwa kwa taarifa, kwa Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa ambamo Halmashauri imo katika muda wa siku saba (7) baada ya kuthibitishwa kwa mihutasari hiyo. (2) Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa wanaweza kupewa, wakiomba, nakala ya mihutasari au sehemu ya mihtasari ya Kamati za Kudumu na Kamati nyingine. (3) Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa hawatabadilisha au kubatilisha au kuagiza kubadilisha au kubatilisha uamuzi wa Halmashauri. Hoja kuhusu matumizi 34. Hoja yoyote isiyotokana na mapendekezo au taarifa ya Kamati ya Fedha na Utawala, na ambayo, kama ikikubaliwa, itaongeza matumizi au kupunguza mapato yaliyo chini ya usimamizi wa Kamati yoyote, au itasababisha matumizi ya Kamati ya Kudumu, baada ya kupendekezwa au kuungwa mkono, itaahirishwa bila majadiliano mpaka Mkutano wa 25 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Kupokelewa kwa taarifa za Kamati kawaida wa Halmashauri unaofuata, na Kamati yoyote inayohusika na hoja hiyo itafikiria iwapo ingependa kutoa taarifa kuhusu athari za kifedha za pendekezo hilo. 35.-(1) Taarifa ya Kamati inapowasilishwa kwenye Halmashauri, hoja itakuwa “kwamba taarifa ipokelewe”na baada ya kupokelewa na Wajumbe taarifa itaanza kujadiliwa kipengele kimoja baada ya kingine. (2) Mapendekezo yoyote yaliyomo katika taarifa hiyo yatapigiwa kura iwapo Mjumbe yeyote atapenda iwe hivyo. Baada ya hapo taarifa nzima itawasilishwa mbele ya Mkutano kwa kupokelewa ikiwa na au bila marekebisho. Kuidhinishw a kwa taarifa ya Kamati 36. Taarifa ya Kamati inapokuwa imepokelewa na itamaanisha kuwa hatua zilizochukuliwa na Halmashauri taarifa hiyo zimeidhinishwa na Kamati iliyowasilisha mapendekezo yaliyomo kwenye taarifa yatatekelezwa na kwamba Mkurugenzi wa Halmashauri atakuwa ameelekezwa kama inavyotakiwa. Uhalali wa majadiliano ya Halmashauri 37. Uhalali wa majadiliano kwenye Halmashauri hautaathiriwa na nafasi yoyote wazi ya Mjumbe, dosari zozote zilizo katika uchaguzi au uteuzi wa Wajumbe wa Kamati au zile za maafisa wake. 38. Halmashauri inaweza kujigeuza kuwa Kamati ya Halmashauri, na mara baada ya kujigeuza, taratibu za kuendesha vikao vya Kamati za Kudumu zitatumika. Uwezo wa Halmashauri kujigeuza kuwa Kamati ya Halmashauri nzima Hoja zinazohusu Watumishi wa Halmashauri 39. Kama litajitokeza jambo lolote katika kikao cha Halmashauri linalomuhusu Mtumishi yeyote wa Halmashauri kuhusu Uteuzi, kupandishwa cheo, kufukuzwa kazi, mshahara, mazingira ya kazi au utendaji kazi kwa ujumla wake, jambo hilo litajadiliwa katika Kamati ya Halmashauri nzima. 26 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Ushiriki wa Umma 40.-(1) Mtu yeyote ambaye ni mkazi katika eneo la Halmashauri anaweza kuhudhuria kikao cha Halmashauri kwa nia ya kuwasilisha hoja mbele ya Halmashauri, baada ya kutoa taarifa kwa maandishi kwa Mkurugenzi, na Mkurugenzi akamkubali kufanya hivyo. Uahirishaji wa vikao Kamati Kudumu za (2) Mtu yeyote ambaye ni mkazi katika eneo la Halmashauri anaweza kualikwa kuhudhuria kikao cha Kamati au Kamati Ndogo kabla uamuzi haujafanyika kuhusu masuala ambayo ana maoni mahsusi. 41.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Kanuni Ndogo ya 18 (2) ya na Kanuni Ndogo ya 2 ya Kanuni hii, Halmashauri haitaahirisha Mkutano wake hadi dondoo zote za agenda ya Mkutano huo zitakapojadiliwa na kutolewa uamuzi. (2) Endapo katika Mkutano wowote wa Halmashauri akidi haikutimia, Wajumbe waliopo wataahirisha Mkutano na utaratibu wa kuitisha Mkutano mwingine utafanyika kwa kuzingatia maelekezo ya Kanuni hii. SEHEMU YA NNE KAMATI 42.-(1) Halmashauri katika Mkutano wake wa Mwaka itateua Wajumbe wa Kamati za Kudumu zifuatazo ambazo zitakuwa na idadi ya Wajumbe (ukimwondoa Meya wa Halmashauri isipokuwa katika Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango) kama au kama inavyoonesha hapa itakavyorekebishwa na Halmashauri mara kwa mara. Isipokuwa katika kuteua Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala, Meya na Mkurugenzi watazingatia uwiano wa uwakilishi wa vyama katika Halmashauri: chini Namba Kamati Idadi wajumbe ya Akidi (a). (b). ya na Kamati Fedha Utawala Kamati ya 28 16 15 9 27 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (c). (d). (e). Uchumi, Afya na Elimu. Kamati ya Mipango Miji na Mazingira Kamati ya Maadili Madiwani Kamati ya UKIMWI ya 19 10 5 7 3 4 (2) Kila Mjumbe wa Halmashauri atakuwa Mjumbe wa angalau Kamati moja ya Kudumu. Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango itakuwa na Wajumbe wafuatao: (a) Meya ambaye atakuwa Mwenyekiti; (b) Naibu Meya; (c) Mbunge au Wabunge wa Majimbo wanaowakilisha Majimbo katika eneo la Halmashauri; wawili wengine wasiozidi (d) Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Halmashauri; na (e) Wajumbe (2) watakaopendekezwa na Meya na kupigiwa kura na Baraza la Halmashauri mmoja kati yao awe mwanamke. (3) Halmashauri yenye Madiwani wasiozidi ishirini (20), idadi ya wajumbe wa Kamati ya Fedha itakuwa kama ilivyooneshwa kwenye Kanuni yaNdogo ya 41(2) ya Kanuni hii. (4) Bila kuathiri masharti ya Kanuni Ndogo ya (3) ya Kanuni hii, Halmashauri yenye idadi ya Madiwani wanaozidi ishirini (20) na wasiozidi thelathini na tano (35) Wajumbe wa Kamati ya Fedha watakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye Kanuni ya 41(2) pamoja na wajumbe wengine wawili (2) watakaotokana na orodha itakayopendekezwa na Meya na kupigiwa kura na Baraza la Halmashauri mmoja kati yao awe wanawake. (5) Bila kuathiri masharti ya Kanuni Ndogo ya (2) na (3) na (4) ya Kanuni hii, Halmashauri yenye idadi ya Madiwani wanaozidi thelathini na tano (35) na zaidi Wajumbe wa Kamati ya Fedha watakuwa kama ilivyooneshwa kwenye Kanuni ya 41(2) pamoja na wajumbe wengine wanne (4) watakaotokana na orodha itakayopendekezwa na Meya na kupigiwa kura na Baraza la Halmashauri wawili kati yao wawe wanawake. 28 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (6) Wajumbe wa Kamati za Kudumu watashika nyadhifa zao kwa muda wa Mwaka mmoja na wataendelea kushika nyadhifa hizo mpaka Mkutano wa Mwaka wa Halmashauri unaofuata, Isipokuwa Wajumbe waliochaguliwa kwenye Mkutano wa kwanza baada Uchaguzi Mkuu watashika nyadhifa zao kwa muda uliobaki kumaliza Mwaka wa Fedha ambapo Uchaguzi utafanyika tena. (7) Halmashauri inaweza wakati wowote kuvunja na kuunda upya Kamati ya Kudumu iliyoteuliwa kwa mujibu wa Kanuni hii ya kudumu, endapo kufanya hivyo kutakuwa ni kwa manufaa ya Halmashauri. (8) Hakuna Halmashauri itakayounda Kamati ya Kudumu mpya zaidi ya Kamati zilizotajwa kwenye Kanuni ya 41(1) hapo juu, isipokuwa baada ya kuomba na kupata idhini ya maandishi kutoka kwa Waziri. (9) Maombi ya Halmashauri ya kuanzisha Kamati mpya ya Kudumu lazima yakidhi na yawe na maelezo yafuatayo: (a) Upekee wa majukumu yanayoombewa kuundwa kwa Kamati ya Kudumu mpya na majukumu hayo yawe ambayo hayawezi kutekelezwa na Kamati za Kudumu zilizopo na zilizotajwa kwenye Kanuni ya 41(1) hapo juu; (b) Gharama za uendeshaji wa Kamati hiyo kwa Mwaka; na (c) Kuundwa kwa Kamati ya Kudumu hiyo mpya ni hitaji la lazima na ni kipaumbele cha Halmashauri na jamii kwa ujumla. (10) Kamati ya Kudumu yoyote itakayoundwa na Halmashauri bila idhini ya Waziri itakuwa batili na maamuzi yake yote yatakua batili. 43. Meya atakuwa Mjumbe wa Kamati zote za Kudumu za Halmashauri. 44. Kamati zote za Halmashauri zitawasilisha taarifa zao kwa Halmashauri, na hakuna hatua itakayochukuliwa kutekeleza uamuzi wowote wa Kamati yoyote mpaka hapo taarifa ya Kamati husika itakapokuwa imekubaliwa na Halmashauri, isipokuwa pale ambapo idhini ya kuchukua hatua imekasimiwa kwa Kamati. 29 Meya kuwa Mjumbe wa Kamati zote Uwezo wa Kamati Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Kamati pamoja za inaweza kukubaliana 45.