Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokoaji wa Maisha, Vifaa Vya Uokoaji
This provision gives the regulations their title: the 2023 Rescue Boat, Rescue Equipment, and Rescue Launching Equipment maintenance, inspection, operational testing, modification, and repair rules.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokoaji wa Maisha, Vifaa Vya Uokoaji
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the regulations their title: the 2023 Rescue Boat, Rescue Equipment, and Rescue Launching Equipment maintenance, inspection, operational testing, modification, and repair rules. The rules apply to Tanzanian and non-Tanzanian ships in Tanzanian waters, especially for maintenance, detailed inspection, operational testing, modification, and repair of life-saving boats and related rescue equipment. This section defines key terms used in the regulations. Shirika must ensure certain equipment inspection, testing, and repair work is done by approved service providers, and manufacturers acting as approved service providers are also subject to regulation 13. The provision requires certain inspections, tests, maintenance, adjustments, and repairs to be carried out by authorized people or providers, and allows an authorized service provider to be the ship operator under stated conditions.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokoaji wa Maisha, Vifaa Vya Uokoaji
Showing 21 of 21
- 1
AI-assisted research summary: This provision gives the regulations their title: the 2023 Rescue Boat, Rescue Equipment, and Rescue Launching Equipment maintenance, inspection, operational testing, modification, and repair rules.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokoaji wa Maisha, Vifaa Vya Uokoaji na Vifaa vya Kushushia Vifaa vya Uokoaji za Mwaka 2023. - 2
AI-assisted research summary: The rules apply to Tanzanian and non-Tanzanian ships in Tanzanian waters, especially for maintenance, detailed inspection, operational testing, modification, and repair of life-saving boats and related rescue equipment.
2.-(1) Kanuni hizi zitatumika kwa meli za Tanzania na meli zisizo za Tanzania zikiwa katika maji ya Tanzania hususan katika matengenezo, uchunguzi wa kina, majaribio ya uendeshaji, marekebisho na ukarabati wa- (a) boti za uokozi wa maisha zikiwemo, boti za uokozi na boti za uokoaji wa haraka; na (b) vifaa vya kutumbukiza chombo cha uokoaji na zana zinazopakia na zinazotoa nje vifaa vya boti za kuokoa maisha ikijumuisha njia za msingi na za kawaida za kutumbukiza boti za uokoaji wa maisha, boti za uokozi, boti za uokozi wa haraka na kifaa cha kushushia vifaa vya uokoaji. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), Kanuni hizi hazitatumika kwa- (a) meli ya kivita au msaada wa kijeshi; (b) meli za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania; (c) ndege za baharini za Jeshi la Ulinzi la Wananchi 3 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) wa Tanzania; na (d) meli zinazomilikiwa au kutumiwa na Serikali na kujihusisha na shughuli za kiserikali zisizo za kibiashara. Tafsiri - 3
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the regulations.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Kanuni za vifaa vya uokozi wa maisha” maana yake ni Kanuni iliyopitishwa na Kamati ya Usalama wa Baharini katika kikao cha 66 (Juni 1996) kwa azimio la Kamati ya Usalama wa Baharini Na. 48(66) au kwa kifupi chake kinachojulikana kama Kanuni ya Kimataifa ya vifaa vya uokozi wa maisha; “mfumo wa ushushaji usiokuwa na mzigo” maana yake ni mfumo wa njia ya kutoa chombo cha uokozi au boti ya uokozi au boti ya haraka ya uokozi pale inapohitajika kushushwa majini au wakati ambao hakuna mzigo kwenye ndoano; “mfumo wa ushushaji wenye mzigo” maana yake ni mfumo wa njia ya kutoa chombo cha uokozi au boti ya uokozi au boti ya haraka ya uokozi pale inapohitajika kushushwa majini au wakati ambao kuna mzigo kwenye ndoano; “Mfumo wa Usimamizi wa Usalama” maana yake ni mfumo ulioandaliwa na kuwekwa katika nyaraka kwa lengo la kuwawezesha watumishi wa kampuni kutekeleza kwa ufanisi Sera ya Usalama na Ulinzi wa Mazingira wa Kampuni; “mkaguzi” maana yake ni mtu aliyeteuliwa kama mkaguzi chini ya kifungu cha 382 cha Sheria; “Mkataba wa Usalama” maana yake ni Mkataba wa Kimataifa wa Usalama wa Maisha Baharini wa mwaka 1974 na Itifaki zake za mwaka 1978 na 1988, pamoja na marekebisho yake, au mbadala wake kama utakavyotumika