Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe ya Mwaka 2025
This provision gives the short title of the by-law: Njombe Town Council Bus Stand By-law, 2025.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe ya Mwaka 2025
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the short title of the by-law: Njombe Town Council Bus Stand By-law, 2025. This by-law applies throughout the whole area under the Njombe Town Council’s authority. This section defines key terms used in the by-law, including authorised officer, vehicle, council, director, owner, bus stand, levy, agent, and yard. Halmashauri lazima itoeza ushuru wa stendi kwa magari na watu wanaoingia au kutoka stendi, na watumishi wa Halmashauri wanaopokea malipo lazima watoe stakabadhi ya kielektroniki. The council must establish a bus station for loading and unloading passengers or cargo, and private parties may run their own bus station only with a special council permit.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe ya Mwaka 2025
Showing 22 of 22
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This provision gives the short title of the by-law: Njombe Town Council Bus Stand By-law, 2025.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe ya Mwaka 2025. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the whole area under the Njombe Town Council’s authority.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya Mji Njombe. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including authorised officer, vehicle, council, director, owner, bus stand, levy, agent, and yard.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni mtumishi yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chombo cha usafiri” maana yake ni chombo chochote kinachotumika kusafirishia bidhaa, abiria au mizigo isipokuwa wanyama; lengo “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Mji Njombe; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mmiliki’’ maana yake ni mmiliki, kondakta au dereva anayetumia chombo cha usafiri katika eneo la kituo cha mabasi; “stendi” au “kituo cha mabasi” maana yake ni eneo maalumu lililotengwa au kujengwa na Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria au mizigo, 1 Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe Tangazo la Serikali Na.143 (Linaendelea.) na inajumuisha kituo cha kupaki malori na vituo vingine vidogo vya kupakia na kushusha abiria vya Halmashauri; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa shughuli au huduma mbalimbali zinazofanywa katika eneo la Halmashauri; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi au kampuni iliyoteuliwa kukusanya ada na ushuru kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii; na “yadi” maana yake ni eneo lililotengwa kwa ajili ya kuhifadhi vyombo vya usafiri. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru kwa vyombo
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itoeza ushuru wa stendi kwa magari na watu wanaoingia au kutoka stendi, na watumishi wa Halmashauri wanaopokea malipo lazima watoe stakabadhi ya kielektroniki.
4.-(1) Halmashauri itatoza ushuru kwa vyombo vyote vya usafiri vinavyoingia na kutoka ndani ya stendi kwa saa ishirini na nne kwa mujibu wa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (2) Halmashauri itatoza ushuru kwa mtu anayeingia na kutoka stendi. (3) Wakala au afisa yeyote wa Halmashauri atakayepokea malipo ya ushuru atatoa stakabadhi ya kielektroniki kulingana na malipo yaliyofanyika na tarehe ya tukio. (4) Kila chombo cha usafiri kinachoingia katika eneo la stendi kinatakiwa kulipiwa ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, malipo hayo yatafanyika kwa siku, mwezi au kwa kadri Halmashauri itakavyoona inafaa. (5) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1) na (2), magari ya kubeba wagonjwa na vyombo vya usafiri vinavyomilikiliwa na Serikali, wanadiplomasia au majeshi na havitatozwa ushuru. - 5 Verify source ↗
(1) Halmashauri itaanzisha kituo cha mabasi
AI-assisted research summary: The council must establish a bus station for loading and unloading passengers or cargo, and private parties may run their own bus station only with a special council permit.
