AI-assisted research summary: The President declares 29 October 2025 a public holiday.
Tamko la Kutangaza Siku ya Uchaguzi Mkuu Kuwa Siku ya Mapumziko ISSN 0856 - 034X Tangazo la Serikali Na. 617 (Linaendelea) THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA Supplement No. 40 24th October, 2025 SUBSIDIARY LEGISLATION To The Gazette of the United Republic of Tanzania No. 37 Vol. 106 Dated 24thOctober, 2025 Printed by The Government Printer, Dodoma by Order of Government TANGAZO LA SERIKALI Na. 617 la tarehe 24/10/2025 SHERIA YA SIKUKUU ZA KITAIFA, (SURA YA 35) ______ TAMKO ______ (Limetolewa chini ya kifungu cha 3) TAMKO LA KUTANGAZA SIKU YA UCHAGUZI MKUU KUWA SIKU YA MAPUMZIKO, 2025 KWA KUWA kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa, Sura ya 35 kinampa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mamlaka ya kuteua siku yoyote tofauti na siku zilizoorodheshwa kwenye Jedwali ya Sheria hiyo na kuitamka siku hiyo kuwa siku ya mapumziko. NA KWA KUWA kwa madhumuni ya kuwawezesha wananchi wote wenye sifa kutumia haki yao ya kikatiba kupiga kura, Rais ameona ni muhimu kutangaza Siku ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kuwa siku ya mapumziko; NA KWA KUWA Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuwa Jumatano ya tarehe 29 Oktoba, 2025, ambayo ni siku ya kazi, kuwa ndiyo siku ya uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025; 1 Tamko la Kutangaza Siku ya Uchaguzi Mkuu Kuwa Siku ya Mapumziko Tangazo la Serikali Na. 617 (Linaendelea) HIVYO BASI, kwa kutumia mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa, Sura ya 35, Mimi, SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatangaza rasmi kuwa tarehe 29 Oktoba, 2025 itakuwa siku ya mapumziko. Hati hii imethibitishwa kwa saini yangu na kuwekwa Lakiri ya Umma leo tarehe 22 Oktoba, 2025. L.S Ikulu Dodoma SAMIA SULUHU HASSAN Rais 2