Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
This provision gives the by-law its official title.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the by-law its official title. This by-law applies within the area of Kilwa District Council. This section defines key terms used in the By-law, including authorized officer, gulio, Council, mixed produce, Director, buyer, transporter, seller, tax, and agent. Halmashauri itatoza ushuru wa mazao mchanganyiko wa 3% ya bei ya kununulia kwa mazao yote yanayosafirishwa yaliyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza, na ushuru huo ulipwe kwa Halmashauri. People liable for this levy must pay at the rate set in regulation 4, may not buy produce in the Council area without an approved business licence, and anyone intending to transport produce out of the Council area must have the special permit listed in the Second Schedule.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Showing 16 of 16
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This provision gives the by-law its official title.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la
AI-assisted research summary: This by-law applies within the area of Kilwa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the By-law, including authorized officer, gulio, Council, mixed produce, Director, buyer, transporter, seller, tax, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “gulio” maana yake ni eneo au sehemu yoyote ya wazi au iliyojengwa ambayo imetengwa na Halmashauri kwa ajili ya shughuli za kuuza na kununua mazao na bidhaa nyingine, na itajumuisha chama cha ushirika cha msingi kilichoteuliwa kuuza mazao mchanganyiko; “Halmashauri” maana yake Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa; “mazao mchanganyiko” maana yake ni mazao ya chakula, mazao ya biashara na mazao ya misitu na maliasili ambayo huzalishwa na kupatikana katika eneo la Halmashauri, isipokuwa zao la korosho; 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na. 1107(linaendelea.) Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa au afisa aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mnunuzi” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu au taasisi yoyote inayojishughulisha na ununuzi wa mazao mchanganyiko katika eneo la Halmashauri kwa nia ya kufanya biashara; “msafirishaji” maana yake ni mtu binafsi, kampuni au taasisi inayosafirisha mazao mchanganyiko; “muuzaji” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, kampuni au taasisi inayojishughulisha na uuzaji wa mazao mchanganyiko katika eneo la Halmashauri; “ushuru” maana yake ni malipo yanayotozwa na kulipwa kwa Halmashauri kama kodi ya bidhaa au huduma inayotolewa; “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, kampuni au taasisi iliyoingia mkataba kutekeleza Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. Utozaji wa ushuru - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa mazao
AI-assisted research summary: Halmashauri itatoza ushuru wa mazao mchanganyiko wa 3% ya bei ya kununulia kwa mazao yote yanayosafirishwa yaliyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza, na ushuru huo ulipwe kwa Halmashauri.
4.-(1) Halmashauri itatoza ushuru wa mazao mchanganyiko kwa kiwango cha asilimia tatu (3%) ya bei ya kununulia mazao kwa ajili ya mazao yote yanayosafirishwa kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (2) Ushuru unaotozwa chini ya Sheria Ndogo hii utalipwa kwa Halmashauri na utakusanywa na Halmashauri Halmashauri itakavyoelekeza. wakala kadri au (3) Mtu yeyote hataruhusiwa- (a) kununua au kusafirisha mazao bila kulipia ushuru; au (b) kuuza au kununua mazao mchanganyiko katika eneo ambalo si gulio. Wajibu wa kulipa ushuru - 5 Verify source ↗
Mtu anayepaswa kulipa ushuru kwa mujibu wa
AI-assisted research summary: People liable for this levy must pay at the rate set in regulation 4, may not buy produce in the Council area without an approved business licence, and anyone intending to transport produce out of the Council area must have the special permit listed in the Second Schedule.