5.-(1) Halmashauri itaanzisha kituo cha mabasi mahsusi kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria au mizigo. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), kampuni, taasisi au mtu binafsi anaweza kuanzisha na kusimamia kituo cha mabasi anayomiliki kwa nia ya kupakia na kushusha abiria na mizigo baada ya kupata kibali maalum cha Halmashauri kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. 2 Ushuru wa stendi Uanzishaji wa Kituo cha mabasi Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe Tangazo la Serikali Na.143 (Linaendelea.) Matumizi ya stendi Wajibu wa kuingiza gari kituo cha mabasi (3) Chombo cha usafiri kinachosafirisha abiria ndani na nje ya Halmashauri kinapaswa kuingia stendi ya Halmashauri na kulipiwa ushuru isipokuwa kwa mmiliki wa chombo cha usafiri aliyepata kibali chini ya kanuni ndogo ya 8(1) ambaye kwa makubaliano na Halmashauri atalipa ushuru wa stendi kwa Afisa Mwidhiniwa kama ilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. (4) Kituo cha mabasi cha Halmashauri kinaweza kutumika kwa ajili ya kuegesha na kulaza vyombo vya usafiri baada ya kibali. - 6 Verify source ↗
(1) Kila mtu yeyote anayefanya biashara ya
AI-assisted research summary: Passenger transport operators must load and unload passengers or their luggage only at the stand, use the stand only during the stated hours unless the council grants permission, start trips at approved stands within the council area (except through-traffic from outside the council area), and passenger drivers may not stop for more than five minutes at a roadside stop.
6.-(1) Kila mtu yeyote anayefanya biashara ya kusafirisha abiria atakuwa na wajibu wa kupakia na kushusha abiria au mizigo yao katika eneo la stendi. (2) Muda wa kutumia stendi utakuwa kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne kamili usiku, isipokuwa kama kuna kibali cha Halmashauri. (3) Isipokuwa kwa magari yanayopita kutoka maeneo mengine ya nje ya Halmashauri, magari yote yanayofanya biashara ya usafirishaji ndani ya Halmashauri yataanzia safari zake stendi zilizoanzishwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii au sheria nyingine yoyote. (4) Dereva wa gari ya abiria hataruhusiwa kusimamisha gari kwa zaidi ya dakika tano katika kituo cha njiani. - 7 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni wajibu kwa kila dereva wa gari la
AI-assisted research summary: Madereva wa magari ya abiria na mizigo lazima waingize magari kwenye eneo lililotengwa kwa kupakia na kushusha, magari ya abiria yaonyeshe yanapotoka na yanakoelekea, na madereva wa magari yanayoingia kituo cha mabasi watumie milango sahihi; Halmashauri pia itaweka utaratibu wa pikipiki kuingia na kutoka.
7.-(1) Itakuwa ni wajibu kwa kila dereva wa gari la abiria na mizigo litokalo ndani na kwenda nje ya Halmashauri na maeneo mengine ndani ya Halmashauri kuingiza gari katika eneo lililotengwa na Halmashuri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na au mizigo. (2) Magari yote ya abiria yatakuwa na maandishi yanayoonesha mahali yanapotoka na yanakoelekea. (3) Dereva wa gari itakayoingia kituo cha mabasi atahakikisha gari inaingia kwa kutumia mlango wa kuingilia na kutoka kupitia katika mlango kutokea. (4) Halmashauri itaweka utaratibu wa pikipiki kuingia na kutoka katika kituo cha mabasi. 3 Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe Tangazo la Serikali Na.143 (Linaendelea.) Vituo vya mabasi binafsi - 8 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kutoa kibali cha
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kutoa au kusitisha kibali cha kuanzisha kituo binafsi cha mabasi, na kusitisha lazima kuwe na taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja kwa mmiliki au mwendeshaji.
8.-(1) Halmashauri inaweza kutoa kibali cha kuanzisha kituo binafsi cha mabasi endapo itaona kuna umuhimu wa kuanzisha kituo hicho. kwa (2) Kibali cha kuanzisha kituo binafsi kitakuwa kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kitatolewa baada ya mwombaji kuzingatia masharti yatakoyotolewa na Halmashauri na kulipia gharama kama zilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. (2) Halmashauri inaweza kusitisha wakati wowote kibali cha kuanzisha kituo binafsi kwa kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja kwa mmiliki au mwendeshaji wa kituo. Kulaza chombo cha usafiri ndani ya stendi - 9 Verify source ↗
(1) Halmashauri itaweka utaratibu wa kulaza
AI-assisted research summary: Halmashauri must set the procedure for parking vehicles at the bus station and charge a fee for parking there.
