Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025
This by-law is named the Dar es Salaam City Council Vehicle Regulation By-Law, 2025.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This by-law is named the Dar es Salaam City Council Vehicle Regulation By-Law, 2025. This bylaw applies throughout the whole area of Dar es Salaam City Council. This section defines key terms used in the by-law, including passenger, fee, authorized officer, vehicle, council, city centre, terminal, parking, heavy goods vehicles, director, station user, and levy. Halmashauri must manage, control, and enforce parking and vehicle movement rules in designated city areas, run a passenger vehicle station, charge fees, identify vehicle owners through registered recognized bodies, and remove illegally parked vehicles. Certain cargo vehicles and similar transport may not enter the city center unless they first get a special permit from the Director; waste vehicles and machinery are also barred from daytime work there unless the Director gives written permission.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025
Showing 17 of 17
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This by-law is named the Dar es Salaam City Council Vehicle Regulation By-Law, 2025.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the whole area of Dar es Salaam City Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including passenger, fee, authorized officer, vehicle, council, city centre, terminal, parking, heavy goods vehicles, director, station user, and levy.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “abiria” maana yake ni mtu yeyote anayesafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine; “ada” maana yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya vibali au leseni mbalimbali zitolewazo na Halmashauri; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chombo cha usafiri” maana yake ni chombo chochote kinachotumika kusafirisha mtu au mizigo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine isipokuwa, wanyama mkokoteni wanaotumika kusafirisha watu au mizigo; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; au 1 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) “katikati ya Jiji” maana yake ni maeneo yote ya Kata za Mchafukoge, Kivukoni, Kisutu, Gerezani, Mchikichini, Kariakoo, Jangwani, Ilala, Upanga Magharibi, Upanga Mashariki, Kipawa, Buguruni, Mnyamani au Vingunguti na maeneo mengine yatakayoidhinishwa na Halmashauri; “kituo cha magari ya abiria” maana yake ni eneo na maalum Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria au mizigo; lililotengwa kujengwa au “maegesho” maana yake ni sehemu yeyote iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha chombo cha usafiri kwa muda; “magari ya mizigo” maana yake ni magari yanayobeba mizigo yenye uzito zaidi ya tani tatu; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam au afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mtumiaji wa kituo” maana yake ni mtu yeyote anayefanya shughuli zake za kila siku ndani ya kituo na ametambuliwa na Halmashauri; na “ushuru” maana yake ni Halmashauri kwa mbalimbali zinazofanywa katika eneo Halmashauri. tozo shughuli inayotozwa na au huduma la Wajibu wa Halmashauri
Part
sehemu yeyote
- 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must manage, control, and enforce parking and vehicle movement rules in designated city areas, run a passenger vehicle station, charge fees, identify vehicle owners through registered recognized bodies, and remove illegally parked vehicles.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kuweka utaratibu wa usimamizi na udhibiti wa vyombo vya usafiri katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya maegesho ya magari; (b) kutenga maeneo ya maegesho kwa kushirikiana na wadau; (c) kuanzisha na kusimamia uendeshaji wa kituo cha magari ya abiria; (d) kusimamia uingiaji na utokaji wa magari na mitambo katikati ya Jiji; (e) kutoza ushuru na ada kwa watumiaji wa kituo cha magari ya abiria na abiria; 2 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) Magari na mitambo kuingia katikati ya Jiji (f) kuwatambua wamiliki wa magari ya abiria kwa mujibu wa vyama au vyombo vilivyosajiliwa na kutambulika; na (g) kuondoa na kuvuta vyombo vya usafiri vilivyoegeshwa maeneo yasiyo rasmi. - 5 Verify source ↗
(1) Magari ya mizigo, kontena, pikipiki ya
AI-assisted research summary: Certain cargo vehicles and similar transport may not enter the city center unless they first get a special permit from the Director; waste vehicles and machinery are also barred from daytime work there unless the Director gives written permission.