5. Mtu anayepaswa kulipa ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii atalipa kwa kuzingatia kiwango kilichoainishwa katika kanuni ya 4 na hataruhusiwa kununua mazao katika eneo la Halmashauri bila kuwa na leseni ya biashara iliyoidhinishwa na Halmashauri. 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na. 1107(linaendelea.) Malipo ya ushuru Stakabadhi za malipo za kieletroniki Ukusanyaji wa madeni (2) Mtu yeyote anayekusudia kusafirisha mazao kutoka katika eneo la Halmashauri atapaswa kuwa na kibali maalum kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. kusafirishia mazao cha - 6 Verify source ↗
(1) Malipo ya ushuru yatafanyika kabla au
AI-assisted research summary: Ushuru unalipwa kabla au wakati wa kupokea huduma inayotozwa ushuru, au kwa muda/mfumo mwingine unaokubaliwa na Halmashauri na mlipa ushuru.
6.-(1) Malipo ya ushuru yatafanyika kabla au wakati wa kupokea huduma inayotozwa ushuru chini ya Sheria Ndogo hii. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), ushuru unaweza kulipwa muda wowote katika siku husika, mwezi husika au kwa namna nyingine itakayokubalika baina ya Halmashauri na mlipa ushuru. - 7 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri must issue an electronic receipt as proof of levy payment, and every mixed-produce levy payer must ask for and verify that receipt.
7.-(1) Halmashauri ya kielektroniki kwa ushuru utakaotozwa na kulipwa kama ushahidi wa malipo yaliyofanyika kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. stakabadhi itatoa (2) Kila mlipa ushuru wa mazao mchanganyiko atakuwa na wajibu wa kudai na kuhakiki stakabadhi ya malipo kulingana na kiasi cha fedha alicholipa. - 8 Verify source ↗
(1) Endapo mlipa ushuru atashindwa kulipa
AI-assisted research summary: If a taxpayer does not pay the mixed produce tax on time, the council may recover the debt by seizing property, then sell it by auction after 30 days, with prior notice of up to 7 days.
8.-(1) Endapo mlipa ushuru atashindwa kulipa ushuru wa mazao mchanganyiko ndani ya muda aliopewa na hivyo kusababisha deni, Halmashauri baada ya kupata amri ya mahakama inaweza kukusanya deni hilo kwa kukamata mali zenye thamani sawa na deni la ushuru pamoja na gharama za kukamata za mtu binafsi, kikundi, kampuni au shirika lililoshindwa kulipa deni husika (2) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuuza mali za mdaiwa kwa njia ya mnada baada ya siku thelathini kupita tangu kukamatwa kwa mali za mdaiwa. (3) Kwa mali zinazoweza kuharibika kwa haraka, Halmashauri baada ya kupata kibali cha mahakama itakuwa na uwezo wa kuuza mali hizo kabla hazijaharibika. (4) Bila kuathiri masharti ya kanuni hii, kabla ya kuuza mali yoyote iliyokamatwa, Halmashauri itatoa taarifa ya siku zisizozidi saba kwa mdaiwa na umma kuhusu kusudio la kuuza mali hizo. 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na. 1107(linaendelea.) (5) Halmashauri haitawajibika kwa hasara itakayotokea wakati wa kukusanya madeni au kwa mali itakayokamatwa na kushikiliwa na Halmashauri, isipokuwa kama hasara hiyo itakuwa imesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri au wakala. Uteuzi wa Wakala - 9 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kuteua wakala kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala, na wakala huyo lazima akusanye na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri.
9.-(1) Halmashauri inaweza kuteua wakala kwa ajili ya kutekeleza majukumu chini ya Sheria Ndogo hii. (2) Wakala atakayeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa: (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria Ndogo hii; na (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. Mamlaka ya kuingia katika eneo la biashara - 10 Verify source ↗
Mkurugenzi au afisa mwidhiniwa atakuwa na
AI-assisted research summary: Mkurugenzi au afisa mwidhiniwa ana mamlaka ya kuingia katika eneo, jengo au chombo cha usafiri wakati wowote kwa ajili ya kukusanya ushuru, kufanya tathmini, au kushughulikia mambo yanayohusu ushuru, leseni au kibali.
