Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Usajili wa Laini za Simu za Mwaka 2025
This provision names the regulations as the Electronic Communications and Postal Services (Mobile Line Registration) Regulations, 2025.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Usajili wa Laini za Simu za Mwaka 2025
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision names the regulations as the Electronic Communications and Postal Services (Mobile Line Registration) Regulations, 2025. These regulations apply to all mobile phone users and all telecommunications service providers in the United Republic, except users of lines issued or registered outside the country that operate in Tanzania through local networks. This section defines terms used in the regulations on SIM card registration. Watu wanaomiliki, kudhibiti, au kutumia laini za simu lazima wazisajili kibayometriki, wafiche PIN zao, na waarifu mtoa huduma kuhusu mabadiliko ya matumizi; wauzaji au wasambazaji wa laini pia lazima wasajili laini za wateja na kuweka rekodi. Watoa huduma lazima wahakikishe mifumo yao ya usajili imeunganishwa na mamlaka husika na inafanya kazi muda wote. Mtoa huduma lazima asajili laini za simu za wateja na atume SMS ya uthibitisho/taarifa baada ya usajili au baada ya ufutaji, ubadilishaji, au uhuishaji wa usajili.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Usajili wa Laini za Simu za Mwaka 2025
Showing 38 of 38
- 1
AI-assisted research summary: This provision names the regulations as the Electronic Communications and Postal Services (Mobile Line Registration) Regulations, 2025.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Usajili wa Laini za Simu za Mwaka 2025. - 2
AI-assisted research summary: These regulations apply to all mobile phone users and all telecommunications service providers in the United Republic, except users of lines issued or registered outside the country that operate in Tanzania through local networks.
2.-(1) Kanuni hizi zitatumika kwa watumiaji wote wa laini za simu na watoa huduma wote wa mawasiliano ya simu katika Jamhuri ya Muungano. (2) Bila kuathiri ujumla wa kanuni ndogo ya (1), Kanuni hizi hazitatumika kwa watumiaji wa laini za simu zilizotolewa au kusajiliwa nje ya nchi ambazo zinafanya kazi nchini kupitia mitandao ya simu ya watoa huduma wa ndani. - 3 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: This section defines terms used in the regulations on SIM card registration.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “aina za usajili wa laini za simu kibayometriki” inajumuisha kampuni, mwanadiplomasia, mtu binafsi, taasisi, mgeni, mtoto, mkimbizi, mgeni wa muda mfupi au aina nyingine yoyote kama itakavyoamuliwa na Mamlaka mara kwa mara; “Idara ya Uhamiaji” maana yake ni Idara ya Uhamiaji iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Tanzania Uhamiaji; 4 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) “kuhuisha matumizi ya laini ya simu” maana yake ni kuifanya laini ya simu iweze kufanya kazi katika mtandao wa simu; “kundi la laini za simu” maana yake ni laini za simu zaidi ya moja zilizosajiliwa kwa pamoja kwa ajili ya mawasiliano ya kielektroniki na kwa kutumia kitambulisho cha taifa na alama za vidole za mwakilishi mmoja pasipo laini za ziada; “laini ya simu” maana yake ni moduli ya utambulisho wa mteja inayojitegemea ni iliyowashwa kielektroniki iliyoundwa kwa ajili ya matumizi pamoja na simu ya mkononi ili kumwezesha mtumiaji kutuma na kupokea mawasiliano ya kielektroniki; ambayo kadi Sura ya 172 Sura ya 356 “laini ya simu hai” maana yake ni laini ya simu inayofanya kazi katika mtandao wa simu; “kifaa cha mawasiliano ya simu” maana yake ni kifaa kinachotumika kwa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ikijumuisha vifaa vinavyotumia huduma za mtandao katika mitandao ya simu; “Mamlaka” maana yake ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania iliyoanzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania; “mawasiliano ya mashine kwa mashine” maana yake ni mawasiliano ya moja kwa moja kati ya vifaa ili kubadilishana taarifa na kufanya vitendo bila uingiliaji wa mwanadamu; “mwanadiplomasia” maana yake ni mtu ambaye yuko kwenye kazi ya kidiplomasia katika Jamhuri ya Muungano kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Kinga na Haki za Kidiplomasia na Kibalozi; “mgeni” maana yake ni mtu asiye raia wa Jamhuri ya Muungano au mwanadiplomasia anayetarajia kukaa katika Jamhuri ya Muungano kwa kipindi cha zaidi ya miezi minne; “mgeni wa muda mfupi” maana yake ni mtu asiye raia ambaye si mwanadiplomasia na anatarajia kukaa katika Jamhuri ya Muungano kwa muda usiozidi miezi minne; 5 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) Sura ya 37 Sura ya 306 “mkataba wa huduma” maana yake ni makubaliano yaliyoingiwa kati ya mtoa huduma na mteja kwa ajili ya utoaji wa huduma zilizotolewa leseni kwa wateja; mkimbizi” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa chini ya Sheria ya Wakimbizi; “mlezi” maana yake ni mtu ambaye ana wajibu, udhibiti au usimamizi kwa mtoto au mtu aliyeteuliwa kwa hati, wosia au amri ya mahakama aliyepewa jukumu la kutunza na kusimamia mali na haki za mtoto; “mteja” maana yake ni mtu yeyote anayepata au aliyeomba kupata huduma ya aina yoyote kutoka kwa mtu anayefanya kazi kwa mujibu wa Kanuni hizi na inajumuisha wateja wa kampuni za simu; “mtoa huduma” maana yake ni mtu aliyepewa leseni na Mamlaka ya kutoa na kuwezesha utoaji wa huduma za mawasiliano ya kielektroniki; “mtoto” maana yake ni mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi na nane na zaidi ya miaka kumi na mbili; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta; “taasisi” maana yake ni serikali au taasisi isiyo ya kiserikali iliyosajiliwa na inayofanya kazi ndani ya Jamhuri ya Muungano; “taasisi ya kidiplomasia” maana yake ni taasisi ya kimataifa yenye vibali vya kidiplomasia kwa Jamhuri ya Muungano; “nambari tambulishi” maana yake ni msimbo wa kipekee unaotumika kutambua simu binafsi katika mtandao wa mifumo ya mawasiliano ya simu ya kimataifa; na “PIN” maana yake ni nambari pekee inayotumika kufungua na kufunga laini ya simu. 6 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) SEHEMU YA PILI USAJILI WA LAINI ZA SIMU Wajibu wa kusajili laini ya simu
Part
SEHEMU YA PILI
- 4
AI-assisted research summary: Watu wanaomiliki, kudhibiti, au kutumia laini za simu lazima wazisajili kibayometriki, wafiche PIN zao, na waarifu mtoa huduma kuhusu mabadiliko ya matumizi; wauzaji au wasambazaji wa laini pia lazima wasajili laini za wateja na kuweka rekodi. Watoa huduma lazima wahakikishe mifumo yao ya usajili imeunganishwa na mamlaka husika na inafanya kazi muda wote.