Tanzania; “mtengenezaji” maana yake ni mtengenezaji wa vifaa halisi au Kampuni yoyote ambayo imechukua majukumu halali na ya kisheria pale ambapo mtengenezaji wa vifaa halisi hayupo au hatengenezi tena vifaa; “mtoa huduma aliyeidhinishwa” maana yake ni Kampuni 4 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) iliyoidhinishwa na Shirika kufanya matengenezo, uchunguzi wa kina, upimaji wa uendeshaji, marekebisho na ukarabati wa boti za uokozi wa maisha na boti za uokozi, vifaa vya kutumbukiza chombo cha uokozi, na utoaji wa zana; “Notisi ya Usafiri Majini” maana yake ni Notisi iliyoainishwa kama Notisi ya Usafiri Majini na kutolewa na Msajili na inajumuisha rejea ya nyaraka yoyote inayorekebisha au kubadili notisi hiyo; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Usafiri Majini; “Shirika” maana yake ni Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania lililoanzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania; Sura ya 165 Sura ya 415 “ukarabati” maana yake ni shughuli zozote zinazohitaji kutenganishwa kwa kifaa, au shughuli nyingine zozote nje ya maelekezo ya eneo la matengenezo ya ndani ya meli na matengenezo ya dharura ya vifaa vya uokozi vilivyoandaliwa kulingana na Kanuni za III/36.2, na III/35.3.18 za Mkataba wa Usalama; “urekebishaji” maana yake ni shughuli ya mara kwa mara inayofanywa na mtengenezaji kwa madhumuni ya kuthibitisha kipindi kilichoanishwa kulingana na matengenezo sahihi; na endelevu ubora kwa “vifaa” maana yake ni boti za kuokoa maisha na boti za uokoaji, vifaa vya kutumbukiza chombo cha uokozi na zana za uokozi. SEHEMU YA PILI UIDHINISHWAJI, VIWANGO VYA UJUZI, UTOAJI WA CHETI, RIPOTI NA KUMBUKUMBU Uidhinishaji
Part
SEHEMU YA PILI
- 4
AI-assisted research summary: Shirika must ensure certain equipment inspection, testing, and repair work is done by approved service providers, and manufacturers acting as approved service providers are also subject to regulation 13.
4.-(1) Shirika litahakikisha kwamba, uchunguzi wa kina, upimaji wa uendeshaji na urekebishaji wa vifaa unafanywa na watoa huduma walioidhinishwa kwa mujibu wa kanuni ya 13 wa Kanuni hizi, kanuni ya III/20 ya Mkataba wa Usalama na miongozo iliyotolewa na Shirika kupitia Notisi ya Usafiri Majini katika uzingatiaji wa vifaa vya baharini na viwango vilivyoidhinishwa. (2) Masharti ya kanuni ya 13 ya Kanuni hizi, yatatumika vilevile kwa watengenezaji wanapokuwa 5 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) wanafanya kazi kama watoa huduma walioidhinishwa. Viwango vya ujuzi na utoaji wa vyeti Ripoti na kumbukumbu - 5
AI-assisted research summary: The provision requires certain inspections, tests, maintenance, adjustments, and repairs to be carried out by authorized people or providers, and allows an authorized service provider to be the ship operator under stated conditions.
5.-(1) Ukaguzi wa kila wiki na kila mwezi na matengenezo ya mara kwa mara yatafanywa na watoa huduma walioidhinishwa au wafanyakazi wa ndani ya meli chini ya maelekezo ya afisa mwandamizi wa meli kama ilivyoainishwa katika kitabu cha mwongozo wa matengezo ya vifaa husika. (2) Uchunguzi wa kina namajaribio ya uendeshajiwa kila mwaka kama ilivyoainishwa chini ya kanuni ya 8, utafanywa na wafanyakazi walioidhinishwa wa mtengenezaji au mtoa huduma kwa mujibu wa kanuni za 13 na 14. (3) Mtoa huduma aliyerejewa chini ya kanuni ndogo ilimradi ya (1), anaweza kuwa opareta wa meli ameidhinishwa kwa mujibu wa kanuni za 4, 13 na 14. (4) Uchunguzi wa kina, urekebishaji, upimaji wa uendeshaji na ukarabati wa miaka mitano utafanywa na watu walioidhinishwa wa mtengenezaji au mtoa huduma aliyeidhinishwa kwa mujibu wa kanuni za 13 na 15. (5) Uchunguzi wa kina au urekebishaji na upimaji wa uendeshaji unaorejewa chini ya kanuni ndogo ya (4), utafanyika mbele ya mpimaji. - 6 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: The inspection and maintenance reports must be prepared and signed by the person who carried out the work, and also signed by the company representative or ship captain. Maintenance and testing records must be updated and kept on the ship for the equipment’s whole working life. After a detailed survey and operational test, the manufacturer or authorized service provider must immediately issue a statement that the lifeboat arrangement is still fit for use, and that statement must be attached to the original certification documents and approval copy.
