Kanuni za Uwekezaji Tanzania za Mwaka 2023
Kanuni hizi zinaweka taratibu za uendeshaji wa taasisi za uwekezaji, maombi ya vivutio, ufuatiliaji wa miradi, na rufaa dhidi ya maamuzi ya Kituo.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Uwekezaji Tanzania za Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This page preserves the statute’s identified version, provision structure, official source link, and stored legal text for reading and research.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Uwekezaji Tanzania za Mwaka 2023
Showing 1 of 1
- document Verify source ↗
Document text
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinaweka taratibu za uendeshaji wa taasisi za uwekezaji, maombi ya vivutio, ufuatiliaji wa miradi, na rufaa dhidi ya maamuzi ya Kituo.
Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) TANGAZO LA SERIKALI Na. 501 la tarehe 21/7/2021 SHERIA YA UWEKEZAJI TANZANIA, (SURA YA 38) ______ KANUNI _____ (Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 5(4) na 35) KANUNI ZA UWEKEZAJI TANZANIA ZA MWAKA 2023 Kanuni Jina MPANGILIO WA VIFUNGU SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI Jina. Tafsiri. SEHEMU YA PILI MAJUKUMU YA BODI Majukumu ya Bodi. Upotezaji sifa kwa wajumbe. Kujaza nafasi zilizoachwa wazi. Akidi. Maamuzi ya Bodi. Azimio kwa maandishi. Mapungufu katika uteuzi. Mgongano wa maslahi. Maslahi yenye manufaa. Katibu wa Bodi. 1 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania SEHEMU YA TATU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA KAMATI YA TAIFA YA UWEKEZAJI NA KAMATI YA WATAALAMU Utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Taifa ya Uwekezaji. Kamati ya Wataalamu. Vikao vya Kamati ya Wataalamu. Majukumu ya Kamati ya Wataalamu. SEHEMU YA NNE UTARATIBU WA UWASILISHAJI WA MASUALA MBALIMBALI KATIKA KAMATI YA TAIFA YA UWEKEZAJI Uwasilishaji wa maombi ya hadhi ya uwekezaji wa kimkakati, nk. Mawasilisho ya masuala mengine. Utaratibu wa kutoa uamuzi. SEHEMU YA TANO CHETI CHA VIVUTIO, UKARABATI NA UPANUZI Ombi la cheti cha vivutio. Cheti kutumika kama uthibitisho. Mabadiliko ya jina, wanahisa au udhibiti. Mabadiliko yasiathiri manufaa. Utaratibu wa kuongeza muda wa uhai wa vivutio vya ziada. Kuongeza muda wa uhai wa cheti cha vivutio. Utaratibu wa kubatilisha cheti cha vivutio. SEHEMU YA SITA UHAMASISHAJI, UWEZESHAJI NA URATIBU WA MASUALA YA UWEKEZAJI Mpango wa kuhamasisha uwekezaji. Utekelezaji wa mpango. 2 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Ufuatiliaji na tathmini ya miradi. Taarifa ya mwaka ya mwekezaji. Maafisa ardhi na utoaji wa hati zisizo za asili kwa wawekezaji. Vibali vya kazi, makazi, n.k. Maafisa waliowekwa Kituoni. Upatikanaji wa dhamana na uhamisho wa faida. SEHEMU YA SABA MASHARTI MBALIMBALI Rufaa. Mapitio. Uratibu wa migogoro ya uwekezaji. Makosa na adhabu Kufutwa. Masharti ya kuhifadhi. ________ MAJEDWALI ________ 3 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Jina Tafsiri SHERIA YA UWEKEZAJI TANZANIA, (SURA YA 38) _______ KANUNI _______ (Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 5(4) na 35) KANUNI ZA UWEKEZAJI TANZANIA ZA MWAKA 2023 SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI 1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Uwekezaji Tanzania za Mwaka 2023. 2. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Bodi” maana yake ni Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 9 cha Sheria; “Kamati ya Taifa ya Uwekezaji” maana yake ni Kamati ya Taifa ya Uwekezaji iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 5(1) cha Sheria; “Kamati ya Wataalamu” maana yake ni Kamati ya Wataalamu iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 5(3) cha Sheria; “Kituo” maana yake ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania kilichoanzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria; “mtu” inajumuisha- mtu halisi, na warithi, wasimamizi wa miradhi au wawakilishi wa mtu huyo, na shirika lolote au taasisi nyingine ambayo imepewa au inajulikana kuwa na hadhi ya mtu kisheria katika nchi yoyote; serikali ya nchi yoyote, mamlaka ya umma hapa Tanzania au popote na shirika lolote la kimataifa bila kujalisha kama wajumbe wake wanaijumuisha Tanzania au lina hadhi ya kisheria; 4 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Sura ya 38 Majukumu ya Bodi Upotezaji sifa kwa wajumbe “mtu anayehusiana” maana yake ni mtu anayehusiana na mtu mwingine ambaye- ni mzazi, mwenza, kaka, dada au mtoto wa mtu huyo; mtu anayefanya kwa nafasi yake kama mdhamini katika udhamani, mnufaika mkuu wa udhamini, mwenza wake au mtoto wake yeyote au taasisi nafsi anayoisimamia; ni mbiya wa