Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Sheria Ndogo hii inaitwa Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Sheria Ndogo hii inaitwa Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. This provision says the by-law applies throughout the area of authority of the Kilwa District Council. This section defines key terms used in the by-law, including fees, market officials, market types, traders, permits, and market charges. Halmashauri lazima itambue maeneo ya masoko, ijenge na kuboresha miundombinu, isajili wadau, isimamie usafi na huduma, ikusanye ushuru na ada, na ikague masoko binafsi. Halmashauri must charge a fee on market, gulio, or auction services listed in the First Schedule.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Showing 52 of 52
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: Sheria Ndogo hii inaitwa Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This provision says the by-law applies throughout the area of authority of the Kilwa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including fees, market officials, market types, traders, permits, and market charges.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “ada” maana yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya vibali au leseni mbalimbali zitolewazo na Halmashauri; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri na Mkurugenzi aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “dalali” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa za sokoni au gulioni kwa njia ya mnada kwa niaba ya mwenye bidhaa kwa mujibu wa Sheria na taratibu za soko, gulio au mnada; “gulio” maana yake ni soko la wazi linalofanyika kwa wakati na siku maalumu, na kwa kibali maalumu cha Halmashauri; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa; 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) “kanda” maana yake ni eneo mahususi lililotengwa na Halmashauri ndani ya soko au gulio kwa ajili ya kufanya aina ya biashara zinazowiana; “kamati ya wadau wa soko” maana yake ni kamati itakayokuwa na majukumu ya kusimamia shughuli za soko ambayo itaundwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “kibali”maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na mkuu wa soko kwa mujibu Sheria Ndogo hii; “kikundi” maana yake ni kikundi cha ushirika au umoja wa wafanyabiashara uliosajiliwa na meneja wa soko kwa kuandikishwa katika daftari maalumu la wafanyabiashara wa soko; iliyojengwa “kizimba” maana yake ni meza au nafasi ya kufanyia na biashara Halmashauri katika soko, gulio au mnada; “kodi ya pango” maana yake ni kodi inayolipwa na mpangaji kwa Halmashauri au mmiliki wa soko kila mwezi au kila siku. kuidhinishwa au “mazao” maana yake ni mavuno ya bustani ndogondogo, shamba au maliasili yanayoingizwa kwenye soko, gulio au mnada ndani ya eneo la Halmashauri; “makasha” maana yake ni vifaa maalum vya kubebea, kufungashia au kuhifadhia bidhaa au mazao na yatajumuisha matenga, viroba, magunia, karatasi ngumu, masanduku ya mbao yanayotumika kubebea nyanya; “mdau wa soko” maana yake ni mfanyabiashara binafsi, taasisi, kampuni, kikundi cha wauzaji au wanunuzi, mnunuzi, dalali, mtumiaji mwingine aliye sajiliwa na mwenye maslahi na shughuli za soko au mtu yeyote anayenufaika na uwepo wa soko; “mnada” maana yake ni eneo maalumu lililotengwa na kumilikiwa na Halmashauri au Serikali ya Kijiji kwa ajili ya wafanyabiashara kununua au kuuza mazao au mifugo katika eneo la Mamlaka ya Halmashauri; “mdau wa soko” maana yake ni mfanyabiashara binafsi, taasisi, kampuni, kikundi cha wauzaji au wanunuzi, mnunuzi, dalali, mtumiaji mwingine aliye sajiliwa 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) na mwenye maslahi na shughuli za soko au mtu yeyote anayenufaika na uwepo wa soko; “meza” maana yake ni kitu au kifaa kinachotumika kuwekea bidhaa za biashara katika soko, gulio au mnada iliyoidhinishwa na Halmashauri; “mfanyabiashara” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa sokoni au katika gulio kwa jumla au rejareja aliyesajiliwa katika daftari rasmi la soko au gulio kwenye eneo ambalo limeruhusiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “meneja wa soko” maana yake ni mtu yeyote aliyeteuliwa au aliyeajiriwa na Halmashauri kusimamia shughuli zote katika soko linalomilikiwa na Halmashauri, au mtu yeyote anayesimamia soko binafsi ambalo limeidhinishwa na Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa pamoja na afisa yeyote atakayeteuliwa na Mkurugenzi kushika nafasi hiyo; “mnada” maana yake soko la wazi ambalo mali au vitu mbalimbali vinauzwa kwa ushindani wa bei kwa kauli na kwa kibali maalumu cha Halmashauri; “mnunuzi” maana yake ni mtu yoyote anayenunua bidhaa au mazao sokoni, gulioni au mnadani katika eneo la Halmashauri; “mpangaji” maana yake ni mtu binafsi, taasisi, kikundi au kampuni yeyote inayolipa kodi ya chumba, meza au kizimba aliyepangishwa na Halmashauri ndani ya soko la Halmashauri au aliyepangishwa na mmiliki wa soko kwa masoko binafsi na ana mkataba au idhini ya maandishi kutoka Halmashauri au mtu binafsi; “muuzaji” maana yake ni mtu yoyote anayeuza bidhaa au mazao katika soko, gulio, mnada au eneo lililoidhinishwa na Halmashauri; “soko” maana yake ni eneo maalum la biashara lililotengwa na kumilikiwa na Halmashauri au watu binafsi kwa matumizi ya kuuza au kununua bidhaa; “uongozi wa soko” maana yake ni watendaji wa Halmashauri wanaosimamia shughuli za kila siku za soko katika masoko ya Halmashauri au wamiliki 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) wa soko wanaosimamia shughuli za soko katika masoko binafsi; “ushuru” maana yake ni malipo yatakayolipwa kwa mujibu wa viwango vilivyopangwa katika Sheria Ndogo hii kutokana na huduma au bidhaaa itakayouzwa, kununuliwa au kuingizwa na mtu yeyote katika soko au gulio lililoidhinishwa na Halmashauri; “vikundi” maana yake ni vikundi vya ushirika, umoja wa vikundi vya wafanyabiashara vilivyosajiliwa au kuandikishwa na kuwasilishwa katika Kamati ya Soko na kwa Mkuu wa Soko; na “wakala” maana yake ni mtu, kikundi, taasisi au kampuni iliyopewa kazi ya kukusanya mapato katika chanzo au vyanzo vya mapato kwa niaba ya Halmashauri. Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itambue maeneo ya masoko, ijenge na kuboresha miundombinu, isajili wadau, isimamie usafi na huduma, ikusanye ushuru na ada, na ikague masoko binafsi.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kuainisha na kutambua maeneo yanayohitaji kuwa na masoko, magulio au mnada; (b) kuanzisha, kuendeleza, na kuboresha miundombinu ya masoko, magulio na minada; kusimamia (c) kusajili wadau wa soko, gulio au mnada; (d) kusimamia usafi wa soko, gulio na mnada; (e) kusimamia ufikishwaji wa huduma za umeme, maji na huduma nyingine za kijamii katika masoko na magulio; (f) kukusanya ushuru na ada mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wa sokoni na gulioni; na (g) kukagua namna ya uendeshwaji wa masoko yote binafsi ili kujiridhisha iwapo sheria, kanuni na taratibu zinafuatwa ikiwa ni pamoja na kuangalia usafi na usalama wa soko na watumiaji wake. Ushuru wa masoko na magulio - 5 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru kwenye huduma
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge a fee on market, gulio, or auction services listed in the First Schedule.