10. Mkurugenzi au afisa mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya kuingia katika eneo, jengo au chombo cha usafiri kwa muda wowote kwa nia ya kukusanya ushuru, kufanya tathmini au kufanya jambo lolote linalohusu ushuru, leseni au kibali kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Bidhaa iliyokamatwa pasipo kulipiwa ushuru - 11 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza kwa kila siku kiasi cha
AI-assisted research summary: Halmashauri hutoza ada ya kila siku ya asilimia tano ya thamani ya bidhaa iliyokamatwa ikiwa zilisafirishwa bila kulipiwa ushuru, na inaweza kuziuza kwa mnada kama mmiliki halipi ushuru ndani ya siku saba.
11.-(1) Halmashauri itatoza kwa kila siku kiasi cha iliyokamatwa thamani ya bidhaa tano ya asilimia ikisafirishwa pasipo kulipiwa ushuru. (2) Mmiliki wa bidhaa iliyokamatwa asipolipa ushuru husika ndani ya siku saba kuanzia siku ambayo bidhaa imekamatwa, Halmashauri itauza bidhaa husika kwa njia ya mnada kwa ajili ya kufidia gharama za kukamata, kuhifadhi bidhaa na ushuru unaodaiwa. (3) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo ya (2), masharti yaliyowekwa kwenye kanuni ya 8 yatatumika. Muda wa ununuzi - 12 Verify source ↗
(1) Muda wa kununua na kuuza mazao utaanza
AI-assisted research summary: Buying and selling produce is allowed only from midnight to noon, unless the Council or Agency has special permission from the Director to trade after that time.
12.-(1) Muda wa kununua na kuuza mazao utaanza saa kumi na mbili alfajiri na kuisha saa kumi na mbili jioni. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri au Wakala, kwa kibali maalum kutoka kwa 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na. 1107(linaendelea.) Mkurugenzi, anaweza kuuza au kununua mazao baada ya muda uliotajwa. Makosa - 13 Verify source ↗
(1) Mtu atatenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu au wakala aliyeteuliwa na Halmashauri anaweza kutenda kosa ikiwa hafanyi au akifanya vitendo vilivyoorodheshwa kuhusu ulipaji na ukusanyaji wa ushuru.
13.-(1) Mtu atatenda kosa endapo- (a) atashindwa kulipa ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) atamshawishi mtu au kundi la watu kukwepa au kukataa kulipa ushuru; (c) atamzuia Mkurugenzi, afisa mwidhiniwa au wakala kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (d) atatoa taarifa za uongo kwa Mkurugenzi, afisa mwidhiniwa au wakala kuhusu huduma zinazohitaji kulipiwa ushuru; (e) atashindwa kuweka kumbukumbu au maelezo yoyote yatakayohitajika na Halmashauri; (f) atashindwa, atadharau, atakaidi au kukataa kutekeleza na Halmashauri kuhusiana na ulipaji wa ushuru chini ya Sheria Ndogo hii; alilopewa lolote agizo (g) atatengeneza, ataidhinisha atatayarisha, kutengeneza au atatunza nyaraka za uongo kwa nia ya kujipatia manufaa yatokanayo na ukusanyaji wa ushuru ndani ya Halmashauri; au (h) atatumia chombo chochote kusafirishia bidhaa ambayo haijalipiwa ushuru. (2) Wakala aliyeteuliwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii atatenda kosa endapo- (a) atatumia nyaraka za kugushi kwa nia ya kujipatia manufaa yatokanayo na ukusanyaji wa ushuru ndani ya Halmashauri; (b) atashindwa kutoa taarifa au atatoa taarifa za uongo Halmashauri kuhusu bidhaa au huduma zinazotakiwa kulipiwa ushuru; (c) hatawasilisha au atawasilisha kwa kuchelewa makusanyo ya ushuru Halmashauri kulingana na muda aliopewa kwa mujibu wa mkataba; au (d) atashindwa kutunza kumbukumbu sahihi za malipo ya ushuru. 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na. 1107(linaendelea.) Adhabu - 14 Verify source ↗
(1) Mtu atakayepatikana na hatia kwa kutenda
AI-assisted research summary: A person convicted of an offence under this bylaw must pay a fine, serve jail time, or both. If the convicted person is an agent, they must also pay the Council the money they were required to pay, or that the taxpayer was required to pay.