mtu huyo; moja kwa moja au vinginevyo, anasimamia au anasimamiwa na mtu huyo; “Sekretarieti” maana yake ni Sekretarieti ya Kamati ya Taifa ya Uwekezaji; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Uwekezaji Tanzania; na “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji. SEHEMU YA PILI MAJUKUMU YA BODI 3. Kwa kuzingatia masharti ya Sheria, Bodi- itafanya mapitio ya majukumu ya Kituo kwa ajili ya kuhakikisha kinafanikisha malengo yake; itafuatilia kila mara hali ya Taifa ya uwekezaji pamoja na mazingira ya uwekezaji kidunia na kupendekeza hatua za kuchukua ili kuweka mazingira ya uwekezaji Tanzania kuwa ya ushindani zaidi; itawasilisha kwa Waziri taarifa za robo mwaka kuhusiana na majukumu ya Kituo; na kuidhinisha kanuni za maadili kwa watumishi wa Kituo. 4. Mjumbe wa Bodi aliyeteuliwa kuendana na masharti ya Sheria atakoma kuwa mjumbe iwapo- ameshindwa kutelekeza majukumu yake kutokana na matatizo ya akili, magonjwa au majeraha; kwa notisi ya maandishi kwenda kwa mamlaka ya uteuzi, kuwa amedhamiria kujiuzulu nafasi yake, na kujiuzulu kutachukuliwa kuanza ambayo notisi tangu imepokelewa na mamlaka ya uteuzi; ametiwa hatiani kwa kosa udanganyifu; amefilisika au ameingia maafikiano maalum na wadai wake linalohusiana na tarehe jinai la 5 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania baada ya kushindwa kulipa madeni; baada ya kupewa notisi ya kikao, ameshindwa kuhudhuria vikao vitatu mtawalia vya Bodi bila ruhusa ya maandishi ya Mwenyekiti, au ikiwa ni Mwenyekiti, bila ruhusa ya maandishi ya Waziri; au mamlaka ya uteuzi imeona kuwa mjumbe huyo ameshindwa kutekeleza majukumu yake, au utenguzi wake ni muhimu kwa ajili ya utekelezaji bora wa majukumu ya Bodi. Kujaza nafasi zilizoachw a wazi 5. Endapo mjumbe wa Bodi amepoteza sifa kwa mujibu wa masharti yaliyoainishwa katika Kanuni hizi, mamlaka ya uteuzi itateua mtu mwingine kujaza nafasi iliyoachwa wazi kwa kipindi kilichosalia. Akidi 6. Akidi katika vikao vya Bodi itakuwa wajumbe wasiopungua watano. Maamuzi ya Bodi 7. Maamuzi ya Bodi yatafanyika kwa njia ya maafikiano, isipokuwa kama maafikiano yameshindikana, maamuzi yatafanyika kwa njia ya kura ambapo kila mjumbe atakuwa na kura moja, na ikiwa idadi ya kura imefungana, Mwenyekiti wa kikao atakuwa na haki ya kura ya turufu. Azimio kwa maandishi 8. Kwa kuzingatia masharti ya Sheria, azimio lililofikiwa kwa njia ya maandishi kwa kusainiwa na wajumbe wa Bodi wanaofikia akidi litakuwa ni halali kama vile lilipitishwa katika maamuzi ya kikao cha Bodi. Mapungufu katika uteuzi wa mjumbe 9. Maamuzi yoyote yaliyofanywa na Bodi au Kamati ya Bodi hatakuwa halali bila kujali kwamba wakati wa kufanya maamuzi kutabainika mapungufu yoyote katika uteuzi wa mjumbe au kwa sababu mjumbe yeyote hakuwa na sifa au hakustahili kushiriki katika kufanya maamuzi. Mgongano wa maslahi 10. Endapo mtu ambaye ni mjumbe wa Bodi, mjumbe wa kamati ya Bodi, Mkurugenzi Mtendaji, mwajiriwa wa Kituo, mshauri, au mtu yeyote anayehusika na Bodi ana maslahi ya kifedha au maslahi mengine katika suala lolote ikiwemo maslahi ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja kwa mtu, shughuli, mali, mkataba au uwekezaji 6 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Maslahi yenye manufaa uliofanyika au unaotarajiwa kufanyika au suala lolote ambalo linatakiwa kuamuliwa na Bodi au kamati ya Bodi, mtu huyo- ataeleza maslahi yake katika kikao cha Bodi kabla ya majadiliano ya suala hilo; ataomba maelezo yake yaandikwe katika muhtasari wa kikao hicho; hatashiriki katika majadiliano ya Bodi kuhusu suala husika; na hatafanya chochote kuhusiana na jambo husika. 11.-(1) Kwa madhumuni ya kanuni ya 10, mtu atachukuliwa kuwa na maslahi yenye manufaa ikiwa- yeye mwenyewe au mtu anayehusiana naye, au mwajiriwa wake au mteule wake ni mwanachama au mbia wa kampuni au taasisi yenye maslahi yoyote na suala lililotajwa katika kanuni ya 10; yeye mwenyewe au mtu anayehusiana naye yupo kwenye ubia au ameajiriwa na mtu mwenye maslahi na suala lolote linalotajwa katika kanuni ya 10; au yeye mwenyewe au mtu anayehusiana naye ni sehemu ya mipango au hayatekelezeki kuhusu suala lolote linalotajwa katika kanuni ya 10. au makubaliano, yanatekelezeka iwe (2) Endapo suala limejitokeza kuwa, mwenendo fulani kama utatekelezwa na mhusika, utasababisha ashindwe kutekeleza masharti ya kanuni ya 10, suala hilo litafanyiwa maamuzi na Bodi, na ufafanuzi wa maamuzi hayo utaandikwa katika muhtasari wa kikao husika. (3) Endapo mtu anayetajwa katika kanuni hii atashindwa kubainisha maslahi yake kuendana na masharti ya kanuni ya 10, mamlaka ya uteuzi itaamua hatua stahiki za kuchukua ikiwemo kuachishwa kazi au kumuondoa katika nafasi yake. Katibu wa Bodi 12.