148 kupitia vilima vya Lugeye hadi GV230. Kisha kuelekea Kusini kufuata Mto
Verify source ↗ AI-assisted research summary: This provision describes a boundary line using rivers, roads, hills, villages, and survey points.
4.148 kupitia vilima vya Lugeye hadi GV230. Kisha kuelekea Kusini kufuata Mto Nyamugogwa hadi GV233 kupitia GV226. Kisha kufuata Mto Nyamugogwa kuelekea Kusini Magharibi kwa umbali wa kilomita 5.423 hadi GV227, kwenye Mto Lwamwizu Magharibi mwa Msitu wa Mienze. Kisha kufuata Mto Lwamwizu kuelekea Kaskazini Magharibi hadi GV64. Kisha kufuata Mto Lwamwizu hadi mdomo wake, kisha kuelekea Kaskazini Magharibi hadi GV231 kupitia GV218 kwenye barabara ya Mwagimagi/Bushishi. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 258 kwa umbali wa kilomita 2.268 hadi GV639, Kaskazini mwa Kijiji cha Msokole. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 296 kwa umbali wa kilomita 3.124 hadi GV701 kwenye Mto Nyalwanzaja. Kisha kufuata Mto Nyalwanzaja hadi GV383 kupitia GV377 na GV378. Kisha kuelekea Kaskazini kupitia vilima vya Ibsabageni hadi GV382. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 334 kwa umbali wa kilomita 2.358 hadi GV444. Kisha kuelekea Kaskazini Magharibi kufuata Bonde kati ya Vijiji vya Mkolani na Buyagu hadi GV445 kwenye barabara ya Buyagu/Mkolani. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 226 kwa umbali wa kilomita 6.182 hadi GV8. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 294 kwa umbali wa kilomita 1.00 hadi GV413 kwenye vilima vya Songambele. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 341 kwa umbali wa kilomita 0.654 hadi GV412. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 316 kwa umbali wa kilomita 1.280 hadi GV411. Kisha kufuata barabara ya Bufunda na Mpomvu kuelekea Kaskazini Magharibi kando ya Hifadhi ya Msitu wa Geita hadi GV417, Kaskazini Magharibi mwa vilima vya Samina. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 341 kwa umbali wa kilomita 5.202 kupitia Hifadhi ya Msitu wa Geita hadi GV425, Magharibi mwa Kijiji cha Nyakabale. Kisha kuelekea Kaskazini Magharibi hadi GV423 kupitia GV kwa umbali wa kilomita 3.3. Kisha kuelekea Kaskazini Magharibi kufuata Mto Komlale kupitia GV112, GV113 hadi GV114. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 90 kwa umbali wa kilomita 8.132 hadi GV111, kwenye makutano ya barabara ya Bugulula/Mtakuja. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 75 kwa umbali wa kilomita 3.595 hadi GV80A. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 313 kwa umbali wa kilomita 4.754 kupitia barabara ya Nzera hadi GV80. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 87 kwa umbali wa kilomita 5.637 hadi GV79. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 107 kwa umbali wa 3 Amri ya Kupandisha Hadhi Halmashauri ya Mji wa Geita Tangazo la Serikali Na.84 (Linaendelea.) kilomita 4.962 hadi GV94 katika Kijiji cha Kamhanga. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 124 kwa umbali wa kilomita 1.874 hadi GV2, kwenye Kilele cha Kanza. Kisha kwenye mwelekeo wa nyuzi 101 kwa umbali wa kilomita 2.085 kupitia barabara ya Kamhanga hadi GV97 kwenye Mto Komoyo. Kisha kuelekea Kaskazini Mashariki kufuata Mto Komoyo kupitia GV181, GV172 hadi makutano ya barabara ya Nyakaduha/Chabulong kwenye mdomo wa Mto Mkoba. Kisha kuelekea Kaskazini Magharibi kufuata Mto Mkoba kando ya mpaka wa Geita/Sengerema hadi daraja lililopo kwenye Kinamasi cha Nyaruhwa mahali pa kuanzia.” _____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 3) NEMBO YA HALMASHAURI Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA 20 Disemba, 2024 Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI 4