5.-(1) Halmashauri itatoza ushuru kwenye huduma soko, gulio au mnada kama mbalimbali katika ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (2) Ushuru utakaotozwa chini ya Sheria Ndogo hii utalipwa kabla au baada au wakati wa kupata huduma. 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) Mamlaka ya usimamizi wa masoko Kibali cha minada Ujenzi na ukarabati (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2), mlipa ushuru anaweza kufanya makubaliano maalumu na Halmashauri kuhusu namna anayoona inafaa kulipa ushuru. - 6 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri ina mamlaka ya kuanzisha na kusimamia masoko na magulio yote ndani ya eneo lake, na mtu yeyote haruhusiwi kuanzisha au kuendesha soko au gulio binafsi bila kibali maalumu cha Halmashauri.
6.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuanzisha na kusimamia masoko na magulio yote katika eneo la Halmashauri. (2) Mtu yeyote hataruhusiwa kuanzisha au kuendesha soko au gulio binafsi isipokuwa kwa kibali maalumu cha Halmashauri. - 7 Verify source ↗
(1) Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine
AI-assisted research summary: Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine inaweza kufanyika kwenye masoko au magulio ikiwa kuna kibali maalum cha Halmashauri.
7.-(1) Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine zitaruhusiwa kufanyika kwenye masoko au magulio kwa kibali maalum cha Halmashauri kitakachotolewa baada ya mwombaji kuwasilisha maombi yake kwa maandishi kwa Mkurugenzi. (2) Kibali cha kufanya mnada katika eneo la soko au gulio kitakuwa kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. - 8 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya ukarabati
AI-assisted research summary: Watu hawaruhusiwi kufanya ukarabati au marekebisho ya baadhi ya vitu vilivyo katika masoko au magulio ya Halmashauri bila idhini ya maandishi ya Mkurugenzi. Pia, mtu anayejenga kibanda au fremu ndani ya soko lazima apate idhini ya maandishi na baadaye akikabidhi kibanda au fremu hiyo kwa Halmashauri baada ya gharama za ujenzi kurejeshwa.
8.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya ukarabati au marekebisho ya chumba, kibanda, meza au kizimba katika masoko au magulio ya Halmashauri bila idhini ya maandishi ya Mkurugenzi. (2) Kibanda au fremu kitakachojengwa ndani ya eneo na mipaka ya soko kitakuwa ni mali ya Halmashauri. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2), mtu yeyote anayekusudia kujenga kibanda au fremu ndani ya eneo na mipaka ya soko atatakiwa kupata idhini ya maandishi kutoka kwa Mkurugenzi na atalazimika kukabidhi kibanda au fremu hiyo kwa Halmashauri baada ya kurejesha gharama zake za ujenzi kwa mujibu wa tathimini ya gharama za ujenzi itakayofanywa na Halmashauri. Maeneo ya kufanyia biashara - 9 Verify source ↗
Mfanyabiashara yeyote hataruhusiwa kufanya
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara hawaruhusiwi kufanya biashara nje ya eneo lililoidhinishwa na Halmashauri, na mtu haruhusiwi kuingiza mifugo sokoni au gulioni isipokuwa ndege na wanyama wadogo kama sungura.
9. Mfanyabiashara yeyote hataruhusiwa kufanya biashara nje ya chumba, kibanda, kizimba, meza au eneo lililoidhinishwa na Halmashauri. 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) Mifugo kutoingizwa sokoni Tahadhari ya moto Matumizi ya soko kwa muda Meneja wa masoko 10 Mtu hataruhusiwa kuingiza mifugo kuingizwa sokoni au gulioni isipokuwa jamii ya ndege na wanyama wadogo wadogo kama sungura. - 11 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwi kupika chakula,
AI-assisted research summary: Watu hawawezi kupika, kuchoma nyama, kuendesha mgahawa, kufanya shughuli nyingine zinazohusisha moto, au kufanya udobi ndani ya soko bila idhini au ruhusa ya maandishi kutoka kwa Mkurugenzi; wamiliki wa masoko binafsi lazima wachukue tahadhari za moto.