-(1) Katibu wa Bodi atakuwa na wajibu wa kutunza vizuri kumbukumbu za mwenendo na maamuzi yote ya Bodi. Bila kujali ujumla wa masharti ya kanuni ndogo ya (1), Katibu- atahifadhi nyaraka, kumbukumbu sahihi na maamuzi 7 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania yaliyotolewa na Bodi; atatunza taarifa zikionesha tarehe ya kuwasilishwa; atatoa notisi za maandishi za kuitisha vikao; ataandaa mada za vikao vya Bodi; atahifadhi orodha ya wajumbe wa Bodi; ataandaa muhtasari wa vikao; atahakikisha nyaraka kwa ajili ya vikao vya Bodi zinawafikia wajumbe kwa wakati; atahifadhi taarifa sahihi za kamati zilizoanzishwa na Bodi; na atawajulisha watu walioteuliwa kuwa wajumbe wa kamati za Bodi. SEHEMU YA TATU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA KAMATI YA TAIFA YA UWEKEZAJI NA KAMATI YA WATAALAMU 13. Katika kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika Sheria, Kamati ya Taifa ya Uwekezaji inaweza- kujenga uelewa wa pamoja ndani ya Serikali ili kurahisisha utekelezaji wa masuala yanayohusu uwekezaji; kutoa maelekezo ya kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyokwamisha masuala ya uwekezaji nchini; kupokea na kushughulikia malalamiko au vikwazo vya kisekta vinavyokwamisha utoaji huduma bora kwenye uwekezaji na kutoa ufumbuzi wa haraka kwa changamoto za kiutawala; na kupokea, kutoa miongozo na kuidhinisha miradi mikubwa yenye mchango mkubwa kwenye uchumi wa taifa kwa kuzingatia ukubwa wa mtaji, uzalishaji ajira na mchango wa teknolojia inayotumika katika mradi huo. 14. Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 5(3) cha itakuwa na wajumbe Sheria, Kamati ya Wataalamu wafuatao- Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana na masuala ya uwekezaji, ambaye atakuwa Mwenyekiti; Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha anayeshughulikia Sera, ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti; Kamishna anayehusika na masuala ya Sera kutoka Wizara 8 Utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Taifa ya Uwekezaji Kamati ya Wataalamu Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania yenye dhamana na fedha; Kamishna wa Ardhi; Mkurugenzi wa Mikataba kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Kamishna wa Idara ya Walipa kodi wakubwa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania; Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uwekezaji kutoka Wizara yenye dhamana na uwekezaji; Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda kutoka Wizara yenye dhamana na viwanda; na mtu yeyote kutoka sekta ambayo suala husika linajadiliwa ambaye anaweza kualikwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam kama mjumbe mwalikwa. Vikao vya Kamati ya Wataalamu 15.-(1) Kamati ya Wataalamu itakutana angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu. (2) Kamati ya Wataalamu itajiwekea utaratibu wa kuitisha na kuendesha vikao vyake. (3) Akidi katika kikao chochote cha Kamati ya Wataalamu itakuwa zaidi ya nusu ya idadi ya wajumbe wa Kamati ya Wataalamu. Majukumu ya Kamati ya Wataalamu 16.-(1) Kamati ya Wataalamu itakuwa na majukumu yafuatayo: kupokea na kuchakata masuala mbalimbali kutoka Sekretarieti yanayolenga kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuishauri Kamati ya Taifa ya Uwekezaji; kupokea na kuchakata maombi ya vivutio vya ziada vya kikodi na visivyo vya kikodi kutoka kwa Sekretarieti na kuishauri Kamati ya Taifa ya Uwekezaji; na kutekeleza jukumu lingine lolote kadri ambavyo Kamati ya Taifa ya Uwekezaji itakavyoelekeza. (2) Wakati wa kuchakata maombi ya wawekezaji katika kanuni ndogo ya (1)(b), Kamati ya Wataalamu inaweza kumwita na kumsikiliza mwombaji na itazingatia masharti ya kifungu cha 19(2) na (3) cha Sheria wakati wa kutoa mapendekezo. UTARATIBU WA UWASILISHAJI WA MASUALA SEHEMU YA NNE 9 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Uwasilishaj i wa maombi ya hadhi ya uwekezaji wa kimkakati, nk. MBALIMBALI KATIKA KAMATI YA TAIFA YA UWEKEZAJI 17.