6.-(1) Ripoti na orodha za ukaguzi zitaandaliwa na kusainiwa na mtu atakayefanya ukaguzi na matengenezo, na kusainiwa pia na mwakilishi wa Kampuni au nahodha wa meli. (2) Kumbukumbu za matengenezo, uchunguzi wa kina, upimaji wa uendeshaji, urekebishaji na ukarabati zitahuishwa na kuwekwa kwenye meli kwa kipindi chote cha utendaji kazi wa kifaa. urekebishaji (3) Pale ambapo uchunguzi wa kina, upimaji wa uendeshaji, umekamilika, na mtengenezaji au mtoa huduma aliyeidhinishwa aliyefanya kazi husika atatoa mara moja taarifa inayothibitisha kwamba mipangilio ya boti ya uokozi wa maisha bado inafaa kutumika. ukarabati (4) Taarifa iliyorejewa chini ya kanuni ndogo ya (3), itaambatishwa na nakala ya hati halisi za uthibitisho na 6 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) idhini. SEHEMU YA TATU UTARATIBU MAALUMU WA UKAGUZI, UTENGENEZAJI, UCHUNGUZI WA KINA, UREKEBISHAJI NA UKARABATI Miongozo ya matengenezo
Part
SEHEMU YA TATU
- 7 Verify source ↗
Miongozo ya matengenezo
AI-assisted research summary: Mmiliki na nahodha wa meli lazima wahakikishe meli ina miongozo ya matengenezo na nyaraka za kiufundi zinazohusiana, na kazi za ukaguzi, matengenezo, uchunguzi wa kina, upimaji wa uendeshaji, urekebishaji na ukarabati zifanywe kwa kuzingatia miongozo hiyo.
7.-(1) Ukaguzi wowote, matengenezo, uchunguzi wa kina, upimaji wa uendeshaji, urekebishaji na ukarabati utafanywa kulingana na miongozo ya matengenezo na nyaraka kiufundi na zilizoandaliwa na mtengenezaji. utunzaji wa zinazohusiana (2) Mmiliki na nahodha wa meli atahakikisha kwamba, seti kamili ya miongozo ya matengenezo inayotumika na nyaraka za kitaalam zinazohusiana na utunzaji zinapatikana kwenye meli. (3) Miongozo ya matengenezo na nyaraka za kiufundi zinazohusiana zitajumuisha vifaa kama vilivyoorodheshwa chini ya kanuni ya 10 kama kiwango cha chini na kuhuishwa na Kampuni kwa kuzingatia taarifa halisi zinazotolewa na mtengenezaji. Uchunguzi wa kina wa kila mwaka na upimaji wa uendeshaji - 8 Verify source ↗
Uchunguzi wa kina wa kila mwaka na upimaji wa uendeshaji
AI-assisted research summary: Orodha ya vifaa vya ukaguzi wa kila wiki na kila mwezi ni sehemu ya uchunguzi wa kwanza wa kina wa mwaka kwa meli.
8. Orodha ya vifaa vya ukaguzi wa kila wiki na kila mwezi chini ya Kanuni za III/20.6 na III/20.7 za Mkataba wa Usalama zitakuwa sehemu ya uchunguzi wa wa kina wa kwanza wa kila mwaka. Mapitio ya vyeti, nk., ya mara kwa mara ndani ya meli - 9 Verify source ↗
Mapitio ya vyeti, nk., ya mara kwa mara ndani ya meli
AI-assisted research summary: Wafanyakazi wa meli lazima waandae kumbukumbu za ukaguzi na matengenezo ya mara kwa mara, na wapitie vyeti vinavyotumika kwa vifaa kwa mujibu wa Mfumo wa Usimamizi wa Usalama.
9. Kumbukumbu za ukaguzi na matengenezo ya mara kwa mara ndani ya meli zitaandaliwa na wafanyakazi wa meli na vyeti vinavyotumika kwa ajili ya vifaa vitafanyiwa mapitio kwa mujibu wa masharti yanayotumika katika Mfumo wa Usimamizi wa Usalama. Vitu vya kuchunguzwa na kuangaliwa - 10 Verify source ↗
Vitu vya kuchunguzwa na kuangaliwa
AI-assisted research summary: Section 10 lists the parts of lifeboats, rescue boats, launch/recovery equipment, and related systems that must be thoroughly examined and checked for condition and operation.