-(1) Halmashauri na Halmashauri nyingine kuteua Kamati ya pamoja kutokana na Wajumbe wao kwa madhumuni yoyote yale ambayo wana maslahi ya pamoja, na Halmashauri hizo zinaweza kukasimu kwa Kamati hiyo ya pamoja, kutegemea na masharti na mipaka itakayoweka kama watakavyoona inafaa, madaraka au kazi ya Halmashauri inayohusiana na madhumuni yaliyozifanya ziunde Kamati hiyo, isipokuwa shughuli zile ambazo Halmashauri haziruhusiwi kukasimu. (2) Muundo na muda wa kazi wa Wajumbe wake na mipaka ya eneo ambamo Kamati hiyo ya pamoja itafanya kazi, itapangwa na Halmashauri zinazoiteua. (3) Kamati ya pamoja haitaingia katika gharama zozote zaidi ya zile ambazo zimeidhishwa na mamlaka iliyoteua Kamati hiyo. Kukasimu madaraka kwenye Kamati 46.-(1) Kwa kuzingatia Kanuni Ndogo ya (2) ya Kanuni hii pamoja na masharti mengine ambayo Halmashauri itaona inafaa, Halmashauri inaweza kukasimu kwa Kamati uwezo wa kutekeleza kazi yoyote kwa niaba yake. (2) Halmashauri haitakasimu kwa Kamati yoyote uwezo wa: (a) Kutunga Sheria Ndogo; (b) Kuweka na kutoza kodi; (c) Kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya Halmashauri; (d) Kutoza Ada na Ushuru; (e) Kuidhinisha mpango na Bajeti ya Halmashauri; (f) Kuingia mikataba mbalimbali ikiwa ni pamoja na mikataba ya kukopa; na (g) Kupitisha mpango wa utoaji huduma. (3) Kazi za kila Kamati ya Kudumu ya Halmashauri ni kama zilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni ya kudumu hii. (4) Halmashauri inaweza kusitisha au kurekebisha uamuzi wa kukasimu madaraka yoyote kwa Kamati, lakini usitishaji au urekebishaji huo hautaathiri lolote lililofanywa kutokana na uamuzi wowote uliochukuliwa kihalali na Kamati. jambo 30 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Kamati Ndogo Mikutano ya Kamati Mwenye kiti wa Kamati (5) Shughuli yoyote iliyotekelezwa na Kamati kutokana na kukasimiwa kwa mujibu wa Kanuni hii itatambuliwa kuwa imefanywa au kutekelezwa na Halmashauri. 47.-(1) Kamati yoyote au Kamati ya pamoja inaweza kuteua Kamati Ndogo kutokana na Wajumbe wake kadri itakavyoona inafaa kwa ajili ya kuchunguza na kutoa taarifa kuhusu jambo lolote, lakini Kamati haitakasimu madaraka yake ya kiutendaji kwa Kamati Ndogo yoyote. (2) Idadi ya Wajumbe wa Kamati Ndogo pamoja na muda watakaotumikia vitaamriwa na Kamati iliyoteua Kamati Ndogo hiyo. (3). Mwenyekiti wa Kamati atakuwa Mjumbe wa Kamati Ndogo yoyote kwa mujibu wa wadhifa wake isipokuwa kama atamfahamisha Mkurugenzi kwa maandishi kuwa hatakuwa Mjumbe wa Kamati hiyo. (4) Kila Kamati Ndogo inaweza kumteua mmoja wa Wajumbe wake kuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo husika. 48.-(1) Mkutano wa kwanza wa Kamati utaitishwa na Mkurugenzi ndani ya mwezi mmoja baada ya Kamati kuteuliwa na baada ya hapo kulingana na ratiba ya Mikutano kama itakavyoidhinishwa na Halmashauri. (2) Taarifa ya angalau Saa ishirini na nne yenye agenda za kikao itabidi kutolewa kwa Wajumbe kabla ya Mkutano wa Kamati. 49.-(1) Katika kikao chake cha kwanza baada ya Mkutano wa Mwaka wa Halmashauri na kabla ya kuendelea na shughuli yoyote nyingine, kila Kamati itamchagua Mwenyekiti wa Kamati kwa Mwaka unaohusika. (2) Mwenyekiti wa Kamati, isipokuwa Kamati ya Fedha na Utawala, atachaguliwa kwa kura ya siri ya Wajumbe walio wengi kwa kupiga kura ya siri kwenye eneo la faragha litakalotengwa na Mkurugenzi kwa ajili hiyo. (3) Meya atakuwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango. (4) Endapo nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati itakuwa wazi katika kipindi cha Mwaka husika, Mkurugenzi atatoa taarifa kwa Wajumbe wote wa Kamati kuwa katika kikao kijacho cha kawaida cha Kamati husika dondoo ya kumchagua 31 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Mwenyekiti wa Kamati kwa kipindi cha Mwaka kilichosalia itakuwa ya kwanza katika agenda. Mkutano maalum wa Kamati 50.-(1). Mkutano Maalum wa Kamati utaitishwa baada ya theluthi mbili ya Wajumbe wa Kamati kuomba kwa maandishi kuwa Mkutano huo ufanyike na kueleza sababu. (2) Taarifa ya Mkutano Maalum wa Kamati itaonesha shughuli itakayofanyika katika Mkutano huo Maalum na hakuna jambo jingine lolote litakalojadiliwa katika Mkutano huo. Agenda Kamati za 51. Mjumbe wa Kamati atakuwa na haki ya hoja zake kuwekwa katika agenda ya Kamati kama atatoa taarifa ya angalau siku nne kabla ya tarehe ya kikao. Mahudhurio katika Mikutano ya Kamati 52.-(1) Mjumbe wa Kamati ya Kudumu au Kamati Ndogo, ambaye ameshindwa kuhudhuria Mkutano wa Kamati, hataruhusiwa kutuma mtu mwingine kumwakilisha kwenye Mkutano wa Kamati au Kamati Ndogo. (2) Mjumbe wa Halmashauri hatakuwa na haki ya kuhudhuria kikao chochote cha Kamati au Kamati Ndogo ambamo yeye si Mjumbe, isipokuwa kama Kamati au Kamati Ndogo inayohusika imemwalika kuhudhuria, na hata hivyo hatakuwa na haki ya kupiga kura au kudai posho kwa kuhudhuria Mkutano huo wa Kamati au Kamati Ndogo. Mjenga hoja kualikwa kwenye Mkutano wa Kamati 53. Mjumbe wa Halmashauri anayewasilisha hoja ambayo imepelekwa kwenye Kamati atapewa taarifa ya Mkutano wa Kamati ambamo hoja yake imepangwa kuzungumzwa na kama atahudhuria atapewa nafasi ya kuizungumzia. Waalikwa wasiokuwa Wajumbe kuhudhuria na kushiriki katika Mikutano ya Kamati 54. Mwenyekiti wa Kamati au Kamati ya pamoja au Kamati Ndogo baada ya kushauriana na Wajumbe wa Kamati au Kamati ya pamoja au Kamati Ndogo, anaweza kumwalika mtu yeyote kuhudhuria na kuzungumza kwenye Mkutano kuhusu suala lolote au kushiriki kwa namna yoyote kwenye kikao cha Kamati, lakini mtu huyo atakayealikwa hatakuwa na haki ya kupiga kura kwenye Mkutano huo. 32 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Mahudhurio ya Umma na vyombo vya habari kwenye Mikutano ya Kamati, Kamati pamoja Kamati Ndogo ya na Athari za nafasi wazi kwenye Kamati 55. Majadiliano katika Kamati au Kamati ya pamoja au Kamati Ndogo hayatakuwa wazi kwa umma na vyombo vya habari, isipokuwa kwa kutokana na azimio la Halmashauri linaloruhusu kuwa Umma na vyombo vya habari vihudhurie. 56.-(1) Kunapotokea nafasi wazi kwenye Kamati au Kamati ya pamoja au Kamati Ndogo, Kamati itaendelea kutekeleza shughuli zake licha ya kuwepo kwa nafasi wazi hiyo au hizo au mpaka nafasi hiyo au hizo zitakapojazwa kwa njia ya uchaguzi au uteuzi. Mjumbe atakayejaza nafasi hiyo atashika nafasi wazi hiyo kwa kipindi kilichosalia cha Mjumbe ambaye nafasi yake imekuwa wazi. (2) Uhalali wa tendo lolote au maamuzi ya Mkutano wowote wa Kamati hautaathiriwa kutokana na hitilafu katika uteuzi wa Mjumbe aliyeshika nafasi hiyo au nafasi hizo kuachwa wazi na Mjumbe, au Wajumbe kuamua kutoka kwenye kikao kwa lengo la kukwamisha jambo linalotaka kutolewa maamuzi na Kamati hiyo. Akidi kwenye Mikutano ya Kamati 57. Endapo Wajumbe waliohudhuria Mkutano hawatafikia akidi ya Mkutano, Mkurugenzi ataahirisha Mkutano huo na kuuitisha tena ndani ya siku saba (7) na endapo akidi haitatimia tena, idadi yoyote ya Wajumbe waliohudhuria itatengeneza akidi ya Mkutano ambapo mkutano huo utaendelea na utakuwa halali na Mkurugenzi atamjulisha Waziri kuwepo kwa hali hiyo. za Kanuni kudumu katika Mikutano ya Kamati 58.-(1) Kanuni ya 17 itatumika kwa kuzingatia maboresho yatakayohitajika kwenye Mikutano ya Kamati za Halmashauri. (2) Mjumbe anapozungumza katika Mkutano wa Kamati atakuwa ameketi na anaweza kuzungumza zaidi ya mara mbili kuhusu jambo linalojadiliwa. 33 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Upigaji kura kwenye Mikutano ya Kamati 59. Masuala yote yanayoletwa mbele ya Kamati yataamuliwa kwa wingi wa kura za Wajumbe waliohudhuria na kupiga kura kwenye Mkutano husika. Endapo kunatokea kura mlingano mtu anayeongoza kikao hicho atakuwa na kura ya turufu. Mihtasari ya Kamati 60.