-(1) Maombi ya hadhi ya uwekezaji wa kimkakati na uwekezaji maalum wa kimkakati kwa ajili ya kupatiwa vivutio vya ziada yatawasilishwa kwa Katibu wa Kamati ya Taifa ya Uwekezaji kwa kutumia Fomu Na.1 iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi pamoja na malipo ya ada iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Kanuni hizi. (2) Maombi chini ya kanuni ndogo ya (1) yataambatishwa na nyaraka zifuatazo: nakala ya cheti cha vivutio; upembuzi wa mradi ukionyesha uhalisia wa gharama, faida kwa taifa na kwa mwekezaji, vivutio vya ziada anavyoomba katika Kamati ya Taifa ya Uwekezaji ili kumwezesha kutekeleza mradi kikamilifu; na maelezo mafupi yanayoonesha masuala ya msingi yaliyoainishwa ndani ya maombi ya mwekezaji kama yalivyotajwa katika aya (b). (1) (3) Maombi chini ya kanuni ndogo ya hayatakubaliwa ikiwa hayajakidhi vigezo vilivyoainishwa katika Sheria. (4) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (3), maombi ya uwekezaji wa kimkakati katika maeneo yenye changamoto yataonesha changamoto zinazokabili mradi na mapendekezo ya hatua za utatuzi. (5) Kwa madhumuni ya Kanuni hizi, changamoto katika maeneo ya pembezoni mwa nchi inajumuisha ukosefu na uhaba wa miundombinu na upungufu wa rasilimali watu wenye ujuzi. Mawasilisho mengine_ 18. Mawasilisho mengine yanayohusiana na uwekezaji, tofauti na migogoro inayohusiana na uwekezaji, yanayohitaji idhini au maamuzi ya Kamati ya Taifa ya Uwekezaji, yatafanywa kwa kutumia Fomu Na. 2 iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi._ Utaratibu wa kutoa uamuzi 19.-(1) Baada ya kupokea maombi kwa mujibu wa kanuni za 17 na 18, Katibu wa Kamati ya Taifa ya Uwekezaji atayawasilisha kwenye Kamati ya Wataalamu 10 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Ombi la cheti cha vivutio itapaswa kuchakata maombi hayo na kutoa ambayo mapendekezo kwa Kamati ya Taifa ya Uwekezaji ndani ya siku kumi na nne baada ya kikao cha mwisho cha uchakataji wa maombi husika. (2) Baada ya kupokea mapendekezo ya Kamati ya Wataalam, Kamati ya Taifa ya Uwekezaji itafanya maamuzi ya kukubali au kukataa mapendekezo ya Kamati ya Wataalam na ikiwa itayakubali itaielekeza Sekretarieti kutoa taarifa ya uamuzi huo kwa Idara za Serikali au mtu anayehusika. CHETI CHA VIVUTIO, UKARABATI NA UPANUZI SEHEMU YA TANO 20.-(1) Taasisi ya kibiashara inaweza, baada ya kulipa ada iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Kanuni hizi na kukidhi matakwa ya Sheria, kuwasilisha ombi la kupatiwa cheti cha vivutio kwenye Kituo kwa kutumia Fomu Na. 3 iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi. (2) Baada ya kupokea ombi chini ya kanuni ndogo ya (1), Mkurugenzi Mtendaji atachakata ombi husika na anaweza- kukubali ombi na kuthibitisha taasisi ya kibiashara; au kukataa ombi hilo. (3) Endapo Kituo kimekubali ombi na kuithibitisha taasisi ya kibiashara chini ya kanuni ndogo ya (2), kitatoa cheti cha vivutio kwa hiyo taasisi iliyothibitishwa. (4) Endapo Kituo kinakataa ombi chini ya kanuni ndogo ya (2) kitamtaarifu mwombaji na kutoa sababu za kukataa. Cheti kutumika kama uthibitisho 21. Cheti cha vivutio kilichotolewa na Kituo kwa taasisi ya kibishara kitakuwa ni uthibitisho tosha kwamba masharti ya Sheria na Kanuni hizi yamezingatiwa. Mabadiliko ya jina, wanahisa au udhibiti Sura za 212 22. Ikiwa taasisi ya kibiashara iliyothibitishwa imebadilisha jina au umiliki au udhibiti wa mtaji unaotokana na wanahisa, Kituo baada ya kupokea uthibitisho wa mabadiliko yaliyofanyika kwa mujibu wa 11 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania na 213 Sheria ya Makampuni, Sheria ya Usajili wa Majina ya Biashara, au sheria yoyote inayohusika kitatoa cheti cha vivutio kilichobadilishwa kukidhi mabadiliko hayo. Mabadiliko yasiathiri manufaa 23. Kwa kuzingatia sharti linalohusu kiwango cha chini cha mtaji katika Sheria, mabadiliko yoyote yaliyorejewa katika kanuni ya 22 hayataathiri haki yoyote au wajibu wa biashara. Utaratibu wa kuongeza muda wa uhai wa vivutio vya ziada 24.-(1) Mwekezaji wa kimkamkati au mwekezaji maalum wa kimkakati aliyepewa vivutio vya ziada anaweza kuomba kuongezewa muda wa kutumia vivutio hivyo kwa kuwasilisha barua kwa Katibu wa Kamati ya Taifa ya Uwekezaji akiainisha sababu za msingi za maombi hayo kabla ya kuisha kwa muda wa awali. (2) Katibu wa Kamati ya Taifa ya Uwekezaji atawasilisha maombi yaliyoletwa chini ya kanuni ndogo ya (1) kwa Kamati ya Taifa ya Uwekezaji ambayo itatoa uamuzi na Katibu wa Kamati ya Taifa ya Uwekezaji atamjulisha mwombaji kwa maandishi. (3) Katika kufanya uamuzi chini ya kanuni ndogo ya (2), Kamati ya Taifa ya Uwekezaji pamoja na mambo mengine itazingatia kama kulikuwa na ucheleweshaji katika kupata ardhi ya mradi, mitaji pamoja na vibali na leseni mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji. Kuongeza muda wa uhai wa cheti cha vivutio 25.-(1) Taasisi ya kibiashara iliyopewa cheti cha vivutio, inaweza kuomba kuongezewa muda wa uhai wa cheti cha vivutio kwa kuwasilisha barua kwenye Kituo ikiainisha sababu za msingi za kuongezewa muda, kabla ya kuisha kwa muda wa awali. (2) Kituo wakati wa kuongeza muda wa uhai wa cheti cha vivutio kwa mujibu wa kanuni hii pamoja na mambo mengine na ucheleweshaji katika kupata ardhi ya mradi, mitaji pamoja na vibali au leseni mbalimbali. kitazigatia kulikuwa kama (3) Kituo kitachakata maombi yaliyowasilishwa chini ya kanuni ndogo ya (1) ndani ya siku saba za kazi tangu tarehe ya kupokea maombi husika na kumjulisha mwombaji kwa maandishi kuhusu uamuzi huo. 12 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Utaratibu wa kubatilisha cheti cha vivutio Mpango wa kuhamasisha uwekezaji 26.