10.-(1) Vitu vifuatavyo vitachunguzwa kwa kina na kuangaliwa kwa ajili ya kujiridhisha na hali yake na uendeshaji katika boti za kuokoa maisha ikiwa ni pamoja na boti za kuokoa maisha zinazoserereka, boti za uokozi na boti za uokozi wa haraka: (a) hali ya muundo wa boti ikijumuisha vifaa vilivyofungwa na ambavyo havijafungwa, ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa kuona mipaka ya nje 7 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) ya eneo la wazi, kadiri inavyowezekana; (b) injini na mfumo ya uzungushaji; (c) mfumo wa kunyunyizia, endapo umewekwa; (d) mfumo wa usambazaji hewa, endapo umewekwa; (e) mfumo wa uendeshaji; (f) mfumo wa usambazaji umeme; (g) mfumo wa utoaji maji; (h) mipangilio ya vizuizi vya meli; na (i) mfumo wa uwekaji boti ya uokozi katika usawa stahiki. (2) Yafuatayo yatachunguzwa kwa kina ili kubaini hali na uendeshaji wa winchi breki inapokuwa na boti tupu au mzigo sawa na huo katika gia ya kutolea boti za kuokoa maisha ikiwa ni pamoja na boti za uokozi wa maisha zinazoserereka, boti za uokozi, boti za uokoaji wa haraka: (a) uendeshaji wa vifaa vya kuwezesha gia ya kutolea; (b) kucheza kunakozidi ikijumuisha hali yake ya uvumilivu; wa (c) mfumo umewekwa; hydrostatiki, endapo (d) kebo za kuzuia na kuruhusu; na (e) vifungia ndoano. (3) Vifaa vifuatavyo vitachunguzwa kwa kina na kuangaliwa kwa ajili ya kujiridhisha na hali yake na uendeshaji katika vifaa vya kutumbukiza boti za kuokoa maisha ikiwa ni pamoja na boti za uokozi wa maisha zinazoserereka, boti za uokozi, boti za uokoaji wa haraka: (a) daviti au miundo ya vifaa vingine vya kushushia, hasa kuhususiana na kutu, kupishana, kubondeka na kucheza kunakozidi; (b) waya, mfuo, uwezekano wa uharibifu kama vile kuharibika kwa kamba na kutu; na (c) ulainishaji wa waya, mfuo na sehemu zinazozunguka; (d) pale inapowezekana- (i) utendaji kazi wa swichi za kikomo; (ii) mifumo ya nishati iliyohifa dhiwa; (iii) mfumo wa kimiminika; na (iv) winchi; 8 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) (e) kukagua mfumo wa breki kwa mujibu wa mwongozo wa kitabu; (f) kubadilisha pedi za breki, pale inapobidi; (g) msingi wa winchi; na (h) pale inapowezekana- (i) mfumo wa udhibi kwa rimoti; na (ii) mfumo wa usambazaji nishati. Masharti ya ziada ya matengenezo na majaribio - 11 Verify source ↗
Masharti ya ziada ya matengenezo na majaribio
AI-assisted research summary: The provision requires great care during inspection and maintenance of launching appliances and sets conditions for testing lifeboats and rescue boats.