-(1) Muhtasari wa kila Kamati, Kamati ya pamoja na Kamati Ndogo, utajumuisha majina ya Wajumbe waliohudhuria na wasiohudhuria, na utasainiwa kwenye Mkutano unaofuata na mtu aliyeongoza Mkutano na muhtasari uliosainiwa hivyo, kama hakuna ushahidi wa kuwa una makosa, utapokelewa kwa ushahidi bila uthibitisho zaidi. (2) Hakuna hoja au mjadala utakaoendeshwa kuhusiana na muhtasari wa Kamati isipokuwa kuhusu usahihi wa suala lolote linalohusu usahihi litatolewa kwa hoja. Kufikiriwa upya maamuzi 61. Pale ambapo suala lililowasilishwa limeamuliwa kwa mujibu wa Kanuni ya 58, suala hilo halitaanza kujadiliwa upya katika Mkutano huo wa Kamati isipokuwa kama hoja hiyo inaungwa mkono na theluthi mbili ya Wajumbe waliohudhuria na kupiga kura. Kutunza siri za majadiliano ya Kamati na Kamati Ndogo 62. Mjumbe wa Kamati au Kamati Ndogo hatatoa nje jambo lolote lililoletwa au kuzungumzwa kwenye Kamati au Kamati Ndogo bila ruhusa ya Kamati hiyo, au kuzungumza kwenye Kamati Ndogo mpaka hapo Kamati au Kamati Ndogo itakapokuwa au itakapokuwa imekamilisha utekelezaji wa jambo hilo. taarifa kwenye Halmashauri imetoa Kujiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Kamati 63. Mwenyekiti wa Kamati anaweza kujiuzulu wadhifa wake kwa kutoa taarifa ya maandishi aliyoisaini na kutuma kwa Mkurugenzi. Kujiuzulu ujumbe wa Kamati na kujazwa kwa nafasi iliyowazi 64.-(1) Mjumbe yeyote wa Kamati anaweza kujiuzulu wadhifa wake kwa kutoa taarifa ya maandishi aliyoisaini na kuituma kwa Mkurugenzi. (2) Nafasi inayotokana na kujiuzulu kwa Mjumbe itajazwa na Halmashauri katika kikao chake cha kawaida baada ya tarehe ya kujiuzulu kwa Mjumbe. 34 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) SEHEMU YA TANO UNUNUZI WA VIFAA, UPATIKANAJI WA HUDUMA NA UJENZI Taratibu za uagizaji Sura ya 290 Kumbukum bu za majadiliano yanayohusu uagizaji 65.-(1) Uagizaji wa mali, huduma na ujenzi katika Halmashauri utazingatia Kanuni za Ununuzi zilizotungwa chini ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa na Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023. (2) Kutakuwa na Bodi ya Zabuni ambayo imeanzishwa kwa mujibu wa Kanuni za Bodi ya Zabuni (Uanzishwaji na Mwenendo) za Serikali za Mitaa na ambayo itasimamia shughuli zote za uagizaji katika Halmashauri. (3) Muhtasari wa Bodi ya Zabuni utapaswa kuwasilishwa kwenye kikao cha Halmashauri kitakachofuata baada ya muhtasari huo kujadiliwa na kupitishwa kwanza na Kamati ya Fedha na Utawala. itaweka 66.-(1) Bodi ya Zabuni ya Halmashauri kumbukumbu ya majadiliano yanayohusu taratibu za ununuzi zikiwa na angalau taarifa zifuatazo: (a) Maelezo mafupi kuhusu vitu, ujenzi au huduma zinazotarajiwa kutolewa na haja iliyosababisha Bodi kuitisha zabuni; (b) Majina na anuani ya Wazabuni waliowasilisha zabuni, maelezo kuhusu sifa au ukosefu wa sifa za wazabuni waliowasilisha zabuhi zao; (c) Bei au msingi wa upangaji wa bei na muhtasari wa masharti mengine muhimu ya kila zabuni na ya kila mkataba wa uagizaji wa mali, huduma na ujenzi; (d) Muhtasari wa tathmini na mlinganisho wa zabuni pamoja na upendeleo uliokuwepo katika tathmini hiyo; (e) Kama zabuni zilikataliwa tamko kuhusu uamuzi huo na sababu za uamuzi huo; (f) Kama utaratibu mwingine wa kupata vitu au huduma mbalimbali ya utaratibu wa zabuni ndio uliotumika, basi tamko kuhusu sababu zilizoifanya Bodi iamue kutumia utaratibu huo mwingine; (g) Kama zabuni ilikataliwa kwa kuwa mzabuni alitoa, alikubali kutoa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kwa mtumishi wa sasa au wa zamani wa Halmashauri, bakshishi ya aina yoyote, ahadi ya 35 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) kumwajiri au kitu chochote kinachohusiana na ajira au chenye thamani, kama hamasisho kwa utendaji au uamuzi au utaratibu wa kutumia, tamko kuhusu jambo hilo; (h) Katika upataji wa huduma, sababu na hali iliyoifanya Bodi kuchagua utaratibu wa kutumia katika upataji huo wa huduma; (i) Katika upataji wa vitu au huduma ambao Bodi imeamua kudhibiti ushiriki kwa misingi ya Taifa, Mkoa au Wilaya, tamko kuhusu sababu na hali iliyofanya Bodi kudhibiti ushiriki huo; (j) Katika upataji wa vifaa na huduma kwa kuwaomba watoaji kutoa mapendekezo yao moja kwa moja tamko la sababu na hali iliyofanya Bodi kuamua kutumia utaratibu huo; na (k) Muhtasari wa maombi yoyote ya ufafanuzi kuhusu mchujo wa zabuni au nyaraka za zabuni na majibu yaliyotolewa pamoja na muhtasari wa marekebisho yoyote yaliyofanywa katika nyaraka hizo. (2) Sehemu ya kumbukumbu zilizotajwa kwenye kanuni ndogo ya (1)(a) na (b) zitatolewa, endapo zitaombwa, kwa mtu yeyote baada ya zabuni kutangazwa, kufunguliwa na kukubaliwa, au baada ya kusimamishwa kwa taratibu za uagizaji bila ya kuingia katika mkataba wa uagizaji. (3) Sehemu ya kumbukumbu zilizoelekezwa katika kanuni ndogo ya (1)(c) hadi (g), endapo zitaombwa, itatolewa kwa wazabuni waliowasilisha zabuni baada ya zabuni kukubaliwa au baada ya kusitishwa bila ya kuingia kwenye mkataba wa utoaji wa vitu au huduma. (4) Isipokuwa kama itaelekezwa hivyo na Mahakama yenye mamlaka na kwa kuzingatia masharti ya maelekezo hayo, Bodi haitatoa taarifa: (a) ikiwa utoaji huo wa tarifa utakuwa kinyume cha Sheria, utazuia utekelezaji wa Sheria, hautakuwa na maslahi kwa umma, utahatarisha maslahi halali ya kibiashara ya wahusika au utazuia ushindani halali; na (b) zinazohusu uchambuzi, tathmini na ulinganisho wa zabuni pamoja na bei isipokuwa muhtasari ulioelezwa kwenye kanuni ndogo ya (1)(e). 36 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (5) Mara baada ya zabuni kujadiliwa na Bodi, Katibu atamjulisha mzabuni aliyefanikiwa ili makubaliano ya nyaraka za mkataba yaweze kufikiwa. (6) Nakala za muhtasari zitapelekwa kwa siri kwa kila Mjumbe wa Bodi, Mkurugenzi, Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani na Mkuu wa Divisheni husika kwa taarifa na kumbukumbu. (7) Kila mzabuni ambaye hakufanikiwa atajulishwa na, pale atakapoomba, atapewa sababu za kutokubaliwa kwa zabuni aliyowasilishwa. (8) Bodi ya Zabuni kwa kuzingatia masharti ya kanuni za uagizaji itaandaa taarifa ya mwenendo na maamuzi ya zabuni zilizoitishwa na kuwasilishwa kwenye Mkutano wa kawaida wa Halmashauri kupitia Kamati ya Kudumu husika. 67. Katika mkataba wowote wa kimaandishi, yatawekwa maneno ambayo yataonesha kuwa Halmashauri itakuwa na haki kusitisha mkataba na kumdai Mkandarasi malipo ya fidia kutokana na kusimamishwa kwa mkataba huo endapo Mkandarasi atabainika kuwa ameahidi kutoa au ametoa, au amekubali kutoa kwa mtu yeyote zawadi yoyote au upendeleo wa aina yoyote kama kishawishi au zawadi kwa kufanya au kumpendelea au kutomkubali mtu yeyote kuhusiana na mkataba na Halmashauri au kama vitendo hivyo vitakuwa vimefanywa na mtumishi yeyote aliyeajiriwa naye au kwa niaba yake iwe Mkandarasi anafahamu au hafahamu atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kudhibiti Rushwa ya Mwaka 2007. Uzuiaji wa rushwa Usimamizi wa mikataba 68.-(1) Mkurugenzi wa Halmashauri atawajibika katika usimamizi na ufuatiliaji mzuri wa Mikataba. (2) Mkataba wa upataji vitu hautabadilishwa kwa namna yoyote ile baada ya kutiwa saini na pande zinazohusika isipokuwa kama mabadiliko hayo ni: (a) kwa faida ya Halmashauri na hayailetei hasara Halmashauri; (b) yamethibitishwa na Bodi ya Zabuni ya Halmashauri; na (c) Upande mwingine unaafiki. (3) Malipo ya mwisho hayatafanywa mpaka mkataba mzima utakapokuwa umekamilika kutokana na kuridhika kwa 37 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Uvunjaji wa mkataba Rejesta ya mikataba Diwani au Afisa kutokuwa na maslahi katika mikataba Halmashauri na kulingana na vipengele vya mkataba unaohusika. (4) Malipo ya fedha za salio hayatalipwa mpaka upite muda wa miezi sita na kazi iwe haina kasoro. 