Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji za Mwaka 2023
These regulations are titled the Internal Review Conduct Regulations of the Energy and Water Utilities Regulatory Authority, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji za Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
These regulations are titled the Internal Review Conduct Regulations of the Energy and Water Utilities Regulatory Authority, 2023. These regulations apply to review procedures for substantive decisions made under delegated authority. Section 3 defines key terms used in the regulations. Mtu ambaye hajaridhika na uamuzi anaweza kuomba mapitio, na ombi hilo lazima liwasilishwe ndani ya siku 14 baada ya kupokea uamuzi. Bodi lazima iunde Kamati ndani ya siku 7 baada ya kupokea maombi chini ya kanuni ya 4, na pia impe Mwenyekiti wa Kamati pamoja na Mkurugenzi Mkuu kumteua Katibu wa Kamati.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji za Mwaka 2023
Showing 22 of 22
- 1 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: These regulations are titled the Internal Review Conduct Regulations of the Energy and Water Utilities Regulatory Authority, 2023.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji za Mwaka 2023. - 2 Verify source ↗
Matumizi
AI-assisted research summary: These regulations apply to review procedures for substantive decisions made under delegated authority.
2. Kanuni hizi zitatumika katika taratibu za mapitio ya maamuzi ya msingi yaliyofanywa kwa mamlaka yaliyokasimiwa. Tafsiri Sura ya 414 - 3 Verify source ↗
Tafsiri
AI-assisted research summary: Section 3 defines key terms used in the regulations.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Sheria” maana yake ni Sheria ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji; “Mleta maombi” maana yake ni mtu ambaye ameomba mapitio ya uamuzi chini ya Sehemu ya Pili; “Mamlaka” maana yake ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ambayo imeainishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria; “Bodi” maana ya Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji iliyoainishwa chini ya kifungu cha 8(1) cha Sheria; “Kamati” maana yake ni Kamati ya Mapitio ya Ndani iliyoundwa kwa mujibu wa kanuni ya 5; “Mkurugenzi Mkuu” maana yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na 2 Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati Na Maji Tangazo La Serikali Na. 599 (Linaendelea) Maji aliyeteuliwa chini ya Sheria; “Jopo” maana yake ni Jopo la Mapitio ambalo limeanzishwa kwa mujibu wa kifungu 26 cha Sheria; “mjibu maombi” maana yake ni mtu ambaye maombi ya mapitio yamewasilishwa hidi yake chini ya kanuni hizo; “uamuzi wa msingi” maana yake ni uamuzi unaofanywa kwa kuzingatia msingi wa jambo na kanuni zinazobainisha haki za mtu tofauti na uamuzi wa kiutaratibu ambao unatokana na kanuni na taratibu zinazotumika kupatahaki za mtu; “Baraza” maana yake ni Baraza la Ushindani lililoanzishwa kwa mujibu ya Sheria ya Ushindani. SEHEMU YA PILI MAOMBI YA MAPITIO
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Maombi ya mapitio
AI-assisted research summary: Mtu ambaye hajaridhika na uamuzi anaweza kuomba mapitio, na ombi hilo lazima liwasilishwe ndani ya siku 14 baada ya kupokea uamuzi.
4.-(1) Mtu ambaye hajaridhika na uamuzi wa msingi uliofanywa kwa niaba ya Mamlaka kwa mamlaka yaliyokasimishwa kwa Mamlaka. kuomba mapitio anaweza Sura ya 285 Maombi ya mapitio (2) Maombi chini ya kanuni ndogo ya (1) yatanyika ndani ya siku kumi na nne baada ya kupokea uamuzi. (3) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo ya (2) tarehe ya kupokea uamuzi itakuwa tarehe ambayo uamuzi uliwasilishwa ipasavyo kwa mujibu wa kanuni 8. (4) Maombi ya mapitio yatakuwa katika fomu iliyoainishwa katika Jedwali. Mamlaka ya uunda Kamati - 5 Verify source ↗
Mamlaka ya kuunda Kamati
AI-assisted research summary: Bodi lazima iunde Kamati ndani ya siku 7 baada ya kupokea maombi chini ya kanuni ya 4, na pia impe Mwenyekiti wa Kamati pamoja na Mkurugenzi Mkuu kumteua Katibu wa Kamati.