4.-(1) Mtu yeyote anayemiliki, anayedhibiti au anayekusudia kutumia inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu- laini ya simu (a) atasajili kibayometriki laini ya simu inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu kwa mtoa huduma husika kwa namna iliyoainishwa katika Kanuni hizi; (b) atahakikisha PIN ya laini yake ya simu haijulikani na mtu mwingine yeyote; na (c) atamtaarifu mtoa huduma wake kuhusu mabadiliko ya mtumiaji au matumizi ya kila laini ya simu anayoimiliki. (2) Mtu yeyote ambaye anauza au kwa namna nyingine yoyote anatoa inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu kwa mteja yeyote- laini ya simu (a) atasajili laini za simu za wateja kwa kutumia taratibu kama zilivyoainishwa katika Kanuni hizi; na (b) atatunza kumbukumbu za taarifa ya usajili wa laini za simu katika kanzidata kama zitakavyochukuliwa kielektroniki kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa au Idara ya Uhamiaji. (3) Kila mtoa huduma atahakikisha kuwa- (a) mfumo wake wa usajili umeunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, unafanya kazi na unapatikana muda wote; (b) mfumo wake wa usajili umeunganishwana mfumo wa Idara ya Uhamiaji, unafanya kazi na unapatikana muda wote; 7 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) (c) mfumo wake wa usajili umeunganishwa na kanzidata kuu ya usajili wa laini za simu ya Mamlaka, unafanya kazi na unapatikana muda wote; au Idara laini ya (d) taarifa za usajili wa simu zilizohakikiwa na Mamlaka ya Vitambulisho ya Uhamiaji vya Taifa zinawasilishwa moja kwa moja kwenye kanzidata kuu ya usajili wa laini za simu ya Mamlaka wakati wa mchakato wa usajili; na (e) ubadilishaji wa laini ya simu iliyoharibika unafanyika baada ya kuhakiki kibayometriki usajili na umiliki wa awali wa mhusika. (4) Mtu hatasajili laini yoyote ya simu kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha mtu mwingine isipokuwa kama ilivyoainishwa katika Kanuni hizi. Wajibu wa mtoa huduma Usajili wa laini ya simu kwa mtu binafsi - 5
AI-assisted research summary: Mtoa huduma lazima asajili laini za simu za wateja na atume SMS ya uthibitisho/taarifa baada ya usajili au baada ya ufutaji, ubadilishaji, au uhuishaji wa usajili.
5.-(1) Mtoa huduma atahakikisha anasajili laini za simu kwa wateja kwa mujibu wa masharti yaliyoainishwa katika Kanuni hizi. (2) Baada ya kukamilisha usajili wa laini ya simu, mtoa huduma atatuma ujumbe mfupi wa maneno kwenye laini zote zilizosajiliwa na mteja ukionesha orodha ya laini zote za simu zilizosajiliwa kwa kutumia kitambulisho cha mteja. (3) Baada ya ufutaji, ubadilishaji au uhuishaji wa usajili wa laini ya simu, mtoa huduma atatuma taarifa ya ujumbe mfupi wa maneno kwenye laini za simu za mteja zilizosajiliwa na orodha kamili ya laini za simu zilizosajiliwa na mteja. - 6
AI-assisted research summary: Usajili wa laini ya simu ya mtu binafsi lazima ufanywe kibayometriki kwa kutumia kitambulisho cha taifa na alama za vidole.
6. Usajili wa laini ya simu kwa mtu binafsi utafanyika kibayometriki kwa namna ifuatayo: (a) mtu binafsi atawasilisha kwa mtoa huduma taifa au namba ya kitambulisho cha kitambulisho cha taifa; (b) mtoa huduma atafanya usajili wa laini ya simu kwa kuhakiki alama za vidole kupitia mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; 8 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) kielektroniki (c) mtoa huduma atatunza taarifa za mteja kama kutoka zilivyochukuliwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; na (d) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa na jina la mtu binafsi kama linavyosomeka katika mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa. - 7
AI-assisted research summary: Kampuni inapotaka kusajili laini ya simu, usajili hufanywa kibayometriki na mwakilishi wa kampuni na mtoa huduma huhakiki alama za vidole.
7. Usajili laini ya simu kwa kampuni utafanyika kibayometriki kwa namna ifuatayo: nakala (a) mwakilishi wa kampuni atawasilisha barua ya utambulisho, halali kilichothibitishwa chenye Namba ya Mlipa Kodi, leseni ya biashara na cheti cha usajili wa kampuni au cheti cha utekelezaji wa kazi husika; cheti ya Usajili wa laini ya simu kwa kampuni (b) mwakilishi wa atawasilisha kitambulisho chake cha taifa au namba ya kitambulisho cha taifa kwa mtoa huduma; kampuni (c) mtoa huduma atasajili laini ya simu kibayometriki kwa kuhakiki alama za vidole za mwakilishi wa kampuni mara moja kupitia mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; (d) mtoa huduma atatunza taarifa za kampuni na za mwakilishi wa kampuni; (e) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa kwa jina la kampuni; na (f) endapo mwakilishi aliyetumika kusajili laini ya simu ya kampuni kibayometriki atakoma kuwa mwakilishi wa kampuni, kampuni itawasilisha maombi kwa mtoa huduma kufuta taarifa za mwakilishi wa awali. Usajili wa laini ya simu kwa mfanyakazi wa kampuni - 8
AI-assisted research summary: Usajili wa laini ya simu ya mfanyakazi wa kampuni lazima ufanywe kibayometriki, kwa kuhusisha kampuni, mfanyakazi, na mtoa huduma.
