Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ya Mwaka 2020
This bylaw is titled the Pangani District Council Environmental Conservation Bylaw, 2020.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ya Mwaka 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This bylaw is titled the Pangani District Council Environmental Conservation Bylaw, 2020. This bylaw applies throughout the area under the Pangani District Council. This section defines key terms used in the by-law, including the authorized officer, the Council, protected areas, environmental protection, and several waste and natural-resource terms. Kila mtu, taasisi au asasi lazima ilinde, itunze na ihifadhi mazingira. Halmashauri must work with Baraza to enforce this by-law, educate the public on environmental management and conservation, protect the environment, and encourage public participation.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ya Mwaka 2020
Showing 52 of 52
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This bylaw is titled the Pangani District Council Environmental Conservation Bylaw, 2020.
1. Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ya Mwaka 2020. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the area under the Pangani District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote lililo chini ya Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including the authorized officer, the Council, protected areas, environmental protection, and several waste and natural-resource terms.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa umma atakayeteuliwa na Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; Sura ya 191; 1 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) “Baraza” maana yake ni Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira lililoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 16(1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “maeneo ya hifadhi’’ ni maeneo ya milima, maeneo ya vyanzo vya maji, hifadhi ya misitu, miteremko na maeneo mengine ambayo yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Pangani; “hifadhi ya mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi, mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji vinavyozingatia masharti na maelekezo yatakayotolewa na Afisa Mwidhinishwa chini ya Sheria Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote; “madini ya ujenzi” maana yake ni kokoto, mawe, changarawe, mchanga, chokaa, marumaru, kifusi, udongo mfinyanzi, au chochote kinachochimbwa na kupatikana katika Mamlaka ya Halmashauri kwa shughuli za ujenzi; “mazingira” maana yake maumbile halisi yawazungukao binadamu ikiwa ni pamoja tabianchi, sauti, na hewa, ardhi, maji, mwanga, harufu, ladha, vijiumbe, hali za kibiolojia za wanyama na mimea, rasilimali za kitamaduni na masuala ya uchumi jamii na inahusisha mazingira asilia na yaliyoundwa na binadamu na jinsi 2 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) yanavyoingiliana; Sura ya 323 “Mkurugenzi”maana yake ni Mkurugenzi wa au Afisa yeyote wa atakayeteuliwa kutekeleza Halmashauri Halmashauri majukumu ya Mkurugenzi; “misitu” maana yake ni eneo la ardhi ambalo limefunikwa angalau kwa asilimia 10 ya miti, uoto wa asili au iliyopandwa, au asilimia 50 au zaidi, ya vichaka na miti na miti inayoota upya ambayo itajumuisha aina yote ya misitu ya hifadhi ambayo itatangazwa chini ya Sheria ya Misitu, na mazao yote ya misitu ikijumuisha majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri; “mifugo” maana yake ni Ng’ombe, punda, kondoo, mbuzi, nguruwe, mbwa na mifugo mingine ifugwao na binadamu; "ndege" inajumuisha kuku, bata, kanga, njiwa na jamii nyingine ya ndege; “taka” maana yake ni kitu chochote kimiminika, kigumu, gesi na mionzi, kinachotoa harufu mbaya, katika mazingira ya hali ya ujazo, uozo au hali nyingine yoyote inayosababisha uharibifu wa mazingira; kilichohifadhiwa au “taka gesi” maana yake ni hewa chafu, moshi, joto, au harufu ambayo inaweza kuleta madhara kwa binadamu, mazingira, na viumbe hai wengine; “taka ngumu” maana yake ni taka ambazo haziko kutoka majumbani, katika majengo ya biashara, umajimaji katika 3 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) Sura ya 191 viwandani na kutoka katika shughuli za kilimo, pamoja na taka za vyakula, karatasi plastic au taka laini zinazotokana na ujenzi au ubomoaji majengo utengenezaji bustani na shughuli za uchimbaji madini, mizoga ya wanyama na mabaki ya magari mabovu (scraps); “taka yenye madhara” maana yake ni kitu chochote kigumu, majimaji, cha gesi au taka majimaji ambayo kwa sababu ya athari athari kwa mazingira na binadamu, maambukizo yake, kiwango chake cha sumu, ulipukaji na kulika/kubabuka kwake kinadhuru afya, maisha ya binadamu au mazingira; zake kikemikali, “taka vimiminika” maana yake ni taka zilizo katika hali ya maji au vimiminika zitokazo majumbani, kwenye kilimo, au viwandani maeneo ya biashara zilivyofanyiwa zisivyofanyiwa usafishaji; au “taka za viwanda” maana yake ni taka zitokanazo na viwanda vinavyozalisha au visivyozalisha, ambayo ni chanzo cha nishati, maji, mitambo ya kusafisha au mawasiliano; “udongo” kama ilivyo katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, maana yake ni pamoja na dunia, mchanga, miamba, miamba tope, madini, uoto wa mimea, mimea na wanyama iliyoko chini ya udongo pamoja na vumbi; “vyanzo vya maji” maana yake ni mahali popote ambapo maji yanapatikana 4 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) katika uhalisia wake na panaweza kuwekwa miundombinu ya maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na viumbe hai wengine. SEHEMU YA PILI UHIFADHI WA MAZINGIRA Wajibu wa kulinda, kutunza na kuhifadhi mazingira
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Itakuwa ni Wajibu wa kila mtu, taasisi au
AI-assisted research summary: Kila mtu, taasisi au asasi lazima ilinde, itunze na ihifadhi mazingira.
