Tanzania Regulation

Parliament of Tanzania

KANUNI ZA UGOMBOAJI NA UONDOSHAJI WA BIDHAA ZA KIPEKEE ZA MWAKA 2025

Kanuni hizi zinaitwa Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee za Mwaka 2025. Kanuni hizi zinatumika kwa Shirika, mteja, au mtu wa tatu wakati wa kutoa au kupokea huduma za ugomboaji na uondoshaji wa bidhaa…

cargo claimscargo clearancecargo damagecargo deliverycargo documentationcargo handlingcargo liabilityclaims for damagesclearance and removal servicescommissioncompensationcomplaints handlingcontract performancecustomer compensationcustomer defaultcustomer fundscustomer informationcustomer propertycustoms clearancedata handlingdebt recoverydelay chargesdelivery confirmationdocument retentionemployee conductescrow accountfee collectionfeesfees and chargesfreight servicesgoods receiptimport/exportinsuranceinvoicingliabilityBusiness registrationlogisticsloss of moneymaritime servicespayment enforcementpayment processingpaymentspublic procurementpublication requirementsregistrationriskservice contractsservice deliveryservice fees and commissionsservice outsourcingservice pricingservice provisionshippingshipping agencyshipping documentationshipping servicesTax lawthird-party service contractingthird-party service paymentsthird-party servicestransaction cancellationtransaction recordstransporttransport and logisticstransport documentationtrust accountvaluation

Publicly available, excluded from search-engine indexing

This page remains available for direct research for the following reasons:

  • The record does not meet this release's canonical indexing criteria. (market-indexing-disabled)
  • The record does not meet this release's canonical indexing criteria. (emergency-noindex)

Professional statute overview

Enactment structure, operative effect and source provenance

Official source

01

Purpose and legislative effect

“Kanuni hizi zinaitwa Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee za Mwaka 2025.”

Kanuni hizi zinaitwa Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee za Mwaka 2025. Kanuni hizi zinatumika kwa Shirika, mteja, au mtu wa tatu wakati wa kutoa au kupokea huduma za ugomboaji na uondoshaji wa bidhaa za kipekee kwa uingizaji au uuzaji nje kutoka Tanzania Bara. This section defines terms used in the regulations, including “Law,” “Board,” cargo documents, chemicals, customer, ship agent documents, shipping documents, and other related terms. Shirika lazima litoe huduma maalum za ugomboaji na uondoshaji kwa bidhaa fulani zinazoingia au kutoka nchini, na linaweza kutoza ada au kamisheni ya huduma hiyo. Shirika must provide specified customs and freight services when performing exclusive functions under regulation 4, and it must follow set performance standards.

02

How the instrument operates

  1. 01

    Start with the recorded version

    Legal dates not recorded. The date shown identifies this source expression and should not be treated as proof that no later change exists.

  2. 02

    Locate the controlling provision

    Use the provision map, part headings and full-text filter to move from the broad subject to the exact legal language.

  3. 03

    Read conditions and exceptions together

    Keep subsections, definitions, provisos and cross-references in context before drawing a legal conclusion.

  4. 04

    Verify currency and official wording

    Confirm later legislation, commencement notices and corrections with the official publisher before advice, filing or reliance.

03

Research entry points

Selected provisions across the instrument. Open any row to continue with the exact stored text.

2

Kanuni hizi zinaitwa Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee za Mwaka 2025.

Section 1

Masharti ya utoaji wa huduma

Mtu wa tatu lazima azingatie masharti ya makubaliano ya kutoa huduma na afanye kazi kwa uangalifu, weledi, uadilifu na uaminifu wakati wa kazi za mkataba na Shirika.

Section 10

Malipo ya sehemu ya utendaji

If a transaction cannot be completed because of customer fault, Shirika may recover the agency fee and completed costs, and the customer must also pay related costs such as applicable taxes and duties.

Section 19

Wastani wa jumla

Shirika linastahili fidia kwa madai ya wastani wa jumla yanayoweza kufanywa dhidi ya mteja, na mteja anatakiwa kutoa dhamana inapohitajika na Shirika.

Section 27

Tathmini ya fidia

Kanuni za Huduma ya Biashara ya Meli Tanzania za Mwaka 2020 zimefutwa.

Section 36

04

Source and current-law status

Source record view

Source record from oagmis.oag.go.tz · Legal dates not recorded

Verify current force

The source record does not state a definitive current-law status. Check the official publisher and later amendments before relying on this text.

Source-indexed provision map

Sections and provisions

Search by section, heading, part or exact legal wording. Every result remains linked to the stored source record.

Showing 36 of 36 provisions

Provision 36
§ 12Provision

Kanuni hizi zinaitwa Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee za Mwaka 2025.

1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee za Mwaka 2025.
§ 23Provision

Kanuni hizi zinatumika kwa Shirika, mteja, au mtu wa tatu wakati wa kutoa au kupokea huduma za ugomboaji na uondoshaji wa bidhaa za kipekee kwa uingizaji au uuzaji nje kutoka Tanzania Bara.