8. Usajili wa laini ya simu kwa mfanyakazi wa kampuni, utafanyika kibayometriki kwa namna ifuatayo: (a) kampuni itawasilisha barua ya utambulisho, nakala ya cheti halali kilichothibitishwa chenye Namba ya Mlipa Kodi, leseni ya 9 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) biashara na cheti cha usajili au cheti cha utekelezaji wa kazi husika; (b) mfanyakazi wa kampuni atakayetumia laini ya simu husika atatakiwa kuwasilisha kwa mtoa huduma kitambulisho chake cha taifa au namba ya kitambulisho cha taifa; (c) mtoa huduma atafanya usajili wa laini ya simu kibayometriki kwa kuhakiki alama za vidole za mfanyakazi wa kampuni kupitia mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; (d) mtoa huduma atatunza taarifa za mfanyakazi na kampuni; (e) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa kwa jina la mfanyakazi; na (f) endapo mfanyakazi ambaye laini ya simu ya kampuni ilisajiliwa kibiometriki kwa jina lake, atakoma kuwa mfanyakazi wa kampuni laini hiyo, kampuni hiyo, au kutumia itawasilisha maombi kwa mtoa huduma kufuta taarifa za mfanyakazi huyo. Usajili wa laini ya simu kwa taasisi - 9
AI-assisted research summary: Taasisi inayosajili laini ya simu lazima itumie usajili wa kibayometriki: mwakilishi wake awasilishe barua ya utambulisho na kitambulisho cha Taifa/Namba ya Kitambulisho cha Taifa, mtoa huduma ahakiki alama za vidole na kuhifadhi taarifa, na laini isajiliwe kwa jina la taasisi.
9. Usajili wa laini ya simu kwa taasisi, utafanyika chini ya usajili wa laini ya simu kibayometriki kwa namna ifuatayo: (a) mwakilishi wa taasisi atawasilisha barua ya utambulisho kutoka katika taasisi husika; (b) mwakilishi wa taasisi atawasilisha kwa mtoa huduma kitambulisho cha Taifa au Namba ya Kitambulisho cha Taifa; (c) mtoa huduma atasajili simu kibayometriki kwa kuhakiki alama za vidole za mwakilishi wa taasisi mara moja kupitia mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; laini ya (d) mtoa huduma atatunza taarifa za taasisi na mwakilishi wa taasisi; (e) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa kwa jina la taasisi; na 10 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) Utaratibu wa usajili wa laini za simu kwa wafanyakazi wa taasisi (f) endapo mwakilishi aliyetumika kusajili laini ya simu ya taasisi kibayometriki amekoma kuwa mwakilishi wa taasisi itawasilisha maombi kwa mtoa huduma kufuta taarifa za mwakilishi wa awali. taasisi, - 10
AI-assisted research summary: Laini za simu za wafanyakazi wa taasisi lazima zisajiliwe kibayometriki, na taasisi, mfanyakazi, na mtoa huduma wote wana hatua maalum za kutekeleza.
10. Usajili wa laini ya simu kwa wafanyakazi wa taasisi, utafanyika kibayometriki kwa namna ifuatayo: (a) taasisi itawasilisha barua ya utambulisho kutoka katika taasisi husika na Namba ya Mlipa Kodi ya taasisi; (b) mfanyakazi wa taasisi atakayetumia laini ya simu husika atatakiwa kuwasilisha kwa mtoa huduma kitambulisho chake cha taifa au namba ya kitambulisho cha taifa; (c) mtoa huduma atafanya usajili wa laini ya simu kibayometriki kwa kuhakiki alama za vidole za taasisi kupitia mfumo wa mfanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; (d) mtoa huduma atatunza taarifa za mfanyakazi na taasisi; (e) laini ya simu iliyosajiliwa kwa mujibu wa kanuni hii itakuwa kwa jina la mfanyakazi; na (f) endapo mfanyakazi ambaye laini ya simu ya taasisi ilisajiliwa kibayometriki kwa jina lake, atakoma kuwa mfanyakazi wa taasisi hiyo, au kutumia laini hiyo, taasisi itawasilisha maombi kwa mtoa huduma kufuta taarifa za mfanyakazi huyo. Usajili wa laini ya simu kwa mtoto - 11
AI-assisted research summary: Laini ya simu ya mtoto inasajiliwa kwa utaratibu wa kibayometriki, kwa nyaraka maalum za mzazi au mlezi na mtoto, na lazima isajiliwe upya mtoto anapofikia utu uzima.
11. Usajili wa laini ya simu kwa mtoto, utafanyika kibayometriki kwa namna ifuatayo: (a) mzazi au mlezi atawasilisha picha ya mtoto (i) husika pamoja na mojawapo kati ya- nakala iliyothibitishwa ya cheti cha kuzaliwa cha mtoto au cheti cha kuasiliwa mtoto; au hati ya kusafiria ya mtoto. (ii) 11 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) (b) mtoto ambaye ni mzawa au mgeni, mzazi au mlezi wake atawasilisha kwa mtoa huduma kitambulisho cha taifa na mtoa huduma simu atafanya kibayometriki kwa kuhakiki alama za vidole za mzazi au mlezi kupitia mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; usajili wa laini ya (c) mtoto ambaye ni mgeni wa muda mfupi, mzazi au mlezi wake atawasilisha kwa mtoa huduma hati ya kusafiria, na mtoa huduma simu atafanya kibayometriki kwa kuhakiki alama za vidole za mzazi au mlezi kupitia mfumo wa Idara ya Uhamiaji; usajili wa laini ya (d) mtoto ambaye ni mwanadiplomasia, mzazi au mlezi wake atawasilisha hati halali ya kidiplomasia cha kidiplomasia kwa ajili ya usajili wa laini ya simu; kitambulisho na (e) mtoto ambaye ni mkimbizi, mzazi au mlezi wake atawasilisha kwa mtoa huduma kitambulisho cha ukimbizi kilichotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, na mtoa huduma atafanya usajili wa laini ya simu kibayometriki kwa ajili ya uhakiki; (f) mtoa huduma atatunza taarifa za mtoto na mzazi au mlezi kwa njia ya kielektroniki; (g) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa kwa jina la mtoto; (h) baada ya kufikia umri wa utu uzima, mtoto atasajili upya laini ya simu kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hizi; (i) mtoa huduma atamtaarifu mtoto miezi mitatu kabla ya kufikia umri wa utu uzima na atampa muda wa nyongeza wa miezi mitatu kwa ajili ya kusajili upya laini ya simu baada ya kufikia umri wa utu uzima; na (j) endapo mtoto atashindwa kusajili upya laini ya simu ndani ya muda wa miezi mitatu baada 12 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) ya kufikia umri wa utu uzima, mtoa huduma atasitisha matumizi ya laini ya simu husika. Usajili wa laini ya simu kwa mgeni wa muda mfupi - 12
AI-assisted research summary: Laini ya simu ya mgeni wa muda mfupi lazima isajiliwe kwa utaratibu wa uthibitishaji unaotegemea Idara ya Uhamiaji, na mtoa huduma anatakiwa kuhifadhi taarifa zinazohusika.