-(1) Kituo kinaweza kubatilisha cheti cha vivutio baada ya kujiridhisha kwamba mwekezaji amekiuka masharti ya Sheria kwa kuzingatia sababu zilizoainishwa chini ya kifungu cha 20(3) cha Sheria. (2) Kituo kitapaswa, baada ya kubaini uwepo wa sababu za kubatilishwa kwa cheti cha vivutio kwa mujibu kwa kanuni ndogo ya (1), kabla ya kufuta cheti hicho, kumpa mmiliki wa cheti notisi ya kumtaka arekebishe tatizo lililobainika katika muda utakaoainishwa katika notisi. tatizo (3) Endapo mmiliki wa cheti cha vivutio hatarekebisha lililobainishwa ndani ya muda ulioainishwa katika notisi kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (2), Kituo kitampa notisi ya siku saba ya kusudio la kufuta cheti hicho na kumtaka awasilishe utetezi akiainisha sababu za kutobatilishwa cheti husika baada ya muda wa notisi kuisha. (4) Endapo mmiliki wa cheti hajawasilisha utetezi au amewasilisha utetezi ambao haujakubaliwa na Kituo ndani ya muda tajwa, Kituo kitabatilisha cheti hicho na kumtaarifu mmiliki wa cheti hicho kuhusu uamuzi huo. SEHEMU YA SITA UHAMASISHAJI, UWEZESHAJI NA URATIBU WA MASUALA YA UWEKEZAJI 27.-(1) Kituo kitatekeleza majukumu ya kuhamasisha uwekezaji kwa mujibu wa Sheria. (2) Katika kutekeleza majukumu chini ya kanuni ndogo ya (1), Kituo kitaandaa mpango wa kuhamasisha uwekezaji na kuuwasilisha Bodi kwa ajili ya kupata idhini. (3) Baada ya kuidhinishwa, Bodi itachukua hatua zote zinazohitajika ili kuhakikisha kuwa mpango wa kuhamasisha uwekezaji unatekelezwa. Utekelezaji wa mpango 28.-(1) Kwa madhumuni ya kutekeleza mpango wa kuhamasisha uwekezaji, Kituo- kitatangaza nchi kama kivutio cha uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje kwa kusambaza taarifa, 13 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Ufuatiliaji na tathmini ya miradi Taarifa mwaka mwekezaji ya ya kuandaa shughuli zinazojumuisha umma na kutangaza fursa za uwekezaji ili kujenga na kuboresha taswira ya Tanzania kama nchi nzuri ya uwekezaji; kitaweka katika mapitio hatua iliyofikiwa katika malengo na madhumuni ya Sheria na kuchapisha ripoti na kutoa taarifa kwa madhumuni ya kuongeza uelewa wa mwekezaji na umma kuhusu maendeleo hayo na changamoto na masuluhisho yaliyopo kuhusiana na mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania; na kuendeleza maarifa ya kitaaluma, ujuzi na uwezo mwingine wa kitaalamu wa kuishauri Serikali kuhusu uhamasishaji wa masuala ya uwekezaji na masuala mengine yanayohusiana na uwekezaji. 29.-(1) Kituo kitakuwa na wajibu wa kufanya ufuatiliaji na tathmini ya miradi iliyosajiliwa. (2) Katika kutekeleza jukumu lililoanishwa katika kanuni ndogo ya (1), Kituo kitaandaa mpangokazi wa utekelezaji na kutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu. (3) Wakati wa kufanya ufuatiliaji na tathmini, Kituo kitazingatia masharti yaliyoainishwa katika kifungu cha 19(2) na (3) cha Sheria. (4) Kituo kitaitaarifu Kamati ya Taifa ya Uwekezaji kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati na miradi maalum ya kimkakati. 30.-(1) Kila taasisi ya kibiashara yenye cheti cha kivutio kilichotolewa chini ya Sheria itakuwa na wajibu wa kuwasilisha katika Kituo taarifa za kila mwaka za maendeleo ya utekelezaji wa mradi. (2) Taasisi ya kibiashara mpya iliyothibitishwa itawasilisha taarifa ya mwaka baada ya miezi kumi na mbili toka tarehe ya kutolewa kwa cheti cha vivutio. (3) Taasisi ya kibiashara inayoendelea itawasilisha taarifa ya mwaka kila baada ya miezi kumi na mbili toka tarehe ya mwisho ya kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi kwa mwaka uliopita. (4) Taarifa iliyoainishwa katika kanuni hii, itaandaliwa kama ilivyoainishwa katika Fomu Na. 4 ya Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi. 14 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Maafisa ardhi na utoaji wa hati zisizo za asili kwa wawekezaji Sura ya 113 31.