5.-(1) Magari ya mizigo, kontena, pikipiki ya magurudumu mawili au matatu, matoroli au maguta hayataruhusiwa kuingia katikati ya Jiji. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), magari ya mizigo, kontena, pikipiki ya magurudumu mawili au matatu yanaweza kuingia katikati ya Jiji baada ya kupata kibali maalum kutoka kwa Mkurugenzi. (3) Kibali cha kuingia katikati ya Jiji kitatolewa baada ya kulipiwa ada na kitajumuisha kupakia na kushusha mzigo. (4) Magari ya taka na mitambo yoyote haitaruhusiwa kuzoa au kukusanya taka au kufanya kazi katikati ya Jiji nyakati za mchana isipokuwa kwa kibali maalumu cha maandishi kutoka kwa Mkurugenzi. Wajibu wa mmiliki wa chombo cha usafiri - 6 Verify source ↗
Mmiliki wa chombo cha usafiri hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Mmiliki wa chombo cha usafiri haruhusiwi kuanzisha kituo cha abiria au kupakia/kushusha abiria au mizigo katika eneo lisilotengwa au lisilotambuliwa kwa kibali cha Halmashauri.
6. Mmiliki wa chombo cha usafiri hataruhusiwa kuanzisha kituo cha magari ya abiria au kushusha au kupakia abiria au mizigo katika eneo ambalo halijatengwa au kutambuliwa kwa kupewa kibali na Halmashauri kwa ajili ya matumiiz kama kituo cha magari ya abiria. Mamlaka ya Afisa Mwidhiniwa - 7 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa ana uwezo wa kuingia eneo lolote ndani ya kituo cha magari ya abiria ili kutoza ushuru na kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii.
7. Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia eneo lolote ndani ya kituo cha magari ya abiria kwa ajili ya kutoza ushuru na kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Usafi wa mazingira - 8 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayetumia kituo cha magari
AI-assisted research summary: Watumiaji wa kituo cha magari ya abiria lazima watunze usafi, wamiliki wa vyombo vya usafiri waweke chombo cha taka na watoe taka mahali palipotengwa, na hakuna biashara inayoruhusiwa ndani ya eneo la maegesho bila idhini ya Halmashauri.
8.-(1) Mtu yeyote anayetumia kituo cha magari ya abiria atapaswa kutunza mazingira kwa kutotupa taka ovyo, kumwaga au kutiririsha maji, kuosha vyombo vya usafiri katika eneo lisilo rasmi isipokuwa katika eneo lililotengwa kwa matumizi hayo. 3 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) Maeneo ya maegesho (2) Kila mmiliki wa chombo cha usafiri atahakikisha kuwa anaweka chombo cha kutunza taka ndani ya chombo cha usafiri na kutupa taka hizo katika maeneo maalumu yaliyotengwa na Halmashauri. (3) Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya biashara kwa kupanga bidhaa chini, kuweka meza za biashara, kuweka vibanda vya biashara, kupika au kufanya biashara ya chakula ndani ya eneo la maegesho bila idhini ya Halmashauri. - 9 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge na kuweka alama maeneo ya maegesho, na watu wanaotaka kuanzisha au kuegesha kwenye baadhi ya maeneo lazima waombe au walipe ushuru kulingana na masharti ya kifungu hiki.