12.-(1) Usajili wa laini ya simu kwa mgeni wa muda mfupi, utafanyika kibayometriki kwa namna ifuatayo: (a) mgeni wa muda mfupi atawasilisha nakala ya nyaraka za kusafiria; (b) mtoa huduma atafanya usajili wa laini ya simu kibayometriki kwa kuhakiki alama za vidole za mgeni wa muda mfupi kupitia mfumo wa Idara ya Uhamiaji; (c) mtoa huduma atatunza taarifa za mgeni wa muda mfupi; (d) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa na jina la mgeni wa muda mfupi; (e) laini ya simu itakuwa hai kwa kipindi ambacho mgeni wa muda mfupi ameruhusiwa kukaa nchini; na (f) mtoa huduma atahuisha muda wa uhai wa laini ya simu iliyosajiliwa na mgeni wa muda mfupi baada ya kuhakiki uhuishwaji wa taarifa za mgeni kupitia Idara ya Uhamiaji. (2) Endapo taarifa za kibayometriki au ya hati ya kusafiria hazipo katika kanzidata ya uhamiaji au kanzidata ya uhamiaji haipatikani, laini ya simu itasajiliwa kwa namna ifuatayo: (a) mgeni wa muda mfupi ataruhusiwa kusajili laini moja tu; (b) mteja atawasilisha hati ya kusafiria kwa ajili ya usajili wa laini ya simu; (c) alama za vidole hazitachukuliwa wakati wa usajili wa laini ya simu; (d) mtoa huduma atatunza nakala ya hati ya kusafiria; (e) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa hai kwa muda ambao mgeni wa muda mfupi ameruhusiwa kukaa nchini; 13 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) (f) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa kwa jina la mgeni wa muda mfupi; na (g) mtoa huduma atatunza taarifa za usajili na kuziwasilisha kwa Mamlaka kwa wakati. Usajili wa laini ya simu kwa mgeni - 13
AI-assisted research summary: A foreigner’s SIM registration must use biometric verification, the foreigner must present a National ID Authority card, and the provider must keep the foreigner’s information.
13. Usajili wa laini ya simu kwa mgeni utafanyika kibayometriki kwa namna ifuatayo: (a) mgeni atawasilisha kitambulisho alichopewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; (b) mtoa huduma atasajili simu kibayometriki kwa kuhakiki alama za vidole kupitia mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; laini ya (c) mtoa huduma atatunza taarifa za mgeni; (d) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa kwa jina la mgeni; na (e) laini ya simu itakuwa hai kwa kipindi ambacho mgeni ameruhusiwa kukaa nchini. - 14
AI-assisted research summary: SIM registration for a refugee must be done biometrically, using the refugee’s ID and fingerprint verification.
14. Usajili wa laini ya simu kwa mkimbizi utafanyika kibayometriki kwa namna ifuatayo: (a) mkimbizi atawasilisha kitambulisho alichopewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; Usajili wa laini ya simu kwa mkimbizi (b) mtoa huduma atasajili simu kibayometriki kwa kuhakiki alama za vidole za mkimbizi kupitia mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; laini ya (c) mtoa huduma atatunza taarifa za mkimbizi na; (d) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa kwa jina la mkimbizi. Usajili wa laini ya simu kwa mwanadiplomasia - 15 Verify source ↗
Wajibu wa kusajili laini ya simu
AI-assisted research summary: Mwanadiplomasia lazima alete pasipoti halali na kitambulisho cha kidiplomasia, na mtoa huduma asajili laini bila kuchukua alama za vidole.
15. Usajili wa laini ya simu kwa mwanadiplomasia utafanyika kwa namna ifuatayo: (a) mwanadiplomasia atawasilisha hati yake halali ya kusafiria na utambulisho halali wa kidiplomasia: (b) mtoa huduma atafanya usajili wa laini ya simu bila kuchukua alama za vidole; 14 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) Usajili wa laini ya simu kwa taasisi ya kidiplomasia Usajili wa laini ya simu itakayotumika kwenye kifaa cha kielektriniki au mashine (c) mtoa huduma atatunza taarifa za mwanadiplomasia; na (d) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa kwa jina la mwanadiplomasia. - 16
AI-assisted research summary: Laini ya simu ya taasisi ya kidiplomasia husajiliwa kwa utaratibu maalum: taasisi na mwakilishi wake wanatoa nyaraka zinazohitajika, na mtoa huduma anasajili bila kuchukua alama za vidole.
16. Usajili wa laini ya simu kwa taasisi ya kidiplomasia utafanyika kwa namna ifuatayo: (a) taasisi ya kidiplomasia itawasilisha barua za utambulisho kutoka kwenye taasisi husika na Wizara yenye dhamana na masuala ya mambo ya nje; (b) mwakilishi wa taasisi ya kidiplomasia atawasilisha hati halali ya kusafiria na kitambulisho halali cha kidiplomasia kwa ajili ya usajili wa laini ya simu; (c) mtoa huduma atafanya usajili wa laini ya simu bila kuchukua alama za vidole; (d) mtoa huduma atatunza taarifa ya taasisi ya kidiplomasia na za mwakilishi; na (e) laini ya simu iliyosajiliwa itakuwa kwa jina la taasisi ya kidiplomasia. - 17
AI-assisted research summary: Laini za simu za mashine au vifaa vingine vya mawasiliano ya kielektroniki zinasajiliwa kibayometriki; kwa kundi la laini za kampuni au taasisi, mtoa huduma hufanya usajili kwa kuhakiki alama za vidole za mwakilishi kupitia mfumo wa NIDA.