2. Kanuni hizi zitatumika kwa Shirika, mteja au mtu wa tatu wakati wa kutekeleza au kupokea huduma za ugomboaji na uondoshaji wa bidhaa za kipekee katika kuingiza ndani ya nchi au kutoa nje ya nchi kutoka Tanzania Bara. Tafsiri Sura ya 415
§ 34Provision

This section defines terms used in the regulations, including “Law,” “Board,” cargo documents, chemicals, customer, ship agent documents, shipping documents, and other related terms.

3. Katika Kanuni hizi isipokuwa kama muktadha unahitaji vinginevyo: “Sheria” maana yake ni Sheria ya Uwakala wa Meli Sura ya 415 “Bodi” maana yake ni Bodi ya Wakurugenzi iliyoanzishwa Tanzania; chini ya kifungu cha 21 cha Sheria; “nyaraka ya mzigo” inajumuisha hati ya usafirishaji, hati ya usafirishaji wa anga, nyaraka ya usafirishaji wa mzigo kwa njia ya barabara, manifesti, nyaraka ya shehena, ankara, nyaraka ya orodha ya usalama wa mizigo, kibali cha kuingiza ndani ya nchi au kutoa 3 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) Sura ya 182 Sura ya 283 nje ya nchi, mpango wa upangaji, mpango wa kuhifadhi, orodha ya upakiaji na orodha ya upakuaji; “kemikali” ina maana kama ilivyoelezwa chini ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, na kwa madhumuni ya Kanuni hizi, inahusiana na: (a) kemikali zilizoagizwa na kampuni ya uchimbaji madini; au (b) kemikali zinazotumiwa na kampuni za uchimbaji madini, bila kujali kama msafirishaji ni kampuni ya uchimbaji madini au siyo kampuni ya uchimbaji madini; “Shirika” maana yake ni Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania lililoanzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria; “mteja” maana yake ni mtu ambaye anapata au anataka kupata huduma kutoka kwa Shirika na inajumuisha msimamizi mkuu wa meli, wakala wa meli, msafirishaji na mwenye mzigo; “kuondoa mzigo kwenye kontena” maana yake ni mchakato wa kutoa mzigo kutoka katika kontena kwa ajili ya kusafirishwa au kufikishwa kama mzigo usio katika kontena; “Mkurugenzi Mkuu” maana yake ni Mkurugenzi Mkuu aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 30 cha Sheria; “wastani wa jumla” maana yake ni mgawanyo wa wajibu wa kifedha kwa msafirishaji, mwenye mzigo au mtu mwenye maslahi na hasara itokanayo na kutupa mzigo kwa dharula; “nyara ya Serikali” maana yake ni nyara ya Serikali kama ilivyorejewa chini ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori; “taratibu za ndani za uendeshaji” maana yake ni taratibu zilizoidhinishwa kwa mujibu wa kifungu cha 22(2)(d) cha Sheria ili kuliongoza Shirika katika kutekeleza majukumu yake; “mnyama hai” maana yake ni aina yoyote ya mnyama mwenye uti wa mgongo na asiye na uti wa mgongo na mnyama mdogo na yai lake, isipokuwa wanyama wa kufugwa; 4 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) “manifesti” maana yake ni nyaraka inayotoa orodha kamili ya mizigo kwenye meli, jina la meli na inajumuisha taarifa na maelezo ya kila hati ya usafirishaji ya mizigo yote, jina la nahodha wa meli na wakala wa meli kwenye bandari husika ya kupakia au kushusha; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na masuala ya usafirishaji kwa njia ya maji; Sura ya 123 “makinikia ya madini” ina maana sawa kama ilivyoelezwa chini ya Sheria ya Madini; “mteja wa mara moja” inahusu mwingizaji ndani ya nchi au msafirishaji nje ya nchi wa bidhaa ambaye hujihusisha na Shirika katika usafirishaji wa mzigo mara moja tu bila matarajio au nia ya kusafirisha mizigo mingine katika siku za usoni; “namba ya udhibiti wa malipo” maana yake ni namba ya kumbukumbu inayotengenezwa kutoka Serikalini pamoja na ankara ya kodi kwa ajili ya kufanya malipo ya mtandaoni kwenye akaunti ya ukusanyaji wa mapato ya Shirika; “viwango vya utendaji” maana yake ni viwango vya utendaji vilivyowekwa na Shirika ili kuzingatiwa na mtoa huduma; Sura ya 166 ”bandari” ina maana sawa kama ilivyoainishwa chini ya Sheria ya Bandari; “msimamizi mkuu wa meli” maana yake ni msafirishaji wa baharini ambaye wakala wa meli hufanya kazi kwa niaba, katika biashara ya usafirshaji wa meli; “nyaraka za wakala wa usafirishaji wa meli” maana yake ni nyaraka zinazotolewa na msafirishaji wa baharini au wakala wa msafirishaji ili kuambatishwa na ombi la kuidhinishwa na forodha au mamlaka nyingine kwa ajili ya usafirishaji kwa meli, mizigo, abiria na huduma za melini na inajumuisha hati ya usafirishaji, hati ya usafirishaji wa anga, manifesti, nyaraka ya uwasilishaji wa mzigo, hati ya usafirishaji kwa meli, au nyaraka nyingine yoyote husika katika tasnia ya usafirishaji wa majini kama inavyoweza kuainishwa na mamlaka husika; “nyaraka ya usafirishaji” maana yake ni nyaraka sahihi ya usafiri inayowezesha ugomboaji wa shehena kupitia 5 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) forodha, bandari na mamlaka nyingine na inajumuisha hati ya usafirishaji, hati ya usafirishaji wa anga, manifesti, ankara, orodha ya kupakia, nyaraka ya uwasilishaji wa mzigo, hati ya usafirishaji wa kwa meli, hati ya bima au nyaraka nyingine yoyote inayohusika na ugomboaji kama itakavyoainishwa na mamlaka husika; “maelekezo maalum” maana yake ni maelekezo ya mteja kwa Shirika kutekeleza hatua fulani wakati wa utoaji wa huduma; “kuweka mzigo kwenye kontena” maana yake ni mchakato wa kupakia mzigo kwenye kontena na kufunga kontena kwa ajili ya kusafirishwa na usafirishaji wa baharini au wasafirishaji wa maji ya ndani; “ankara ya kodi” ina maana sawa kama ilivyoelezwa chini ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani; na “mtu wa tatu” maana yake ni mkandarasi, mkandarasi mdogo, msimamizi wa mkataba wa forodha, wakala au wafanyakazi wao waliopewa kazi na Shirika kufanya majukumu yake kwa niaba yake kama ilivyoainishwa kwenye Sheria na kanuni ya 4. Sura ya 148 SEHEMU YA PILI UTOAJI WA HUDUMA ZA KIPEKEE ZA UGOMBOAJI NA UONDOSHAJI Huduma za kipekee za ugomboaji na uondoshaji Sura ya 283