5.-(1) Baada ya kupokea maombi chini ya kanuni ya 4 na kwa vyovyote vile siozaidi ya siku saba, Bodi itaunda Kamati itakayokuwa na: (a) Wajumbe wawili kutoka kwenye Jopo ambapo, mmoja kati yao atakuwa mwanasheria na mwingine atakuwa mtu mwenye sifa stahiki katika suala linalohusika katika maombi;na (b) Mjumbe mmoja wa Bodi ambaye hakushiriki 3 Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati Na Maji Tangazo La Serikali Na. 599 (Linaendelea) Maombi ya kufanya mawasilaino katika uamuzi ambao unahusiana na mapitio yenyewe. (2) Bodi itateua Mwenyekiti wa kamati kutoka miongoni mwa wanakamati waliochaguliwa katika kifungu kidogo cha 5(1) (3) Mkurugenzi Mkuu atateua mtu mmoja kutoka miongoni mwa wajumbe wa maofisa wa Mamlaka wenye taaluma ya sheria kuwa Katibu wa Kamati. - 6 Verify source ↗
Mwaliko wa kufanya mawasilisho
AI-assisted research summary: Kamati inaweza kuwaalika watu kufanya mawasilisho kuhusu maombi ya mapitio, na mtu aliyealikwa lazima ayatume mawasilisho yake ndani ya siku 21 kutoka tarehe ya mwaliko.
6.-(1) Kamati itaelekeza maombi ya mapitio kuwasilishwa kwa watu wa fuatao ikiwaalika kufanya mawasilisho katika maombi husika: (a) mjibu maombi; (b) Waziri; (c) Waziri husika sekta; (d) pande zenye maslahi, kamazipo (e) Baraza la Ushauri la Watumiaji; na (f) Mtu yeyote ambaye Baraza litamuona muhimu kumualika. (2) Mtu atakayepata mualiko wa kufanya mawasilisho chini ya kanuni ndogo ya (1) ataandaa mawasilisho yanayounga mkono au kupinga maombi na kuyawasilisha kwa Kamati ndani ya siku ishirini na moja kutoka tarehe ya mwaliko. (3) Mtu ambaye amewasilisha mawasilisho chini atakuwa kanuni ya nahakiyakuhudhuriambeleyaKamatiwakatiwausikilizaji. ndogo (2) ya Uongezaji muda wa kufanya maombi - 7 Verify source ↗
Nyongeza ya muda wa kufanya maombi
AI-assisted research summary: An applicant may ask for more time to file a review application if they show good cause.
7.-(1) Mletamaombi anaweza kuomba nyongeza ya muda wa kuwasilisha maombi ya mapitio kwa kuonyesha sababu za msingi. (2) Maombi chini ya kanuni ndogo ya (1) yatafanywa kwa Mkurugenzi Mkuu ambaye baada ya kupokea atayawasilisha kwa Kamati kwa uamuzi. (3) Baada ya kupokea wa maombi chini ya kanuni ndogo ya (2) kamati ijadili na kutoa mapendekezo kwa Bodi. (4) Wakati wa kujadili maombi, Kamati itatoa fursa kwa pande zote kufanya mawasilisho. 4 Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati Na Maji Tangazo La Serikali Na. 599 (Linaendelea) Upelekaji wa nyaraka - 8 Verify source ↗
Uwasilishaji wa nyaraka
AI-assisted research summary: Nyaraka chini ya Kanuni hizi lazima ziwasilishwe kwa njia ya binafsi, posta yenye risiti ya upokeaji, au kuchapishwa katika magazeti mawili yenye mzunguko mkubwa Tanzania chini ya masharti fulani.