17. Usajili wa laini ya simu kwa matumizi ya mashine au kifaa kingine cha mawasiliano cha kielektroniki utafanyika kibayometriki kwa namna ifuatayo: (a) endapo mashine au kifaa kingine cha mawasiliano cha kielektroniki kinamilikiwa na mtu binafsi, usajili wa laini ya simu utafanyika kama ilivyoainishwa katika kanuni ya 6; kwa mtu binafsi (b) endapo mashine au kifaa kingine cha mawasiliano cha kielektroniki kinamilikiwa na kampuni au taasisi, usajili wa laini ya simu utafanyika kama ilivyoainishwa katika kanuni ya 7 au ya 9; na (c) endapo kundi la laini za simu zitahitajika kusajiliwa kwa ajili ya kampuni au taasisi, mtoa huduma atafanya usajili wa kundi la 15 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) Usajili wa laini ya simu kwa watumiaji wenye kasoro kwenye vidole au wasio na vidole laini za simu kibayometriki kwa kuhakiki alama za vidole za mwakilishi wa kampuni au taasisi mara moja kupitia mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa. - 18
AI-assisted research summary: For SIM registration involving a customer without fingerprints or with fingerprint defects, the customer and provider must follow a verification process with the National Identification Authority before registration can proceed without fingerprints.
18.-(1) Usajili wa laini ya simu kwa mteja asiye na vidole au mwenye kasoro katika alama za vidole utafanyika kwa namna ifuatayo: (a) mteja atatembelea Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuhuisha taarifa za kasoro za alama za vidole kwenye kanzidata; (b) mteja atawasilisha kitambulisho chake cha taifa au Namba ya Utambulisho wa taifa kwa ajili ya usajili wa laini ya simu; (c) mtoa huduma atawasilisha kwa Mamlaka ya Vitambulisho ya vya Taifa utambulisho wa mteja kwa uhakiki wa usajili wa laini ya simu kielektroniki; namba (d) baada ya kupokea maombi kwa ajili ya uhakiki, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa itatoa maswali mbalimbali yasiyo na mpangilio moja kwa moja kwa mteja kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zake kabla ya kukamilika kwa mchakato wa usajili; (e) mtoa huduma atamuuliza maswali mteja kama alivyopokea kutoka kwenye kanzidata ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; (f) endapo mteja atajibu angalau maswali matatu kati ya matano kwa usahihi, uhakiki utakuwa umefaulu na usajili utafanyika bila kutumia alama za vidole. (2) Mtoa huduma atatunza kumbukumbu zilizohakikiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa. (3) Endapo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa itaweka utaratibu mwingine wa uhakiki kwa wateja wenye kasoro za alama za vidole, Mamlaka itatoa utaratibu mwingine wa uhakiki kama itakavyoona inafaa. 16 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) Usajili wa laini ya simu kwa baadhi ya watu - 19
AI-assisted research summary: Kwa mgeni wa muda mfupi mwenye zaidi ya miaka 65 au mwenye tatizo la alama za vidole, usajili wa laini ya simu hufanywa kwa njia ya uthibitisho wa pasipoti na maswali ya uhakiki badala ya alama za vidole.
19.-(1) Usajili wa laini ya simu endapo mteja ni mgeni wa muda mfupi na ana umri zaidi ya miaka sitini na tano, ana kasoro katika alama za vidole, hana vidole au ameingia kupitia mipaka ambayo haina vifaa vya kibayometriki utafanyika kwa namna ifuatayo: (a) Idara ya Uhamiaji itaweka kanzidata maalumu kwa ajili ya wageni wa muda mfupi wenye umri zaidi ya miaka sitini na tano, walio na kasoro katika alama za vidole, wasiokuwa na vidole au walioingia kupitia mipaka isiyokuwa na vifaa vya usajili wa kibayometriki; (b) mteja atawasilisha hati yake ya kusafiria kwa ajili ya usajili wa laini za simu; (c) mtoa huduma atawasilisha kielektroniki kwa Idara ya Uhamiaji, namba ya hati ya kusafiria ya mteja kwa ajili ya uhakiki wakati wa usajili wa laini ya simu; (d) baada ya kupokea maombi kwa ajili ya uhakiki, Idara ya Uhamiaji itatoa maswali mbalimbali yasiyo na mpangilio moja kwa moja kwa mteja kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zake kabla ya kukamilika mchakato wa usajili; (e) mtoa huduma atatumia chaguo la maswali mengi kumhakiki mteja na atauliza maswali kama kwenye kutoka alivyoyapokea kanzidata ya Idara ya Uhamiaji; na (f) endapo mteja atajibu angalau maswali matatu kati ya matano kwa usahihi, uhakiki utakuwa umefaulu na mtoa huduma atafanya usajili wa laini ya simu bila kutumia alama za vidole. (2) Mtoa huduma atatunza kumbukumbu zilizohakikiwa na Idara ya Uhamiaji. (3) Endapo Idara ya Uhamiaji itaweka utaratibu mwingine wa uhakiki kwa wateja wenye kasoro za alama za vidole, Mamlaka itatoa utaratibu mwingine wa uhakiki kama itakavyoona inafaa. 17 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) Utaratibu wa kusajili upya laini ya simu Zuio la kusajili laini kwa matumizi ya mtu mwingine - 20
AI-assisted research summary: Mteja ambaye jina lake limesajiliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akibadili jina, anatakiwa kupeleka taarifa za mabadiliko hayo kwa Mamlaka hiyo.
20. Endapo mteja ambaye jina lake limesajiliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, amebadili jina, mteja huyu atatuma taarifa za mabadiliko hayo kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na utaratibu wa kusajili upya laini ya simu utakuwa kama ulivyoainishwa chini ya Kanuni hizi. - 21
AI-assisted research summary: Mtu hatakiwi kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine, au kuruhusu laini yake itumike na mtu mwingine, isipokuwa kama Kanuni hizi zinaruhusu.