Part

SEHEMU YA PILI

§ 45Provision

Shirika lazima litoe huduma maalum za ugomboaji na uondoshaji kwa bidhaa fulani zinazoingia au kutoka nchini, na linaweza kutoza ada au kamisheni ya huduma hiyo.

4.-(1) Shirika litatoa huduma za kipekee za ugomboaji na uondoshaji wa bidhaa za kipekee zifuatazo zinazoingizwa ndani ya nchi au kusafirishwa nje ya nchi: (a) silaha na risasi; (b) makinikia ya madini; (c) kemikali zinazotumiwa na kampuni za madini; (d) nyara za Serikali; na (e) wanyama hai chini ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori. (2) Mteja bidhaa hazichanganywi na bidhaa za kipekee zilizopo chini ya mamlaka ya Shirika, katika nyaraka moja ya shehena. atahakikisha kuwa, (3) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (2), endapo nyaraka moja ya shehena imechanganya mizigo mingine iliyo chini ya mamlaka ya kipekee ya Shirika, Shirika 6 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) Huduma zitakazotole wa na Shirika litagomboa shehena yote. (4) Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ndogo ya (3), Shirika litatoza ada, tozo au kamisheni ya ugomboaji.
§ 56Provision

Shirika must provide specified customs and freight services when performing exclusive functions under regulation 4, and it must follow set performance standards.

5.-(1) Shirika litatoa huduma zifuatazo wakati linatekeleza majukumu ya kipekee chini ya kanuni ya 4: (a) ugomboaji wa forodha; (b) uwakala wa usafirishaji wa mizigo; (c) ushauri wa kiforodha na usafirishaji wa mizigo; na (d) huduma nyingine kama zitakavyokubaliwa kati ya Shirika na mteja kwa kila shehena. zozote Kutekeleza kazi ya wakala binafsi wa meli (2) Katika kutoa huduma zilizotajwa katika kanuni ndogo ya (1), Shirika litazingatia viwango vya utendaji vilivyowekwa. (3) Endapo mteja anahitaji huduma iliyopo chini ya mamlaka ya kipekee ya Shirika kama ilivyoainishwa katika Sheria, kutakuwa na ombi kwa Shirika kutekeleza huduma za ugomboaji na uondoshaji wa shehena.
§ 6JinaProvision

If a private ship agent fails to do its work, Shirika must arrange for the work to be done, require the agent to hand over shipping documents and information within three days, and require the ship manager to pay the related service fees.