8. Uwasilishaji wa araka kwa upande wowote chini ya Kanuni hizi utakuwa kwa njia ya- (a) uwasilishaji binafsi au mwakilishi wake ambaye atakiri kupokea kwa kutiasaini na kurudisha nakala ya nyaraka kwa Mamlaka; kwa mhusika (b) posta pamoja na risiti ya upokeaji; au (c) Uchapishaji katika magazeti mawili yenye mzunguko mkubwa Tanzania, moja kwa Kiingereza na jingine kwa Kiswahili pale ambapo Mamlaka ya meona kwamba; (i) (ii) (iii) na nyingine haziwezi kunasababu za kuamini kwamba mhusika anakwepa uwasilishaji wa nyaraka kwa makusudi; kutokana sababu yoyote, nyaraka kuwasilishwa kwa njia ya kawaida; kunaushahidi wa maandishi kutoka katika mamlaka ya Serikali ya mtaa juhudi za kuwasilisha kwamba husika upande kwa nyaraka zilichukuliwa na kwamba juhudi hizo zimeshindwa kutokana na sababu zilizotolewa chini ya aya ndogo za (i) na (ii). - 9 Verify source ↗
Akidi ya Kamati
AI-assisted research summary: A Committee meeting must have at least three members as quorum.
9. Akidi katika kikao chochote cha Kamati itakuwa angalau wajumbe walau watatu. itatoa - 10 Verify source ↗
Taarifa ya usikilizwaji
AI-assisted research summary: Kamati lazima itoe taarifa ya maandishi kwa wahusika kuhusu tarehe na mahali pa usikilizwaji, na taarifa hiyo isainiwe na Mwenyekiti au Katibu wa Kamati.
10. Kamati taarifa ya maandishi kwa wahusika ikihamisha tarehe na mahali pa usikilizwaji na taarifa hiyo itasainiwa na Mwenyekiti au Katibu wa Kamati. Akidi ya Kamati Taarifa ya usikilizwaji Usikilizaji wa maombi - 11 Verify source ↗
Usikilizwaji wa maombi
AI-assisted research summary: Kamati lazima ianze kusikiliza maombi baada ya siku 21 kupita tangu mawasilisho ya watu waliotajwa chini ya kanuni ya 5 yalipostahili kuwasilishwa.
11.-(1) Baada ya kuisha kwa siku ishirini na moja ambazo watu waliotajwa chini ya kanuni ya 5 wanatakiwa kuwasilisha mawasilisho yao, kamati itaanza usikilizwaji wa maombi. 5 Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati Na Maji Tangazo La Serikali Na. 599 (Linaendelea) Utaratibu endapo mhusika hawatahdhuria Maombi ya mapito Uondoaji wa maombi Mapendekezo ya Kamati (2) Wakati wa usikilizaji pande zinaweza kuhudhuria binafsi au kupitia wakili au mwakilishi aliyeteuliwa rasmi. (3) Wakati wa usikilizwaji, mawasilisho yatafanywa kwa mdomo au kwa maandishi. - 12 Verify source ↗
Utaratibu endapo wahusika hawatahudhuria
AI-assisted research summary: If the applicant or respondent does not attend the hearing without good reason, the Committee or Board may take procedural steps, including recommending dismissal, hearing the matter in the absence of a party, or setting aside those orders on a showing of good cause.
12.-(1) Endapo mleta maombi haja hudhuria siku iliyopangwa kwa ajili ya usikilizwaji bila ya sababu ya msingi, Kamati inaweza kupendekeza kwa Bodi kufuta maombi husika. (2) Endapo mleta maombi amehudhuria na mjibu maombi hajahudhuria bila sababu ya msingi, maombi yanaweza kuendelea kusikilizwaupande mmoja. (3) Upande unaweza, baada ya kuonesha sababu za msingi, kuiomba Bodi kutengua amri ya kufuta maombi chini ya kanuni ndogo ya (1) au amri ya kusikiliza upande mmoja chini ya kanuni ndogo ya (2). - 13 Verify source ↗
Maombi ya mpito
AI-assisted research summary: The Committee may receive and decide transitional applications and applications for extension of time, and it must let both parties make submissions when considering them.
13.-(1) Kamati itakuwa na mamlaka ya kupokea na kuamua maombi yoyote ya mpito yaliyofanywa na pande kabla ya uamuzi wa maombi ya msingi pamoja na maombi ya uongezaji muda. (2) Wakati wa kujadili maombi chini ya kanuni ndogo ya (1), Kamati itatoa fursa kwa pandezote kufanya mawasilisho. - 14 Verify source ↗
Uondoaji wa maombi
AI-assisted research summary: Mleta maombi anaweza kuondoa maombi yake kabla ya uamuzi; Kamati lazima iondoe maombi hayo na kuwasilisha mapendekezo kwa Bodi baada ya kupokea ombi la kuondoa.
