Kanuni za Mabalozi wa Hiari wa Utalii za mwaka 2025
These regulations are titled the Voluntary Tourism Ambassadors Regulations, 2025.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Mabalozi wa Hiari wa Utalii za mwaka 2025
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
These regulations are titled the Voluntary Tourism Ambassadors Regulations, 2025. This section defines key terms used in the regulations, including tourism volunteer ambassador, the Board, the Executive Director, tourist, the Act, the Minister, and the Ministry. Mtu anaweza kuzingatiwa kwa uteuzi kama balozi wa hiari wa utalii ikiwa ana sifa njema, ni mashuhuri, ana mtandao mpana, anaweza kutangaza utalii wa Tanzania, na hana historia ya kosa la jinai. A person who wants to be appointed as a volunteer tourism ambassador must submit an application to the Executive Director in Form No. 1. Mkurugenzi Mtendaji lazima achunguze sifa za mwombaji, awasilishe taarifa na mapendekezo kwa Bodi kwa ridhaa, na akiona maombi hayaridhishi, amjulishe mwombaji ndani ya siku 30 na sababu.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Mabalozi wa Hiari wa Utalii za mwaka 2025
Showing 14 of 14
- 1
AI-assisted research summary: These regulations are titled the Voluntary Tourism Ambassadors Regulations, 2025.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Mabalozi wa Hiari wa Utalii za mwaka 2025. - 2 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the regulations, including tourism volunteer ambassador, the Board, the Executive Director, tourist, the Act, the Minister, and the Ministry.
2. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “balozi wa hiari wa utalii” maana yake ni mtu mashuhuri, mwenye kipaji na ushawishi ambaye ameridhia kujitolea muda wake, kipaji na mapenzi ya kuitangaza Tanzania kama kivutio cha utalii kinachopendelewa zaidi ndani na nje ya Tanzania; “Bodi” maana yake ni Bodi ya Utalii Tanzania iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria; “Mkurugenzi Mtendaji” maana yake ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 6 cha Sheria; “mtalii” maana yake ni mtu ambaye anasafiri kwenda sehemu nje ya eneo lake la makazi ya kawaida kwa muda kati ishirini na nne na mwaka mmoja na ya saa 2 Kanuni za Mabalozi wa Hiari wa Utalii Tangazo la Serikali Na. 77 (Linaendelea) madhumuni ya safari yake ni tofauti na utekelezaji wa shughuli inayompatia kipato kutoka ndani ya sehemu aliyotembelea: Isipokuwa shughuli kwamba, inatekelezwa na mkazi wa Tanzania, mtu huyo atajulikana kama mtalii wa ndani; iwapo “Sheria” maana yake ni Sheria ya Bodi ya Utalii Tanzania; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya masuala ya utalii; na “Wizara” maana yake ni Wizara yenye dhamana ya masuala ya utalii. SEHEMU YA PILI UTEUZI WA BALOZI WA HIARI WA UTALII Sifa za uteuzi
Part
SEHEMU YA PILI
- 3
AI-assisted research summary: Mtu anaweza kuzingatiwa kwa uteuzi kama balozi wa hiari wa utalii ikiwa ana sifa njema, ni mashuhuri, ana mtandao mpana, anaweza kutangaza utalii wa Tanzania, na hana historia ya kosa la jinai.
3. Mtu anaweza kufikiriwa kwa ajili ya uteuzi kama Maombi balozi wa hiari wa utalii ikiwa atakuwa na sifa zifuatazo: (a) ana sifa njema na mwenendo mzuri katika jamii; (b) ni mtu mashuhuri na mwenye utayari wa kutangaza malengo ya utalii wa Tanzania kwa hiari; (c) ana mtandao mpana wa kijamii; (d) ana uwezo wa kushawishi na kutangaza mazao ya utalii, mikakati na shuguli za kitalii za Tanzania; na (e) hana historia ya kutenda kosa la jinai. - 4
AI-assisted research summary: A person who wants to be appointed as a volunteer tourism ambassador must submit an application to the Executive Director in Form No. 1.
4.-(1) Mtu ambaye anakusudia kuteuliwa kuwa balozi wa hiari wa utalii atawasilisha maombi kwa Mkurugenzi Mtendaji katika namna iliyoainishwa kwenye Fomu Na. 1 iliyoainishwa katika Jedwali la Kanuni hizi. (2) Fomu ya maombi iliyojazwa itaambatana na- (a) kitambulisho cha Taifa; (b) cheti cha taaluma katika masuala ya utalii, ikiwa anacho; na (c) barua ya mapendekezo kutoka kwa taasisi au kampuni ya utalii inayotambuliwa na Bodi. Uchakataji wa maombi - 5
AI-assisted research summary: Mkurugenzi Mtendaji lazima achunguze sifa za mwombaji, awasilishe taarifa na mapendekezo kwa Bodi kwa ridhaa, na akiona maombi hayaridhishi, amjulishe mwombaji ndani ya siku 30 na sababu.