4. Itakuwa ni Wajibu wa kila mtu, taasisi au asasi yoyote kulinda, kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kuhakikisha kwamba- (a) anafanya shughuli au kusababisha uharibifu au uchafuzi wa mazingira; zisizoathiri (b) anashiriki katika jitihada mbalimbali za utunzaji, uhifadhi na uendelezaji wa mazingira; na (c) anatoa taarifa kwa Halmashauri au mamlaka nyingine husika kuhusu uwepo wa inayoathiri au inayoweza kuathiri mazingira au uwepo wa viashiria vya uharibifu wa mazingira. shughuli yoyote Jukumu la Halmashauri na Baraza - 5 Verify source ↗
Itakuwa ni jukumu la Halmashauri kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri must work with Baraza to enforce this by-law, educate the public on environmental management and conservation, protect the environment, and encourage public participation.
5. Itakuwa ni jukumu la Halmashauri kwa kushirikiana na Baraza- (a) kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; (b) kutoa elimu ya usimamizi, utunzaji na uhifadhi wa mazingira; (c) kulinda mazingira; na (d) kuhamasisha umma kushiriki katika masuala ya usimamizi wa mazingira. Maeneo ya hifadhi - 6 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na jukumu la
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ihakikishe maeneo yaliyohifadhiwa hayavamwi, na mtu au taasisi inayotaka kufanya shughuli huko lazima iombe kibali cha Halmashauri.
6. (1) Halmashauri itakuwa na jukumu la 5 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) kuhakikisha maeneo yaliyohifadhiwa hayavamiwi. (2) Mtu yeyote, taasisi au asasi inayotaka kufanya shughuli yoyote katika sehemu au maeneo yaliyohifadhiwa ataomba kibali cha Halmashauri. Siku ya Mazingira - 7 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Siku ya Mazingira
AI-assisted research summary: Watu wote wanapaswa kushiriki katika shughuli za kuhamasisha usimamizi na uhifadhi wa mazingira, na kila mtu anaendelea na wajibu wa kutunza mazingira katika eneo lake.
7. (1) Kutakuwa na Siku ya Mazingira ambayo watu wote watashiriki katika uhamasishaji wa shughuli za usimamizi na uhifadhi wa mazingira. (2) Siku hii inaweza kutumika kutoa elimu ya usimamizi wa mazingira kwa umma na kutoa tuzo kwa mtu yeyote, taasisi au asasi ambayo imeshiriki vyema katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na Halmashauri. (3) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1) hapo juu, kila mtu ataendelea kutekeleza wajibu wa kusimamia, kutunza na kuhifadhi mazingira katika maeneo yake. Uchimbaji wa madini ya ujenzi - 8 Verify source ↗
(1) Kwa lengo la usimamizi wa mazingira
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge maeneo maalumu ya kuchimba madini ya ujenzi, na mtu yeyote haruhusiwi kuchimba madini hayo kwenye makazi ya watu, maeneo yaliyohifadhiwa kando ya mito, ndani ya mto au bwawa, isipokuwa kwa ruhusa maalumu ya Halmashauri.
8. (1) Kwa lengo la usimamizi wa mazingira Halmashauri itatenga maeneo maalumu kwa ajili ya kuchimba madini ya ujenzi. Karakana na gereji (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba madini ya ujenzi katika makazi ya watu, maeneo yaliyohifadhiwa kando kando ya mito, ndani ya mto, bwawa au katika maeneo yasiyoruhusiwa isipokuwa kwa ruhusa maalumu ya Halmashauri. - 9 Verify source ↗
Matengenezo ya magari, pikipiki au
AI-assisted research summary: Matengenezo ya magari, pikipiki au mitambo yanapaswa kufanyika katika karakana, gereji au maeneo maalumu yaliyoruhusiwa na Halmashauri.
9. Matengenezo ya magari, pikipiki au mitambo yatatakiwa kufanyika katika karakana, gereji au maeneo maalumu yaliyoruhusiwa kwa kibali cha Halmashauri. 6 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) Uoshaji wa vyombo vya moto - 10 Verify source ↗
Ni marufuku kwa mtu yeyote kuosha gari,
AI-assisted research summary: It is forbidden for anyone to wash a car, motorcycle, or machine in road-related or open public areas, or to change the use of land not set aside for those activities.
10. Ni marufuku kwa mtu yeyote kuosha gari, pikipiki au mtambo kwenye eneo la barabara, hifadhi ya barabara, njia ya waenda kwa miguu, mtaa, maeneo ya wazi, kando ya mito, maziwa, au kubadilisha matumizi ya eneo lolote ambalo halikutengwa kwa shughuli za aina hizo. Usimamizi wa mazingira ya machinjio - 11 Verify source ↗
Halmashauri
AI-assisted research summary: The Halmashauri must regularly inspect slaughterhouse areas and make sure they do not pollute the environment and meet the listed sanitation and infrastructure conditions.