11.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwi kupika chakula, kuchoma nyama au kuendesha shughuli za mgahawa au shughuli nyingine yeyote inayohusisha moto ndani ya eneo la soko la Halmashauri isipokuwa kwa idhini ya maandishi kutoka kwa Mkurugenzi. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), wamiliki wa masoko binafsi watawajibika kuchukua tahadhari ya moto katika utekelezaji wa shughuli zote katika masoko yao. (3) Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya shughuli ya udobi ndani ya soko la Halmashuri isipokuwa kwa ruhusa ya maandishi na Mkurugenzi kupitia kwa mkuu wa soko. - 12 Verify source ↗
(1) Mfanyabiashara ambaye hajasajiliwa katika
AI-assisted research summary: A non-registered trader may use the market temporarily only after applying for and obtaining a special temporary-market permit from the Director.
12.-(1) Mfanyabiashara ambaye hajasajiliwa katika daftari la wafanyabiashara anaweza kutumia soko kwa matumizi ya muda baada ya kuomba na kupata kibali maalum cha kutumia soko kwa muda kutoka kwa Mkurugenzi. (2) Maombi ya kibali cha kutumia soko kwa muda yatawasilishwa kwa Mkurugenzi kwa kutumia Fomu Na. 1 ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu . (3) Kibali cha kutumia soko kwa muda kitatolewa katika Fomu Na. 2 kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Nne. - 13 Verify source ↗
(1) Kutakuwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi humteua Meneja wa Soko, na meneja huyo anapaswa kusimamia shughuli za maendeleo ya soko na kutekeleza majukumu yaliyoorodheshwa.
13.-(1) Kutakuwa na Meneja wa Soko atakayeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia shughuli za uendelezaji wa soko na atakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kukusanya ushuru na ada mbalimbali kwenye masoko ya Halmashauri na binafsi kama zilivyoainishwa katika Sheria Ndogo za Ada na Ushuru za Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa; (b) kuratibu huduma za ulinzi, maji na umeme katika soko; (c) kusimamia usajili wa wadau wa soko kwa kushirikiana na Kamati ya soko; 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) Uteuzi wa wakala Kuanzishwa kwa kanda za soko (d) kusimamia usafi na uondoshaji wa taka katika soko; (e) kuhakikisha kuwa bidhaa haziuzwi kwenye eneo ambalo haliruhusiwi kwa shughuli hiyo; (f) kuzuia ujenzi holela katika soko; (g) kwa idhini ya Mkurugenzi, kusaini kibali cha muda cha kutumia soko; na (h) kutekeleza majukumu mengine yoyote atakayoelekezwa na Mkurugenzi kuhusu shughuli za soko. - 14 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kumteua wakala
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumteua wakala, na wakala huyo lazima akusanye ushuru kwa mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa mujibu wa mkataba wa uwakala.
14.-(1) Halmashauri inaweza kumteua wakala ambaye atawajibika katika kutekeleza majukumu ambayo Halmashauri itaona inafaa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. (2) Wakala atakusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. - 15 Verify source ↗
(1) Kwa madhumuni ya uendeshaji bora wa
AI-assisted research summary: The provision divides the market into zones by similar products, bars sales of products in unplanned or unapproved market zones, requires every trader to register in their zone and with specified market bodies, and provides for elected zone leaders.
15.-(1) Kwa madhumuni ya uendeshaji bora wa shughuli katika soko, zitagawanywa kanda mbalimbali katika soko kulingana na bidhaa zinazowiana na bidhaa zote zinazowiana na kufanana zitakuwa kwenye kanda moja. (2) Mtu hataruhusiwa kuuza bidhaa yoyote kwenye ambayo haikupangwa na kuruhusiwa na kanda Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (3) Kila mfanyabiashara kwenye soko atawajibika kujisajili katika kanda yake na atakuwa mjumbe wa kanda hiyo na atapaswa kujisajili kwa kiongozi wa kikundi, Kamati ya Wadau na Mkuu wa Soko. (4) Kila kanda itakuwa na viongozi wafuatao watakaochaguliwa katika uchaguzi mkuu wa soko utakaofanyika kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii: (a) Mwenyekiti wa kanda; (b) Makamu Mwenyekiti wa kanda; (c) Katibu wa kanda; (d) Katibu Msaidizi wa kanda; (e) Mweka hazina wa kanda; na 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) Kamati ya wadau wa soko (f) wajumbe wanne wa kanda. - 16 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Kamati ya Wadau wa Soko
AI-assisted research summary: Kuna Kamati ya Wadau wa Soko inayopaswa kuundwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, na Meneja wa soko husimamia uchaguzi wa wajumbe watano.
16.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Wadau wa Soko ambayo itaundwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Wajumbe wa Kamati ya Wadau wa Soko watapatikana kwa kuchaguliwa kwa utaratibu ufuatao: (a) Mwenyekiti na Katibu kutoka kwenye kila Kanda ya soko; na (b) wajumbe wengine watano watakachaguliwa katika mkutano wa wafanyabiashara wote katika soko ambapo kati yao kutakuwa na wanawake wawili. (3) Meneja wa soko ndiye atakayesimamia uchaguzi wa wajumbe watano watakaochaguliwa katika mkutano wa wafanyabiashara wote katika soko. Muda wa madaraka kwa viongozi wa kanda na kamati ya wadau soko - 17 Verify source ↗
Viongozi wa Kanda na Kamati ya Wadau
AI-assisted research summary: Regional leaders and the stakeholder committee serve for three years from the date they are elected, and they may be elected again for another three-year term.