69. Endapo mkataba uliotiwa lakiri au muhuri na Halmashauri haukufuatwa na mkandarasi, ikiwa ni pamoja na ucheleweshaji usiokuwa wa kimsingi, Mkurugenzi atashauriana mapema iwezekanavyo na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa kwenye mkataba, itaamua hatua muafaka za kuchukua na kumfahamisha Mkandarasi juu ya uamuzi. 70.-(1) Mkurugenzi atatunza maelezo yote ya mikataba kwenye rejesta ya mikataba na atafanya ulinganifu wa malipo halisi na yale yaliyoidhinishwa. (2) Taarifa ya matumizi yote ya ziada lazima yapelekwe kwenye Bodi ya Zabuni yakiambatana na maelezo kutoka kwa Mkurugenzi. 71.-(1) Endapo Diwani au Afisa wa Halmashauri ana maslahi ya kifedha ya moja kwa moja au vinginevyo katika mkataba wowote, mkataba unaopendekezwa au jambo lolote, na yupo kwenye Mkutano wa Halmashauri au Kamati ambapo mkataba huo, au mkataba unaopendekezwa au jambo lingine lolote linajadiliwa, atatangaza jambo hilo mara Mkutano unapoanza na hatashiriki wala kuwepo katika majadiliano au kupiga kura kuhusu jambo linalohusu mkataba au mkataba unaopendekezwa au jambo lingine lolote ambalo ana maslahi nalo. (2) Kanuni hii haitatumika kuhusiana na maslahi katika mkataba au suala lingine ambalo Mjumbe au Afisa wa Halmashauri ana maslahi nalo kama mlipa kodi au mkazi katika eneo lililo katika himaya ya Halmashauri. (3) Diwani atahesabika kuwa na maslahi ya moja kwa moja katika mkataba au suala lingine endapo: (a) yeye au mtu aliyemchagua ni Mjumbe wa kampuni au chombo kingine au anayo hati ya hisa katika kampuni ambayo itaingia, au imependekezwa 38 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) iingie katika mkataba, au anauhusiano wa kifedha katika jambo linalojadiliwa; au (b) yeye ni mbia au ameajiriwa na mtu ambaye mkataba unafanywa naye, au utakuwa chini yake, au anao uhusiano wa kifedha wa moja kwa moja katika suala linalojadiliwa au kuzungumzwa. (4) Katika Kanuni hii maslahi ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja ya mwanandoa au ndugu wa familia kama inafahamika kwa Mjumbe wa Halmashauri itachukuliwa kuwa ni maslahi ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja. (5) Taarifa ya jumla itakayotolewa kwa Mkurugenzi na Diwani au Afisa wa Halmashauri kuhusiana na yeye, mwenza wake au ndugu yake kwamba ana maslahi ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja katika mkataba unaokusudiwa au jambo lingine na akieleza aina ya maslahi itachukuliwa, isipokuwa pale atakapoondoa taarifa hiyo, kuwa ametoa taarifa ya kutosha ya maslahi yake kuhusiana na suala ambalo limo katika mjadala. (6) Mkurugenzi ataandika taarifa za watu wenye maslahi waliotoa taarifa chini ya Kanuni Ndogo ya (1) na taarifa yoyote iliyomo katika Kanuni Ndogo ya (5) itakuwa wazi kwa ukaguzi wakati wa Saa za kazi. (7) Halmashauri inaweza baada ya kupata kibali cha Waziri, kuondoa kizuizi chini ya Kanuni hii kinachoifanya ishindwe wakati wowote kufanya Mkutano pale ambapo idadi ya Wajumbe wenye maslahi ni kubwa mno kiasi cha kukwamisha shughuli za Halmashauri au itakuwa ni kwa maslahi ya wakazi wa Halmashauri kuondoa kikwazo hicho. (8) Katika Kanuni za Kudumu hizi ,ndugu wa familia itachukuliwa kuwa ni pamoja na wazazi au walezi, mtoto, kaka, au dada na wanandoa wao. SEHEMU YA SITA MASUALA MENGINE na Kiapo kukubali wadhifa 72.-Kila Diwani kabla ya kushika wadhifa wake kama Diwani na kabla ya Mkutano wa kwanza wa Halmashauri: (a) atakula kiapo kama kilivyooneshwa kwenye Jedwali la Pili la Kanuni hii ya Kudumu kitakachosimamiwa na Hakimu Mkazi au Hakimu wa Wilaya; na 39 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (b) atatoa tamko la kimaandishi lililoandikwa kwa Mkurugenzi akiahidi kutekeleza jambo linalohusiana na tamko la maslahi katika shughuli za kibiashara, mali, na kadhalika na kuzifuata Kanuni za Maadili ya Madiwani. Majukumu ya Diwani 73.-(1) Diwani atakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuwa karibu na wapiga kura na kupata ushauri wa Wananchi katika mambo yanayotarajiwa kujadiliwa kwenye Halmashauri; (b) kutoa maoni na mapendekezo ya wananchi kwa Halmashauri; (c) kuhudhuria Mikutano ya Halmashauri na ya Kamati au Kamati Ndogo ambamo yeye ni Mjumbe; (d) kutenga angalau siku moja kila mwezi kukutana na wananchi katika eneo lake la uchaguzi; (e) kutoa taarifa kwa wapiga kura kuhusu maamuzi ya jumla ya Halmashauri na hatua zilizochukuliwa na Halmashauri kuondoa matatizo yaliyowahi kuelezwa na wakazi wa eneo lake la uchaguzi; (f) kuchangia ujuzi na uzoefu wake katika majadiliano yanayofanyika katika Mikutano ya Halmashauri na Kamati za Halmashauri; na (g) kushiriki katika shughuli za pamoja za maendeleo katika eneo lake la uchaguzi na katika eneo zima la Halmashauri. (2) Katika kutekeleza wajibu wake, diwani atazingatia: (a) maslahi ya Taifa na maslahi ya wananchi katika eneo la Halmashauri; (b) Katiba, sheria na kanuni; na (c) Kanuni za Maadili ya Madiwani, mwongozo kuhusu mahusiano ya madiwani na watumishi na miiko mingine. Nafasi wazi 74.-(1) Kiti cha Mjumbe wa Halmashauri kitakuwa wazi endapo Mjumbe: (a) atafariki; (b) atakubali ajira kama mtumishi wa Halmashauri; (c) kwa mujibu wa Sheria yoyote atatangazwa kuwa hana akili timamu; 40 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (d) yuko chini ya hukumu ya kifo au kifungo kinachozidi miezi sita kilichotolewa kwake na mahakama; (e) kwa mujibu wa Sheria yoyote anatamkwa kuwa anapoteza sifa za kuendelea kuwa Mjumbe; (f) atakoma kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichompendekeza kuwa mgombea wa kiti cha udiwani; (g) anapokuwa amepatikana na kosa kutokana na Kanuni za Maadili ya Madiwani na adhabu ya kosa alilotenda ni pamoja na kumwondoa Mjumbe madarakani; (h) anapoteza ujumbe kwa mujibu wa kanuni ndogo ya 71(2); (i) anahukumiwa kwa kosa la kutotaja maslahi yake; (j) amejiuzulu kutoka kwenye kiti chake; (k) Halmashauri imevunjwa na kuathiri mipaka ya majimbo ya uchaguzi; (l) uchaguzi wa Mjumbe umetangazwa kuwa batili; au (m) bila sababu ya kuridhisha au bila idhini au kibali cha maandishi cha Mwenyekiti, Mjumbe anakosa kawaida kuhudhuria Mikutano mitatu inayofuatana ya Halmashauri au Kamati ambayo yeye ni Mjumbe. ya Sura ya 288 Kutokuwep o kwa Wajumbe (2) Waziri atatangaza kiti kuwa wazi pale atakapojulishwa na Meya kwa maandishi kwamba kiti kiko wazi kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 42(1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji). 75.-(1) Halmashauri yaweza kutoa idhini ya kutokuwepo katika Mikutano yake kwa muda usiozidi miezi kumi kwa Mjumbe yeyote anayetaka kwenda nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (2) Pale ambapo Mjumbe kwa sababu yoyote ile amekuwa nje ya nchi kwa muda unaozidi miezi kumi kiti chake cha udiwani kitachukuliwa kuwa kipo wazi. Taratibu za kutunga 76.-(1) Pale ambapo Halmashauri inakusudia kutunga Sheria Ndogo itatoa tangazo kwa wakazi wa eneo husika kuhusu 41 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Sheria Ndogo Ukaguzi wa nyaraka itahakikisha kuwa kusudio hilo katika namna ambayo watakaoathirika na Sheria Ndogo inayokusudiwa kutungwa wanafahamu vilivyo na kuwaomba wanaopenda kutoa pingamizi lolote au mapendekezo yao kwa maandishi katika muda uliowekwa. (2) Pale ambapo baada ya muda wa taarifa kumalizika hakuna pingamizi au malalamiko yaliyowasilishwa, au hakuna mtu yeyote aliyetoa kipingamizi kinachokubalika mbele ya Halmashauri, Halmashauri itaendelea kutunga Sheria Ndogo ikizingatia malalamiko na pingamizi zilizotolewa. (3) Sheria Ndogo zikishatungwa na Halmashauri zitapelekwa kwa Waziri ili aweze kuziidhinisha. (4) Waziri anaweza kuidhinisha, kukubali au kukataa kuidhinisha Sheria Ndogo au kutoa au kusimamisha kibali chake kwa kutoa masharti atakayoyaeleza na anaweza baada ya kutoa idhini yake, kupanga tarehe ya kuanza kutumika kwa Sheria Ndogo hizo. (5) Waziri anaweza, kabla ya kuidhinisha Sheria Ndogo zenye athari kwenye maeneo yaliyotengwa au maeneo maalum au kwa Sheria nyingine yoyote, kushauriana na Waziri anayehusika na Sheria husika au na jambo lililotungiwa Sheria Ndogo kadri itakavyokuwa. (6) Sheria Ndogo yoyote iliyotungwa na Halmashauri lazima itangazwe katika Gazeti la Serikali kabla ya kuanza kutumika. 