Tanzania Regulation

Parliament of Tanzania

Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji wa Kijamii za mwaka 2023

These regulations are titled the Electronic Communications and Posts Regulations for supervising social broadcasting services, 2023. Kanuni hizi zinatumika kwa huduma za utangazaji za jamii Tanzan…

advertising time limitsbroadcast content compliancebroadcastingbroadcasting compliancecommunity broadcastingcommunity mediacontent restrictionscontent retentionlanguage requirementBusiness registrationmedia operationsoperating revenuereligious sensitivityservice operationssponsorshiptafsiri za istilahitechnical infrastructure compliancetechnical standardstelevision stationuendeshaji wa kituo cha utangazaji wa jamii

Publicly available, excluded from search-engine indexing

This page remains available for direct research for the following reasons:

  • The record does not meet this release's canonical indexing criteria. (market-indexing-disabled)
  • The record does not meet this release's canonical indexing criteria. (emergency-noindex)

Professional statute overview

Enactment structure, operative effect and source provenance

Official source

01

Purpose and legislative effect

“These regulations are titled the Electronic Communications and Posts Regulations for supervising social broadcasting services, 2023.”

These regulations are titled the Electronic Communications and Posts Regulations for supervising social broadcasting services, 2023. Kanuni hizi zinatumika kwa huduma za utangazaji za jamii Tanzania Bara, na zinalenga kutoa miongozo kwa waombaji wa leseni na wamiliki kuhusu kuanzisha, kusimamia, na kuendesha huduma hizo. Sehemu hii inaweka maana za maneno muhimu yanayotumika katika Kanuni hizi, ikiwemo huduma za utangazaji za jamii, jamii, Mamlaka, matangazo ya jamii, maudhui, mtoa huduma ya maudhui ya kijamii na Sheria. A community broadcasting station must serve its local community on a non-commercial basis and cannot be run for religious or political purposes. Kituo cha utangazaji wa jamii lazima kiendeshwe na makundi yanayoruhusiwa, na waombaji wa leseni lazima wawasilishe tamko lililosainiwa la kuzingatia Kanuni hizi.

02

How the instrument operates

  1. 01

    Start with the recorded version

    Legal dates not recorded. The date shown identifies this source expression and should not be treated as proof that no later change exists.

  2. 02

    Locate the controlling provision

    Use the provision map, part headings and full-text filter to move from the broad subject to the exact legal language.

  3. 03

    Read conditions and exceptions together

    Keep subsections, definitions, provisos and cross-references in context before drawing a legal conclusion.

  4. 04

    Verify currency and official wording

    Confirm later legislation, commencement notices and corrections with the official publisher before advice, filing or reliance.

03

Research entry points

Selected provisions across the instrument. Open any row to continue with the exact stored text.

Jina

These regulations are titled the Electronic Communications and Posts Regulations for supervising social broadcasting services, 2023.

Section 1

Vyanzo vya mapato

Kituo cha huduma ya utangazaji cha jamii lazima kisipate mapato kutoka kwa biashara yoyote, na mapato ya uendeshaji yake yanaelezwa kutoka kwenye michango, misaada, matangazo ya kijamii, washirika wa maendeleo walioidhinishwa, na udhamini wa Serikali au…

Section 7

Maudhui yanayokatazwa

Kituo cha huduma ya utangazaji cha jamii hakiruhusiwi kutangaza vipindi vyenye maudhui yaliyokatazwa.

Section 10

Kituo cha televisheni

Kituo cha televisheni cha jamii kinaweza kujenga studio kwa kufuata viwango vya kiufundi vilivyoidhinishwa na Mamlaka, na lazima kitumie mbeba maudhui (MUX) wa eneo husika na kuingia naye makubaliano ya huduma.

Section 13

04

Source and current-law status

Source record view

Source record from oagmis.oag.go.tz · Legal dates not recorded

Verify current force

The source record does not state a definitive current-law status. Check the official publisher and later amendments before relying on this text.

Source-indexed provision map

Sections and provisions

Search by section, heading, part or exact legal wording. Every result remains linked to the stored source record.

Showing 13 of 13 provisions

Provision 13
§ 1JinaProvision

These regulations are titled the Electronic Communications and Posts Regulations for supervising social broadcasting services, 2023.

1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji wa Kijamii za mwaka 2023. Matumizi
§ 2MatumiziProvision

Kanuni hizi zinatumika kwa huduma za utangazaji za jamii Tanzania Bara, na zinalenga kutoa miongozo kwa waombaji wa leseni na wamiliki kuhusu kuanzisha, kusimamia, na kuendesha huduma hizo.