17. Viongozi wa Kanda na Kamati ya Wadau watakaa madarakani kwa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe ya kuchaguliwa kwao na wanaweza kuchaguliwa tena kushika nafasi hizo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu. Vikao vya kamati ya wadau wa soko - 18 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Kikao cha Kamati ya Wadau
AI-assisted research summary: The market stakeholders committee must meet once a month and carry out listed market-management duties.
18.-(1) Kutakuwa na Kikao cha Kamati ya Wadau wa Soko kitakachofanyika mara moja kila mwezi ambapo Meneja wa Soko atakuwa katibu wa kikao na Mwenyekiti atachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Wadau wa Soko. (2) Kamati ya Wadau wa Soko inaweza kukutana kwa jinsi itakavyoona inafaa nje ya vikao vya lazima kwa ajili ya kutekeleza maazimio yaliyoainishwa katika kikao cha kamati ya wadau wa soko au kupata ufumbuzi wa jambo la dharula. (3) Kamati ya Wadau wa Soko itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuunganisha wadau wote waliopo sokoni bila kujali tofauti zao za vyama, kabila, dini au vikundi vilivyopo sokoni; (b) kushirikiana na serikali katika kuwaletea maendeleo wadau wa soko kulingana na sera na mipango iliyopo; 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) (c) kuwasilisha taarifa za kamati ya wadau wa soko kwa Halmashauri; (d) kuboresha ustawi wa wadau wa soko; (e) kuhakikisha kwamba nidhamu inakuwepo katika shughuli za soko; (f) kuinua ubora wa mfumo wa biashara katika soko; (g) kudhibiti na kufichua upotevu wa mapato ya soko na kuhakikisha mapato yanapanda na hayapotei kwa kushirikiana na mkuu wa soko; na (h) kuhamasisha watumiaji wa soko kutekeleza wajibu wa ulipaji ada, ushuru pamoja na tozo zilizoamriwa kwa mujibu wa sheria ndogo za ada na ushuru za Halmashauri. Usajili wa wafanyabiasha ra - 19 Verify source ↗
(1) Wafanyabiashara wote wa soko watasajiliwa
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wote wa soko lazima wasajiliwe na Meneja wa soko ili watambulike na waandikwe kwenye rejista maalumu.
19.-(1) Wafanyabiashara wote wa soko watasajiliwa na Meneja wa soko kwa lengo la kuwatambua na kuwaorodhesha kwenye rejista maalumu. (2) Rejesta wa wafanyabiashara wa soko itaonesha taarifa muhimu kuhusu mfanyabiashara ikiwa ni pamoja na: (a) tarehe ya usajili; (b) jina la mfanyabiashara; (c) jinsi; (d) aina ya biashara anayoifanya sokoni; (e) kikundi chake kama mfanyabiashara, ni mfanyabiashara binafsi au mwanachama wa kikindi; (f) aina ya mfanyabishara, kama ni kikundi, ushirika au mfanyabiashara binafsi; na kwa nyingine muhimu (g) taarifa kadiri zitakavyohitajika. Kuundwa kwa Kamati Ndogo - 20 Verify source ↗
(1) Kamati ya Wadau wa Soko itaunda Kamati
AI-assisted research summary: Kamati ya Wadau wa Soko lazima iunde kamati ndogo za kazi.
20.-(1) Kamati ya Wadau wa Soko itaunda Kamati Ndogo ambazo zitakuwa na wajumbe watatu kutoka miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Wadau kama ifuatavyo: (a) kamati ndogo ya Miundombinu; (b) kamati ndogo ya Fedha, Biashara na Utawala; na 9 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) (c) Kamati Ndogo ya ulinzi na Usalama. Udhibiti wa nidhamu - 21 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kufanya vitendo vilivyotajwa ndani ya soko au gulio, na mfanyabiashara anayeonyesha kukosa nidhamu anaweza kuitwa na kuagizwa kurekebisha hali hiyo.
21.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kufanya mambo yafuatayo katika soko au gulio: (a) kubandika au kubandua tangazo lolote bila idhini ya Meneja katika eneo la soko au bila idhini ya Afisa Mwidhiniwa katika gulio; (b) kuweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la soko au gulio; (c) kufanya shughuli za siasa ndani ya soko au gulio; (d) kuharibu miondombinui ya soko au gulio; (e) kufanya ujenzi au ukarabati bila kibali cha Mkurugenzi; (f) kutumia lugha ya matusi, kufanya vurugu au ugomvi; (g) kufanya shughuli yoyote kwenye eneo ambalo haliruhusiwi au halijatengwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (h) kutupa taka ovyo au kutiririsha maji machafu; (i) kuwasha moto maeneo yasiyoruhusiwa; (j) kufunga chumba cha biashara kwa madai ya kukitumia kama stoo au matumizi mengine yasiyoainishwa katika mkataba au leseni; (k) kuendelea na biashara baada ya muda wa kufanya biashara ulioruhusiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Mfanyabiashara ambaye atakosa nidhamu, licha ya kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria anaweza kuitwa na Meneja wa soko au Afisa Mwidhiniwa katika gulio kwa vyovyote itakavyokuwa, na baada ya kupewa nafasi ya kujijitea, Meneja au Afisa Mwidhiniwa anaweza kumtaka mtu huyo kurekebisha hali aliyoisababisha ambayo haitakiwi. Mkutano Mkuu wa Kanda - 22 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Kanda
AI-assisted research summary: A regional general meeting must be held every three months and include leaders from all regions.
