AI-assisted research summary: Mwombaji lazima atimize masharti ya kibali cha ujenzi kwa kujenga kituo cha gesi asilia kulingana na viwango na taratibu zilizotajwa.
3. Mwombaji anapewa kibali cha ujenzi cha kujenga kituo cha gesi asilia katika eneo la pembezoni mwa Barabara ya Nyerere kwenye Kiwanja Na. 112, Eneo la Kipawa, Dar es Salaam kwa vigezo na masharti yafuatayo: (a) ujenzi hautaanza mpaka mwombaji awe amepata cheti cha tathmini ya athari za mazingira kutoka mamlaka husika; (b) kuzingatia muundo ulioidhinishwa,vipimo vya kiufundi, taratibu (ufungaji, ujenzi, uchomeleaji, majaribio na uendeshaji), mkuza na sheria 1 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Kituo cha Gesi Asilia kwa Kampuni ya Victoria Services Station Limited Katika Eneo la Kipawa Tangazo la Serikali Na. 122 (Linaendelea) nyingine zinazohusika; (c) kuhakikisha kuwa kituo cha gesi asilia na vifaa vyake vinajengwa kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango la Taifa au sheria zingine husika; (d) kuhakikisha kuwa ukaguzi wa ujenzi wa kituo na vifaa vyake wakati wa ujenzi unafanyika kadri inavyohitajika ili kuhakikisha kuwa ujenzi, vifaa, uchomeleaji, maunganisho na ujaribuji wa kituo baada ya kukamilika unafanyika kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango la Taifa; (e) kuhakikisha kuwa- (i) hakuna au kupunguza usumbufu kwa wakazi walio karibu na eneo la ujenzi na usalama kwa umma unapewa kipaumbele; (ii) iwapo ulipuzi utafanyika, ufanywe kwa kuzingatia taratibu za kisheria zilizopo na kufanywa na mtu mwenye sifa za kazi ya ulipuzi kwa kuzingatia usalama kwa umma, mifugo, wanyama, majengo, umeme, miundombinu miundombinu ya chini ya ardhi na mali nyingine eneo kunakofanyika ulipuzi; karibu zilizo simu, ya na (f) kuhakikisha kuwa- (i) zinkuwepo juhudi za kupunguza uharibifu kwenye ardhi na kuzuia mazingira yatakayosababisha kuziba kwa mifereji ya kupitisha maji na mmomonyoko wa udongo; (ii) baada ya ujenzi, ardhi inarudishwa katika kadri iliyokuwepo kwa hali itakavyowezekana; (g) kuzingatia- (i) viwango vya mazingira, afya na usalama vilivyoainishwa na sheria; (ii) afya na usalama wa watu na vifaa na matumizi ya vifaa vya usalama wakati wote kama vile kofia ngumu, miwani na viatu vya usalama na matumizi ya kizima 2 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Kituo cha Gesi Asilia kwa Kampuni ya Victoria Services Station Limited Katika Eneo la Kipawa Tangazo la Serikali Na. 122 (Linaendelea) moto; na (h) kuhakikisha kuwa miundombinu yote ya utoaji huduma kwa umma bila kujali kuwa inadhibitiwa na Mamlaka au la inalindwa dhidi ya uharibifu na kuwaarifu wamiliki wake wawepo eneo la ujenzi wakati wa kujenga. Ukomo wa kibali cha ujenzi