11.-(1) Uangalifu mkubwa utachukuliwa wakati wa kufanya shughuli zote za ukaguzi na matengenezo kwenye kifaa cha kushushia kwa kuwa mpangilio na matengenezo ya kifaa cha kushushia ni shughuli muhimu kuhusiana na kudumisha utendaji kazi salama wa boti za kuokoa maisha ikiwa ni pamoja na boti za uokozi wa maisha zinazoserereka, boti za uokozi, boti za uokoaji wa haraka na boti zinazoteremshwa kwa kutumia daviti. (2) Matengenezo au marekebisho ya kifaa cha kushushia hayatafanywa wakati ndoano ikiwa na mzigo. (3) Upimaji wa uendeshaji wa boti zinazoshushwa kwa kifaa cha daviti na boti za uokozi kwa mfumo wa ushushaji wenye mzigo utafanywa kama ifuatavyo: (a) weka boti kwa kiasi fulani ndani ya maji ili kwamba uzito wa boti kwa kiasi kikubwa kuwa umeshikwa na vishikizo na mfumo wa hydrostatiki, ukiwa haujaanzishwa; umefungwa, endapo (b) endesha kifaa cha ushushaji chenye mzigo; (c) rekebisha kifaa cha ushushaji chenye mzigo; na (d) kuchunguza gia ya kutoa na kufunga ndoano ili kuhakikisha kuwa ndoano imewekwa upya na hakuna uharibifu wowote uliotokea. (4) Upimaji wa uendeshaji wa boti za kuokoa maisha zilizozinduliwa na daviti na boti za uokoaji kutolewa kwenye mzigo utafanywa kama ifuatavyo: (a) weka boti ili isiweze kupita maji kabisa; (b) endesha kifaa cha kushushia kisichokuwa na mzigo; (c) rekebisha kifaa cha kushushia kisichokuwa na mzigo; na 9 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) (d) rejesha boti mahali palipowekwa na kujiandaa kwa utayari wa kufanya kazi. (5) Wakati wa upimaji, kabla ya kuinua, kifaa cha kushushia itaangaliwa ili kuhakikisha kuwa imewekwa kikamilifu na ipasavyo na ugeuzaji wa boti utafanywa bila mtu yeyote kuwa ndani. (6) Upimaji wa uendeshaji wa boti za kuokoa maisha zinazoserereka kwa mfumo wa kuiachia itafanywa kama ifuatavyo: (a) tumia maandalizi ya upimaji bila kuiachia boti ya kuokoa maisha, kama inavyohitajika na aya ya - 4
AI-assisted research summary: The provision describes operational tests for lifesaving appliances, including releasing, resetting, and checking lifeboat and rescue-boat launching gear.
4.7.6.4 ya Kanuni za Kimataifa za Vifaa vya Uokozi wa Maisha, kama ilivyobainishwa katika miongozo kwa uendeshaji mtengenezaji; kutoka ya (b) iwapo atahitajika kuwa ndani ya meli, hakikisha na kwamba mwendeshaji ameshikiliwa vizuri katika eneo la kiti ambapo mfumo wa ushushaji unapaswa kuendeshwa; (c) endesha mfumo wa ushushaji ili kuachia boti ya ameketi vizuri uokoaji wa maisha; (d) rekebisha boti ya kuokoa maisha katika mpangilio uliowekwa; (e) rudia taratibu zilizorejewa katika aya (b) hadi (d), kwa kutumia utaratibu mbadala wa mfumo wa kuachia, endapo unatumika; (f) ondoa mipangilio ya uendeshaji kwa kujaribu bila kuiachia boti ya kuokoa maisha, kama inavyohitajika katika aya ya 4.7.6.4 ya Kanuni za Kimataifa za Vifaa vya Uokozi wa Maisha; na (g) thibitisha kuwa boti ya kuokoa maisha iko tayari kuachia mipangilio iliyowekwa. (7) Upimaji wa uendeshaji wa kifaa cha uokoaji kinachoshushwa kwa kifaa cha ushushaji cha daviti utazingatia yafuatayo: (a) toa kwa mkono ndoano yenye mzigo wa kilo 150 kwenye ndoano; (b) achia ndoano moja kwa moja yenye uzito wa kilo 200 kwenye ndoano inaposhushwa chini; na (c) chunguza ndoano ya kuachia na vifungia ndoano 10 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) kuwa ndoano kuhakikisha ili imewekwa kikamilifu kabisa na hakuna uharibifu uliotokea. (8) Pale ambapo kifaa cha uokoaji kinatumiwa kwa jaribio badala ya uzani wa dumi, kitendakazi cha kuachia kiotomatiki kitaachia kifaa cha uokoaji pale ambapo kifaa hicho kimefika kwenye maji. (9) Kwa winchi za vifaa vya kushushia boti za kuokoa maisha ikiwa ni pamoja na boti za kuokoa maisha zinazoserereka, boti za uokozi na boti za uokozi wa haraka, majaribio ya kila mwaka ya uendeshaji yatafanywa kwa kushusha chomboau boti tupu au mzigo sawa na huo. (10) Pale ambapo chombo kimefikia kiwango chake cha juu cha kasi ya ushushaji na kabla ya chombo kuingia ndani ya maji, breki itawekwa kwa ghafla na kufuatana na majaribio chini ya kanuni ndogo ya (9), sehemu za muundo zilizosisitizwa zitakaguliwa upya pale ambapo muundo unaruhusu kukaguliwa upya. Majaribio ya miaka mitano kuhusiana na utendaji wa vifaa - 12 Verify source ↗
Majaribio ya miaka mitano kuhusiana na utendaji wa vifaa
AI-assisted research summary: This provision requires five-year operating and maintenance tests for listed rescue and lifeboat equipment, using specified test loads and inspection steps.