14.-(1) Wakati wowote kabla ya uamuzi wa maombi, mleta maombi anaweza kuondoa maombi yake. (2) Baada ya kupokea wa maombi ya kuondoa maombi, Kamati itayaondoa maombi na kuwasilisha mapendekezo kwa Bodi. - 15 Verify source ↗
Mapendekezo ya Kamati
AI-assisted research summary: Kamati lazima ishughulikie maombi, iandae mapendekezo, na iyawasilishe kwa Bodi ndani ya siku 21 baada ya kupokea mawasilisho chini ya kanuni ya 6.
15.-(1) Ndani ya siku ishirini na moja baada ya kupokea mawasilisho chini ya kanuni ya 6, Kamati itashughulikia maombi pamoja na mawasilisho yoyote yaliyopokelewa, itaandaa mapendekezo na kuyawasilisha kwa Bodi kwaajili ya uamuzi. (2) Wakati kuaandaa mapendekezo chini ya kanuni ndogo ya (1), Kamati itaamua iwapo gharama zilipwe na 6 Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati Na Maji Tangazo La Serikali Na. 599 (Linaendelea) kiasi stahiki. (3) Uamuzi wa Kamati utafikiwa kwa nji ya ikiwa hakuna makubaliano, uamuzi makubaliano na utafikiwa kwa njia ya wingi wa kura. Mahali tarehe na - 16 Verify source ↗
Mahali na tarehe
AI-assisted research summary: Kamati inaamua tarehe na mahali pa usikilizwaji.
16.-(1) Kamati itaamua tarehe na mahali kwa ajili ya usikilizwaji. (2) Katika kuamua tarehe na mahali chini ya kanuni ndogo ya (1) Kamati itazingatia urahisi kwa pande na mashahidi na ufinyu wa kibajeti Kamati inaweza kusimamia mwenendo wake Uamuzi wa Bodi - 17 Verify source ↗
Kamatiinaweza kusimamia mwenendo wake
AI-assisted research summary: Kamati ina mamlaka ya kusimamia mwenendo wake kuhusu vikao na uendeshaji wa vikao vyake, kwa kuzingatia Kanuni hizi.
17. Kwa kuzingati Kanuni hizi, Kamati itakuwa na mamlaka ya kusimamia mwenendo wake kuhusiana na vikao na uendeshaji wa vikao vyake. - 18 Verify source ↗
Uamuzi wa Bodi
AI-assisted research summary: Bodi lazima ishughulikie mapendekezo ya Kamati ndani ya siku 21 baada ya kuyapokea, na inaweza kuyakubali kama yalivyo, kuyakubali pamoja na maboresho, au kuyarejesha kwa Kamati ya yapitiwe upya.
18. Baada ya kupokea mapendekezo ya Kamati chini ya kanuni ya 15 na kwa vyovyote vile si zaidi ya siku ishirini na moja kutoka tarehe ya kupokea, Bodi itashughulikia mapendekezo hayo na inaweza: (a) kukubali mapendekezo kamayalivyo wasilishwa na Kamati; (b) kukubali mapendekezo pamoja na maboresho; au (c) kurejesha mapendekezo kwenye Kamati na maelekezo kuwa yaangaliwe upya; Rufaa - 19 Verify source ↗
Rufaa
AI-assisted research summary: A person dissatisfied with a decision of the Board under regulation 18 may appeal to the Baraza within 21 days from the date of the decision.
19. Mtu yeyote hujaridhika na uamuzi wa Bodi chini ya kanuni ya 18 anaweza, ndani ya siku ishirini na moja kutoka tarehe ya uamuzi, kukata rufaa kw Baraza. SEHEMU YA TATU MASHARTI YA JUMLA Uteuzi wa wajumbe wa Jopo la Mapitio
Part
SEHEMU YA TATU
- 20 Verify source ↗
Uteuzi wa wajumbe wa Jopo la Mapitio
AI-assisted research summary: The Board must appoint Review Panel members from among Authority staff, including specified qualified members.