11. Halmashauri itasimamia maeneo ya machinjio kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika machinjio na kuhakikisha kuwa- (a) shughuli za machinjio hazichafui mazingira; (b) eneo lote la kuchinjia limejengwa na kusakafiwa kwa saruji au marumaru; (c) mifugo inachinjwa katika eneo la kuchinjia; (d) kuna upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama; na (e) kumetengwa eneo maalumu zitokanazo na machinjio. la kukusanyia taka Usimamizi na utunzaji wa fukwe na mialo - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itawajibika kuweka utaratibu
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima iandae utaratibu wa kusimamia, kutunza, na kusafisha fukwe au mialo; biashara kwenye maeneo hayo zinahitaji kibali cha Halmashauri; na wenye nyumba au hoteli zilizo karibu hawaruhusiwi kumwaga maji taka au kutupa taka humo.
12. (1) Halmashauri itawajibika kuweka utaratibu wa kusimamia, kutunza, na kusafisha fukwe au mialo katika maeneo yao. (2) Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya shughuli za biashara katika maeneo ya fukwe au mialo bila kibali cha Halmashauri. (3) Mmiliki wa nyumba au Hoteli iliyo karibu na fukwe au mialo hataruhusiwa kutiririsha maji taka au 7 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) kutupa taka ya aina yoyote katika maeneo hayo. SEHEMU YA TATU USIMAMIZI WA TAKA Usimamizi wa taka
Part
SEHEMU YA TATU
- 13 Verify source ↗
Halmashauri itaweka utaratibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima iandae utaratibu wa kukusanya na kutupa taka, itenge maeneo maalumu ya kukusanyia taka, na itoe elimu ya kuchambua aina za taka.
13. Halmashauri itaweka utaratibu wa ukusanyaji na utupaji wa taka ambapo- (a) itatenga maeneo maalumu ya kukusanyia taka; na (b) itatoa elimu ya uchambuzi wa aina za taka. Uchambuzi wa taka - 14 Verify source ↗
(1) Ili kutoa nafasi ya usimamizi,
AI-assisted research summary: Waste must be sorted and collected by category before supervision, transport, and disposal.
14. (1) Ili kutoa nafasi ya usimamizi, usafirishaji na utupaji taka, taka zote zitachambuliwa na kukusanywa kulingana na makundi yafuatayo: (a) taka zenye madhara au hatarishi; (b) taka zenye ncha kali; (c) taka za hospitali; na (d) taka rejea. Uhifadhi wa viwandani taka za - 15 Verify source ↗
(1) Kila kiwanda kitakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila kiwanda lazima kitenge na kitumie maeneo maalumu ya kukusanya taka za kiwandani, na viwanda vinavyozalisha taka ngumu au taka vimiminika lazima vihifadhi au visafishe taka hizo kabla ya kuzipeleka kutupwa katika maeneo maalumu.
15. (1) Kila kiwanda kitakuwa na wajibu wa kutenga na kutumia maeneo maalumu ya kukusanya taka zinazotokana na shughuli za kiwandani. (2) Kiwanda kinachozalisha taka ngumu, kitahakikisha kwamba taka hizo zinahifadhiwa katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili hiyo kabla ya kusafirishwa kwenda kutupwa katika maeneo maalumu. (3) Kiwanda kinachozalisha taka vimiminika kitahakikisha kwamba taka hizo zinasafishwa ili zisiwe na madhara kwa mazingira na kwa afya na zinahifadhiwa katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili hiyo kabla ya kusafirishwa kwenda kutupwa katika maeneo maalumu yaliyotengwa. 8 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) Ukaguzi wa viwanda Marufuku ya kutiririsha taka vimiminika Ukusanyaji na uzoaji wa taka Taka za Hospitali - 16 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikague viwanda ili kuona kama vimetenga na kutumia maeneo maalumu ya kukusanya taka.
16. Halmashauri itakuwa na wajibu wa kukagua viwanda kama vimetenga na kutumia maeneo maalumu ya kukusanya taka kwa mujibu wa masharti ya Sheria Ndogo hii. - 17 Verify source ↗
Itakuwa ni marufuku kutiririsha au
AI-assisted research summary: It is prohibited to discharge or direct wastewater, liquid waste, or rainwater from factories, homes, or other buildings into water sources, roads, corridors, rivers, open areas, or any place not set aside for that purpose.
17. Itakuwa ni marufuku kutiririsha au kuelekeza maji taka, taka vimiminika au maji ya mvua kutoka viwandani, majumbani, majengo mengine kwenda kwenye vyanzo vya maji, barabarani, ushoroba, mtoni, maeneo ya wazi au sehemu yoyote isiyotengwa kwa ajili hiyo. - 18 Verify source ↗
(1) Halmashauri itasimamia shughuli
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima isimamie ukusanyaji na uzoaji wa taka, na shughuli hizo zinaweza kufanywa na Halmashauri au wakala wake.
18. (1) Halmashauri itasimamia shughuli za ukusanyaji na uzoaji wa taka kutoka katika maeneo ya masoko, biashara na maeneo mengineyo zitakusanywa, kuzolewa na kutupwa kulingana na aina ya taka husika. (2) Shughuli za ukusanyaji na uzoaji wa taka zinaweza kufanywa na Halmashauri au wakala wake. - 19 Verify source ↗
Ukusanyaji, usafirishaji na utupaji wa
AI-assisted research summary: Hospital waste and expired medicines must be collected, transported, and disposed of according to procedures set by law, regulations, and health service guidelines.