21.-(1) Mtu hatatumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa kitambulisho cha mtu mwingine au kuruhusu laini ya simu iliyosajiliwa kwa kitambulisho chake itumiwe na mtu mwingine isipokuwa kwa mujibu wa Kanuni hizi. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kanuni ndogo (1), anatenda kosa, na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu (3) au kifungo cha muda usiopungua miezi sita au vyote. Haki ya kusajili laini ya simu bila uthibitisho wa kibayometriki - 22
AI-assisted research summary: Mteja wa taasisi ya Serikali au wakala aliyeidhinishwa na Serikali anayehitaji msamaha wa usajili wa laini ya simu kwa njia ya kibayometriki lazima aandike barua kwa Mamlaka, alete kitambulisho cha taifa au namba yake pamoja na kibali cha Mamlaka kwa mtoa huduma, na mtoa huduma asajili laini hiyo kwa idhini ya Mamlaka.
22. Mteja kutoka taasisi ya Serikali au wakala aliyeidhinishwa na Serikali ambaye anahitaji msamaha wa usajili wa laini ya simu kwa njia ya kibayometriki atatumia utaratibu ufuatao: (a) ataandika barua kwa Mamlaka ili kupata kibali cha msamaha wa usajili wa laini ya simu kwa njia ya kibayometriki; (b) atawasilisha kitambulisho chake cha taifa au Namba ya kitambulisho cha taifa na kibali cha Mamlaka kwa mtoa huduma kwa ajili ya usajili wa laini ya simu; na (c) mtoa huduma atasajili laini ya simu kwa idhini ya Mamlaka. Taarifa ya ziada - 23
AI-assisted research summary: A person selling, registering, or otherwise providing certain mobile or communication devices may ask a customer for extra information about SIM registration.
23. Mtu yeyote anayeuza, kusajili au kwa namna nyingine yoyote anatoa inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu anaweza kuomba taarifa ya ziada kutoka kwa mteja inayohusiana na usajili wa laini ya simu. laini ya simu SEHEMU YA TATU KUHUISHA NA KUSITISHA MATUMIZI YA LAINI ZA SIMU 18 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) Kuhuisha matumizi ya laini za simu
Part
SEHEMU YA TATU
- 24
AI-assisted research summary: Mtoa huduma hapaswi kuhuisha matumizi ya laini ya simu isipokuwa usajili umefanywa; pia lazima ahakikishe PIN, chaguo la kuwasha/kuzima PIN, na elimu kwa wateja.
24.-(1) Mtoa huduma hatahuisha matumizi ya laini ya simu inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu kwenye mfumo wake wa mawasiliano ya kielektroniki isipokuwa kama usajili wa laini ya simu umefanyika kwa mujibu wa Kanuni hizi. (2) Usajili wa laini ya simu yoyote inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu ambao haujahakikiwa kupitia kanzidata ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Idara ya Uhamiaji au kama ilivyoainishwa katika Kanuni hizi, utakuwa batili. (3) Laini ya simu iliyosajiliwa kwa ajili ya mgeni wa muda mfupi itakuwa hai kwa muda ambao mgeni ameidhinishwa kukaa nchini. (4) Mtoa huduma atahakikisha kuwa- (a) laini yoyote ya simu ambayo ni mpya, inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu inakuwa na PIN; (b) PIN ya laini ya simu imezimwa wakati wa usajili wa laini ya simu; (c) wateja wamewekewa chaguo la kuwasha au kuzima PIN kwa ajili ya usalama wa laini ya simu; (d) elimu na ushauri kuhusu umuhimu na namna ya kutumia PIN kwenye laini ya simu inatolewa kwa wateja. Uhuishaji wa matumizi ya PIN ya kufungua na kufunga laini ya simu - 25
AI-assisted research summary: Mtoa huduma lazima amwambie mteja kuhusu PIN ya laini wakati wa usajili, na mteja akikosea PIN mara tano mfululizo laini itasitishwa hadi aombe kuhuishwa.
25.-(1) Uhuishaji wa matumizi ya PIN ya laini ya simu kwenye simu za mkononi utakuwa kwa namna ifuatayo: (a) mtoa huduma atamfahamisha mteja wakati wa usajili wa laini ya simu kwamba laini za simu zimewezeshwa PIN na kumshauri mteja kutumia PIN kwa usalama wake binafsi; 19 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) (b) baada ya kuweka laini ya simu kwenye simu ya mkononi, ujumbe mfupi utapokelewa moja kwa moja na taarifa kuhusu utaratibu wa kuwezesha, kubadilisha na kuzima PIN; na (c) endapo PIN ya laini ya simu imehuishwa, itatakiwa kufanya kazi wakati wote simu itakapowashwa au kuzimwa. (2) Endapo mteja ataweka PIN kwenye laini ya simu kwa kukosea mara tano mfululizo, laini ya simu itasitishwa matumizi na mteja atatakiwa kumuomba mtoa huduma kuhuisha laini ya simu husika. Uzimaji wa laini za simu zisizotumika laini ya simu - 26
AI-assisted research summary: Laini ya simu inaweza kusitishwa baada ya siku 90 za kutotumika, lakini mtoa huduma asisitishe ikiwa mteja ametoa taarifa ya maandishi ya kutotumia kwa hadi miezi 12 au kama laini imeripotiwa kuhusika na uhalifu ambao bado unaendelea kuchunguzwa.
26.-(1) Endapo inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu haijatumika katika mawasiliano kwa muda wa siku tisini mfululizo, laini hiyo ya simu itasitishwa kutumika. (2) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (1), mtoa huduma hatasitisha matumizi ya laini ya simu inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu iwapo- (a) mteja ametoa taarifa kwa maandishi kuwa laini hiyo ya simu haitatumika kwa kipindi cha mfululizo cha miezi isiyozidi kumi na miwili; au (b) laini ya simu husika imeripotiwa kuhusika katika uhalifu, na uchunguzi wa uhalifu huo bado haujakamilika. (3) Mteja ambaye laini yake ya simu inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu kimesitishwa matumizi anaweza kuwasilisha maombi mapya ya usajili ili kupata namba yake ya awali ikiwa bado ipo. (4) Endapo mteja atafariki, ndani ya siku tisini baada ya kifo- 20 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) (a) mume, mke, ndugu au jamaa wa karibu atatoa taarifa ya kifo hicho kwa mtoa huduma husika; (b) msimamizi wa mirathi ndani ya kipindi cha miezi sita atawasilisha taarifa za mtu atakayerithi laini ya simu na mtoa huduma hatasitisha matumizi ya laini hiyo na mrithi huyo atatakiwa kufuata taratibu zote za usajili wa laini ya simu; (c) endapo hakuna mrithi wa laini ya simu, msimamizi wa mirathi atarudisha laini hiyo ya simu kwa mtoa huduma husika kabla ya kuisha kwa kipindi cha miezi sita. Utaratibu kwa ajili ya mizani au bakaa ya fedha Sura ya 437 - 27
AI-assisted research summary: Mtoa huduma lazima aweke utaratibu wa kushughulikia salio la fedha lililopo kwenye laini ya simu inayoweza kuondolewa katika simu au kifaa cha mawasiliano, ikiwa matumizi ya laini hiyo yamehuishwa chini ya Sheria ya Mfumo wa Malipo wa Taifa.
