Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Kifungu hiki kinaweka jina la Sheria Ndogo kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Kifungu hiki kinaweka jina la Sheria Ndogo kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. This by-law applies in the area of Kilwa District Council. This section defines key terms used in the by-law. The operator of a transport vehicle must comply with the conditions set by this by-law. Wamiliki wa magari ya abiria na mizigo yanayotoka au kwenda mikoani na maeneo ya ndani na nje ya Halmashauri lazima waingie katika eneo lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na mizigo.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Showing 19 of 19
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaweka jina la Sheria Ndogo kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la
AI-assisted research summary: This by-law applies in the area of Kilwa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni malipo yanayolipwa Halmashauri kwa ajili ya kibali cha kuegesha chombo cha usafiri; “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “gari” maana yake ni chombo chochote kinachotumika kusafirisha abiria au mizigo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine isipokuwa mikokoteni, baiskeli na wanyama wanaotumika kubeba watu au mizigo; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, “kituo cha basi” maana yake ni kituo cha basi kilichoidhinishwa na Halmashauri ambapo mabasi 1 Sheria Ndogo Ya Ushuru Wa Stendi Na Maegesho Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa Tangazo la serikali Na.1106 (linaendelea) yanatoa huduma ya kushusha na kupakia abiria na mizigo; “maegesho” maana yake ni sehemu iliyotengwa au iliyoidhinishwa na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha magari; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa au afisa ya aliyeteuliwa Mkurugenzi; majukumu kutekeleza “mmiliki” maana yake ni mwenye gari na inajumuisha dereva au kondakta anayetumia gari; “stendi kuu” maana yake ni eneo lililoidhinishwa na Halmashauri ambapo magari yanayotoa huduma ya usafiri kwa umma kuelekea mikoani na maeneo yaliyo ndani na nje ya Halmashauri huanzia na kumalizia safari; “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, kampuni au taasisi iliyoingia mkataba kutekeleza jukumu lolote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. Wajibu wa muegeshaji - 4 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa muegeshaji wa chombo
AI-assisted research summary: The operator of a transport vehicle must comply with the conditions set by this by-law.
4. Itakuwa ni wajibu wa muegeshaji wa chombo cha usafiri kufuata masharti yaliyowekwa katika Sheria Ndogo hii. Wajibu wa mmiliki wa magari ya abiria na mizigo - 5 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa magari ya
AI-assisted research summary: Wamiliki wa magari ya abiria na mizigo yanayotoka au kwenda mikoani na maeneo ya ndani na nje ya Halmashauri lazima waingie katika eneo lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na mizigo.
5. Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa magari ya abiria na mizigo yanayotoka au kwenda mikoani na maeneo yaliyo ndani na nje ya Halmashauri, kuingia katika eneo lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na mizigo. Wajibu wa Halmashauri - 6 Verify source ↗
Halmashuri itakuwa na wajibu wa kusimamia
AI-assisted research summary: Halmashuri must supervise all parking areas established within the areas it administers and ensure this by-law is implemented.
6. Halmashuri itakuwa na wajibu wa kusimamia maegesho yote yatakayoanzishwa katika maeneo yote inasimamia ndani ya Halmashauri na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Maeneo ya maegesho - 7 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na uwezo wa kutenga
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kutenga maeneo ya maegesho ya magari na maeneo maalumu kwa pikipiki, bajaji na baiskeli, na pia lazima ibainishe idadi ya magari yanayopaswa kuegeshwa katika eneo lililotengwa.
7.-(1) Halmashauri itakuwa na uwezo wa kutenga eneo lolote la Halmashauri kwa madhumuni ya maegesho ya magari. 2 Sheria Ndogo Ya Ushuru Wa Stendi Na Maegesho Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa Tangazo la serikali Na.1106 (linaendelea) (2) Halmashauri itabainisha idadi ya magari yanayotakiwa kuegeshwa katika eneo lililotengwa kwa ajili ya maegesho. (3) Halmashauri au wakala anaweza kuainisha baadhi ya maeneo katika vijiji kuwa ni sehemu ya maegesho yaliyotengwa. (4) Halmashauri itatenga maeneo maalumu ya maegesho yatakayotumiwa na pikipiki na bajaji kwa ajili ya biashara na baiskeli. - 8 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa chombo cha usafiri cha
AI-assisted research summary: Wamiliki wa vyombo vya usafiri vya biashara wanaotaka kuegesha kwenye maeneo yaliyotengwa lazima wasajili chombo na wapate kibali, walipe ada ya kibali, na wasipark bila kibali kutoka Halmashauri.