19. Ukusanyaji, usafirishaji na utupaji wa taka za Hospitali na dawa zilizofikia ukomo wa matumizi utafanyika kutokana na taratibu zilizowekwa na Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali ya utoaji wa huduma za afya. Udhibiti wa taka gesi - 20 Verify source ↗
(1) Uzalishaji wa taka gesi
AI-assisted research summary: Halmashauri inasimamia uzalishaji wa taka gesi, hutenga maeneo maalumu ya viwanda hivyo, na hupiga marufuku matumizi ya samadi kama nishati ya kupikia ndani ya nyumba.
20. (1) Uzalishaji wa taka gesi utadhibitiwa na Halmashauri kwa- (a) kutenga maeneo maalumu ya ujenzi wa viwanda vinavyozalisha taka gesi; na (b) kupiga marufuku matumizi ya samadi kama nishati ya kupikia ndani ya nyumba. (2) Viwanda vya kuzalisha taka gesi vitajengwa katika maeneo yaliyombali na makazi ya watu. - 21 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni wajibu wa kila Mchuuzi wa
AI-assisted research summary: Wachuuzi wa miwa, matunda au mbogamboga lazima wahakikishe wana vyombo maalumu vya kuhifadhia maganda au mabaki ya bidhaa, na biashara hiyo imepigwa marufuku katika maeneo yasiyoruhusiwa.
21. (1) Itakuwa ni wajibu wa kila Mchuuzi wa miwa, matunda au mbogamboga kuhakikisha kuwa ana Wachuuzi wa miwa, matunda na mboga mboga 9 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) wa Udhibiti taka zinazozalishwa kutoka katika vya usafiri vyombo chombo maalumu cha kuhifadhia maganda au mabaki ya bidhaa. (2) Ni marufuku mtu yeyote kufanya biashara ya au mbogamboga katika maeneo miwa, matunda yasiyoruhusiwa. - 22 Verify source ↗
(1) Magari au mabasi yote yanayobeba abiria
AI-assisted research summary: Magari na mabasi yanayobeba abiria lazima yaweke vyombo vya taka na kuwaelekeza abiria kuyatumia; pia ni marufuku kwa mtu aliye ndani ya chombo cha usafiri kutupa kitu nje.
22. (1) Magari au mabasi yote yanayobeba abiria- (a) yatapaswa kuweka vyombo maalumu vya kutupia taka zinazozalishwa na kuwataarifu abiria matumizi ya vifaa hivyo; na (b) yatakusanya na kutupa taka katika eneo ajili ya lililotengwa kwa kukusanya na uzoaji wa taka katika kama vituo na itakavyokuwa Halmashauri. vya mabasi imeelekezwa au (2) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote akiwa ndani ya gari, basi au chombo chochote cha usafiri kutupa nje kitu chochote. Chukizo au kero - 23 Verify source ↗
Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuweka
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kuweka au kujenga kitu kinachoweza kusababisha kero au uchafu na kuleta madhara, kelele, au magonjwa.
23. Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuweka au kujenga kitu chochote kinachoweza kusababisha kero au kilicho katika hali ya uchafu ambacho kinaweza kusababisha- (a) madhara kwa maisha ya binadamu, wanyama au viumbe hai wengine; (b) adha, kero, chukizo au kelele kwa watu wengine; na (c) magonjwa. Ilani ya kuondoa kero - 24 Verify source ↗
(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa akigundua kero katika eneo, mmiliki, mpangaji, mtumiaji au aliyesababisha kero anatakiwa kuiondoa ndani ya muda ulioainishwa kwenye Ilani.
24. (1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwepo kwa eneo lenye kero ya aina yoyote atamtaka mmiliki wa eneo husika, mpangaji, mtumiaji au mtu yeyote aliyesababisha kero hiyo kuondoa kero hiyo ndani ya muda utakaoainishwa kwenye Ilani. 10 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) Utupaji mbalimbali wa taka Huduma ya maeneo ya kutupa taka (2) Endapo Halmashauri italazimika kuondoa kero, gharama za kuondoa kero husika zitalipwa na mtu aliyesababisha kuwepo kwa kero hiyo. - 25 Verify source ↗
Wazalishaji wa taka zitokanazo na madawa ya
AI-assisted research summary: Wazalishaji wa taka hizi lazima wakusanye, wazoe, watupe au wasafirishe taka kwa kufuata taratibu za Halmashauri.
25. Wazalishaji wa taka zitokanazo na madawa ya mifugo na kilimo, kemikali, shughuli za kilimo, au aina nyingine yoyote ya taka watakusanya, watazoa na kutupa au kusafirisha taratibu zitakazowekwa na Halmashauri. taka hizo kwa mujibu wa itatenga, - 26 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri must build and operate waste disposal, transfer, and collection facilities, and it may use an agent or partnership to do so.
26.(1) Halmashauri na kuendesha maeneo makuu ya kutupa taka (Sanitary Landfills), maeneo ya kutunza taka kwa muda (Transfer statations) na vituo vya kukusanyia taka (Collection Points) kabla ya kusafirisha kwenda Dampo Kuu. itajenga (2) Halmashauri inaweza kumpa wakala au kuingia ubia katika kujenga na kuendesha maeneo ya kutupa taka. - 27 Verify source ↗
Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote,
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote, kampuni, taasisi au kikundi kufanya shughuli yoyote katika maeneo yaliyotengwa kuwa dampo bila kibali maalumu kutoka Halmashauri.
27. Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote, kampuni au taasisi au kikundi kufanya shughuli yoyote katika maeneo yaliyotengwa kuwa dampo isipokuwa kwa kibali maalumu kitakachotolewa na Halmashauri. - 28 Verify source ↗
Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote, taasisi,
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote, taasisi, au asasi yoyote kutupa, kutiririsha, au kufanya shughuli zinazoingiliana na taka katika maeneo yaliyotajwa.
28. Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote, taasisi, au asasi yoyote- la Zuio shughuli madampo kufanya katika Marufuku ya kutupa taka ovyo (a) kuzalisha na kutupa taka katika maeneo yasiyotengwa kwa ajili hiyo; (b) kutupa taka kwenye mifereji, mitaro, mito, barabara, ufukweni au maeneo ya wazi; (c) kutiririsha maji taka na taka vimiminika kwenye mifereji, mitaro, mito, barabara, au maeneo ya wazi; (d) kufanya biashara, maonyesho ya biashara au shughuli nyingine yoyote katika maeneo ya karibu au ndani au juu ya mifereji au mitaro ya maji, au katika maeneo ya kukusanyia taka, au kwenye dampo; na 11 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) (e) kuweka mabango au kufanya shughuli yeyote itakayozuia matumizi ya maeneo ya hifadhi ya barabara. Wajibu wa Halmashauri SEHEMU YA NNE MASHARTI YA UFUGAJI NA KILIMO
Part
SEHEMU YA NNE
- 29 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge maeneo ya malisho, itenge njia za kupitisha mifugo, ifanye sensa ya mifugo, na itoe kadi inayoonyesha idadi na aina ya mifugo.
29. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya idadi ya malisho kwa kuzingatia mifungo ndani ya Halmashauri; (b) kutenga njia maalumu ya kupitisha mifugo kwenda na kurudi kutoka malishoni, kwenye majosho, malambo au mnadani; (c) kufanya sensa ya mifugo; na (d) kutoa kadi itakayoonyesha idadi na aina ya mifugo. 12 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) Wajibu wa mfugaji - 30 Verify source ↗
Kila mfugaji atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila mfugaji lazima asimamie, atunze na ahifadhi mazingira, na afuate masharti ya Halmashauri kuhusu idadi, malisho, njia za kupitisha mifugo, majosho, chanjo, alama, mafunzo, taka na kuzuiya mifugo kuzurura.
30. Kila mfugaji atakuwa na wajibu wa kusimamia, kutunza na kuhifadhi mazingira kwa- (a) (b) (c) (d) (e) (f) (g) (h) (i) (j) (k) (l) ya mifugo idadi maalumu kufuga idadi ya mifugo kadri itakavyoamriwa na Halmashauri; kufuga na kulisha mifugo katika maeneo ya malisho yaliyotengwa na Halmashauri; kupitisha mifugo katika njia (stock routes) zilizopangwa na kutengwa na Halmashauri; kuwa na kadi ya mifugo itakayoonyesha idadi na aina ya mifugo; kufuga atakayoelekezwa na Halmashauri; kuchukua tahadhari zote muhimu ili kuondoa au kuzuia uwezekano wa kusababisha kero kwa wakaazi wengine wa eneo hilo; kupeleka mifugo katika majosho kama itakavyoagizwa na halmashauri; kupeleka mifugo katika vituo vya chanjo kama itakavyoamriwa na Halmashauri; kuhakikisha mifugo inawekwa alama katika viungo vinavyopendekezwa; kuhudhuria mafunzo ya ufugaji kama atakavyo hitajiwa na Halmashauri; kukusanya na kutupa taka zote zitokanazo na wanyama au ndege wafugwao katika maeneo maalumu ya kutupa taka; kuwa na eneo la kutosha kutunza wanyama hao, na kuhakikisha wanafungwa katika eneo la pamoja na si kuzurura ovyo; na (m) kutokata miti ovyo. 13 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) Masharti ya mfugaji (a) - 31 Verify source ↗
Ni marufuku kwa mfugaji yeyote
AI-assisted research summary: Mfugaji yeyote haruhusiwi kufanya baadhi ya shughuli za mifugo katika maeneo yasiyotengwa au bila kibali cha Halmashauri.
31. Ni marufuku kwa mfugaji yeyote- kunywesha maji kuchunga, kulisha, au mifugo katika mashamba au maeneo yasiyotengwa kwa ajili ya kuchunga, kulishia na kunywesha mifugo; Kudhibiti mifugo inayozurura ovyo (b) (c) kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani au kuhamisha mifugo kutoka eneo moja hadi lingine bila kibali cha Halmashauri; kuuza au kununua mifugo katika maeneo yasiyo ya mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoidhinishwa na Halmashauri; na (d) kufuga mifugo mingi katika eneo dogo kinyume cha maelekezo ya Halmashauri. - 32 Verify source ↗
(1) Mifugo yoyote haitatakiwa kuzurura ovyo
AI-assisted research summary: Livestock must not roam freely in council areas; if seized, the owner must pay the fine within 7 days or the Director may sell the livestock by auction with court approval.
