Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge za Mwaka 2025
Kanuni hizi zinaweka utaratibu wa kufungua, kuwasilisha, kusikiliza, na kuhitimisha mashauri ya uchaguzi wa wabunge, pamoja na ada na nyakati mbalimbali za kufuata.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge za Mwaka 2025
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This page preserves the statute’s identified version, provision structure, official source link, and stored legal text for reading and research.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge za Mwaka 2025
Showing 1 of 1
- document Verify source ↗
Document text
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinaweka utaratibu wa kufungua, kuwasilisha, kusikiliza, na kuhitimisha mashauri ya uchaguzi wa wabunge, pamoja na ada na nyakati mbalimbali za kufuata.
Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) TANGAZO LA SERIKALI NA. 431 la tarehe 11/7/2025 SHERIA YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI, (SHERIA NA. 1 YA 2024) ______ KANUNI ______ (Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 146(1)) _______ KANUNI ZA MASHAURI YA UCHAGUZI WA WABUNGE ZA MWAKA 2025 MPANGILIO WA KANUNI Kanuni Maelezo SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI 1. 2. Jina. Tafsiri. SEHEMU YA PILI UWASILISHAJI WA SHAURI LA UCHAGUZI NA DHAMANA YA GHARAMA ZA SHAURI 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. Kupinga uchaguzi. Anayeweza kufungua shauri la uchaguzi. Muundo na maudhui ya hati ya shauri. Wahusika katika shauri. Kuongeza au kubadilisha wahusika katika shauri. Kuwasilisha hati ya shauri. Kukataliwa au kurekebishwa kwa hati ya shauri wakati wa uwasilishaji. Kupeleka hati ya shauri na kuwasilisha majibu. Dhamana ya gharama za shauri. 1 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) SEHEMU YA TATU ORODHA YA KURA ZINAZOPINGWA NA MALALAMIKO DHIDI YA MATOKEO YA UCHAGUZI KATIKA KITUO CHA UCHAGUZI Orodha ya kura zinazopingwa. 12. 13. Malalamiko dhidi ya matokeo ya uchaguzi katika kituo cha uchaguzi. Kupanga tarehe ya kusikiliza shauri. 14. SEHEMU YA NNE UTARATIBU WA KUSIKILIZA MASHAURI YA UCHAGUZI Kuunganisha mashauri. Shauri kusikilizwa na Jaji zaidi ya mmoja. Utoaji wa nyaraka. Usikilizwaji wa awali. Uainishaji wa hoja bishaniwa. Usikilizwaji wa shauri. Utaratibu wa kusikiliza shauri. Shahidi wa mahakama. 15. Mahali na muda wa usikilizwaji wa shauri. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. Matumizi ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai. 25. Sababu ambazo hazikuainishwa kwenye hati ya shauri. 26. Kuahirishwa kwa usikilizwaji wa shauri. 27. Katazo la kuahirisha shauri. 28. Jaji kushindwa kuendelea na shauri. 29. Mlalamikaji kushindwa kuhudhuria. 30. Mlalamikiwa kushindwa kuhudhuria. 31. 32. 33. 34. 35. 36. Kuhudhuria kupitia wakili. Kuondoa shauri. Ukomo wa shauri. Shauri kutotupiliwa mbali kwa sababu ya kasoro ya kiutaratibu. Ada. Kufutwa kwa Kanuni. ___________ MAJEDWALI ___________ 2 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) SHERIA YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI, (SHERIA NA. 1 YA 2024) ______ KANUNI ______ (Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 146(1)) _______ KANUNI ZA MASHAURI YA UCHAGUZI WA WABUNGE ZA MWAKA 2025 SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI Jina Tafsiri Sheria Na. 1 ya 2024 1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge za Mwaka 2025. 2. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “mahakama” maana yake ni Mahakama Kuu ya Tanzania au Mahakama Kuu ya Zanzibar, kadri inavyowezakuwa; “mtendaji wa uchaguzi” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa na Sheria; “msajili” maana yake ni msajili au mrajisi wa mahakama, kaimu msajili au kaimu mrajisi, naibu msajili au kaimu naibu msajili; na “Sheria” maana yake ni Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani. SEHEMU YA PILI UWASILISHAJI WA SHAURI LA UCHAGUZI NA DHAMANA YA GHARAMA ZA SHAURI Kupinga uchaguzi 3. Uchaguzi wa Mbunge utapingwa kwa njia ya shauri la uchaguzi. 3 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) Anayeweza kufungua shauri la uchaguzi 4. Shauri la uchaguzi linaweza kuwasilishwa na mtu yeyote aliyebainishwa chini ya kifungu cha 140(1) cha Sheria. Muundo na maudhui ya hati ya shauri 5.