2.-(1) Kanuni hizi zitatumika katika huduma za utangazaji za jamii Tanzania Bara. (2) Malengo ya Kanuni hizi yatakuwa kuweka 2 Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii Tangazo La Serikali Na. 598 (Linaendelea) miongozo kwa- (a) waombaji wa leseni wanaotaka kuanzisha huduma za utangazaji za jamii; na (b) wamiliki wa namna leseni watakavyosimamia na kuendesha huduma za utangazaji za jamii. kuhusu Tafsiri
§ 3TafsiriProvision

Sehemu hii inaweka maana za maneno muhimu yanayotumika katika Kanuni hizi, ikiwemo huduma za utangazaji za jamii, jamii, Mamlaka, matangazo ya jamii, maudhui, mtoa huduma ya maudhui ya kijamii na Sheria.

3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- "huduma za utangazaji za jamii" maana yake ni huduma za maudhui ya utangazaji yanayotolewa bila kipato kwenye jamii husika. "jamii" maana yake ni kundi la watu wanaoishi katika eneo moja la kijiografia na yenye sifa za kipekee au maslahi ya pamoja; Sura ya 172 "Mamlaka" maana yake ni Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania; "matangazo ya jamii" maana yake ni matangazo madogo yasiyokuwa na sura ya kibiashara yenye lengo la kuchangia gharama za uendeshaji wa kituo cha utangazaji wa jamii; "maudhui" maana yake ni taarifa kwa namna ya hotuba au sauti, data, maandishi au picha mnato au jongefu, isipokuwa pale ambapo taarifa hiyo inarushwa kwa ajili ya mawasiliano binafsi; "mtoa huduma ya maudhui ya kijamii" maana yake ni chombo kilichoidhinishwa kutoa huduma za utangazaji kwa njia ya redio au televisheni katika jamii fulani, chombo kinamilikiwa na jamii hiyo na kutoa huduma kwa msingi usio wa kibiashara; na "Sheria" maana yake ni Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta. 3 Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii Tangazo La Serikali Na. 598 (Linaendelea) SEHEMU YA PILI UENDESHAJI WA KITUO CHA HUDUMA ZA UTANGAZAJI WA JAMII Misingi ya kituo cha huduma za utangazaji wa jamii

Part

SEHEMU YA PILI

§ 4Misingi ya kituo cha huduma za utangazaji wa jamiiProvision

A community broadcasting station must serve its local community on a non-commercial basis and cannot be run for religious or political purposes.

4. Kituo cha huduma za utangazaji wa jamii kitakuwa na misingi ifuatayo- (a) vipindi vitakuwa mahsusi kwa ajili ya wanajamii wa jamii husika kwa madhumuni yasiyokuwa ya kibiashara; (b) kitakusudia kutoa huduma katika eneo husika au jamii yenye maslahi, mienendo na utamaduni unaofanana; (c) kitatoa fursa kwa wanajamii wa jamii husika kuwasiliana na kushiriki katika uandaaji wa vipindi vya kituo cha utangazaji; (d) kitahudumia jamii iliyokusudiwa; (e) kitawajibika kwa jamii husika; (f) kitamilikiwa, kusimamiwa na kuendeshwa na jamii husika; (g) hakitaendeshwa kwa madhumuni ya kibiashara; (h) hakitaanzishwa au kuendeshwa kwa misingi ya kidini au kisiasa; (i) muundo na uendeshaji wake utazingatia muundo wa uongozi wa jamii husika; na (j) vipindi vitalenga mahitaji ya elimu, maendeleo, jamii na utamaduni wa jamii husika. Umiliki wa kituo cha huduma ya utangazaji wa jamii
§ 5Umiliki wa kituo cha huduma ya utangazaji wa jamiiProvision

Kituo cha utangazaji wa jamii lazima kiendeshwe na makundi yanayoruhusiwa, na waombaji wa leseni lazima wawasilishe tamko lililosainiwa la kuzingatia Kanuni hizi.

5.- (1) Umiliki na uendeshaji wa kituo cha utangazaji wa jamii utakuwa kupitia- (a) taasisi za elimu ya juu na taasisi nyingine za elimu; (b) mamlaka za serikali za mtaa; (c) chama cha kijamii, bodi ya udhamini au mifuko ya kijamii; (d) mashirika yasiyo ya kiserikali; na (e) jamii nyingine yeyote kama Mamlaka itakavyoona 4 Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii Tangazo La Serikali Na. 598 (Linaendelea) inafaa. Majukumu ya kituo cha huduma za utangazaji za kijamii (2) Kwa kuzingatia kanuni ya 5(1)(a) hadi (e) kituo cha huduma ya utangazaji wa jamii hakitaruhusiwa kumilikiwa na kuendeshwa na wafuatao- (a) vyama vya kisiasa; (b) watu binafsi; (c) taasisi za kidini; (d) mashirika ya kibiashara; na (e) makundi mengine yeyote ambayo hayajihusishi na maslahi ya jamii. (3) Waombaji wa leseni ya huduma za utangazaji wa jamii watawasilisha azimio lililosainiwa na wawakilishi wa jamii husika likiahidi kutii Kanuni hizi.
§ 6Majukumu ya kituo cha huduma za utangazaji za kijamiiProvision

Kituo cha huduma za utangazaji za kijamii kina majukumu kadhaa ya kutoa huduma ya utangazaji wa jamii na kuendeleza maendeleo, uelewa, utawala bora, utamaduni na mshikamano wa jamii.