32. (1) Mifugo yoyote haitatakiwa kuzurura ovyo katika maeneo ya Halmashauri. (2) Mifugo yoyote itakayokamatwa kwa kuzurura ovyo it (3) Endapo mwenye mifugo atashindwa kulipa faini ndani ya siku saba (7) tangu kukamatwa kwa mifugo hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri atakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mifugo hiyo baada ya kupata idhini ya Mahakama. (4) Baada ya mauzo kwa mnada mifugo hiyo, Mkurugenzi atatakiwa kukata fedha za faini, gharama za mnada na gharama za ulinzi na fedha zitakazobaki zitarudishwa kwa mmiliki wa mifugo. (5) Endapo mmiliki wa mifugo hataonekana ndani ya siku kumi na nne (14) fedha hizo zitaingizwa katika vyanzo vya mapato vya Halmashauri. (6) Endapo mwenye mifugo atakuwa na sababu za msingi za kutofika kwake katika muda wa siku kumi na nne (14) Halmashauri inaweza kurudisha fedha za mauzo ya mifugo hiyo. (7) Halmashauri haitawajibika kwa gharama zozote end 14 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) Ukaguzi wa mifugo - 33 Verify source ↗
Halmashauri itafanya ukaguzi kwa kuingia
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuingia katika nyumba, jengo au zizi lolote wakati wowote ili kukagua na kuhesabu mifugo.
33. Halmashauri itafanya ukaguzi kwa kuingia katika nyumba, jengo au zizi lolote wakati wowote kwa madhumuni ya kukagua na kuhesabu idadi ya mifugo iliyomo katika nyumba, jengo au zizi hilo. Wajibu wa Halmashauri - 34 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must set aside special grazing areas and livestock routes, and it must conduct a livestock census and issue livestock cards showing the number and type of animals.
34. (1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya- (a) malisho kwa kuzingatia idadi ya mifugo ndani ya eneo la Halmashauri; na (b) njia maalumu ya kupitisha mifugo kwenda na kurudi kutoka malishoni au minadani. (2) Halmashauri itafanya sensa ya mifugo na kutoa kadi za mifugo itakayoonyesha idadi na aina ya mifugo. Taratibu za kilimo - 35 Verify source ↗
Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za kilimo
AI-assisted research summary: A person who wants to carry out farming activities in a council area must follow farming procedures that do not harm the environment.
35. Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za kilimo katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuzingatia taratibu za kilimo zisizoharibu mazingira. Masharti ya kilimo - 36 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima au kutumia vibaya ardhi katika maeneo ya maji na pia kuchoma moto kusafisha shamba bila kibali maalumu cha Halmashauri.
36. (1) Ni marufuku kwa mtu yeyote- (a) kulima katika miteremko, karibu au katika vyanzo oevu yaliyotengwa, kandokando au kwenye kingo za mito, mabwawa na maziwa; au maeneo vya maji (b) kutumia ardhi iliyotengwa kwa ajili ya kilimo jambo jingine kinyume na kwa kufanya kilimo; (c) kusafisha shamba kwa ajili ya kilimo kwa njia ya kuchoma moto isipokuwa kwa kibali maalumu kwa Halmashauri; au cha maandishi kutoka (d) kufanya jambo lolote litakalohatarisha au 15 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) kuleta uharibifu wa mazingira katika maeneo hayo. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1)(c), muda utakaoruhusiwa kuchoma moto rafiki kwa mujibu wa kifungu hiki utakuwa ni kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 4.00 asubuhi. (3) Kwa lengo la usimamizi wa mazingira itakuwa ni Matumizi ya viuatilifu - 37 Verify source ↗
Halmashauri kwa kushirikiana na mamlaka
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima, pamoja na mamlaka za udhibiti wa viuatilifu, iwaelekeze watumiaji kutumia viuatilifu kwa usahihi na ifanye ukaguzi kubaini vile ambavyo si rafiki kwa mazingira.
37. Halmashauri kwa kushirikiana na mamlaka husika za udhibiti wa viuatilifu zitaelekeza matumizi sahihi ya viuatilifu hivyo, na kufanya ukaguzi ili kubaini viuatilifu ambavyo si rafiki kwa mazingira. SEHEMU YA TANO USIMAMIZI WA VYANZO VYA MAJI Wajibu wa kulinda vyanzo vya maji
Part
SEHEMU YA TANO
- 38 Verify source ↗
Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri must manage and protect water sources by placing boundaries, signs, and warning notices to prevent damage or pollution.
38. Halmashauri itawajibika kusimamia na kulinda vyanzo vya maji kwa kuweka mipaka, alama na mabango ya ilani ya kuzuia uharibifu au uchafuzi katika maeneo hayo. Kulinda eneo la hifadhi Uchafuzi wa vyanzo vya maji - 39 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima,
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kulima, kukata miti, kuchunga mifugo, au kuharibu chanzo cha maji ndani ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji; Halmashauri ina wajibu wa kupanda miti rafiki katika vyanzo vya maji.
39. (1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima, kukata miti, kuchunga mifugo katika umbali wa mita sitini (60) toka vyanzo vya maji au kufanya jambo lolote linaloharibu kwa namna yoyote chanzo cha maji na hifadhi ya mazingira. (2) Itakuwa ni wajibu wa Halmashauri kupanda miti rafiki katika vyanzo vya maji. (3) Mtu yeyote hataruhusiwa kumiliki eneo la chanzo cha maji isipokuwa Halmashauri. - 40 Verify source ↗
Bila kuathiri masharti ya kifungu cha 12, ni
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote, kiwanda, taasisi au shirika kufanya jambo lolote linalosababisha uchafunzi wa vyanzo vya maji kwa matumizi ya binadamu, wanyama au viumbe vingine vilivyo hai.
