AI-assisted research summary: Rais anatamka kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia 3 Agosti 2025.
Hati ya Kuvunjwa Kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ISSN 0856 - 034X Tangazo la Serikali Na. 486 (Linaendelea) THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA Supplement No. 28 25th July, 2025 SUBSIDIARY LEGISLATION To The Gazette of the United Republic of Tanzania No. 27 Vol. 106 Dated 25th July, 2025 Printed by The Government Printer, Dodoma by Order of Government TANGAZO LA SERIKALI NA. 486 la tarehe 25/7/2025 KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Y A MWAKA, 1977 (SURA YA 2) _____ HATI _____ (Imetengenezwa chini ya Ibara ya 90(2)(a)) HATI YA KUVUNJWA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2025 KWA KUWA, Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka 2025; NA KWA KUWA, kwa mujibu wa kifungu cha 49 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sheria Na. 1 ya Mwaka 2024, uteuzi wa wagombea kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu hauwezi kufanyika isipokuwa kama Bunge limekwishavunjwa; NA KWA KUWA, kwa mujibu wa Ibara ya 90(2)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka, 1977, Rais anaweza kulivunja Bunge iwapo limemaliza muda wa uhai wake wa miaka mitano kwa mujibu wa Ibara ya 65 ya Katiba au wakati wowote ndani ya kipindi cha miezi kumi na mbili ya mwisho ya uhai wa Bunge; HIVYO BASI, mimi, SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka niliyopewa chini ya Ibara ya 90(2)(a) ya Katiba ninalivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia tarehe 3 Agosti, 2025 ili kutoa fursa kufanyika kwa uteuzi wa wagombea katika Uchaguzi Mkuu na kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu. 1 Hati ya Kuvunjwa Kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tangazo la Serikali Na. 486 (Linaendelea) Hati hii imethibitishwa kwa saini yangu na Lakiri ya Umma leo tarehe 20 Julai, 2025. L.S Ikulu, Dodoma SAMIA SULUHU HASSAN Rais 2