AI-assisted research summary: Mwombaji anapewa kibali cha ujenzi, lakini lazima azingatie masharti kadhaa ya ujenzi, usalama, mazingira, na ulinzi wa miundombinu.
3. Mwombaji anapewa kibali cha ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupokelea gesi asilia ndani ya eneo la kiwanda cha Alliance One Tobacco Tanzania Limited katika Kata ya Kingolwira, Manispaa ya Morogoro, kwa masharti yafuatayo: (a) kuzingatia michoro iliyoidhinishwa, viwango vya kiufundi, michakato ya ujenzi ikijumuisha usimikaji, ujenzi, uchomeleaji, majaribio ya kituo na uagizaji na uwekaji mpaka wa haki ya njia iliyotolewa au kuzingatia sheria nyingine inayotumika; 1 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Kupokelea Gesi Asilia kwa Kampuni ya Nishati ya Puma Tangazo la Serikali Na.140 (Linaendelea.) (b) kuhakikisha kuwa kituo cha kupokelea gesi asilia au miundombinu mingine inayohusika inajengwa viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania au sheria nyingine inayotumika; kuzingatia kwa (c) kuhakikisha kuwa ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha kupokelea gesi au miundombinu mingine inayohusika yanakidhi matakwa ili kuhakikisha matakwa ya viwango vilivyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania yanazingatiwa katika vifaa, ujenzi, uchomeleaji, uunganishaji na majaribio ya kituo; (d) kuhakikisha kuwa- (i) kuna usumbufu mdogo kwa wakazi walio karibu na eneo la ujenzi na usalama unapewa kipaumbele cha msingi; umma kwa (ii) iwapo ulipuzi unahusika, utafanyika kwa kuzingatia kanuni na utafanywa na mfanyakazi mwenye uwezo na sifa za kazi ya ulipuzi na kuhakikisha usalama kwa umma, mifugo, wanyama, simu, majengo, miundombinu ya telegrafia, nyaya za umeme, majengo yaliyopo chini ya ardhi na mali nyingine yoyote iliyo jirani na eneo la ulipuzi; (e) kuhakikisha- jitihada (i) iwapo ni wakati wa kusawazisha eneo la ujenzi, ili kupunguza uharibifu kwenye ardhi na kuzuia mtiririsho usio wa kawaida na mmomonyoko wa udongo; zinafanyika (ii) iwapo ni baada ya ujenzi, ardhi inarudishwa katika hali iliyokuwepo kwa kadri inavyowezekana; (f) kuzingatia- (i) viwango vya mazingira, afya na usalama vilivyoainishwa na sheria zinazotumika; 2 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Kupokelea Gesi Asilia kwa Kampuni ya Nishati ya Puma Tangazo la Serikali Na.140 (Linaendelea.) (ii) afya na usalama wa wafanyakazi na vifaa na wakati wote kunakuwa na matumizi ya vifaa vya usalama vinavyojumuisha kofia ngumu, miwani ya usalama na viatu vya usalama na matumizi ya kifaa cha kuzima moto; na (g) kuhakikisha kuwa miundombinu yote iliyopo, iwe inasimamiwa na Mamlaka au la, inalindwa dhidi ya uharibifu na kuwaarifu rasmi waendeshaji wa miundombinu hiyo kwa kuwaomba uwepo wao katika eneo la ujenzi wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi. Ukomo wa Kibali