22.-(1) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Kanda utakaohusisha viongozi wa kanda zote utakaofanyika kila baada ya miezi mitatu na utajadili mambo yafuatayo: 10 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) (a) kupokea na kujadili taarifa za utendaji kazi za Kamati ya Wadau na Kamati Ndogo zilizoundwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) kupokea taarifa zinazohusu soko; (c) kujadili namna ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo watu wote walio kwenye kanda zao; (d) kuboresha ustawi wa wadau wa soko; (e) kuinua ubora wa mfumo wa biashara katika soko; (f) kupokea taarifa za maendeleo ya soko; (g) kujadili masuala yanayohusu miundombinu na mazingira katika soko. Mkutano mkuu wa wafanyabiasha ra - 23 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa
AI-assisted research summary: Hutoa ratiba na wajumbe wa mkutano mkuu wa wafanyabiashara na wadau wa soko, pamoja na mkutano wa uongozi wa soko.
23.-(1) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa wafanyabiashara na wadau wote wa soko utakaofanyika kila baada ya miezi sita, wajumbe wa mkutano huu watakuwa ni: (a) kamati ya Wadau wa soko; (b) viongozi wote wa kila kanda zilizopo sokoni; (c) mwenyekiti na katibu wa vyama vyote vilivyoko sokoni vinavyotambulika na meneja wa soko na kamati ya wadau wa soko; (d) waalikwa kutoka ndani au nje ya soko; (e) uwakilishi wa viongozi kutoka Halmashauri. (2) Kazi za Mkutano huu zitakuwa ni kama ifuatavyo: (a) kupokea juu kutoa taarifambalimbali za uendeshaji wa soko ushauri na ya (b) kuwasilisha mapendekezo ya ufanyaji wa maboresho ya uendeshaji wa soko, kamati ya wadau na menejimenti ya soko na Halmashauri juu ya uendeshaji bora wa utoajiwa huduma za soko; (c) kupokea taarifa za miundo mbinu ya soko na kuwasilisha mapendekezo ya wadau; (d) kuishauri kamati ya wadau na Halmashauri namna bora ya kuimarisha na kudhibiti mapato ya soko. (3) Kutakuwa na mkutano wa uongozi wa soko kwa lengo la kufanya tathimini wa mwenendo wa shughuli zote 11 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) Kuundwa kwa kamati Ndogo katika Masoko, Magulio na minada ambao utafanyika mara moja kwa kila mwezi na utajumuisha watumishi wote wa Halmashauri wanaofanya kazi kwenye soko husika na Meneja wa Soko atakuwa mwenyekiti wa kikao. - 24 Verify source ↗
(1) Uongozi wa wa Soko utaunda Kamati Ndogo
AI-assisted research summary: Uongozi wa Soko lazima iunde kamati ndogo tatu, kila moja ikiwa na wajumbe watatu kutoka miongoni mwa wafanyabiashara.
24.-(1) Uongozi wa wa Soko utaunda Kamati Ndogo zifuatazo ambazo zitakuwa na wajumbe watatu kutoka miongoni mwa Wafanyabiashara: (a) kamati Ndogo ya Miundombinu na Usafi; (b) kamati Ndogo ya Fedha, Biashara, Utawala na Nidhamu; (c) kamati Ndogo ya Ulinzi na Usalama. Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Soko - 25 Verify source ↗
(1) Uongozi wa Soko katika masoko ya
AI-assisted research summary: Viongozi wa soko la halmashauri na mmiliki wa soko binafsi wanaweza kutunga kanuni za uendeshaji wa soko, lakini kanuni hizo zitumike tu baada ya kuidhinishwa na Halmashauri.
25.-(1) Uongozi wa Soko katika masoko ya Halmashauri utakuwa na uwezo wa kutunga Kanuni za uendeshaji wa shughuli za soko, uendeshaji wa kamati, kamati ndogo na Uongozi wa wafanyabiashara ambazo zitatumika baada ya kuidhinishwa na Halmashauri. (2) Mmiliki wa Soko binafsi kwa kushirikiana na Uongozi wa Wafanyabiashara kwenye soko husika atakuwa na uwezo wa kutunga Kanuni za uendeshaji wa shughuli za soko uendeshaji wa kamati, kamati ndogo na Uongozi wa ya wafanyabiashara kuidhinishwa na Halmashauri. zitatumika ambazo baada Kibali cha kufanya biashara katika soko - 26 Verify source ↗
(1) Mfanyabiashara yeyote anayefanya au
AI-assisted research summary: Traders who are doing or planning to do business must apply to the Council for a permit using the form in the Fourth Schedule.
26.-(1) Mfanyabiashara yeyote anayefanya au anayekusudia kufanya biashara ataomba kibali kwa Halmashauri kwa kujaza fomu kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Nne. (2) Kibali hicho kitatolewa kwa mwombaji kupitia kwa Mkuu wa Soko na mwombaji atalipia ada ya kibali kama ilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii ambacho kitadumu kwa muda wa mwaka mmoja tangu siku ya kutolewa. atakayehitaji (3) Mfanyabiashara kuendelea kufanya biashara katika soko mara baada ya kibali chake kuisha muda wake, atatakiwa kuomba tena kibali kwa Halmashauri kwa utaratibu ulioelekezwa katika kanuni ndogo ya (1). 12 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) Kufuta kibali - 27 Verify source ↗
(1) Meneja wa Soko anaweza kufuta kibali
AI-assisted research summary: Meneja wa Soko anaweza kufuta kibali cha mwenye kibali akitokea hali fulani.