8.-(1) Kila mmiliki wa chombo cha usafiri cha biashara ambaye anataka kuegesha chombo chake katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya maegesho kwa vyombo vya biashara, atatakiwa kusajili chombo chake na kupewa kibali. Ada ya kibali (2) Kila mmiliki wa chombo cha usafiri cha biashara atatakiwa kulipa ada ya kibali ambacho kitamuwezesha kuegesha chombo chake kwa muda na kama utaratibu inavyoelekezwa katika Jedwali la Kwanza. na Halmashauri utakaowekwa Usimamizi wa kituo cha mabasi (3) Itakuwa ni marufuku kwa mmiliki yeyote wa chombo cha usafiri cha biashara kuegesha chombo chake katika maegesho yaliyotengwa kwa ajili ya kuegesha vyombo vya biashara bila kuwa na kibali cha kuegesha katika maeneo hayo kutoka Halmashauri. (4) Mtu yeyote atapaswa kuegesha chombo chake cha usafiri katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya maegesho kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. - 9 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni marufuku kwa basi lolote
AI-assisted research summary: Buses may only load or unload passengers at designated bus stations in the Council area, and buses on local trips must stop there for no more than five minutes; the Council can also designate bus station or parking areas.
9.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa basi lolote kushusha au kupakia abiria katika eneo la Halmashauri isipokuwa kwenye maeneo yaliyoainishwa kuwa vituo vya mabasi. lolote (2) Mabasi yote yanatakiwa kuanza safari zake katika vituo vya mabasi vilivyoainishwa na Halmashauri, isipokuwa kwa kibali maalum kutoka Halmashauri. (3) Mabasi yote yanayofanya safari za ndani ya eneo la Halmashauri yatatakiwa kusimama katika kituo cha mabasi kwa lengo la kushusha au kupakia abiria kwa 3 Sheria Ndogo Ya Ushuru Wa Stendi Na Maegesho Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa Tangazo la serikali Na.1106 (linaendelea) muda usiozidi dakika tano, isipokuwa kwa kituo cha kuanzia na kumalizia safari. (4) Itakuwa ni marufuku kwa mmiliki wa basi au gari la aina nyingine kufanya matengenezo ndani ya kituo cha basi au katika eneo lililotengwa kwa ajili ya maegesho. (5) Bila kuathiri masharti mengine ya Sheria Ndogo hii, Halmashauri itakuwa na uwezo wa kutangaza au kutenga eneo lolote kuwa kituo cha mabasi au maegesho kama itakavyoona inafaa. - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru kutoka kwa kila
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge parking fees from each vehicle owner who parks in parking areas or a bus station, using the rates set out in the Second Schedule.
10.-(1) Halmashauri itatoza ushuru kutoka kwa kila mmiliki wa gari lililoegeshwa katika sehemu za maegesho au kituo cha mabasi kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. (2) Ushuru wa maegesho unaweza kulipwa kwa saa, siku, mwezi au mwaka. (3) Mmiliki wa gari atakayelipia ushuru wa maegesho kwa siku, mwezi au kwa mwaka ataruhusiwa kuegesha gari lake katika eneo lolote lililotengwa kwa ajili ya maegesho kwa muda aliolipia bila kudaiwa tena.
Part
Jedwali la Pili.
- 11 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakayehitaji kupangiwa
AI-assisted research summary: Anyone who wants private parking must apply to the Council or Agency.
11.-(1) Mtu yeyote atakayehitaji kupangiwa maegesho binafsi atawasilisha maombi kwa Halmashauri au Wakala. (2) Baada ya maombi kukubaliwa, mwombaji atawajibika kulipa ushuru wa maegesho yaliyotengwa kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili na ataruhusiwa kutumia sehemu hiyo peke yake bila kuingiliwa. (3) Mtu aliyetengewa eneo kwa ajili ya maegesho binafsi atalipia ushuru wa maegesho endapo atatumia maegesho tofauti na eneo alilotengewa. - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa stendi kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri inatoza ushuru wa stendi kwa magari yanayoingia maeneo ya stendi, na wamiliki wa magari yanayotumia stendi kuu lazima walipe ushuru huo.