40. Bila kuathiri masharti ya kifungu cha 12, ni marufuku kwa mtu yeyote, kiwanda, taasisi, shirika kufanya jambo lolote ambalo litasababisha uchafunzi wa vyanzo vya maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama au viumbe vingine vilivyo hai. 16 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) Uchenjuaji wa madini - 41 Verify source ↗
Ni marufuku kufanya shughuli za uchenjuaji
AI-assisted research summary: It forbids mining-related processing and placing poisonous substances near or inside water sources, rivers, or other areas used by people or other living things.
41. Ni marufuku kufanya shughuli za uchenjuaji wa madini au kuweka kitu chochote chenye sumu karibu au ndani ya chanzo cha maji au katika mito au maeneo mengine yanayotumiwa na binadamu au viumbe hai wengine. SEHEMU YA SITA HIFADHI YA MISITU Uhifadhi wa uoto wa asili
Part
SEHEMU YA SITA
- 42 Verify source ↗
(1) Kwa lengo la usimamizi wa mazingira
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima zitenge na zitunze maeneo maalumu ya hifadhi za misitu, uoto wa asili, na viumbe hai wengine, na zikihitajika ziyarudishe katika hali ya kawaida ikiwa yameharibiwa.
42. (1) Kwa lengo la usimamizi wa mazingira Halmashauri zitawajibika kutenga na kuyatunza maeneo maalumu kwa ajili ya hifadhi za misitu, uoto wa asili na viumbe hai wengine. (2) Endapo maeneo hayo yatakuwa yameharibiwa, Halmashauri itahakikisha kuwa inayarudisha katika hali yake ya kawaida kwa kupanda miti au kutoendelea kuharibu mazingira na kuwezesha uoto urudi katika hali yake. Uchomaji moto wa misitu - 43 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma
AI-assisted research summary: It is forbidden for anyone to burn a forest, and if a fire starts in the council area, the local leader must warn residents and order them to put it out.
43.(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma moto msitu kwa namna yoyote ile. (2) Iwapo moto utatokea katika eneo la Halmashauri, kiongozi wa eneo husika atawajibika kutoa ishara ya hatari kwa kutumia njia iliyozoeleka kwa kuamuru wakazi wa eneo hilo kwenda kuzima moto huo kabla ya kusababisha madhara na uharibifu wa mazingira. Kibali cha kuchoma moto rafiki - 44 Verify source ↗
Mtu yeyote aliyepata kibali cha kuchoma moto
AI-assisted research summary: A person with a permit to burn must give nearby neighbours 7 days’ notice before burning and put in place fire prevention measures.
44. Mtu yeyote aliyepata kibali cha kuchoma moto rafiki atalazimika kutoa taarifa ya siku saba (7) kwa majirani anaopakana nao kabla ya kuchoma moto katika eneo analokusudia na ataweka njia za kuzuia moto. Ukataji wa miti - 45 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kukata miti
AI-assisted research summary: Inaweka marufuku ya kukata miti, kubangua magome, na kuvuna miti katika maeneo fulani ya misitu; pia inahitaji kibali cha maandishi kwa baadhi ya ukataji na kuagiza Halmashauri kuhakiki ukomavu wa miti kabla ya kibali kutolewa.
45. (1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kukata miti au kubangua magome katika maeneo ya misitu iliyohifadhiwa na isiyohifadhiwa. (2) Mtu yeyote anayetaka kukata miti au mti kwa 17 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) matumizi ya kuchonga vifaa, kujenga nyumba, kutengeneza zizi au shughuli nyinginezo ikiwemo kubangua magome atalazimika kupata kibali cha maandishi toka kwa Mtendaji wa Kijiji au kibali cha Afisa Maliasili wa Halmashauri au wasaidizi wake kwa miti iliyopandwa na kuhifadhiwa na Halmashauri. (3) Kabla ya kutolewa kwa kibali cha kukata miti Halmashauri itatakiwa kuhakiki kama miti inayotarajiwa kuvunwa imekomaa na inafaa kwa ajili ya matumizi. (4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuvuna miti katika msitu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe maalumu ambao ni rasilimali kwa Taifa. Wachoma mkaa na kuni - 46 Verify source ↗
(1)Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga
AI-assisted research summary: The council must set aside designated areas for charcoal burning, and anyone who wants to burn charcoal or collect firewood must get a permit from the council.
46.(1)Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kuchoma mkaa. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1) mtu yeyote anayetaka shughuli ya kuchoma mkaa au kukusanya kuni atatakiwa kupata kibali cha Halmashauri. (3) Kibali cha Halmashauri kitatakiwa kuonyesha eneo na muda wa kufanya shughuli ya uchomaji na ukusanyaji wa kuni. Wajibu wa kupanda miti - 47 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote, taasisi au asasi iliyoko katika
AI-assisted research summary: Watu, taasisi, au asasi zilizo katika Halmashauri lazima zipande na zitunze miti katika eneo litakalotajwa na Halmashauri; mtu yeyote pia anaweza kupanda miti katika shamba lake kadiri anavyoona inafaa.