9.-(1) Halmashauri itatenga maeneo ya maegesho kulingana na matumizi ya eneo husika kwa kuainisha maeneo ya umma na binafsi au taasisi. (2) Halmashauri itaweka alama au michoro maalumu itakayoonesha au kuashiria maeneo ya maegesho ya vyombo vya usafiri. (3) Mtu yeyote ambaye anakusudia kuanzisha eneo kwa ajili ya maegesho atatakiwa kuomba kibali kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii kutoka Halmashauri na atawajibika kulipia asilimia kumi ya makusanyo yanayopatikana kila mwezi. (4) Halmashauri inaweza kutoa kibali kwa ajili ya maegesho katika maeneo maalumu kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii endapo mwombaji atalipa ushuru wa maegesho kwa kipindi cha kuanzia wiki moja. (5) Mtu yeyote anaweza kulipia ushuru wa maegesho kwa jumla ya gharama za siku, wiki au mwezi kwa mkupuo na atapewa kibali maalumu kitakachomruhusu kuegesha katika eneo lolote lililotengwa na Halmashauri kwa maegesho bila malipo katika kipindi hicho. (6) Maeneo ya maegesho yatafunguliwa kuanzia saa kumi na moja kamili alfajiri hadi saa kumi na mbili kamili jioni katika maeneo ya kawaida na kuanzia saa moja kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni katika maeneo ya fukwe za bahari. (7) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (6), Halmashauri inaweza kubadili muda wa kufungua 4 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) Uondoaji na uvutaji wa vyombo vya usafiri katika maegesho yasiyo rasmi au kufunga maegesho kulingana na mahitaji au hali halisi ya maeneo hayo. (8) Halmashauri inaweza kufunga maegesho kwa ajili ya matengenezo au sababu nyingine yoyote kadri itakavyoona na itatoa taarifa ya maandishi kwa watumiaji au kuweka matangazo sehemu ya maegesho ya magari ya abiria. (9) Mtu anayekusudia kuegesha chombo cha usafiri katika maegesho ya Halmashauri atapaswa kulipa ushuru wa maegesho kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika sheria ndogo inayosimamia masuala ya ada na ushuru katika Halmashauri. - 10 Verify source ↗
(1) Itakuwa marufuku kuegesha chombo
AI-assisted research summary: Ni marufuku kuegesha chombo cha usafiri mahali pasipotengwa au kwa namna isiyoruhusiwa.
10.-(1) Itakuwa marufuku kuegesha chombo chochote cha usafiri katika maeneo yasiyotengwa kwa ajili ya maegesho au kuegesha kwa namna isiyoruhusiwa. (2) Halmashauri itamchukulia hatua dereva au mtu yeyote atakayeegesha vibaya chombo cha usafiri au kuegesha katika eneo lisiloruhusiwa ikiwa ni pamoja na kufunga mnyororo au kifaa maalum kwenye chombo cha usafiri kilichoegeshwa vibaya na kumtaka mmiliki au mtumiaji wa kituo kulipa faini kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii. (3) Chombo cha usafiri ambacho kitakuwa kimefungwa mnyororo au kifaa maalumu zaidi ya saa mbili bila ya kulipiwa, kitavutwa na kupelekwa kwenye eneo maalumu lililotengwa na Halmashauri kwa gharama za mmiliki wa chombo cha usafiri kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Nne la Sheria Ndogo hii. (4) Halmashauri haitahusika na uharibifu utakaotokea wakati wa uvutwaji wa chombo cha usafiri isipokuwa utakuwa umesababishwa na uzembe wa Halmashauri au watumishi wake. uharibifu kama huo (5) Chombo cha usafiri ambacho kitahifadhiwa katika eneo maalumu lililotengwa kwa muda wa siku 5 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) thelathini bila kukombolewa, kitahesabika kama kimetelekezwa. itapeleka maombi mahakamani (6) Baada ya kipindi cha siku thelathini kupita ili Halmashauri kuiomba mahakama itamke kuwa chombo hicho kimetelekezwa na hivyo itoe kibali chombo hicho kiuzwe kwa njia ya mnada wa hadhara. (7) Bila kuathiri masharti yaliyowekwa katika kanuni ndogo ya (6), kabla ya Halmashauri kuuza mali yoyote iliyokamatwa, Mkurugenzi atatoa taarifa ya siku saba kwa mdaiwa na umma kuhusu kusudio la kuuza mali hiyo. (8) Fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo ya chombo cha usafiri kilichouzwa kwa mnada zitatumika kulipia ushuru unaodaiwa, pamoja na gharama za kukamata na fedha zitakazobaki zitarejeshwa kwa mmiliki au mwakilishi wake. - 11 Verify source ↗
Halmashauri haitatoza ushuru wa maegesho
AI-assisted research summary: Halmashauri haipaswi kutoza ushuru wa maegesho kwa aina fulani za magari yaliyoorodheshwa.