77.-(1) Mjumbe anaweza, kwa madhumuni ya kutekeleza wajibu wake kama Mjumbe, na si vinginevyo, kukagua waraka wowote ambao umejadiliwa na Kamati ya Halmashauri na kama nakala zinapatikana, anaweza kupewa, akiomba, nakala kwa madhumuni hayo hayo. (2) Mjumbe hatakagua kwa makusudi au kutaka apewe nakala ya waraka wowote unaohusu jambo ambalo yeye ana maslahi nalo kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji),. Hata hivyo Kanuni hii haitamzuia Mkurugenzi kuzuia kukaguliwa kwa waraka wowote ambao umezuiliwa kutolewa kwa mujibu wa Sheria yoyote au Kanuni zilizotungwa chini ya Sheria hizo. 42 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Uanzishaji wa Bodi za Huduma Diwani kutembelea maeneo, shughuli au miradi mbalimbali 78.-(1) Halmashauri inaweza, kwa mujibu wa kifungu cha 88 cha Sheria, kwa madhumuni ya kutekeleza kazi zake katika eneo lililo chini ya Mamlaka yake, kuunda Bodi za Huduma kwa hati rasmi iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali, kama itakavyoona inafaa kufanya hivyo. (2) Bodi ya Huduma iliyotajwa katika kanuni ndogo ya (1) itawajibika moja kwa moja kwenye Halmashauri kupitia Kamati ya Kudumu husika na itatekeleza kazi zake kama ilivyofafanuliwa katika hati inayoianzisha. 79.-(1) Mjumbe wa Halmashauri anaweza kutembelea jengo, shughuli au miradi mbalimbali za miradi eneo, zinazotekelezwa na au kwa niaba ya Halmashauri na anaweza kutuma taarifa kwa Mkurugenzi akieleza sababu za matembezi yake ili aweze kupangiwa Wataalam wa mradi au shughuli husika kwa ajili ya kupata maelekezo ya kitaalam. (2) Mjumbe wa Halmashauri anapotembelea shughuli au miradi ya maendeleo inayotekelezwa na au kwa niaba ya Halmashauri hataruhusiwa kutoa maelekezo au maagizo ya kitaalam awapo kwenye eneo la mradi. (3) Baada ya Diwani kutembelea maeneo au majengo kama ilivyoainishwa kwenye kanuni ndogo ya (1) ataona kuna umuhimu wa kutoa maoni au mang’amuzi yake juu ya matembezi hayo atafanya hivyo kwa kuwasilisha maoni au mang’amuzi yake kwa Mkurugenzi ambaye atafanyia kazi au kuyapeleka kwa Afisa anayesimamia kazi husika kwa utekelezaji. (4) Endapo maoni au mang’amuzi ya Diwani hayawezi kufanyiwa kazi na Mkurugenzi au Afisa mhusika, basi atamshauri Diwani kupeleka maoni na mang’amuzi yake kwa Kamati inayohusika ili yachunguzwe zaidi na kuamuliwa. (5) Kamati za Kudumu za Halmashauri zinaweza kutembelea miradi ya maendeleo au shughuli yoyote inayotekelezwa na au kwa niaba ya Halmashauri ili mradi katika kutembelea miradi hiyo Kamati itaongozana na Wataalam wa mradi au shughuli husika ili kupata maelekezo ya kitaalam. (6) Kamati ya Kudumu itatembelea miradi au shughuli za maendeleo kabla ya Kikao cha Kamati ambacho kitajadili mradi au shughuli hiyo. 43 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Uhifadhi wa Lakiri ya Halmashau ri Utiaji Muhuri kwenye nyaraka 80. Lakiri ya Halmashauri itatunzwa kwa usalama na kufungiwa katika Kasiki kwenye Ofisi ya Mkurugenzi mwenyewe. 81.-(1) Lakiri ya Halmashauri haitabandikwa katika Hati yoyote mpaka ubandikaji huo umeidhinishwa na azimio la Halmashauri likiidhinisha kukubaliwa kwa zabuni, ununuzi, uuzaji au upangishaji au kuchukua mali yoyote, utoaji wa Hati yoyote ya ukopeshaji fedha, uwasilishaji wa madai yoyote, uwekaji wa viwango vya kodi, uingiaji kwenye mkataba, kutunga Sheria Ndogo, au hati yotote iliyo rasmi ambayo kwa mujibu wa Sheria au Kanuni yoyote inahitaji kuwekwa lakiri ya Halmashauri. (2) Lakiri itashuhudiwa au kuthibitishwa na Meya au Naibu Meya na Mkurugenzi, na hati zilizowekwa lakiri zitasainiwa na Meya au Naibu Meya, kama hali itakavyokuwa. Uandikisha ji wa anuani 82.-(1) Itakuwa wajibu wa kila Mjumbe katika kikao cha kwanza cha Halmashauri, baada ya uchaguzi kutoa taarifa ya maandishi kwa Mkurugenzi juu ya anuani yake ya kudumu ya kupokelea taarifa. Taarifa zilizopelekwa kwa kutumia anuani iliyoandikishwa itachukuliwa kama ndiyo sahihi na inatosheleza kwa matumizi yote. (2). Iwapo Mjumbe atatoa taarifa ya maandishi kwa Mkurugenzi kuwa angependa taarifa ya Mikutano ya inatumwa kwake kwa kutumia anuani iwe Halmashauri atakayoitaja kwenye taarifa hiyo ambayo ni tofauti na ile katika Kanuni Ndogo ya (1), itakayoachwa au itakayotumwa kwa njia ya posta kwa kutumia anwani hiyo itachukuliwa kuwa taarifa inayotakiwa kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu hii. inatosha kwa ajili ya kutoa taarifa yoyote Uteuzi wa Wajumbe kwenye Taasisi za nje 83.-(1) Katika Mkutano wake wa kwanza, Halmashauri itateua wawakilishi wake kwenye Bodi na Taasisi za nje ambazo Halmashauri inastahili kuwakilishwa. (2) Mjumbe au Wajumbe, wanaoiwakilisha Halmashauri kwenye Bodi na Taasisi za nje, watatakiwa kuwasilisha kwa Mkurugenzi taarifa kuhusu shughuli za Bodi au Taasisi 44 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) zinazogusa Sera na maslahi ya Halmashauri na wakazi wake kijumla na Mkurugenzi atachukua hatua zinazofaa. Kumwondo Meya a madarakani 84.-(1) Halmashauri inaweza kumwondoa Meya madarakani kwa azimio linaloungwa mkono na theluthi mbili ya Wajumbe kutokana na hoja au sababu yoyote kati ya sababu zifuatazo: (a) Kutumia nafasi yake vibaya; (b) Kushiriki katika vitendo vya rushwa; (c) Kushindwa kutekeleza majukumu yake; (d) Mwenendo mbaya au ukosefu wa maadili; au (e) Ulemavu wa kimwili au kiakili kwa kiasi cha kumfanya kushindwa kutekeleza majukumu yake kama Meya. (2) Hoja au sababu zitakazotolewa lazima iwe imetimiza masharti yafuatayo: (i) Iwe na tuhuma mahsusi yenye ushahidi wa kutosha; au (ii) Iwe imetolewa maelezo kamili na yenye kueleweka kuhusu tuhuma zinazohusika. (3) Kwa madhumuni ya kumwondoa Meya madarakani, kwa sababu zozote zilizotamkwa chini ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri itatumia taratibu zilizotolewa katika Taratibu za Kumwondoa Meya zilizotangazwa kwenye gazeti la Serikali na Waziri kwa mujibu wa Sheria. SEHEMU YA SABA POSHO KWA WAJUMBE Aina posho za 85.-(1) Wajumbe wa Halmashauri watalipwa posho mbalimbali kama itakavyopendekezwa na Halmashauri na kuidhinishwa na Waziri. (2) Posho zitakazolipwa kwa Wajumbe wa Halmashauri zitakuwa za aina zifuatazo: (a) posho ya usafiri; (b) posho ya kuhudhuria kikao; (c) posho ya madaraka; (d) posho ya kujikimu; (e) posho ya mwezi; na (f) kiinua mgongo. 45 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (3) Endapo Mjumbe wa Halmashauri ataugua au ataumia wakati akifanya kazi aliyotumwa na Halmashauri, gharama za matibabu yake zitalipwa na Halmashauri. Posho endapo Mkutano utaahirishwa 86. Endapo Mkutano wa Halmashauri au Kamati utaahirishwa kwa sababu ya kukosekana kwa akidi, Mjumbe au Wajumbe waliofika kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano huo ulioahirishwa watastahili malipo yaliyotajwa katika kanuni ya 84(2)(a) na (d) iwapo wamelazimika, bila kukusudia, kulala njiani au kwenye Makao makuu ya Halmashauri. Hakuna malipo ya posho ya kuhudhuria kikao yatakayofanywa katika hali ya namna hiyo. SEHEMU YA NANE MABADILIKO KWENYE KANUNI ZA KUDUMU Kusitisha utumiaji wa Kanuni za Kudumu 87.