27.-(1) Meneja wa Soko anaweza kufuta kibali kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hii endapo mwenye kibali hicho: (a) atakuwa na malimbikizo ya madeni ya ada au ushuru zaidi ya miezi mitatu mfululizo; (b) atakuwa amesimamisha shughuli zake kwa muda wa miezi mitatu mfulumizo bila ya kutoa taarifa ya Maandishi kwa Mkurugenzi; (c) atakuwa amekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii hata baada ya kuonywa kwa maandishi; (d) atawashawishi wafanyabiashara wengine kutofuata Sheria Ndogo hii na kusababisha uvunjaji wa amani au atashiriki katika vitendo vya uvunjifu wa amani katika eneo la Soko; (e) atatumia chumba, kibanda, meza au kizimba alichopanga kinyume na madhumuni ya kufanyia biashara kama ilivyoainishwa kwenye mkataba wa upangishaji au kinyume na maelekezoyatakayotolewa na Halmashauri; (f) atapangisha eneo lake la biashara kwa mtu idhini ya maandishi ya mwingine bila Halmashauri. Saa za kazi - 28 Verify source ↗
(1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa
AI-assisted research summary: The market must be open every day from 12:00 a.m. to 12:00 p.m.; the council and market traders’ leadership may extend trading time or close the market for maintenance or other suitable reasons.
28.-(1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni. kwa (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri na Uongozi wa kushirikiana wafanyabiashara sokoni inaweza kuongeza muda wa kufanya biashara katika soko au maeneo maalumu yaliyoruhusiwa kulingana na mahitaji au hali halisi ya eneo husika. (3) Halmashauri kwa kushirikiana na Uongozi wa wafanyabiashara sokoni wanaweza kufunga soko kwa ajili ya matengenezo au sababu nyingine yoyote itakayoonekana inafaa kwa kutoa taarifa ya maandishi kwa Uongozi wa wafanyabiashara sokoni na kuweka matangazo kwenye sehemu za wazi. 13 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) Usafi wa soko Uingizaji wa bidhaa
Part
sehemu za wazi.
- 29 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabiashara anayefanya shughuli za
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wa soko lazima waweke maeneo yao katika usafi, wawe na chombo cha kuhifadhia taka, washiriki usafi wa soko, wafuate kanuni za afya, na walipe ada ya taka na huduma nyingine za Halmashauri.
29.-(1) Kila mfanyabiashara anayefanya shughuli za biashara katika soko atawajibika kuweka eneo lake la biashara katika hali ya usafi wakati wote, na atatakiwa awe na chombo maalum chenye mishikio na mfuniko kwa ajili ya kuhifadhia taka. (2) Meneja wa soko kwa kushirikiana na uongozi wa soko watapanga siku, namna na muda maalum mara moja kila mwezi kwa ajili ya kufanya usafi katika eneo lote la soko. (3) Kila mfanyabiashara katika soko atatakiwa kushiriki katika usafi wa soko. (4) Kila mfanyabiashara katika soko atatakiwa kufuata Kanuni za afya. (5) Kila mfanyabiashara atawajibika kulipa Ada ya taka na huduma nyingine zitakazotolewa na Halmashauri katika soko, gulio au mnada. - 30 Verify source ↗
(1) Bidhaa zote zitakazoingizwa katika soko
AI-assisted research summary: Goods brought into the market must be kept in special transport crates, and most leaf-wrapped goods may not be brought into the market unless the Market Manager gives special permission.
30.-(1) Bidhaa zote zitakazoingizwa katika soko zitatakiwa kuhifadhiwa kwenye makasha maalumu ya kusafirishia bidhaa. (2) Isipokuwa kwa ruhusa maalumu itakayotolewa na Meneja wa Soko, ni marufuku kwa mkulima, mfanyabiashara, dalali au mtu mwingine yeyote kuingiza sokoni bidhaa zilizofungwa kwa majani. (3) Mtu yeyote atakayeruhusiwa kuingiza sokoni bidhaa zilizofungwa kwa majani atawajibika mwenyewe kusafirisha majani hayo hadi sehemu ya kutupia uchafu na akishindwa kufanya hivyo atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Umiliki na ukusanyaji wa kodi, ada na ushuru - 31 Verify source ↗
(1) Vibanda vyote vya biashara vilivyoko katika
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wa sokoni katika masoko ya Halmashauri wanatakiwa kulipa kodi, ada au ushuru kwa Halmashauri au wakala wake, na vibanda vya biashara vya masoko ya Halmashauri vinamilikiwa na Halmashauri.
31.-(1) Vibanda vyote vya biashara vilivyoko katika masoko ya Halmashauri vitamilikiwa na Halmashauri na wafayabiashara wote watakuwa wapangaji. (2) Kila Mfanyabiashara sokoni atatakiwa kulipa kodi, ada au ushuru kwa Halmashauri au wakala wake kwa kila huduma atakayopatiwa au bidhaa atakayouza kwa mujibu wa viwango na utaratibu uliobainishwa katika Sheria Ndogo hii au Sheria Ndogo zinazosimamia ada na ushuru katika Halmashauri. 14 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) Kodi ya kupangisha eneo Huduma ya usafi, ulinzi, maji na umeme Makosa (3) Meneja wa Soko atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa ukusanyaji wa ada na ushuru katika soko. - 32 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza kodi ya kupanga eneo la
AI-assisted research summary: Halmashauri inatoza kodi ya kupanga eneo la biashara, kizimba au kibanda; mfanyabishara aliyesajiliwa katika masoko ya Halmashauri lazima ailipie kodi hiyo.
32.-(1) Halmashauri itatoza kodi ya kupanga eneo la Biashara, kizimba au kibanda cha kufanyia biashara ambayo italipwa na mfanyabishara yeyote aliyesajiliwa kufanya biashara katika maeneo yote ya masoko ya Halmashauri. (2) Kodi hiyo italipwa kwa Halmashauri au wakala kwa mujibu wa Mkataba wa pango kwa viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. - 33 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara katika soko atawajibika
AI-assisted research summary: Kila mfanyabiashara katika soko lazima alipe gharama za ulinzi, usafi, maji na umeme kila mwezi kulingana na mahitaji yake na utaratibu wa Halmashauri.