-(1) Kila hati ya shauri itakuwa na jina linaloshabihiana na Fomu A iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi na itaainisha: (a) maelezo binafsi ya mlalamikaji ikiwemo jina, mahali anapoishi, anwani ya barua pepe, namba ya nukushi, namba ya simu na msimbo wa posta iwapo unapatikana; (b) maelezo binafsi ya mlalamikiwa ikiwemo jina, mahali anapoishi, anwani ya barua pepe, namba ya nukushi, namba ya simu na msimbo wa posta, endapo vinafahamika; (c) sababu za kuleta shauri; na (d) nafuu zinazoombwa. (2) Kila hati ya shauri itakuwa katika aya zenye aya, kwa kadri namba zinazofuatana, na kila inavyowezekana, itajikita katika maudhui tofauti. Wahusika katika shauri 6.-(1) Mwanasheria Mkuu wa Serikali atakuwa miongoni mwa walalamikiwa katika kila shauri, isipokuwa kwa shauri alilowasilisha mwenyewe. aliyeshinda (2) Endapo shauri lina madai yanayohusu mwenendo mbaya au ukiukwaji wa masharti yoyote ya Sheria au masharti ya sheria nyingine yoyote uliofanywa na mgombea au na mtu yeyote anayemwakilisha au kwa niaba ya mgombea aliyeshinda, mgombea aliyeshinda ataunganishwa kama mhusika katika shauri pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. (3) Endapo shauri lina madai ya mwenendo mbaya au ukiukwaji wa masharti yoyote ya Sheria au sheria nyingine yoyote uliofanywa na mtendaji wa uchaguzi, mtendaji huyo wa uchaguzi ataunganishwa kama mhusika katika shauri pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. (4) Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaweza kuwaunganisha kama walalamikiwa watu wote ambao wanaweza kuathirika endapo nafuu anayoiomba katika shauri aliloliwasilisha itatolewa. 4 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) Kuongeza au kubadilisha wahusika katika shauri Kuwasilisha hati ya shauri Kukataliwa au kurekebishwa kwa hati ya shauri wakati wa uwasilishaji 7. Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mhusika pekee katika shauri na kwa madhumuni ya kuamua masuala husika mahakama inaona inafaa au ni muhimu mgombea aliyeshindwa au mtu mwingine yeyote aunganishwe kuwa mhusika katika shauri, mahakama inaweza kutoa amri ya kumuunganisha mgombea aliyeshindwa au mtu huyo mwingine kuwa mhusika katika shauri, na amri hiyo itakapotolewa, shauri litaahirishwa hadi wakati ambapo mtu ambaye anapaswa kuunganishwa katika shauri amepewa nakala ya hati ya shauri. 8.-(1) Hati ya shauri itawasilishwa ndani ya siku thelathini tangu tarehe ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi kwa kuiwasilisha kwa msajili na kwa kulipa ada iliyoainishwa. (2) Shauri litafunguliwa katika masjala ya mahakama iliyopo katika jimbo ambalo uchaguzi wake unakusudiwa kupingwa. (3) Shauri linaweza kuwasilishwa na mlalamikaji au wakili wake. 9.-(1) Endapo hati ya shauri haijaandaliwa kwa namna inaweza iliyoainishwa katika kanuni ya 8, kukataliwa na kurudishwa kwa mlalamikaji kwa ya muda kurekebishwa madhumuni utakaopangwa na msajili. ndani ya (2) Endapo msajili atakataa hati ya shauri lolote, ataandika sababu za kufanya hivyo na kuandika tarehe ya kuwasilishwa na kukataliwa kwa hati hiyo. (3) Mtu yeyote asiyeridhika na uamuzi wa msajili chini ya kanuni hii, anaweza kupeleka maombi ya masahihisho kwa Jaji kwa uamuzi wa upande mmoja utakaotolewa ndani ya siku nne za kuwasilishwa kwa maombi ya masahihisho. (4) Maombi chini ya kanuni hii yanaweza kuwasilishwa kwa maandishi ndani ya siku tano za uamuzi. (5) Endapo uamuzi wa msajili utabadilishwa na Jaji, mlalamikaji anaweza kuwasilisha tena hati ya shauri lake na muda uliotumika tangu alipowasilisha shauri 5 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) lililokataliwa hadi uamuzi wa Jaji katika maombi ya masahihisho katika kuhesabu muda wa ukomo wa kufungua shauri chini ya kifungu cha 144(1) cha Sheria. hautajumuishwa ulipotolewa Kupeleka hati ya shauri na kuwasilisha majibu 10.-(1) Endapo hati ya shauri imewasilishwa na haijakataliwa au kurudishwa kwa mlalamikaji, msajili ndani ya siku tano: (a) atatuma kwa mtendaji wa uchaguzi nakala ya hati ya shauri pamoja na notisi iliyoainishwa katika Fomu B iliyopo katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi; (b) ataagiza kila mlalamikiwa kupelekewa nakala ya hati ya shauri pamoja na notisi iliyoainishwa katika Fomu C iliyopo katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi; na (c) atabandika katika ubao wa matangazo wa shauri mahakama nakala ya hati ya iliyothibitishwa. (2) Upelekaji wa nyaraka zilizotajwa katika kanuni ndogo hii utakuwa kwa njia ya makabidhiano binafsi. (3) Endapo mahakama imeridhika kwamba: (a) mlalamikiwa hawezi kupatikana; (b) mlalamikiwa amekataa kupokea nyaraka; (c) makabidhiano binafsi hayawezi kufanyika bila kucheleweshwa au bila gharama kubwa; au (d) ni vyema kufanya hivyo, inaweza kuelekeza upelekaji wa nyaraka ufanyike kwa njia mbadala kwa namna ambayo mahakama inaweza kuelekeza. (4) Mara baada ya kupokea nakala ya hati ya shauri, mjibu maombi atawasilisha mahakamani majibu yake ndani ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kupokea hati hiyo, isipokuwa kama hana nia ya kupinga shauri. Dhamana ya gharama za shauri 11.