47. (1) Mtu yeyote, taasisi au asasi iliyoko katika Halmashauri atawajibika kupanda na kutunza miti katika eneo itakayoelekezwa na Halmashauri. lake kulingana na idadi (2) Mtu yeyote anaweza kupanda miti katika shamba lake kadiri atakavyoona inafaa. Siku ya kupanda miti - 48 Verify source ↗
Kwa lengo la usimamizi na utunzaji wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must plan a special day for planting trees for environmental management and care.
48. Kwa lengo la usimamizi na utunzaji wa mazingira Halmashauri itapanga siku maalumu kwa ajili ya kupanda miti. SEHEMU YA SABA MAKOSA NA ADHABU Makosa
Part
SEHEMU YA SABA
- 49 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akifanya moja ya vitendo vilivyokatazwa chini ya kifungu hiki, kama vile kushughulika na mifugo, kilimo, taka, maji, misitu au kuzuia afisa bila kibali.
49. Itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote ambaye- (a) ataingiza katika eneo la Halmashauri au atasafirisha 18 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) mifugo ndani au nje ya eneo la Halmashauri bila kibali; (b) atalisha mifugo katika maeneo yasiyoruhusiwa; (c) atafuga mifugo zaidi ya idadi iliyoruhusiwa; (d) atakiuka masharti ya kilimo kwa kulima katika miteremko, vyanzo vya maji, kingo za mito na maziwa, kutumia viuatilifu visivyoruhusiwa kisheria, au atafanya shughuli za kilimo katika maeneo ya lolote malisho ya mifugo au eneo lisiloruhusiwa; jingine (e) atachimba madini ya ujenzi katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri; (f) atatupa taka kwenye mitaro, barabarani, hifadhi ya lolote au vichaka katika eneo barabara, lisiloruhusiwa; (g) atashindwa kushiriki katika siku ya usafi na mazingira iliyopangwa na Halmashauri; (h) ataharibu vyanzo vya maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji; (i) atachafua kwa namna yoyote au kuweka sumu, kemikali au madawa ya aina yoyote kwa namna yoyote ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu na viumbe hai katika vyanzo vya maji au miundombinu ya maji; (j) atachoma moto shamba bila kibali; (k) atavuna mazao ya misitu bila kibali; (l) atakata mti, atachoma mkaa, atakata kuni au kubangua magome ya miti bila kibali katika maeneo ya hifadhi au eneo lolote lisiloruhusiwa bila kibali 19 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) cha Halmashauri; (m) atatupa taka ovyo, atatiririsha maji machafu, kuosha magari au mitambo au kufanya jambo jingine lolote linaloweza kusababisha kero, adha au chukizo kwa watu wengine au kuharibu mazingira; (n) atamzuia afisa mwidhiniwa kutekeleza majukumu yake; au (o) atakwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hii; atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii. - 50 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetenda kosa kwa mujibu wa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote akitenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii na akitiwa hatiani, anaweza kutozwa faini ya hadi shilingi laki tatu, kifungo cha hadi miezi 12 jela, au vyote viwili.
50. Mtu yeyote atakayetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. - 51 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa endapo
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa ikiwa mtu anakiri kosa chini ya Sheria Ndogo hii na baada ya kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Pili; kiasi kinachotozwa hakipaswi kuzidi shilingi 200,000.
51. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa endapo mtu atakiri kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa kumtoza kiasi kisichozidi shilingi laki mbili (200,000) baada ya kujaza fomu maalumu iliyoambatishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii Adhabu Kufifilisha kosa Tangazo la Serikali Namba 96 la Mwaka 2010
Part
Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii
- 52 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii inafuta Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This section repeals the Pangani District Council Environmental Conservation by-law.
52. Sheria Ndogo hii inafuta Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani. 20 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) _____________ JEDWALI LA KWANZA ______________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 32(2)) ____________________ VIWANGO VYA FAINI KWA MIFUGO INAYOZURULA HOVYO. NA. AINA YA MIFUGO Ng'ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Mbwa Ndege Punda KIASI CHA FAINI KWA SIKU 5000 3000 3000 4000 2000 2000 5000 _______________ JEDWALI LA PILI ________________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 51) _______________ HATI YA KUFIFILISHA KOSA Mimi ........................................................................ nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya....................................................... ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwamba tarehe ..........ya Mwezi ................... Mwaka................. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha ……. cha 21 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ya Mwaka 2020. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri niko tayari kulipa kiasi cha shilingi laki mbili badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe ......................ya Mwezi ................................Mwaka …… Jina: ..................................................... Saini: .................................................... Mbele ya: Jina……............................................... Cheo: .................................................. Saini: .................................................. Tarehe: .......................................... 22 Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya Ya Pangani Tangazo La Serikali Na 228 (linaendelea) Muhuri wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani umebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa kufuatia Azimio lililopitishwa kwenye vikao husika vya kamati mbalimbali za Baraza la Madiwani lililofanyika tarehe 03/03/2018 na Mhuri huu ulibandikwa mbele ya:- SEIF ALLY SAID Mwenyekiti wa ) Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ISAYA MUGISHAGWE MBENJE Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Pangani L.S NAKUBALI, DODOMA, 03 Machi, 2020 SELEMANI JAFO, Waziri wa Nchi-OR-TAMISEMI 23
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya (Hifadhi ya Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ya Mwaka 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in