6.-(1) Endapo wakala binafsi wa meli anashindwa kutekeleza kazi zake, Shirika litahakikisha kazi hiyo inatekelezwa na kumtaka- (a) wakala binafsi wa meli, ndani ya siku tatu, kukabidhi nyaraka zote muhimu za usafirishaji na taarifa kwa Shirika ili kuwezesha huduma hiyo kutolewa kama ilivyokusudiwa; na (b) msimamizi mkuu wa meli kulipa ada zote za huduma ya uwakala wa meli zitakazofanyika. (2) Shirika litaamua na kugawa hisa yoyote ya ada hiyo ya wakala binafsi wa meli ambaye leseni yake imesitishwa au kufutwa kwa huduma yoyote ambayo inaweza kuwa ilitolewa kabla ya kusitishwa au kufutwa kwa leseni yake. SEHEMU YA TATU MAKUBALIANO NA MTU WA TATU Kutekeleza

Part

SEHEMU YA TATU

§ 78Provision

Shirika may contract with a licensed or registered third party to provide unloading and shipping agency services when appropriate.

7.-(1) Shirika linaweza kuingia mkataba na mtu wa 7 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) majukumu ya Shirika Kushirikish wa kwa mtu wa tatu aliye na leseni au aliyesajiliwa Upatikanaji wa mtu wa tatu Sura ya 410 Masharti ya utoaji wa huduma tatu, pale litakapoona inafaa, kwa ajili ya kutoa huduma ya- (a) uondoshaji kwa bidhaa za kipekee; na (b) uwakala wa meli iwapo wakala binafsi wa meli ameshindwa kutekeleza majukumu yake. (1), (2) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya makubaliano yanaweza kuingiwa kupitia mkataba, makubaliano, ubia, ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi au njia nyingine zinazoonekana zinafaa kwa Shirika.
§ 89Provision

Shirika halipaswi kupanga au kushirikisha mtu wa tatu kutoa huduma kwa niaba yake, isipokuwa mtu huyo ana leseni au amesajiliwa na mamlaka au taasisi husika.

8. Shirika au halitapanga, halitashirikisha mtu wa tatu kutoa huduma zozote kwa niaba yake, isipokuwa kama mtu wa tatu ana leseni au amesajiliwa na mamlaka au taasisi husika kutoa huduma hiyo. halitakasimu
§ 910. Masharti ya utoaji wa hudumaProvision

When an organization uses a third party to do its work, it must follow the Public Procurement Law.

9. Shirika linaposhirikisha mtu wa tatu kufanya kazi zake, litafuata Sheria ya Ununuzi wa Umma.
§ 10Masharti ya utoaji wa hudumaProvision

Mtu wa tatu lazima azingatie masharti ya makubaliano ya kutoa huduma na afanye kazi kwa uangalifu, weledi, uadilifu na uaminifu wakati wa kazi za mkataba na Shirika.

10.-(1) Mtu wa tatu atafuata vigezo na masharti ya makubaliano ya kutoa huduma yaliyoingiwa na Shirika. (2) Wakati wa utekelezaji wa kazi za mkataba na Shirika, mtu wa tatu- (a) atafanya kazi kwa uangalifu, weledi na uadilifu; (b) atazingatia utendaji viwango vya vilivyoainishwa na Shirika; na (c) atatekeleza majukumu kwa uaminifu. Kamisheni inayolipwa kwa mtu wa tatu Uwajibikaji wa mtu wa tatu
Section 10Verify source
§ 1112Provision

Shirika lazima lilipie mtu wa tatu aliyeshirikishwa kutoa huduma ya uondoshaji mzigo kamisheni au malipo mengine ndani ya siku saba baada ya kila mwisho wa mwezi wa kalenda.

11.-(1) Shirika litalipa kamisheni au malipo mengine kwa mtu wa tatu aliyeshirikishwa kutoa huduma ya uondoshaji mzigo, ndani ya siku saba baada ya kila mwisho wa mwezi wa kalenda. (2) Kiasi kitakacholipwa katika kanuni ndogo ya (1) kitaainishwa katika makubaliano.
Section 11Verify source
§ 12Kamisheni inayolipwa kwa mtu wa tatuProvision

Mtu wa tatu anawajibika kwa hasara, uharibifu au gharama zinazotokana na kushindwa, uzembe, uvunjaji wa sheria, kitendo kisicho halali, au kuacha kutenda wakati wa kufanya kazi za uwakala kwa niaba ya Shirika.

12. Mtu wa tatu atawajibika kwa hasara yoyote, uharibifu au gharama itakayoingiwa na mtu yeyote kwasababu ya kushindwa, uzembe, uvunjaji wa sheria au kitendo kingine kisicho halali au kuacha kufanya jambo wakati wa kutekeleza kazi zake za huduma ya uwakala kwa niaba ya Shirika. 8 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) SEHEMU YA NNE ADA, TOZO NA KAMISHENI Ada, tozo na kamisheni zinazotumika
Section 12Verify source

Part

SEHEMU YA NNE

§ 1314Provision

Bodi inaweka ada, tozo, na kamisheni zinazolipwa na wateja kwa Shirika kwa huduma chini ya Kanuni hizi, kwa mujibu wa Sheria na kwa kutangazwa katika Gazeti la Serikali.