12.-(1) Majaribio ya miaka mitano ya uendeshaji wa winchi za vifaa vya uokoaji yatafanywa na mzigo wa uthibitisho sawa na mara 1.1 ya uzito wa kifaa cha kuokoa au boti ya uokoaji na ukamilishaji wake wa watu na vifaa na wakati mzigo wa uthibitisho umefika kiwango cha juu cha kasi ya ushushaji, breki itatumika kwa ghafla. (2) Kufuatia majaribio yaliyorejewa chini ya kanuni sehemu za kimuundo zilizosisitizwa ambapo muundo unaruhusu tena pale (1), ndogo ya zitakaguliwa kukaguliwa upya. (3) Majaribio ya uendeshaji na urekebishaji katika vipindi vya miaka mitano ya kifaa cha kushushia boti za kuokoa maisha ikiwa ni pamoja na boti za kuokoa maisha zinazoserereka, boti za uokoaji, boti za uokoaji wa haraka na vifaa vya uokoaji yatajumuisha- (a) kuvunjwa kwa vifaa vya kutoa ndoano; (b) uchunguzi wa uvumilivu na mahitaji ya muundo; (c) marekebisho ya mfumo wa kifaa cha kushushia vifaa vya uokoaji baada ya kufungwa; (d) majaribio ya uendeshaji kama yanavyotumika, lakini yenye mzigo unaolingana na mara 1.1 ya 11 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) uzito wa boti ya kuokoa maisha na ukamilishaji wake kamili wa watu na vifaa; (e) uchunguzi wa kasoro na nyufa katika sehemu muhimu; na (f) urekebishaji mwingine wowote ukihitajika utafanywa kwa mujibu wa kanuni ya 5(3). SEHEMU YA NNE MASHARTI YA UIDHINISHAJI WA WATOA HUDUMA Masharti ya uidhinishwaji wa watoa huduma
Part
SEHEMU YA NNE
- 13 Verify source ↗
Masharti ya uidhinishwaji wa watoa huduma
AI-assisted research summary: Uidhinishaji wa watoa huduma lazima ujumuishe mahitaji ya wafanyakazi waliothibitishwa, zana, vipuri, miongozo ya mtengenezaji, na mfumo wa ubora uliorekodiwa.
13.-(1) Uidhinishaji wa watoa huduma utajumuisha- (a) ajira na nyaraka za wafanyakazi waliothibitishwa kwa mujibu wa viwango vinavyotambulika vya kitaifa, kimataifa au sekta husika, au mpango ulioanzishwa na mtengenezaji wa uthibitishaji na kwa vyovyote vile, programu ya uthibitishaji itazingatia kanuni ya 16 kwa huduma inayopaswa kutolewa kwa kila aina ya kifaa; (b) upatikanaji wa zana za kutosha, na hasa zana maalum zilizoainishwa katika mwongozo wa mtengenezaji, zana zinazobebeka kama zinahitajika kwa kazi itakayofanywa kwenye meli; ikiwa ni pamoja na (c) upatikanaji wa vipuri na vifaa sahihi kama ilivyoainishwa kwa ajili ya matengenezo na ukarabati; (d) upatikanaji wa miongozo ya mtengenezaji kwa ajili ya kazi ya ukarabati inayohusisha kufunguliwa au marekebisho ya mfumo wa ushushaji wenye mizigo na winchi za daviti; na (e) mfumo wa ubora uliorekodiwa na kuthibitishwa, ambao unajumuisha angalau yafuatayo: (i) kanuni za maadili kwa wafanyakazi wanaohusika katika shughuli husika; (ii) matengenezo na urekebishaji wa zana za kupimia na vipimo; (iii) mipango ya mafunzo na vyeti kwa wafanyakazi; (iv) usimamizi na uhakiki ili kuhakikisha uzingatiaji wa taratibu za uendeshaji; 12 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) (v) kurekodi na kuripoti habari; (vi) usimamizi wa ubora wa tanzu na mawakala; (vii) maandalizi ya kazi; na (viii) ikiwa kutakuwa na mazingira ya kufutwa kwa cheti kilichotolewa kwa mfanyakazi yeyote, notisi ya kuonyesha sababu atakayopewa; (ix) mapitio ya mara kwa mara ya taratibu za kufanya kazi, malalamiko, hatua za kurekebisha na utoaji, utunzaji na udhibiti wa nyaraka. (2) Mfumo wa ubora uliorekodiwa unaozingatia toleo la kisasa zaidi la mfululizo wa ISO 9000 na unaojumuisha masuala yaliyoainishwa chini ya kanuni ndogo ya (1) utachukuliwa kuwa unakubalika. (3) Shirika taarifa zinazowahusu watoa huduma walioidhinishwa zinapatikana kupitia Notisi ya Usafiri Majini. litahakikisha kwamba Utoaji na utunzaji wa nyaraka za matengenezo (4) Pale ambapo mtengenezaji ameacha biashara au kutoa usaidizi wa kiufundi, Shirika linaweza kuwaidhinisha watoa huduma wa kifaa kwa kuzingatia idhini ya awali ya kifaa au uzoefu wa muda mrefu na utaalam utakaoonyeshwa kama mtoa huduma aliyeidhinishwa. - 14 Verify source ↗
Utoaji na utunzaji wa nyaraka za matengenezo
AI-assisted research summary: After a successful initial inspection, the Organization must issue an approval document, state the expiry date clearly, carry out regular inspections, and cancel approval for non-compliant service providers.