-(1) Kanuni yoyote inaweza kusitishwa kwa azimio lililoungwa mkono na theluthi mbili za Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Halmashauri kwa hoja iliyopendekezwa bila taarifa kwa madhumuni ya kuwezesha shughuli yoyote iliyofafanuliwa ili ishughulikiwe na Halmashauri kama jambo la dharura au lenye manufaa. (2) Halmashauri haitasitisha matumizi ya Kanuni yoyote kama kusitisha huko kutasababisha kufanya jambo ambalo limezuiliwa na Sheria au kutofanya linalotakiwa kufanywa chini ya Sheria yoyote. jambo Marekebish o na mabadiliko ya Kanuni za Kudumu 88. Halmashauri inaweza kubadilisha, kuongeza, kurekebisha au kutengua Kanuni ya kudumu hii kwa azimio lililoungwa mkono kwa wingi usiopungua theluthi mbili ya kura na baada ya kupata idhini ya Waziri. Kanuni za Kudumu kutolewa kwa Wajumbe Kutafsiri Kanuni za Kudumu 89. Nakala iliyochapishwa ya Kanuni ya Kudumu hii itatolewa na Mkurugenzi kwa kila Mjumbe. 90. Uamuzi wa Meya kuhusu maana ya matumizi ya Kanuni hii au mwenendo wa Mkutano wa Halmashauri hautapingwa wakati wa Mkutano wowote wa Halmashauri. 46 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) SEHEMU YA TISA ZIARA ZA WAJUMBE Ziara Wajumbe za 91.-(1) Wajumbe wa Halmashauri wanaweza kwenda ziara mbalimbali za mafunzo ili mradi ziara hizo ziwe zimeainishwa kwenye mpango na Bajeti ya Halmashauri, isipokuwa kwa ziara ambazo gharama zake hazihusiani na Bajeti ya Halmashauri, Wajumbe watafanya ziara hizo kwa mujibu wa ratiba ya mpango huo. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1) Halmashauri kabla ya kuruhusu kufanyika kwa ziara itahaikikisha kwamba: (a) shughuli ya ziara hiyo zinazofanywa na Halmashauri; inafanana na shughuli (b) ziara hiyo inapata kwanza kibali cha Mkuu wa Mkoa; (c) Wajumbe wanakitu cha kwenda kuonesha kule wanakokwenda kujifunza; (d) ziara zinazofanyika nje ya Mkoa zihusishe wadau mbalimbali wa Halmashauri kutegemeana na ziara husika; ziara iwe na matunda yanayoonekana; (e) (f) Wajumbe walioshiriki kwenye ziara warejeapo wanatakiwa kuandaa na kuwasilisha ripoti ya maandishi kwa Halmashauri kuhusu mambo mapya na ya msingi waliyojifunza na kuweka utaratibu mzuri wa kuyatekeleza kwenye Kata zao na kwenye Halmashauri; na Wimbo wa Taifa, Dua au Sala ya kuiombea Halmashau ri (g) ziara zinafanywa kwa vikundi vya Wajumbe wachache kadri itakavyokubalika na Halmashauri. 92. Kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Halmashauri, utaimbwa Wimbo wa Taifa na kufuatiwa na Dua au Sala ya kuiombea Halmashauri ifuatayo: “Ewe MWENYEZI MUNGU Mtukufu, Muumba wa Mbingu na Dunia umeweka katika Dunia Serikali za Wanadamu ili haki yako itendeke. Twakuomba, uibariki Halmashauri yetu ya Jiji la Dar es Salaam idumishe Uhuru, Umoja, Haki na Amani. Uwajalie viongozi wetu wa Halmashauri hekima, afya njema na 47 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) maisha marefu ili pamoja na wanaowashauri wadumishe Utawala Bora. Utuongezee hekima na busara sisi Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na utupe uwezo wa kujadili kwa dhati, mambo yatakayoletwa mbele yetu leo, ili tufanye maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na ustawi wa Halmashauri yetu. Amina”. 93.Kanuni ya Kudumu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ya Mwaka 2015 na Kanuni ya Kudumu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ya Mwaka 2019 zinafutwa. Kufutwa kwa Kanuni za Kudumu TS. Na. 615 la 2015 535 la 2019 48 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) ________ JEDWALI LA KWANZA ________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 45(3)) HADIDU ZA REJEA ZA KAMATI ZA KUDUMU ZA HALMASHAURI YA JIJI Madhumuni ya jumla: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. Kuishauri Halmashauri kutengeneza malengo yanayozingatia matakwa ya Miji na kuchukua hatua ambazo zitaonekana zinafaa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Kuishauri Halmashauri kufanya maamuzi juu ya Sera muhimu. Kuishauri Halmashauri kufanya maamuzi juu ya utoaji wa huduma kulingana na rasilimali walizo nazo. Kuiwezesha Halmashauri kutengeneza taratibu zitakazoongoza utendaji wa Kamati, Kamati Ndogo, na ule wa watumishi ili watimize wajibu wao. Kufanya mapitio yatakayowezesha Halmashauri kuamua juu ya kuongeza, kupunguza, kubinafsisha au kuwashirikisha wadau katika utoaji wa huduma. Kuhakikisha kuwa miundo na taratibu za utendaji wa Halmashauri tija katika kufikia malengo ya zinazingatia ufanisi, uthabiti na Halmashauri, na Kuiwezesha Halmashauri kujenga mahusiano imara kati yake na Serikali kuu, Serikali zingine za Mitaa na Umma kwa ujumla. A. Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango: Majukumu ya jumla: Kamati hii inawashirikisha Wenyeviti wa Kamati zote za kudumu na inapaswa kukutana kila mwezi mara moja. Aidha, madaraka ya Kamati hii ni kama ya Kamati zingine za kudumu na hivyo hairuhusiwi kisheria kufanya kazi au majukumu ya Kamati zingine za kudumu. Kwa ujumla, majukumu yake ni pamoja na kusimamia na kudhibiti ukusanyaji wa mapato na matumizi ya mali ya Halmashauri kwa kupitia vikao vyake. Majukumu Maalum ya Kamati: (i) (ii) (iii) (iv) Kuweka mikakati na kupendekeza uongezaji wa mapato; Kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti na mpango wa Maendeleo kwenye Halmashauri ili kuidhinishwa na Halmashauri; Kusimamia utunzaji wa hesabu za fedha ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mali za Halmashauri, ukusanyaji wa mapato, kufuta madeni, na kuomba vibali maalum kwa matumizi yanayohitaji kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa; Kufikiria na, pale inapowezekana, kupendekeza kwenye Halmashauri masuala yanayohusu Sheria Ndogo na utendaji katika ngazi za chini za Halmashauri; 49 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (v) (vi) (vii) (viii) (ix) (x) (xi) (xii) (xiii) (xiv) (xv) (xvi) (xvii) (xviii) (xix) (xx) (xxi) (xxii) Kupokea na kuzingatia mapendekezo ya kubadili matumizi ya mafungu ya fedha (re-allocation) yaliyopo katika makisio yaliyoidhinishwa na kuyapeleka kwa Halmashauri; Kuratibu mapendekezo kutoka kwenye Kamati zingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi na kuyawasilisha kwenye Halmashauri; Kufikiria na kupendekeza kwenye Halmashauri mikopo yote ya Halmashauri; Kutoa mapendekezo ya vitega uchumi kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290; Kupokea na kujadili taarifa za wakaguzi wa fedha na mali ya Halmashauri na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na maelekezo na maoni ya wakaguzi kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa, Sura ya 290; Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za Halmashauri, kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Waziri na taratibu nyingine zitakazowekwa na Halmashauri; Kupitia marekebisho yote yaliyopendekezwa hususan kuhusu taratibu za fedha, ikiwa ni pamoja na mapitio ya mara kwa mara yanayohusu thamani ya fedha ambapo Kanuni mbalimbali za manunuzi ya mali na vifaa hutumika; Kufikiria na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali, vinavyotolewa na Halmashauri; Kufikiria mapendekezo ya Bajeti na Mipango ya Maendeleo ya kila Kamati ya Kudumu na kuiwasilisha kwenye Halmashauri ili kupata idhini; Kushughulikia tofauti ya mapato na matumizi katika bajeti yote na kupendekeza hatua stahiki ya kuchukua kuondoa mapungufu katika mapato au ziada matumizi; Kufikiria mapendekezo yote yanayohusu matumizi makubwa ya fedha kabla hayajawasilishwa kwenye Halmashauri ili kupata idhini; Kupokea mahesabu ya Mwaka ya Halmashauri na kuhakikisha taarifa ya mahesabu ya Mwaka inawasilishwa kwa wakati kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali; Kupitia na kuidhinisha mpango wa manunuzi wa Halmashauri kwa kuzingatia mpango wa Bajeti uliopitishwa na Halmashauri; Kupitia taarifa ya kila robo Mwaka kuhusu Manunuzi iliyowasilishwa na Afisa Masuuli; Kusimamia utekelezaji wa mikataba ya Halmashauri kwa kukagua miradi inayotekelezwa na vifaa vilivyopokelewa; Kumwelekeza Mkurugenzi kufanya