27. Mtoa huduma ataweka utaratibu wa kushughulikia salio la fedha lililopo katika laini ya simu inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu ambacho kimehuishwa matumizi yake kwa mujibu wa Sheria ya Mfumo wa Malipo wa Taifa. Uwasilishaji wa maelezo ya uzimaji wa laini za simu kwa Mamlaka - 28 Verify source ↗
Usajili wa laini ya simu kwa taasisi za kidiplomasia
AI-assisted research summary: Mtoa huduma lazima awasilishe kwa Mamlaka taarifa za laini za simu zilizoainishwa, kwa wakati na katika muundo utakaoamuliwa na Mamlaka.
28. Mtoa huduma atawasilisha kwa Mamlaka taarifa za laini za simu zinazoweza kuondolewa, zilizojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano cha simu kinachotumia laini za simu ambazo zimesitishwa matumizi yake kwa wakati na katika muundo utakaoamuliwa na Mamlaka. SEHEMU YA NNE UBADILISHAJI WA TAARIFA AU UMILIKI Ubadilishaji wa taarifa na umiliki
Part
SEHEMU YA NNE
- 29
AI-assisted research summary: Maombi ya kubadilisha umiliki wa laini ya simu huwasilishwa kwa mtoa huduma, ambaye lazima aombe ridhaa ya mmiliki wa awali.
29.-(1) Maombi ya kubadilisha umiliki wa laini ya simu yatawasilishwa kwa mtoa huduma, ambapo mtoa huduma atatafuta ridhaa ya mabadiliko hayo kutoka kwa mmiliki wa awali. (2) Mmiliki wa awali anaweza kuridhia au kukataa maombi ya kubadilisha umiliki wa laini ya simu yaliyowasilishwa kwa mtoa huduma. 21 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) (3) Endapo mmiliki wa awali ataridhia, mtoa huduma atasajili laini ya simu kwa njia ya kibayometriki na kuhifadhi taarifa za mmiliki wa awali na mmiliki mpya. Jukumu la kutoa taarifa ya kupotea kwa laini ya simu - 30
AI-assisted research summary: Mteja anapopoteza au kuibiwa laini ya simu, lazima aripoti polisi na apate taarifa au ripoti ya awali ndani ya siku 7; pia anapohitaji ubadilishaji wa laini, atoe kitambulisho cha Taifa, namba ya utambulisho wa Taifa, au pasipoti kwa mtoa huduma.
30. Mteja wa inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu atalazimika- laini ya simu (a) kutoa taarifa ya kupotea au kuibiwa kwa laini ya simu inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu katika kituo cha polisi na kupata taarifa ya kupotea kwa laini ya simu husika au ripoti ya uchunguzi wa awali ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya kupotea au kuibiwa kwa laini hiyo ya simu; (b) kuwasilisha kitambulisho cha Taifa, namba ya utambulisho cha Taifa au hati ya kusafiria kwa mtoa huduma wake wakati atakapohitaji inayoweza kubadilisha kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi cha mawasiliano au kinachotumia laini ya simu. laini ya kifaa simu Ubadilishaji wa laini ya simu - 31
AI-assisted research summary: Mtoa huduma lazima abadilishe laini ya simu iliyopotea, iliyoibiwa au iliyoharibika baada ya kuthibitisha umiliki, na mteja akabidhi laini/kipengele kilichoharibika kabla ya kubadilishwa.
31.-(1) Mtoa huduma atabadilisha laini ya simu iliyopotea, iliyoibiwa au iliyoharibika baada ya uhakiki wa umiliki wake. (2) Mteja atakabidhi laini ya simu inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya mkononi au kifaa cha mawasiliano kinachotumia laini ya simu ambayo imeharibika, kabla ya kuibadilisha. (3) Mtoa huduma atahakikisha kuwa laini ya simu iliyotajwa katika kanuni ndogo ya (2) inatunzwa kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na miwili. Kubadili taarifa kwenye simu - 32 Verify source ↗
Ubadilishaji wa taarifa na umiliki
AI-assisted research summary: Mtoa huduma lazima ahakikishe laini zote zilizobadilishwa zimehakikiwa kibayometriki au kwa njia iliyoainishwa, na pia atoe na kuhifadhi taarifa fulani kwa Mamlaka.
32.-(1) Mtoa huduma atahakikisha kuwa laini za simu zote zilizobadilishwa zimehakikiwa kibayometriki 22 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) au zimehakikiwa kwa namna iliyoainishwa katika Kanuni hizi. (2) Bila kujali kanuni ndogo ya (1), mtoa huduma- (a) atawasilisha kwa Mamlaka taratibu zake za kubadili laini ya simu; (b) atahifadhi taarifa za usajili wa laini ya simu zilizobadilishwa; laini au ya simu (c) atatunza inayoweza kuondolewa, iliyojengwa ndani ya simu ya cha mawasiliano kifaa mkononi kinachotumia laini ya simu iliyoharibika; (d) atarekodi na kuhifadhi taarifa za mtu yeyote mwenye uwezo wa kuingilia na kutumia kanzidata inayotunza uhamishaji wa taarifa kwenye laini mpya; na (e) atatunza taarifa zote alizozipata chini ya kanuni hii kwenye kanzidata itakayofikika kwa urahisi kwa kipindi cha miezi kumi na miwili. SEHEMU YA TANO MASHARTI YA JUMLA Uwasilishaji wa taarifa za usajili Kuzuia udanganyifu
Part
SEHEMU YA TANO
- 33
AI-assisted research summary: Mtoa huduma lazima ahakikishe usajili wa laini za simu unafanyika kwa mujibu wa sheria na Kanuni hizi, na awasilishe taarifa ya usajili kwa Mamlaka mara tu baada ya usajili kukamilika.