-(1) Ndani ya siku kumi na nne baada ya kufungua shauri, mlalamikaji atapeleka maombi kwa ajili uamuzi wa kiwango kinachopaswa kulipwa kama dhamana ya gharama za shauri. 6 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) (2) Utaratibu wa kuweka dhamana ya gharama za shauri utakuwa kama ulivyoainishwa chini ya kifungu cha 140 cha Sheria. (3) Endapo mlalamikaji ana uwezo wa kifedha na yuko tayari kuweka kiwango cha juu cha dhamana ya gharama za shauri kilichoainishwa chini ya kifungu cha 140(2) cha Sheria, hatahitajika kupeleka maombi kwa ajili ya uamuzi wa kiwango kinachopaswa kulipwa kama dhamana ya gharama za shauri, isipokuwa ataweka kiwango hicho ndani ya siku kumi nne tangu kufungua shauri. (4) Hakuna dhamana ya gharama za shauri itakayowekwa na mlalamikaji ambaye amepewa msaada wa kisheria chini ya Sheria ya Msaada wa Kisheria. Sura ya 21 SEHEMU YA TATU ORODHA YA KURA ZINAZOPINGWA NA MALALAMIKO DHIDI YA MATOKEO YA UCHAGUZI KATIKA KITUO CHA UCHAGUZI Orodha ya kura zinazopingwa 12.-(1) Endapo mlalamikaji au mlalamikiwa anaomba uchunguzi wa kura chini ya kifungu cha 145(1)(d) cha Sheria, atawasilisha kwa msajili orodha ya kura anazokusudia kuzipinga na pingamizi kwa kila kura ndani ya siku zisizopungua sita kabla ya siku iliyopangwa kwa ajili ya usikilizwaji wa shauri, na hakuna ushahidi utakaotolewa wakati wa usikilizwaji wa shauri dhidi ya uhalali wa kura yoyote au kuunga mkono pingamizi lolote ambalo halijaainishwa kwenye orodha hiyo, isipokuwa kwa ruhusa ya mahakama na kwa masharti ambayo mahakama inaweza kutoa. (2) Nakala ya orodha chini ya kanuni hii itatumwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi na kwa kila mhusika katika shauri. Malalamiko dhidi ya matokeo ya uchaguzi katika kituo cha uchaguzi 13.-(1) Endapo mlalamikaji anadai kuwa mgombea mwingine yeyote tofauti na mlalamikiwa alichaguliwa kihalali, atawasilisha kwa msajili orodha ya matokeo ya uchaguzi ya kituo cha kupigia kura anayokusudia kuitumia ndani ya siku zisizopungua sita 7 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) Kupanga tarehe ya kusikiliza shauri kabla ya siku iliyopangwa kwa ajili ya usikilizwaji wa shauri. (2) Nakala ya orodha chini ya kanuni hii itatumwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi na kwa kila mhusika katika shauri. (3) Mlalamikaji hatasikilizwa juu ya sababu yoyote ya malalamiko ambayo haijaainishwa katika orodha inayotakiwa kuwasilishwa chini ya kanuni hii, isipokuwa kwa ruhusa ya mahakama na kwa masharti ambayo mahakama inaweza kutoa. 14.-(1) Kwa kuzingatia Kanuni hizi, baada ya kukamilika kwa uwasilishwaji wa nyaraka za shauri, msajili atawapangia, mapema iwezekanavyo, wahusika wote au mawakili wao kufika mbele yake kwa madhumuni ya kupanga tarehe ya kusikilizwa kwa shauri. (2) Endapo mhusika yeyote katika shauri atashindwa kufika mbele ya msajili baada ya kutakiwa kufanya hivyo, msajili ataendelea kupanga tarehe ya usikilizaji bila uwepo wa mhusika huyo na atamtaarifu mhusika huyo kwa maandishi tarehe ya usikilizaji iliyopangwa. (3) Bila kujali masharti mengine yoyote ya Kanuni hizi, endapo suala linapaswa kusikilizwa au endapo wahusika wanapaswa kufika mbele ya mahakama, usikilizaji huo au kufika huko, kama inavyoweza kuwa, kunaweza kuwa kwa njia ya: (a) mkutano kwa njia ya video; au (b) mkutano kwa njia ya simu. SEHEMU YA NNE UTARATIBU WA KUSIKILIZA MASHAURI YA UCHAGUZI Mahali na muda wa usikilizwaji wa shauri 15.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 139 cha Sheria, usikilizwaji wa shauri utafanyika katika muda na mahali kadri msajili anavyoweza kuamua. (2) Msajili anaweza, na atapaswa kama ataelekezwa na mahakama kufanya hivyo, kutoa notisi ya siku, muda na mahali ambapo shauri litasikilizwa kwa kila mhusika katika shauri na kubandika notisi hiyo kwenye ubao wa matangazo wa mahakama au kutangaza katika 8 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) magazeti kama anavyoweza kuona inafaa au kama mahakama inavyoweza kuelekeza. (3) Kila shauri litasikilizwa katika mahakama ya wazi. Kuunganisha mashauri Shauri kusikilizwa na Jaji zaidi ya mmoja Utoaji wa nyaraka Usikilizwaji wa awali 16. Endapo mashauri mawili zaidi yamewasilishwa kuhusiana na uchaguzi mmoja, mahakama inaweza kuelekeza kwamba baadhi au mashauri hayo yote yaunganishwe na kusikilizwa kama shauri moja. au 17.