-(1) Kwa mujibu wa masharti ya vifungu vya 6(e) na 18(2) vya Sheria, maafisa ardhi waliopo katika Kituo watakuwa na jukumu la kuharakisha masuala ya uwezeshaji yanayohusiana na ardhi kwa madhumuni ya masuala ya uwekezaji chini ya Sheria. (2) Maafisa ardhi waliopo katika Kituo watapokea na kushughulikia maombi ya hati zisizo asili kwa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na watamshauri Mkurugenzi Mtendaji kutoa hati hizo kwa wawekezaji kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi. (3) Mkurugenzi Mtendaji ndani ya siku saba za kazi baada ya kupokea ushauri wa maafisa ardhi na baada ya kuridhika kwamba ushauri huo unazingatia sheria, atampa mwekezaji hati isiyo asili ya ardhi iliyoidhinishwa. Vibali vya kazi, makazi, n.k. 32. Kwa mujibu wa masharti ya vifungu vya 6(1)(f) na 18(1) vya Sheria, Kituo kitawasaidia wawekezaji kupata vibali vya makazi, kazi, vyeti vya usajili wa biashara na leseni pamoja na vibali vingine vinavyohitajika ndani ya siku saba za kazi baada ya kupokea maombi hayo. Maafisa waliowekwa kwenye Kituo Upatikanaji wa dhamana na uhamisho wa faida Sura za 123 na 392 33. Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 18(2) cha Sheria, maafisa wa idara mbalimbali za Serikali waliopo katika Kituo wataratibu na kusaidia uchakataji wa vibali na leseni mbalimbali kwa misingi ya maombi yaliyowasilishwa kupitia Kituo na kutoa vibali ndani ya siku saba za kazi baada ya kupokea maombi hayo. 34. Kituo kitatoa moja kwa moja cheti cha vivutio kwa mwekezaji yeyote mwenye haki ya madini inayotolewa chini ya Sheria ya Madini au leseni iliyotolewa chini ya Sheria ya Petroli ili kuwawezesha kunufaika na dhamana ya uhamisho wa mtaji, faida na gawio iliyotolewa chini ya kifungu cha 28 cha Sheria; na dhamana dhidi ya utwaaji kama ilivyoainishwa chini ya kifungu cha 29 cha Sheria, vikisomwa pamoja na kifungu cha 2(3) cha Sheria. SEHEMU YA SABA MASHARTI MBALIMBALI 15 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Rufaa_ 35.-(1) Mtu ambaye hajaridhika na uamuzi uliotolewa na Kituo kuhusu-_ kukataliwa kupewa cheti cha vivutio; kukataliwa kupewa vivutio kwa ajili ya ukarabati au upanuzi wa mradi; kukataliwa kuongezewa muda wa uhai wa cheti cha vivutio; au kufutiwa cheti cha vivutio, anaweza kukata rufaa kwa Waziri kwa kuandika barua ndani ya siku ishirini na moja kuanzia tarehe alipopokea uaamuzi huo. _ (2) Baada ya kupokea rufaa, Waziri anaweza kuthibitisha, kufuta au kurekebisha au kutoa maelekezo mahsusi kuhusu uamuzi uliotolewa na (3) Uamuzi wa Waziri utakaotolewa chini ya kanuni ndogo Kituo. __ ya (2) utakuwa wa mwisho.___Mapitio_ 36.-(1) Mwekezaji ambaye hajaridhika na uamuzi wa Kamati ya Taifa ya Uwekezaji kuhusu uidhinishaji wa vivutio au suala lingine lililowasilishwa chini ya kanuni ya 18 anaweza kuwasilisha maombi ya mapitio kwa kuandika barua kwa Kamati ya Taifa ya Uwekezaji akianisha sababu za mapitio hayo ndani ya siku ishirini na moja tangu tarehe ya kupokea uamuzi.__ (2) Maombi ya mapitio kwenda Kamati ya Taifa ya Uwekezaji yatawasilishwa kwa kupokea Katibu wa Kamati ya Taifa ya Uwekezaji.__ (3) Baada maombi hayo, Kamati itapitia na kutoa uamuzi, na uamuzi huo utakuwa wa mwisho. ___Uratibu wa migogoro ya uwekezaji_ 37.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 33 cha Sheria, Kituo kitapokea na kushughulikia, ndani ya siku thelathini tangu tarehe ya kupokea, migogoro inayohusiana na uwekezaji wa miradi iliyosajiliwa na Kituo inayowasilishwa kwake. __ (2) Mwekezaji anayekabiliwa na mgogoro wowote atatakiwa kuwasilisha taarifa ya mgogoro husika kwa maandishi ndani ya siku ishirini na moja kuanzia tarehe ya kutokea kwa mgogoro huo pamoja na mapendekezo ya nafuu inayoombwa.__ kupokea mawasilisho chini ya kanuni ndogo ya (2), Kituo kitajitahidi kuitisha mkutano na wahusika kwa madhumuni ya kusuluhisha mgogoro husika kwa njia ya maridhiano na kwa wakati.___ (3) Baada ya ya Makosa na adhabu Kufutwa TS. Na. 38. Mtu yeyote anayekiuka masharti ya Kanuni hizi anatenda kosa na endapo atatiwa hatiani atawajibika kwa adhabu kama ilivyoainishwa katika Sheria. 16 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania 381A 2002 la Masharti ya kuhifadhi 39. Kanuni za Uwekezaji Tanzania za mwaka 2002 zinafutwa. 40. Bila kujali kufutwa kwa Kanuni za Uwekezaji Tanzania za mwaka 2002, masuala yote yaliyofanyika chini ya Kanuni zinazofutwa yataendelea kuwa halali kama vile yametolewa chini ya Kanuni hizi hadi yatakapobatilishwa kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hizi._ FOMU NA. 1 ______________ JEDWALI LA KWANZA _____________ FOMU (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 17(1)) MAOMBI YA HADHI YA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI/ UWEKEZAJI MAALUM WA KIMKAKATI NA VIVUTIO VYA ZIADA Kwa: Mkurugenzi Mtendaji na Katibu kwa Kamati Ya Taifa Ya Uwekezaji, Kituo cha Uwekezaji Tanzania, S. L.P 938, DAR ES SALAAM. Jina la mkurugenzi /mwakilishi wa …………………………………………. Jina la taasisi ya biashara inayoomba hadhi ya uwekezaji wa Kimkakati/Kimkakati Maalum …………………………...