13. Ada, tozo au kamisheni zinazolipwa na wateja kwa Shirika kwa huduma inayotolewa chini ya Kanuni hizi zitapangwa na Bodi kama ilivyoainishwa katika Sheria na kutangazwa katika Gazeti la Serikali. Akaunti ya amana ya mteja
Section 13Verify source
§ 1415. Matumizi ya bakaa ya fedha ya mtejaProvision

The company must open and use a customer escrow account, and the customer may pay certain service-related amounts into it.

14.-(1) Shirika litafungua akaunti ya amana ya mteja ya Shilingi za Tanzania, Dola za Marekani au sarafu nyingine yoyote kwa uhifadhi salama na usimamizi wa malipo ya awali ya mteja. (2) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (1), mteja anaweza kulipa kwenye akaunti ya amana ya wateja iliyofunguliwa ya Shirika, kiasi cha fedha kulipia gharama za huduma zinazotozwa kwa mteja, ikiwa ni pamoja na ada za uwakala, tozo, kamisheni na pesa inayorejeshwa. (3) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (2), ada za uwakala, tozo, kamisheni, na pesa inayorejeshwa zitakatwa kutoka katika kiasi kilichowekwa amana, na Shirika litampa taarifa mteja baada ya kukamilika kwa miamala. (4) Taarifa ya miamala ya mteja inayotolewa chini ya kanuni ndogo ya (3) itaonesha- (a) kiasi kilichowekwa; (b) kiasi kilichotumika; (c) salio lolote la kurejeshewa fedha kwa mteja; au (d) madai yoyote ya nyongeza ya Shirika. Matumizi ya bakaa ya fedha ya mteja
Section 14Verify source
§ 15Matumizi ya bakaa ya fedha ya mtejaProvision

Bakaa ya fedha kwenye akaunti ya amana ya mteja baada ya muamala kukamilika inaweza kutumika kwa miamala ya baadaye au kurejeshwa baada ya maelekezo ya mteja.

15. Bakaa ya fedha iliyosalia katika akaunti ya amana ya mteja baada ya kukamilika kwa muamala inaweza kutumika kwa miamala ya siku zijazo au kurejeshwa baada ya maelekezo ya mteja kwa Shirika. Njia na masharti ya malipo
Section 15Verify source
§ 1617Provision

Shirika must issue a tax invoice telling the customer to pay the stated agency fees, levies or commission plus applicable tax, and customers must pay the invoiced amount to Shirika’s revenue collection account; certain customers must pay within 24 hours of the invoice date.

16.-(1) Shirika, kupitia utoaji wa ankara ya kodi, litamjulisha mteja kulipa kiasi kikuu cha ada za uwakala, tozo au kamisheni pamoja na kodi inayotumika kwa huduma zitakazotolewa. (2) Mteja atafanya malipo ambayo yameainishwa katika ankara ya kodi moja kwa moja kwenye akaunti ya makusanyo ya mapato ya Shirika kwa kutumia namba ya 9 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) udhibiti wa malipo iliyopatikana kutoka kwa Shirika (3) Bila kujali ujumla wa kanuni ndogo ya (2), wateja wa mara moja na wateja wenye mizigo inayopita kupitia vituo vya mpaka watafanya malipo kama ilivyoainishwa katika ankara ya ushuru ndani ya masaa ishirini na manne kutoka tarehe ya ankara. Kushindwa kufanya malipo
Section 16Verify source
§ 1718. Malipo ya kamisheniProvision

Ikiwa mteja hajalipa kwa muda uliowekwa, Shirika halitaendelea kutoa huduma na mteja atalipa riba ya ziada.

17. Kwa kuzingatia kanuni ya 16, endapo mteja ameshindwa kufanya malipo ndani ya muda ulioainishwa- (a) Shirika halitaendelea kutoa huduma; (b) kwa kuongezea katika jumla iliyoainishwa katika ankara ya kodi, mteja atatakiwa kulipa riba kumi kitakachojumuishwa kila mwezi au sehemu ya malipo ya awali. kiwango asilimia kwa cha Malipo ya kamisheni
Section 17Verify source
§ 18Malipo ya kamisheniProvision

Mteja lazima alipe ankara zote za huduma; ikiwa Shirika litalipa fedha zake kwa VAT au malipo mengine ya mteja baada ya kuchelewa au kushindwa kulipa, linaweza kutoza kamisheni ya malipo ya 2.5% kwa mwezi.

18.-(1) Mteja atawajibika kulipia ankara zote zinazohusiana na huduma zilizotolewa. Malipo ya sehemu ya utendaji (2) Endapo Shirika litatumia fedha zake kulipa- (a) kodi ya ongezeko la thamani baada ya mteja kuchelewa au kushindwa kulipia ankara ya kodi iliyotolewa ndani ya muda ulioainishwa; au (b) malipo mengine yoyote yaliyotakiwa kulipwa na mteja, Shirika litatoza kamisheni ya malipo kwa kiwango cha asilimia 2.5 kinachojumuishwa kila mwezi, au sehemu ya fedha zilizotumika.
Section 18Verify source

Part

sehemu ya

§ 19Malipo ya sehemu ya utendajiProvision

If a transaction cannot be completed because of customer fault, Shirika may recover the agency fee and completed costs, and the customer must also pay related costs such as applicable taxes and duties.