-(1) Jaji Mkuu anaweza kuelekeza kuwa shauri lolote lisikilizwe na Jaji zaidi ya mmoja endapo kwa maoni yake, ataona kuwa shauri hilo linaweza kuibua hoja ngumu za kisheria au zisizo za kisheria au zote kwa pamoja. (2) Pale shauri linaposikilizwa na Jaji zaidi ya mmoja, litaamuliwa kulingana na maamuzi ya majaji walio wengi. 18.-(1) Kabla au siku ya usikilizaji wa awali, wahusika katika shauri au mawakili wao, watatoa ushahidi wote wa nyaraka ulio katika milki au mamlaka yao, wanaokusudia kuutumia na ambao bado haujawasilishwa mahakamani pamoja na nyaraka zote ambazo mahakama imeamuru zitolewe. (2) Mahakama itapokea nyaraka zilizotolewa ikiwa tu zimeambatana na orodha sahihi iliyoandaliwa katika namna ambayo mahakama inaweza kuelekeza. 19.-(1) Mara baada ya kukamilika kwa uwasilishwaji wa nyaraka za shauri, mahakama itafanya usikilizaji wa awali mbele ya wahusika au mawakili wao ili kuainisha masuala yasiyobishaniwa kati ya wahusika wa shauri na yatakayowezesha usikilizwaji wa shauri kwa haki na haraka. (2) Mahakama itajiridhisha kutoka kwa wahusika na kupitia nyaraka za shauri, masuala ya kisheria au yasiyo ya kisheria yasiyobishaniwa. (3) Mwishoni mwa usikilizaji wa awali chini ya itaandaa hati ya masuala kanuni hii, mahakama 9 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) yasiyobishaniwa na hati hiyo itasomwa na kufafanuliwa kwa wahusika wa shauri au mawakili wao. (4) Hati iliyoandaliwa chini ya kanuni hii itasainiwa na wahusika wa shauri au mawakili wao pamoja na Jaji. (5) Suala lolote au nyaraka yoyote iliyokubaliwa na kuainishwa katika hati iliyoandaliwa chini ya kanuni hii, itachukuliwa kuwa imethibitishwa. (6) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (5), endapo wakati wa usikilizwaji wa shauri mahakama ina maoni kwamba maslahi ya haki yanahitaji hivyo, mahakama suala lililokubaliwa au nyaraka iliyopokelewa katika hati iliyoandaliwa chini ya kanuni hii vithibitishwe rasmi. kuelekeza kwamba inaweza Uainishaji wa hoja bishaniwa Usikilizwaji wa shauri 20. Baada ya usikilizaji wa awali kukamilika, mahakama itaainisha masuala ambayo wahusika wa shauri wanabishania na kuandika hoja bishaniwa ambazo uamuzi sahihi wa shauri unaonekana kuzitegemea. 21.-(1) Usikilizwaji wa mashauri ya uchaguzi utakuwa kwa njia ya maelezo ya maandishi ya mashahidi badala ya ushahidi wa msingi wa kuhojiwa. (2) Mashahidi wataitwa na kuapishwa kwa namna sawa na ile ya usikilizwaji wa mashauri ya madai katika utekelezaji wa mamlaka ya awali, na bila kuathiri masharti ya sheria nyingine yoyote, watawajibika kwa adhabu sawa na ile ya kutoa ushahidi wa uongo au kutohudhuria mahakamani. (3) Baada ya usikilizaji wa awali, na ndani ya saa zisizopungua arobaini na nane kabla ya muda uliopangwa na mahakama kusikiliza shauri la uchaguzi, mlalamikaji atawasilisha kwa msajili maelezo ya maandishi ya kila shahidi ambaye anakusudia kumuita wakati wa usikilizaji yakielezea msingi wa ushahidi wake. (4) Ndani ya saa arobaini na nane za kufungwa kwa shauri la upande wa mlalamikaji, mlalamikiwa atawasilisha kwa msajili maelezo ya maandishi ya kila shahidi anayekusudia kumuita wakati wa utetezi, yakielezea msingi wa ushahidi wake. 10 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) (5) Maelezo ya maandishi ya shahidi chini ya kanuni hii- (a) yatatolewa kwa kiapo au uthibitisho; (b) yatabainisha jina, umri, anwani na kazi ya shahidi; (c) kwa kadri inavyowezekana, yatakuwa katika maneno ya shahidi aliyekusudiwa; (d) yatatambua kikamilifu yoyote inayorejewa katika maelezo bila kurudia yaliyomo isipokuwa kama ni muhimu ili kuitambua nyaraka husika; nyaraka (e) hayatajumuisha masuala ya kutaarifiwa au imani ambayo hayawezi kupokelewa kama ushahidi na endapo yanaweza kupokelewa, yataelezea chanzo cha taarifa au imani; (f) hayatakuwa na nukuu ndefu kutoka kwenye nyaraka au kujikita katika hoja za kisheria au nyinginezo; (g) yatajumuisha tamko la shahidi aliyekusudiwa anaamini kilichoelezwa katika kwamba maelezo hayo ni cha kweli; (h) yatakuwa na tarehe, saini au kuthibitishwa vinginevyo na shahidi aliyekusudiwa; (i) yatakuwa katika aya zilizo na namba; na (j) yatakuwa katika lugha ya mahakama. (6) Ikiwa shahidi haelewi lugha ya mahakama vizuri, lakini anaweza kujieleza na kueleweka na anaweza kuelewa lugha ya mahakama iliyo katika maandishi, maelezo yake yanaweza yasiwe katika maneno yake mwenyewe: Isipokuwa kwamba, litapaswa kubainishwa katika maelezo husika na kuandikwa ili kuelezea kwa usahihi iwezekanavyo msingi wa ushahidi wake. suala hilo (7) Maelezo shahidi yatashabihiana na Fomu D iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi. ya maandishi ya Utaratibu wa kusikiliza shauri 22.