14.-(1) Mtu atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichopungua miezi sita jela na kisichozidi miezi kumi na mbili jela au vyote kwa pamoja. (2) Endapo mtu aliyepatikana na hatia ni wakala, pamoja na adhabu iliyoainishwa katika kanuni ndogo ya (1) atalipa Halmashauri kiasi cha pesa alizopaswa kulipa au zilizopaswa kulipwa na mlipa ushuru. Kufifilisha kosa - 15 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza faini ya hadi shilingi laki mbili kwa mtu aliyevunja Sheria Ndogo hii ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu.
15. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu. 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na. 1107(linaendelea.) _________________ JEDWALI LA KWANZA __________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(2)) MAZAO MCHANGANYIKO YATAKAYOLIPIWA USHURU MAZAO KIASI CHA USHURU 3% ya bei ya kununulia mazao Na.
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaonyesha fomu ya kibali cha kusafirisha mazao na fomu ya kukiri kosa, pamoja na uidhinishaji wa afisa na mkurugenzi.
16. Mahindi Mpunga Ufuta Mbaazi Kunde Choroko Maharage Machungwa Nanasi Ndizi Machenza Tikiti Nyanya Vitunguu Maembe Nazi 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na. 1107(linaendelea.) ____________ JEDWALI LA PILI ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5(2)) KIBALI CHA KUSAFIRISHA MAZAO Namba ya kibali…………………….. Tarehe ……………………... Msimu…………………………. Zao ……………………… Jina la mnunuzi………………………………………………………………………….. Idadi ya Tani/Kilo za awali…………………………………………………………… Kiasi kilichonunuliwa………………………………………………… Jumla ya Tani/Kilo…………………………………………………………………. Kiasi kinachosafirishwa………………………………………………………………… Kiasi kilichobaki……………………………………………………………………….. Namba ya stakabadhi ya ushuru……………………………………………………….. PDN ya chama cha msingi/Stakabadhi………………………………………………… Tarehe ya kusafirisha………………………………………………………………….. Jina la Dereva………………Na. ya Gari……………… Jina la Afisa aliyeidhinisha mzigo……………………….Saini……………………… Mhuri na saini ya Mkurugenzi/Mweka hazina 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na. 1107(linaendelea.) ________________ JEDWALI LA TATU ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 15) FOMU YA KUKIRI KOSA Mimi ……………………………………………………..………… NAKIRI KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Kilwa, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024. NAKUBALI kulipa ushuru ninaodaiwa kwa kiasi cha shilingi ..................... pamoja na faini ya kufifilisha kosa kwa kiasi cha shilingi ................... NATHIBITISHA KWAMBA, maelezo niliyotoa hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa MIMI MWENYEWE na kwa hiari yangu kadri ya ufahamu wangu. Leo hii tarehe………….ya mwezi…………..… mwaka 20……………. Jina………………………………..... Saini………........………………...... MBELE YA MKURUGENZI Jina:…………………..................................... Saini:…………………..….............................. Tarehe:.............................................................. 9 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tangazo la Serikali Na. 1107(linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imegongwa kwenye Sheria ndgo hizo kufuatia azimio lililopitishwa katika Mkutano mkuu wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya kilwauliofanyika tartehe 9/11/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- HANAN M. BAFAGHI, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya wilaya, Kilwa MHE. ISSA B. MATEKA, Mwenyekiti, Halmashauri ya wilaya, Kilwa L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Oktoba, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI 10
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao Mchanganyiko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in