19.-(1) Endapo Shirika kwa kiasi fulani limefanya muamala ambao hauwezi kukamilika kutokana na kosa la mteja, Shirika litakuwa na haki ya kupokea malipo ya ada iliyotumika kwa huduma za uwakala na gharama iliyokamilika kabla ya kusitishwa kwa muamala huo. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), mteja atatakiwa kulipia gharama nyingine zinazohusiana, ikiwa ni pamoja na kodi na ushuru unaotumika kama inavyoweza kutakiwa na sheria nyingine. (3) Kwa madhumuni ya kanuni hii, “kosa la mteja” litajumuisha yafuatayo: (a) kushindwa kufanya malipo yanayohitajika; (b) ufilisi au kufilisika kwa mteja; 10 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) (c) iwapo mali yoyote ya mteja inahusishwa katika tozo yoyote, kushikiliwa kwa mali, mgao wa jumla kwa manufaa ya wadai, maombi au mauzo kwa mdai au wakala wa Serikali; (d) kufutiwa usajili, kusitishwa au kufutwa kwa leseni ya mteja; (e) kushindwa kuwasilisha inayohitajika na Shirika; au nyaraka yoyote (f) sababu nyingine yoyote itakayosababishwa na kuzuia Shirika mteja kutekeleza kazi zake chini ya Kanuni hizi. inaweza ambayo SEHEMU YA TANO VIGEZO NA MASHARTI YA BIASHARA Utaratibu wa bima
Section 19Verify source

Part

SEHEMU YA TANO

§ 2021. Maelekezo ya mtejaProvision

Shirika linaweza, kwa maelekezo ya mteja, kuweka utaratibu wa bima wakati wa kutoa huduma chini ya Kanuni hizi, isipokuwa katika hali zilizotajwa.

20.-(1) Shirika linaweza, kwa maelekezo ya mteja, kuweka utaratibu wa bima wakati wa kutoa huduma chini ya Kanuni hizi isipokuwa iwapo- Maelekezo ya mteja (a) mteja amelipia bima na gharama za mchakato inavyoweza zinazoingiwa na Shirika kama kukubaliwa na mteja; na (b) bima inategemea masharti na vigezo vya kawaida vya sera za mtoaji bima au mnufaika aliye hatarini.
Section 20Verify source
§ 21Maelekezo ya mtejaProvision

Shirika lazima lihudumie kwa kuzingatia maelekezo ya mteja, na linaweza kurekebisha utaratibu wa huduma na ushughulikiaji wa shehena.

21.-(1) Shirika litatoa huduma kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na mteja. (2) Maelekezo yanayotolewa na mteja chini ya kanuni ndogo ya (1) yatakuwa sahihi, kamili au kwa mujibu wa vigezo na masharti yaliyowekwa chini ya Kanuni hizi. (3) Endapo mteja atatoa maelekezo yasiyo sahihi au kamili na yakasababisha hasara au uharibifu kwa Shirika au mtu wa tatu, Shirika litadai fidia ya hasara hiyo kutoka kwa mteja pamoja na gharama nyingine zozote zinazohusiana. (4) Bila ya kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Shirika linaweza- (a) kupanga utaratibu wa kutoa huduma na kuchagua; au (b) kubadili katika kushughulikia, kuhifadhi na kusafirisha shehena. utakaofuatwa utaratibu 11 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) Uwasilishwa ji wa shehena
Section 21Verify source
§ 2223Provision

Shirika lazima liwasilishe shehena kwa mteja ndani ya muda uliowekwa; vinginevyo, mteja anaweza kulichukulia shehena kuwa limepotea na kudai fidia baada ya siku 120.

22.-(1) Shirika litawasilisha shehena kwa mteja ndani ya muda uliowekwa kwa mujibu wa mpango wa ugomboaji shehena. kwa kukosekana (2) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (1), mteja unaothibitisha anaweza, ushahidi vinginevyo, kuchukulia kuwa, shehena limepotea na kuwasilisha madai ya fidia kwa Shirika baada ya siku mia moja na tarehe iliyopaswa mzigo kufikishwa. ishirini mfululizo kupita, baada ya Upokeaji wa shehena
Section 22Verify source
§ 2324Provision

Mteja lazima asaini hati ya kupokea mzigo ili kuthibitisha kupokea shehena.

23.-(1) Mteja atathibitisha kupokea shehena kwa kusaini hati ya kupokea mzigo. (2) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (1) hati ya kupokea mzigo itakuwa ni ushahidi tosha kuwa shehena ilifikishwa katika hali nzuri na salama. (3) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (1) na (2), iwapo mteja hajasaini hati ya kupokelea mzigo lakini amelipatia Shirika notisi ya maandishi wakati wa uwasilishwaji, ikibainisha hali ya jumla ya hasara au uharibifu wa shehena, itakuwa ushahidi tosha kuwa shehena hiyo haikufikishwa katika hali nzuri na salama. Dhamana ya shehena
Section 23Verify source
§ 2425Provision

Shirika linaweza kushikilia shehena ya mteja, mali, au nyaraka zinazohusiana kama dhamana ya kiasi kinachodaiwa, na kutumia dhamana hiyo kwa mujibu wa sheria.