33. Kila mfanyabiashara katika soko atawajibika kugharamia huduma ya ulinzi, usafi, maji na umeme kulingana na mahitaji yake kila mwezi kufuatana na utaratibu utakaowekwa na Halmashauri. - 34 Verify source ↗
(1) Mtu atakuwa anatenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akifanya mojawapo ya vitendo vilivyokatazwa ndani ya soko, ikiwemo kuandika au kuondoa tangazo bila idhini ya Mkuu wa Soko.
34.-(1) Mtu atakuwa anatenda kosa endapo- (a) atabandika au kubandua tangazo lolote bila ya idhini ya Mkuu wa Soko; (b) ataweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la Soko; (c) atafanya shughuli za siasa ndani ya soko; (d) ataingiza sokoni kuuza au bidhaa zisizoruhusiwa kwa mujibu wa Sheria za nchi; (e) ataharibu miundombinu ya soko. (f) atatumia lugha inayoudhi ndani ya soko na udhalilishaji wa aina yoyote; (g) atafanya shughuli isiyoruhusiwa ndani ya soko; (h) atauza, kurithisha, kuhawilisha au kupangisha kibanda au eneo la biashara la Halmashauri kwa mtu mwingine bila ya idhini ya Halmashauri; (i) ataingiza sokoni bidhaa zilizofungwa kwa majani bila ruhusa au bidhaa zilizoharibika; (j) atatupa taka hovyo au kutiririsha maji machafu; (k) atafunga chumba cha biashara kwa madai ya kukitumia kama stoo au matumizi mengine yasiyoainishwa katika mkataba isipokuwa kwa ridhaa ya Halmashauri na kwa maeneo maalum kama ambavyo Halmashauri itaona inafaa; au 15 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) Adhabu Kufifilisha kosa (l) atafanya kitendo chochote ambacho kitapelekea uvunjifu wa amani na usalama au kukwamisha shughuli za soko. - 35 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa
AI-assisted research summary: A person convicted of an offence under the subsidiary legislation must pay a fine, face imprisonment, or both.
35. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo atawajibika kulipa faini ya kiasi kisichopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 36 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi ana uwezo wa kufifilisha kosa na kumtoza mtenda kosa shilingi 200,000 ikiwa anakiri kosa, yuko tayari kujaza fomu maalum ya Jedwali la Tano, na analipa ada au ushuru unaodaiwa.
36. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Tano na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. 16 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) ________________ JEDWALI LA KWANZA _________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5(1)) USHURU WA MASOKO NA MAGULIO Soko la Kawaida kwa siku 500 300 300 500 Soko la Kisasa kwa siku 1000 500 500 1500 Kwa mwezi Soko la kawaida 10,000 5000 5000 10,000 Kwa mwezi Soko la kisasa 20,000 10,000 10,000 30,000 1500 2,000 2500 3,000 3500 4,000 4500 5000 1000 2000 Na. Chanzo
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 5 Verify source ↗
Vyumba vya Biashara/Duka / Bucha
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaorodhesha aina za vyumba/vibanda na mipaka ya eneo kwa mita za mraba.
5. Vyumba vya Biashara/Duka / Bucha Namba 1 / Vibanda vya sokoni/Sehemu ya kuhifadhia Mizigo/Stoo/ Ofisi za sokoni/Vyumba vya barafu a. Eneo lenye mita za mraba 0-9 b. Eneo lenye Mita za mraba 10-15 c. Eneo lenye Mita za mraba 16-20 d. Eneo lenye Mita za mraba 21- na kuendelea. - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: The section lists how many items are counted for a tenga of different produce types.
6. Kuingiza sokoni gunia, tenga, robota la mitumba na kiroba (Tafsiri ya Tenga) a. Tenga tikiti 15 b. Tenga nanasi 35 c. Tenga la fenesi 10 d. Tenga la staferi 50 e. Tenga la maboga 15 - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaorodhesha madaraja ya gari linaloingiza mizigo kulingana na tani: 0–2.9, 3–3.9, na 4–6.9.
7. Gari inayoingiza mizigo yenye tani: a. 0 – 2.9 b. 3 – 3.9 c. 4 – 6.9 - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaonyesha ada/ushuru wa soko kwa uuzaji wa vichwa na miguu ya ng’ombe, mbuzi na kondoo katika eneo la Matenga, pamoja na viwango kadhaa vya fedha vilivyoorodheshwa.
8. d. 7 - na kuendelea Eneo la Matenga Uuzaji wa vichwa na miguu ya ng’ombe, mbuzi na kondoo 500/= 1,000/= 1,500/= 2000/= 2,500/= 3,000/= 3,500/= 3,000/= 500 kwa mtu 1000 kwa mtu 17 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) - 11 Verify source ↗
Ada ya Eneo la Machinjio ya Kuku ya
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinataja ada/eneo la machinjio ya kuku na namba 500 hadi 1000 kuku kwa mtu.
11. Ada ya Eneo la Machinjio ya Kuku ya 500 1000 kuku kwa mtu - 12 Verify source ↗
Wachukuzi wa mizigo walipe kwa
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaorodhesha ada/ushuru wa baadhi ya shughuli na watu wa soko, ikiwemo malipo ya kiasi fulani kwa wahusika kama wachukuzi wa mizigo na mafundi nguo kwa cherehani.
12. Wachukuzi wa mizigo walipe kwa 300 300 mtu Parking za Sokoni 13 14 Madalali 15 Magulio 16 Mafundi Nguo kwa Cherehani 500 kwa saa 1000 kwa mtu 500 kwa mtu 500 kwa mtu 1000 kwa saa 1500 kwa mtu 500/= kwa mtu 18 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) _____________ JEDWALI LA PILI ______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 7) KIBALI CHA MNADA
Part
JEDWALI LA PILI
- 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Hii ni fomu ya kuandika taarifa za mwombaji na taarifa za kibali, ikiwemo eneo la matumizi, muda wa kibali, masharti, na maelezo ya idhini.