-(1) Mhusika wa shauri ambaye kwa niaba yake maelezo ya maandishi ya shahidi yamewasilishwa atahakikisha kuwa shahidi wake anahudhuria wakati wa 11 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) usikilizaji kwa madhumuni ya kutoa rasmi maelezo yake na kuwasilisha vielelezo, kama vipo. (2) Shahidi aliyehudhuria kwa ajili ya utoaji rasmi wa maelezo yake na uwasilishaji wa vielelezo ataapishwa kwa namna iliyoainishwa na sheria inayotumika katika kuapisha mashahidi. (3) Mara baada ya maelezo ya maandishi ya shahidi kutolewa rasmi mahakamani, yatakuwa sehemu ya kumbukumbu ya usikilizwaji wa shauri na yatasomwa kwa sauti kubwa na, au kwa niaba ya, shahidi. (4) Shahidi ambaye maelezo yake yametolewa rasmi anaweza kuhojiwa na upande wa pili wa shauri na kuhojiwa tena na upande uliomuita kutoa ushahidi. (5) Shahidi ambaye maelezo yake hayajatolewa chini ya kanuni ndogo ya (3) au (4) hataruhusiwa kutoa ushahidi bila idhini ya mahakama, na mahakama haitatoa idhini hiyo isipokuwa kama ameonesha sababu za msingi za kushindwa huko. 23.-(1) Wakati wa usikilizwaji wa shauri la uchaguzi, mahakama inaweza kutoa amri ya kumtaka mtu yeyote ambaye inaona kuwa amehusika katika uchaguzi unaohusiana na shauri kuhudhuria kama shahidi. (2) Mahakama inaweza kumhoji shahidi yeyote aliyetakiwa kuhudhuria chini ya kanuni hii na baada ya kumhoji, shahidi huyo anaweza kuhojiwa na au kwa niaba ya mlalamikaji, mlalamikiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali au mwakilishi wake, ikiwa yupo, au yeyote kati yao. (3) Mtu yeyote atakayekataa kutii amri ya mahakama chini ya kanuni hii atakuwa ametenda kosa la kuidharau mahakama chini ya Sheria ya Kanuni za Adhabu na Sheria ya Adhabu. (4) Masharti ya kanuni ya 22 na 23 ya Kanuni hizi hayatatumika kwa shahidi aliyeitwa na mahakama chini ya kanuni hii. Shahidi wa mahakama Sura ya 16 na Sheria Na. 6 ya 2018 ya Zanzibar Matumizi ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai 24. Kwa kuzingatia masharti ya Sheria na Kanuni hizi, usikilizaji, utaratibu na mwenendo wa shauri utatumia, kwa kuzingatia maboresho muhimu kwa kadri yatakavyohitajika, kanuni zinazosimamia utaratibu na 12 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) Sura ya 33 na Sura ya 8 ya Zanzibar mwenendo wa mashauri ya madai kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai na Amri ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai. Sababu ambazo hazikuainishwa kwenye hati ya shauri 25. Mlalamikaji hataleta hoja au kusikilizwa kuhusiana na sababu yoyote ambayo haikuainishwa katika hati ya shauri, isipokuwa kwa ruhusa ya mahakama. Kuahirishwa kwa usikilizwaji wa shauri 26.-(1) Mahakama, kwa maamuzi yake yenyewe au kufuatia maombi ya mhusika katika shauri yaliyoungwa mkono na hati ya kiapo, na baada ya notisi kwa wahusika, inaweza kuahirisha kuanza kwa usikilizwaji wa shauri mpaka siku ambayo inaweza kuelekeza. (2) Mahakama itatuma nakala ya notisi na amri ya kuahirisha iliyotolewa chini ya kanuni hii kwa kila mhusika katika shauri na kubandika nakala nyingine kwenye ubao wa matangazo wa mahakama. (3) Endapo usikilizaji wa shauri hauwezi kuanza au endapo umeanza, hauwezi kuendelea kwa siku iliyopangwa kutokana na kutokuwepo kwa Jaji, usikilizwaji wa shauri hilo utaahirishwa hadi siku inayofuata, au tarehe yoyote inayofaa kwa mahakama hadi hapo Jaji atakapopatikana kusikiliza shauri hilo. (4) Endapo kuanza kwa usikilizaji wa shauri kumeahirishwa chini ya masharti ya kanuni hii na hakuna uwezekano kuwa Jaji aliyepangiwa shauri hilo atapatikana ndani ya siku thelathini zijazo, Jaji mwingine atapangiwa kuendelea na usikilizaji huo. Katazo la kuahirisha shauri 27. Usikilizwaji wa shauri unapoanza, utaendelea mfululizo, isipokuwa kama mahakama itaona kuwa kuahirishwa kwa usikilizwaji zaidi ya siku inayofuata ni muhimu kwa sababu zitakazoandikwa katika mwenendo wa shauri. Jaji kushindwa kuendelea na shauri 28.