………………………………………………………... Viambatisho; Cheti cha Vivutio cha TIC; Nakala ya muhtasari wa mradi ukionesha mradi unavyokidhi vigezo chini ya kifungu 23 cha Sheria ya Uwekezaji Na. 10 ya 2022; na Ratiba ya utekelezaji na tarehe ya uendeshaji. Mtaji uliopangwa kuwekezwa kwenye mradi kwa mujibu wa kifungu cha 23(2) cha Sheria ni Tshs./US$ ……………………………………………….. 17 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Uthibitisho Mimi, ……………………………………….. wa S. L. P. …………………… kwa uaminifu ninathibitisha kwamba ni Mkurugenzi/mwakilishi aliyeidhinishwa wa ………………………………, NA kwamba matakwa ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya mwaka 2022 kuhusiana na usajili wa taasisi ya kibiashara chini ya Sheria na masuala yote yanayohusiana yamezingatiwa, NA ninatoa uthibitisho huu nikiamini kwa utashi wangu kuwa uthibitisho huu ni kweli. Imesainiwa Dar es Salaam } …………………………. Mwombaji Siku ya …… Mwezi…… Mwaka……...} Mbele yangu: ………………………. Kamishna wa Viapo MUHTASARI WA MAOMBI YA HADHI YA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI/KIMKAKATI MAALUM Jina la Kampuni: ………………………………………………………………… Namba ya Cheti cha Vivutio: ………………….…………………………………. Muda wa Cheti cha Vivutio Kutumika: ………………………………………….. S. L. P: ……………………... Halmashauri: ……………….. Mkoa ……………………….. Sekta: ……………………….. Sekta Ndogo: ………………………… Mpango wa kuwekeza fedha katika milioni za US$/Tshs. 18 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Mtaji Mbia wa Nje Mtaji Mbia wa Ndani Mkopo wa Nje Mkopo wa Ndani Malengo ya Mradi: …………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………... Uwezo wa Mradi wa Kuzalisha: ………….…………………………………… Ajira za moja kwa moja: wageni: ..…… watanzania: .…… Jumla: ………… Ajira zisizo za moja kwa moja ……………………………..., Jumla …………. Kiasi cha fedha za kigeni kinachoweza kupatikana kutokana na mradi ………………………………………………………………………………… Kuchangia technolojia mpya (aina na usajili) …………………………………………..……………………………………….... Makadirio ya mchango wa kodi na mapato ambayo zi kodi kwa mwaka …………………………………………………………………………………….. Michango mingine ya mradi kwa uchumi na mipango ya maendeleo ya nchi ………………………….………………………………………………………….. ……………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………… Muda wa utekelezaji: Kuanzia……………… mpaka……………………, kama utekelezaji ni wa awamu onesha hapa………………………………………………. ………………………………………………………………………………………. Mradi Ulipo 19 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Eneo/Kitalu Na. ……, Mtaa: …………… Halmashauri: ……………, Mkoa ……... (Weka ramani kuonesha mradi ulipo) Taarifa za wanahisa Jina Uraia % ………………………….. …………………. …….. ………………………….. …………………. …….. ………………………….. …………………. …….. ………………………….. …………………. …….. Taarifa za Mawasiliano: Jina: …………………………………… Cheo: ……………………………… Simu: ………………………………………. Barua Pepe: …………………………………… Vivutio vya nyongeza vinavyoombwa S/N_Aina ya kivutio_Jina la Kifungu_Kipimo_Idadi_Thamani ya Vivutio (US$)_Uhalali__1.________2.________3.________ 20 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 18) FOMU NA. 2 FOMU YA MAPENDEKEZO KWA KAMATI YA TAIFA YA UWEZESHAJI UWEKEZAJI KUHUSU MABORESHO YA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA Kwa: Mkurugenzi Mtendaji na Katibu kwa Kamati Ya Taifa Ya Uwekezaji, Kituo cha Uwekezaji Tanzania, S. L.P 938, DAR ES SALAAM. Jina la Taasisi ya Kibiashara:……….……………………………………………… Nakala za viambatisho vifuatavyo zimeambatishwa pamoja na maombi haya: Mapendekezo ya maeneo ya maboresho kwa ajili ya kujadiliwa na kuamuliwa na KAMATI YA TAIFA YA UWEKEZAJI. Jina…………………………………………….. Cheo …………………… Saini………………………………….. Tarehe………mwezi……….mwaka……...... Muhtasari wa Mapendekezo kwa KAMATI YA TAIFA YA UWEKEZAJI kwa masuala ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Na Maelezo ya suala Taasisi/Sekta ya Umma inayohusika Madhara kwa biashara, uwekezaji na uchumi wa nchi Hatua za awali zilizochukuliw a na matokeo Mapendekezo ya hatua kwa KAMATI YA TAIFA YA UWEKEZAJI 1. 2. 21 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania FOMU NA. 3 (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 20(1)) FOMU YA MAOMBI YA CHETI CHA VIVUTIO Kwa: Mkurugenzi Mtendaji, Kituo cha Uwekezaji Tanzania, S.L.P 938, DAR ES SALAAM Jina na hadhi ya Mwombaji …………………………………………………………… Jina la taasisi ya kibiashara ya mwombaji …………………………..………. Anwani na eneo ilipo taasisi ya kibiashara ya mwombaji: …..…………………………………… Viambatisho kwenye maombi: Katiba ya Taasisi ya Kibiashara/Hati ya Makubaliano ya Ubia; Cheti cha usajili; Andiko la Mradi; Ushahidi wa fedha za kugharamia mradi; Ushahidi wa upatikanaji wa ardhi kwa ajii ya mradi; Muhtasari wa kikao cha bodi kwa usajili wa TIC na utekelezaji wa Mradi; Ushahidi wa malipo ya ada ya usajili; na Ramani kuonesha eneo la mradi. Majina na mawasiliano ya Watendaji Wakuu wa Taasisi: …....