9.-(1) Halmashauri itaweka utaratibu wa kulaza vyombo vya usafiri ndani ya stendi. (2) Halmashauri itatoza ushuru wa kulaza chombo cha usafiri ndani ya stendi. Wajibu wa kutunza usafi - 10 Verify source ↗
Kila mmiliki, dereva au kondakta wa chombo
AI-assisted research summary: Wamiliki, madereva, makondakta, wasafiri na watumiaji wa stendi au eneo la maegesho lazima wasichafue eneo hilo kwa taka, maji au mafuta.
10. Kila mmiliki, dereva au kondakta wa chombo cha usafiri na kila msafiri au mtumiaji yeyote wa stendi au eneo lolote lililotengwa kwa ajili ya maegesho anatakiwa kuhakikisha kuwa hachafui au kusababisha uchafuzi wowote wa eneo la stendi au maegesho kwa kutupa taka, kumwaga au kusababisha kumwagika kwa maji au mafuta ya aina yoyote kwenye kituo cha mabasi. Uteuzi wa Wakala - 11 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kuteua Wakala kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua Wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba yake.
11.-(1) Halmashauri inaweza kuteua Wakala kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kwa ajili ya kukusanya ushuru kwa niaba yake. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa- (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii; na (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. 4 Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe Tangazo la Serikali Na.143 (Linaendelea.) Biashara ndogondogo Mamlaka ya Afisa Mwidhiniwa Kukamata na kuzuia chombo cha usafiri - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote anayefanya biashara ndogo ndogo
AI-assisted research summary: Mtu anayefanya biashara ndogo ndogo anaweza kufanya biashara ndani ya eneo la stendi bila masharti, lakini anaweza kukubaliana na uongozi wa stendi kuhusu ulinzi na usalama wa yeye na mali zake.
12. Mtu yeyote anayefanya biashara ndogo ndogo ataruhusiwa kufanya biashara ndani ya eneo la stendi bila masharti, isipokuwa anaweza kukubaliana na uongozi wa stendi kuhusu utaratibu wa ulinzi na usalama wake na mali zake. - 13 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kukamata na kuondoa chombo cha usafiri kinachopakia au kushusha abiria nje ya stendi.
13.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya kukamata na kuondoa chombo cha usafiri ambacho kitapakia au kushusha abiria nje ya eneo la stendi. (2) Chombo cha usafiri kilichokamatwa kwa mujibu wa masharti ya kanuni ndogo ya (1) kitaondolewa na kuhifadhiwa kwenye yadi ya Halmashauri au sehemu yoyote kama itakavyoamriwa na Mkurugenzi. (3) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuuza chombo kilichokamatwa baada ya kupata idhini ya mahakama endapo mmiliki wa chombo hicho atashindwa kulipa gharama za uangalizi pamoja na gharama za kukamata chombo hicho ndani ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kukamatwa. (4) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (3), kabla ya Halmashauri kuuza chombo kilichokamatwa, Mkurugenzi atatoa taarifa ya maandishi kwa umma ya siku zisizozidi saba kuhusu kusudio la kuuza chombo hicho. (5) Halmashauri haitawajibika kwa hasara yoyote itakayotokea wakati wa kukamata au kushikilia chombo itakuwa cha usafiri, imesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri au wakala. isipokuwa kama hasara hiyo - 14 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kukamata na kuzuia
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kukamata na kuzuia chombo cha usafiri kisicholipiwa ushuru au kilichokiuka sharti; baada ya kukamatwa, mmiliki au dereva lazima alipe ndani ya siku mbili, na kabla ya kuuza kwa mnada Mkurugenzi atoe taarifa ya siku saba.