6. Kituo cha huduma za utangazaji za kijamii kitakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kutoa huduma ya utangazaji ya jamii katika eneo husika la kijiografia; (b) kukuza vipaji na utengenezaji wa maudhui ya ndani; (c) kuhamasisha jamii kushiriki kwenye shughuli za maendeleo; (d) kujengeana uwezo kupitia kubadilishana taarifa ndani ya jamii husika; (e) kuhamasisha utawala bora katika jamii husika; (f) kuchochea ukuaji wa maendeleo ya kijamii kwa kutengeneza vipindi vyenye maudhui yanayokidhi mahitaji ya elimu, afya, uchumi, biashara, maendeleo, mazingira, sayansi na utamaduni kwa kushirikisha jamii husika; (g) kuhamasishana juu ya uelewa wa masuala mbalimbali ili kukabiliana na changamoto kwenye jamii husika; (h) kusaidia kufikia muafaka na kuendeleza malengo ya pamoja kupitia midahalo na majadiliano ya masuala ya kijamii; 5 Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii Tangazo La Serikali Na. 598 (Linaendelea) (i) kukuza utamaduni wa sanaa na ubunifu wa jamii husika; na (j) kuhamasisha amani, umoja, ulinzi na usalama, mshikamano, utulivu na utaifa. Vyanzo vya mapato
§ 7Vyanzo vya mapatoProvision

Kituo cha huduma ya utangazaji cha jamii lazima kisipate mapato kutoka kwa biashara yoyote, na mapato ya uendeshaji yake yanaelezwa kutoka kwenye michango, misaada, matangazo ya kijamii, washirika wa maendeleo walioidhinishwa, na udhamini wa Serikali au mashirika yasiyo ya kibiashara.

7.-(1) Vyanzo vya mapato vya kituo cha huduma ya utangazaji cha jamii yatakayotumika kwa ajili ya gharama za uendeshaji wa kituo cha utangazajivitakuwa kama ifuatavyo- (a) fedha zitokanazo na michango, misaada, matangazo ya kijamii, na vyanzo vinginevyo vya kihisani; (b) fedha kutoka kwa washirika mbalimbali wa maendeleo walioidhinishwa na mamlaka husika; na (c) udhamini wa Serikali au mashirika yasiyo ya kibiashara. (2) Kituo cha huduma ya utangazaji cha jamii hakiruhusiwi kuwa na chanzo chamapato kinachotokana na biashara yoyote. SEHEMU YA TATU MAUDHUI YA KITUO CHA UTANGAZAJI CHA JAMII Maudhui ya vipindi

Part

SEHEMU YA TATU

§ 8Maudhui ya vipindiProvision

Kituo cha utangazaji cha jamii lazima kizingatie maudhui yanayoakisi mahitaji ya jamii, kuhakikisha angalau 80% ya maudhui yanahusisha kituo kilipoanzishwa, kutumia Kiswahili isipokuwa kwa kibali maalum cha Mamlaka, na kuhifadhi maudhui ya vipindi kwa miezi mitatu kuanzia siku ya kurushwa.

8. Maudhui ya kituo cha utangazaji chaijamii yatazingatia yafuatayo: (a) kuakisi mahitaji muhimu na malengo ya jamii katika kuhamasisha maendeleo, afya, elimu, mazingira, ustawi wa jamii, maendeleo ya jamii, uchumi, sayansi, teknolojia na utamaduni; (b) maudhui yanayotangazwa na kituo yanapaswa asilimia themanini (80%) za jamii katika eneo kuwa vipindi vinavyoshirikisha kituo kilipoanzishwa; angalau (c) kutumia lugha ya taifa ya Kiswahili isipokuwa pale Mamlaka itakapotoa kibali maalum; na (d) kutunza maudhui ya vipindi vinavyotangazwa kwa 6 Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii Tangazo La Serikali Na. 598 (Linaendelea) miezi mitatu kuanzia siku ya urushaji wa vipindi husika. Maudhui ya matangazo
§ 9Maudhui ya matangazoProvision

Matangazo ya kijamii yanapaswa kuhusiana na eneo husika na huduma za maendeleo; wadhamini wa vipindi hawapaswi kuingilia uendeshaji wa kituo, maudhui, au namna vipindi vinavyoendeshwa; na matangazo ya kijamii pamoja na udhamini hayapaswi kuzidi dakika tano kwa saa, kwa kuzingatia masharti ya kanuni hii.