5.-(1) Mkurugenzi Mtendaji, baada ya kupokea maombi chini ya Kanuni hizi, atafanya upekuzi juu ya sifa za mwombaji. (2) Upekuzi chini ya kanuni ndogo ya (1) utakuwa kwa madhumuni ya- 3 Kanuni za Mabalozi wa Hiari wa Utalii Tangazo la Serikali Na. 77 (Linaendelea) (a) kujiridhisha na uzoefu wa mwombaji ili kuhakikisha kuwa sifa na utaalamu ana utakaomwezesha kutekeleza majukumu yake chini ya Kanuni hizi; (b) kubainisha utayari wa mwombaji kujitolea kutangaza utalii; na (c) kubainisha masuala mengine yeyote muhimu. (3) Mkurugenzi Mtendaji baada ya kufanya upekuzi juu ya sifa za mwombaji, na baada ya kuridhika ipasavyo, atawasilisha taarifa na mapendekezo yake kwa Bodi kwa ajili ya ridhaa. (4) Endapo Mkurugenzi Mtendaji hataridhika na maombi, atamtaarifu mwombaji ndani ya siku thelathini na kumpa sababu za kutoridhika. Mapendekezo ya uteuzi - 6
AI-assisted research summary: Bodi lazima ichunguze maombi na iamue kuyaidhinisha au kuyaikataa; ikikataa, iwajulishe waombaji sababu za kukataa.
6. Bodi, baada ya kupokea taarifa na mapendekezo kwa mujibu wa kanuni ya 5, Bodi itafanya mapitio ya maombi na kufanya uamuzi wa kuridhia maombi au kukataa maombi kumjulisha mwombaji sababu za kukataliwa kwa maombi. Uteuzi wa balozi wa hiari wa utalii - 7
AI-assisted research summary: Bodi must send the applicant’s name to the Minister for approval, and the Minister may appoint a qualified person as a voluntary tourism ambassador.
7.-(1) Bodi baada ya kuridhia maombi chini ya kanuni ya 6, itawasilisha jina la mwombaji kwa Waziri kwa ajili ya kuidhinishwa. (2) Waziri baada ya kumuidhinisha mwombaji atamteua mtu aliyependekezwa kuwa balozi wa hiari wa utalii na kutoa cheti kwenye Fomu Na. 2 kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kanuni hizi. (3) Bila kujali masharti ya kuwasilisha maombi ya kuteuliwa kuwa balozi wa hiari wa utalii, Waziri anaweza, kwa kushauriana na Bodi, kumteua mtu yeyote mwenye sifa zilizoainishwa chini ya Kanuni hizi kuwa balozi wa hiari wa utalii. Muda wa kuhudumu - 8
AI-assisted research summary: Balozi wa hiari wa utalii anahudumu kwa miaka miwili kuanzia tarehe ya uteuzi, na anaweza kuteuliwa tena.
8. Balozi wa hiari wa utalii atahudumu kwa muda wa miaka miwili kuanzia tarehe ya uteuzi na anaweza kuteuliwa tena. Majukumu ya balozi wa hiari wa utalii - 9 Verify source ↗
10. Masharti ya balozi wa hiari wa utalii
AI-assisted research summary: Balozi wa hiari wa utalii lazima ahamasishe utalii na uwekezaji, atalaze uhifadhi wa rasilimali, aitangaze Tanzania kama kivutio cha utalii, na alinde taswira ya nchi katika masuala ya utalii.
9. Balozi wa hiari wa utalii atakuwa na wajibu na majukumu yafuatayo: (a) kuhamasisha watalii na wawekezaji kutembelea au 4 Kanuni za Mabalozi wa Hiari wa Utalii Tangazo la Serikali Na. 77 (Linaendelea) kuwekeza nchini Tanzania; (b) kuhamasisha uhifadhi wa rasilimali asilia, za kiutamaduni na za kihistoria; (c) kuitangaza Tanzania kama kituo kinachoongoza katika vivutio vya utalii duniani; (d) kulinda taswira ya nchi katika masuala ya utalii. Katazo - 10 Verify source ↗
Masharti ya balozi wa hiari wa utalii
AI-assisted research summary: A person appointed as a voluntary tourism ambassador must not engage in discriminatory, disorderly, fraudulent, misleading, personally beneficial, or conflict-of-interest conduct while carrying out their duties.