14.-(1) Halmashauri inaweza kukamata na kuzuia chombo cha usafiri ambacho hakijalipiwa ushuru au ambacho mmiliki au dereva wake amekiuka sharti lolote katika Sheria Ndogo hii. (2) Mmiliki au dereva wa chombo cha usafiri kilichokamatwa atapaswa kulipa ushuru unaodaiwa ndani ya muda wa siku mbili. (3) Endapo ushuru hautalipwa baada ya muda wa siku mbili kupita tangu kukamatwa kwa chombo cha usafiri, Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuuza chombo husika kwa njia ya mnada baada ya kupata idhini 5 Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe Tangazo la Serikali Na.143 (Linaendelea.) ya mahakama. (4) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (3), kabla ya Halmashauri kuuza chombo kilichokamatwa, Mkurugenzi atatoa taarifa ya siku saba kwa mdaiwa na umma juu ya kusudio la kuuza chombo husika. (5) Halmashauri haitawajibika kwa hasara yoyote itakayotokea wakati wa kukamata au kuhifadhi chombo cha usafiri kilichokamatwa na kushikiliwa na Halmashauri ikiwa ni pamoja na mali zilizo ndani ya chombo cha usafiri husika, itakuwa imesababishwa kwa uzembe wa watumishi wa Halmashauri au Wakala. isipokuwa hasara kama hiyo Wajibu wa kuvaa sare na vitambulisho Makosa - 15 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara au wakala wa basi, muuza
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara na wahudumu walioko stendi lazima wawe na kitambulisho maalumu kutoka Halmashauri na wavae sare maalumu wanapofanya kazi zao.
15. Kila mfanyabiashara au wakala wa basi, muuza tiketi, mbeba mizigo, mfanyabiashara ndogondogo, mama lishe au baba lishe ndani ya stendi- (a) anapaswa kuwa na kitambulisho maalumu kitakachotolewa na Halmashauri; na (b) ana wajibu wa kuvaa sare maalumu wakati wote anapofanya shughuli zake katika eneo la stendi. - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Anyone commits an offence if they refuse or induce refusal to pay taxes, load or unload passengers or goods outside a designated bus stand area, tout at the stand, repair or wash vehicles there, park a vehicle there without permission, sell goods without registration, or start a bus stand or bus station contrary to the stated procedure.
16. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atakataa, atashindwa au atamshawishi mtu yeyote kukataa kulipa ushuru; (b) atapakia au kushusha abiria au mizigo katika tofauti na stendi au eneo ambalo eneo halikutengwa kwa ajili hiyo; (c) atapiga debe katika eneo la stendi; (d) atafanya matengenezo au kuosha gari katika eneo la stendi; (e) atalaza chombo cha usafiri katika eneo la stendi bila kibali; (f) atauza chakula au vinywaji au bidhaa nyingine bila kusajiliwa; au (g) ataanzisha stendi au kituo cha mabasi kinyume na utaratibu ulioainishwa. Adhabu - 17 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa
AI-assisted research summary: Anyone found guilty of an offence under this by-law may have to pay a fine, go to prison, or both.
17. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ngodo hii atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi 6 Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe Tangazo la Serikali Na.143 (Linaendelea.) Kufifilisha kosa milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote kwa pamoja. - 18 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumaliza kosa kwa kumtoza mkosaji shilingi 200,000 ikiwa anakiri kosa kwa hiari, anajaza fomu maalum, na analipa ushuru unaodaiwa.
18. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii na kulipa ushuru anaodaiwa. Kufutwa kwa Sheria Ndogo TS. Na. 124 la 2008 - 19 Verify source ↗
Sheria Ngodo hii inafuta Sheria Ndogo za
AI-assisted research summary: This section repeals the Njombe Town Council Bus Stand By-laws of 2008.
19. Sheria Ngodo hii inafuta Sheria Ndogo za (Stendi ya Mabasi) za Halmashauri ya Mji Njombe za Mwaka 2008. 7 Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe Tangazo la Serikali Na.143 (Linaendelea.) _________ JEDWALI LA KWANZA ________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(1)) A: USHURU WA STENDI (KUINGIA NA KUTOKA) Na. Aina ya Chombo cha usafiri
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: This section lists fees for different vehicle types and passenger-capacity bands at a stand, with payment noted as due each time the vehicle departs.
9. Basi lenye uwezo wa kubeba abiria 5 hadi 15 Basi lenye uwezo wa kubeba abiria 16 hadi 25 Basi kubwa lenye uwezo wa kubeba abiria 26 hadi 35 Basi kubwa lenye uwezo wa kubeba abiria 35 na zaidi Teksi Pikipiki ya magurudumu mawili Pikipiki ya magurudumu matatu Gari dogo aina ya Noah Gari lolote dogo lisilotajwa hapo juu Kiwango cha ushuru (Shilingi) Muda wa kutoza 2,000/= Kila linapotoka 2,000/= 2,000/= 3,000/= 1,000/= 3,00/= 3,00/= 500/= 500/= Kila linapotoka Kila linapotoka Kila linapotoka Kila linapotoka Kila linapotoka Kila linapotoka Kila linapotoka Kwa linapotoka B: USHURU WA STENDI (KULAZA CHOMBO CHA USAFIRI) Na. Aina ya Chombo cha usafiri - 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: This section lists daily station tax amounts for several vehicle types.