14.-(1) Baada ya kufanikiwa kwa ukaguzi wa awali wa mtoa huduma, hati ya idhini itatolewa na Shirika inayofafanua wigo wa huduma zinazotolewa na tarehe ya kuisha itaandikwa kwa uwazi kwenye hati. (2) Shirika litahakikisha kwamba kazi inaendelea, kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa mujibu wa masharti haya, na idhini ya watoa huduma wasiozingatia. itafuta (3) Shirika linaweza kukubali au kutambua watoa huduma walioidhinishwa na mamlaka ya nchi nyingine au na Mashirika yao Yanayotambuliwa. SEHEMU YA TANO MASHARTI YA UTHIBITISHAJI WA WAFANYAKAZI 13 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) Wafanyakazi
Part
SEHEMU YA TANO
- 15 Verify source ↗
Wafanyakazi
AI-assisted research summary: Wafanyakazi waliotajwa katika kanuni ya 5 lazima wahakikishiwe na mtengenezaji au mtoa huduma aliyeidhinishwa.
15. Wafanyakazi kama ilivyoainishwa katika kanuni ya 5, watathibitishwa na mtengenezaji au mtoa huduma aliyeidhinishwa kwa kila utengenezaji na aina ya vifaa vitakavyofanyiwa kazi kwa mujibu wa masharti ya kanuni hii. Masharti ya udhibitisho - 16 Verify source ↗
Masharti ya uthibitisho
AI-assisted research summary: Wafanyakazi waliohitimu elimu, mafunzo, na tathmini ya uwezo wanaweza kupewa uthibitisho wa awali.
16.-(1) Udhibitisho wa awali utatolewa kwa wafanyakazi waliohitimu elimu, mafunzo na tathmini ya uwezo. (2) Elimu inayorejewa katika kanuni ndogo ya (1) itashughulikia- (a) sheria na kanuni husika, ikijumuisha mikataba ya kimataifa; (b) ubunifu na ujenzi wa boti za kuokoa maisha zikiwemo boti za kuokoa maisha zinazoserereka, boti za uokozi na boti za uokozi wa haraka, ikijumuisha vifaa vya kushushia vyenye mizigo na vifaa vya uokoaji; (c) sababu za ajali za boti za uokoaji; (d) elimu na mafunzo kwa vitendo katika taratibu zilizoainishwa chini ya Sehemu ya Tatu ya Kanuni hizi yanayohitaji uthibitisho; (e) taratibu za kina za uchunguzi wa kina, upimaji wa uendeshaji, urekebishaji na ukarabati wa boti za kuokoa maisha zikiwemo boti za kuokoa maisha zinazoserereka, boti za uokozi na boti za uokozi wa haraka, vifaa vya kushushia na vifaa vya kushushia vyenye mizigo, kama inavyotumika; (f) taratibu za kutoa ripoti ya utumishi na taarifa ya kufaa kwa madhumuni kulingana na kanuni ya 6(3); na (g) masuala ya kazi, afya na usalama wakati wa kufanya kazi melini. (3) Mafunzo yatajumuisha mafunzo ya kiufundi kwa vitendo juu ya mbinu za uchunguzi wa kina, upimaji wa uendeshaji, matengenezo, ukarabati na urekebishaji kwa kutumia ambavyo wafanyakazi wanatakiwa kuthibitishwa. vifaa (4) Mafunzo ya kiufundi chini ya kanuni ndogo ya (3) yatajumuisha kutenganisha, kuunganisha upya, uendeshaji 14 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) Uhalali wa vyeti na uhuishaji Tathmini na kuwasilisha taarifa sahihi na marekebisho ya vifaa. (5) Mafunzo ya darasani yatakamilishwa na mafunzo ya vitendo katika uendeshaji ambao uthibitisho unahitajika, chini ya usimamizi wa mtu aliyethibitisha. (6) Kabla ya utoaji wa uthibitisho, tathmini ya uwezo itakamilika kwa njia ya kuridhisha, kwa kutumia vifaa ambavyo wafanyakazi wanatakiwa kuthibitishwa. - 17 Verify source ↗
Uhalali wa vyeti na uhuishaji
AI-assisted research summary: Certificates are issued after training and competency assessment, last three years from issue, and may be suspended if performance is deficient.