20.-(1) Bodi itateua wajumbe wa Jopo la Mapitio kutoka miongoni mwa watumishi wa Mamlaka kama ifuatavyo: 7 Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati Na Maji Tangazo La Serikali Na. 599 (Linaendelea) (a) watu wawili wenye uzoefu katika sheria kwa muda usiopungua miaka kumi; na (b) watu wawili ambao ni wahitimu wa chuo kikuu katika kinachotambulika, wenye masuala ya udhibiti na angalau uzoefu wa miaka kumi katika nyanja ya uchumi, fedha, uhandisi au utawala. uzoefu (2) Bodi sharti iteue wajumbe hao wa jopo kwa kipindi cha miaka mitatu kwa maelezo na masharti ambayo Bodi yataona yanafaa na kama yatakavyo ainishwa katika Sheria ndogo za Jopo la Mapitio na Kamati ya Ndani ya Mapitio. Kuzuia mwenendo wa kamati - 21 Verify source ↗
Kuzuia mwenendo wa Kamati
AI-assisted research summary: Mtu yeyote asizuiE mwenendo wa Kamati; anayefanya hivyo anaweza kupatikana na hatia na kupewa faini isiyozidi shilingi milioni tatu au kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote.
21. Mtu yeyote ambaae atazuia mwenendo wa Kamati atatenda kos ana akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiozidi shilingi milioni tatu au kifungo kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu au vyote. Kuweka wazi mgongano wa maslahi - 22 Verify source ↗
Kuweka wazi mgongano wa maslahi
AI-assisted research summary: Kamati member with a conflict of interest must disclose it to the Committee and step aside from discussing and deciding that matter.
22. Mjumbe wa Kamati ambaye ana mgongano wa maslahi ama mwenyewe, mwenza wake au mtoto wake, katika suala lolote linalojadiliwa na Kamati, ataweka wazi maslahi hayo kwa Kamati na kujitoa katika kujadilina kuamua suala hilo. 8 Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati Na Maji Tangazo La Serikali Na. 599 (Linaendelea) ______ JEDWALI ________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(4)) FOMU YA MAOMBI YA MAPITIO (1) Maelezo ya Mleta maombi: Jina: _________________________________________________________ Anuani: ____________________________________________ Anuani ya Makazi: _________________________________________ Mji:_______________________________________________________ Simu: ______________________________________________________ Simu yaMkononi: ____________________________________________ Anuaniya Barua Pepe:________________________________________ (2) Maelezo ya Mjibu maombi: Jina:______________________________________________________ Anuani: __________________________________________________ Anuani ya Makazi___________________________________________ Mji: __________________________________________________ Namba ya Simu ya Ofisi: _______________________________________ Simu yaMkononi: ____________________________________________ Anuaniya Barua Pepe: ______________________________________ (3) Maelezo ya uamuzi unaoombewa mapitio ( ambatanisha nakala ya uamuzi ): ___________________________________________________________________________ ___________________________________________________________________________ ___________________________________________________________________________ ______________________________________________________ (4) Hoja za mapitio: ___________________________________________________________________________ ___________________________________________________________________________ ___________________________________________________________________________ ______________________________________________________ (5) Nafuu zinazo ombwa : ___________________________________________________________________________ ___________________________________________________________________________ ___________________________________________________________________________ ______________________________________________________(6) Maelezo mengine yeyote muhimu kwenye maombi haya: ___________________________________________________________________________ ___________________________________________________________________________ ______ (7) Nathibitisha kwamba maelezo yote yaliyotolewa kwenye malalamiko haya ni kweli tupu kwa ufahamu wangu. ___________________ Saini ya Muombaji/Ofisa Mkuu wa Muombaji 9 Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati Na Maji Tangazo La Serikali Na. 599 (Linaendelea) Tarehe______________________________________ Siku Mwezi Mwaka Kwa Matumizi ya Mamlaka tu: Tarehe Faili:____________________________ Iliyopokelewa:___________________Namba ya Dodoma ……….………., 2023 JAMES A. MWAINYEKULE Mkurugenzi Mkuu 10
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Mwenendo wa Mapitio ya Ndani za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji za Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in