10. Basi lenye uwezo wa kubeba abiria 5 hadi 15 Basi lenye uwezo wa kubeba abiria 16 hadi 25 Basi kubwa lenye uwezo wa kubeba abiria 26 hadi 35 Basi kubwa lenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 35 Teksi Pikipiki ya magurudumu mawili Pikipiki ya magurudumu matatu Gari dogo aina ya Noah Gari lolote dogo lisilotajwa hapo juu Magari ya mizigo Kiwango cha ushuru (Shilingi) kwa siku 3,000/= 3,000/= 3,000/= 3,000/= 1,000/= 1,000/= 1,000/= 1,500/= 1,000/= 5,000/= C: USHURU WA STENDI (MENGINEYO) Na. Aina ya Ushuru Kiwango (Shilingi) cha ushuru Idadi - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: This section lists fees for entering or leaving the bus stand, carrying luggage, small traders without entrepreneur IDs, and using the toilet, and it also includes a form for voluntarily admitting an offence.
4. Mtu anayeingia au kutoka stendi Wabeba mizigo stendi Wafanyabiashara biashara ndogo ndogo wasio na vitambulisho vya ujasiliamali Choo cha stendi 200/= 1,000/= 1,000/= kila anapoingia au kutoka kwa siku kwa siku 300/= kila anapoingia chooni 8 Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe Tangazo la Serikali Na.143 (Linaendelea.) _____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 8 (1)) FOMU YA KIBALI CHA KUANZISHA KITUO CHA MABASI BINAFSI Kibali Na. ................... Jina: ................................................................................................ Anwani: ........................................................................................... Namba ya NIDA: .............................................SIMU......................... Namba ya Stakabadhi: .....................amelipa Sh.................................. Eneo Kituo kilipo: Mtaa:..……………Barabara:……..Jengo:………......… Ukubwa wa eneo la Kituo au Maegesho (mita za mraba):…....... Kiasi kilicholipwa kwa miezi ………….. Jumla ya sh............................... Muda wa kibali ni mwaka mmoja kuanzia ...................... hadi ...................... Maelezo ………………………………………………..………......……… ………………………………………………………………………………………………………… ……………… yatakayohitajika mengine (kama yapo): Kimetolewa tarehe…………mwezi……………….mwaka……….........….. Kimetolewa na: Jina: ……………………………………………………….......…………….. Wadhifa:………………………………………………….…………………. Saini.................................................. Muhuri wa Ofisi:.………….................... “Fomu hii itawekwa katika Ofisi ya Kituo cha basi. Kumbuka kuzingatia Sheria zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria Ndogo za Halmashauri”. 9 Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe Tangazo la Serikali Na.143 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA TATU __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 18) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ..................................................................... nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya ..................................................................... ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, kwamba mnamo tarehe .......... ya mwezi .......................mwaka ........................... nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya...............ya Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe ya Mwaka 2025. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, niko tayari kulipa ushuru ninaodaiwa wa kiasi cha shilingi …………………. pamoja na faini ya kufifilisha kosa ya kiasi cha shilingi ………………………. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU NA KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe .....................ya Mwezi ......................... Mwaka ...................................... Jina .................................................... Saini ............................................................. MBELE YA: Jina: ....................................................... Wadhifa: .................................................... Saini .......................................................... Tarehe ........................................................ 10 Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe Tangazo la Serikali Na.143 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Mji Njombe imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia Azimio lililopitishgwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri yam ji Njombe uliuofanyika tarehe 3/5/2023 na kushuhudiwa lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- KURUTHUM A. SADIK, Mkurugenzi, Halmashauri ya Mji Njombe ERASTO B. MPETE, Mwenyekiti, Halmashauri ya Mji Njombe L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Agosti, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB.), Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Mji Njombe ya Mwaka 2025
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in