AI-assisted research summary: Rais anatisha Mkutano wa Bunge Jipya ufanyike Dodoma tarehe 10 Novemba 2020 saa 3:00 asubuhi.
Hati ya Kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya ISSN 0856-1001X THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA SPECIAL SUPPLEMENT Supplement No. 44 5th November, 2020 to the Special Gazette of the United Republic of Tanzania No. 44 Vol. 101 dated 5th November, 2020 Printed by the Government Printer, Dodoma by Order of Government TANGAZO LA SERIKALI NA. 942A la tarehe 05/11/2020 KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 (SURA YA 2) _____ HATI _____ (Imetolewa kwa Mujibu wa Ibara ya 90(1)) HATI YA KUITISHA MKUTANO WA BUNGE JIPYA KWA KUWA, Uchaguzi Mkuu ulifanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; NA KWA KUWA, masharti ya Ibara Ndogo ya (1) ya Ibara ya 90 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, yanamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya kabla ya kupita siku saba tangu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu; NA KWA KUWA, matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 yalitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 30 Oktoba, 2020; HIVYO BASI, MIMI, JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka niliyonayo chini ya Ibara ya 90(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, ninaitisha Mkutano wa Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ufanyike katika Ukumbi wa Bunge uliopo mjini Dodoma, tarehe 10 Novemba, 2020, kuanzia saa 3:00 asubuhi. 1 Hati ya Kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya KWA KUTHIBITISHA, ninaweka saini yangu na Mhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Hati hii, leo tarehe 5 Novemba, 2020. L.S Dodoma, 5th Novemba, 2020 JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI Rais 2