24. Shirika linaweza kushikilia shehena ya mteja na mali au nyaraka yoyote inayohusiana, kama dhamana ya kiasi chochote kinachostahili kulipwa kwa Shirika na kutumia dhamana hiyo kwa mujibu wa sheria. Uthibitisho wa taarifa sahihi
Section 24Verify source
§ 2526Provision

The customer must provide all cargo-related documents to the company.

25.-(1) Mteja atawasilisha kwa Shirika nyaraka zote zinazohusiana na shehena, na nyaraka hizo zitachukuliwa kuwa zinajumuisha taarifa sahihi kuhusiana na shehena, ikijumuisha maelezo asili ya jumla ya shehena, maelezo ya mzigo, alama na idadi, uzito, kiasi na wingi na uhatari wa shehena, kama yalivyotolewa na yeye binafsi au kwa niaba yake. (2) Endapo mteja atashindwa kutoa taarifa sahihi chini ya kanuni ndogo ya (1), Shirika halitawajibika kwa kosa lolote, hasara au uharibifu unaohusiana na shehena hiyo. Fidia
Section 25Verify source
§ 2627. Wastani wa jumlaProvision

Shirika must act according to these Regulations, and the customer must indemnify Shirika for liabilities incurred while clearing/removing goods on the customer’s behalf.

26.-(1) Shirika litawajibika kwa kiwango na kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hizi. 12 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) (2) Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ndogo ya (1), mteja atafidia Shirika kwa jukumu lolote lililofanywa wakati wa utekelezaji wa utoaji wa huduma za ugomboaji na uondoshaji kwa niaba ya mteja. Wastani wa jumla
Section 26Verify source
§ 27Wastani wa jumlaProvision

Shirika linastahili fidia kwa madai ya wastani wa jumla yanayoweza kufanywa dhidi ya mteja, na mteja anatakiwa kutoa dhamana inapohitajika na Shirika.

27. Shirika litalipwa fidia kuhusiana na madai yoyote ya wastani wa jumla ambayo yanaweza kufanywa kwa mteja, na mteja atatoa dhamana kama itakavyohitajika na Shirika. SEHEMU YA SITA MASHARTI YA JUMLA Ukomo wa madai ya hasara au uharibifu Wajibu wa Shirika
Section 27Verify source

Part

SEHEMU YA SITA

§ 2829. Wajibu wa ShirikaProvision

Shirika haliwajibiki kwa hasara au uharibifu unaotokana na ukomo au hitilafu zilizo nje ya uwezo wake.

28. Shirika halitawajibika kwa hasara au uharibifu wowote unaotokana na ukomo au hitilafu yoyote iliyo nje ya uwezo wa Shirika.
Section 28Verify source
§ 29Wajibu wa ShirikaProvision

Shirika lazima litekeleze uangalizi wa kina na hatua zinazofaa ili kuhakikisha usalama na ulinzi wa shehena.

29. Shirika litatekeleza wajibu wa uangalizi ikiwa ni pamoja na kufanya uangalizi wa kina na hatua zinazofaa, kuhakikisha usalama na ulinzi wa shehena. Tathmini ya fidia
Section 29Verify source
§ 3031Provision

Shirika must compensate a customer within a reasonable time for cargo loss or damage, or loss of money caused by a breach of the duty of care.

30.-(1) Shirika, ndani ya muda unaofaa, litamfidia mteja kwa hasara au uharibifu wa shehena au upotevu wa fedha unaotokana na ukiukaji wa wajibu wa uangalizi. linatakiwa kulipa (2) Endapo Shirika fidia kuhusiana na sehemu ya au shehena yoyote, tathmini itaamuliwa kwa kurejea thamani ya kawaida ya shehena ya aina na ubora unaofanana au njia nyingine yoyote kama Shirika litakavyoona inafaa. Ukomo wa fidia
Section 30Verify source
§ 3132Provision

Shirika’s liability for cargo loss or damage is capped at USD 2,000 per lost or damaged shipment, and other losses under the Regulations are capped at USD 3,000 per occurrence, unless a larger amount is recovered from the person the Shirika is liable to.

31.-(1) Shirika halitawajibika kwa hasara yoyote au uharibifu wa shehena, kwa kiasi kinachozidi Dola za Marekani elfu mbili au sawa na Shilingi za Tanzania kwa shehena iliyopotea au kuharibika, isipokuwa kama kiasi kikubwa zaidi kimerejeshwa na mtu ambaye Shirika linawajibika kwake. (2) Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ndogo ya (1), uwajibikaji wa Shirika kwa aina yoyote ya hasara ambayo haijatajwa chini ya Kanuni hizi, hautazidi jumla ya kiasi cha Dola za Marekani elfu tatu au kwa kiasi sawa na Shilingi za Tanzania kwa kila tukio isipokuwa kama kiasi 13 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) kikubwa kimepokelewa kutoka kwa mtu ambaye Shirika linawajibika kwake. Ukomo wa uwajibikaji kwa kuchelewaji Jukumu la usiri
Section 31Verify source
§ 3233Provision

Shirika linaweza kuwajibika kulipa tozo za uchelewaji wa kutoa huduma iwapo itathibitika uchelewaji ulisababishwa na Shirika pekee, na uwajibikaji huo hauwezi kuzidi gharama za huduma iliyosababisha ucheleweshaji.