11. Halmashauri haitatoza ushuru wa maegesho kwa vyombo vya usafiri vifuatavyo: (a) magari ya Serikali; (b) magari ya Kibalozi; (c) magari yaliyoegeshwa katika sehemu za ibada wakati wa ibada; (d) magari yaliyo na vibali maalumu kutoka Halmashauri; (e) magari yaliyoegeshwa katika maeneo ya maegesho wakati wa shughuli maalumu za kitaifa; (f) magari ya Wabunge na Madiwani wa Halmashauri; (g) magari yaliyoegeshwa katika maeneo ya makaburi wakati wa mazishi; na (h) magari ya wagonjwa. - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: This section makes it an offence for any person to obstruct enforcement officers, damage parking or station infrastructure, park in prohibited areas, use passenger vehicle stations without paying, or do other listed misconduct.
12. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atamzuia Afisa Mwidhiniwa kutekeleza majukumu yake ya kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; 6 Magari yasiyotozwa ushuru wa maegesho Makosa Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) (b) ataharibu kwa namna yoyote miundombinu ya barabara, kifaa, kamera za usalama au taa za barabarani katika maeneo ya maegesho au kituo cha magari ya abiria; (c) ataegesha chombo cha usafiri katika maeneo yasiyoruhusiwa kwa ajili ya maegesho; (d) ataingiza gari la kuzoa taka au kufanya kazi ya kukusanya taka katikati ya Jiji nyakati za mchana bila kibali cha maandishi kutoka Halmashauri; (e) ataingia au kutumia kituo cha magari ya abiria pasipo kulipia ushuru husika; (f) atalaza chombo cha usafiri, ataosha, atatengeneza au atafanya shughuli yoyote kwenye eneo ambalo halijatengwa kwa shughuli hiyo ndani ya kituo cha magari ya abiria; (g) atachafua mazingira kwa kutupa taka ndani ya kituo cha magari ya abiria au atatupa taka kutoka kwenye chombo cha usafiri; (h) atatumia lugha ya matusi, zenye kuleta uchochezi kubughudhi zinazohatarisha usalama na amani ndani ya kituo; (i) ataghushi kinachotolewa kibali au na za Halmashauri; (j) atashindwa kuingiza chombo cha usafiri katika kituo cha magari ya abiria; na (k) atatenda jambo lolote kinyume cha Sheria Ndogo hii. Adhabu - 13 Verify source ↗
Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa
AI-assisted research summary: A person convicted of any offence against this bylaw is liable to a fine, imprisonment, or both.
13. Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa lolote kinyume cha Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini ya kiasi kisichopungua shilingi laki mbili na kisichozidi au kifungo shilingi milioni moja kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. 7 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) Kufifilisha kosa - 14 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji hadi shilingi laki mbili ikiwa mkosaji anakiri kwa hiari, anajaza fomu maalumu, na analipa ada au ushuru anaodaiwa.
14. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari kosa na kujaza fomu maalumu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tano la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. Kufutwa kwa Sheria Ndogo TS Na. 41 la 2017
Part
Jedwali la Tano la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au
- 15 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Vyombo vya
AI-assisted research summary: This section repeals the 2017 by-law on vehicle transport regulation and revenue improvement for Dar es Salaam City Council.
15. Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri na Uboreshaji wa Mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2017 inafutwa. 8 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) _________ JEDWALI LA KWANZA _______ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 9(3)) KIBALI CHA KUANZISHA MAEGESHO Kibali S.L.P………………. hiki kimetolewa kwa Bw/Bi:………………………………………………wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ameridhia Ndugu mtajwa hapo juu, kuanzisha maegesho katika eneo la…………………….kwa kipindi cha ………………………… TAMKO LA MWOMBAJI: MIMI…………………………………………………………nipo tayari kuzingatia masharti ya kibali hiki cha maegesho ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Nathibitisha kwa hiari yangu kuwa nimeelewa vema masharti ya kibali hiki. Jina: …………………………… Saini …………………..Tarehe ………………… KWA MATUMIZI YA OFISI: Mwombaji amelipa shilingi ……………..….. tarehe……….mwezi……….mwaka………….. (Ambatanisha stakabadhi ya malipo na fomu hii) Jina la Afisa aliyetoa kibali………………… Saini …………… Tarehe ………… Wadhifa ................................ Muhuri:……………………………… ________________ JEDWALI LA PILI ______________ Limetengenezwa chini ya kanuni ya 9(4)) KIBALI KWA AJILI YA MAEGESHO KATIKA MAENEO MAALUMU Kibali Bw/Bi:………………………………………………wa S.L.P………………. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ameridhia Ndugu mtajwa kimetolewa kwa hiki 9 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) katika kuegesha hapo siku/wiki/mwezi………………………… baada ya kulipia huduma hiyo. la…………………….kwa eneo juu, kipindi cha TAMKO LA MWOMBAJI MIMI…………………………………………………………nipo tayari kuzingatia masharti ya kibali hiki cha maegesho ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Nathibitisha kwa hiari yangu kuwa nimeelewa vema masharti ya kibali hiki. Jina: …………………………… Saini …………………..Tarehe ………………… KWA MATUMIZI YA OFISI Mwombaji amelipa shilingi ………………………….. tarehe……….mwezi……….mwaka………….. (Ambatanisha stakabadhi ya malipo na fomu hii) Jina la Afisa aliyetoa kibali……………………… Saini ……… Tarehe ………… Wadhifa ...................................... Muhuri:………………………………… 10 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) __________ JEDWALI LATATU __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 10(2)) TOZO KWA AJILI YA MAEGESHO YASIYO RASMI NA KULAZA VYOMBO VYA USAFIRI Namba Aina ya chombo cha usafiri
Part
JEDWALI LATATU
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: This section lists charges for informal parking, daily storage of a vehicle, and removal/towing fees for different types of vehicles.
4. Bajaji au pikipiki Gari dogo lenye uwezo wa kubeba uzito chini ya tani 2 Gari lenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 2 hadi 4 Gari lenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 4 na kuendelea Tozo ya maegesho yasiyo rasmi (Shilingi) 50,000/= 50,000/= 120,000/= 200,000/= Tozo ya kulaza chombo cha usafiri kwa siku (Shilingi) 20,000/= 20,000/= 20,000/= 30,000/= __________ JEDWALI LA NNE __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 10(3)) USHURU WA KUONDOA NA KUVUTA CHOMBO CHA USAFIRI Namba Aina ya Chombo cha Usafiri Basi kubwa la abiria Basi dogo la abiria Teksi Gari dogo binafsi Malori na Matrela zaidi ya tani 3 hadi 7 Kiwango cha ushuru (Shilingi) 300,000/=
Part
JEDWALI LA NNE
- 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: This section is a form for voluntarily admitting an offence before the Director and agreeing to pay a fine and any owed fee or levy.
9. Malori na Matrela tani 7.1 na zaidi Gari la mizigo Pikipiki Bajaji 400,000/= 80,000/= 10,000/= 50,000/= 11 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) __________ JEDWALI LA TANO __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 14) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ........................................................................nakiri KWA HIARI YANGU MIMI MWENYEWE mbele ya........................................................... ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwamba tarehe .......... ya mwezi .................. mwaka................ nilitenda kosa kwa kukiuka masharti ya kanuni ya …….. ya Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, NINAKUBALI kulipa kiasi cha shilingi.....................kama faini ya kufifilisha kosa na kiasi cha shilingi .....................ambacho ni ada au ushuru ninaodaiwa. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo Tarehe ......................ya Mwezi ................................Mwaka …… Jina: ..................................................... Saini: .................................................... MBELE YA MKURUGENZI: Jina……............................................... Saini: .................................................. Tarehe: ............................................... 12 Sheria Ndogo ya Udhibiti wa vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 82 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar salaam imegongwa kwenye Sheria ndogo hizi kufutia Azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar esalaa uliofanyika tareha 06 Mwezi Machi Mwaka 2023 na kushuhudiwa lakari hiyo ikigongwa mbele ya:- JAMAARY MRISHO SATURA, Mkurugenzi wa Jiji, Halmashauri ya Jiji, Dar Salaam MHE OMARI KUMBILAMOTO, Mstahiki Meya, Halmashauri ya Jiji Dar Salaam L.S NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA 29 Agositi ,2024 Waziri wa Nchi -OR-Tamisemi 13
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2025
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in