-(1) Endapo Jaji alieanza kusikiliza shauri atashindwa kuhitimisha shauri kwa sababu ya ugonjwa, kifo au sababu nyingine ya msingi, Jaji mwingine anaweza kupangiwa shauri hilo ndani ya siku kumi na nne na Jaji huyo aliyepokea shauri anaweza kushughulikia 13 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) Mlalamikaji kushindwa kuhudhuria Mlalamikiwa kushindwa kuhudhuria ushahidi wowote au hati iliyopokelewa kama vile ushahidi huo au hati hiyo imepokelewa au kuandaliwa na yeye mwenyewe na anaweza kuendelea na shauri hilo kuanzia hatua ambayo mtangulizi wake aliishia. (2) Jaji aliyepokea shauri ataandika sababu za kupokea shauri hilo kabla ya kuendelea na usikilizaji. 29.-(1) Endapo mlalamikaji atashindwa kufika mbele ya mahakama siku ambayo shauri limepangwa kwa kwa ajili ya usikilizaji, mahakama inaweza kutupilia mbali shauri hilo. (2) Endapo shauri limetupiliwa mbali chini ya kanuni hii, mahakama inaweza, baada ya maombi kuletwa ndani ya siku kumi na nne tangu kutupiliwa mbali, kulirejesha shauri ikiwa mlalamikaji atairidhisha mahakama kwamba kutofika kwake siku ya usikilizaji kulitokana na sababu ya msingi. 30.-(1) Endapo mlalamikiwa atashindwa kufika mbele ya mahakama siku ambayo shauri limepangwa kwa ajili ya usikilizaji, mahakama inaweza kuendelea kusikiliza shauri hilo bila uwepo wake. (2) Mlalamikiwa ambaye amri au uamuzi wa upande mmoja umetolewa dhidi yake atakuwa na haki ya kuomba kutenguliwa kwa amri au uamuzi huo ndani ya siku kumi na nne tangu amri au uamuzi huo ulipotolewa. Kuhudhuria kupitia wakili 31. Kwa madhumuni ya Kanuni hizi, kuhudhuria kwa wakili kutachukuliwa kuwa ni kuhudhuria kwa mhusika wa shauri anayewakilishwa. Kuondoa shauri 32.-(1) Mlalamikaji anaweza, kwa notisi ya maandishi, kuondoa shauri wakati wowote baada ya shauri kufunguliwa na kabla ya uamuzi kutolewa, kwa kuzingatia masharti yanayohusiana na gharama za shauri ambazo mahakama inaweza kuona inafaa kutoa. ataondoa shauri, hatakuwa na haki ya kufungua shauri jipya kuhusiana na uchaguzi huo isipokuwa wakati wa kuondolewa kwa shauri hilo, mahakama inaweza kutoa amri ya kumruhusu kufungua shauri jipya kuhusiana na uchaguzi huo kwa (2) Endapo mlalamikaji 14 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) Ukomo wa shauri Shauri kutotupiliwa mbali kwa sababu ya kasoro ya kiutaratibu kuzingatia sheria ya ukomo wa muda na endapo itajiridhisha kuwa uondoaji wa shauri umesababishwa na kasoro yoyote ya kiutaratibu ambayo ingesababisha shauri hilo kushindwa. (3) Endapo kuna walalamikaji wawili au zaidi, shauri hilo halitaondolewa isipokuwa kwa maombi ya maandishi ya walalamikaji wote. 33.-(1) Shauri litakoma baada ya- (a) kifo cha mlalamikaji aliyekuwa mhusika pekee au mlalamikaji pekee aliyekuwa amebaki hai; au (b) kifo cha mgombea aliyeshinda. (2) Endapo shauri litakoma kwa sababu ya kifo cha mlalamikaji aliyekuwa mhusika pekee au mlalamikaji pekee aliyekuwa amebaki hai mahakama inaweza, ikiwa itaona ni sawa na haki kufanya hivyo, kumpa mlalamikiwa au, endapo kuna walalamikiwa wawili au zaidi, kila mlalamikiwa, gharama za shauri ambazo mahakama inaweza kuona inafaa: Isipokuwa kwamba, kiwango cha gharama za shauri atakazopewa mlalamikiwa chini ya kanuni hii hakitazidi kiwango cha gharama za shauri ambacho mlalamikaji aliweka kama dhamana kwa ajili ya mlalakiwa huyo. 34.-(1) Isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo katika Kanuni hizi, hakuna shauri litakalotupiliwa mbali kwa sababu tu ya kutozingatia masharti yoyote ya Kanuni hizi au kasoro nyingine yoyote ya kiutaratibu isipokuwa kama mahakama ina maoni kwamba kutozingatia huko au kasoro hiyo inaweza kusababisha upotoshaji wa haki. imesababisha au (2) Endapo masharti yoyote ya Kanuni hizi hayajazingatiwa au kumekuwa na kasoro nyingine yoyote ya kiutaratibu, mahakama inaweza kumtaka mlalamikaji kurekebisha kutozingatia huko au kasoro hiyo kwa namna ambayo inaweza kuelekeza na kwa masharti ya kulipa au kutolipa gharama kadri itakavyoamua. (3) Endapo mahakama amri ya marekebisho chini ya kanuni hii, na mlalamikaji imetoa 15 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) anashindwa kuzingatia amri hiyo ndani ya muda ulioelekezwa, mahakama inaweza kufukuza shauri hilo. Ada Sura ya 21 na Sheria Na. 13 ya 2018 ya Zanzibar 35.-(1) Ada za mahakama ni kama zilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Kanuni hizi. (2) Mhusika wa shauri ambaye amepewa msaada wa kisheria chini ya Sheria ya Msaada wa Kisheria hatalipa ada. Kufutwa kwa Kanuni TS. Na. 782 la 2020 934 la 2020 36. Kanuni za Uchaguzi za Serikali za Mitaa za Mwaka 2020 zinafutwa. 