…………………………………………... ………………………………………………… ………………………………………………… Mtaji ulioidhinishwa kwa mradi …………………………………… Mtaji utakaowekezwa kulingana na kifungu cha 2(2) au 23(2) cha Sheria ni Tshs./US$ ……………………………….. Uthibitisho Mimi, ……………………………………….. wa S. L. P. …………………… kwa uaminifu ninathibitisha kwamba ni Mkurugenzi/mwakilishi aliyeidhinishwa wa ………………………………, NA kwamba matakwa ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya mwaka 2022 kuhusiana na usajili wa taasisi ya kibiashara chini ya Sheria na masuala yote yanayohusiana 22 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania yamezingatiwa, NA ninatoa uthibitisho huu nikiamini kwa utashi wangu kuwa uthibitisho huu ni kweli. Imesainiwa Dar es Salaam Siku ya……Mwezi ……./20…..} Mbele ya: }………………………… Mwombaji ……………………………… Wakili MUHTASARI WA MAOMBI Jina la Taasisi ya Kibiashara: ………………………………………………… Namba ya CoI: …………., Tarehe ya CoI: ……………., Hali/Hadhi: …………… Sekta: …………………….……., Sekta ndogo: ………………………………… Mpango wa Kugharamia Uwekezaji ( U S$/TShs) Mtaji wa Mbia Nje Mtaji wa Mbia Ndani Mkopo wa Nje Mkopo wa Ndani …………… …….……………. ……….………. …….………… Shughuli za Mradi:…………………………………………………………………. ……………………………………………………………………………………….. Uwezo wa kuzalisha: …………… …………………………………………… Ajira: Wageni: ……….. Wazawa: ………. Jumla:……………. Kipindi cha Utekelezaji:………………………………………………… Eneo Mradi: Eneo/kiwanja/kitalu Na.: ……, Kijiji/Mtaa: ………………, Halmashauri: ………… Mkoa: ………................... 23 % …….. …….. …….. …….. …….. Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Jina la Mbia Uraia ………………………….. …………………. ………………………….. …………………. ………………………….. …………………. ………………………….. …………………. ………………………….. …………………. Mgawanyo wa Uwekezaji US$/TShs. Ardhi/Majengo Mitambo Magari Samani Gharama za Awali Nyinginezo ………………….. …………………. ………………… ………………… ………………… ………………… Mtaji wa Kufanyia Kazi ………………… Jumla ………………… 24 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 30(4)) FOMU NA. 4 FOMU YA TAARIFA YA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI Ni takwa la kisheria kwa wawekezaji wenye miradi iliyosajiliwa na Kituo kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi kila baada ya miezi sita. Tafadhali andaa na kuwasilisha taarifa Maelezo (a)………………… (b)……………… (c)……………… (c)……………… (d)…………….. hiyo kulingana na jedwali lifuatalo: Na. Kipengele 1. Taarifa za wabia 2. Anwani na mawasiliano ya Taasisi ya Kibiashara 3. Mtu wa kuwasiliana naye 4. 5. 6. Usajili Namba ya mlipa kodi Taarifa za Mradi 7. Ajira za moja kwa moja 8. Ajira zisizo za moja kwa moja Kipengele Kidogo Majina, uraia na asilimia ya umiliki wa mradi (eneo, Halmashauri, Kumb: Kama wapo zaidi ya watano ambatanisha karatasi yenye taarifa zao Barua pepe Simu ya mkononi Mahali ilipo: kijiji/mtaa, mkoa) Jina Wadhifa Simu na barua pepe Namba ya Cheti cha Usajili (BRELA) Namba ya mlipa kodi (TIN) Shughuli za Mradi Uwezo wa jumla wa Mradi Uwezo wa mradi unaotumika Wanaume wageni Wanawake wageni Wanaume Watanzania Wanawake Watanzania Jumla ya ajira Maeneo waliyoajiriwa 1. Matumizi ya Fedha za Mradi (USD/TShs): Fedha za Nje Fedha za Ndani Jumla (USD/TShs) (USD/TShs) (USD/TShs) Ardhi na majengo Mitambo na Mashine 25 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania Magari/Ndege/Boti/nk. Thamani Vifaa vya Ofisi Bima Gharama za awali Gharama za uendeshaji JUMLA KUU 2. Ugharamiaji wa Mradi Elezea vyanzo vya Fedha vya Mradi CHANZO KIASI (USD/TSHS.) NCHI Wenye Mradi wa ndani Mikopo ya Tanzania Wenye Mradi wa Nje Mikopo ya Nje JUMLA Tanzania Tanzania 3. Changamoto na Hatua Zilizochukuliwa Elezea changamoto ulizokutakana nazo wakati wa kutekeleza mradi na hatua za kutatua changamoto hizo zilizochukuliwa. 4. Mipango ya Baadaye Elezea mipango ya mradi kwa wakati unaofuata. 5. Ushauri na maoni mengineyo 26 Tangazo la Serikali na. 501 (Linaendelea.) Kanuni Za Uwekezaji Tanzania ____________ JEDWALI LA PILI ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 17(1) na 20(1)) __________ ADA HUDUMA 1. 2. 3. 4. Maombi ya Cheti Maombi ya Uwekezaji wa Kimkakati Maombi ya Upanuzi na Ukarabati wa mradi Huduma ya Kituo cha pamoja ADA KWA DOLA YA MAREKENI AU KIWANGO KINACHOFANANA NA SHILINGI ZA KITANZANIA 1,200 3,000 1,200 10% ya ada zinazotozwa na mamlaka husika katika utoaji wa vibali na leseni vinavyotolewa katika Kituo cha Huduma ya Pamoja Dodoma, 4 Julai, 2023 ASHATU K. KIJAJI, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara 27
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Uwekezaji Tanzania za Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in