9. Jina la Mwombaji ………………………………………........................ Anuani ya mwombaji ……………………………………….................. Kibali cha ………………………………………………….................... Eneo ambalo kibali hicho kitatumika………………………................... Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe……hadi tarehe………….................. Masharti ya kutumia kabali hicho a. b. c. d. Tarehe ya kikao iliyoidhinisha kibali………………………................... Muhtasari Na.……………....................................................................... a. Imesajiliwa na: b. Jina ………………………………. c. Saini……………………………… - 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: This section shows the application form for a temporary permit to use a market, with signature, date, and stamp lines.
12. Mkuu wa Soko Saini ya Mwombaji Tarehe …………………….....................Tarehe…………………… Mhuri…………………………………… 19 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) _____________ JEDWALI LA TATU _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 12(2)) FOMU YA MAOMBI YA KIBALI CHA KUTUMIA SOKO KWA MUDA FOMU NA. 1
Part
JEDWALI LA TATU
- 1 Verify source ↗
Jina la mwombaji ……………………………………..…………
AI-assisted research summary: Hii ni sehemu ya fomu inayotaja jina la mwombaji.
1. Jina la mwombaji ……………………………………..…………. - 2 Verify source ↗
Anwani/ Namba ya simu ya mwombaji ………………..……
AI-assisted research summary: This section is a form field for the applicant’s address and phone number.
2. Anwani/ Namba ya simu ya mwombaji ………………..…… - 5 Verify source ↗
Saini ya Mwombaji ………………Jina…………………………
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaonyesha nafasi ya saini ya mwombaji na jina lake.
5. Saini ya Mwombaji ………………Jina………………………… - 6 Verify source ↗
Tarehe …………………
AI-assisted research summary: This section contains a permit application form with spaces for local government opinions and a final council director decision approving or rejecting the application.
6. Tarehe ………………… MAONI YA UONGOZI WA SERIKALI YA KIJIJI Tarehe …………….. Muhuri ........................... Jina la kiongozi wa Mtaa ……………..……Saini……….…. MAONI YA AFISA MASOKO WA HALMASHAURI Tarehe …….. Muhuri Jina la kiongozi wa Mtaa …………Saini…………….…. MAONI YA AFISA MIPANGO MIJI WA HALMASHAURI ……………………………………………………………… Tarehe ……………………….. Jina la kiongozi wa Mtaa ……….………Saini……….…. Muhuri ……………. MAONI YA YA AFISA AFYA WA HALMASHAURI Tarehe ……………… Muhuri …………….……… Jina la kiongozi wa Mtaa ………………………Saini………………….…. MAAMUZI YA MKURUGENZI WA HALMASHAURI. Maombi ya Kibali yamekubaliwa /yamekataliwa kwa sababu…………………………........................ Tarehe ……………….. Muhuri …………………… Jina la Afisa Mwidhiniwa …………………………….… Saini……………………………………………..………… Cheo…………………………………………………………… 20 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) ___________ JEDWALI LA NNE ____________ (Limetengenezwa hini ya kanuni ya 26(1) KIBALI CHA KUTUMIA SOKO FOMU NA 2
Part
JEDWALI LA NNE
- 4 Verify source ↗
Eneo ambalo kibali hicho kitatumika…………………………………………………
AI-assisted research summary: This section is about the area where the permit applies.
4. Eneo ambalo kibali hicho kitatumika………………………………………………… - 5 Verify source ↗
Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe………hadi tarehe…………
AI-assisted research summary: The permit period runs from one date to another date.
5. Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe………hadi tarehe………… - 6 Verify source ↗
Masharti ya kutumia kibali hicho
AI-assisted research summary: Section 6 is titled “Masharti ya kutumia kibali hicho” (conditions for using that permit), but the visible text does not show the actual conditions.
6. Masharti ya kutumia kibali hicho (a)…………………………………………… (b)….. ……………………………………… (c)…………………………………………… (d)…………………………………………… - 7 Verify source ↗
Tarehe ya kikao iliyoidhinisha kibali……………………………
AI-assisted research summary: Heading: the date of the meeting that approved the permit.
7. Tarehe ya kikao iliyoidhinisha kibali…………………………….. - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: This section is a form for admitting a breach of the Kilwa District markets, fairs and auctions by-laws and stating willingness to pay the owed fee or tax plus a fine instead of being prosecuted in court.
8. Muhtasari Na.…………… Imesajiliwa na: Jina ……………………………………… Saini…………………………………….. Mkuu wa Soko Saini ya Mwombaji Tarehe …………………. Tarehe …………… Mhuri………………………………………….. 21 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) ______________ JEDWALI LA TANO ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 36) HATI YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi …………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya ………………………………………….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Kilwa, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. Jina…………………….. ya Mwezi…… Mwaka ……………. Saini……………………… MBELE YANGU : Jina:……………………………………..……………………... Saini………………………….…………………………..… Wadhifa: …………………………………………………… Tarehe…………………………………… 22 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la serikali Na. 1104 (linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imegongwa kwenye Sheria ndgo hizo kufuatia azimio lililopitishwa katika Mkutano mkuu wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya kilwauliofanyika tartehe 9/11/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- HANAN M. BAFAGHI, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya wilaya, Kilwa MHE. ISSA B. MATEKA, Mwenyekiti, Halmashauri ya wilaya, Kilwa L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Oktoba, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI 23
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko, Magulio na Minada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in