manunuzi au ukaguzi wa huduma au vifaa vilivyonunuliwa ili kupata thamani halisi, itadhihirika kwamba, maelezo yaliyotolewa kuhusu manunuzi ya vifaa au huduma hayaridhishi; Kuidhinisha majina ya wajumbe wa Bodi ya zabuni na wa Bodi zingine kwa mujibu wa Sheria husika; Kushughulikia itakayokayowasilishwa mapendekezo ya hatua za kuchukua; itafanyika hivyo endapo kwenye Kamati wote kutoa wadaiwa orodha ya na 50 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (xxiii) (xxiv) (xxv) (xxvi) (xxvii) (xxviii) (xxix) (xxx) (xxxi) (xxxii) (xxxiii) (xxxiv) Kupendekeza njia na taratibu za kuondosha vifaa chakavu. Uondoshaji wa vifaa unaweza kufanyika kwa njia ya kuuza au kuviharibu; Kujadili na kupitia taarifa za fedha za kila mwezi na kila robo Mwaka; Kupendekeza kwa Halmashauri hatua za kuchukua kuhusu kufuta madeni ya Halmashauri; Kushughulikia Sera kuhusu kukopa na uwekezaji; Kubuni na kupendekeza mpango wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano na Halmashauri nyingine; Kurekebisha na kusimamia makusanyo na matumizi ya mapato ya vijiji na miji midogo kwa mujibu wa Sheria; Kuteua wakaguzi wa fedha/mali za Serikali za Vijiji kwa mujibu wa Sheria, Sura ya 290); Kujadili na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kuhusu mambo yote ya yanayohusu masuala ya ajira na kinidhamu ya wafanyakazi na watumishi; Kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yanayohusu nyumba za Halmashauri; Kupokea na kutoa uamuzi juu ya mapendekezo ya watumishi wanaokwenda masomoni; Kujadili na kupendekeza masuala yote yanayohusu maslahi ya jumla ya watumishi, ikiwa ni pamoja na mikopo, nyumba, usafiri, matibabu, rambirambi na motisha nyinginezo; na Kupitisha mapendekezo ya kuthibitisha watumishi kazini baada ya kumaliza kipindi cha majaribio kulingana na miundo husika ya utumishi. B: Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya: Majukumu ya Jumla Kushughulikia mambo yote yanayohusu afya ya jamii, elimu na huduma za maji. Kamati hii pia itashughulikia mambo yanayohusiana na jitihada za wananchi Mitaani kujiletea maendeleo yao kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushauri, kushawishi, kuzindua, kuelimisha na kushirikisha wananchi hao hasa katika kutayarisha, kutekeleza, kusimamia na kutathmini mipango yao ya maendeleo. Majukumu maalum ya Kamati: (i) (ii) (iii) (iv) Kuandaa mipango madhubuti ya maendeleo ya upanuzi na ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na zahanati; Kuandaa mipago ya maendeleo ya upanuzi na ujenzi wa shule za awali na msingi na elimu ya watu wazima kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya 1978 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2020; Kupendekeza mipango ya ujenzi au upanuzi wa vituo, viwanja, majengo na mazingira ya burudani, starehe, mapumziko na michezo; Kuamua juu ya mambo yanayohusu uhifadhi wa mambo ya kale na mandhari mbalimbali yenye sura nzuri; 51 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (v) (vi) Kuandaa na kuratibu njia bora juu ya uhifadhi wa nyaraka muhimu kwa ajili ya kumbukumbu hizo zitahifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288; Kupendekeza njia bora juu ya uhifadhi wa sanaa mbalimbali za ufundi na za maonyesho kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288; (vii) Kupendekeza matumizi mazuri ya lugha ya taifa; (viii) (ix) (x) (xi) Kupendekeza namna ya malezi ya vijana ili waweze kuwa wazalishaji katika Taifa; Kusimamia uanzishaji wa uendelezaji wa vikundi vya jamii na vya hiari vya wananchi katika Halmashauri kwa mujibu wa Sera ya maendelo ya jamii; Kusimamia na kuhakiki maeneo ya misitu, mapori, na mbuga zilizotengwa kama hifadhi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa; Kupendekeza na kufanya tathmini ya uendelezaji wa mabonde, mito na mabwawa; (xii) Kubuni na kupendekeza namna ya kudhibiti moto; (xiii) (xiv) (xv) Kubuni na kupendekeza mikakati ya utumiaji wa nishati mbadala, kuzuia ukataji miti ovyo, na kuhimiza upandaji miti kwa wingi; Kuhakikisha kwamba ukaguzi wa majengo unafanyika mara kwa mara; Kupendekeza mipango madhubuti ya ujenzi wa barabara vijijini na wilayani kwa ujumla; na (xvi) Kupendekeza Sheria Ndogo zinazohusu Kamati hizi. C: Kamati ya Kudumu ya Kudhibiti Ukimwi Majukumu ya Kamati: 1. 2. 3. 4. Kushirikisha wadau tofauti katika maeneo husika ili kuongeza uchangiaji wa mawazo na au nyenzo, usimamizi, uratibu na utekelezaji wa kazi za Tume za kudhibiti UKIMWI. Kusimamia uundaji wa Kamati zote za kudhibiti UKIMWI. Kupendekeza na kuchambua hali ya UKIMWI au Mipango na utekelezaji wake na kufikisha katika ngazi husuka kwa hatua zaidi. Kutathmini hali ya UKIMWI katika eneo lake: (i) (ii) Idadi ya waathirika: wagonjwa, yatima, wajane; Kasi ya maambukizo; (iii) Mazingira maalum yanayochangia maambukizo; 52 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (iv) Uelewa wa wananchi juu ya janga hili; (v) (vi) (vii) (viii) Serikali haitatoa fedha kwa Halmashauri isiyokuwa na mipango madhubuti ya kudhibiti UKIMWI; Kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shule anafanya hivyo; Kuweka mikakati ya makusudi juu ya njia bora za kuchangia baadhi ya huduma za Elimu na Afya; Kubuni na kupendekeza njia bora za kuzuia na kudhibiti magonjwa ya milipuko; na (ix) Kupendekeza Sheria Ndogo za Kamati hii. D: Kamati ya Mipango Miji na Mazingira: Majukumu ya jumla Kamati hii itashughulikia masuala ya uzalishaji mali ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, madini, Biashara. Aidha, itashughulikia pia miundombinu na suala zima la maendeleo ya Ardhi na hifadhi ya mazingira. Majukumu maalum ya Kamati: (i) (ii) Kupendekeza kwa Halmashauri mipango ya kupanua biashara na jinsi ya kukusanya mapato yatokanayo na upanuzi huo; Kupendekeza mipango ya matumizi ya ardhi katika eneo la Halmashauri; (iii) Kusimamia na kushawishi matumizi ya nguvu kazi; (iv) (v) (vi) Kuandaa mipango madhubuti ya maendeleo ya upanuzi wa kilimo katika Halmashauri; Kusimamia na kuhakiki miradi ya ujenzi wa masoko, minada, majosho na vituo vya mifugo; na Kushughulikia uanzishaji na uendelezaji wa vyama vya ushirika kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika. FAHARASA – HALMASHAURI ZA MIJI A Agenda za Kamati Akidi katika Mikutano ya Halmashauri Akidi kwenye Mikutano ya Kamati Kanuni Namba 50 9 56 53 Kifungu cha Sheria Sura ya 288 Kifungu 36 Sura ya 288 Kifungu 51(2) na (3) Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Athari za nafasi wazi kwenye Kamati 55 Sura ya 288 Kifungu 51(1);51(3) B C D Diwani au Afisa kutokuwa na maslahi katika mikataba Diwani kutembelea maeneo, shughuli mbalimbali za ujenzi nk. Wimbo wa Taifa na Dua ya kuiombea Halmashauri E F Fujo zinazosababishwa na umma Fujo zinazosababishwa na Wajumbe G H Haki ya kujibu Hoja kuhusu matumizi Hoja na marekebisho ya hoja Hoja za Meya Hoja Halmashauri Hoja zinazoweza kutolewa bila taarifa I J K Kamati za Kudumu Kamati za pamoja Kanuni za kudumu kutumika katika Mikutano ya Kamati Kanuni za kudumu kutolewa kwa Wajumbe Kauli zenye kashfa Kiapo na kukubali wadhifa Kuidhinishwa kwa Taarifa ya Kamati Kufikiriwa upya maamuzi Kufutwa kwa Kanuni zilizopo zinazohusu watumishi wa Kujiuzulu ujumbe wa Kamati na kujazwa kwa nafasi iliyoachwa wazi. Kujiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Kamati Kumbukumbu ya mahudhurio. Kumwondoa Meya madarakani Kupokelewa kwa taarifa za Kamati Kuruhusu watu na vyombo vya Habari kwenye Mikutano ya Halmashauri. Sura ya 288 Kifungu 43 Sura ya 288 kifungu 40 (2) Sura ya 288 kifungu 25(5); GN 263 ya 1995 Sura 288 kifungu 39(1) 70 78 91 19 18 22 33 20 16 38 21 41 44 57 88 28 71 35 60 92 63 62 12 83 34 13 54 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Ushiriki wa Umma Kusitisha utumiaji wa Kanuni