12.-(1) Halmashauri itatoza ushuru wa stendi kwa magari yote yanayoingia katika Stendi Kuu ya mabasi na maeneo mengine yaliyotengwa kwa matumizi ya stendi kwa namna na kiasi kilichoainishwa katika Jedwali la Tatu. (2) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa gari au chombo chochote cha usafiri kinachotumia stendi kuu au 4 Ushuru wa maegesho Maegesho maalum Ushuru wa stendi Sheria Ndogo Ya Ushuru Wa Stendi Na Maegesho Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa Tangazo la serikali Na.1106 (linaendelea) Ushuru wa kulaza gari Gari lililotelekezwa eneo lingine linalotumika kama stendi kulipa ushuru wa stendi. (3) Ushuru wa stendi utalipwa kila gari linapotoka kituoni kuanza au kuendelea na safari zake. - 13 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa kulaza gari
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itozeshe ushuru wa kulaza gari kwa magari yanayolazwa stendi au eneo jingine lililotengwa.
13.-(1) Halmashauri itatoza ushuru wa kulaza gari stendi au katika eneo lingine lililotengwa kwa matumizi hayo. (2) Ushuru wa kulaza gari utatozwa kwa kila gari lililolazwa stendi au eneo lililotengwa kwa siku kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Nne . - 14 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kuegesha gari zaidi ya muda ambao tayari amelipia ushuru.
14.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuegesha gari zaidi ya muda aliolipia ushuru. (2) Mtu yeyote atakayekiuka kanuni ndogo ya (1) atahesabika kuwa ametelekeza gari na Halmashauri au Wakala anaweza kulifunga gari hilo kwa minyororo hadi hapo mtu huyo atakapolipa ushuru anaodaiwa pamoja na faini. (3) Gari ambalo litakuwa limefungwa minyororo zaidi ya saa mbili bila kulipiwa ushuru pamoja na faini litavutwa na kupelekwa kwenye eneo litakaloainishwa na Halmashauri na gharama za kulivuta zitakuwa juu ya mmiliki. (4) Mmiliki wa gari ambalo litavutwa na kuhifadhiwa na Halmashauri ataruhusiwa kuchukua gari baada ya kulipa ushuru unaodaiwa, gharama ya utunzaji, gharama za uvutaji na gharama nyingine ambazo kwa namna moja au nyingine Halmashauri au Wakala atakuwa amegharimia na mmiliki atapewa gari hilo baada ya kutoa uthibitisho wa umiliki wa gari. (5) Gharama ya utunzaji wa gari itakuwa ni shilingi elfu thelathini kwa siku. Zuio la kuegesha gari. - 15 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kuzuia maegesho ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuzuia maegesho ya magari kwa kuweka alama ya “hakuna kuegesha hapa” au “no parking”.
15. Halmashauri inaweza kuzuia maegesho ya magari katika sehemu yoyote kwa kuweka alama “hakuna kuegesha hapa” au “no parking” kwa sababu zifuatazo: (a) kurahisisha mzunguko wa magari; (b) ujenzi au ubomoaji unafanyika katika eneo husika; na 5 Sheria Ndogo Ya Ushuru Wa Stendi Na Maegesho Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa Tangazo la serikali Na.1106 (linaendelea) Magari yaliyosamehewa kulipa ushuru Makosa (c) ikiwa magari kuegeshwa katika sehemu hiyo inayofanyika kwa kutakwamisha shughuli wakati huo. - 16 Verify source ↗
(1) Magari yafuatayo yamesamehewa kulipa
AI-assisted research summary: Baadhi ya magari yamesamehewa kulipa ushuru wa maegesho, na Halmashauri inaweza kutoa msamaha wa ziada kwa gari lingine kwa kibali maalum.