32.-(1) Shirika kwa malipo yanayotokana na uchelewaji katika kutoa huduma iwapo itathibitika kuwa, uchelewaji huo ulisababishwa na Shirika pekee. litawajibika (2) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (1), iwapo imethibitika kuwa, Shirika linawajibika kulipa tozo za uchelewaji katika kutoa huduma, kuwajibika huko kutakuwa kwa kiasi kisichozidi gharama zinazohusiana na huduma iliyosababisha ucheleweshaji huo.
Section 32Verify source
§ 3334Provision

Shirika lazima lilinde taarifa za mteja na kuzitunza kuwa siri; wafanyakazi, mawakala au wawakilishi wake hawapaswi kuzifichua au kuziwasiliana kwa ajili ya maslahi binafsi.

33.-(1) Mwajiriwa, wakala au mwakilishi wa Shirika hatatumia kwa maslahi binafsi wakati wowote au kwa namna yoyote moja kwa moja au vinginevyo, kufichua au kuwasiliana kwa njia yoyote, taarifa yoyote ambayo ni miliki ya mteja. (2) Bila kujali kifungu kidogo cha (1), Shirika litatakiwa kulinda taarifa yoyote ya mteja na kuzichukulia kama za siri, isipokuwa inapohitajika kufichua taarifa hizo kwa mujibu wa sheria. Uzingatiaji wa taratibu zilizoanzish wa za biashara
Section 33Verify source
§ 3435Provision

Shirika lazima lifuate taratibu za kutoa huduma, ikiwemo huduma saa 24 kila siku, kuonyesha ada/tozo/kamisheni, kuweka mfumo wa malalamiko, kukusanya nyaraka fulani, na kuwajulisha wateja hatua za usafirishaji wa mizigo.

34. Katika kutekeleza shughuli zake, Shirika, pamoja na sheria na kanuni husika, litazingatia taratibu za kutoa huduma, zikijumuisha- (a) kutoa huduma kwa saa ishirini na manne kila siku kwa siku saba za wiki ikijumuisha siku za mwisho wa juma na sikukuu za kitaifa; (b) kuweka wazi ada, tozo na kamisheni zinalipwa na mteja; (c) kuanzisha malalamiko; mfumo wa kushughulikia (d) kukusanya nyaraka za kupokelea mzigo; (e) kukusanya nyaraka za uhifadhi; na (f) kumjulisha mteja kuhusu hatua za usafirshaji wa mizigo. Utaratibu wa kushughuliki a
Section 34Verify source
§ 3536Provision

Mtu aliye na mgogoro unaohusu utekelezaji wa majukumu ya Shirika au wa Sheria na Kanuni hizi anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa mujibu wa Kanuni za Kushughulikia Malalamiko.

35. Endapo mtu ana mgogoro wowote unaohusiana na jambo lolote linalotokana na- (a) utekelezaji wa majukumu ya Shirika; au 14 Kanuni za Ugomboaji na Uondoshaji wa Bidhaa za Kipekee Tangazo la Serikali Na. 197 (linaendelea) malalamiko TS. Na. 338 ya 2018 Kufuta TS. Na. 386 la 2020 (b) utekelezaji wa Sheria na Kanuni hizi, anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa mujibu wa Kanuni za Kushughulikia Malalamiko.
Section 35Verify source
§ 36Tathmini ya fidiaProvision

Kanuni za Huduma ya Biashara ya Meli Tanzania za Mwaka 2020 zimefutwa.

36. Kanuni za Huduma ya Biashara ya Meli Tanzania za Mwaka 2020 zimefutwa. Dodoma, 5 Machi, 2025 MAKAME M. MBARAWA Waziri wa Uchukuzi 15
Section 36Verify source

Legislative relationships

0 referenced instruments

Names are derived from the stored provision headings and citation-enrichment layer. Treat this as a research index and verify each relationship against the source text.

No structured legislative relationships were detected

The statute remains fully searchable by provision. Consult the source text for amendments and cross-references that have not yet been indexed.

Recorded versions and source checkpoint

1 version available in this collection

Current-law checkpoint
  • Undated version · currentSwahili

Source-linked research

Ask AI about this statute

The overview, provisions, and source records above are public. Continue in a separate conversation with this statute’s jurisdiction and source version attached.

About this LexChat collection

Statute information is organised from identified legislative sources for professional research. Corrections can be reported to hello@esheria.ai.