za Kudumu Kutafsiri Kanuni za Kudumu Kuthibitisha muhtasari Kutokuwepo kwa Wajumbe Kutunza siri za Majadiliano ya Kamati na Kamati Ndogo. L M Maamuzi ya Mikutano ya Halmashauri Mahudhurio katika Mikutano ya Kamati Majukumu ya Diwani Marekebisho na mabadiliko ya Kanuni za kudumu Maswali Maswali ya papo kwa papo Mihtasari ya Kamati za maendeleo za Kata na Mitaa. Mihtasari kupelekwa kwa Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa. Mihtasari ya Kamati Mikutano ya Kamati Mikutano ya kawaida ya Halmashauri Mtoa hoja kualikwa kwenye Mkutano wa Kamati. Mkutano wa Bajeti Mkutano wa Mwaka Mkutano maalum wa Halmashauri Mkutano maalum wa Kamati Mwaliko wa wasiokuwa Wajumbe N Nafasi wazi P Aina za posho Posho endapo Mkutano utaahirishwa Q 39 86 89 15 74 61 29 51 72 87 23 24 31 32 59 47 3 52 6 7 5 49 30 73 84 85 55 Taz.pia Sura ya 290 Kifungu 47 Sura ya 288 Kifungu 40(1) Sura ya 288 Kifungu 34(1) Sura ya 288 Kifungu 34(3) Sura ya 288 Kifungu 45, 50 Sura ya 288 Kifungu 42(2) Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Sura ya 288 Kifungu 35 Sura ya 288 Kifungu 38 Sura ya 288 Kifungu 45(1) R Rejesta ya mikataba S T Taarifa za Kamati Taarifa kutoka kwenye kata Taarifa za Mikutano Tafsiri Taratibu za kutunga Sheria Ndogo Taratibu za Majadiliano Taratibu za Uagizaji U Uahirishaji wa vikao Uandikishaji wa Anwani Uandishaji wa Bodi za Huduma Uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Halmashauri Uhalali wa majadiliano ya Halmashauri Uhuru wa kutoa mawazo wakati wa majadiliano Ukaguzi wa nyaraka Akidi kwenye Mikutano ya Kamati Upigaji kura kwenye Mikutano ya Kamati Usimamiaji wa mikataba Utaratibu wa shughuli za Mikutano Uteuzi wa Wajumbe kwenye Taasisi za nje Utiaji mhuri kwenye Nyaraka Uvunjaji wa mkataba Uwezo wa Halmashauri kujigeuza kuwa Kamati ya Halmashauri nzima. Uwezo wa Kamati Uzuiaji wa Rushwa V W Waalikwa wasiokuwa Wajumbe kuhudhuria na kushiriki katika Mikutano ya Kamati. X Y Z Ziara za Wajumbe 69 25 26 8 2 75 17 64 40 81 77 10 36 27 76 56 58 67 14 82 80 68 37 43 66 53 90 56 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) ______________ JEDWALI LA PILI ______________ (Limetengezwa chini ya kanuni ya 71(a)) JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KIAPO CHA DIWANI Mimi ………………………………………………………...... naapa au natamka kwa dhati kwamba nitaitumikia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa wadhifa wangu wa Udiwani na kwamba nitahifadhi, nitalinda na kutetea, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria za Tanzania, Maadili ya Madiwani na Kanuni za Kudumu za Halmashauri kama zilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria na kwamba nitaitumikia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa uaminifu, kwa uwezo na moyo wangu wote. (Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie) Kiapo au Tamko hili limetolewa hapa: ……………………………………… Na…………………………………………………………………………….. Leo tarehe……………… Mwezi wa…………………..Mwaka 20………. Mbele ya:……………………………………….. Jina:……………………………………………… Cheo:……………………………………………. Saini:…………………………………………… Anuani………………………………………….. 57 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA TATU _________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 71(b)) JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAMKO LA VIONGOZI WA UMMA KUHUSU RASILIMALI NA MADENI (Kwa mujibu wa Kifungu cha 9 na cha 11 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma) Mimi……………………………………………………………….……………… Anuani; …………………… baada ya kuchaguliwa au kuteuliwa na kuapishwa katika wadhifa wa…….……...tarehe………………….Mwaka 20……. Ninatamka rasmi na kwa moyo mnyofu kwamba hadi sasa nina rasilimali na madeni yafuatayo: (1) Fedha taslimu, Amana katika benki au taasisi ya fedha; taja namba ya akaunti, benki au taasisi ya fedha na kiasi: ………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………….………… 2) Hawala za Hazina na dhamana nyingine maalum:- ………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………..…………………….. ....................................................................... 3) Faida ya akiba, mafungu ya mgawanyo wa faida zinazotokana na hisa ………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………….…………………………… ………………………………………………….. 4) Nyumba au majengo ya kupangisha, taja mahali yalipo na ukubwa au eneo: ………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………..…………………………… …………………………………………………. * Rasilimali zinazotakiwa ni pamoja na zifuatazo, ambazo ni zako binafsi, za mume au mke au watoto wadogo wasiooa au kuolewa wa Kiongozi wa Umma. (a) Fedha taslimu na amana katika Benki au Taasisi nyingine ya fedha. (b) Hawala za Hazina na nyinginezo za dhamana maalum zinazotolewa au kudhaminiwa na Serikali au Vyombo vya Serikali. (c) Faida itokanayo na fedha iliyowekwa akiba Benki, Chini ya Ujenzi au Taasisi nyingine ya fedha. (d) Mgao wa fedha kutokana na fungu la rasilimali ya Kampuni au hisa za Kiongozi wa Umma katika Kampuni au Shirika lolote. 58 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) (e) Maslahi katika chombo cha biashara kisichokuwa na mkataba na Serikali, na kisichokuwa na au kisichotawala amana zinazouzwa bayana na vyombo vya umma. (f) Mashamba ya kibiashara. (g) Mali halisi zisizohamishika ambazo si rasilimali zisizotakiwa kutajwa; na (h) Rasilimali zinazoleta faida, ambazo si rasilimali zisizotakiwa kutajwa na ambazo zinamilikiwa kwa mbali. (5) Mashamba ya kibiashara, mifugo, madini n.k. ………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………… ....................................................................... umma ambayo nyinginezo au maslahi shughuli nyingine za kibiashara au kiongozi wa (6) Magari na aina nyingine za usafiri wa kibiashara; ………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………… ....................................................................... (7) Mashine za kusaga nafaka, viwanda na mitambo:……………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………................................................ .......................................... (8) Rasilimali kutaja:………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………… ....................................................................... (9)Madeni;…………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………… ....................................................................... Tamko hili linatolewa na kusainiwa mbele yangu …………………………………………………………......................................... na (mtoa tamko)………………………………………....................................... ninayemfahamu binafsi, au aliyetambulishwa kwangu na …………………………………………………………………............................. ….…………........................................................................................................ ambaye ninamfahamu leo tarehe ………………………….........Mtoa tamko Mwezi wa ……………………………………………………............................. saini…………………………………………………………… Wadhifa:……………………………………………………… Anuani:………………………………………………………. …………………………………………………………………. (Tamko hili lazima litolewe mbele ya Kamishna wa Viapo) anapenda KWA: KAMISHINA WA MAADILI, SEKRETARIETI YA MAADILI, S.L.P 13341, DAR ES SALAAM. 59 Kanuni Za Kudumu Za Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo La Serikali Na.1075 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutano wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam uliofanyika tarehe 6/3/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- OMAARY MRISHO SATURA, Mkurugenzi wa Jiji, Halmashauri ya Jiji, Dar es Salaam MHE. OMARY KUMILAMOTO, Mstahiki Meya, Halmashauri ya Jiji, Dar es Salaam L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Agosti, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa ncvhi OR-TAMISEMI, 60
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in