16.-(1) Magari yafuatayo yamesamehewa kulipa ushuru wa maegesho chini ya Sheria Ndogo hii: (a) magari yote ya mabalozi na wanadiplomasia; (b) magari ya kubebea wagonjwa; (c) magari ya Serikali; (d) magari ya Jeshi; (e) magari ya Zimamoto; na (f) magari yote yanayotumika kwa ajili ya usafi katika eneo la Halmashauri. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri inaweza kusamehe gari lingine lolote kulipa ushuru wa maegesho iwapo itaridhika na sababu za mwombaji na msamaha huo utatolewa kwa kibali maalum kutoka kwa Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa. - 17 Verify source ↗
Mtu yeyote anatenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaorodhesha vitendo vinavyotendwa kosa kuhusu ada/ushuru, maegesho, kuzuia maafisa, na wajibu wa wakala aliyechaguliwa na Halmashauri.
17. Mtu yeyote anatenda kosa endapo- (a) atashindwa kulipa ada au ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) atamshawishi mtu au kundi la watu kukwepa au kukataa kulipa ada au ushuru; (c) atamzuia Mkurugenzi, afisa mwidhiniwa au wakala kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (d) atashindwa, atadharau, atakaidi au kukataa kutekeleza alilopewa na Halmashauri kuhusiana na ulipaji wa ada au ushuru chini ya Sheria Ndogo hii; lolote agizo (e) ataegesha gari, pikipiki au bajaji bila kulipa ushuru wa maegesho; (f) ataegesha gari, pikipiki au bajaji katika eneo lisiloruhusiwa; (g) ataegesha gari nje ya mstari uliochorwa kuainisha eneo la kuegesha gari; (h) ataosha gari, pikipiki au bajaji kwenye maegesho; 6 Sheria Ndogo Ya Ushuru Wa Stendi Na Maegesho Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa Tangazo la serikali Na.1106 (linaendelea) (i) atafanya matengenezo ya gari, pikipiki au bajaji kwenye kituo cha basi au kwenye eneo la maegesho; au (j) ataegesha vibaya na kuzuia magari mengine la kuegeshwa au kutoka kwenye eneo maegesho. (2) Wakala aliyeteuliwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii atatenda kosa endapo- (a) atatumia nyaraka za kugushi kwa nia ya kujipatia manufaa yatokanayo na ukusanyaji wa ada au ushuru ndani ya Halmashauri; (b) atashindwa kutoa taarifa au atatoa taarifa za uongo Halmashauri kuhusu bidhaa au huduma zinazotakiwa kulipiwa ada au ushuru; (c) hatawasilisha au atawasilisha kwa kuchelewa makusanyo ya ada au ushuru Halmashauri kulingana na muda aliopewa kwa mujibu wa mkataba; au (d) atashindwa kutunza kumbukumbu sahihi za malipo ya ada au ushuru. - 18 Verify source ↗
(1) Mtu atakayepatikana na hatia kwa kutenda
AI-assisted research summary: Mtu akitiwa hatiani kwa kosa chini ya Sheria Ndogo hii anaweza kutozwa faini, kufungwa jela, au vyote viwili.
18.-(1) Mtu atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote. (2) Endapo mtu aliyepatikana na hatia ni wakala, pamoja na adhabu iliyoainishwa katika kanuni ndogo ya (1) atalipa Halmashauri kiasi cha pesa alizopaswa kulipa au zilizopaswa kulipwa na mlipa ada au ushuru. - 19 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa na kumtoza mkosaji kiasi kisichozidi shilingi laki mbili ikiwa mkosaji anakiri kwa hiari na anajaza fomu maalumu.
19. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tano. 7 Adhabu Kufifilisha kosa Sheria Ndogo Ya Ushuru Wa Stendi Na Maegesho Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa Tangazo la serikali Na.1106 (linaendelea) Na. i. ii. iii. iv. v. vi. vii. viii. ix. ____________________ JEDWALI LA KWANZA _____________________ (Limetenegenezwa chini ya kanuni ya 8(2) ADA YA KIBALI Aina ya Gari Teksi Gari dogo la mizigo Lori kuanzia chini ya tani 5 Lori kuanzia tani 5 hadi tani 10 Lori zaidi ya tani 10 Pick up Aina nyingine za magari Pikipiki ya matairi mawili Pikipiki ya matairi matatu/Bajaji ______________ JEDWALI LA PILI ______________ Kiasi cha Ada 7,500/= 6,500/= 8,000/= 10,000/= 15,000/= 5,000/= 10,000/= 5,000/= 5,000/= (Limetenegezwa chini ya kanuuni ya 10(1) na 11(2)) USHURU WA MAEGESHO Na. Aina ya Gari i. ii. iii. iv. v. vi. vii. viii. ix. x. Teksi Gari dogo Lori kuanzia chini ya tani 5 Lori kuanzia tani 5 hadi tani 10 Lori zaidi ya tani 10 Pick up Aina magari Pikipiki ya matairi mawili Pikipiki ya matairi matatu Magari ambayo hayakutajwa nyingine mengine za Kiasi cha ushuru kwa saa 200/= 200/= 300/= Kiasi cha ushuru kwa siku 1,000/= 1,000/= 2,000/= cha Kiasi ushuru kwa mwezi 20,000/= 20,000/= 50,000/= Egesho lililotengwa kwa mwaka 200,000/= 200,000/= 500,000/= 400/= 4,000/= 100,000/= 1,000,000/= 500/= 200/= 200/= 5,000/= 1,000/= 1,000/= 130,000/= 20,000/= 20,000/= 1,300,000/= 200,000/= 200,000/= 100/= 100/= 3,000/= 36,000/= 100/= 100/= 3,000/= 36,000/= 200/= 1,000/= 20,000/= 200,000/= 8 Sheria Ndogo Ya Ushuru Wa Stendi Na Maegesho Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa Tangazo la serikali Na.1106 (linaendelea) _______________ JEDWALI LA TATU _______________ (Limetenegezwa chini ya kanuni ya 12(1)) USHURU WA MAGARI YANAYOINGIA STENDI Na. Aina ya Gari Kiasi cha ushuru kwa safari moja (Tripu) i. ii. iii. iv. v. vi. vii. viii. ix. x. xi. Teksi Bajaji Pikipiki Basi la abiria kuanzua 5-15. Basi la abiria chini ya 25 Basi la abiria kuanzia 26-65 Gari dogo la mizigo Gari kubwa la mizigo Magari mengineyo madogo Magari mengineyo makubwa Magari mengine ambayo hayakutajwa 500/= 300/= 200/= 500/= 1,000/= 3,000/= 500/= 2,000/= 500/= 2,000/= 2,000/= Na. i. ii. iii. iv. v. vi. vii. viii. ix. x. xi. xii. xiii. xiv. xv. _____________ JEDWALI LA NNE ______________ (Limetenegezwa chini ya kanuni ya 13(2)) USHURU WA KULAZA MAGARI Aina ya Gari Basi la abiria zaidi ya 40. Basi la abiria chini ya 40 Basi la abiria chini ya 20 Teksi Gari dogo la kawaida Pick up/ Station Wagon Guta Pikipiki ya matairi mawili Pikipiki ya matairi matatu Gari la mizigo chini ya tani 5 Gari la mizigo kuanzia tani 5 hadi 10 Gari la mizigo zaidi ya tani 10 Magari mengineyo madogo Magari mengineyo makubwa Magari mengine ambayo hayakutajwa 9 Sheria Ndogo Ya Ushuru Wa Stendi Na Maegesho Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa Tangazo la serikali Na.1106 (linaendelea) ______________ JEDWALI LA TANO _______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 19) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi …………………………………………… NAKIRI KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya ………………………….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Kilwa, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. NAKUBALI kulipa ada au ushuru ninaodaiwa kwa kiasi cha shilingi ................ pamoja na faini ya kufifilisha kosa kwa kiasi cha shilingi ................... NATHIBITISHA KWAMBA, maelezo niliyotoa hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa MIMI MWENYEWE na kwa hiari yangu kadri ya ufahamu wangu. Leo hii tarehe………….ya mwezi…………..… mwaka 20……………. Jina………………………………..... Saini………........………………...... MBELE YA MKURUGENZI Jina:…………………..................................... Saini:…………………..….............................. Tarehe:.............................................................. 10 Sheria Ndogo Ya Ushuru Wa Stendi Na Maegesho Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilwa Tangazo la serikali Na.1106 (linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imegongwa kwenye Sheria ndgo hizo kufuatia azimio lililopitishwa katika Mkutano mkuu wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya kilwauliofanyika tartehe 9/11/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- HANAN M. BAFAGHI, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya wilaya, Kilwa MHE. ISSA B. MATEKA, Mwenyekiti, Halmashauri ya wilaya, Kilwa L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Oktoba, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in