16 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) _____________ JEDWALI LA KWANZA ______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5, 10 na 21) _______________ KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA/ ZANZIBAR Masjala ya ........................................ Mahali ………………………. FOMU A SHAURI LA UCHAGUZI NA… ....... LA MWAKA 20……...... Katika Shauri la Uchaguzi chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge za Mwaka 2025. ........................................................................................ Mlalamikaji/ Walalamikaji dhidi ya ..... ..................................................................................Mlalamikiwa/ Walalamikiwa HATI YA SHAURI LA UCHAGUZI [Kanuni ya 5(1)] 17 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) FOMU B KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA/ ZANZIBAR Masjala ya........................................ Mahali ………………………. SHAURI LA UCHAGUZI NA… ....... LA MWAKA 20……..... Katika Shauri la Uchaguzi chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge za Mwaka 2025. ........................................................................................................................ Mlalamikaji/ Walalamikaji dhidi ya ....... .................................................................................... Mlalamikiwa/ Walalamikiwa NOTISI YA KUFUNGULIWA KWA SHAURI LA UCHAGUZI [Kanuni ya 10(1)(a)] Kwa: Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi. DODOMA Unataarifiwa kuwa shauri hili, ambalo nakala ya hati yake imeambatishwa pamoja na notisi hii, lilifunguliwa katika Mahakama ya …………................. ya ………….. tarehe ................ 20 ......... Tarehe .................................... .......................................... Msajili/Mrajisi 18 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) FOMU C KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA/ ZANZIBAR Masjala ya ........................................ Mahali ………………………. SHAURI LA UCHAGUZI NA… ....... LA MWAKA 20……..... Katika Shauri la Uchaguzi chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge za Mwaka 2025. ..................................................................................................................... Mlalamikaji/ Walalamikaji dhidi ya ..... .................................................................................. Mlalamikiwa/ Walalamikiwa NOTISI YA KUWASILISHA MAJIBU YA SHAURI LA UCHAGUZI NA KUHUDHURIA [Kanuni ya 10(1)(b)] ......................................................................................................................... Kwa: ...................................................................................................................................... ............................................................. (jina na anwani ya mlalamikiwa). Unataarifiwa kuwa shauri hili, ambalo nakala ya hati yake imeambatishwa pamoja na notisi hii, lilifunguliwa katika mahakama hii tarehe ................ 20 ......... Unatakiwa kuwasilisha majibu ya shauri hilo ndani ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kupokea nakala ya hati ya shauri na kufika mbele yangu katika mahakama saa ya…………………………..………. ………………….kamili mchana kwa madhumuni ya kupanga tarehe ya usikilizwaji wa shauri. ………………….. tarehe Tarehe ....... ................ .................................... Msajili/Mrajisi Nakala kwa: (jina na anwani ya mlalamikaji). 19 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) FOMU D KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA/ ZANZIBAR Masjala ya ........................................ Mahali ………………………. SHAURI LA UCHAGUZI NA… ....... LA MWAKA 20……..... Katika Shauri la Uchaguzi chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge za Mwaka 2025. ........................................................................................ Mlalamikaji/ Walalamikaji dhidi ya ......................................................................................Mlalamikiwa/ Walalamikiwa MAELEZO YA MAANDISHI YA SHAHIDI [Kanuni ya 21(7)] Kwa ajili ya ……………..………. (andika jina la mhusika ambaye maelezo yanatolewa kwa ajili yake) Yametolewa na: Bw/Bibi/Bi ……………………………………………………………................ wa S.L.P……………………………………………………………………………………… …. Maelezo ya shahidi wa Kwanza/ Pili/ Tatu/ Nne/ Sita / Saba……………………………………. Nyaraka/vitu vinavyorejewa ………………………………………………………………. Tarehe ……………………………………………………………………………………… 1. Kiini cha Maelezo ya Shahidi 1.1. Isipokuwa kama haiwezekani, maelezo ya shahidi yatakuwa katika maneno ya shahidi aliyekusudiwa, maelezo hayo yatatolewa katika nafsi ya kwanza na yataeleza: (a) jina kamili la shahidi, makazi yake na ikiwa anatoa maelezo hayo kwa taaluma yake au wadhifa wake, anwani ya mahali pa kazi, wadhfa wake na jina la kampuni yake au mwajiri; na (b) kwamba yeye ni mhusika katika shauri. 2. Maelezo ya shahidi yataonyesha: (a) ni maelezo yapi yanatokana na uelewa wake binafsi na ni yapi yanatokana na kutaarifiwa au imani; na (b) chanzo cha taarifa au msingi wa imani katika aya husika. 3. Rejea ya nyaraka / vitu 20 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) 3.1. Nyaraka/vitu vilivyotumika pamoja na maelezo ya shahidi vitathibitishwa na kutambuliwa na shahidi na kutenganishwa na maelezo ya shahidi. 3.2. Endapo shahidi anarejea nyaraka/kitu, ataeleza “Ninarejea (maelezo ya kitu/nyaraka) iliyowekwa alama ....................... ......................... ". 3.3. Kwenye kona ya juu kulia katika ukurasa wa kwanza (na katika ukurasa wa nyuma) wa kila nyaraka /kitu kutaandikwa kwa ufasaha: (a) mhusika wa shauri ambaye maelezo hayo yanakusudiwa kutolewa kwa niaba yake; (b) herufi za mwanzo za jina na jina la ukoo la shahidi; (c) namba ya maelezo kuhusiana na shahidi husika; na (d) herufi na namba za utambulisho za kila nyaraka/ kitu kilichorejewa. 3.4. Endapo shahidi atatoa maelezo zaidi ya mara moja ambayo yana nyaraka/vitu, katika shauri hilo hilo, namba katika nyaraka /vitu zitafuatana kwa mfululizo na hazitaanza upya kwa kila maelezo ya shahidi. 4. Muundo wa maelezo ya shahidi 4.1. Maelezo ya shahidi: (a) yatatolewa katika karatasi ya A4 yenye ubora madhubuti yenye mstari wa pambizo wa sentimita 3.5; (b) yatasomeka kikamilifu na yatachapishwa katika upande mmoja tu wa karatasi; (c) pale itakapowezekana, yatafungwa kwa usalama kwa namna ambayo haitakwamisha kuweka kwenye jalada, au vinginevyo kila ukurasa utaandikwa namba ya shauri na kuwekwa herufi za mwanzo za majina ya shahidi; (d) yatakuwa na kurasa zenye namba mfululizo kama maelezo tofauti (au kama moja ya maelezo kadhaa yaliyomo kwenye jalada); (e) yatagawanywa katika aya zenye namba; (f) yataainisha namba zote kwa tarakimu, ikiwa ni pamoja na tarehe; na (g) yatatoa rejea ya nyaraka yoyote au zozote zilizotajwa katika pambizo au katika maandishi yenye wino mzito kwenye kiini cha maelezo hayo. 4.2. Maelezo ya shahidi yatafuata mlolongo wa matukio au masuala yanayoelezewa. Kila aya, kwa kadri itakavyowezekana, itajikita katika kipengele tofauti cha mada. 5. Uthibitisho 5.1. Maelezo ya shahidi ni sawa na ushahidi wa mdomo ambao shahidi huyo angeutoa iwapo angeitwa kutoa ushahidi; lazima yajumuishe tamko la shahidi aliyekusudiwa kwamba anaamini taarifa zilizomo ndani yake ni za kweli. 5.2. Ili kuthibitisha maelezo ya shahidi ithibati ya ukweli itakuwa kama ifuatavyo: “Ninathibitisha kuwa taarifa zilizoelezwa katika maelezo haya ni za kweli”. 6. Kiapo (jurat) Kila kamishna wa viapo ambaye maelezo ya shahidi yamechukuliwa au kutolewa mbele yake ataandika jina lake na kueleza kwa ukweli katika kiapo cha uthibitisho mahali ambapo na tarehe ambayo maelezo hayo yamechukuliwa au kutolewa na atagonga muhuri wake. 21 Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge Tangazo la Serikali Na. 431 (Linaendelea) _______________ JEDWALI LA PILI _______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 35(1)) _______________ ADA 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. TZS. 200,000/= TZS. 50,000/= Kufungua shauri Kuwasilisha hati ya shauri iliyorekebishwa au kurekebisha hati ya shauri Kuwasilisha majibu ya hati ya shauri Kuwasilisha majibu ya hati ya shauri yaliyorekebishwa Kuwasilisha maombi kwa ajili ya kuamua dhamana ya gharama za shauri TZS. 20,000/= Kuwasilisha kiapo kinzani Kuwasilisha orodha chini ya kanuni ya 12(1) TZS. 50,000/= TZS. 50,000/= Kuwasilisha orodha ya mapingamizi chini ya kanuni ya 13(1) Kwa suala lingine lolote TZS. 100,000/= TZS. 50,000/= TZS. 50,000/= Ada sawa na inayopaswa kulipwa kwa suala kama hilo kwenye mashauri ya madai mahakamani. Dodoma, 10 Julai, 2025 GEORGE MCHECHE MASAJU Jaji Mkuu 22
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge za Mwaka 2025
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in