33. -(1) Mtoa huduma atahakikisha usajili wa laini za simu unafanyika kwa mujibu wa sheria na Kanuni hizi. (2) Mtoa huduma atawasilisha kwa Mamlaka taarifa ya usajili wa laini za simu, papo kwa papo mara baada ya kukamilisha usajili. - 34
AI-assisted research summary: Watoa huduma wote lazima wachukue hatua kadhaa kudhibiti udanganyifu wakati wa usajili wa laini za simu.
34. Watoa huduma wote watadhibiti vitendo vya udanganyifu wakati wa usajili wa laini za simu kwa kuzingatia yafuatayo: (a) kutekeleza taratibu za ndani za kudhibiti vitendo vya udanganyifu wakati wa usajili wa laini za simu; 23 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) (b) kusitisha matumizi ya laini zote za simu ambazo zimebainika kuwa zimesajiliwa kwa udanganyifu; (c) kushirikiana pale inapowezekana, kuzuia vitendo vya udanganyifu au vitendo ambavyo havijaidhinishwa wakati wa usajili wa laini za simu na kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahusika wa vitendo vya udanganyifu; (d) kuhakikisha ulinzi na usiri wa taarifa kwa kufuata sheria husika zinazotumika pamoja na sheria nyingine za makampuni na biashara; (e) kufidia waathirika wa upotevu wowote wa pesa na mali utakaotokana na vitendo vya udanganyifu unaohusiana na usajili wa laini za simu ambapo mtoa huduma alishindwa kumtambua mhusika aliyefanya udanganyifu; (f) kuweka zuio la kuendelea kutumika katika simu, namba za usajili wa kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria iliyotumika kusajili laini ya simu ambayo imebainika katika kitendo cha udanganyifu; (g) kuweka zuio la kuendelea kutumika kwa tambulishi za vifaa vyote vya namba kielektroni ambavyo na mawasiliano vimebainika kutumika katika vitendo vya udanganyifu; laini za (h) kuwasilisha kwa Mamlaka, taarifa zote za namba ya kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria, namba ya laini ya simu na namba tambulishi ya kifaa ambazo zimefungiwa kwa ajili ya kuwataarifu watoa huduma wengine ili waweze kuzizuia kutumika katika mitandao yao; na (i) kutekeleza utaratibu mwingine wowote kama utakavyoidhinishwa na Mamlaka. Ukomo wa umiliki wa idadi za laini za simu - 35
AI-assisted research summary: Kanuni hii inaweka kikomo cha idadi ya laini za simu mtu binafsi, kampuni au taasisi inaweza kusajili au kumiliki, na inakataza kutumia laini iliyosajiliwa kwa madhumuni tofauti na yaliyoombwa.
35.-(1) Mtu anayekusudia kumiliki na kutumia laini ya simu inayoweza kutolewa, laini ya simu 24 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) iliyojengewa ndani cha mawasiliano kilichowezeshwa na laini ya simu ataruhusiwa kusajili- au kifaa (a) ikiwa ni mtu binafsi- (i) laini ya simu moja pekee kwa kila mtandao wa simu kwa ajili ya matumizi ya sauti, ujumbe mfupi na huduma za kimtandao; na laini za simu zisizozidi tano kwa kila mtandao wa simu kwa ajili ya matumizi ya mawasiliano ya mashine kwa mashine; na (b) ikiwa ni kampuni au taasisi, atasajili- (ii) (i) (ii) laini za simu zisizozidi mia moja kwa kila mtandao wa simu kwa ajili ya matumizi ya sauti, ujumbe mfupi na huduma za mtandao; na laini za simu zisizozidi mia mbili kutoka kwa kila mtandao wa simu kwa ajili ya matumizi ya mawasiliano ya mashine kwa mashine. (2) Laini ya simu iliyosajiliwa chini ya kanuni ndogo ya (1) haitatumika kwa matumizi tofauti na yaliyokusudiwa wakati wa usajili. (3) Bila kujali kanuni ndogo ya (1), mtu binafsi, kampuni au taasisi inaweza kuruhusiwa na mtoa huduma wake kusajili au kumiliki zaidi ya idadi ya laini za simu zilizoainishwa baada ya mtoa huduma kuhakiki na kujiridhisha matumizi sahihi ya laini hizo za ziada kwa kuzingatia masharti ya Kanuni hizi. (4) Mamlaka inaweza kuweka ukomo wa laini za ziada kwa aina ya usajili. (5) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (3), mtu binafsi, kampuni au taasisi itawasilisha kwa mtoa huduma wake sababu za msingi kwa kila ombi la laini za simu za ziada. (6) Mtu ambaye anakiuka kanuni hii anatenda kosa chini ya Sehemu ndogo (b) ya Sehemu ya IV ya Sheria. 25 Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu Tangazo la Serikali Na.59 (Linaendelea.) Kosa kwa utumiaji mbaya wa taarifa - 36
AI-assisted research summary: Mtoa huduma haruhusiwi kutumia taarifa ya mteja vibaya kwa usajili wa laini ya simu; akipatikana na hatia, anaweza kupewa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo cha angalau miezi kumi na miwili, au vyote viwili.
36. Mtoa huduma atakayetumia taarifa ya mteja vibaya kwa ajili ya usajili wa laini ya simu, anatenda kosa na akitiwa hatiani atalipa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo cha kipindi kisichopungua miezi kumi na miwili au vyote. Adhabu ya jumla - 37 Verify source ↗
Uwasilishaji wa taarifa za usajili
AI-assisted research summary: A person who violates these Regulations commits an offence, and if no specific penalty is provided, is liable on conviction to the penalty specified under the law.
37. Mtu anayekiuka masharti ya Kanuni hizi na iwapo hakuna adhabu mahususi iliyoainishwa, anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kwa adhabu iliyoainishwa chini ya Sheria. Kufutwa TS Na. 60 la 2023 - 38
AI-assisted research summary: Sheria hii inafuta Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Usajili wa laini za Simu za Mwaka 2023.
38. Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Usajili wa laini za Simu za Mwaka 2023 zinafutwa. Dodoma 21 Januari, 2025 JERRY WILLIAM SILAA, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 26
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Usajili wa Laini za Simu za Mwaka 2025
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in