10. Mtu aliyeteuliwa kuwa balozi wa hiari wa utalii hatatakiwa, katika utekelezaji wa wajibu na majukumu yake: (a) kujihusisha na vitendo vyovyote vya ubaguzi; (b) kujihusisha matukio yanayosababisha uvunjifu wa amani au uhalifu wa aina yoyote; vitendo au na (c) kujihusisha katika vitendo vinavyochafua taswira ya sekta ya utalii; (d) kujihusisha na vitendo vya udanganyifu, utapeli au upotoshaji; (e) kutumia taarifa na nyenzo za utangazaji alizopata katika utekelezaji wa wajibu na majukumu yake kwa manufaa binafsi; na (f) kujihusisha na biashara ya utalii au shughuli zinazoweza kusababisha mgongano wowote wa maslahi. Kutenguliwa kwa uteuzi - 11 Verify source ↗
Kutengua uteuzi
AI-assisted research summary: Waziri anaweza kutengua uteuzi wa balozi wa hiari wa utalii ikiwa kuna mojawapo ya sababu zilizotajwa katika Kanuni hizi.
11. Waziri anaweza kutengua uteuzi wa balozi wa hiari wa utalii endapo: (a) atashindwa kutekeleza majukumu yake kama ilivyoainishwa katika Kanuni hizi; (b) atapoteza sifa za kuteuliwa kuwa balozi wa hiari wa utalii zilizoainishwa katika Kanuni hizi; (c) atakuwa na mwenendo unaochafua taswira ya sekta ya utalii Tanzania; (d) atatiwa hatiani kwa kosa la jinai; (e) atashindwa kuzingatia masharti yaliyoanishwa katika kanuni ya 10; na (f) kuna jambo linalohusu maslahi ya umma. SEHEMU YA TATU MASHARTI MENGINEYO 5 Kanuni za Mabalozi wa Hiari wa Utalii Tangazo la Serikali Na. 77 (Linaendelea) Rejesta ya mabalozi wa hiari wa utalii wa hiari wa utalii.
Part
SEHEMU YA TATU
- 12
AI-assisted research summary: The Board must prepare and keep a register of voluntary tourist ambassadors.
12.-(1) Bodi itaandaa na kutunza rejesta ya mabalozi Kutambuliwa kwa mabalozi wa hiari wa utalii (2) Rejesta iliyoandaliwa chini ya kanuni ndogo (1) itakuwa na maelezo ya mabalozi wa hiari wa utalii. - 13
AI-assisted research summary: Balozi wa hiari wa utalii anatambuliwa na mamlaka husika, na wadau wa utalii wanapaswa kushirikiana naye; pia anaweza kupewa taarifa, nyenzo za utangazaji, na motisha za safari.
13. Balozi wa hiari wa utalii aliyeteuliwa chini ya Kanuni hizi- (a) atatambuliwa na Wizara, Balozi za Tanzania nje ya nchi na wadau wa utalii ambao watatakiwa kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake; (b) anaweza kupewa taarifa na nyenzo za utangazaji kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi; (c) anaweza kunufaika na motisha za safari zinazoandaliwa na Bodi na wadau wengine wanaotambulika kwenye maeneo yenye vivutio kwa ajili ya kujijengea uelewa. Adhabu - 14 Verify source ↗
Rejista ya mabalozi wa hiari wa utalii
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kujitangaza kuwa balozi wa hiari wa utalii bila kuteuliwa kwa mujibu wa Kanuni hizi.
14. Mtu yeyote atakayejitangaza kuwa balozi wa hiari wa utalii bila kuteuliwa kwa mujibu wa Kanuni hizi atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini ya kiasi kisichozidi shilingi laki sita au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi kumi na mbili. 6 Kanuni za Mabalozi wa Hiari wa Utalii Tangazo la Serikali Na. 77 (Linaendelea) ________ JEDWALI ________ (Imetengenezwa chini ya kanuni 4(1) na 7(2)) TTB Fomu Na. 1 FOMU YA MAOMBI YA UTEUZI WA BALOZI WA HIARI WA UTALII Mimi ……………………………………. wa anuani. …………..….. ninaomba kuteuliwa kuwa balozi wa hiari wa utalii. sifa za kuweza kuteuliwa kuwa balozi wa hiari wa utalii kama Nina ifuatavyo:………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ………………………. ……………………………………………………………………………………………… ……………………… Wadhamini wangu ni: ………………………………………………….. …………………………………………………. …………………………………………………. Ninaahidi kufuata masharti yote yanayohusiana na utendaji wa balozi wa hiari wa utalii. ………………………………….. ……………………… Tarehe Saini ya mwombaji 7 Kanuni za Mabalozi wa Hiari wa Utalii Tangazo la Serikali Na. 77 (Linaendelea) TTB Fomu Na.2 CHETI CHA UTEUZI WA BALOZI WA HIARI WA UTALII Na. ………….. HII ni kuthibitisha kuwa …………………. Ameteuliwa kuwa Balozi wa Hiari wa Utalii. Imetolewa leo tarehe ……..…. mwezi………………… 20……….. ………………….. Tarehe Jina Saini ………………… ………… Waziri wa Maliasili na Utalii Dodoma 3 Februari, 2025 PINDI HAZARA CHANA, Waziri wa Maliasili na Utalii 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Mabalozi wa Hiari wa Utalii za mwaka 2025
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in