17.-(1) Baada ya kukamilika kwa mafunzo na tathmini ya uwezo, cheti kitatolewa kinachofafanua kiwango cha sifa na upeo wa uthibitisho. (2) Tarehe ya kuisha kwa cheti kilichorejewa chini ya kanuni ndogo ya (1), itaandikwa kwa uwazi na itakuwa kwa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe ya kutolewa. (3) Uhalali wa cheti chochote unaweza kusitishwa iwapo kuna upungufu wowote katika utendaji kazi na kutolewa upya baada ya tathmini ya uwezo ya ziada. (4) Tathmini ya uwezo itafanywa ili kufanya upya uthibitishaji na katika hali ambapo mafunzo ya kujiendeleza yataonekana kuwa muhimu tathmini zaidi itafanywa baada ya kukamilika. SEHEMU YA SITA MASHARTI YA JUMLA
Part
SEHEMU YA SITA
- 18
AI-assisted research summary: Msajili lazima afanye tathmini ya masharti ya udhibiti, aandike ripoti ya hitimisho, na awasilishe taarifa kwa Waziri.
18.-(1) Msajili atapaswa- (a) kufanya tathmini ya masharti ya udhibiti yaliyomo katika Kanuni hizi; ripoti (b) kuandaa inayoeleza hitimisho kwa tathmini; na (c) kuwasilisha taarifa kwa Waziri. (2) Taarifa ya kwanza chini ya kanuni hii itachapishwa kabla ya mwaka wa tano wa tarehe ambayo Kanuni hizi zitaanza kutumika. (3) Taarifa zinazofuata zitachapishwa kwa vipindi visivyozidi miaka mitano. (4) Taarifa iliyotayarishwa na kuwasilishwa chini ya kanuni hii, itapaswa- (a) kuweka malengo yanayokusudiwa kufikiwa na masharti ya udhibiti yanayorejewa katika kanuni 15 Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokozi wa Maisha, Vifaa vya Uokozi na Vifaa Vya Kushushia Vifaa Vya Uokoaji Tangazo la Serikali Na. 502 (Linaendelea.) ndogo ya (1)(a); (b) kutathmini kiwango ambacho malengo hayo yanafikiwa; (c) kutathmini kama malengo hayo bado yanafaa; na (d) pale ambapo malengo yataonekana kuwa yanafaa, kutathmini kiwango ambacho yanaweza kufikiwa kwa njia nyingine ambayo inahusisha masharti mepesi ya udhibiti. Adhabu za jumla - 19
AI-assisted research summary: Kukiuka masharti ya Kanuni hizi ni kosa, na mtu akitiwa hatiani anaweza kupewa faini, kifungo cha hadi miezi sita, au vyote kwa pamoja.
19. Mtu anayekiuka masharti ya Kanuni hizi anatenda kosa na endapo atatiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua dola za Marekani elfu moja au kiwango kinacholingana katika shilingi za Kitanzania au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi sita au vyote kwa pamoja. Kushughulikia malalamiko TS. Na. 338 la 2018 - 20 Verify source ↗
Tathmini na utoaji wa taarifa
AI-assisted research summary: A person unhappy with a decision made under these Regulations may apply to the Agency for review.
20. Mtu ambaye hajaridhika na uamuzi uliotolewa chini ya Kanuni hizi anaweza kuwasilisha maombi ya mapitio kwa Shirika kwa mapitio kwa mujibu wa Kanuni za Ushughulikiaji wa Malalamiko za Wakala wa Meli Tanzania. Dodoma, 28 Juni, 2023 MAKAME M. MBARAWA, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi 16
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Masharti ya Matengenezo, Uchunguzi wa Kina, Majaribio ya Uendeshaji, Marekebisho na Ukarabati wa Boti za Uokoaji wa Maisha, Vifaa Vya Uokoaji
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in