9. Matangazo na udhamini vitazingatia yafuatayo- (a) matangazo ya kijamii yatahusu eneo husika na huduma za maendeleo; (b) wadhamini wa vipindi hawatakiwi kuingilia uendeshaji wa kituo, maudhui na namna vipindi vinavyoendeshwa; (c) kwa kuzingatia masharti ya kanuni hii, urushaji wa matangazo ya kijamii na udhamini hautazidi dakika tano kwa saa. Maudhui yanayokatazwa
§ 10Maudhui yanayokatazwaProvision

Kituo cha huduma ya utangazaji cha jamii hakiruhusiwi kutangaza vipindi vyenye maudhui yaliyokatazwa.

10. Kituo cha huduma ya utangazaji cha jamii hakiruhusiwi kutangaza vipindi vyenye maudhui yafuatayo: (a) yasiyo na staha na yenye kukosa uadilifu kwa mujibu wa mila na desturi za jamii husika; (b) yanayochochea ubaguzi au kushambulia imani za kidini, itikadi za kisiasa, jamii, kabila, ishara au kuleta madhara yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani katika jamii; (c) yanayohamasisha vitendo vya ngono, ponografia, udhalilishaji, kashfa, uongo, udanganyifu au upotoshaji; (d) yanayotweza shughuli na mienendo ya serikali, bunge na mahakama; (e) yanayochochea ponografia ya watoto. Vipindi vya dini jamii
Section 10Verify source
§ 11Vipindi vya diniProvision

Kituo cha huduma ya utangazaji lazima kiwe makini kuhusu vipindi vya dini na kuepuka masuala yanayoweza kuudhi dini au kufanya kosa kuhusu imani za kikundi fulani.

11. Kituo cha huduma ya utangazaji cha kitahakikisha kwamba kinakua makini kuhusu vipindi vya dini na kuepuka yafuatayo: (a) masuala nyeti yanayoweza kuibua hisia hasi za kidini; na (b) kufanya kosa juu ya maoni ya dini na imani kwa walio katika dini au dhehebu fulani. 7 Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii Tangazo La Serikali Na. 598 (Linaendelea) SEHEMU YA NNE VIGEZO VYA KIUFUNDI Kituo cha redio Kituo cha televisheni
Section 11Verify source

Part

SEHEMU YA NNE

§ 12Kituo cha redioProvision

Community radio stations may build technical broadcasting infrastructure if it is approved by the Authority, and must broadcast in line with Service Quality Regulations and any other regulations approved by the Authority.

12. Kituo cha redio ya jamii- (a) kitaruhusiwa kujenga miundombinu ya utangazaji kiufundi kwa vilivyoidhinishwa na Mamlaka; na kuzingatia viwango vya (b) kitarusha matangazo kwa kuzingatia Kanuni za Ubora wa Huduma na kanuni nyinginezo kama zitakavyokuwa zimeidhinishwa na Mamlaka.
Section 12Verify source
§ 13Kituo cha televisheniProvision

Kituo cha televisheni cha jamii kinaweza kujenga studio kwa kufuata viwango vya kiufundi vilivyoidhinishwa na Mamlaka, na lazima kitumie mbeba maudhui (MUX) wa eneo husika na kuingia naye makubaliano ya huduma.

13. Kituo cha televisheni cha jamii- (a) kitaruhusiwa kujenga studio ya kuandaa na kurusha matangazo kwa kuzingatia viwango vya kiufundi vilivyoidhinishwa na Mamlaka; (b) kitarusha maudhui yake kupitia kwa mbeba maudhui (MUX) aliye katika eneo la kijiografia la jamii husika; na (c) kitaingia makubaliano ya huduma na mbeba maudhui kwa ajili ya usambazaji wa matangazo. Dar es Salaam, JABIRI K. BAKARI ................., 202 Mkurugenzi Mkuu 8
Section 13Verify source

Legislative relationships

0 referenced instruments

Names are derived from the stored provision headings and citation-enrichment layer. Treat this as a research index and verify each relationship against the source text.

No structured legislative relationships were detected

The statute remains fully searchable by provision. Consult the source text for amendments and cross-references that have not yet been indexed.

Recorded versions and source checkpoint

1 version available in this collection

Current-law checkpoint
  • Undated version · currentSwahili

Source-linked research

Ask AI about this statute

The overview, provisions, and source records above are public. Continue in a separate conversation with this statute’s jurisdiction and source version attached.

About this LexChat collection

Statute information is organised from identified legislative sources for professional research. Corrections can be reported to hello@esheria.ai.