AI-assisted research summary: The applicant is granted a construction permit for a fuel station only if the listed safety, layout, equipment, and reporting conditions are met.
3. Mwombaji anapewa kibali cha ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mafuta katika Kiwanja Na. P20810, Eneo la Toangoma, Wilaya ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam kulingana na masharti yafuatayo: (a) kituo cha mafuta kitajengwa kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Na. TZS 1115:2009 na TZS 1079:2008 na taratibu bora za kimataifa zinazokubalika kwenye sekta ya mafuta; 1 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Mafuta kwa Amos Site Mabena - Majengo (b) kuzingati ubora, umakini na utaalamu wakati wa uchimbaji na uwekaji wa matenki ya mafuta chini ya ardhi; (c) mpangilio wa kituo cha mafuta utatakiwa kukidhi matakwa ya kiusalama kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Na. TZS 1115:2009 na TZS 1079:2008 na taratibu bora za kimataifa zinazokubalika kwenye sekta ya mafuta; (d) ufukiaji wa matenki ya kuhifadhi mafuta pamoja na mabomba chini ya ardhi ufanyike kwa namna ambayo italinda usalama wa vifaa hivyo ikiwemo kuzuia kutu; (e) matenki ya kuhifadhia mafuta, pampu na mabomba husika pamoja na vifaa vyote vinavyounganishwa pamoja vitafungwa ili kuzuia uvujaji wowote wa mafuta; (f) mfumo wa automatik (ATGs) utajengwa kwenye kila tenki kwa ajili ya kupima kiasi cha ujazo wa mafuta kwenye tenki. Mfumo wa ATGs utaunganishwa na mfumo wa EWURA wa NPGIS kwa ajili ya kuwasilisha taarifa; (g) kuhakikisha kila tenki la kuhifadhia mafuta linaunganishwa na bomba la hewa lenye urefu usiopungua mita 3.6 kutoka ardhini na bomba hilo linatakiwa kuwa angalau mita 1.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja na angalau mita 4.5 kutoka kwenye dirisha au kifaa chochote cha kuvuta hewa ikiwemo kiyoyozi; (h) matenki ya kuhifadhia mafuta na pampu ya mafuta itafanyiwa uhakiki wa usahihi wa vipimo na Wakala wa Vipimo Tanzania aliyeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Tanzania; (i) eneo la mbele la kituo cha mafuta na kuzunguka eneo la pampu litasakafiwa kwa zege madhubuti isiyoweza kupenyeza mafuta na kuhakikisha kuwepo kwa mitaro ambayo itakusanya maji na mafuta wakati wa mvua na kuyaelekeza kwenye chemba ya kutenganisha maji na mafuta; 2 Sura 340 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Mafuta kwa Amos Site Mabena - Majengo (j) kuweka swichi ya dharura katika eneo linaloonekana na kufikika kirahisi ili iwe rahisi kuzima umeme wa kituo kizima wakati wa dharura; (k) kuhakikisha uwepo wa vyoo vya kutosha vya wanawake na wanaume vilivyo safi wakati wote; (l) kuhakikisha kuwa alama za usalama zinawekwa eneo la pampu na sehemu ya kushushia mafuta zikijumuisha “zima injini”, “zima simu” na “usivute sigara”; (m) mifumo ya upakuaji wa mafuta kwenye kituo cha mafuta itajengwa kwa kufuata Kanuni na taratibu bora zinazokubalika kwenye sekta ya mafuta; (n) pampu zinazotumika kuuzia mafuta na sehemu ya kushushia mafuta inatakiwa kuwa angalau umbali wa mita 8 kutoka kwenye kifaa chochote ambacho kinaweza kuwa chanzo cha moto ikiwemo jokofu na angalau mita 10 kutoka kwenye nyaya za kusafirishia umeme; (o) pampu zinazotumika kuuzia mafuta na sehemu ya kushushia mafuta zinatakiwa kuwa angalau umbali wa mita 15 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja ikiwa kiwanja kinapakana na nyumba ya makazi au ofisi; (p) kuhakikisha kila pampu ya mafuta inalindwa na kizuizi chenye urefu wa mita moja kutoka juu ya ardhi; (q) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na paa linalofunika eneo lote lenye pampu za mafuta na linajengwa kwa mujibu wa viwango na taratibu zinazokubalika katika sekta ya mafuta; na (r) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na bango la bei ambalo litawekwa mahala ambapo panaonekana kirahisi ili wateja waweze kuona bei za mafuta kabla ya kuingia kituoni. 3 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Mafuta kwa Amos Site Mabena - Majengo Ukomo wa kibali cha ujenzi